Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Uzalendo wa watanzania

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 31
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16306
      Likes Given
      8390

      Default Uzalendo wa watanzania

      Kwa karibu miaka kama miwili hivi, hisia za uzalendo na kuionea fahari nchi yetu imeanza kuingia na kukita kwa nguvu katika mioyo ya Watanzania. Sitaogopa kusema kuwa hakuna watu katika Afrika ukiondoa labda Waghana wenye kuona fahari sana na nchi yao kama Watanzania hivi sasa. Hata hivyo kwa maoni yangu uzalendo huu wa picha ni uzalendo uliopotoka na unaoficha hasa hisia za wananchi kwa viongozi wao. Kwa namna moja naamini Watanzania wameanza kutofautisha kupenda viongozi wao na kuipenda nchi yao. Sasa hivi hisia hii ya uzalendo imefikia mahali pa kusema "waache waendelee kula, lakini nchini mwetu twalala".

      Ni hapa ninapojikuta najiuliza kuwa uzalendo huu wa picha una faida gani katika utendaji na uongozi wa nchi. Je, tunaipenda nchi yetu kweli na kufikia mahali pa kutovumilia uzembe, ugoigoi wa uongozi, na ufinyu wa ubunifu? Je mapenzi yetu ya nchi yanatufanya tusiwaonee haya viongozi uchwara wapendao masihara ambao hutawala kwa mikwara? Ni uzalendo gani tulionao hasa wale walio katika madaraka wa kuona fahari ya nchi yao!.

      Katika picha nyingi nilizoziona leo, inaonekana wenye mapenzi sana na wenye kuona fahari zaidi kwa nchi yao ni watu wa kawaida. Tukichukulia mavazi na vibendera kama ishara ya mapenzi hayo, sijaona kiongozi au mfadhili yoyote iliyevaa kitu chochote chenye rangi au alama za Taifa! Na hapa sizungumzii nia na makusidio ya mioyo ya watu, ninajiuliza tu je ni kweli sisi ni wazalendo kwa kuvaa rangi za Taifa na kupepea vibendera vya "Rangi Nne"?

      Ni kitu gani hasa kinaweza kutufanya tuoneshe uzalendo wetu pasipo kuvaa rangi hizi za Taifa?
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. Miaka 50

    3. #2
      Gamba la Nyoka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st May 2007
      Posts : 1,642
      Rep Power : 958
      Likes Received
      266
      Likes Given
      97

      Default Uzalendo Tanzania

      Nimelala nimekesha,Jambo nimefikiria
      Bongo nimezichemsha,sipati jibu sawia
      Hivi kweli umekwisha?,uzalendo Tanzania?

      Ni nani anayejali,adha za Mtanzania?
      Yule aliye mkweli,moyoni anaumia
      lamuuma Jambo hili, kwa dhati anachukia

      Ona walivyoziuza, rasilimali za Watanzania
      Kwa kweli inashangaza, mikataba wanayoingia
      Kisha tukiwauliza,hawana la kutuambia

      Rushwa imekua ngao,kumdhulumu raia
      Ubinafsi kwao nguo,vazi la kujivunia
      Hizi ndio sera zao?,hawana la kutuambia?

      Wananchi amkeni,haki kujitafutia
      Mtalala mpaka lini?,saa imeisha wadia
      Uwongo ukataeni,waache kuwatania

      Hivi ni faida ya nani?,kuvunja demokrasia
      Kuwakwaza wapinzani,hili mmeliridhia?
      Hivi kweli hatuoni?,yale yanayotokea?

      Toeni kauli zenu,wapate kuzisikia
      Na mkipiga kura zenu,chagueni wenye nia
      Waonyesheni watoto wenu,muelekeo na njia

    4. #3
      Gamba la Nyoka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st May 2007
      Posts : 1,642
      Rep Power : 958
      Likes Received
      266
      Likes Given
      97

      Default

      Wana malenga kazi kwenu sasa!
      Chadema kama mnapokea misaada kutoka nje bila kufanya tathmini, angalieni mkishika dola msije mkaiuza Tanzania na watu wake kwa vijimisaada vichache- Hao wanaowapa misaada hawana permanent Friends/Enemies, bali wana permanent Interests.

