Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuna Usanii Kwenye Bajeti ya Elimu?

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 21
    1. #1
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default Kuna Usanii Kwenye Bajeti ya Elimu?

      Hotuba ya Waziri wa Fedha Bungeni (iko kwenye tovuti ya taifa yaani http://www.tanzania.go.tz) inaonyesha kwamba serikali imetenga shilingi trilioni 1.0861 kwa ajili ya sekta ya Elimu, kwa kipindi cha 2007/08.

      Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na Ufundi inaonekana kwenye hiyo sehemu ya tovuti ya taifa vile vile, na inaonyesha kwamba kwa mwaka 2007/08, fedha zilizotengwa kwa ajili ya wizara hiyo ni
      sh. 265,679,865,700 (shilingi bilioni 265.68).

      Hotuba ya Wizara ya Sayansi na Elimu ya Juu haionekani kwenye hiyo tovuti ya taifa. Hata hivyo, ukiondoa fedha zilizotengewa Wizara ya Mama Sitta kweny hizo 1.0861 tr/- za Elimu, utakuta zinabaki
      sh. 820,320,134,300 (shilingi bilioni 820.32). Kwa vile ziko Wizara mbili tu za Elimu, ina maanisha Wizara ya Waziri Msola imetengewa 820.32 bn/- ? Hizi ni 308.76% zaidi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Mama Sitta! Naamnini kuna udanganyifu hapa.

      Ifahamike vile vile kwamba ukilinganisha Bajeti ya Mama Sitta ya mwaka jana na hii ya sasa, utaona fedha zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida zimeongezeka kwa 16% (toka 133,964,077,900/- hadi 155,447,119,000) wakati fedha za matumizi ya maendeleo zimeongezeka kwa 4% tu (toka 105,686,632,100/- hadi 110,232,746,700/-).

      Serikali ambayo kila siku inasema inakazania Elimu itaongezaje fedha za matumizi ya maendeleo za Wizara ya Elimu na Ufundi kwa asilimia 4 tu? Tunajidanganya wenyewe. Tunaficha ugonjwa tulionao wa kuinyima Elimu fedha, lakini tukumbuke Waswahili husema "Anayeficha ugonjwa, kifo kitamsema".

      Augustine Moshi
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.


    2. #2
      Kichuguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th October 2006
      Location : Popote Porini
      Posts : 6,857
      Rep Power : 3280
      Likes Received
      1342
      Likes Given
      930

      Default

      Mwalimu Moshi,

      Nilivyoangalia bajeti ya Mama Sita kwa mwaka huu ambayo ilikuwa TShs 265,679m ikiwa na matumizi ya kawaida ya TSh 155,447m; niliona kabisa kuwa kulikuwa na degradation ya quality ya elimu kwa kiwangi cha kukithiri iwapo ni kweli kuwa idadi ya shule za sekondari na idadi ya wanafunzi imeongezekawa kwa asilimia 65% kama aliyosema Waziri Mkuu. Degradation ya elimu ya sekondari kutoka 2005 kwenda 2006 ilikuwa ni zaidi ya 63%; kwa mwaka huu nina wasiwasi kuwa degradation hiyo itakuwa ni zaidi ya 300% kwa vile bajeti nzima ya wizara haitoshi kukidhi mahitaji ya sekondari kwa viwango vya mwaka jana baada ya ongezeko la sekondari kwa kiwango cha 65%.
      Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

    3. #3
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default

      Kichuguu,

      Kipimo ulicholeta cha degradation naona ni kizuri sana. So, we are degrading Education while lying to the masses that we are improving it!

      Tukumbuke vile vile kuweka kasi ya mfumuko wa bei kwenye haya matumizi. Umeanza mchezo wa kuficha hizi takwimu: ukiangalia Monthly Economic Review for June 2007 kwenye site ya BoT utaona wamefanya jitihada za KUFICHA hiyo takwimu. Hawasemi rate ya inflation ilikuwa kiasi gani June 2007. Wanaogopa ule uwazi alioacha Mkapa.

      Kasi ya mfumuko wa bei ni zaidi ya hilo ongezeko la 4% la fungu la matumizi kwa ajili ya maendeleo. Kwa vile kasi ya mfumuko wa bei ni angalau 7% kwa mwaka, (it is almost certainly much more than that, as transportation costs alone have shote up by 50% recently), basi maana yake ni kwamba kuna SHRINKAGE ya 3% au zaidi kwenye hilo fungu.

