Hivi kweli United States of Africa ndiyo ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili bara la africa?
Hivi kweli United States of Africa ndiyo ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili bara la africa?
Mimi ninaamini kuwa kwa Afrika kuungana kunaweza kuwa njia mojawapo ya kuondoa matatizo ya Africa. Africa ikiungana itakuwa taifa moja lenye nguvu duniani. Africa ikiwa nchi moja tutaweza kuwa na sauti moja kwenye soko la dunia kwa mazao yanayotoka Africa hasa mali asili kama vile madini. Nina imani pia kuwa kama Africa ikiungana vita ya wenyewe kwa wenyewe itapungua. Tunasikia kwa mfano kuwa kabla ya kuungana nchi ambazo sasa zinaunda USA zilizokuwa zinatwangana, lakini sasa baada ya muungano wao vita haipo. Mimi ninaunga mkono Afrika tuungane. UMOJA NI NGUVU. Mataifa makubwa yanajua kuwa kama nchi za Afrika zitaungana, Afrika itakuwa na nguvu na ndiyo maanda huwa wanafanya kila njama kututenganisha. Mfano mdogo ni kufa kwa ile iliyokuwa Jumuia ya Africa Mashariki. Baada ya kuona kuwa ile jumuia ilikuwa inafanikiwa Kiuchumi, nchi kubwa zilitafuta njia ya kuisambaratisha. Naomba kutoa hoja.
Am always dreaming of this!
Nasikia Tz ishatia ngumu kuingia kwenye Umoja huo endapo utafikiriwa kuundwa. Kama wanaukataa huu kwanini wanakimbilia ule wa EAF?
Kazi ipo!
Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' |Click HERE for Details
Mimi sioni kama kuungana ni ufumbuzi. Kinachohitajika ni nguvu ya uchumi, siyo muungano wa kisiasa. Ukiangalia Afrika utaona kuwa uchumi wetu ni kukatika katika, hivyo itakuwa ngumu sana kuwa na muungano ambao ni endelevu. Otherwise itakuwa ni nguvu ya soda.
.....They may forget what you said, but they will never forget how you made them feel....
Viongozi wa Afrika wamekuwa na kasumba, yaani wakisikia Europe wameamua kuungana basi wanasema sisi tunachelewa nini? Hivi wanafahamu EU muungano wao uko namna gani? Wazungu wakiwaambia unganeni hata hawaulizi tena wanasema ndio mfumo endelevu, endelevu kwa nani? Europe wanapopanga sera wanapanga kwa maslahi yao sio yetu. Waliigawanya Africa ili watutawale vizuri na walifanikiwa.
Matakwa yao ya wakati ule yamekwisha hivi sasa wanataka tuungane ili waweze kutumia rasilimali zetu vizuri kwa sababu wanafahamu kukiwa na nchi ambazo ziko stable watapata matatizo baadaye hivyo ni lazima kutuweka wote katika same level kwa kisingizio cha kutusaidia. What Europe does is to create conducive atmosphere for their endeavours.
Dua la kuku halimpati mwewe
Take note:
Hatua muhimu kufikia muungano wa kweli (unaohusu watu)
1: Kila Mtu aunganishe akili zake (Nina mashaka na utimamu wetu afrika)!
2: Akili za watu wote ziunganishwe (Bara moja, Fikra moja)
(Source: Own opinion)
USA waliungana baada ya kupitia hatua hizo, waliungana baada ya kuwa na maendeleo (japo states hazikulingana kiuwezo), waliungana ili kuimarisha nguvu za uchumi kutokana na uelewa wao!
Afrika bado ina matatizo mengi, bila shaka tukiungana sasa TWAUNGANISHA MATATIZO YETU YAKUE!! Consequences za ubinafsi, ulafi, ubadhilifu, ukabila, etc etc ZITAMALIZA Afrika!!
Ni bora kuungana, lakini ni kitu gani ambacho waafrika twatakiwa tuunganishe sasa??? AKILI NA FIKRA ZETU Bila shaka, kisha mengine yatafuata!!
Kwa sasa ingetosha kuimarisha ushirikiano wa kimasoko, lakini hata hilo halifanyiki kwani mawakala wa neo-colonialism bado wamejaa ktk serikali nyingi za kiafrika, bahati mbaya wengi wao hata hawajijui kama ni mawakala!
"More than 40 years of African Independence have offered to the world a sad spectacle of a continent looted and humiliated with the complicity of its own sons and daughters."
-- L. D. Kabila.
Tanzania je?
Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo
Hivi Kabila nani ali asasinate yeye?
Maana MUGABE alimpa tafu sana kupambana Mganda na Mnyarwanda waliokuwa wakipewa tafu na marekani.
Sasa MTOTO WAKE NAYE AKACHUKUA MADARAKA.
N yeye VIPI?
Sasa naweza kuona kuwa labda hata nchi yetu ilikuwa HATARINI!
Mungu aepushie mbali!
Kwani kitendo cha BENDERA ZETU VZ ZA USA!
Utata!
