Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Waziri Adanganya Bunge

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 27
    1. #1
      MegaPyne's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Posts : 589
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Waziri Adanganya Bunge

      Hello JFers

      Below is an extract from the speech of minister for infrastructure development specifically on issues related to ICT... the whole budget speech is found at ministry website... http://www.infrastructure.go.tz/HOTU...6_07_Final.pdf

      thanks that the website is now looks at least good.

      Things to note, there is enough emphasize on IXPs, hope that this time it will happen!!! However I have one concern... especially....

      I quote
      "....Watoa huduma za takwimu na tovuti waliendelea kujiunga kwenye mitambo ya mawasiliano ya Kitaifa (Internet Exchange Point) iliyopo Dar es Salaam. Faida ya kutumia kituo hiki ni kupunguza gharama kwani watumiaji hawatumii njia ya masafa ya kimataifa wakati wa kufanya mawasiliano hayo ndani ya nchi. Kufanya hivyo kunapunguza uwezekano wa kuvuja kwa siri za kibiashara na kiutawala."-
      according to my knowledge the last service provider to join TIX was TTCL and it was June 22, 2005, that means it is about TWO (2) years now since the last peer joined TIX ...

      source http://www.tix.or.tz/peers.html ..


      list of prospective TIX peers could have been all of these organizations listed here if after all regulation are in place and they are enforced

      http://www.tcra.go.tz/licensing/CLFlicensed_operators.php#AS

      I need to be educated on "watoa huduma wanaoendelea kujiunga na IXP" ??? how many since June 2005 and what are those organizations?


      The speech.....
      ---------------------------------START----------------------------------
      Huduma za Mawasiliano

      12. Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mawasiliano, mkakati uliowekwa ni ule wa kuhakikisha kwamba huduma za mawasiliano zinafika vijijini hasa kwenye maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara. Mkakati huo unahusisha kuanzishwa kwa Mfuko wa Mawasiliano (Universal Communications Services Access Fund-UCSAF). Lengo la mfuko huu ni kuhakikisha kuwa huduma za mawasiliano zinafika katika maeneo ambayo hayana maslahi mazuri kibishara (hasa vijijini). Aidha, hivi sasa Serikali iko kwenye mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Mkonga wa Mawasiliano wa Kitaifa (National Communications Infrastructure Backbone) utakaokidhi matumizi ya teknolojia ya kisasa. Mkonga huo utakuwa na urefu wa km 6,000 na utaunganisha Makao Makuu ya Wilaya zote nchini kwa kuanzia.

      13. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2006/07 mawasiliano kupitia njia ya tovuti yaliendelea kuimarika ambapo kampuni za watoa huduma (Internet Service Providers) 30 zilitoa huduma hii na watoa huduma za tovuti waliosajiliwa walifikia 400. Hata hivyo, gharama za mawasiliano ya tovuti ziliendelea kuwa juu kutokana na
      kukosekana kwa miundombinu na huduma nyingine zinazohitajika katika kuwezesha utoaji wa huduma za mawasiliano. Watoa huduma za takwimu na tovuti waliendelea kujiunga kwenye mitambo ya mawasiliano ya Kitaifa (Internet Exchange Point) iliyopo Dar es Salaam.

      Faida ya kutumia kituo hiki ni kupunguza gharama kwani watumiaji hawatumii njia ya masafa ya kimataifa wakati wa kufanya mawasiliano hayo ndani ya nchi. Kufanya hivyo kunapunguza uwezekano wa kuvuja kwa siri za kibiashara na kiutawala.

      Ili kueneza mitambo ya tovuti nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea na ujenzi wa mtambo wa kupitisha taarifa za tovuti (Internet Exchange Point - IXPs) jijini Arusha ambao unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Julai 2007. Mtambo huo utakapokamilika utakabidhiwa kwa Chama cha Watoa Huduma za Tovuti ili wauendeshe na kuunganishwa na mtambo uliopo Dar es Salaam.

      14. Mheshimiwa Spika, TCRA imeendelea kusimamia na kudhibiti shughuli za Mawasiliano, Teknolojia ya Mawasiliano na Habari na Utangazaji. Katika kipindi cha mwaka 2006/2007, Mamlaka ilianzisha taasisi iitwayo Tanzania National Information Center (tzNIC) ambayo jukumu lake kubwa ni kugawa na kusajili anuani pepe (e - mail) kwa watumiaji wa huduma za tovuti nchini na majina ya mitandao (domain names registration) kwa watoa huduma za tovuti. Lengo ni kurahisisha utambuzi wa chanzo cha habari inayotumwa kutoka kwa mtumiaji mmoja wa mtandao kwenda kwa mtumiaji mwingine na kupunguza gharama za ada zinazolipwa na watoa huduma kwa
      wasajili wa majina ya mitandao nje ya nchi.

