JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

  Report Post
  Page 16 of 24 FirstFirst ... 61415161718 ... LastLast
  Results 301 to 320 of 480
  1. Baija Bolobi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th February 2009
   Location : Bosnia
   Posts : 685
   Rep Power : 864
   Likes Received
   401
   Likes Given
   0

   Default "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Mod Tafadhali usiunganishe thread hii. Najua iko inayoripoti kifo, iko ya maswali.

   Hii inahusu majibu na revelations zilizoingia kwenye dish langu.
   ===========

   -Kamanda Barlow alikuwa na mwanamke ndani ya gari wakiwa peke yao wawili
   -Mwanamke si dada yake wala ndugu yake
   -Lilikuwa gari la binafsi na Kamanda aliendesha mwenyewe.
   -Walitoka kwenye kikao La Kairo Hotel na siyo Florida Hotel kama IGP alivyosema katika taarifa yake
   -Walipofika Kitangiri, Kamanda aliamua kumpeleka yule mama ndani kwnye uchochoro badala ya kumwacha barabarani
   -Si mara ya kwanza Kamanda kumpeleka mama yule eneo lile
   -Walipoingia uchochoroni, waliwakuta the so called "polisi jamii" wakiwa kwenye doria
   -Kamanda alishusha kioo na kuwauliza ni kina nani, na wao walimjibu kuwa ni polisi jamii.
   -Aliwahoji kwa nini wamevaa mikanda ya polisi wakati waliishazuiwa
   -Ulitokea ubishi kidogo
   -Kamanda akainua redio call kuwaita vijana wake waje kuwakamata
   -Polisi jamii wakamdaka kumnyanganya redio call hiyo na kumpiga risasi ya shingoni
   -Wakamvuta na kumlaza chini ya uvungu wa gari
   -Yule mama ndiye aliyemwita mlinzi wa RPC na kumwambia aje kumchukua "mzee" maana ameuawawa
   -Mama anaisaidia polisi hata sasa.

   MY Take:

   -Jeshi la polisi linajaribu kusafisha hali ya hewa kwa kufanya damage control
   -Mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake
   -Kuna uwezekano, polisi jamii walijua kamanda anakuja saa ile na yule mama, na walitekeleza maagizo waliyopewa
   -Kuna other underlying issues ndani ya jeshi la polisi Mwanza
   -Uchunguzi hautapata ushirikiano wa kutosha kwa sababu ya chuki kubwa kati ya jamii na jeshi hilo.

   HERI KUFIA MAWAZO YANAYOISHI KULIKO KUISHI KWA MAWAZO YALIYOKUFA.


  2. #301
   FJM's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Posts : 8,099
   Rep Power : 82810706
   Likes Received
   6092
   Likes Given
   4766

   Default Re: Exclusive: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Quote By Bukyanagandi View Post

   Mimi katika maisha yangu yote hapa TANZANIA na nje ya Tanzania sijawahi kusikia Commander wa Polisi kauwawa eti na majabazi!!! - hii inaleta picha mbaya katika TAIFA letu, we unafikili RAIA na Wageni wanapo kisikia kwamba mlinzi mkuu wa Usalama wa mkoa kauwawa na majambazi si itaonekana TAIFA letu alina USALAMA tena - TAIFA linapaswa kufanya kazi ya ziada kurudisha imani ya usalama kwa RAIA na wageni wanao tembelea TANZANIA, tukilaza damu mahasimu wetu jambo hili watalikuza out of proportion kwa kutujengea jina BAYA.

   R.I.P kamanda Barlow.

   Bukyanagandi, nilipopata habari za hayo mauaji, swali la kwanza nililojiuliza ni hili, hivi kuna RPC mwingine alishauwawa hapa Tanzania? Na hapo nikakumbuka Mexico! It is increadibly sad Tanzania tunaingia kwenye huu ukurasa wa mauaji.

