Nina swali dogo tu au pengine linaweza likawa kubwa kulingana na wachangiaji watakavyo jitokeza kuchangia.
Na huenda si mimi peke yangu ninaetaka kufahamu nini chanzo cha kuanzishwa kwa chama cha demokrasia na maendeleo?
kwa nijuavyo mimi baadhi ya viongozi walionzisha chama hiki walitokea NCCR Mageuzi, lakini sina uelewa wa nini kilitokea mpaka wakajitoa NCCR Mageuzi Na kuanzisha Chama cha CHADEMA.
Naomba mtusaidie historia hii mzuri ya vyama hivi viwili.
Last edited by PISTO LERO; 4th January 2013 at 12:51.
Waanzilishi wa CHADEMA ni hawa hapa nani chama cha kisiasa hakikuwahi kubadilishwa.
Edwin Mtei (Arusha),
Makani (Shinyanga),
Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
Edward Barongo (Kagera),
Mary Kabigi (Mbeya),
Menrad Mtungi (Kagera),
Costa Shinganya (Kigoma),
Evalist Maembe (Morogoro) na
Steven Wassira (Mara)
Ficha upumbavu wako
nashukuru kaka nilitaka nimtajie wazilishi wa CHADEMA lakn naona umemaliza kazi. Ila tu ni chama kilichoazishwa baada ya kuwepo mfumo wa vyama vingi ya maltiparty system. Hvy mtoa mada ajue hilo.
Asante: ila ndiya sababu nikaomba kujua nini kilitokea.
Samaki mkunje angali m'bichi... Nccr haikupata dira mathubuti, ilikua tayari imekwisha corruptiwa na mfumo chakavuu.. Kuliko mlio wa punda, bora upate punda mwenyewe... Cha muhimu ni kujivunia sasa tuna CHADEMA imara...
If you want to ignore PAIN, first ignore SORROW... Am not responsible for your Happiness.
Waanzilishi wa CHADEMA ni hawa hapa nani chama cha kisiasa hakikuwahi kubadilishwa.
Edwin Mtei (Arusha),
Makani (Shinyanga),
Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
Edward Barongo (Kagera),
Mary Kabigi (Mbeya),
Menrad Mtungi (Kagera),
Costa Shinganya (Kigoma),
Evalist Maembe (Morogoro) na Steven Wassira (Mara)
Ficha upumbavu wako
Ni George Wasira, nduguye Steven.
If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. Tutu
Hadithi hiko namna hii
Mwishoni mwa mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90, Watanzania kadhaa (hususan wasomi wa UDSM) walianza kuhoji mifumo mbalimbali ya nchi ambayo walikuwa hawalidhiki nayo, ukiwemo mfumo wa demokrasia nchini uliofinywa na katiba na utaratibu wa chama kushika hatamu. Mawazo yao, haraka haraka yaliwavutia viongozi wa zamani wa serikali au umma, ambao kwa namna moja ama nyingine waliwahi kusigishana na Mwalimu. Hawa wako wengi, kutaja wachache hapa; Mzee Edwin Mtei, Marehemu Chifu Abdallah Fundikira, Christopher Kasangatumbo, na James Maparaka.
Kukutana kwa pande hizi mbili (critical wasomi, na wenye dukuduku lao) kukapelekea kuundwa kwa kamati ya kudai mabadiliko ya katiba nchini (NCCR), mnamo mwaka 1991. Kamati hii ikapata viongozi; Mwenyekiti - Fundikira, Makamu - Maparara, na Katibu -Marando.
Ilipofika mwaka 1992, Mzee Ruksa 'akaruksu' mfumo wa vyama vingi. Basi Fundikira akaanzisha chama chake (UMD), Maparara naye chake (CCW, ambacho baadaye kikaungana na KAMAURU ya Zanzibar kuunda CUF). Marando akabaki na NCCR, ikageuzwa kuwa chama cha NCCR-Mageuzi na yeye akawa Mwenyekiti.
Wakati Marando na wana NCCR wangine wakijiandaa kusajili chama, waliwaza sana kutafuta jina la kiswahili ili wawe na radha ya kitanzania zaidi. Ndipo Mzee Mtei akatoa wazo; "Jamani ee, kwanini tusitumie kaulimbiu yetu ikawa ndio jina la chama?" Tangia mwanzo NCCR ilikuwa ikutumia maneno; 'Demokrasia na Maendeleo' kama kaulimbiu yake. Maneno hayo, yako kwenye nembo ya chama cha NCCR-Mageuzi hadi leo.