      15. Mheshimiwa Spika, mfumo mpya wa leseni za mawasiliano (converged licensing framework) uliendelea kutekelezwa kwa kutoa leseni mpya kwa watoa huduma na kusimamia utekelezaji wa viwango vya huduma. Mfumo huu unazingatia umuhimu wa kuharakisha usambazaji wa huduma za mawasiliano nchini. Mfumo huu ulianzisha leseni ya mawasiliano na utangazaji katika ngazi ya kijamii (community) ili kufikisha huduma hizo vijijini. Hatua hii itawawezesha wananchi walio wengi kupata huduma za mawasiliano na taarifa mbalimbali kutoka katika vituo 47 vya redio na vituo 29 vya televisheni vilivyopo nchini. Aidha, Mamlaka imeandaa mpango utakaowezesha kuondoa tatizo la masafa katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha inayotokana na kuanzishwa kwa vituo vingi vya utangazaji. Mpango huo unazingatia sera iliyowekwa kimataifa ya kubadili teknolojia ya utangazaji kutoka analogue
      kwenda digital.

      16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2007/08, Wizara kwa kupitia TCRA itaendelea kusimamia, kudhibiti, kutoa elimu, kuhamasisha na kusaidia utoaji wa huduma bora za mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa mitambo ya tovuti katika Manispaa za Dodoma, Mbeya na Mwanza. Aidha, mradi wa kuunganisha mitambo ya IXPs ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki umekwishaanza ambapo mkandarasi ameshateuliwa kutekeleza mradi huo. Mitambo hiyo itarahisisha mawasiliano katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki Ili kudhibiti wizi wa simu za mikononi, TCRA itaendelea kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano ya simu kuandaa utaratibu utakaohakikisha kuwa watoa huduma wote wanashirikiana kujenga mtambo wa kudhibiti simu za mkononi zilizoibiwa kwa kuzifunga zisitumike kwenye mtandao wowote katika Afrika Mashariki. Vile vile kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomu (Tanzania Atomic Energy Commission), TCRA itapima viwango vya mionzi inayozalishwa na miundombinu ya mawasiliano ili kuhakikisha kuwa haizidi viwango vinavyotolewa na Tume ya
      Kudhibiti Mionzi Ulimwenguni.

      17. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2006/07, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imekamilisha Mradi wa uboreshaji wa huduma ya takwimu na Intaneti kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya Asymetric Digital Subscriber Lines (ADSL) katika Makao Makuu ya Mikoa yote Tanzania. Kazi nyingine iliyokamilika ni ya kuweka mitambo mipya ya Digital Microwave Radio katika njia kuu ya Dodoma hadi Mbeya kupitia Iringa na Nyororo, Mwanza - Bukoba –
      Kigoma na Mwanza – Musoma. Aidha, mitambo kama hiyo (Digital Microwave Radio) inawekwa kati ya Dar es salaam - Morogoro – Dodoma, Dar es salaam – Tanga – Arusha, Dodoma – Arusha kupitia Kondoa, Mbeya – Sumbawanga na Mtwara – Newala – Masasi – Nachingwea. Kazi hii ipo katika hatua za mwisho na itakamilika
      rasmi ifikapo mwishoni mwa Julai, 2007. Aidha, TTCL ipo katika hatua za kubadilisha njia kuu za mawasiliano kati ya Dar es salaam – Zanzibar – Pemba – Tanga itakayohusisha pia njia za kwenda Makunduchi, Bububu, Chake Chake, Mkoani na Wete. Miradi hii inategemewa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2007.
      Kazi inayoendelea hivi sasa ni kuondoa mitambo ya simu za kukoroga (Magneto) kwa kutumia huduma ya simu za mikononi zinazotumia teknolojia ya ‘Code Division Multiple Access -(CDMA)’ katika maeneo ya Mwakaleli, Lwanga, Itigi, Misungwi, Ngudu, Malya, Urambo, Sikonge, Mtera, Mvumi, Ruangwa, Nachingwea, Ndanda, Liwale na
      Kaliua. Kazi hii inategemewa kukamilika mwishoni mwa Julai, 2007.