   Na tutakuwa tunakosea sana kama tutaangalia haya mauaji kwa kioo cha 'mke wa mtu'. Kwanza tunatakiwa kujadili umiliki wa silaha. Hili limekuwa tatizo kubwa sana sana. Kama sikosei ni wakati wa Mkapa biashara ya silaha ilishamiri na watu wengi wanamiliki silaha. Sasa hivi karibu kila mwanasiasa (including wabunge) wanatembea na bastola! Tanganyika firearms wanafanya biashara nzuri sana siku hizi na hata kwenye maonesho wanahudhuria!.

   Pili, Jeshi la Polisi likae chini na kuangalia upya mahusiano yake na jamii.

  3. Chiya Chibi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th July 2011
   Location : Penye Oxygen
   Posts : 485
   Rep Power : 626
   Likes Received
   105
   Likes Given
   12

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Quote By Moony View Post
   Watasema ni majangili toka kenya yalikuwa yanaenda SAA NANE Island
   Yap, sure. Tusibiri, Usishangae comment yako ukaikuta mbele ya magazeti kesho, mana wapo humu wanapeluzi..!

  4. ngonani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 27th August 2012
   Posts : 1,116
   Rep Power : 693
   Likes Received
   375
   Likes Given
   305

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Ni bora jeshi la polisi likajitahidi kuwa wazi zaidi hasa kwenye zama hizi za utandawzi kuliko kufichaficha mambo ambayo tayari yanajulikana,mfano hadi leo bado wanaleta story kuwa mwanamke aliyekuwa na marehemu ni dada yake,labda kama wana maana ya dada yake kwa kuwa wote ni wachaga.Pia story za kutoka kwenye kikao ni sawa,lakini elewa hakuna kikao cha harusi kinachoenda hadi saa 9 usiku kwani wengi kwenye viako uwa ni wake za watu na watu wenye familia,vikao vingi mwisho uwa saa 4 usiku kama kikao kimecchelewa sana,ni bora polisi pia wakaeleza baada ya kikao marehemu na huyo Dorcas walienda wapi na walikuwa wanafanya nini hadi hiyo saa 9 mauti ilipomkuta,na walipokuwa walikuwa in a public place au walikuwa wamejifungia ndani N.K Hizi sio zile zama za kudanganya wananchi ,inawezekana ukweli tukaujua kabla ya polisi hawajakamilisha.

  5. KISHOKA_ZUMBU's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 4th April 2012
   Location : DAR ES SALAAM
   Posts : 146
   Rep Power : 519
   Likes Received
   41
   Likes Given
   16

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Time will tell!

  6. Meljons's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th June 2012
   Location : Arusha
   Posts : 2,333
   Rep Power : 85901559
   Likes Received
   606
   Likes Given
   854

   Default

   Quote By Rapherel View Post
   wewe ni nani 1.RPC?? 2'MAMA YULE' 3. POLICE JAMII
   Kama sio mmoja kati ya watajwa umejuaje yakiyojiri eneo la tukio??
   labda huyu mama a.k.a mwalimu wa S.Y.M Nyamagana anaweza kutujuza zaidi.


  7. christine ibrahim's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th February 2012
   Location : earth
   Posts : 10,444
   Rep Power : 314919683
   Likes Received
   3448
   Likes Given
   32752

   Default

   Quote By Moony View Post
   Mume wa mtu? THUKARI???????
   Ha ha ha

  8. Mwera's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th October 2010
   Posts : 971
   Rep Power : 765
   Likes Received
   87
   Likes Given
   3

   Default

   Quote By Mtukuru View Post
   Ati huyo jike anashikiliwa na polisi?
   ndio huyo jike anashikiliwa na polisi na kuna mtuhumiwa 1 amekamatwa na polis kwatuhuma zakuhusika na mauwaji ya barlow,sourse star tv.

  9. Thanda's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Location : Multiple Destination
   Posts : 1,917
   Rep Power : 1743
   Likes Received
   586
   Likes Given
   1552

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Polisi jamii na "flying objects"....poor Barlow.