      Augustine Moshi
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    4. #4
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default Maajabu ya Bajeti

      Hotuba za bajeti za Mawaziri Meghji, Sitta na Msolla zote zinapatikana kwenye webiste ya serikali sasa. Hotuba ya Waziri Meghji inaonyesha kwamba Bunge limetenga sh. 1,086.1 billion kwa ajili ya Elimu, mwaka huu wa 2007/08.

      Ukijumlisha fedha zilizotengwa na Bunge kwa ajili ya Wizara ya Waziri Mama Sitta (sh. 265.6799 billion) na zile za Wizara ya Waziri Msolla (sh. 287.8758 billion), zinafika sh. 533.5557 billion. Hii inaacha baki la sh. 553.1443 billion toka fedha zote zilizotengwa na Waziri Meghji kwa ajili ya Elimu. Hizi zitakwenda wapi?

      Jumla ya fedha zilizotengwa na Bunge kwa ajili ya wizara zetu mbili za Elimu ni 9% ya Bajeti yote. Kwa nini serikali inadai kwamba imetengea Elimu 18% ya Bajeti yote?

      Kenya wanaendelea kutumia sehemu kubwa ya bajeti yao kwenye Elimu (zaidi ya 20% kila mwaka tangu baada ya Uhuruhadi leo). Mwaka huu wa fedha wametengea Elimu TSh.2.151 trillion. Hii ni mara nne ya fedha ambazo sisi tumetengea Elimu. Kenya wanatarajia kuajiri walimu wapya 11,000 mwaka huu wa 2007/08.

      Kwa nini sisi tunaendelea kufanya mzaha kwenye Elimu?

      Augustine Moshi
      Last edited by Augustine Moshi; 7th August 2007 at 10:21.
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    5. #5
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,102
      Rep Power : 1445
      Likes Received
      485
      Likes Given
      72

      Default

      Bwana Moshi,

      CCM wanataka kututawala maisha na wanajua kufanikiwa kwao kunategemea elimu duni kwa mwananchi. Ndiyo sababu washa anza kuwaingiza watoto wao kwenye siasa.
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)


    6. #6
      Katibu Tarafa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2007
      Posts : 1,201
      Rep Power : 871
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Labda mh Zitto anaweza kutusaidia juu ya hili.

    7. #7
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default

      Tatizo ni kwamba Watanzania wengi hawajali mambo ya msingi kama Elimu. Hata hapa JF, angali watu wanachangamkia majadiliano ya gossip kama "Mkapa ana share Kiwira" lakini Elimu wala hawataki kuzungumzia.

      JF Members: stop dwelling on gossip and engage in meaningful developmental dialogue. Kwani Mkapa akiwa na share Kiwira kuna mbaya gani? Au share zote zikichukuliwa na wageni ndiyo mtafurahi? Mnakuwa kama Waswahili wa vijiji vya Pangani ambako nimeona mtu akijenga nyumba nzuri wenzake wanamsema!

      Acheni kuchangamkia posts za kusema "fulani anatembea na fulani", na badala yake tuangalie chanzo cha nchi yetu kuendelea kuwa ya mwisho kimaendeleo Afrika Mashariki, na ya pili au tatu kutoka mwisho dunia nzima!

      Kwa sasa, naomba kama kuna anayefahamiana na Wabunge awaombe waulize ufafanuzi kuhusu udanganyifu uliofanywa na serikali kwenye bajeti ya Elimu.

      Augustine Moshi
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    8. #8
      Masanja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st August 2007
      Location : Benaco
      Posts : 1,647
      Rep Power : 941
      Likes Received
      159
      Likes Given
      0

      Default

      AM nadhani tumekosea kidogo, hivi tusipowapigia kelele akina Mkapa na wenzake wanaoiba hicho kidogo tulicho nacho, hiyo bajeti ya elimu itatoka wapi? wewe unataka tuongelee elimu wakati wanaoiba hela ambayo ingesupport elimu wamekaa kimya wakizidi kutuibia? Naomba unieleweshe. Na tukijadili elimu bila kujadili chanzo cha haya matatizo mwisho wake ni nini?

      Ukiuliza kwa nini elimu haipewi kipaumbele utaambiwa serikali haina pesa! na pesa zimekwenda wapi? ndo hapa JF wata wanapiga kelele, Na ninaamini wahusika wanapata ujumbe! Mkapa kuwa na hisa Kiwira siyo shida, shida ni pale anapotumia madaraka yake, kutuingiza kwenye mikataba feki. Kama kweli kuna wizi wa jamii ya IPTL, basi hatuna budi kupiga kelele na hawa wezi.

