Hotuba ya Seif Shariff! - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jukwaa la Siasa


Jukwaa la Siasa Tanzania & World Politics General Discussion Forum. You need to be registered in order to post your comment(s)


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rating: Thread Rating: 1 votes, 4.00 average. Display Modes
Old 27th July 2007, 09:26 PM   #1
Hotuba ya Seif Shariff!
JokaKuu JokaKuu is offline 27th July 2007, 09:26 PM
Rating: (1 votes - 4.00 average)

Hotuba ya Maalim Seif Kibanda Maiti
Waheshimiwa naomba niungane na Mwenyekiti wa Wilaya kuwashukuruni nyote ambao jioni hii mmeamua kushiriki kwa ukamilifu katika kikao hiki au mkutano huu ambao ni miongoni mwa mikutano yetu ya kampeni. Mimi nadhani ukikaa hapa kwenye jukwaa utadhani kuna bahari hivi sio watu.

Waheshimiwa, leo tumekutana hapa, ni mkutano maalum. Asubuhi leo nilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, na ilikuwa mada yetu kubwa ni elimu, tayari nishazungumza na waandishi juu ya mada ya Uchumi na mkutano unaokuja tutazungumza na waandishi juu ya mada ya Afya. Sasa kuna suala moja ambalo ni muhimu sana sana nimehisi nilizungumze na wazanzibari moja kwa moja. Ndio maana ya mkutano huu. Na naamini Wazanzibari wengine ambao hawakuwahi kufika naamini wananisikiliza, naomba wanisikilize kwa makini.

Mada ya leo ni kuhusu hatma ya nchi yetu, hatma ya Zanzibar yetu, Zanzibar katika Muungano. Waheshimiwa, napenda nianze mada hii kwa kusema kwamba Zanzibar ina historia ndefu. Katika sehemu hii ya Afrika; Afrika mashariki na Afrika ya kati, Zanzibar ndio ilikuwa kwa kweli ni Dola ya kwanza. Dola hii ni Dola ambayo ilisambaa kuanzia hapa visiwani kwetu moja kwa moja... Tanganyika ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar, Kenya ilikuwa sehemu ya Dola ya Zanzibar, Uganda ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar, Mashariki ya Congo ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar, Kaskazini ya Malawi ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar. Kwa hiyo, Zanzibar ni nchi, sehemu au Dola yenye historia ndefu kabisa.

Katika sehemu hizi za Afrika Mashariki na kati dola ambayo ilitambulikana katika miaka ya karne ya 19 ni Zanzibar. Hapa Zanzibar palikuwa na Mabalozi wa nachi mbali mbali Wakiziwakilisha nchi zao.

Hii Zanzibar ilikuwa ni Dola kabla ya Tanganyika, Kenya, Uganda na katika nchi nyingine Afrika ya Mashariki na ya kati. Huo ndio utukufu wa Zanzibar.

Katika miaka ya 1880 na 1885, Wakoloni walianza kuingia sehemu hizi... Wakaamua kugawana Afrika. Katika mkutano uliofanyika Berlin 1885 wakamnyang'anya mtawala wa Zanzibar sehemu yote ya Afrika. Zanzibar wakaachiwa visiwa pamoja na Mwambao wa maili kumi kwenda ndani. Kuanzia kaskazini mwa Kenya mpaka kusini ya Tanganyika. Ilikuwa yote hayo ni mamlaka ya Zanzibar. Wajerumani wakaamua kuununua ule mwambao wa maili kumi wa Tanganyika. Kenya Wajerumani hawakuinunua, mwambao wa Kenya ulibaki sehemu ya Zanzibar, Lamu ilikuwa sehemu ya Zanzibar mpaka mwaka 1963, Kenya ilipopata Uhuru wakakubaliana waache. Tukabaki na Unguja na Pemba kama nchi.

Katika miaka ya 1950, 56, 57, Wazanzibari wakaunda vyama vya siasa, kumwondoa mkoloni.

Tukawa na Afro - Shirazi Party, Zanzibar Nationalist Party au Hizbu, Zanzibar and Pemba People's Party (ZPPP), tukawa na Umma Party.

Hivi ni vyama vilivyotafautiana kwa sera, kwa itikadi, lakini vyote vilishirikiana kumuondoa mkoloni Zanzibar.

Zanzibar ikapata uhuru tarehe 10/12/1963. Hapo Muingereza akaondoka. Alipoondoka Muingereza, Mkuu wa nchi akawa Sultani.

Zanzibar na Kenya zikajiunga na Umoja wa Mataifa kama wanachama kamili 13/12/1963 na bendera ya Zanzibar ilipanda katika Umoja wa Mataifa kama nchi nyingine.

12/1/1964 tukapinduana. Afro-Shiraz Party wakafanya mapinduzi, wakaipindua serikali ya Sultan, na Sultan akakimbia nchi.

Sasa, baada ya hapo ikaundwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ... ilikuwa ni serikali kamili, ni dola yake ya Wazanzibari. Tukawa na wimbo wetu wa Taifa. Tukawana Rais wetu Zanzibar.

Bahati mbaya uhuru huu wa Zanzibar ulidumu kwa siku 137 tu. Ilipofika tarehe 26/4/1964, Wazanzibari wakasikia ikitangazwa kuwa Zanzibar na Tanganyika zimeungana kufanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siku 137 ikawa Zanzibar kama nchi, kama dola imekwisha, haipo tena.

Kwahivyo wazee wetu hawa wakaunganisha nchi. Lakini tuangalie nini kilitokea katika kuunganisha nchi.