   Unaposema polisi jamii, unamaanisha walipaswa kuwa na uniforms za kuwatambulisha. Hiyo ni pamoja na Mikanda kama ya polisi, yenye kuonesha uzawa (rangi ya bendera ya taifa). kwani kuivaa ilikuwa kosa?, Kinachonipa maswali hapo ni kuhusu silaha za moto....hapo tu.
   I am a Democratic Figure,Opposer of Non reality Proposers.
   Thanda Similane

  10. andrewk's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th April 2010
   Posts : 2,996
   Rep Power : 1193
   Likes Received
   414
   Likes Given
   118

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   kwa maelezo haya......ina maana huyo mama alikuwa na mawasiliano ya karibu na marehem, maana hata simu ya msaidizi wake alikuwa nayo!.....huyo mama ni lazima akae ndani kwa sababu 2 kubwa....usalama wake, kwani kwa vyovyote vile aliwaona wauaji, kama hahusiki ni raisi wao kumdhuru, pili, kama ni vinginevyo, ataisaidia polisi kupata taarifa muhimu

   Quote By Baija Bolobi View Post
   Mod Tafadhali usiunganishe thread hii. Najua iko inayoripoti kifo, iko ya maswali.

   Hii inahusu majibu na revelations zilizoingia kwenye dish langu.
   ===========

   -Kamanda Barlow alikuwa na mwanamke ndani ya gari wakiwa peke yao wawili
   -Mwanamke si dada yake wala ndugu yake
   -Lilikuwa gari la binafsi na Kamanda aliendesha mwenyewe.
   -Walitoka kwenye kikao La Kairo Hotel na siyo Florida Hotel kama IGP alivyosema katika taarifa yake
   -Walipofika Kitangiri, Kamanda aliamua kumpeleka yule mama ndani kwnye uchochoro badala ya kumwacha barabarani
   -Si mara ya kwanza Kamanda kumpeleka mama yule eneo lile
   -Walipoingia uchochoroni, waliwakuta the so called "polisi jamii" wakiwa kwenye doria
   -Kamanda alishusha kioo na kuwauliza ni kina nani, na wao walimjibu kuwa ni polisi jamii.
   -Aliwahoji kwa nini wamevaa mikanda ya polisi wakati waliishazuiwa
   -Ulitokea ubishi kidogo
   -Kamanda akainua redio call kuwaita vijana wake waje kuwakamata
   -Polisi jamii wakamdaka kumnyanganya redio call hiyo na kumpiga risasi ya shingoni
   -Wakamvuta na kumlaza chini ya uvungu wa gari
   -Yule mama ndiye aliyemwita mlinzi wa RPC na kumwambia aje kumchukua "mzee" maana ameuawawa
   -Mama anaisaidia polisi hata sasa.

   MY Take:

   -Jeshi la polisi linajaribu kusafisha hali ya hewa kwa kufanya damage control
   -Mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake
   -Kuna uwezekano, polisi jamii walijua kamanda anakuja saa ile na yule mama, na walitekeleza maagizo waliyopewa
   -Kuna other underlying issues ndani ya jeshi la polisi Mwanza
   -Uchunguzi hautapata ushirikiano wa kutosha kwa sababu ya chuki kubwa kati ya jamii na jeshi hilo.


  11. mtemiwaWandamba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd May 2011
   Location : MTONI RUIPA
   Posts : 450
   Rep Power : 629
   Likes Received
   83
   Likes Given
   96

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Quote By Elungata View Post
   Comment zingine zinatia kinyaa.kama nimekometi vibaya mungu anisamehe.na leo nimekaa jf masaa 12.sielewi hata huko dunia ingine mambo yameenda vipi.
   Sijui uturuki wameshakinusha huko syria.ngoja nimove site za mbali.OVER AND OUT.
   Ni NATO Uturuki ni kituo .
   Maajabu ya Kenge; anakimbia Mvua anaingia Mtoni.

