Kaka tafadhali weka kwanza kusudi la kunielewa, vinginevyo hata nikiongea mwaka mzima kama umedhamiria tu kubishana hakuna tunachoweza kuongea.
Kiwanda cha Mbolea kilichoahidiwa, malighafi ni ya kutengenezea mbolea ni mabaki ya uchafu unaotokana na shughuli ya gesi. Kama gesi haijachimbwa bado, kiwanda kitazalisha mbolea kutumia hewa? Hapa utaona kwamba, ni mpaka gesi izalishwe ndio mbolea itapatikana, AU?
Twende kwenye hili la umeme. Tata
Mwita Maranya, naomba ujiulize mwenyewe, ikiwa wewe ndio kiongozi wa nchi hii, utafanya nini kwanza kati ya haya:
1. Kujenga mtambo wa umeme kwa ajili ya Dar es Salaam ambayo ina uhaba wa umeme na mahitaji ni makubwa, au kujenga mtambo Lindi na Mtwara ambapo hata uliopo hautumiki wote? (Hata hivi sasa, Mtwara kuna uzalishaji wa 11MW ambapo ni 5MW tu ndio zinatumika) sasa mnataka ufahari wa kwamba kuna zingine 306MW hazitumiki au ni nini?
2. Unaweza kuniambia Mtwara kama Mtwara inanufaika nini na ujenzi wa njia ya umeme unaoenda Singida ikizingatiwa hakuna mkoa unaolipwa fedha kwa kuwa mkoa huo kuna power station au power lines zimepita?
Mwita Maranya, gesi matumizi yake si umeme tu. Gesi lazima ifike Dar es Salaam liliko soko kubwa. Hebu jenga picha ni akili gani itakuwa imetumika, kuleta bomba Dar kwa ajili ya kusupply gesi viwandani, majumbani na kwenye magari, halafu wewe huyo huyo ujenge tena njia ya umeme toka Mtwara hadi Dar kuuingiza kwenye Grid ya Taifa!!!
Maneno yako ya kumalizia ya No more, no less hayaambatani na logistic reasoning ni ushabiki na si zaidi.
Tusipende kuwa washabiki ndugu zangu. Acha nikwambie kitu. Amin Dangote (yule Mnigeria tajiri mkubwa kuliko wote Africa) anaplan kujenga kiwanda cha Cement Mtwara. Mawazo ya kujenga kiwanda yanakuja kwa kuwa tu anajua atapata malighafi ya kutengenezea cement kutokana na machimbo na uchakataji wa gesi. Hapa utasikia wengine wanasema tumeahidiwa kiwanda mbona hakijengwi, jibu linakuja pale pale, cement atazalisha kwa mabaki ya gesi. Sasa nyie mnatakaje?
Follow Us Here