      Otherwise point zako ni safi na utafiti wako, lakini bila kupiga kelele na hawa jamaa we cant get get money to finance our priorities!

    9. #9
      Field Marshall ES's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 27th April 2006
      Posts : 13,740
      Rep Power : 0
      Likes Received
      329
      Likes Given
      208

      Default

      Quotes:

      "JF Members: stop dwelling on gossip and engage in meaningful developmental dialogue. Kwani Mkapa akiwa na share Kiwira kuna mbaya gani? Au share zote zikichukuliwa na wageni ndiyo mtafurahi?"

      Mzee Moshi,

      With all due respect mkuu, kweli akutukanaye hakuchagulii tusi, kwa nini unaamini kuwa engaging in a meaningful development dialoque, lazima iwe kama unavyofikiri wewe yaani on elimu? na isiwe gossip za share za Mkapa kiwira, ambazo through my definition ya engagement on meaningful development dialoque ninaweza kuishia ku-establish legally, kuwa source yake ni Mkapa kuiba hela zetu za taifa kwenye sekta ya elimu?

      Na kwamba asingeziiba, taifa letu lingesogea kidogo kwa kuwalipia elimu ya juu wananfunzi wetu kule Ukraine, ambao sasa hivi wamekwama na kushindwa kuendelea na elimu hiyo, ambayo wangerudi na kuitumia katika kulisogeza mbele japo kidogo taifa letu?

      Share zote hazichukuliwi na wageni, kwa sababu as a nation tume-establish kwa kuzigawanya kisheria share zinazopaswa kuwa za wageni na za wazawa, katika any-investment ndani ya nchi yetu, ambayo pia tumesema kisheria kuwa ni lazima iwe joint between wazawa na wageni.

      Mkapa kuwa na share Kiwira, hakuna mbaya! Yes ila the mbaya comes, amepata wapi hela za kununua hizo share, hoja ambayo ni lazima iwe established, kwanza through gossip za our prominent papers Kulikoni/Thisday, halafu baadaye sisi JF, kabla ya kuchukua polls za public opinion on the ishu, na ku-move on mahakamani.

      Tukiwa tunafuatilia tu mifano ya waliotuzidi kimaendeleo, ambao kwao Monica Lewinsky case ilianza kama sisi na hii Kiwira share, as a gossip, baadaye ikaishia kumhukumu na kumu-impeach the then most powerful man on the earth, President Clinton,

      Sasa Mzee Moshi, what part of gossip on Mkapa's Kiwira shares you do not understand kuwa ni healthy discussion for our nation, ndio maana ikaripotiwa na the most trusted papers on our Tanzania's soil, Kulikoni and Thisday? How about you for once showing some respect for the JF members, kwamba we know what is good gossip like this Kiwira's thing, and a bad gossip like kujitenga majimbo?

      Ahsante Mkuu

    10. #10
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default

      Komandoo ES,

      Salamu sana!

      Unauliza "Mkapa amepata wapi fedha za kununua hisa Kiwira?" Kwa nini asiwe nazo? Mshahara na marupurupu ya Rais ya miaka 10 pamoja na mishahara na marupurupu aliyokuwa nayo miaka mingine kama 30 ya Uwaziri, Ubalozi, etc., havitoshi kumpa vimilioni vichache vya kununua hisa Kiwira? Mimi nadhani angeweza hata kununua Kiwira yote, kihalali kabisa.

      Komandoo ES hujanunua share za Breweries, Twiga Cement au CRDB? Kama hujafanya hivyo una makosa makubwa sana! Fedha unakula tu?

      Unasema sheria zetu zinataka mwekezaji lazima awe na ubia na wenyeji. Mbona kwenye madini si hivyo?

      Naona wengine wanampakazia Mkapa mambo ya IPTL! Wanasahau kwamba Mkataba wa IPTL ulisainiwa wakati Rais ni Mwinyi na Waziri wa Nishati ni Jakaya Kikwete? Mkapa aliupiga vita huo mkataba kandamizi hadi mahakamani London? Mnasahau upesi mno!

      Kama nilivyosema, vipo vijiji Uswahilini ambapo hakuna mtu anathubutu kujenga nyumba ya bati. Ukijenga wanauliza fedha amepata wapi? Ni kama mnavyouliza hapa: Mkapa atapataje fedha za kununua share za Kiwira? Hii ni kukumbatia umaskini.

