| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 1610
|
||||||||||||
|
#2
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Muda wake umefika labda naye anatayarishiwa mashitaka ya kupelekwa mahakamani.. maana sasa hana ofisi.. itakuwa vizuri labda wakafuata ushauri wa kamati ya Mwakyembe wa kuwajibisha wote kwenye scandal ya Richmond. Naomba kujua wakuu amestafu yeye mwenyewe au ndio umiri wake umefika au amembiwa kufanya hivyo??
__________________
Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber. ~Plato
|
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mambo haya ndio yanasababisha serikali kuonekana inalichezea Bunge. Kama amekubaliwa kustaafu, manake hajachukuliwa hatua zozote za kinidhanimu kama ilivyoshauriwa na Bunge. Kwa kweli kama Mwanyika amekubaliwa kustaafu bila ya kulazimishwa kisheria (Kuwajibishwa) basi kwa mara nyingine serikali yetu imetuthibitishia kuwa in wenyewe, na wenyewe ni wale waliomtuma Mwanyika kukubaliana na RICHMOND kama ilivyo na wao watamlinda, na kweli wamemlinda mpaka amestaafu.
Tatizo naona mkataba kati ya Mwanyika na walimtuma ni kumlinda akiwa kazini, nafikiri akitoka hapo itabidi atafute pa kujificha kwani uchaguzi unakaribia na JK anatafuta kura za imani, asije akawa mhanga wa sifa za serikali.
__________________
Now is the time to cut off the infected parts of society from active public life, before they endanger the entire body politic. |
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Wakuu ile dana dana iliyokuwepo ya kumshtaki sasa imejionesha wazi ilikuwa inafanywa makusudi ili jamaa astaafu n apate mafao yake, walah haki ya mafisadi, hafungwi mtu hapo!!
|
|
#5
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Huu ni mwendelezo wa Tanzania zaidi ya uijuavyo! Hakuna hata mmoja aliyewajibishwa tangu varangati la Richmond lianze licha ya kuwepo kwa ushahidi wa wazi. Itakuwa si haki kumwajibisha Mwanyika peke yake ilhali vigogo wenzake wameachiwa kuendelea na pensheni zao. Serikali yetu inajali "watu wake" na imeapa kuwalinda kwa kila hali.
Watafanya watakalo maana wanajua hamuwezi kuwafanya lolote. Hata uraisi bado wataendelea nao mwakani.
__________________
"Chunguza Mjomba, Utabaini!" |
|
#6
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
nchi haina rais makini unategemea nini.those kind of games utazisikia sana na hilo bunge lijalo hakuna cha maana kitakachoaamuliwa juu ya RICHMOND,wataanza kubishana tu kwa nini kuna mgao wa umeme and that is it
__________________
_______________________________ Kagatui kamusii atiagwako ageni=The Oilskin of the house is not for rubbing on the skin of strangers |
|
#7
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Sioni ubaya wowote kustaafu. Kwanza keshatimiza miaka 60 ambao ni umri wa lazima wa mtumishi wa serikali kustaafu. Ingawa inaweza kuonekana ni kulea maovu lakini watumishi wa serikali wafanyapo makosa (ingawa makosa mengine hayatangazwi) na kuwajibika kuadhibiwa, na hasa suala la kufukuzwa kazi, mara nyingi umri wao huangaliwa kabla ya adhabu kutolewa. Hii haiko kisheria lakini ni suala la ubinadamu tu. Hata mahakamani inatokea adhabu kupunguzwa kwa sababu ya umri.
Wakati mwingine lazima Serikali ionekane imara kuwa haishurutishwi na chombo chochote. Bunge litakapokaa mwezi November itatolewa taarifa kuwa Mwanasheria Mkuu kastaafu kwa lazima. Azimio la bunge litakuwa limetekelezwa. Wakianza kufukuzana kwa kila kosa linalotokea habaki mtu serikalini. Kastaafu mwacheni aende. Mengine baadae. Halafu kama ni suala la kuwajibishana kuhusu Richmond wa kuondoka ni wengi. |
|
#8
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
aaah siasa za bongo
__________________
2010 niko kikazi zaidi |
|
#9
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Labda kuna kitu kinaweza kufuat baada ya huyu jamaa kusitaafu, na ukichukulia kustaafu kweneyewe kumekuwa kwa lazima.
__________________
Praise is well, compliment is well, but affection--that is the last and final and most precious reward that any man can win, whether by character or achievement |
|
#10
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Mimi natamani wote wanaohusika na Richmond waondoke kabisa serikalini. Hata kama Kikwete naye ni mhusika aondoke. Nina hakika nchi inaweza kuenda mbele vizuri bila wababaishaji hawa wezi wakubwa. Hakuna lolote litakaloharibika hata kama serikali yote iliyo madarakani ikiondoka. Ilimradi tubaki na serikali safi yenye hofu ya Mungu kwa kuwajibika kwao. Lakini kwa sababu ya ujinga wao na wa baadhi ya watu wanadhani wakiondoka wao basi nchi haitabaki. Ni uongo na udanganyifu wao tu. Tumechoka na wezi wa mali za nchi yetu hii tuliyopewa wote na mwenye enzi Mungu wetu.
__________________
If OUR God offends you, then I suggest you consider another part of the world as your new home, because OUR God is part of our culture.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 02:09 PM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||