      18. Mheshimiwa Spika, TTCL imeendelea na kazi ya kubadilisha mitambo ya zamani na kuweka mipya katika miji ya Arusha, Mkoani (Pemba), Moshi, Tanga, Singida, Bukoba na Kigoma. Mitambo ya simu za kukoroga imeondolewa na kufungwa ya kisasa katika maeneo ya Utete, Kibiti, Ikwiriri, Mafia na Kilwa Masoko. Aidha, Kampuni inaendelea na ujenzi wa njia kuu za mawasiliano kwa kutumia mkonga wa kigae (Optical fibre cable) ili kuimarisha njia za mawasiliano na kutekeleza azma ya Serikali kuwa na mawasiliano bora, imara na ya kisasa kwa nia ya kuunganisha nchi za Afrika Mashariki. Kampuni imeendelea na hatua ya awali ya ujenzi wa mkonga wa kigae kati ya Arusha – Musoma – Mwanza kupitia mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti, Mwanza – Shinyanga –Isaka – Rusumo (Rwanda) – Kabanga (Burundi) na Nyakanazi – Bukoba. Wakandarasi wa kazi hiyo wameshapatikana na inategemewa kukamilika ifikapo mwishoni mwa 2007. Aidha, mkonga wa kigae utajengwa kati ya Morogoro – Iringa – Mbeya na Somanga – Lindi – Mtwara. Ujenzi wa njia kuu kati ya Mbeya – Kasumulo Songwe Malawi utakaounganisha mawasiliano kwenda hadi umekamilika.

      19. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2007/08, TTCL imepanga kutekeleza mipango ya kuboresha na kupanua njia kuu za mawasiliano (Digital Microwave Backbone) katika njia za Morogoro – Ifakara – Mahenge, Songea – Tunduru – Masasi – Mtwara, Njombe – Makete – Ludewa na Moshi – Marangu – Rombo Mkuu. Aidha, kampuni itaanza kutoa huduma za simu za mikononi katika Wilaya zote nchini na kupeleka mkonga wa kigae kwa wateja wakubwa ili kuboresha huduma za simu. Kwa kuanzia kampuni imetoa zabuni ya kuweka mtandao unaotumia teknolojia ya Optic Fibre kwenda Ikulu ya Zanzibar na hoteli zote za kitalii zilizoko maeneo ya Kiwengwa, Zanzibar. Pia mitambo tisa ya kuunganisha simu kwenda katika maeneo ya Mtwara – Tandahimba – Newala – Masasi, Dodoma – Kondoa na Sumbawanga – Namanyere – Mpanda itabadilishwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2007

      20. Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Simu 2000 Limited katika mwaka 2006/07, iliendelea na majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuuza mali ilizokabidhiwa na kufuatilia malipo ya pensheni za waliokuwa wafanyakazi wa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki. Majukumu mengine ni kufuatilia kesi zilizorithiwa na zinazojitokeza katika uendeshaji wa Kampuni. Aidha, Kampuni iliweza kuuza nyumba tatu na viwanja viwili. Kampuni inaendelea na kazi zake hadi hapo itakapokoma na kukabidhi majukumu yake kwa Consolidated Holding Corporation (CHC) Desemba, 2007.

      Huduma ya Simu za Mkononi

      21. Mheshimiwa Spika, huduma za simu za mkononi zimeendelea kupanuka katika mikoa yote Tanzania Bara na Tanzania Zanzíbar. Huduma hizi zinatolewa na Kampuni za TTCL, Vodacom, Celtel, Tigo na Zantel. Mwaka 2006 Kampuni hizi zilikuwa na wateja 6,557,970 waliounganishwa kwenye huduma ya simu za mkononi ikilinganishwa
      na wateja 3,118,157 kwa mwaka 2005. Ongezeko hili la asilimia 100 kwa mwaka linaonyesha kuwa huduma ya simu za mkononi imekuwa sehemu ya mahitaji muhimu ya kila siku kwa wananchi katika shughuli zao.