Basi wazo la Mzee Mtei likakubalika, chama kiitwe CHADEMA. Ndipo wanasheria ndani ya chama, mfano Dr. Sengondo Mvungi wakapewa jukumu la kuaandaa katiba na sera ili zitumike kusajili chama kwa jina hilo.
Baada ya kukamilika kwa maandalizi hayo, msafara wa viongozi ukaelekea ofisi ya msajili wa vyama kufanya kazi inayotakiwa. Akina Mvungi walipofika kwa Mhe. George Liundi, akawambia "Nyie vipi, mbona chama hiki tumeishakisajili?"
Wakapigwa butwaa. Kumbe Mtei na wenzake alifanya kitu timing kama ya Essau na Yakobo wa Kwenye Biblia.
Anyway, akina Mvungi na Marando wakaona hakujaharibika neno, ikabidi wasajili chama kwa jina la awali; NCCR-MAGEUZI.
Sasa, kuhusu swali la kwanini viongozi wengi wa CHADEMA leo ndio hao hao walikuwa NCCR? Ieleweke kwamba si wote, bali hapa wanatajwa kama akina Mhe. Tundu Lissu, Mhe. Marando, Mhe. Chiku Abwao, Mhe. John Mnyika, Mhe. Joseph Selasini, Marehemu Chacha Wangwe ... orodha ni ndefu.
Sababu mojawapo ya kuhama kwao, ni 'kupasuliwa kwa ngoma' mwaka 1996 kule jijini Tanga.
Sababu nyingine ni mwendelezo wa 'crossing the floor' kwa mfano, mwezi uliopita kuna kiongozi wa NCCR kaenda CHADEMA na Mwezi huu (in fact leo), kiongozi wa CHADEMA kahamia NCCR.
The two parties are twin sisters, sometimes hugging sometimes hating each other.
Lengo kuu la Chadema ni Kutetea Demokrasia na kuleta Maendeleo. Si kweli viongozi wote wa Chadema walitoka NCCR. Zitto, Dr Slaa etc hawajawahi kuwa wanachama wa NCCR
Jamaaa kaongelea waanzilish wa chama so Zitto na Dr Slaa si miongoni wa waanzilishi wa Chama cha CHADEMA.
Je? Hivi vyama vya UMD na CCW Bado vipo?
Na kuna ukweli wowote kuwa Mh.Tundu Lisu alishawahi kuikimbia nchi chini ya utawala wa Raisi Benjamin Mkapa?
Kama ni kweli sababu ilikuwa nini na alikimbilia nchi gani?
Mkuu Pisto Lero,
Unafanya utafiti? Sema wazi uambiwe vyanzo mbalimbali vya data.
CCW ambayo kirefu chake Kilikuwa Chama cha Wananchi, hakipo tena, ila kilimzaa CUF, ndio maana hadi leo utawasikia CUF wakisema; 'Chama cha Wananchi - CUF'.
Mapalala alianzisha kingine CHAUSTA
Edwin Mtei (Arusha), Makani (Shinyanga),
Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
Edward Barongo (Kagera),
Mary Kabigi (Mbeya),
Menrad Mtungi (Kagera),
Costa Shinganya (Kigoma),
Evalist Maembe (Morogoro) na
Steven Wassira (Mara)
By MAFILILI
Ukweli umejulikana kuwa CDM ina mahusiano na maendeleoya kanisa Tanzania, waanzilishi ni WAKRISTO!
Sina tabia ya kuangalia kwa majina lakini kwa kumbukumbu zangu za karibuni kwenye mazishi ya Makani nijua kuwa ni mwislam baada ya kutazama mazishi yake sina uhakika na wengine nita kujuza siku ya vifo vyao kama watanitangulia ikiwa kinyume basi endelea na usaa wako masikioni na tongo tongo machoni huku mdomoni ukiwa umejaza kinyesi...
Nobody can give you freedom. Nobody can give you equality or justice or anything. If you're a man, you take it.... Malcolm X Nasubiri 'breaking news... '
Follow Us Here