  12. Mwanaweja's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th February 2011
   Posts : 3,575
   Rep Power : 1266
   Likes Received
   498
   Likes Given
   1132

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   huyu mama amejiaibisha sana maana inaonekana wale watoto alio zaa pengine alichukua fungu kwa wanaume wengine ndio waliofanya hivyo. polisi wampeleleze kwa undani anajua kila kitu wala si majambazi ni huyo mama

  13. Ndebile's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th September 2011
   Posts : 2,113
   Rep Power : 2429830
   Likes Received
   522
   Likes Given
   787

   Default

   Quote By Ruttashobolwa View Post
   Kweli kabisa ina onekana kabisa hii ishu ili pangwa kabisa na mwenye mke!

   Mke wa mtu ni sumuuu
   yaaayaayaaa,yaayaayaayaaaah
   usijribu chombezaaaaaaaaaaaaaaa
   yatakuja ya kukutee, yaaaaaaaaa
   yaliyo mkuta kamandaaaaa!
   Yayayayaayaaah.
   'Utakuja kojoa dagaaaaa...!'

  14. mtemiwaWandamba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd May 2011
   Location : MTONI RUIPA
   Posts : 450
   Rep Power : 629
   Likes Received
   83
   Likes Given
   96

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Hapa kuna mkanganyiko.Wale jamaa wanamfahamu Kamanda nje ndani ,na ndiyo maana walikuwa maeneo yale
   wakivinjari ili kazi waliyotumwa waimalize. Hapa huyo mwanamke hana makosa ila yupo chini ya ulinzi kwa usalama wake tu.
   Hapa wataalamu wa upekuzi waangalie zaidi juu ya Uhasiano wa Kamanda na Mapolisi walio chini yake, Mambo ya madili ya kibiashara
   Kati Kamanda Barlow washirika wake kama alikuwa na aina yoyote ya Biashara. Lakini kwa mwanamke mie nionavyo wamebugi step.
   Hata huyo kamanda wa Uhamiaji wala siye,
   Maajabu ya Kenge; anakimbia Mvua anaingia Mtoni.

  15. tajirijasiri's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 13th October 2012
   Posts : 773
   Rep Power : 617
   Likes Received
   277
   Likes Given
   23

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Tangu lini polisi jamii wakawa na bunduki za moto? Au mi ndo sielewi maana ya polisi jamii? Na inawezekanaje kamanda wa polisi atembee bila walinzi? Na iweje majambazi haya yawe na uhakika kiasi hiki juu ya muda na mahali atakaposimama? Na kama ni majambazi kweli yawezekanaje yakamuacha yule mwanamke akiwa hai ambaye ni shahidi tosha?
   Polisi polisi polisi kuna kitu nyuma ya pazia!

  16. Gama's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 9th January 2010
   Posts : 6,204
   Rep Power : 1815
   Likes Received
   879
   Likes Given
   1099

   Default

   Quote By Ruppy karenston View Post
   Yani waböngo kwa kushadadia vitu,haya sasa kila mtu anasema ni mke wa mtu kwa kusikia.Trust me huyo alikuwa ni dada yake kabisa and there's more to the story than just assumptions
   kwani dada yako hawezi kuwa mke wa mutu?!, nidada wa distance gani genetically?!.

  17. cooper's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th November 2011
   Posts : 321
   Rep Power : 573
   Likes Received
   59
   Likes Given
   446

   Default Re: Exclusive: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Quote By zenmoster View Post
   nadhani hii ni information ya uhakika... kuhusu polisi jamii wapo wengi sana mwanza..tena inaonekana vijana hao walitumia bunduki ya kamanda na kummaliza papo papo....ila ninachojiuliza kama kweli walitumwa why walimuacha huyo jike hai??
   Pengine walitumwa na mwenye mali

  18. issenye's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd February 2011
   Posts : 301
   Rep Power : 611
   Likes Received
   151
   Likes Given
   2

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Quote By Chitemo View Post
   Mkuu mbona unanena kwa lugha ndugu yangu, kulikoni tena.
   Pole sana kwa msiba wa kamanda wako.
   the shit on shit Thank God died there be the end of all lies and sin no longer weep henceforth, his dear wife and sons RIP. its not'm not happy for this true, but so sad

  19. Logician's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 5th November 2010
   Posts : 175
   Rep Power : 599
   Likes Received
   22
   Likes Given
   35