      Kila anayeweza kuweka pembeni vimilioni vichache anashauriwa kununua share Kiwira na kwingineko. Mkapa ameonyesha mfano mzuri.

      Kama kuna ushahidi kaiba, basi huo ndio tuujadili. La hakuna ushahidi wakuvunja sheria, basi tumpongeze kwa kununua share.

      Augustine Moshi
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    11. #11
      Choveki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2006
      Posts : 477
      Rep Power : 770
      Likes Received
      88
      Likes Given
      163

      Default

      Mwl Moshi nimefurahi "kukuona"

      Hii analysis yako nimeipenda na ahsante kwa hi post. Kuna post moja nilisema kuwa watanzania tujuacho ni blah! blah! Na nadhani hata wewe umeshafahamu hivyo tangia kule...bcs..etc.

      Hizi hesabu za bajeti inabidi mtu ukae chini ufikiri, na utafakari; kutokana na elimu duni tuliyopatiwa tangia wakati wa UPE hadi leo hii madhara yake ndo haya unayoyaona humu...vichwa vyetu ni vizito mno kufikiri na ku analyze vitu vya msingi kama hivyo. Tunachopenda ni gumzo na mzaha tu, ndo maana maswali ya dini tunachangia sana kwani pale hakuna kufikiri ni kuangalia majina tu ya viongozi na ku assume ni mkristo au mwislam.

      Pia inabidi tuwe makini ili hii topiki isije ikabadilika na kuwa kama zingine, yaani tukahamia kwenye mengineyo, badala ya bajeti ya elimu.
      -------choveki

    12. #12
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,102
      Rep Power : 1445
      Likes Received
      485
      Likes Given
      72

      Default Moshi, nakubaliana na wewe!!

      Tatizo la bajeti ndongo kwenye elimu ilianza tangu enzi za JKN. Ingawa watu tulisoma lakini shida na msoto tuliupata kisawasawa kwa kula dona na maharage yaliyooza kama wafungwa na bado tuliridhika na kukata shule.

      Siasa za CCM hazijazingatia elimu toka zamani ila kwa wale tu wachache walioweza kuendelea. Kwa kuwa bajeti sasa imeingezeka kwenye elimu may be tujaribu kuwapa walau hongera hawa jamaa ingawa sidhani kama wanastahili. May be tatizo la hiyo bajeti kutokubalance inawezekana ndiyo hilo ni fungu la safari na entertainment za wazee wenyewe.

      Si umesikia billion kibao zimeshatengwa kwa ajili ya safari? Nisikilizie JK karibu ataanza tena kupiga trip zake. Alitulia kidogo kwa vile fungu liliisha na akaoverspend. This year ndiyo sababu vote ya safari imeongezewa pesa. Sasa imagine hizo pesa zingelekwa elimu zingesaidia kwa kiasi gani??? But who cares???

      My conclusions ni kwamba CCM hawana nia ya kuinvest kwenye elimu na ndiyo sababu TZ ni ya mwisho kwa elimu in Eastern and Central Africa. Elimu yetu ni ya kusoma na kuandika tu!!!!!!
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)

    13. #13
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,915
      Rep Power : 2990
      Likes Received
      2548
      Likes Given
      3634

      Default

      Dr.Moshi,
      1.Mimi nadhani watu hawakuchangia mada hii kwasababu uliweka kila kitu clear na wengine hatukuwa na cha kuongeza.

      2.Suala la Elimu na umakini wa serikali vilizungumziwa kwa kirefu katika mada, "Majibu ya Mwanakijiji kwa Waziri Mkuu."

      Mr.Zero,
      Wizara ya Mambo ya Nje imeomba toka Bungeni sh Billioni 8 kwa ajili ya gharama za safari za viongozi wakuu-Raisi,VP,na PM.

    14. #14
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default

      Choveki anasema Watanzania tu wavivu wa kufikiria. Hata hivyo, hakuna dalili za kuonyesha wale wanaopanga mipango ya kuchota fedha za walalahoi wana uvivu.

      Mr. Zero: Ni kweli kuwa kuinyima Elimu fedha kulianza tangu awamu ya kwanza. Tulipata Uhuru tukiwa na bajeti ya Elimu ambayo ilikuwa 20% ya bajeti yote. Ikaanza kupungua, na kufika miaka ya 80, bajeti ya Elimu ilikuwa 5% ya bajeti yote. Leo ni 9%. Inatajwa kuwa ni 18%, lakni wizara zetu mbili za Elimu zimetengwa, kwa pamoja, 9% tu ya bajeti yote.

