JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

  Report Post
  Page 7 of 8 FirstFirst ... 5678 LastLast
  Results 121 to 140 of 156
  1. nngu007's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd August 2010
   Posts : 15,931
   Rep Power : 840916
   Likes Received
   5660
   Likes Given
   614

   Default Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


   Telephone: 255-22-2114512,2116898
   E-mail:
   [email protected] / [email protected]
   Fax: 255-22-2113425
   PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE,
   P.O. BOX 9120,DAR ES SALAAM
   Tanzania


   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

   RAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Francois Hollande.

   Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulayakwa ajili ya ziara hiyo.

   Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles DeGaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride nakupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa, Mheshimiwa Paschal Canfin.

   Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko Private Fund na baadaye atakutana na Mama Marie Christine Saragosse, Mtendaji Mkuu wa Redio France International (RFI).

   Mkutano huo utafuatiwa na kikao kati ya Rais Kikwete na Jumuiya yaWatanzania wanaoishi nchini Ufaransa.

   Keshokutwa, Jumatatu, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Francois Hollande, Rais wa Ufaransa kwenye Kasri ya nchi hiyo ya Elysee Palace.

   Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Hollande yatafuatiwana chakula cha mchana ambako Rais Kikwete atakaribishwa na Waziriwa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mheshimiwa Laurent Fabius. Baada ya chakula hicho cha mchana, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na Bwana Yves Louis Darricarere, Rais wa Kampuni ya Mafuta yaKimataifa ya Total.

   Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mazungumzo mengine kati yaRais Kikwete na Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani H.H TheAga Khan na baada ya hapo, Rais Kikwete atakwenda Kasri la Luxemburg kukutana na kuzungumza na Rais wa Bunge la Seneti la Ufaransa, Mheshimiwa Jean Pierre Bel.

   Usiku wa Jumatatu, RaisKikwete atakula chakula cha usiku naRais wa zamani wa Ufaransa, Mheshimiwa Valery Giscard d’Estaingambaye ni Mwenyekiti waTanzania Wildlife Conservation Foundation. Jumanne, Rais Kikwete atakuwa na siku nyingine yenye shughuli nyingi ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana nakufanya mazungumzo na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zaokatika Ufaransa, na atakutana na Mheshimiwa Abdou Diouf, KatibuMkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Nchi Zinazongumza Lugha yaKifaransa na Rais wa zamani wa Senegal.

   Rais Kikwete pia atashiriki majadiliano kuhusu masuala yakimataifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa yaUfaransa – Institute Francais Des Relations International (IFRI) naatakutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Ufaransa (AFD).

   Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea Makao Makuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich na baadaye kwenda Davoskuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Uchumi Duniani – World Economic Forum (WEF).

   Imetolewa na:
   Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
   Ikulu
   Dar es Salaam.
   19 Januari, 2013
   Quote By Dingswayo View Post


   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, kesho Rais Jakaya Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na MAMA FRANNIE LEAUTIERA,anayetajwa kuwa ni Mtendaji Mkuu wa MFUKO PRIVATE FUND.

   Nimejaribu kufanya utafiti mtandaoni lakini jina la karibu linaloshabihiana na la mwanamama huyo ni FRANNIE LEAUTIER (pichani juu)

   Lakini jitihada zangu za kutafuta MFUKO PRIVATE FUND (taasisi ambayo taarifa hiyo ya Ikulu inaeleza kuwa Mama Leautiera ni Mtendaji Mkuu) hazijazaa matunda.

   Je, Ikulu walimaanisha Frannie Leautier lakini wakaongeza herufi 'A' kimakosa, hivyo kusomeka LEAUTIERA badala ya LEAUTIER?

   Tukiamini hilo ni kosa dogo tu la kiuandishi, je MFUKO PRIVATE FUND ni taasisi gani? Na kwanini Rais akutane na Mtendaji Mkuu wake?