Kwanza tujue tulikuwa na mkataba wa Muungano. Mkataba huo ulionesha kwamba kutakuwa na mamlaka tatu. Kwahiyo wakakubaliana yako mambo yatakuwa ni ya Muungano na yapo ambayo si ya Muungano. Kwahiyo wakakubaliana pawe na mamlaka tatu. Moja itasimamia mambo ya Muungano, mamlaka ya pili itasimamia mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Zanzibar ikawekwa mamlaka yake tofauti (halikadhalika) Tanganyika. Lakini serikali zikawa mbili. Tukaambiwa ati Zanzibar watakuwa na serikali yao kusimamia mambo ambayo si ya Muungano.

Lakini Tanganyika mambo yao yatasimamiwa na serikali hiyo hiyo ya Muungano. Hapo ndipo kilipoanza "Kizungumkuti" hapo. Hapo ndio mwanzo wa "Kizungumkuti" hapo.

We una mamlaka, kwa serikali ya Muungano ilipaswa isimamie mambo ya Muungano. Na Tanganyika serikali yao isimamie mambo yao yasiyo ya Muungano. Lakini tukaambiwa kwamba, serikali ya Muungano ndiyo itakayosimamia (pia) mambo yote ya Tanganyika.

Sasa maana yake nini! Maana yake Tanganyika ikajivika joho la Muungano.

Na angalia baada ya Muungano, Katiba iliyoendelea kutumika ni katiba ya Tanganyika. Bendera iliyotumika ni bendera ya Tanganyika iliyofanyiwa marekebisho madogo. Nembo ile Adam na Hawa ni ile ile iliyokuwa ya Tanganyika ikaambiwa sasa ni ya Muungano.

Kwahiyo kila lililokuwa jambo la Tanganyika likafanywa la Muungano. Kwa hiyo sisi Zanzibar tukatoa madaraka yetu tukidhani tunaikabidhi serikali ya Muungano na Tanganyika watatoa madaraka yao wayakabidhi serikali ya Muungano, lakini lililotendeka, Tanganyika wakawa ndio Muungano. Kwahiyo tuliopoteza ni sisi Wazanzibari. Sio Tanganyika. Tanganyika ndio maana mpaka leo ukizungumzia serikali tatu wanakuwa wakali kweli kweli.

Kwasababu ikiwepo serikali tatu kutakuwa na chombo tofauti chakusimamia mambo ya Muungano. Na hapo watakuwa wao wametoa na sisi tumetoa.

Suala la katiba hiyo ambayo ilikuwa ya Tanganyika ikaambiwa sasa ya Muungano, kwa mujibu wa makubaliano ya Muungano ni kwamba katiba hiyo ilikuwa idumu kwa muda usiozidi mwaka mmoja tu basi. Kabla ya mwaka kuisha ilikuwa Rais aunde Tume ya kuandaa mapendekezo ya katiba. Halafu aitishe Bunge maalum la katiba kufanya katiba ya Jamhuri ya Muungano. Mwaka ulimalizika halikufanyika hilo.

Tukaendelea na utaratibu huo (katiba ya Tanganyika) kuanzia 1964 mpaka 1977 baada ya TANU na Afro kuungana, ile ile kamati ya TANU na Afro ndio zikaambiwa sasa itayarishe katiba ya Jamhuri ya Muungano. Miaka 13 imeshapita. Na bunge lile lile ndio ikaambiwa litunge katiba mpya.

Kwa hiyo hata yale makubaliano ya muungano hayakufuatwa.

Kwa mujibu wa mkataba wa Muungano, ilikuwa baada ya huwekewa saini Muungano, basi bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar kila mmoja kwa upande wake lithibitishe makubaliano ya Muungano. Bunge la Tanganyika lilifanya hivyo, lakini kumbukumbu zote zinaonyesha Baraza la Mapinduzi halikufanya kazi hiyo, Baraza la Mapinduzi mpaka hii leo haijathibitisha makubaliano ya Muungano. Kwahiyo nataka mjue mazingira ya Muungano ni hayo, ujanja ujanja, ulaghai.

Tumeungana 1964 na mambo ambayo yamo katika mkataba wa Muungano, waasisi walikubaliana ni 11 tu.

Naona niwasomee myajue: Jambo la kwanza ilikuwa ni Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania.

La pili, mambo ya nchi za nje. Tatu, Ulinzi. Nne, polisi. Tano, mamlaka juu ya mambo yanayohusu kutangaza hali ya hatari. Sita, Uraia. Saba, Uhamiaji. Nane, mikopo na biashara ya nje.

Tisa, utumishi katika serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kumi, Kodi ya mapato, ushuru wa forodha na kumi na moja Bandari, usafiri wa anga na posta na simu.

Lakini kuanzia hapo mpaka leo mambo hayo yamekuwa yakiongezwa hadi sasa yashafika 23. Na ukijayachambua moja moja yanafika 36. Na kama nilivyosema mwanzo, waliosarenda mamlaka ni Zanzibar.

Hiyo ni historia fupi tu. Nataka sasa nije kwenye kiini cha mazungumzo yangu.

Tuangalie athari gani zimepatikana kwa Muungano huu.

Athari ya kwanza ni kuviza na kudunisha uchumi wa Zanzibar. Kwanini. Kwa sababu chombo ambacho kinaweza kusimamia uchumi kwa ufanisi ni Benki Kuu ya nchi yoyote ile.

Tuiangalie Benki Kuu yetu. Kwanza niwaambie Wazanzibari hatuna Benki Kuu. Ndio kusema hatuna chombo cha kudhibiti, kuratibu uchumi wetu.

Benki Kuu iliyopo ni ya Tanzania. Na tuangalie Benki Kuu (hii) imepatikanaje.