    5. BAK
      #4
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,532
      Rep Power : 44950
      Likes Received
      8273
      Likes Given
      8280

      Default Sumaye: CCM inajichimbia kaburi

      Naam hata JK kaupata Urais kwa kutumia rushwa

      Sumaye: CCM inajichimbia kaburi

      na Mwandishi Wetu
      Tanzania Daima~Sauti ya Watu


      WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amekitahadharisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kinajichimbia kaburi endapo kitaendeleza vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi pamoja na ufisadi.

      Sumaye alitoa kauli hiyo nzito juzi wakati akihojiwa kwenye kipindi cha ‘Jicho Letu Wiki Hii’, kilichorushwa hewani na kituo cha Radio Clouds cha jijini Dar es Salaam.

      Alisema wapo wagombea wa CCM ambao wameingia madarakani kwa rushwa na hali hiyo ikiachwa ni hatari na itakuwa sawa na kukichimbia kaburi chama.

      Aliitaka jamii inayopokea rushwa kutambua kuwa kiongozi anayeingia kwa rushwa, hawezi kuchapa kazi ipasavyo, kwani atakuwa akitamba kwamba uongozi wake umetokana na rushwa.

      “Kiongozi wa aina hiyo hawezi kuwa mchapakazi na atakachokifanya kila anapoingia madarakani, kazi yake ni kukusanya hela kwa njia halali na haramu, ili ukifika wakati wa uchaguzi, awanunue wapiga kura. Kwa hiyo mchezo wake utakuwa hivyo na mwisho wa siku ni sawa na kukichimbia kaburi chama, na hii ni kwa vyama vyote,” alisema Sumaye.

      Akitolea mfano kwa upande wake, Sumaye alisema amekuwa kiongozi kwa muda mrefu, lakini hajawahi kutoa rushwa kwa mtu yeyote, ili ampigie kura.

      “Mimi nimekuwa kiongozi kwa muda mrefu, sijawahi kutoa rushwa kwa mpiga kura, hata wakati wa uchaguzi wa kuwania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), nilikuwa nikiwakuta watu wamekaa vikundi, lakini niliwaambia wazi wazi kuwa siwezi kutoa rushwa, maana lazima niwe kiongozi wa mfano ndani ya chama changu,” alisema Sumaye.

      Hata hivyo, Sumaye alisema gharama wakati wa uchaguzi haziepukiki, lakini zisitokane na watu kutoa rushwa.

      “Gharama kwenye uchaguzi huwezi kuzikwepa. Kwa mfano, unatoka hapa unakwenda Mwanza kuomba kura, lazima utatumia pesa kusafiri, ila tujitahidi kabisa kuachana na rushwa,” alisema.

      Kuhusu suala la kuwania tena kiti cha urais mwaka 2015, Sumaye alisema hafikirii kujaribu tena nafasi hiyo, lakini kama Watanzania watajitokeza na kumtaka awanie kiti hicho, anaweza kufikiria.

      Sumaye alitetea uamuzi wake wa kwenda nje kusoma kuwa haukuwa na malengo ya kisiasa, bali alitaka kupumzika na kubadilishana mawazo na watu wa mataifa mengine.

      “Baada ya kumaliza muda wangu, niliamua nikapumzike, lakini sikutaka kupumzika bila kufanya kitu fulani, hivyo nikaamua kwenda shule, nikawa naishi maisha ya kawaida kabisa bila walinzi, nilikuwa najipikia, nafua na hata kunyoosha nguo zangu mwenyewe, lakini sikuwa na nia ya kuongeza elimu ili niwe rais,” alisema.

      “Urais tena basi, kwa sababu ya umri na nimeshakuwa kiongozi kwa muda mrefu. Kwa sasa tuna mzee Kikwete, bado ana miaka saba, tumwombee heri, lakini itakapofika muda huo, tutaangalia, ila binafsi sitaki tena kuwania nafasi hiyo,” alisema Sumaye.