      Inashtusha unaposema huko kutobalance bajeti labda ni wazee wamejiwekea fedha kidogo. Tofauti iliyopo ni zaidi ya shilingi bilioni 500. Ni kiasi kinachokaribia kabisa bajeti yote ya Elimu.

      Huu mfumo wa Bunge kutenga kiasi fulani cha fedha kwenye sekta na wizara zinazohusika kutengewa chini ya hicho kiasi naona unahusu wizara nyingi. Kwa mfano, Waziri wa Fedha aliliomba Bunge litenge sh. 777.2 billion kwa ajili ya BARABARA peke yake. Hilo lilipitishwa. Lakini Bunge hilo hilo limeidhinisha jumla ya sh. 687.0 billion kwa ajili ya WIZARA NZIMA ya Miundombinu!

      Tuwaeleweje?

      Augustine Moshi
      ============================
      Naweka hapa chini dondoo kutoka ukurasa wa 36 wa hotuba ya bajeti nya Waziri Meghji. Inaonyesha fedha zilizotengewa sekta muhimu. Linganisha na fedha zilizotolewa kwenye wizara za hizo sekta (angali hotuba za bajeti kwenye national website) ili uone tofauti zilivyo kubwa.

      (1) Education Shillings 1,086.1 billion (1.086 trillion) equal to
      18 percent of the budget,

      (2) Roads, Shillings 777.2 billion
      equal to 12.8 percent of the budget,

      (3) Health, Shillings 589.9 billion
      equal to 10.0 percent of the
      budget,

      (4) Agriculture, Shillings 379
      billion equal to 6.2 percent of
      the budget, and

      (5) Water Shillings 309.1 billion
      equal to 5.1 percent of the
      budget.
      Last edited by Augustine Moshi; 9th August 2007 at 07:33.
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    15. #15
      Nungunungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th February 2007
      Posts : 314
      Rep Power : 694
      Likes Received
      8
      Likes Given
      0

      Default

      Augustine Moshi,

      Unaweza kujenga hoja zako vema na kueleweka bila ya kuja na utetezi wa Mkapa.

      Tuliomo humu tuna uwezo wa kupima mambo - Mkapa ana mazuri yake na mapungufu pia. Kipi kimezidi kingine ni suala la mjadala.

      Kifupi kwa sasa Mtazania wa kawaida anachohitaji ni unafuu wa maisha na hilo haliletwi na takwimu za uchumi ambazo umekuwa ukizileta humu mara kwa mara kama sehemu ya utetezi wako kwa Mkapa.

      Otherwise mjadala na uendelee!

    16. #16
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default

      Quote By Nungunungu View Post
      Augustine Moshi,

      Kifupi kwa sasa Mtazania wa kawaida anachohitaji ni unafuu wa maisha na hilo haliletwi na takwimu za uchumi ambazo umekuwa ukizileta humu

      Otherwise mjadala na uendelee!
      Mimi siposti "unafuu wa maisha humu". Natoa maoni. Na nikitoa bila takwimu kuna mnaosema mbona hakuna data? Nimeweka data na matoke yake unasema "data hazileti unafuu wa maisha". I can't win, can I?

      Kama kuna mtu anatafuta unafuu wa maisha humu, basi atasubiri sana. Huku uingie kupata mawazo tu, na baada ya hapo ukahangaike ili upata unafuu wa maisha.

      Augustine Moshi
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    17. #17
      Nungunungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th February 2007
      Posts : 314
      Rep Power : 694
      Likes Received
      8
      Likes Given
      0

      Default

      Ni mwenye matatizo ya akili tu ndiye anayeweza kuja humu ili apate unafuu wa maisha - nami si katika hao.
      Neno forum linajitosheleza kujua tupo hapa kwa ajili gani.

      Husemwa mara kadhaa kuw JF inawasemea raia wa kawaida ambao wengi wao hawana hata uwezo wa kuingia humu.

      Any way kwakuwa sentensi zangu za mwanzo umezielewa, I can drop the rest!

    18. #18
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default

      Jamani jamani niazidi kumtetea baba wa Taifa mwl. JKN tena kwa mara ya kumi ktk kila mada inayohusu takwimu.. naomba mtu yeyote mweny takwimu za kabla ya Uhuru na wakati Nyerere akiwa madarakani!... maanake naona kila siku uzushi mpya huzaliwa hata baada ya kusawazisha.