Huko nyuma mambo ambayo yalikuwa yafanywe na Benki Kuu kwa Afrika Mashariki nzima, Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar yakifanywa na chombo kilichoitwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (East African Currency Board).

Sisi kama nchi Zanzibar na mwanachama wa Bodi hiyo tulikuwa na mwakilishi wetu mwenye sauti.

Lakini baada ya muungano tu, viongozi wa Tanganyika wakafanya njama kumtoa mwakilishi wetu kwa kisingizio cha muungano.

Watu wa Bodi wakasema, hatuwezi kwani kwa mujibu wa Muungano wenu, mambo ya sarafu, mabenki, fedha za kigeni haya si mambo ya muungano. Wakakwama.

Lakini wakafanya mbinu wakahakikisha mambo ya sarafu, mabenki, fedha za kigeni yanaingizwa kwenye muungano. Nathubutu kusema yaliingizwa kinyemela. Ghafla likatiwa. Kwamba hili nalo ni jambo la muungano.

Baada ya hapo wakapata nguvu wakarudi katika bodi. Wakadai Zanzibar watolewe, hawana mamlaka juu ya sarafu na mabenki. Kwahiyo watolewe. Tukatolewa Zanzibar. Ikawa sasa sisi tunawakilishwa na Tanganyika katika hiyo Bodi.

Sasa ukaja wakati 1965 kila nchi ikataka iwe na Benki Kuu yake. Ile Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki ikaamua kuzisaidia nchi hizi kwakuzipa mitaji. Kenya wakapewa pesa zao, Uganda wakapewa pesa zao, Tanganyika wakapewa pesa zao. Pesa za Zanzibar je, wakazidai Tanganyika. Wakafanya mbinu mpaka wakazipata.

Ikaanzishwa Benki Kuu ya Tanzania. Kwa maana kwamba, mtaji ni fedha kutoka Tanganyika na Zanzibar.

Sasa kile kima ambacho kilitolewa ikawa kama ni mtaji wa Zanzibar, ni kama asilimia 11.4. Maana yake sisi ni Share holders. Benki ifanye shughuli zake mwisho wa mwaka tugawane faida kwa uwiano huo. Sisi tupate 11.4%. Nadhani kwa miaka zaidi ya 20 tulikuwa hatupati hata senti moja.

Sasa wameamua kutupa wametupa asilimia 4.5. Na anakuja Dkt, Omar anajisifu, Rais Mkapa anawapenda Wazanzibari, anawapa fedha sijui anawapanini.

Hatupi Bwana. Ile ni haki yetu tena tunadhulumiwa. Kwahiyo asizuke akasifu huyu mtu anaipenda sana Zanzibar. Haipendi hata kidogo.

Kama nilivyosema, Benki ndio inadhibiti mambo yote. Ikawa Waziri wetu wa Fedha wa Zanzibar yupo pale kama kusema "dignified clerk" karani aliyevishwa kilemba cha ukoka. Hana madaraka juu ya sera za fedha, sasa atawezaje kujenga uchumi wa Zanzibar.

Na ushahidi upo. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilishaamua kuanzisha kitu kinachoitwa "Off shore Companies" . Ilitumia dola laki moja kwa kazi hiyo. Lakini Waziri wa Fedha wa Tanganyika akasema No. Hakuna ruhsa.

Hili ni suala ambalo lingetumika kujenga uchumi wa Zanzibar kwa mashali ya Wazanzibari. Lakini wenzetu wanasema No. Hivyo nawaambieni uchumi umeathirika kiasi kikubwa.

Sheria iliyoanzisha Benki Kuu ya Tanzania kuna kipengele katika sheria ile kinasema: "Any Political Sub-division in the United Republic is just like a local government." Yaani mgawanyo wowote wa madaraka kisiasa unaofanywa ndani ya Jamhuri hii, basi kama serikali ya mtaa tu basi.

Kwahivyo, kwa sheria ya Benki Kuu serikali ya Zanzibar ni serikali ya mtaa tu basi.

Wakati ule waziri wa Fedha Zanzibar alikuwa marehemu Abdul-Aziz Twala. Marehemu Twala alipigania sana sana haki za Zanzibar. Na yeye alitaka kuanzisha Benki Kuu ya Zanzibar. Wakapigwa stop. Wakaambiwa hapana sheria hairuhusu. Wakataka waanzishe State Bank or National Bank, wakaambiwa hapana. Hii people's Bank mnayoiona hii, waliambiwa anzisheni kama kampuni ya kawaida tu.

Waliambiwa anzisheni kama kampuni ya kawaida tu, halafu watapewa leseni wafanye shughuli za kibenki. Kwahiyo Zanzibar People's Bank imeanzishwa kama kampuni sio kama benki.

Lakini kwanini kwa Zanzibar tu? Wakati Bara walipotaka kuanzisha mabenki yao walitunga sheria maalum ya kuanzishwa mabenki hayo.

Hii benki ya Taifa ya Biashara ilianzishwa kwa waraka au kwa sheria ya 1967, hivyo hivyo kwa CRDB na Mabenki yote. Lakini ya Zanzibar wakaambiwa hapana. Kwahiyo muone jinsi tulivyobanwa. Muone jinsi gani hatuwezi kufurukuta. Hatuwezi kujenga uchumi wetu kwa namna tunavyotaka sisi wenyewe. Hapo ndipo tulipofikishwa Wazanzibari. Hiyo ndiyo hali yetu.

Tunaambiwa kama nilivyosema kabla, kama serikali mbili. Lakini hebu nambieni jamani, mambo ya muungano yanajulikana ni machache tu.