   Unaweza kudhani maswali haya hayana umuhimu lakini kwa vile taarifa zimeshasambaa duniani kuwa tuna utajiri 'mpya' wa gesi, basi ni vema kufahamu viongozi wetu wanakutana na watu wa aina gani wanapokuwa ziarani huko nje.

   Kama mnavyojua, kabla na wakati wa ukoloni akina Karl Peters walipita huko na kule kusaini mikataba ya kilaghai ya kuchukua ardhi na raslimali zetu. Siku hizi, baadhi ya viongozi wa Afrika ndio wamegeuka akina Karl Peters kwa aidha kukaribisha 'wakoloni wapya' au kuwafuata huko makwao kusaini mikataba ya kuuza nchi yetu.

   Ni matarajio yangu kuwa Ikulu itajitahidi kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili.

   Mama Frannie Leautiera Atakayekutana na Kikwete Ufaransa ni Nani? Na MFUKO PRIVATE FUND ni nini? ~ Kulikoni Ughaibuni  2. Candid Scope's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th November 2010
   Posts : 11,856
   Rep Power : 366017343
   Likes Received
   6654
   Likes Given
   4629

   Default Re: RAIS KIKWETE KWENYE ZIARA ya KISERIKALI NCHINI UFARANSA

   Quote By THE BIG SHOW View Post
   kimpango wakee,na hizo safari za ajabu ajabu zisizo na tija wala maana yoyote kwetu sisi lazima zije zimtokee puani,waziri wa mambo ya nje anafanya nini??na sikun hizi anakuja na janja kwamba kaalikwa nani amwalike yeye??aliikwe ana nini??

   Na huko uswisw anakokwenda haendi kutembelea shirikisho la soka wala nini??anaenda kuzidi kuweka 10 percent za gsei yetu tuu,tulaani dhulma kama hizi
   Kama kaalikwa na Rais wa Ufaranza iweje apokelewe na mawaziri na kufanyiwa dhifa na mawaziri? Jambo la msingi hapa ni kampuni ya mafuta ya TOTAL vinginevyo ni mapambizo tu.

  3. nngu007's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd August 2010
   Posts : 15,931
   Rep Power : 840916
   Likes Received
   5660
   Likes Given
   614

   Default Re: RAIS KIKWETE KWENYE ZIARA ya KISERIKALI NCHINI UFARANSA

   Quote By chama View Post
   Alaa sasa mbona wewe ndiye unayejihami? mkuu nngu007 lugha za kishairi zinaeleweka ni tangu lini unaweka jema la mh. kikwete mpaka leo nishangae?

   Chama
   Gongo la mboto DSM
   Oh... Kwanini Unadhani siweki JEMA la RAIS KIKWETE? kukosoa chama cha CCM sio kuchukia UONGOZI; Asiyekubali kukosolewa ni DIKTETA unajua???

  4. Sibhonike's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 10th April 2011
   Posts : 155
   Rep Power : 573
   Likes Received
   14
   Likes Given
   6

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Mzee huyu kwa kukata mitaa?
   Wallah, hajambo!!
   Kila maandamano yanapotokea nchini mwake, yeye huwa safarini.
   Wonderful...

  5. chama's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th August 2010
   Posts : 8,010
   Rep Power : 94047022
   Likes Received
   2391
   Likes Given
   1476

   Default Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Quote By Candid Scope View Post
   Kama kaalikwa na Rais wa Ufaranza iweje apokelewe na mawaziri na kufanyiwa dhifa na mawaziri? Jambo la msingi hapa ni kampuni ya mafuta ya TOTAL vinginevyo ni mapambizo tu.
   Mkuu Ritz
   Hawa vijana wa Chadema wamekuwa kama machizi; ratiba inaonyesha wazi raisi atakutana na raisi wa ufaransa Hollande; bado wanahoji vitu ambavyo mtoto mdogo hawezi kuhoji; kila nchi ina utaratibu wake wa kupokea viongozi; kuna tatizo gani akikutana na mkuu wa Total? Acheni siasa za fitina na majungu viongozi wa mataifa mawili watakutana kujadili mustakabali wa mataifa yao; ziara haikuzuka jana hana sababu ya kuambiwa kakimbia mgogoro kwanza ni mgogoro upi? Nyie endeleeni na ziara zenu za M4C ya majungu sisi tunapiga M4C ya kumuendeleza mtanzani.
   Chama
   Gongo la mboto DSM


   Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   "Nyumba ya kamanda wa vita haina msiba wala matanga"

   Chama
   Gongo la mboto "the town"
   Dar Es Salaam


  6. Mahebe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th February 2009
   Posts : 321
   Rep Power : 719
   Likes Received
   57
   Likes Given
   134

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Quote By Ranks View Post
   Mbona taarifa haijitoshelezi,haina list kamili ya alioandamana nao?
   Ni Prof.Sospeter Muhongo, Dr. John Magufuli na Bernard K Membe

   Bila kukosa mashushushu wake (ngumu kupata majina Yao)


  7. Ranks's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2012
   Posts : 1,443
   Rep Power : 750
   Likes Received
   219
   Likes Given
   715

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Quote By Mahebe View Post
   Ni Prof.Sospeter Muhongo, Dr. John Magufuli na Bernard K Membe Bila kukosa mashushushu wake (ngumu kupata majina Yao)
   anaelekea msafara ni mkubwa wa kuteketeza vijisenti vyetu hulu manufaa tunayopata kama taifa ni zero.

  8. Pady's Avatar
   Member Array
   Join Date : 13th January 2013
   Posts : 30
   Rep Power : 456
   Likes Received
   2
   Likes Given
   8

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Huyo anajiandaa pa kukimbilia coz kikinuka huyoooo Mama jk, Lizi 1 a.k.a 'mwizi 1' na yeye direct kwa kina PATRICE EVRA...

  9. kibugumo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th June 2011
   Location : arusha
   Posts : 1,106
   Rep Power : 1145
   Likes Received
   201
   Likes Given
   210

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Ni aibu anapokelewa na waziri wa misaada,Uswiss kuna nini?Mpaka amalize muda wake atakuwa amemaliza dunia nzima.

  10. Masanilo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd October 2007
   Location : Swat valley, Keta Keta
   Posts : 22,185
   Rep Power : 85897712
   Likes Received
   4159
   Likes Given
   2484

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Tafadhali asiache kupima afya ya akili akiwa huko.

  11. Bayyo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd April 2012
   Posts : 307
   Rep Power : 552
   Likes Received
   34
   Likes Given
   15

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Ziara ya ngapi mazee?

  12. matawi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th March 2010
   Posts : 2,026
   Rep Power : 1001
   Likes Received
   227
   Likes Given
   91

   Default Re: RAIS KIKWETE KWENYE ZIARA ya KISERIKALI NCHINI UFARANSA

   Quote By mdeki View Post
   Vasco da gama again? Sjui kwanini TZ ni maskiniSent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
   Mzee wa bakuli huyoooo, huwezi sikia kagame au kibaki akizungukazunguka ovyo kama huyu wetu

  13. MIGNON's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 23rd November 2009
   Posts : 1,498
   Rep Power : 974
   Likes Received
   541
   Likes Given
   439

   Default Re: RAIS KIKWETE KWENYE ZIARA ya KISERIKALI NCHINI UFARANSA

   Quote By afsa View Post
   Aibu gani hii watanzania tunayotwikwa ameshindwa kushughulikia sakata la mtwara huyoooooo kiguu na njia.
   Ni upepo,utapita kama yalivypita mengine.Zikimwagwa fulana na kofia za CCM,TOT wakikata mauno,hakuna tena kitu.