      Sumaye hadi sasa ni waziri mkuu pekee mstaafu nchini aliyetumikia nafasi hiyo kwa miaka 10 mfululizo, chini ya serikali ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    6. #5
      Rev. Kishoka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th March 2006
      Location : USA
      Posts : 4,352
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      243
      Likes Given
      185

      Default CCM Haina Uzalendo!

      Wakati Kolimba aliposema CCM imekosa dira na mwelekeo, walimkalisha chini Dodoma na kupitia vitisho na hata hongo akapata mshituko na kupoteza maisha yake.

      Natamka wazi kuwa CCM haina Uzalendo!

      Zaidi ya kuwa ilishapoteza dira na mwelekeo tangu ilipokumbatia Azimio la Zanzibar, CCM tangu wakati huo imepoteza Uzalendo.

      Tulipigana vita dhidi ya Wakoloni na mamluki mpaka makaburu. Ukweli ni kuwa adui wa maendeleo ya Tanzania ni CCM.

      Waliowajamaa China, Urusi, Cuba, Korea na kwingineko pamoja na kuingia katika mfumo mpya wa uchumi na demokrasia, wameweka Uzalendo mbele.
      CCM wanaendelea kuuza nchi na kukosa Uzalendo, hawana hata woga au aibu.

      CCM haitufai Watanzania, CCM si Wazalendo, CCM ni makuwadi wa Mabepari na Wanyonyaji!
      Amani Iwe Nanyi,

      Camerlengo

      Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka

      "Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun

      'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,487
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16306
      Likes Given
      8390

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Je chama tawala chaweza kukosa uzalendo? na mzalendo ni nani hasa?
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    9. #7
      Rev. Kishoka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th March 2006
      Location : USA
      Posts : 4,352
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      243
      Likes Given
      185

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Mzee Mwanakijiji,

      CCM chama tawala inajipende nafsi yake kwanza. Ibara ya 15.1 inasema hivyo. Matendo ya CCM na viongozi wake ni dhahiri si kwa manufaa ya Taifa bali manufaa ya CCM hivyo kwa mfumo wa kisiasa tulionao CCM haina Uzalendo.

      Sikupata tafsiri kamili kwa kiswahili lakini merriam-webster inatupa tafsiri kwa kiingereza maana ya Uzalendo na Mzalendo.

      Main Entry: pa·tri·ot Pronunciation: \ˈpā-trē-ət, -ˌät, chiefly British ˈpa-trē-ət\ Function: noun Etymology: Middle French patriote compatriot, from Late Latin patriota, from Greek patriōtēs, from patria lineage, from patr-, patēr father Date: 1605 : one who loves his or her country and supports its authority and interests

      Main Entry: pa·tri·ot·ism Pronunciation: \ˈpā-trē-ə-ˌti-zəm, chiefly British ˈpa-\ Function: noun Date: circa 1726 : love for or devotion to one's country
      Amani Iwe Nanyi,

      Camerlengo

      Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka

      "Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun

      'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"

    10. #8
      Rev. Kishoka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th March 2006
      Location : USA
      Posts : 4,352
      Rep Power : 2557
      Likes Received
      243
      Likes Given
      185

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Wikipedia wanaendelea kutoa ufafanuzi wa Uzalendo

      Patriotism denotes positive and supportive attitudes to a 'fatherland' (Latin patria < Greek patris, πατρίς), by individuals and groups. The 'fatherland' (or 'motherland') can be a region or a city, but patriotism usually applies to a nation and/or a nation-state. Patriotism covers such attitudes as: pride in its achievements and culture, the desire to preserve its character and the basis of the culture, and identification with other members of the nation. Patriotism is closely associated with nationalism, and the terms are often used synonymously. Strictly speaking, nationalism is an ideology - but it often promotes patriotic attitudes as desirable and appropriate. (Both nationalist political movements, and patriotic expression, may, yet need not, be negative towards other people's 'fatherland').
      Patriotism has ethical connotations: it implies that the 'fatherland' (however defined) is a moral standard or moral value in itself. The expression my country right or wrong—perhaps a misquotation of the American naval officer Stephen Decatur, but also attributed to Carl Schurz—is the extreme form of this belief. Patriotism also implies that the individual should place the interests of the nation above their personal and group interests. In wartime, the sacrifice may extend to their own life. Death in battle for the fatherland is the archetype of extreme patriotism.
      Amani Iwe Nanyi,