Wizara zinazojulikana za muungano ni nne tu, Mambo ya Ndani, Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Elimu ya Juu na Teknolojia.

Hizi ni wizara za Muungano. Lakini nambie, Wizara ya Kilimo Bara, kilimo si suala la Muungano. Waziri wa (kilimo) mwisho wake Chumbe, hawezi kuingia huku. Lakini huyu anaitwa Waziri wa kilimo wa Muungano. Kaipata wapi hii?

Waziri wa Elimu - Sekondari na primari, mamlaka yake yanamalizika Chumbe. Lakini anaitwa Waziri wa Elimu na Utamaduni wa Muungano. Waziri wa Afya wa Bara, yeye ni kwa ajili ya Bara tu, sisi tuna Waziri wetu wa Afya huku. Lakini mbona yule mmoja anaitwa wa Muungano? Kapata wapi mamlaka hayo? Mnakiona kizungumkuti hicho? Mnakiona mkizungumkuti hicho?

Sasa matokeo yake nini. Tanzania ni mwanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloitwa UNESCO, ambalo linaloshughulika na mambo ya elimu na utamaduni. Na kila mwaka mawaziri wanakutana. Anayeiwakilisha Tanzania ni nani? Ni waziri wa bara sio wa Zanzibar.

Tanzania ni mwanachama wa shirika la Afya Duniani (WHO). Kila mwaka wanakutana mawaziri. Anayeiwakilisha Tanzania ni nani? Ni Waziri wa Afya wa Bara, sio wa Zanzibar.

Tanzania ni mwanachama wa shirika la chakula duniani, FAO. Anayewakilisha Tanzania ni nani? Ni waziri wa kilimo wa Bara.

Sasa anakwenda kule huu Utanzania kaupata wapi? Ajaaliwe tu amfikirie mwenziwe amchukue katika safari yake basi. Lakini mwenye mamlaka ni yeye. Akiamua asimchukue mtu kutoka Unguja hachukui. Na hakuna wa kumuuliza.

Mashirika hayo yanasaidia sana maendeleo ya nchi hizo. Sisi Waziri wetu hana mamlaka kule. Kinachotoka atakipata?

Unasema serikali mbili hizi hizi, unajua kubaki kwa serikali mbili ni kuendelea kuonewa, kupunjwa, kudhulumiwa na kudhalilishwa Zanzibar? Unajua hayo wewe? Unajua hivyo wewe?

Tunaendelea kudhalilishwa. Ndio maana tunasema ukitaka kuondoa matatizo ya muungano mbadili mfumo wa muungano waserikali mbili uwe wa serikali tatu.

Mimi sifahamu kwanini wenzetu wa Tanganyika hawalitaki hili. Wataathirika nini wao. Wakiwa na serikali yao wataathirika nini wao! Nini litawaathiri hamna.

Mfano mwingine.

Suala la michezo si suala la muungano. Sisi tunayo wizara yetu ya michezo huku nao wanayo yao. Au hatuna? Lakini leo hata sisi kuwakilishwa katika vyombo vya kilimwengu vya michezo, wenzetu hawataki. Ndio maana ZFA wanataka iwe mjumbewa FIFA lakini Bara wameweka mguu wao. Hawataki. Jamani kwani sisi Zanzibar tukiwa wajumbe na nyinyi mkawa wajumbe, nyinyi mtaathirika nini hasa? Nini wataathirika wenzetu hawa!

Waangalieni wenzenu Waingereza. United Kingdom. Uingereza nchi moja. Lakini Scotland inawakilishwa pale, ile Uingereza yenyewe au England inawakilishwa, Wales inawakilishwa na ni nchi moja; Ireland inawakilishwa. Wana timu nne. FIFA nne, wapi nne kila pahali nne, nne. Wenzetu wanaona choyo, hata sisi kuwa wanachama wa FIFA, mnaona choyo! Jamani; jamani!

Sasa mnapotaka serikali mbili ziendelee mnataka yaendelee haya? Unataka yaendelee kunyanyaswa kwa Zanzibar? Ndio maana yake.

Nasema kwahiyo basi matokeo ya muungano ni kwamba hatuna chombo cha kusimamia uchumi wetu. Ni lazima tukapige magoti kwa wenzetu Bara. Waziri wa Fedha wetu hana mamlaka yoyote. Sasa nchi itaendeelaaje kama huwezi kudhibiti uchumi wako.

Sasa hivi kuna shirika hili linaloitwa TRA. Shirika la kod la Tanzania. Sasa hawa wana branchi yao Zanzibar. Na hapa pana Kamishna na Msaidizi wa TRA. Ilikuwa fedha zinazokusanywa hapa zinakwenda People's Bank; Benki ya Watu wa Zanzibar ambayo ni Benki ya Serikali ya Zanzibar.

Kwa hiyo zile pesa zikitiwa Zanzibar serikali ya Zanzibar inaweza kuzitumia. Lakini kuanzia mwezi uliopita Agosti, mwezi wa nane mwaka huu, Bwana Mkapa anatoa amri, fedha zote zinazokusanywa na TRA ziende BoT yaani Benki Kuu ya Tanzania.

Serikali ya Zanzibar haina madaraka katika Benki Kuu ya Tanzana. Jamani kimebaki nini!

Bendera hatuna, wimbo wa Taifa hatuna, sarafu hatuna, hata kuamua mambo ya nje hatuna uwezo. Basi jamani hata hizi fedha ambazo zinakusanywa katika nchi yetu, hata kuzitumia hatuna ruhusa? Hata kutumia kodi hatuna ruhusa? Maana hata baraza la mji likikusanya manispaa taxes (kodi) wana uwezo wa kuzitumia wenyewe. Leo fedha zinakusanywa katika nchi yetu, serikali ya Zanzibar hawana ruhusa ya kuzitumia. Kumebaki nini jamani? Kumebaki nini?