  14. Mthuya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th June 2011
   Posts : 1,273
   Rep Power : 787
   Likes Received
   163
   Likes Given
   7

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Wa Tanzania tunakazi kwelikweli

  15. #134
   FJM's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Posts : 8,099
   Rep Power : 82810706
   Likes Received
   6092
   Likes Given
   4766

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Quote By Ritz View Post
   Nyie Pro-Chadema JF mna vitu sana, rais asipo safiri mnasema kawekewa vikwanzo na UN kwa sababu ya kifo cha Mwangosi, akisafiri mnasema safari haina umuhimu.
   Ritz,

   Hata kwa viwango vyako, kweli ni inaingia akilini rais apande ndege kwenda kufanya mazungumzo na Radio ya kifaransa?

  16. BINARY NO's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th December 2011
   Posts : 1,345
   Rep Power : 773
   Likes Received
   450
   Likes Given
   73

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Ama kweli hii kali...Yani mwenyeji wake yupo lakini anaempkoea ni waziri wa MISAADA hii inaleta picha gani kwa Taifa? kuna nchi fulani walishawahi kum summon baloz wa inchi fulani baada ya rais wao kupokelewa kwa dharau kiasi hiki...Ebu angalia jinsi ratiba alizopangiwa za kukutana nazo hazina mbele wala nyuma zaidi ya kutuongezea ugumu wa maisha sisi walipa kodi...Kilichoniua zaidi ni kuruka hadi USWIS kwenda makao makuu ya FIFA yani hizo garama tu apo tunapata ZAHANATI MBILI AU TATU ZAKISASA...Nakitu kingine RAIS wetu hajawahi miss world economic forum je ajiulize hizo semina zote zimemuinua vipi kiulewa na akaja na idea zipi za kutekeleza? Na nini kazi ya FM wa TZ?????????

  17. Bukyanagandi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th June 2009
   Location : BLACKPOOL
   Posts : 3,974
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1780
   Likes Given
   2691

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Quote By Salary Slip View Post
   Labda anataka kuzuga kuwa anapunguza gharama.Sijui nafsi yake inamsuta?
   Mkuu hapo sifikili kama anazuga! Tuwe wakweli nia yake ni kupunguza gharama, no buts kwa hilo - kumbuka JK ana mamlaka hata ya kutumia jetfighter kumpeleka popote duniani, lakini mbona afanyi hivyo.

   Ninacho taka kusema hapa wakati mwingine tusiwe overly concern na mambo madogo madogo, taarifa kutoka IKULU inasema wazi wazi amekwenda huko kutokana na mwaliko wa Rais wa Ufaransa - sasa tatizo liko wapi, sisi hatujuhi wamepangiana vipi ratiba zao ambazo huwa zinawasilishwa well in advance na kukubaliana - ili la baadhi ya wana JF kusema JK amekuwa snubbed na Rais wa Ufaransa aliye toa mwaliko in the first place linashangaza sana!!

   Kwenye mambo ya teknolojia kuna kitu kinajulika kama counters, zinatumika sana kwenye mitambo inayo jiendesha yenyewe na kwenye komputa, sasa ukitaka sequence fulani ifanyike ndani ya sekunde 20 kwa mfano - una uhuru wa kuchagua i-count UP au DOWN i.e ianzie 0,1,2..20 au 20.19.18...0 either way muda unabaki ni ule ule yaani sekunde 20 bila ya kujali kama una-cout UP au DOWN - Nimetoa mfano huu kuonyesha kwamba hajalishi kama JK atakutana na Rais wa Ufaransa kwanza kabla ya kuonana na watu wengine muhumi au anakutana na Rais Ufaransa mwishoni baada ya kuonana/kukutana na maafisa wengine muhimu - end result zinabaki zile zile, alicho kusudia kukifanya huko atafanikisha bila ya kujali ameanzia juu au chini.

  18. j4marunda's Avatar
   Member Array
   Join Date : 6th November 2010
   Posts : 87
   Rep Power : 581
   Likes Received
   15
   Likes Given
   1

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Mwenyeji yaani Rais wa Ufaransa Francis Hollande huwezi kuacha kazi zake za kuwatumikia wananchi wa Ufaransa akampokee mtalii Airport! Wenzetu sio kama sisi hawawezi kuacha kufanya kazi za kitaifa wakahangaike na mtalii! Nadhani iko haja Watanzania tukawa makini hasa wakati wa mchakato wa kuchagua viongozi kwani mambo haya yanakuwa aibu.