      Muhimu tuyazungumze ya leo lakini mnapokuja na hizi habari za Nyerere kuwa watu sijui walisoma kwa kadi za TANU ama CCM mara sijui makanisa ni habari za uzudhi mtupu na naomba data zinazothibitisha habari hizi.

      Mchango wangu kwa leo ni kipande hiki cha Elimu nchini toka mwaka 1994 hadi 2004..Jaribuni kutazama onegezo la wanafunzi vs walimu..
      http://www.tanzania.go.tz/haliyauchu...nne/jed83.html

      Kisha chukua wanafunzi walioanza darasa la kwanza mwaka 1994 ambao ni laki 674 baada ya miaka saba 2001 utaoona kuwa walifikia darasa la saba ni laki 470 .. laki 2 nzima wamelala!
      Haya tazama basi mwaka uliofuata 2002 hesabu ya wanafunzi waliojiunga na sekondary kidato cha kwanza ni elfu 56101 kati ya wanafunzi wangapi?... Mtaona kuwa ni asilimia kama 10 naa!. Haya tazama hesabu ya shule zetu ndio utakoma kabisa hakuna uuwiano hata kidogo!..
      Kweli mahesabu haya yanaingia akilini ama ni vichekesho tu! Kisha wanajivuna sana na bajeti zetu kuwa elimu imepewa kipaumbele....since when?
      Nina hakika hesabu hii bado inaendelea hapo hatujagusa vyuo vikuu!..
      Exploration of reality

    19. #19
      Augustine Moshi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2006
      Posts : 1,832
      Rep Power : 1853
      Likes Received
      184
      Likes Given
      85

      Default

      Mkandara mbona umeweka takwimu ambazo hazieleweki hata kidogo?

      Unasema, and I quote: "Wanafunzi walioanza darasa la kwanza mwaka 1994 ambao ni laki 674 baada ya miaka saba 2001 utaoona kuwa walifikia darasa la saba ni laki 470 .. laki 2 nzima wamelala!"

      Unaposema laki 674 unaelwa maana yake? Unataka kusema 674,000? Hiyo ni laki sita na sabini na nne elfu. Ulitaka takwimu ipi hasa? Na waliofika darasa la saba baada ya miaka saba ni 470,000? Hiyo SIO laki 470. Ni laki nne na sabini elfu

      Unajua kila laki 10 ni milioni moja? Kwa hiyo laki 470 ni milioni 47.

      Unaendelea kuandika: "Mwaka uliofuata 2002 hesabu ya wanafunzi waliojiunga na sekondary kidato cha kwanza ni elfu 56101"

      Bila shaka ulitaka kusema 56,101. Badala yake umesema ELFU 56101 ambayo 56,101,000.

      Naomba tutumie takwimu vizuri ili tuelewane.

      Augustine Moshi
      Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

    20. #20
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default

      Mzee wangu samahani ni lugha ya uandishi ambayo nimeitumia na kama imekupotosha basi naomba radhi lakini nilichojaribu kusema ndivyo ulivyoandika nikichukulia laki ni sifuri tatu. Kiswahili safi nadhani nilitakiwa kuandika 56 elfu mia....blaa blaa blaaa!, sawa ndio kujifunza kwenyewe huku mwalimu darasa safi! Unajuua tena uandishi ulinipita kando na sii mara ya kwanza kupewa zero!
      Muhimu nimeiweka hiyo site yenye Takwimu, usije nipa zero!
      Exploration of reality

    Page 1 of 2 12 LastLast

    Similar Topics

    1. Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, hii sasa ni usanii kama serikali ya kikwete
      By zomanyakahu in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 2
      Last Post: 24th October 2011, 06:54
    2. Hivi wanawake wanapolia kwa machozi kuna ukweli au usanii?
      By Excellent in forum Mahusiano, mapenzi, urafiki
      Replies: 16
      Last Post: 20th May 2011, 16:37
    3. Usanii Elimu ya juu.
      By KakaJambazi in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 2
      Last Post: 8th March 2011, 13:10
    4. Nina wasiwasi na wataalamu tulionao kwenye wizara ya Elimu kuhusu Elimu zao
      By kabila01 in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 5
      Last Post: 3rd June 2009, 17:31
    5. Bajeti ya Elimu
      By Augustine Moshi in forum Jukwaa la Elimu (Education Forum)
      Replies: 13
      Last Post: 2nd June 2007, 04:58

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...