Juzi nasikia wameleta watu kutoka Bara kuja kuwasimamia hawa wafanyakazi wa TRA akiwemo huyu Kamishna msaidizi, yaani hawa wamepewa madaraka waendeshe shughuli zaolakini hawaaminiwi. Kwahivyo wameletwa wanyapara kuja kuwasimamia.

Jamani tuna nchi? Mna nchi? Wazanzibari mna nchi? Ndio hali tulipofikishwa.

Wamesema Rais Mkapa anaipenda Zanzibar. Lakini mapenzi haya sijui mapenzi gani. Maana mapenzi haya tukiamka viboko. Tukilala bakora, ukitembea jela! Sasa haya mapenzi gani? Kwanini Mkapa anatoa amri sisi wana CUF tuteswe hapa, kwanini hasa? Kwanini. Mimi nasema amri hii niya Mkapa moja kwa moja. Kwasababu Mkapa ndiye Jemedari Mkuu wa majeshi yote. Usalama wanamwarifu mambo yanayofanywa Zanzibar na yeye anasema endeleeni.

Sasa mnajua maana yake? Maana yake moja ni kumsaidia mtu wake ashinde. Ati nyinyi wana CUF mtavunjika moyo mtachoka.

Ya pili ni kwamba anataka mateso yazidi ili Wazanzibari wafike pahala, waseme, si basi hiyo serikali moja ije? Maana nakumbuka wakati wanataka kuunganisha vyama vya Afro na TANU, Zanzibar walishawishiwa na mipango ikafanywa, ikawa hali ya maisha ni ngumu kweli kweli Zanzibar.

Kwahiyo lilipokuja pendekezwa kuunganisha vyama watu wakasema afadhali huenda tukapata ahueni. Na hivyo Wazanzibari wengi wakaunga mkono Afro-Shiraz na TANU vikaunganishwa. Ili kuona vipi, watapata ahueni. Mwalimu Nyerere mwenyewe akasema hapo Amani, kwamba ile furaha aliyoiona katika nyuso za Wazanzibari hajapata kuonapo, kwa kuunganisha vyama.

Mkakati ulikuwa vipi, wataabishe, wapate taabu, baada ya hapo ukija na pendekezo hili watakubali.

Wanadhani wakiwatesa kiasi walichowatesa mtachoka wakisema, basi si afadhali tuwe na serikali moja mtasema ndiooo.

Wazanzibari nimesema hapa kwanini wenzetu ukiwatajia serikali tatu hawataki. Hawa Bwana nitawaambieni sasa hivi hapa. Nchi yenu Zanzibar ni tajiri sana.

Kwa ule ule ulaghai, suala la mafuta na gesi lilitiwa kama ni jambo la muungano.Lakini dhahabu si jambo la muungano. Almasi si jambo la Muungano, mkaa wa mawe si jambo la muungano.

Kitu cha muungano ni mafuta. na kwanini walifanya hivyo. Walifanya vile walishajua Zanziba kuna mafuta mengi sana.

Mwaka 1996/97, serikali ya Muungano iliiomba shirika moja la Canada kufanya uchunguzi. Shirika hilo likagundua mafuta mengi sana.

Sasa ikawa wafanye mipango yachimbwe chini ya serikali ya Muungano. Serikali ya Zanzibar wakachachamaa. Wakatafuta kampuni nyingine ya Kimarekani. Sikilizeni ripoti yao. Wanasema Zanzibar mafuta yaliyopo yakianza kuchimbwa, yatachimbwa kwa miaka 80. Kila mwaka Zanzibar inaweza ikapata dola za Kimarekani bilioni 100.

Sasa kwa mpango wa sasa kwavile ni suala la muungano, wakiyachimba wao sisi tutapata asilimia 4.5 tu. Zilizobaki zote wachukue wao.

Basi hiyo ndiyo sababu mnapigwa. Hiyo ndiyo Bwana Mkubwa (Mkapa) anashikilia lazima mtu wake (Karume) apite ili amalize kazi.

JokaKuu
JF Premium Member
Points: 970,785, Level: 100 Points: 970,785, Level: 100 Points: 970,785, Level: 100
Activity: 8% Activity: 8% Activity: 8%
Join Date: Mon Jul 2006
Posts: 3,389
Thanks: 298
Thanked 432 Times in 244 Posts
Views: 5083
Reply With Quote
  #2  
Old 27th July 2007, 10:32 PM
DAR si LAMU DAR si LAMU is offline
DAR si LAMU has no status.
JF Premium Member
Points: 176,724, Level: 100 Points: 176,724, Level: 100 Points: 176,724, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sat Mar 2007
Posts: 2,519
Thanks: 0
Thanked 8 Times in 6 Posts
Rep Power: 28
DAR si LAMU will become famous soon enoughDAR si LAMU will become famous soon enoughDAR si LAMU will become famous soon enoughDAR si LAMU will become famous soon enoughDAR si LAMU will become famous soon enoughDAR si LAMU will become famous soon enoughDAR si LAMU will become famous soon enoughDAR si LAMU will become famous soon enough
Default kwahiyo...

..zenj ni ya waarabu!

..kwa kuwa wao ndo waliokuwa wakimiliki eneo hilo la afrika kipindi hicho.

..zenj ni nchi kubwa ijitawalie yenyewe mambo yake na si kuwa kama mkoa!

..ina maana kwamba zenj imedhulumiwa aridhi yake iliyo bara mashariki mwa afrika!