  19. Mkulima's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th February 2007
   Posts : 637
   Rep Power : 887
   Likes Received
   121
   Likes Given
   12

   Default Re: Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

   Unajua dunia hii kama hujui jambo bora kuuliza.

   Uliona lini rais wa Ufaransa anaenda airport kupokea wageni? Tafuta hata kwenye google au Youtube na hutaona kitu kama hicho.

   Hivyo hivyo hutaona rais wa USA anaenda airport kupokea wageni. Hata PM wa Uingereza hata siku moja hutaona anaenda kupokea wageni airport hata kama mgeni huyo ni Obama.

   Kila nchi ina utaratibu wake linapokuja suala la kupokea na kukutana na marais wanaotembelea nchi zao.

   Ni sisi Afrika hatuna kazi nyingi za kufanya na viongozi wetu wanajazana airport kupokea wageni. Hata PM eti akitoka Dodoma anapokelewa Dar na viongozi wa mkoa. Huko ni kupoteza muda bure.

   Kwa JK ongeeni lingine lakini sio hili la kapokewa na nani maana ndio utaratibu wao ulivyo.
   Quote By BINARY NO View Post
   Ama kweli hii kali...Yani mwenyeji wake yupo lakini anaempkoea ni waziri wa MISAADA hii inaleta picha gani kwa Taifa? kuna nchi fulani walishawahi kum summon baloz wa inchi fulani baada ya rais wao kupokelewa kwa dharau kiasi hiki...Ebu angalia jinsi ratiba alizopangiwa za kukutana nazo hazina mbele wala nyuma zaidi ya kutuongezea ugumu wa maisha sisi walipa kodi...Kilichoniua zaidi ni kuruka hadi USWIS kwenda makao makuu ya FIFA yani hizo garama tu apo tunapata ZAHANATI MBILI AU TATU ZAKISASA...Nakitu kingine RAIS wetu hajawahi miss world economic forum je ajiulize hizo semina zote zimemuinua vipi kiulewa na akaja na idea zipi za kutekeleza? Na nini kazi ya FM wa TZ?????????

  20. Muke Ya Muzungu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 17th June 2009
   Posts : 3,454
   Rep Power : 0
   Likes Received
   204
   Likes Given
   31

   Default Kikwete Ameenda Kumuombea Nani Misaada Ufaransa, Nyuma Tanzania Inaungua

   Aiingii Akilini Rais wa Tanzania kulakiwa na Waziri wa Misaada wa ufaransa huku wasaidizi wake wakidai amelikwa na Rais Mpya wa Ufaransa. Amealikwa kwa lipi? Wakati wanajua anauza nchi yake. Wamwalike kwa lipi wakati nchi yake ina mali nyingi, tena ya kuwapa wachina sawa na bure kama anavyotaka kufanya Mtwara? Jamani Rais wetu ni kwamba amechoka na Tanzania au kuna tatizo fulani. Kwa nini ajidhalilishe kulakiwa na waziri wa MISAADA, nyuma anaiacha nchi yake ikiungua. Maandamano ya Mtwara ni madogo? Hiyo misaada Atamletea nani akirudi na kuikuta nchi vipande vipande?

  21. kiwatengu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Location : Sing'isi Meru
   Posts : 11,598
   Rep Power : 429499238
   Likes Received
   6692
   Likes Given
   4150

   Default Re: Kikwete Ameenda Kumuombea Nani Misaada Ufaransa, Nyuma Tanzania Inaungua

   Hajaalikwa wala nini...tokea jana nimeona baadhi ya maandiko huku, amekwenda kucheki show ya koffi olomide. akitoka hapo ataenda uswisi atatembelea FIFA! possible anakwenda kuomba mipira.. Anapenda starehe kuliko kazi!!


  Page 7 of 8 FirstFirst ... 5678 LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...