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Quote By kibol View Post
   ukweli uwekwe mezani watu wafahamu ila am very sorry cuz sina uhakika kama jeshi letu la polisi litafanya hivyo kwasababu mazingira ya mauaji yenyewe yamegubikwa na utata mkubwa,sasa ili kutokujivua nguo mchana kweupe kama kawaida yao usanii lazima ufanyike(mambo ya flying object),kwa uelewa wangu mdogo naona mauaji hayo yametoka na visasi,na kama kweli kamanda alikua anatembea na mke halali wa mtu,na mwenye mali alishajua we unadhani jamaa angeweza kuvumilia adi lini?mke anauma jamani,wengine wanawakatalii jamaa zao kwa kutembea na mahawara wao tu sembuse uyu mke?any way ngoja nigeukie upande wa pili,hao wajambazi wamechukua nini?walijuaje kamanda atakuwepo eneo hilo mda huo?walikua wanahitaji nini kutoka kwake?otherwise inavyoonekana hapo ni matumizi mabaya ya madaraka kuchukua mali za wanyonge though the case doesnt justify the kind of punishment awarded to him.ni maoni yangu jamani and i stand to be corrected.
   Looking beyond relationship matters would be worthwhile. How capable was he? Conspiracy is also an angle to drill on. the so-called thugs might have their own electronic devices........

  20. mwanamapinduko's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 24th January 2011
   Posts : 157
   Rep Power : 584
   Likes Received
   33
   Likes Given
   52

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   Quote By kilimasera View Post
   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow
   APIGWA RISASI SHINGONI NA WATU WASIOJULIKANA
   Frederick Katulanda, Mwanza
   SIMANZI imegubika Jiji la Mwanza na vitongoji vyake baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (55), kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa manane wa kuamkia jana.Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Said Mwema alithibitisha tukio hilo akieleza kuwa amemwagiza Kamishna wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba kwenda kuchunguza mauaji hayo.“Tunasikitishwa kwa mauaji hayo na ninawaomba Watanzania wawe watulivu wakati tukishughulikia kuwakamata watu waliohusika katika tukio hilo,” alisema IGP Mwema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.


   Mbali ya kumuua Kamanda Barlow, wauaji hao waliokuwa wamevalia makoti yanayovaliwa na watu wa ulinzi shirikishi (Polisi Jamii), walichukua na bastola ya kamanda huyo, simu mbili za mkononi pamoja na ‘radio call’ ya Jeshi la Polisi.

   Hili ni tukio la tatu kwa Ofisa wa juu wa Polisi kuuawa mkoani Mwanza. Tukio la awali lilitokea mwaka 2007, ambapo aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza, ASP Mahende aliuawa kwa kupiga risasi eneo la Bugando saa 4:00 usiku wakati akifuatilia majambazi waliokuwa wakijitayarisha kuvamia.
   Mwaka 1987, Inspekta Gamba aliuawa na majambazi katikati ya Jiji la Mwanza.
   Kamanda Barlow aliuawa wakati akiendesha gari lake binafsi, aina ya Toyota Hilux Double Cabin na wakati wa tukio hilo hakuwa na mlinzi wake kwa kuwa kamanda huyo alikuwa katika shughuli binafsi.
   Hata hivyo, mauaji hayo yamezua hisia tofauti huku wengine wakieleza kuwa ni kifo cha bahati mbaya na kwamba, wauaji walidhani ni mwananchi wa kawaida na wengine wakisema huenda ulikuwa mpango maalumu uliolenga kumwangamiza kwa kulipiza kisasi.
   Taarifa ya Mkuu wa Mkoa
   Akizungumza na waandishi wa habari jana saa 2:57 asubuhi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa kifo cha Kamanda Barlow kimetokea saa 8:00 usiku katika eneo la Kitangiri, Barabara ya Kona ya Bwiru karibu na Hoteli ya Tai Five.

   Alisema kuwa kamanda huyo aliuawa alipokuwa akimrejesha mmoja wa wanawake waliokuwa nao katika kikao cha maandalizi ya harusi ya ndugu yake.
   Mkuu huyo wa mkoa alimtaja mwanamke huyo aliyekuwa na marehemu kuwa ni Doroth Asasia Moses ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyamagana B.
   “Marehemu alikuwa katika kikao cha harusi ya anayedaiwa kwamba ni mtoto wa dada yake, Semburi Moleto kilichofanyika katika Hoteli ya Florida, Mtaa wa Rufiji. Kikao kilipomalizika tunaambiwa majira ya kati ya saa 4 hadi 5 usiku, alimchukua mwanamke huyo kama ‘lift’ ili kumsaidia kufika nyumbani kwake,”alieleza.
   Alisema kuwa alipofika nyumbani kwa mwanamke huyo aliona watu waliokuwa wakimulika tochi waliokuwa wakilalamika kuwa wameumizwa na mwanga wa taa za gari lake.
   Mkuu huyo wa Mkoa alisema walipofika katika gari, aliwauliza iwapo wanamfahamu na waliposhindwa kumjibu Kamanda Barlow alichukua radio ya mawasiliano ya kipolisi ili kuwasiliana na askari wake, ndipo wauaji hao walimpiga risasi eneo la shingo na kufariki papohapo.
   “Kamanda wetu inaonekana amefariki kutokana risasi hiyo, ambayo imemvunja shingo yake na imepigwa kutokea upande wa kiti cha abiria na kumpitia begani na kuingia shingoni,” alisema Ndikilo na kufafanua:

   “Baada ya kumuua, watu hao walipora bastola yake, ‘radio call’ hiyo pamoja na simu zake mbili za mkononi na mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kusaidia upelelezi.”

   Kilichomponza RPC
   Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinamkariri shuhuda wa tukio hilo (Dorah) akieleza kwamba, kilichomponza Kamanda Barlow ni kuwadharau wauaji hao baada ya kuona wamevalia vikoti vyenye rangi ya kijani vilivyokuwa na maandishi ya Polisi Jamii, alidhani kuwa na watu wa ulinzi shirikishi.

   Baadhi ya maofisa wa polisi wameeleza kuamini kuwa watu hao walikuwa ni Polisi Jamii ndiko kulikomponza marehemu Barlow kwa kuwa aliamini kuwa alikuwa katika mikono salama, hali ambayo ilimfanya kutojiandaa kupambana nao.
   Mwalimu Doroth
   Mwalimu Doroth aliyekuwa na marehemu wakati wa tukio hilo, ambaye kwa sasa anashikiliwa kuhusiana na mauaji hayo ni mjane wa marehemu Modest Lyimo ambaye zamani alikuwa ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), aliyefariki mwaka 1997 wakati huo Kamanda Barlow akiwa na OCD wa Kituo cha Kati.

   Lyimo alifariki na kumwacha Doroth akiwa na mtoto mmoja, lakini baadaye mwalimu huyo alizaa watoto wawili na mwanamume mwingine hivyo kuwa na watoto watatu (majina yanahifadhiwa kwa sasa).

   Eneo la mauaji
   Mwandishi wa gazeti hili alipofika nyumbani kwa Mwalimu Moses alikuta askari watatu wa jeshi la polisi wakilinda na kumkagua kila mtu aliyekuwa akiingia katika nyumba hiyo na kutoka.

   Mauaji yalivyotokea
   Mmoja wa watoto wa mwalimu huyo, Kenrogers Edwin, ambaye alishuhudia tukio hilo la kuuawa kwa Kamanda Barlow, aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa siku hiyo usiku kabla ya tukio, alipigiwa simu na mama yake aliyemwarifu kuwa alikuwa amefika na kumtaka amfungulie mlango.

   Edwin alisema kuwa anakumbuka pia katika maongezi ya simu mama yake alimweleza kwamba alikuwa akija na mgeni kwa ajili ya kutambua nyumbani anapoishi.

   Alisema kuwa wakati akifungua geti ili gari alilokuwamo mama yake (Doroth), pamoja na mgeni wao (Kamanda Barlow) liingie ndani, aliona watu wakiwa wamezunguka gari hilo.

   “Ilikuwa saa 8 usiku, nilipofungua geti ili aingie, niliona watu watatu wakiwa upande wa dereva wa gari na wawili upande mwingine aliokaa,” alisema na kuongeza:
   “Niliona wakimnyang’anya mama mkoba na simu na nilisikia wakibishana, lakini baadaye nilisikia mlio wa risasi.”
   Alieleza kwamba anakumbuka kuwa baada ya mlio huo wa risasi alilazimika kulala chini kwa kuogopa na kwamba baada ya Kamanda Barlow kupigwa risasi, wauaji hao walikimbia walipoona pikipiki ikija eneo hilo kwa kasi.

   Aliyemhudumia Baa
   Mhudumu wa baa, Benard Kanyabukala, ambaye alimhudumia Kamanda Barlow katika kikao hicho alisema kuwa baada ya kikao hicho kumalizika, kamanda huyo aliagiza sanduku moja la bia kwa ajili ya wajumbe waliokuwapo katika kikao hicho na yeye (mhudumu) alinunuliwa kinywaji aina ya Alivaro.

   “Aliomba bili na nilipompa alinifokea akidai nimemzidishia bei. Awali nilimweleza kuwa bei ya kreti ni Sh36,000, lakini kutokana na baadhi ya watu kutokunywa bia na kubadilisha vinywaji bei ilizidi na kuwa Sh40,700, ingawa baada ya kumwelewesha alilipa na kuongeza bia nyingine kwa raundi ya mwisho zenye thamani ya Sh 30,800,” alisema Kanyabukala.
   Alieleza kwamba, wakati wa kikao hicho Kamanda Barlow alikuwa akinywa bia aina ya Serengeti, lakini mara ya mwisho alipoagiza vinywaji alikunywa maji ya Kilimanjaro na waliondoka hapo saa 8:30 usiku akiwa na mwanamke mmoja.
   Mmiliki wa baa
   Mmiliki wa baa ya Florida, kilipofanyika kikao hicho, Ritha Mosha alielezea kuwa, Kamanda Barlow alifika katika baa hiyo kwa mwaliko wa Semburi Moleto, ambaye yeye na Kamanda Barlow wote ni Wachaga waliozaliwa Kijiji cha Kiyou, Tarafa ya Vunjo Marangu, mkoani Kilimanjaro.

   “Mimi ilikuwa ni mara yangu ya pili kuonana naye siku hiyo. Kijana anayetarajia kuoa alinieleza kuwa, alimwomba Kamanda Barlow amsimamie kama mzazi wake katika arusi yake na ndiye aliyesimamia kikao hicho, ndiyo aliyeongoza sala ya kufungua kikao hicho,” alieleza Ritha.
   Alisema kuwa kikao hicho kilichelewa kuanza kutokana na wajumbe kuchelewa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini hapo.
   Alifahamisha kuwa kikao hicho kilianza saa 2:21 usiku na kwamba kamanda huyo alikuwa msemaji wa familia.
   Idadi ya wanawake
   Ritha alifahamisha kuwa, kikao hicho kilitarajiwa kuwa na wajumbe 100, lakini walifika kati ya 55 hadi 60 na kati ya hao kulikuwa na wanawake wawili ambao aliwataja kwa majina ya Christina Mosha, mkazi wa Nyakato na Doroth ambaye alisindikizwa na kamanda huyo.
   Hapa polisi wataficha ukweli huyo Doroth wamwache tu. Kuna jambo kubwa liko nyuma hapo na linawahusu hao hao polisi wauaji wametafuta Achilles heel ya kamanda wakaipata wakaitumia kufanya mauaji hayo.

  21. Mhoja's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 13th August 2010
   Posts : 206
   Rep Power : 617
   Likes Received
   20
   Likes Given
   0

   Default Re: "Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

   tusubiri tuone.
   "PLEASE VISIT www.deomhoja.wordpress.com"


  Page 16 of 24 FirstFirst ... 61415161718 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...