Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka - Page 5 - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jukwaa la Siasa


Jukwaa la Siasa Tanzania & World Politics General Discussion Forum. You need to be registered in order to post your comment(s)


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 6th October 2009, 09:36 AM  
Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka
Bill Bill is online now 6th October 2009, 09:36 AM

RAIS Jakaya Kikwete amekubali kustaafu kwa lazima kwa Mwansheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, ifikapo Novemba 6, mwaka huu.
Bw. Mwanyika anastaafu kwa lazima katika kipindi ambacho Mkutano wa 17 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utakuwa ukiendelea, ukitarajia kuhitimisha sakata la mkataba tata wa Richmond, ambao ulisainiwa wakati akiwa Mshauri Mkuu wa Serikali wa mambo yote ya kisheria.

Habari za kustaafu kwa lazima Bw. Mwanyika ambaye amekanusha mara kadhaa kuhusika kwake na Richmond, zimethibitishwa Dar es Salaam jana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Majibu ya maandishi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa gazeti hili, iliyosainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano (OR-MUU) Bi. Zamarad Kawawa, ilieleza; "Bw. Mwanyika amekubaliwa kustaafu atakapofikisha umri wa kustaafu kwa lazima wa miaka 60 ifikapo tarehe 6 Novemba, 2009."

Hatua ya Bw. Mwanyika kukubaliwa kutaafu kwa lazima inaibua maswali mengi, hasa kwa kuzingatia kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 59, haina kipengele kinachoeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atastaafu baada ya kufikisha umri wa miaka 60.

Kifungu kidogo cha (5) kinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atashika madaraka yake mpaka (a) uteuzi wake utakapofutwa na Rais au (b) mara tu kabla ya Rais mteule kushika madaraka ya Rais.

Kwa maana hiyo ya katiba Bw. Mwanyika angeweka kuacha kushika wadhifa huo ama kwa kuachishwa na Rais au kusubiri mwakani baada ya Uchaguzi Mkuu, kabla ya Rais mteule kushika wadhifa wa rais.

Kutokana na wadhifa wake huo, baada ya mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC kusainiwa, na baadaye bunge kuuda Kamati Teule ya kuchunguza utata uliogubika mkataba huo chini ya Dkt. Harrison Mwakyembe (Kyela), ilibainika kuwa utiaji saini mkataba huo ulisheheni makosa mengi.

Wakati akiwasilisha taarifa ya kamati iliyochungusa utiaji saini mkataba huo bungeni, Dkt. Mwakyembe alisema;

"Mkataba umesheheni makosa mengi ya kisheria yanayoashiria udhaifu mkubwa wa kitaalamu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali au ukosefu wa umakini katika kuiwakilisha serikali."

Dkt. Mwakyemba alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wakili wa Serikali, Bw. Donald Chidowu ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yoyote, hivyo, "Wawajibishwe na mamlaka ya juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu," alisema Dkt. Mwakyembe wakati akiwasilisha mapendekezo ya Kamati yake kwa bunge kuhusu hatua alizopaswa kuchukuliwa Mwanyika.

Baada ya Kamati hiyo kutoa mapendekezo hayo, Serikali kupitia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, ilitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya kamati, akisema kikatiba, Mamlaka ya Nidhamu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kwa hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji wakuu watatu waliokuwa wanaishauri Serikali, suala lake la kuhusishwa kwake katika mchakato mzima wa mkataba huo linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, IKULU," alisema Bw. Pinda.

Hata hivyo, katika Mkutano wa 16 wa Bunge uliomalizika mjini Dodoma, Serikali kupitia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Adam Malima, ilitangaza utekelezaji wa awamu ya pili mapendekezo ya Kamati ya Dkt. Mwakyembe, ambapo alisema Bw. Mwanyika hakuwa na kosa analoonekana kutenda kutokana na wadhifa wake huo.

Bw. Malima alisema iwapo mtumishi yeyote wa umma atatajwa na watuhumiwa walioko mahakamani kuwa alihusika katika makosa ya jinai, Serikali haitasita kumfikisha mahakamani

Hata hivyo utekelezaji wa mapendekezo hayo pamoja na yaliyohusu maofisa wengine ulikataliwa na Bunge na kuiagiza Serikali kuwasilisha upya utekelezaji mwingine wa maazimio yake katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanzia Oktoba 27, mwaka huu siku tisa kabla ya Bw. Mwanyika kustaafu.

Source: Majira 06 October 2009
Mwandishi: Reuben Kagaruki


Bill
JF Senior Expert Member
Points: 196,715, Level: 100 Points: 196,715, Level: 100 Points: 196,715, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
Join Date: Fri Oct 2007
Posts: 628
Thanks: 32
Thanked 30 Times in 19 Posts
Views: 1693
Reply With Quote
  #41  
Old 9th October 2009, 11:16 AM
EMMANUEL SHOMBE EMMANUEL SHOMBE is offline
EMMANUEL SHOMBE Chapa ya ng`ombe
Senior Member
Points: 57,101, Level: 100 Points: 57,101, Level: 100 Points: 57,101, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Fri Oct 2009
Posts: 85
Thanks: 0
Thanked 5 Times in 4 Posts
Rep Power: 21
EMMANUEL SHOMBE will become famous soon enoughEMMANUEL SHOMBE will become famous soon enoughEMMANUEL SHOMBE will become famous soon enoughEMMANUEL SHOMBE will become famous soon enoughEMMANUEL SHOMBE will become famous soon enoughEMMANUEL SHOMBE will become famous soon enoughEMMANUEL SHOMBE will become famous soon enoughEMMANUEL SHOMBE will become famous soon enough
Default Re: Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka

Afunguliwe kesi ya kutokuwajibika katika nafasi yake. kabla ya kustaafu
Reply With Quote
  #42  
Old 9th October 2009, 11:31 AM
Shishye's Avatar
Shishye Shishye is offline
Shishye has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 72,974, Level: 100 Points: 72,974, Level: 100 Points: 72,974, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Thu Feb 2009
Location: On earth
Posts: 258
Thanks: 0
Thanked 42 Times in 22 Posts
Rep Power: 22
Shishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enough
Default Re: Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka

Quote:
View Post
Kila la heri J. Mwanyika!!! Ukweli ninao ufahamu jamaa hakuwa na raha kabisa na huo wadhifa (from reliable sources). Cheo kile kinakulazimisha kufanya uproffessional decissions!!!! Hakupenda!!! Believe it or not. Ni kwa muda mrefu alitaka ajiuzulu!!! Ingeleta mtikisiko!!!
Kumbe sisi wenyewe ndio tunawapalilia mafisadi halafu baadae tunakuja kujilaumu. Kama ulichosema ni kweli basi tutakuwa hatuna sababu ya kumtaka Kikwete na serikali yake kuwa wasafi. Mie nimechoka kabisa.

Kila mtu kwenye nafasi yake ajue kwamba halazimishwi kufanya kitu chochote asichokubaliana nacho. Kuna taratibu za kupinga na kupiga kelele, kujiuzulu ni hatua ya mwisho kbisa. Tusidanganyane eti nchi ingetingishika! Kama kweli ingetingishika basi wangekubaliana na uamuzi wako, kwa nini wewe ndio ukubaliane na uamuzi wao?? Lol!
__________________
"Chunguza Mjomba, Utabaini!"
Reply With Quote
  #43  
Old 9th October 2009, 11:48 AM
Mtu B Mtu B is offline
Mtu B has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 115,656, Level: 100 Points: 115,656, Level: 100 Points: 115,656, Level: 100
Activity: 7% Activity: 7% Activity: 7%
 
Join Date: Tue Dec 2008
Posts: 455
Thanks: 43
Thanked 147 Times in 87 Posts
Rep Power: 22
Mtu B will become famous soon enoughMtu B will become famous soon enoughMtu B will become famous soon enoughMtu B will become famous soon enoughMtu B will become famous soon enoughMtu B will become famous soon enoughMtu B will become famous soon enoughMtu B will become famous soon enough
Default Re: Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka

Hayatabiriki. Tuliyaona kwa Gray Mgonja: alistaafu, yakafuata mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka. Tuliyaona hapo kabla kwa Omar Mahita: alistaafu, yuko nyumbani kwake analima mboga, hakuna anayemsumbua. Tuliyaona pia kwa Ben Mkapa: alistaafu, tukaambiwa 'mwacheni mzee wa watu apumzike'. Nchi yetu hii hii.
Reply With Quote
  #44  
Old 9th October 2009, 12:26 PM
Shishye's Avatar
Shishye Shishye is offline
Shishye has no status.
JF Senior Expert Member
Points: 72,974, Level: 100 Points: 72,974, Level: 100 Points: 72,974, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Thu Feb 2009
Location: On earth
Posts: 258
Thanks: 0
Thanked 42 Times in 22 Posts
Rep Power: 22
Shishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enoughShishye will become famous soon enough
Default Re: Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka

Bora waachwe wapumzike kama baba lao kuliko kusumbua fedha zaidi kuchezesha video za kina Mgonja zisizokuwa na tija. Wote wezi tu, hakuna mwenye uwezo, dhamira wala nia ya dhati ya kumwajibisha mwenzake.
__________________
"Chunguza Mjomba, Utabaini!"
Reply With Quote
  #45  
Old 11th October 2009, 04:44 PM
JokaKuu JokaKuu is offline
JokaKuu has no status.
JF Premium Member
Points: 967,820, Level: 100 Points: 967,820, Level: 100 Points: 967,820, Level: 100
Activity: 14% Activity: 14% Activity: 14%
 
Join Date: Mon Jul 2006
Posts: 3,389
Thanks: 298
Thanked 432 Times in 244 Posts
Rep Power: 111
JokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of lightJokaKuu is a glorious beacon of light
Default Re: Kikwete amkubalia Mwanyika kung'oka

..Mwanyika,Mwakapugi,na Mrindoko, walikuwa wanatekeleza amri za wakubwa zao tu.

..hata Dr.Mwakyembe analielewa hilo na ndiyo maana akasema kuna mambo ambayo Kamati yake iliamua yasiwekwe ktk ripoti ili serikali isiaibike.
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
amkubalia, kikwete, kungoka, mwanyika


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
Nidhamu ya Chama: Kiini cha Kudorora Viongozi wa CCM! Mzee Mwanakijiji Jukwaa la Siasa 94 13th May 2009 01:45 AM
Urithi wa Kikwete na haiba iso sababu Pundit Jukwaa la Siasa 25 27th December 2008 07:42 AM
Miaka miwili Kikwete Ikulu, tumaini lililopotea Bubu Ataka Kusema Jukwaa la Siasa 2 16th December 2007 10:40 PM
Kikwete Relieved As Mkapa Opts Out Nyamgluu Habari na Hoja mchanganyiko 0 14th July 2006 06:43 AM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 12:43 PM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com