..ina maana zenj ni ile ya zamani,na haiwezi badilika moyoni mwa watu!

..ina maana zenj haipo tena,lilobaki ni jina!
__________________
Dar na Lamu yote ni miji ya pwani,lakini haifanani!
Reply With Quote
  #3  
Old 27th July 2007, 11:09 PM
Mzalendohalisi Mzalendohalisi is offline
Mzalendohalisi has no status.
JF Premium Member
Points: 430,274, Level: 100 Points: 430,274, Level: 100 Points: 430,274, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Sun Jun 2007
Posts: 3,708
Thanks: 36
Thanked 12 Times in 12 Posts
Rep Power: 30
Mzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enough
Default

JokaKuu,
Pokea 5 kwa hii thread! JF inatupa mwanga kweli!
Niniuliza swali moja dogo- "kizungumkuti" maana yake ni nini? Neno linatumika tu Zenj au pia Pwani/bara?
Reply With Quote
  #4  
Old 28th July 2007, 12:48 AM
Mkandara Mkandara is offline
Mkandara Aviator
JF Premium Member
Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Thu Mar 2006
Location: T dot
Posts: 7,289
Thanks: 463
Thanked 747 Times in 325 Posts
Rep Power: 80
Mkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the rough
Default

Quote:
Mada ya leo ni kuhusu hatma ya nchi yetu, hatma ya Zanzibar yetu, Zanzibar katika Muungano. Waheshimiwa, napenda nianze mada hii kwa kusema kwamba Zanzibar ina historia ndefu. Katika sehemu hii ya Afrika; Afrika mashariki na Afrika ya kati, Zanzibar ndio ilikuwa kwa kweli ni Dola ya kwanza. Dola hii ni Dola ambayo ilisambaa kuanzia hapa visiwani kwetu moja kwa moja... Tanganyika ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar, Kenya ilikuwa sehemu ya Dola ya Zanzibar, Uganda ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar, Mashariki ya Congo ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar, Kaskazini ya Malawi ilikuwa ni sehemu ya Dola ya Zanzibar. Kwa hiyo, Zanzibar ni nchi, sehemu au Dola yenye historia ndefu kabisa.
Mawazo ya kikoloni kweli kweli.. maanake hata Mrumi (Romans) anaweza dai kuwa dunia nzima dola yake ndio ilikuwa ya kwanza!..Na upofu wa akili unazidi pale mtawaliwa huyu Kaizali mwenye asili ya Kiafrika akisifia eneo la nchi yake kutawaliwa!

Mengine yote safi lakini kisha likoroga,siwezi hata kummaliza!
Wakati wenzetu nchi kama Marekani wanajaribu kwa kila hali kufuta kasumba za kutawaliwa ktk elimu zao na kufundisha mwanzo mpya wenye mwanga, leo kiongozi anaturudisha karne 10 nyuma tukumbukie Dola ambayo ilitukuza zaidi biashara ya Utumwa wa mwafrika!.Huyu jamaa hawezi kabisa kuzungumza nje ya asili yake mwenyewe na hii ni hatari sana. Ni sawa na Ian Smith ahutubie kwa kuanza kusikifia historia ya Utawala wa kaburu!
__________________
Exploration of reality

Last edited by Mkandara; 28th July 2007 at 12:58 AM..
Reply With Quote
  #5  
Old 28th July 2007, 01:27 AM
Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is online now
Mzee Mwanakijiji anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100
Activity: 94% Activity: 94% Activity: 94%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,477
Thanks: 8,503
Thanked 4,689 Times in 1,320 Posts
Rep Power: 44
Mzee Mwanakijiji is on a distinguished roadMzee Mwanakijiji is on a distinguished road
Send a message via MSN to Mzee Mwanakijiji Send a message via Skype™ to Mzee Mwanakijiji
Default

Mkandara kumbuka kuna tofauti kubwa sana kati ya mtazamo wa watu weusi wa Marekani ambao kwao ukichanganya damu na mtu mweupe japo kiduchu basi wewe ni mtu mweusi hata kama una rangi nyeupe vipi. Mtazamo huo ukasababisha watu weusi wawe na mtazamo hasi wa watu weupe na kujivunia weusi wao. Hata hivyo ukienda Zanzibar na sehemu nyingine ambapo watu wamechangia damu na waarabu watu hujitukuza kwa kuwa na damu ya kiarabu na kutojivunia weusi wao. Utaona kuwa hata kama mtu ni mweusi vipi kwa vile ana nasaba ya kiarabu basi hujiita yeye mwarabu hata kama kwa waarabu wenyewe yawezekana asiwe mwarabu.

Ni hapa ndipo inapokuja dhana ya uarabu siyo rangi au ancestry bali ni tamaduni, mila, n.k Hivyo baadhi yao huhalalisha uarabu wao kwa kudai kuwa uarabu ni nasaba bora. Katika hili utaona mgongano wa mawazo kati ya weusi ambao hawajachangia damu kule Zanzibar na weusi ambao wamechangia damu.
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Reply With Quote
  #6  
Old 28th July 2007, 01:39 AM
Mkandara Mkandara is offline
Mkandara Aviator
JF Premium Member
Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100 Points: 580,633, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Thu Mar 2006
Location: T dot
Posts: 7,289
Thanks: 463
Thanked 747 Times in 325 Posts
Rep Power: 80
Mkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the rough
Default

Mzee Mwanakijiji,
Nimekupata na ndivyo navyoelewa matatizo ya Zanzibar yalipotokea!..
hawa jamaa mpaka leo hii kuna watu hujatambulisha kama Wapemba! na hujisifia kwa Upemba wao. Hao wengine akina point five nao hujiita Ma - colored, kiasi kwamba kuna ujinga fulani ktk baadhi ya watu hawa ambao hujaribu sana kuutangaza bara, sasa wanapokuja huku na kukuta sisi hatuelewi kitu wanashindwa kuelewa kabisa kwa nini hatuwezi kuelewa na kuzitukuza tofauti hizo.