      Camerlengo

      Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka

      "Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun

      'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"

    11. #9
      Kibunango's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2006
      Location : Tampere
      Posts : 6,802
      Rep Power : 44129
      Likes Received
      368
      Likes Given
      1424

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Naona BAK sie mzalendo, kwani amepindisha sana kichwa cha hiyo habari....
      Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problem,
      But, if you think again, neither does milk."
      Vituko Vya Zenj

    12. #10
      Kinto's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 105
      Rep Power : 654
      Likes Received
      4
      Likes Given
      7

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Sumaye naye kama ni muumini wa uzalendo ilitakiwe aulizwe kwa nini aliwahi kutamka kuwa "kama mtu anataka mambo yake yamnyookee aingie CCM"....mie naona ana tu-enjoy tu, Sumaye hana lolote la kuikosoa CCM wakati yeye ameshiriki dhambi zao nyingi, ni sawa na Basil Mramba leo aliyekuwa anakosoa Sera za Biashara na Viwanda wakati anachangia bungeni wakati yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara juzi tu...Watu kama hawa wanatakiwa kusutwa mchana kweupe...Tunayapa hasara masikio yetu kuwasikiliza.

    13. #11
      Mwiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Posts : 4,593
      Rep Power : 2084
      Likes Received
      223
      Likes Given
      19

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Mnapoambiwa CCM imepoteza dira haina maana ya jina ila hao viongozi na waongozwa wote hawajui wanachokifanya,walichonacho ni kila mmoja kutafuta njia za kuiba akimbie au ajiuzulu.
      Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.

    14. #12
      Hofstede's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2007
      Posts : 3,604
      Rep Power : 21340
      Likes Received
      981
      Likes Given
      988

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Quote By Rev. Kishoka
      Wakati Kolimba aliposema CCM imekosa dira na mwelekeo, walimkalisha chini Dodoma na kupitia vitisho na hata hongo akapata mshituko na kupoteza maisha yake.

      Natamka wazi kuwa CCM haina Uzalendo!

      Zaidi ya kuwa ilishapoteza dira na mwelekeo tangu ilipokumbatia Azimio la Zanzibar, CCM tangu wakati huo imepoteza Uzalendo.

      Tulipigana vita dhidi ya Wakoloni na mamluki mpaka makaburu. Ukweli ni kuwa adui wa maendeleo ya Tanzania ni CCM.
      Waliowajamaa China, Urusi, Cuba, Korea na kwingineko pamoja na kuingia katika mfumo mpya wa uchumi na demokrasia, wameweka Uzalendo mbele.
      CCM wanaendelea kuuza nchi na kukosa Uzalendo, hawana hata woga au aibu.

      CCM haitufai Watanzania, CCM si Wazalendo, CCM ni makuwadi wa Mabepari na Wanyonyaji!
      Take five REV

    15. #13
      Selous's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2008
      Posts : 1,257
      Rep Power : 830
      Likes Received
      84
      Likes Given
      59

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Quote By Kinto
      Sumaye naye kama ni muumini wa uzalendo ilitakiwe aulizwe kwa nini aliwahi kutamka kuwa "kama mtu anataka mambo yake yamnyookee aingie CCM"....mie naona ana tu-enjoy tu, Sumaye hana lolote la kuikosoa CCM wakati yeye ameshiriki dhambi zao nyingi, ni sawa na Basil Mramba leo aliyekuwa anakosoa Sera za Biashara na Viwanda wakati anachangia bungeni wakati yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara juzi tu...Watu kama hawa wanatakiwa kusutwa mchana kweupe...Tunayapa hasara masikio yetu kuwasikiliza.
      Hivi hili gazeti au redio wana agenda gani na Sumaye? Wameshindwa kumuuliza swali kama hili au?

    16. #14
      Selous's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2008
      Posts : 1,257
      Rep Power : 830
      Likes Received
      84
      Likes Given
      59

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Je chama tawala chaweza kukosa uzalendo? na mzalendo ni nani hasa?
      Mwenye uwezo wa kuonyesha uzalendo kwa vitendo?