      Jamii Habari

      22. Mheshimiwa Spika, mchakato wa ujenzi na uimarishaji wa Jamii Habari ni zoezi la kudumu na endelevu. Jamii Habari ni nyenzo muhimu katika kuwawezesha wananchi kuwasiliana, kujifunza na kupashana habari. Katika kipindi cha 2006/07, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imetekeleza uanzishaji wa somo la teknolojia ya habari na mawasiliano mashuleni. Aidha, Umoja wa Afrika (AU) kwa niaba ya nchi wanachama, Tanzania ikiwa mojawapo, imeingia makubaliano ya awali na Serikali ya India. Makubaliano hayo yanahusu uanzishwaji wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa Mawasiliano ya wakuu wa Nchi za Afrika, vyuo vya elimu ya juu, vyuo vya ualimu na hospitali za rufaa nchini (e-government, e-education na e-health). Lengo la mradi huu ni kuboresha utoaji wa elimu huria na huduma za afya (tele-education and tele-medicine services) ili kupunguza gharama za elimu na matibabu. Mradi huu utagharamiwa na Serikali ya India kwa muda wa miaka mitano.

      23. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2006/07, Serikali imeendelea kuimarisha vituo vya mawasiliano nchini. Vituo hivyo ni pamoja na Tanzania Global Distance Learning Centre (TGDLC) kilichopo Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mkoani Dar es Salaam. Kituo hiki kimeendelea kutoa mafunzo kwa viongozi na wataalamu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA). Tunategemea kutumia uzoefu huo kupeleka mafunzo hayo katika mikoa na Wilaya zote nchini. Kwa kuanzia Wizara itapeleka mafunzo hayo katika vituo ambavyo vimeshaanzishwa ikiwa ni pamoja na Sengerema Tele Centres kilichopo mkoani Mwanza, Chuo cha Ualimu
      Kasulu kinachotumia nishati ya kinyesi cha ng’ombe na Ngara UNHCR Tele Centre kilichoko mkoani Kagera. Vituo vingine ni Wino Tele Centre cha mkoani Ruvuma na Multipurpose Tele Centres zilizoko Kinampanda mkoani Singida, Mpwapwa mkoani Dodoma na kituo cha Mtuwetu kilichopo mkoani Mtwara. Vituo hivyo vimeendelea
      kutumiwa na jamii katika kukuza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Wananchi wameendelea kufaidika katika maeneo ya bishara, elimu, afya, utawala na uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Katika mwaka 2006/07 wataalamu wa Wizara walivitembelea vituo vilivyopo katika mikoa ya Singida, Mtwara, Kilimanjaro na Shinyanga kwa lengo la kupata taarifa na kufanya tathmini ya utendaji ya vituo hivyo na kuendelea kushauri na
      kuviimarisha. Katika mwaka 2007/08, Wizara ina mpango wa kuanzisha vituo vipya vya Tele Centre na kuhamasisha matumizi ya tekinolojia ya Habari katika sehemu za Ukerewe, Tabora, Same, Hai, Sumbawanga na
      Lindi. Aidha, Wizara itaendelea kuviboresha vituo vilivyopo na kuviongezea uwezo.

    2. RukaaJuu Final

    3. #2
      Bi. Senti 50's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2007
      Posts : 395
      Rep Power : 698
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default

      sasa ni wapi alipoliongopea Bunge?

    4. #3
      Halisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th January 2007
      Posts : 3,037
      Rep Power : 2178
      Likes Received
      455
      Likes Given
      243

      Default

      Maelezo hapo juu yanatosheleza kuwa Waziri kaongopa

      I quote "....Watoa huduma za takwimu na tovuti waliendelea kujiunga kwenye mitambo ya mawasiliano ya Kitaifa (Internet Exchange Point) iliyopo Dar es Salaam. Faida ya kutumia kituo hiki ni kupunguza gharama kwani watumiaji hawatumii njia ya masafa ya kimataifa wakati wa kufanya mawasiliano hayo ndani ya nchi. Kufanya hivyo kunapunguza uwezekano wa kuvuja kwa siri za kibiashara na kiutawala."-
      according to my knowledge the last service provider to join TIX was TTCL and it was June 22, 2005, that means it is about TWO (2) years now since the last peer joined TIX ... "

      "

    5. #4
      ViciousRecklessSavage!!!'s Avatar
      Banned Array
      Join Date : 23rd June 2007
      Posts : 143
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Yes, its clear based on the evidence provided above, that this so called "minister for infrastructure development" definitely lied to his peers in the so called "parliament".

      It just goes to show how any incompetent bozo with only a semblance of college education but having the right connections and tons of reputation for being poodle/henchman/sycophant to the sitting president can expect a career as top bureaucrat in the government.

      I remember once, sometime in the late 80's, listening to "professor" and "minister in the government" Mark Mwandosya deliver a speech in English on the radio, and was utterly shocked to discover how poor his command of the language actually was.