"One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato
Survival is a roots reggae album by Bob Marley & The Wailers released in 1979.
In the song Africa Unite, Marley proclaims Pan-African solidarity. The song "Zimbabwe" is a hymn dedicated to later-independent Rhodesia. The song has been performed at Zimbabwe's Independence Celebration in 1980, just after the official declaration of Zimbabwe's independence. "Zimbabwe" is seen as an unofficial national song.
Survival was primarily called Black Survival to underscore the urgency of African unity, but the name was shortened to prevent misinterpretations of the album's theme. Marley originally planned to publish Survival as the first part of a trilogy, followed by Uprising in 1980 and Confrontation in 1983.
In South Africa the album has been partly censored (scratched with knives on arrangement of the local governments).
NB:This might be "HISTORY ON THE MAKE!"
"One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato
Mwenye LYRICS ZA AFRIKA UNITE NA ZIMBABWE WAZIMWAGE HAPA ILI MJADALA UANZE KUNOGELE!
NB:Wale waliokuwa wakidai MANDELA ALISHATOLEWA KWENYE TERRORIST WATCH LIST WALIKOSEA!
KWANI NIMEONA HAPA WAMETANGAZA KWENYE MSNBC KUWA MAREKANI NDIO WAMEFANYA HIVYO SASA HIVI!
Sasa sijui wangejua kuwa huwezi kumwambia mwafrika kitu cha kufanya wakati shujaa wao mnamwita GAIDI!
Kwani kama MADIBA mwenyewe angepingana nao...Basi wangeweza kumsweka ndani kwa mara nyingine!
"One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato
Jmushi..sijui tufanye nini na wewe...
[email protected]
Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji
Post yako sikuielewa yote sawasawa. Kabila aliuwawa na mmoja wa askari waliokuwa vipenzi vyake mwenyewe. Kulitolewa maelezo kuwa vijana wale walikuwa wamepigana vita kwa nguvu sana kwenye jeshi la Kabila kwa ajili ya kumng'oa Mobutu. Baada ya Mobutu kuanguka na Kabila kuingia madarakani, inasemekana kuwa "aliwasahau" vijana wale, ndipo wakaamua "kumrudi." Katika hali ya kusikitsha sana, mpango wa kumwua Kabila ulifanywa na ndugu yake mwenyewe.
Kuhusu mapambano ya Rwanda, Zimbabwe, na Uganda ndani ya Kongo ilikuwa ni kwa ajili ya dhahabu. Mugabe alikuwa akizitaka, wakati Kagame naye anazitaka na Museveni naye anazitaka. Sina uhakika na kuhusika kwa marekani kwenye vita ile ingawa kuna habari za Andrew Young, na familia ya Rais George H. W. Bush kuwa na connections na biashara ile ya dhahabu wakati wa utawala wa Mobutu.
Sikuielewa hiyo point yako ya mwisho kuhusu Tanzania kuwa hatarini na bendera ya TZ Vs USA.
Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo
Sasa kama msimamo wa KABILA MKUBWA ulikuwa kupata sapoti ya Mugabe.
Mbona ni wazi Kabila mdogo anapata sapoti ya mmarekani anayempinga Mugabe?
Haoni kuwa MUGABE ALIMSAIDIa baba yake asipinduliwe?
"One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato
Inabidi ufahamu kuwa Mugabe alianza kubadilika mwaka 1999 baada ya kuwa ameshindwa kujenga uchumi na upinzani wa ndani dhidi yake kuanza kupata nguvu kwa vile watu wengi walikuwa hawana kazi na hali ya maisha ilikuwa ngumu kwao huku cronies wake wakiwa wananeemeka. Sina uhakika kama kweli Mugabe kumsaidia Kabila ilikuwa ni kwa ajili ya mapenzi ya amani afrika au ilikuwa ni kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kupata dhahabu zile.
Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo
CUF wanamsapoti TSIVANGIRAI!
Kiasilia na kihistoria ya nchi yetu...ccm ni wazi walitakiwa wamsapoti Mugabe.
Hata hapo sinza Mugabe unapajua...Na uhusiano wa ZANU na ccm ni wa kihistoria.
Mmarekani alikuwa anajuwa siri za kashfa za JK.
Hivyo hawezi kusema MUGABE JUU!
Kichaka alivyokuja bongo kitendo cha kushusha bendera ni kukabidhi nchi kwa marekani...Hiyo ni ITIFAKI pale inapokuja kwenye koloni lako...BENDERA YAKO HUPANDISHWA PEKE YAKE BILA YA KUWEPO YA NCHI UNAYOITAWALA.
Jinsi ulinzi wa kichaka na hao mapolisi waliosemekana kuwa ni kulinda ujasusi!
Hao wangetaka kumpa nchi mtu yoyote yule iwe CUF or whoever...Wangeweza!
Mmesahau Aristide?
Wamarekani walimpandisha ndege na akapanda mwenyewe na mtu alikuwa RAIS!
Hivyo basi huo ni uchanganuzi wangu tu. Ila naweza kuwa wrong.