Ndio maana hata ktk Mapinduzi utawasikia wakizungumzia Uarabu ama Uislaam kama vile Mapinduzi ni tukio lililokuja kuondoa Uislaam ama rangi za watu. Na kibaya zaidi ni pale wanapozidi kuleta historia za nyuma ambazo ni kumbukumbu mbaya sana kwa mtu mweusi. It's not fun at all!
Hawa watu wameshindwa hata kuona kuwa kuundwa kwa CCM Kulikuwa na malengo ya kuondoa kabisa ile historia ya vyama kuwa wawakilishi wa ASILI zao!..wameipoteza historia ya vyama vyao kuwakilisha asili za watu na kuifanya kama ni vyama vyenye demokrasia. That was then leo hii haiwezekani kabisa demokrasia kusimamia rangi za watu.

Na kwamba huo ulikuwa mwanzo mpya pamoja na kwamba ni mgumu sana lakini wameshindwa kabisa kutazama mazuri ya mseto huo kwa faida ya kizazi hiki cha Wazanzibar wenye asili tofauti. Lakini bado tu watajaribu kuvuta hawa Masultan ktk hutuba zao jambo ambalo linazidi kuwapa nguvu CCM kuwa hawa jamaa wanamkumbuka sana Sultan. Ndio maana huyu jamaa sina kabisa imani naye hata siku moja!
Even Amerika nyenyewe kama taifa, mshikaji wewe unaishi huko! umeona hata sehemu moja wakizungumzia sana mazuri ya Utawala wa Muingereza kabla ya Mapinduzi yao?.. Hapana!... historia kubwa ya nchi hiyo inaanza kwa Abraham Lincon. Sidhani kama kuna asilimia 1 ya wamarekani wanamkumbuka Mtawala wao wa mwisho kama vile sisi tunavyo jaribu kumbuka utawala wa Sultan.
__________________
Exploration of reality
Reply With Quote
  #7  
Old 28th July 2007, 02:29 AM
Mtanzania Mtanzania is offline
Mtanzania has no status.
JF Premium Member
Points: 645,736, Level: 100 Points: 645,736, Level: 100 Points: 645,736, Level: 100
Activity: 5% Activity: 5% Activity: 5%
 
Join Date: Thu May 2006
Location: UK
Posts: 4,923
Thanks: 62
Thanked 234 Times in 105 Posts
Rep Power: 33
Mtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enoughMtanzania will become famous soon enough
Default

Mkandara,

Mbona neno kasumba unalitumia vibaya sana? Ukifuatilia sana basi kila kitu ni kasumba tu, kuanzia wakataoliki kwenye makanisa yao, elimu madarasani, music tunayocheza na kusikiliza nk.

Elewa maana ya culture (the way we do things here)utakuta kwa mtu aliyekulia katika jamii fulani hawezi kukwepa baadhi ya mambo ambayo yanatendeka hapo mahali. Utakuwa unamwonea huyu mtu ukimhusisha na kasumba kila saa.

Inabidi ukae na Wazanzibar na uwasome na kuwajua ndio utajua mawazo ya Hamad ndio mawazo ya Wazanzibari walio wengi. je hilo ni kasumba? Mimi sina jibu.

Kushindwa kutambua historia na culture ya sehemu fulani ndio mwanzo wa migogoro mbalimbali duniani. Ndio maana akina Bush na Blair wanafikiri wanaweza kupeleka democracy Iraq, kumbe sehemu kama zile , bila a very powerful figure mambo hayaendi.
Reply With Quote
The Following User Says Thank You to Mtanzania For This Useful Post:
Mzenji73 (12th December 2009)
  #8  
Old 28th July 2007, 02:32 AM
T_Tonga T_Tonga is offline
T_Tonga has no status.
Senior Member
Points: 79,769, Level: 100 Points: 79,769, Level: 100 Points: 79,769, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Tue Jul 2007
Posts: 83
Thanks: 0
Thanked 3 Times in 3 Posts
Rep Power: 23
T_Tonga will become famous soon enoughT_Tonga will become famous soon enoughT_Tonga will become famous soon enoughT_Tonga will become famous soon enoughT_Tonga will become famous soon enoughT_Tonga will become famous soon enoughT_Tonga will become famous soon enoughT_Tonga will become famous soon enough
Default

ikiwa kweli hiyo ndio hali basi ipo dhulma kubwa sana inamaana chako kiwe chako changu kiwe chetu duh inafaa muungano kweli uangaliwe tena kwa nini mtu mzima anafanya urafiki na mtoto mdogo hapo pana nini kama si kutaka kumuharibu maana bara ni kubwa sana kuliko visiwa vya zanzibar lakini kosa sio tanganyika bali kosa liko kwa upande wa visiwani wao wakipewa ubalozi tu wa muda hujisahau mpaka watimuliwe ndio huanza tena kulalamika lakini wakiwa kwenye serekali hukaa kimya juzi nilion kwene gazeti waziri wa mambo ya nje kasema kuanzia sasa akienda safari za nje atachukua wajumbe wa baraza la wawakilishi japo mmoja alisema hayo kwenye mwaka koga makunduchi duh jamani kweli huo ni muungano au mtengano mimi nimesema muungano huu hauna muda iko siku watu watagawana mbao mungu ajaalie hiwe hivyo
Reply With Quote
  #9  
Old 28th July 2007, 02:32 AM
Mzalendohalisi Mzalendohalisi is offline
Mzalendohalisi has no status.
JF Premium Member
Points: 430,274, Level: 100 Points: 430,274, Level: 100 Points: 430,274, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Sun Jun 2007
Posts: 3,708
Thanks: 36
Thanked 12 Times in 12 Posts
Rep Power: 30
Mzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enoughMzalendohalisi will become famous soon enough
Default