    6. #5
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,263
      Rep Power : 36770
      Likes Received
      9630
      Likes Given
      686

      Default

      Mwandosya a minister in the government in the late 80's? Not sure 'bout that one...you may wanna double check
      As for his command of English...I'll give him a pass...(1)his faculty for learning languages may not be all that and (2) English is probably his third or fourth language...so it may not be that easy for him to command it as a native speaker or someone whom it is a second language.
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    7. Miaka 50

    8. #6
      ViciousRecklessSavage!!!'s Avatar
      Banned Array
      Join Date : 23rd June 2007
      Posts : 143
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Whatever top position he used to hold in the government at that time, one thing I know for sure is he had already started calling himself "professor" and his spoken English skills were less than satisfactory for someone of his academic and professional background.

    9. Sam
      #7
      Sam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2006
      Posts : 602
      Rep Power : 784
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default

      Nyani
      Nadhani hawa watu kama ViciousRecklessSavage hawajakaribishwa vizuri humu ndani. ViciousRecklessSavage, Mwandoysa hakuwa "professor" wala "waziri" in 80s tunaomba u-double check kitu ambacho ulikuwa unataka kusema halafu utueleze vizuri ulikuwa unataka kusema nini. Pili, 80s ni zaidi ya miaka 20 iliyopita, je unadhani hiyo miaka bado hajajifunza kitu?

    10. Sam
      #8
      Sam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2006
      Posts : 602
      Rep Power : 784
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default

      ViciousRecklessSavage,
      kwa hiyo u-professor alionao ni wakujipa mwenyewe au kujiita mwenyewe kama professor Maji Marefu? Do you need spoken english skills to be a "professor'?

    11. #9
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,670
      Rep Power : 21816
      Likes Received
      736
      Likes Given
      3195

      Default

      Vicious

      UTUMWA NI KITU KIBAYA SANA.........!!!,

    12. #10
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,282
      Rep Power : 5568
      Likes Received
      289
      Likes Given
      77

      Default

      Unamwongelea Prof. Mwandosya au mtu mwingine. Nafikiri umechanganya majina.

      Prof. Mwandosya ni katika mawaziri wenye uwezo kwenye serikali ya
      JK na pia kwenye serikali iliyopita.

      Uwezo wa waziri wa Tanzania hata siku moja hauwezi kutegemea umahiri wake wa kuongea Kiingereza. Lakini Mwandosya ninayemfahamu mimi ana uwezo wa kutosha kuongea Kiingereza. Kuanzia Bachelor mpaka Ph.D kasomea Uingereza, alikaa UK miaka hiyo ya 70 ambayo lugha ilikuwa moja tu na sio kama sasa ambapo
      unaweza ku survive hata kama hujui lugha yao.

      Prof. Mwandosya ameingia bungeni mwaka 2000 na kuchaguliwa moja kwa moja kuwa waziri. Hiyo miaka ya 80 unayoisema alikuwa mlimani akifundisha.

    13. #11
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,263
      Rep Power : 36770
      Likes Received
      9630
      Likes Given
      686

      Default

      Quote By ViciousRecklessSavage!!!
      Whatever top position he used to hold in the government at that time, one thing I know for sure is he had already started calling himself "professor" and his spoken English skills were less than satisfactory for someone of his academic and professional background.
      Have you listened to one of Mwanakijiji's English podcasts..? Have you read one of his English articles...? Well, if you haven't done either...they are day and night (No Disrespect to you Mwanakijiji). For none native speakers it is not surprising to find some that are better at spoken than written and vice versa. If you listen to Mwnakijiji's English podcasts you'll get what I'm saying. Mwanakijiji can hardly pronounce some seemingly easy English words right...to him the words "rise" and "raise" for example, are pronounced the same when they shouldn't. I'm sure he knows what they mean...but for some reason he just can't say 'em right. So the same may apply to Mwandosya...he may be good or better than average at written English but he is below average at spoken. You're profession and academic background does matter too...afterall he is an Electical Engineering Professor and not and an English or Foreign Languages Professor
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    14. #12
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,282
      Rep Power : 5568
      Likes Received
      289
      Likes Given
      77

      Default

      Nyani,

      Hivi kumbe rise na raise yanatofauti? Ha ha ha haaaaa!!!!

      Mimi huwa nayachanganya tu. Wacha nijaribu rise= raizi na raise= reizi kama nimechemsha basi nikosoeni.

      Hizi sio lugha zetu, hata ujue namna gani kuandika lakini kuzungumza balaa tupu. Wanangu kila siku wananipiga pardon? Lakini wengine English ni lugha ya tatu au nne kwahiyo hanibabaishi mtu. Nawafundisha wanangu namna ya kuandika kiingereza kizuri lakini kwenye kuongea inabidi niwaachie lugha yao.