Lakini jinsi mataifa ya Afrika yalivyogawanyika kwa kweli mambo yako wazi kwa wachambuzi kama sisi.
Hata Mwanawaswa mwenyewe namshangaa sana. Taifa lake kama letu...Lina mikataba mikubwa sana na UCHINA..Yenye kuhusisha makampuni.
Lakini wakati huo huo rais wake naye anampa sapoti BUSH licha ya kwamba Wachina hao hao wanaotawala uchumi wao ndio hao hao wanaompa sapoti Mugabe.
Sasa kama bado hujaona AFRIKA ILIKUWA IWAKE MOTO...Then unahitaji darasa.
"One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato
Twende mbele turudi nyuma, matatizo yetu mengi Afrika tumejitakia wenyewe, tumejaa ubinafsi mno, wengi wetu hatuoni mbele let alone mbali, tumekalia kulaumu wazungu, waarabu, wachina, wahindi n.k.
Kama tunasubiri Bush, Brown au Jintao waweke interests za Afrika mbele tutaula wa chuya! Wao wanatanguliza interests za nchi zao na ndivyo inavyotakiwa, sisi viongozi wetu wanachekelea vi- 10% huku wakigawa rasilimali zetu halafu tunageuka na kuanza kulia na akina Bush...wapi na wapi, wabaya wetu tunawajua ila tunaendelea kuwachagua kila kukicha kisa tumepewa wali, t-shirt na tujisenti! We are not serious... no wonder JF's own Nyani Ngabu has already deduced kwamba "ndivyo tulivyo"!
We are champions of our own poverty! We create it, we share it, we preserve it... - Pangu Pakavu
Bob Marley did this Song in the 1980's...imagine how relevant this song is today....this mas was Genius.
Africa Unite .....the last verses
Unite for the benefit of your children
Unite for its later than you think
Africa awaits its creators, africa awaiting its creators
Africa, youre my forefather cornerstone
Unite for the africans abroad, unite for the africans a yard
Africa, unite
Ubinafsi chanzo cha migogoro barani Afrika- JK
2008-07-02 09:42:14
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete, amesema migogoro mingi inayotokea katika bara la Afrika, husababishwa na viongozi ambao hujali maslahi yao binafsi badala ya wananchi.
Rais Kikwete aliyasema hayo juzi mjini Sharm El Sheikh, Misri, katika mkutano wa 11 wa wakuu wa nchi za AU.
Alisema migogoro mingi ikiangaliwa kwa undani inaonyesha haina sababu ya kuwepo.
``Migogoro mingi inasababishwa na sisi viongozi kwa sababu zetu ambazo nyingi hazina maslahi ya wananchi tunaowaongoza,`` alisema katika nakala ya hotuba yake iliyopatikana jijini Dar es Salaam.
Alisema wananchi wa Afrika wameteseka na kuchoshwa na migogoro ambayo ni kikwazo kikubwa cha kupatikana maendeleo katika bara hili.
``Bila amani hakuna maendeleo, sisi viongozi tunaowajibu wa kuwaondolea wananchi tunaowaongoza mateso haya,`` alisema.
Aidha, Rais Kikwete, alisema ingawa kuna dalili nzuri za kuimarika kwa uchumi katika nchi za Afrika, mafanikio hayo yanatishiwa matatizo yanayoukabili uchumi wa dunia.
Alitaja matatizo hayo kuwa ni kupanda kwa bei ya mafuta ambayo hakuna dalili zinazoonyesha kuwa yatashuka bei.
Aidha, alisema kupanda kwa bei ya vyakula ni tatizo lingine la kidunia linalosababisha nchi nyingi duniani zikiwemo za kiafrika.
Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo nchi za Kiafrika hazina budi kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano.
``Bila kushirikiana itakuwa vigumu kwa nchi zetu kushinda changamoto hizi kutokana na uchanga wetu kiuchumi,`` alisema.
Akizungumzia suala la majisafi na majitaka, Rais Kikwete alisema licha ya bara la Afrika kuwa na vyanzo vingi vya maji, takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa rasilimali inazidi kupungua siku hadi siku.
Alisema kupungua huko kunatokana na kuongezeka kwa uharibifu wa mazingira.
Aliongeza kuwa asilimia 40 ya vifo vya watoto duniani vinavyosababishwa na ugonjwa wa kuhara hutokea Afrika na chanzo chake kikuu ni watu kutumia maji yasiyo safi na salama.
Akitoa mfano, alisema takwimu zinaonyesha kuwa katika nchi 27 za kiafrika, watu watatu kati ya 10 hawapati maji safi.
``Kutokana na hali hii wananchi wanalazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma hii, na pale yanapopatikana mara nyingi maji hayo yanakuwa siyo safi na salama kwa matumizi ya binadamu na hivyo kuwa chanzo cha magonjwa ya milipuko,`` alisema.
SOURCE: Nipashe
"One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato
Chanzo cha matatizo ya Afrika ni Ndivyo Tulivyo......
Miafrika Ndivyo Tulivyo.
Follow Us Here