Duh, Mulugo analiaibisha Taifa, Tanzania ilitokana na muungano wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe.... nani amemuandalia huyu hii hotuba? Mungu wangu, anakuwaje waziri wa Elimu huyu ilihali yeye mwenyewe Elimu yake ina walakini? Hawezi hata kulocate Zimbabwe katika ramani ya dunia?
update: Kuna makosa mengi ukiachilia mbali hilo la Zimbabwe. Katika speech yake anaanza na Tanzania ilizaliwa mwaka one nineteen sixty four. Wewe unaifahamu hiyo 1-1964? lakini cha ziada anasema NACTE inaoffer master na PhD. Wewe unaifahamu NACTE ni nini? NACTE inatolea wapi hizi degree? Yaani at the level of waziri wa elimu huwezi kutofautisha NACTE, TCU na vyuo vikuu? What are you doing katika wizara ya elimu kama vitu vidogo kama hivi kwako ni shida?
Kwa level ya waziri wa wizara ya elimu alitakiwa awe na uwezo wa kufafanua vizuri nini ni nini katika elimu ya Tanzania. Kwa watu ambao hawajui NACTE ni nini wanaweza kudhani ni chuo kikuu. Na wengi watakuwa wanashangaa sana kwamba ni chuo kikuu gani hicho kinachopigiwa chapuo kiasi hicho na Naibu waziri ilihali kuna vyuo vikuu vingine vingi nchini vinavyo award hiyo master na PhD. Ulikuwa ni wajibu wake kudefine NACTE na kueleza institution zinazounda NACTE na namna ambavyo NACTE inafanya kazi ya kuassure quality ya hizo institutions, na si ku award Master na PhD.
Picha kwa hisani ya global publishers

Reply With Quote


Follow Us Here