    17. #15
      CottonEyeJoe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th January 2008
      Posts : 321
      Rep Power : 648
      Likes Received
      50
      Likes Given
      135

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Je chama tawala chaweza kukosa uzalendo? na mzalendo ni nani hasa?
      Chama Cha CCM kinauzalendo tele... tatizo ni wanachama wake..

    18. #16
      Mpita Njia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 6,684
      Rep Power : 3250
      Likes Received
      973
      Likes Given
      745

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Tatizo wanachama!?! Kwani chama kinaweza kuwa chama bila wanachama? Hivi unaweza kwua na chama safi chenye wanachama wachafu?
      I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.

    19. #17
      WildCard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 6,453
      Rep Power : 1978
      Likes Received
      1797
      Likes Given
      59

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Mwambieni ataje MALI zake kama alivyofanya mwaka 1995 halafu tuupime UZALENDO wake.

    20. #18
      CottonEyeJoe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th January 2008
      Posts : 321
      Rep Power : 648
      Likes Received
      50
      Likes Given
      135

      Default Re: CCM Haina Uzalendo!

      Quote By Mpita Njia
      Tatizo wanachama!?! Kwani chama kinaweza kuwa chama bila wanachama? Hivi unaweza kwua na chama safi chenye wanachama wachafu?
      Ninacho maanisha ni CCM in baadhi ya wanachama ambao sio wazalendo ndiyo wanafanya chama chote kionekane sio wazalendo, " Its kind of unfair to judge the whole party by the actions of a few....

    21. #19
      Lusajo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Posts : 447
      Rep Power : 662
      Likes Received
      9
      Likes Given
      1

      Angry Viongozi wetu hawana Uzalendo!

      Ninaona viongozi wetu hawana uzalendo na nchi yao kwa sababu ya matendo yao na vitu wanavyofanya wakiwa viongozi, natolea mfano vitu vichache na kama kuna vingine naomba wana JF muongezee,

      1. Mikataba ya madini ambayo imefanywa bila maslahi au kutokujali wananchi pamoja na nchi (Tanzania) halafu kinachosikitisha zaidi hata kiongozi mkuu Raisi anajua hilo na hajafanya lolote kuhusu mikataba. Mikataba ambayo pia iliwekwa wakati wa Raisi aliyepita na yeye alikaa kimya bila ya kufuatilia mikataba iliyowekwa na kibaya zaidi hata yeye mwinyewe anahusika na kujiuzia kwa bei ya kutuba migodi ya Kiwira. Sasa ninachojiuliza je hao maraisi, Mawaziri na makatibu wakuu waliokuwa wanaingia mikataba hiyo je wana Uzalendo?
      2. Kuuza karibu kila kitu kwa makampuni ya nje mfano Kilimanjaro Hotel, na mashirika mengine mengi. kwani Wa-Tanzania hatuwezi kuendesha kitu chochote? au kwa sababu viongozi hawana uzalendo na wanajiona hawawezi kuongoza ndio maana wanaona wageni ndio wanafaa?
      3. Viongozi kupokea misaada ya ki-Chama mf CCM walipokea Mil 400 kwa ajili ya UVCCM, ni kwa nini huwa hawafanyi hivyo mara nyingi kwenye mambo ya maendeleo? mara nyingi ni watu wa kawaida wanaofanya hivyo ili kusaidia watu kwa nini viongozi hawafanyi? na wakati wa kampeni wanatumia hela nyingi kutoa t-shirts, khanga na pilau badala ya kutoa mambo ya maendeleo? mf Trekta. Je ni kwa sababu hawana Uzalendo?
      4. Kununua vitu vya zamani/takataka, vitu vilivyotumika na vibovu vinanunuliwa kwa bei ambayo ni kubwa kuliko bei ya kitu kipya, mf rada, helkopta na magari ya kijeshi, ndege za ATCL, mitambo ya RDC/Dowans?. Kuna siku hapa JF niliwahi kuuliza bei ya mtambo kama wa Dowans nilipewa bei ya mtambo mpya na wenye waranty within 1 hour, kweli wanashindwa kupata vipya? au hata si waje kuuliza hapa? au ndio hivyo kwa sababu ya kukosa Uzalendo?-- Naomba kuuliza hivi magari wanayoletewa wabunge yanakuwa mapya au yamechoka? (kama mapya kwa sababu ni ya kwao ndio maana?)
      5. Nimesoma humu leo kwamba Waziri Mkuu analalamika/anaongelea kuhusu magari ya kifahari 800 yaliyoagizwa na sio kitu cha maendeleo kama ma-trekta ambayo yangesaidia wananchi, je kiongozi aliyeagiza na kupitisha hayo magari kuagizwa hana uzalendo?
      6. Viongozi wengine familia zao zinaishi nje ya nchi mf Mgonja. Ni kweli hawa watu wanauzalendo? na kwa nini wanapewa uongozi?
      7. Wabunge wetu baada ya kuchaguliwa tuu walidai mishahara mipya/ mikubwa na marupurupu na vitu vingine na wakati wakijua kwamba mishahara ya wananchi ni midogo na haiwatoshelezi, je kweli hawa viongozi wana uzalendo?


      -hii kitu sijui ni kwa Wa-Tanzania woote au ni nini? nakumbuka wakati najiandaa kuingia UDSM (ingawa sikusoma hapo) wanafunzi wengi walisema wakipewa mikopo hawana mpango wa kuirudisha na walitoa sababu nyingi nyingi kwa nini wasilipe!, je ndiyo akili ambayo viongozi wengi wanaingia nayo wakiwa madarakani? ni ukosefu wa uzalendo au ndivyo wa-Tanzania tulivyo tukiwa nje ya uongozi tuna kelele ila tukiingia kwenye uongozi uzalendo unatushinda na kuanza kuwa ccm (chukua chako mapema)?
      -Mambo mengi yanapitishwa Bungeni na ni wabunge wachache wanasimama na kupinga, je wabunge wasio pinga mambo ambayo hayana faida kwa Taifa/wananchi hawana Uzalendo!.

    22. #20
      Lole Gwakisa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2008
      Posts : 2,959
      Rep Power : 1132
      Likes Received
      462
      Likes Given
      330

      Default Re: Viongozi wetu hawana Uzalendo!

      Lusajo , naungana na wewe kwa asilimia mia moja na moja.
      Uongozi wa nchi hii sasa hivi unakosa maadili yanayo hitajika kwa ajili ya kuongoza wananchi.
      Mwalimu alisema ili kuendelea twahitaji vitu vinne
      1 watu
      2 ardhi
      3 siasa safi
      4 uongozi bora

      Mwalimu aliona mbali, na huu si ukomunisti wala usoshalisti.
      Tatizo kubwa kati ya viongozi wetu ni kutokuwa na dira ya uongozi wa umma.
      Sasa hivi kuna
      - oungozi wa kurithishana,
      -uongozi wa kujinuafaisha(kuuziana nyumba,miradi kupelekwa kwa walio kwenye madaraka)
      -uongozi ambao umekaa madrakani(baadaya kurithishana) muda mrefu mno, hivyo kuanza wizi,ulaghai, mikataba ya kujinufaisha n.k.
      Hii inayoitwa grand corruption ambayo mheshimiwa JK anaishughulikia sasa hivi ,ni jitihada za kutatua mapungufu makubwa yanayo tokana na kukosekana na utashi wa uongozi wenye uadilifu.

    23. Study Abroad
    Page 1 of 2 12 LastLast

    Similar Topics

    1. JKT na Uzalendo; Uzalendo kwa Nani?
      By Nyota Ndogo in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 13
      Last Post: 2nd September 2011, 16:56
    2. Replies: 13
      Last Post: 25th March 2011, 22:48
    3. Eti Uzalendo!!!
      By Twilumba in forum Sports
      Replies: 3
      Last Post: 17th March 2011, 11:22
    4. Uzalendo ni ni?
      By engmtolera in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 0
      Last Post: 7th December 2010, 07:07

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...