Wandugu,
1. Seif anaongelea historia ya Wakati wa Usultani na Utumwa ambapo ushawishi wa Zanzibar ulifika mbali hado Kongo! Anashindwa kutambua leo ni 2007, miaka zaidi ya 140 baada ya utumwa na nchi hizi ziko huru na bara lote la Afrika pia! Kwa hiyo yeye angependa Zanzibar itawale eneo la Afrika Mash. Kama wakati wa Usltani? Hayo ni mabo ya zamani- na hapo anakosea!
2. Nyerere na Karume waliona mwanzoni kuwa na serikali tatu- hiyo ya tatu intagharmiwa na nani na kwa utaratibu gani? Manake Zanzibar ina watu 1 milion- halafu Bara 37 milion- total commitment ya kuchangia hii ya Muungano (Serikali ya tatu) ingekuwa taabu kiasi- mwanzoni ilikuwa hivyo. Sijui kama jawabu sasa ni serikali tatu tu! Kwa hiyo zikishakuwepo serikali tatu matatizo ya Zanzibar yataisha?
3. Je matatizo anayeyaongelea Seif- je yahusiana na Muundo wa Muungano tu? Mbona ukiangalia mfano mgawo wa misaada wa 4.5% bado ni mkubwa ukilinganisha na idadi ya watu- actually ingebidi iwe 2.6% ukifanya cross multiplication.
Halafu kama ni hii dhana ya misaada- ndo siku zote inaturidisha nyuma Watanzania- eti Muungano unawakatia msaada- je Comoro, Madagaska- leo wako wapi- wana nafuu zaidi ya Tanzania?
4. Haya anayoongelea Seif- hayajengi yanaangalia upande mmoja tu wa udhaifu wa Muungano- hakuna ndoa ambayo haina matatizo- ila hatuwezi kuangalia matatizo tu siku zote- vi vema naye Seif ajenge positive image over Muungano- yeye ukisoma hutuba yake ni malalamiko zaidi- mengine ya kweli, ila anayatumia kisiasa kujijenga!
5. Tatizo jingine pia hakuna uzalishaji- hakuna viwanda- vichache vilivyokuwepo kama cha sukari kilifungwa- je hii inatokana na Muungano? Bei ya karafuu imeshuka- kama ilivyo bei ya kahawa- je Seif atalaumu Muungano? Hayo mafuta yanaongelewa- siku nyingi- je ni Muungano ulikataa yasichimbwe?
Inaonekana kila tatizo Zanzibar Seif analaumu Muungano na bara- kwa hiyo watu wamebaki kulaumu tuu- Wapemba wengi wengi wapo Bara, pia Waunguja- wana maduka makubwa ya jumla ya nguo kariakoo- je kuna mtu toka Bara amelaumu!
Seif atambue tu watu wa Visiwani ni Watanzania wenzetu- na tunaishi kwa pamoja, hatubaguani- miaka 40 sasa!
Swala la kutafuta Mchawi wa matatizo ya Zanzibar na kusema ni Muungano- tu nafikiri Seif anakosea!
Reply With Quote
  #10  
Old 28th July 2007, 03:05 AM
Mzee Mwanakijiji's Avatar
Mzee Mwanakijiji Mzee Mwanakijiji is online now
Mzee Mwanakijiji anawashangaa wanaoitetea sheria mbovu
JF Premium Member
Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100 Points: 12,987,839, Level: 100
Activity: 94% Activity: 94% Activity: 94%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: Kijijini
Posts: 18,477
Thanks: 8,503
Thanked 4,689 Times in 1,320 Posts
Rep Power: 44
Mzee Mwanakijiji is on a distinguished roadMzee Mwanakijiji is on a distinguished road
Send a message via MSN to Mzee Mwanakijiji Send a message via Skype™ to Mzee Mwanakijiji
Default

labda hapa naomba tusaidiwe, mtumwa alikuwa na haki gani chini ya utawala wa waarabu, na wakati utawala wa Sultani unaota mizizi watu weusi (waislamu na wasio waislamu) walikuwa wanafurahia haki gani? Naomba nisaidiwe ni kitu gani mimi kama mtu huru leo hii kinishawishi ili niutamani utawala wa Sultani? Na kwa upande wa ndugu zetu wa Zanzibari, je ni kitu gani ambacho wanakimiss sana toka utawala wa Sultani?
__________________
Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
hotuba, seif, shariff


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Maalim Seif kuingia Serikali ya Karume Lunyungu Habari na Hoja mchanganyiko 28 11th December 2009 03:11 PM
Hotuba za Rais kila mwezi JokaKuu Jukwaa la Siasa 681 2nd December 2009 08:38 AM
Hongera Seif Mwingiliko!! na Pole sana.. Mzee Mwanakijiji Habari na Hoja mchanganyiko 5 29th January 2007 06:50 PM
HOTUBA ZA VIONGOZI...hotuba zimezidi!! Kitia Jukwaa la Siasa 1 4th December 2006 07:49 AM
Huyu Seif Hamad anadhani ye' ni nani? Mzee Mwanakijiji Jukwaa la Siasa 23 1st November 2006 04:02 PM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 02:02 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com

You Rated this Thread: