Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

    Report Post
    Page 3 of 17 FirstFirst 1234513 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 338
    1. #1
      AL sadat's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Posts : 62
      Rep Power : 368
      Likes Received
      33
      Likes Given
      1

      Default CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Mjumbe wa Almashauri kuu na kamati kuu ya CCM captain Abdulharaman kianana amejiuzulu nafasi zota alizonazo ndani ya CCM kwa madai ya kuachana na siasa uchwara.

      Kinana amekuwa mjumbe wa NEC kwa zaidi ya miaka 22 pia amewahi kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa.

      Jumatano ndio mambo yote, baada ya NEC huenda viongozi wengi wa CCM wakahamia upinzani.

      Quote By Nnauye Jr
      Uamuzi wa Kinana kutogombea umepokewa kwa hisia tofauti lakini kuna watu wanajaribu kupotosha ....ETI NI KUACHANA NA SIASA UCHWARA...!!!!! hii hapa chini ndio sehemu ya maneno yake binafsi juu ya uamuzi wake huu....

      "SIJAGOMBEA KWAKUWA MIAKA 25 YA KUSHIRIKI KATIKA KAMATI KUU NADHANI INATOSHA NA NI VIZURI KUNG'ATUKA. NAAMINI KUNA WANACCM WENGI WAZURI WENYE SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA CHAMA. UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI NA NI WAKATI WANGU KUKABIDHI WENGINE KIJITI HIKI"

      Sasa wanaosema eti siasa uchwara wanayatoa wapi........ Uzushi mwingine ni wa ajabu sana..

      Quote By Pasco
      Mkuu Nape, kwanza asante kujitokeza mapema kuujibu ule uzushi!, lakini kusema tuu ni uzushi hakutoshi!. Ile thread unayoiita ya uzushi, inazungumzia barua Kinana aliyoiandika!, wewe unazungumzia maneno Kinana aliyoyatamka, hivyo ni vitu viwili tofauti!.

      Sasa ili kanusho lako liwe na maana, tungeshukuru kama ungetufafanulie
      1. Jee Kinana ameandika barua?.
      2. Kwenye barua hayo uliyoyasema wewe ndiyo yaliyomo kwenye hiyo barua?.
      3. Kama ameandika barua, na hayo uliyoyasema ni matamshi ya mdomo, then ile thread still stands mpaka uthibitishe hata kwenye barua, yale hayapo!.
      4. Mode, Nape akithibitisha ule ni uzushi, then funge ile thread na kumpatia muanzisha thread haki yake!.
      5. Nape, tunakushauri, karibu tena na tena sio tuu kukanusha thread za uzushi, bali pia jitokeza kujibu baadhi ya hoja valid kuhusu CCM!.

      Asante.

      Pasco.

      ****************************** *****

      UPDATE (Kutoka Magazetini)

      Mwananchi | Sept 24, 2012

      Kinana Ang'atuka!

      KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana ametangaza kung’atuka rasmi katika siasa baada ya kukitumia chama chake kwa miaka 25 akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Kamati Kuu (CC) na Kamati ya Maadili.

      Kinana ambaye amekuwa Meneja wa Kampeni za mgombea urais wa CCM tangu mwaka 1995 ulipoanza uchaguzi wa vyama vingi, alisema kwamba baada ya kutumikia chama katika nyadhifa za juu kwa robo karne sasa, ameamua kupumzika ili kuwaachia vijana waendelee kukijenga chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.

      “Nimekuwa Mjumbe wa NEC kwa miaka 25, bila shaka muda huu unatosha, kwani wanaCCM wamenipa heshima ya kuwa katika vikao vya juu vya chama kwa robo karne. Sasa ni wakati wa kung’atuka, nimetoa mchango kwa kadri nilivyoweza katika vikao mbalimbali na katika shughuli nyingi,” alisema.

      Alisema anaamini kuachana kwake na siasa hakutakuwa na madhara kwa chama chake, kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa na wanaweza kuongoza chama hicho kuelekea Uchaguzi wa 2015.

      “Uongozi ni kupokezana vijiti. Wako wanaCCM wazuri, walio na uwezo mkubwa na sifa za kutosha kuongoza. Nawashukuru wanaCCM na viongozi kwa heshima waliyonipa wakati wote huu,” alisema Kinana ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Benjamin Mkapa kwa vipindi viwili na Rais Jakaya Kikwete kwa vipindi viwili vya uchaguzi.

      Kinana alisema anajivunia kufanya kazi na marais wote wa Tanzania kuanzia Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais Kikwete kwa uadilifu mkubwa na kuheshimiana.

      ”Ushauri wangu katika vikao umekuwa ukiheshimika sana. Nimekuwa nikiheshimiwa na uongozi wote wa CCM na hata wapinzani nao tunaheshimiana. Nimesimamia kampeni za kistaarabu na ambazo zimeleta ushindi mkubwa kwa CCM tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi,” alisema.

      Kinana ambaye pia alikuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ameshauri vijana ndani ya CCM watangulize masilahi ya taifa mbele na wasikilize wananchi.

      Ni muhimu washikamane, wabuni mikakati ya kusaidia kukuza uchumi kwa haraka zaidi na kuendeleza umoja na undugu wetu,” alisema.

      Ushauri wa viongozi wapya CCM
      Kinana alishauri viongozi wapya ambao wanatarajiwa kuchaguliwa ndani ya chama chake, iwapo wataona upungufu wake wausahihishe.

      “Ni matumaini yangu kuwa watakaopata uongozi wataona upungufu na watasahihisha makosa yangu,” alisema.

      Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015, Kinana aliwaasa viongozi wasiwaze nani anafaa kuwa mgombea urais bali washughulikie kero za wananchi.

      “Bado tuna kazi kubwa ya kutekeleza Ilani. Tusiwasumbue Watanzania kuwa ni nani anafaa kuwa Rais bali tushughulikie matatizo yao. Kwa sasa ajenda ya CCM ni kutekeleza ahadi zetu katika sekta zote siyo kutafuta nani atakuwa Rais 2015," alisema na kuongeza:

      "Hata wapinzani wawaeleze Watanzania yale ambao wamedhamiria kutekeleza. Kueleza upungufu wa CCM ni mtaji mdogo kwa wapinzani, ajenda kubwa ni watafanya nini? Hapa bado wana kazi kubwa. Wanapoona upungufu wasisite kutusema,”

      Kinana ambaye ana shahada ya uzamili katika utawala na masuala ya sera kutoka Chuo Kikuu cha Harvad nchini Marekani, alisema anatarajia kufundisha na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika moja ya vyuo vikuu vya hapa nchini.

      “Baada ya kustaafu kuna mambo mawili ambayo natarajia kufanya. La kwanza ni kuona kama naweza kufundisha. Pili kusoma katika mojawapo ya vyuo vikuu vyetu,” alisema.

      Mbali na nyadhifa zilizotajwa huko juu, Kinana ametumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa muda mrefu na kupanda cheo hadi kufikia Kanali.

      Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Arusha Mjini.

      Nape alisema Kinana ni miongoni mwa wanasiasa waadilifu wa CCM ambao wamekitumikia chama kwa muda mrefu na kwa uaminifu wa hali ya juu.

      Ni kweli hajagombea, lakini kutokugombea kwake hakujafungwa milango kwa CCM kumtumia au kutumia uzoefu wake pale watakapomhitaji.

      Alisema "Kwa mfano Mwenyekiti wa CCM ana nafasi alizopewa kikatiba kuteua wajumbe wa NEC, huwezi kujua anaweza akamwona anafaa na akamteua,"

    2. FemaTV & Radio

    3. #41
      Honey K's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2008
      Posts : 628
      Rep Power : 521
      Likes Received
      67
      Likes Given
      0

      Default Uzushi dhidi ya Kinana kujiuzulu unasikitisha; mwenyewe kasema anang'atuka

      Uamuzi wa Kinana kutogombea umepokewa kwa hisia tofauti lakini kuna watu wanajaribu kupotosha ....ETI NI KUACHANA NA SIASA UCHWARA...!!!!! hii hapa chini ndio sehemu ya maneno yake binafsi juu ya uamuzi wake huu....

      "SIJAGOMBEA KWAKUWA MIAKA 25 YA KUSHIRIKI KATIKA KAMATI KUU NADHANI INATOSHA NA NI VIZURI KUNG'ATUKA. NAAMINI KUNA WANACCM WENGI WAZURI WENYE SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA CHAMA. UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI NA NI WAKATI WANGU KUKABIDHI WENGINE KIJITI HIKI"

      Sasa wanaosema eti siasa uchwara wanayatoa wapi........ Uzushi mwingine ni wa ajabu sana..

    4. #42
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,606
      Rep Power : 15261
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2866

      Default re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Aliyeleta mada kaingia mitini, hayuko hapa kujibu hoja za source ya habari. Nichangie nini kama hata moderator hajathibitisha wasiwasi wa wengi kuhusu ukweli wa habari hii? Namwona Mod Buchanan akiwamo ndani ya uzi huu kushuhudia kinachoendelea.?
      Ndahani likes this.

    5. #43
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Kumbe ni kweli the soldier with iron face has lowered down his guards?
      Janjaweed, FJM and Bondpost like this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    6. #44
      BHULULU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th June 2012
      Posts : 3,014
      Rep Power : 8379
      Likes Received
      833
      Likes Given
      696

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Ukweli utajulikana tu ni suala la mda tu!

    7. #45
      Dr F. Ndugulile's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th July 2012
      Location : Kigamboni
      Posts : 125
      Rep Power : 370
      Likes Received
      173
      Likes Given
      117

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.
      Pasco and Yericko Nyerere like this.
      Kigamboni na Tanzania kwanza

    8. Miaka 50

    9. #46
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Quote By Candid Scope
      Aliyeleta mada kaingia mitini, hayuko hapa kujibu hoja za source ya habari. Nichangie nini kama hata moderator hajathibitisha wasiwasi wa wengi kuhusu ukweli wa habari hii?
      Mbona nasikia kaamua kuachia ngazi kwa hiari kuwapisha wengine? Huko mbele kuna taflani na wengine hawataki kuwa sehemu ya historia ya yatakayotokea.
      FJM likes this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    10. FJM
      #47
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,172
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5321
      Likes Given
      4587

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Quote By Dr F. Ndugulile
      Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.
      Naaaaaah... ile habari nyingine yaweza kuwa taarifa za kina za 'kung'atuka'. Hii kitu inakwenda mrama.

    11. #48
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,744
      Rep Power : 1317
      Likes Received
      720
      Likes Given
      147

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Nape labda kwa mdomo kuna baadhi aliwaambia kuwa CCM inaendekeza siasa uchwara na kwenye barua kaandika vingine

      Je kuna ukweli kwamba kuna kundi kubwa mumewatibua watatimuka
      FJM likes this.

    12. #49
      Njowepo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Location : Santiago
      Posts : 7,606
      Rep Power : 22057
      Likes Received
      997
      Likes Given
      784

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Nape on a serious note Kinana deep moyoni mwake anakerwa na jinsi CCM inavyoendeshwa. Naona ameamua kungatuka ili asiwe sehemu huo ubovu.

      Nilitegemea angejiuzuru mara tuu baada ya uchaguzi wa 2010 bse kuna mambo yeye kama yeye yalikuwa yanamkera. Ila nampongeza ni zamu ya damu changa sasa kushika hatamu za chama
      WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

    13. #50
      Dark City's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2008
      Location : Roaming
      Posts : 11,555
      Rep Power : 23552
      Likes Received
      6973
      Likes Given
      11321

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Nape anaweza kuweka source ya maneno hayo? au naye anataka tuyaamini kavu kavu kama mleta thread ya mwanzo?

      Wote wameshindwa kuweka barua ya Kinana na hakuna anaweza ku-claim kwamba aaminiwe kavu kavu bila ushahidi!!
      jmushi1, MpendaTz, genekai and 3 others like this.
      "WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE....LOOKING BEYOND THE 31 OKTOBA 2010 LANDMARK"

      Retired Maj Gen DC (1947)...[email protected]

    14. #51
      Gaspery Lasway's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2011
      Posts : 1,143
      Rep Power : 619
      Likes Received
      242
      Likes Given
      22

      Default re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Jamaa anapima mashabiki

    15. #52
      Gaspery Lasway's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2011
      Posts : 1,143
      Rep Power : 619
      Likes Received
      242
      Likes Given
      22

      Default re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Jamaa unapima mashabiki,ushawachonganisha hapo unawaendesha utakavo kwa kuwapima upeo,kweli si kila aliye jamiiforum ni great thinker

    16. #53
      mhondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2011
      Posts : 828
      Rep Power : 3808
      Likes Received
      172
      Likes Given
      36

      Default re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Nnauye Jr amekanusha kuhusu chanzo cha kung'atuka. Ipo thread nyingine inayotoa ufafanuzi.

    17. #54
      marejesho's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : MULA
      Posts : 3,365
      Rep Power : 13047
      Likes Received
      1556
      Likes Given
      1137

      Default re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Naona Nape kaanzisha uzi mwingine kukanusha 'kuachana na siasa uchwara'!!Ila ni kweli Mzee Kinana hagombei!!!

    18. FJM
      #55
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,172
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5321
      Likes Given
      4587

      Default re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Kwa maelezo ya Nape ni kweli Kinana ameng'atuka. Ila anasema (Nape) kuwa taarifa iliyoletwa imepotishwa. Link ya uzi wa Nape hii hapa.

      http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...sikitisha.html

      Quote By Candid Scope
      Aliyeleta mada kaingia mitini, hayuko hapa kujibu hoja za source ya habari. Nichangie nini kama hata moderator hajathibitisha wasiwasi wa wengi kuhusu ukweli wa habari hii? Namwona Mod Buchanan akiwamo ndani ya uzi huu kushuhudia kinachoendelea.?

    19. #56
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,190
      Rep Power : 5038
      Likes Received
      2425
      Likes Given
      2224

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Uamuzi mzuri wa Kinana. Kila lenye mwanzo halikosi mwisho.
      "To greed, all nature is insufficient"

    20. #57
      IsayaMwita's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2008
      Location : Tarime
      Posts : 1,046
      Rep Power : 871
      Likes Received
      82
      Likes Given
      6

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Quote By Dr F. Ndugulile
      Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.
      Mh. tujipe muda kuna mengi nyuma ya pazia, tafakari there is something behind the screne

    21. #58
      Dark City's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2008
      Location : Roaming
      Posts : 11,555
      Rep Power : 23552
      Likes Received
      6973
      Likes Given
      11321

      Default Re: CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

      Ni habari za kweli hiz ila bado kuna utata wa nini kakisema...

      Haya hapa ni maneno ya Nape mwenyewe HAPA!

      Quote By Nnauye Jr
      Uamuzi wa Kinana kutogombea umepokewa kwa hisia tofauti lakini kuna watu wanajaribu kupotosha ....ETI NI KUACHANA NA SIASA UCHWARA...!!!!! hii hapa chini ndio sehemu ya maneno yake binafsi juu ya uamuzi wake huu....

      "SIJAGOMBEA KWAKUWA MIAKA 25 YA KUSHIRIKI KATIKA KAMATI KUU NADHANI INATOSHA NA NI VIZURI KUNG'ATUKA. NAAMINI KUNA WANACCM WENGI WAZURI WENYE SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA CHAMA. UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI NA NI WAKATI WANGU KUKABIDHI WENGINE KIJITI HIKI"

      Sasa wanaosema eti siasa uchwara wanayatoa wapi........ Uzushi mwingine ni wa ajabu sana..

      ##nakuomba mods msiunganishe hii thread na ile ya uzushi tafadhali!
      "WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE....LOOKING BEYOND THE 31 OKTOBA 2010 LANDMARK"

      Retired Maj Gen DC (1947)...[email protected]

    22. #59
      NasDaz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2009
      Location : Ushenzini
      Posts : 3,057
      Rep Power : 5345
      Likes Received
      1412
      Likes Given
      1646

      Default Re: Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

      Quote By Nnauye Jr
      Uamuzi wa Kinana kutogombea umepokewa kwa hisia tofauti lakini kuna watu wanajaribu kupotosha ....ETI NI KUACHANA NA SIASA UCHWARA...!!!!! hii hapa chini ndio sehemu ya maneno yake binafsi juu ya uamuzi wake huu....
      "SIJAGOMBEA KWAKUWA MIAKA 25 YA KUSHIRIKI KATIKA KAMATI KUU NADHANI INATOSHA NA NI VIZURI KUNG'ATUKA. NAAMINI KUNA WANACCM WENGI WAZURI WENYE SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA CHAMA. UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI NA NI WAKATI WANGU KUKABIDHI WENGINE KIJITI HIKI"

      Sasa wanaosema eti siasa uchwara wanayatoa wapi........ Upuuzi mwingine ni wa ajabu sana..
      ##nakuomba mods msiunganishe hii thread na ile ya uzushi pls
      Quote By Dr F. Ndugulile
      Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.
      Mbona hili mmefanya mapema hivi kuja kukanusha?! I can sense the sign of RED FLAG! Nafahamu wazi kwamba udhaifu mkubwa wa CCM ni ama kupuuza moja kwa moja au kuchelewa kuchukua hatua za kujibu tuhuma mbalimbali dhidi ya chama hususani zinazotolewa hapa JF! Au ndo tuseme Idara ya Uenezi imezaliwa upya na kwa kasi mpya?! Hata hivyo msisahau kwamba, mashahidi wa tuhuma za Richmond, including Dr. Msabaha ndani ya kiapo alisema vingine na nje ya kiapo "akawang'ata sikio" kwamba mzigo ni wa bwana mkubwa na yeye anatolewa kafara tu....so, inawezekana kabisa Kinana kwenye barua ameandika kwamba anang'atuka kupisha damu changa na nje ya barua akawang'ata watu sikio kwamba hawezi kuendelea na siasa uchwara!
      August, Peasant, Njowepo and 4 others like this.
      I am a free thinker! It's only my free thinking that leads me, to what am commenting. Thus, I've no doubt that today I can be your fellow but tomorrow your enemy, and the agent between us being my comments!! So, If today we agree with cheers, tomorrow we'd not disagree with jeers!

    23. #60
      Elba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : Ubungo
      Posts : 305
      Rep Power : 502
      Likes Received
      86
      Likes Given
      60

      Default

      Mbona nape unajaa upepo wakati ni kweli kaachana na siasa uchwara za CCM! Huu ndio ukweli...

    Page 3 of 17 FirstFirst 1234513 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...