    15. #13
      ViciousRecklessSavage!!!'s Avatar
      Banned Array
      Join Date : 23rd June 2007
      Posts : 143
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By sam
      Nyani
      Nadhani hawa watu kama ViciousRecklessSavage hawajakaribishwa vizuri humu ndani. ViciousRecklessSavage, Mwandoysa hakuwa "professor" wala "waziri" in 80s tunaomba u-double check kitu ambacho ulikuwa unataka kusema halafu utueleze vizuri ulikuwa unataka kusema nini. Pili, 80s ni zaidi ya miaka 20 iliyopita, je unadhani hiyo miaka bado hajajifunza kitu?
      As far as I can see, Mark Mwandosya was associate professor at UDSM since at least 1983: so its safe to say he had attained full professorship by end of 80s.

      And yes, I now recall he used to be Principal Secretary in the Ministry of Energy when I last heard him speak what I considered appalling English on national radio for someone of his academic calibre.

      http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp...username=GUEST

    16. #14
      ViciousRecklessSavage!!!'s Avatar
      Banned Array
      Join Date : 23rd June 2007
      Posts : 143
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Ogah
      Vicious

      UTUMWA NI KITU KIBAYA SANA.........!!!,
      Meaning what Ogah? By your reasoning, all modern academia might as well be equated with (mental?) slavery, and the biggest slaves of them all would then be individuals who inhabit the ivory tower like professors, doctors, deans, and other elite scholars at top of the academic pecking order.

    17. #15
      Halisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th January 2007
      Posts : 3,037
      Rep Power : 2178
      Likes Received
      455
      Likes Given
      243

      Default

      Turudi katika hoja ya je, Waziri kadanganya bunge? Mhe Zitto kama upo chukua hiyo uhoji, nadhani kuna kifungu cha kumbana

    18. #16
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,282
      Rep Power : 5568
      Likes Received
      289
      Likes Given
      77

      Default

      Hiyo ilikuwa radio ya wapi ambayo alikuwa anaongea Kiingereza? Radio zote za Tanzania miaka hiyo walikuwa wanatumia Kiswahili.

      Pili Mwandosya alikuwa principal secretary kuanzia 1990 na sio miaka ya 80.

      Madai na facts zako sidhani kama zikoko sahihi.

    19. #17
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,282
      Rep Power : 5568
      Likes Received
      289
      Likes Given
      77

      Default

      CMB,

      Hiyo link uliyotuma mbona kama ni budget ya mwaka 2006/07 na sio ya mwaka huu.

      Check vizuri link uliyotuma.

    20. #18
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,670
      Rep Power : 21816
      Likes Received
      736
      Likes Given
      3195

      Default

      Vicious,

      Unaanzia na Associate Professor kabla ya kuwa Full Professor, halafu wewe humjui Prof Mark Mwandosya, kwa sababu mpaka sasa hivi hakuna hata inf moja uliyoitaja kuhusu yeye ambayo ni sahihi.

      Niliposema UTUMWA nilimaanisha wewe unakuwa MTUMWA wa lugha na kwa zaidi Msome Nyani hapo juu utaelewa matatizo unayojaribu kuyaweka hapa

    21. #19
      ViciousRecklessSavage!!!'s Avatar
      Banned Array
      Join Date : 23rd June 2007
      Posts : 143
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      For all I care, it could well have been in the beginning of 90s, and he was on RTD External Service talking broken English with the most clear and confident voice (which was rather hilarious in itself).

      Now, if anyone out there still doesn't want to believe it, then I suggest you go look for the tape of the meeting in the vaults of the RTD archive. BASTA!!

    22. #20
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,263
      Rep Power : 36770
      Likes Received
      9630
      Likes Given
      686

      Default

      Who cares about his fluency in some foreign language....apparently...only you
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    Page 1 of 2 12 LastLast

    Similar Topics

    1. Waziri adanganya walimu
      By tyadcodar in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 0
      Last Post: 12th September 2011, 19:47
    2. Waziri wa Kikwete alidanganya Bunge
      By Fareed in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 13
      Last Post: 21st July 2011, 16:27
    3. Waziri Mkuu amelidanganya Bunge
      By Candid Scope in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 10
      Last Post: 13th February 2011, 23:03
    4. Replies: 5
      Last Post: 26th January 2011, 08:52

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...