Ndiyo wakuu, heshima kwenu. Katika kutimilika kwa kauli ya mjinga akijitambua,mwelevu upo matatani ,hali imeendelea kujidhihirisha wiki hii ktk jimbo la Busanda, mkoani geita.
Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Mawazo Seleman, diwani wa zamani wa kata ya Sombetini, Arusha, aliye jivua gamba na kuvaa gwanda ni kuwa katika kata ya Katoro walivuna wanachama 150, kata ya Kaseme ktk vijiji vya kaduda na magenge walivuna wanachama 200, jana ktk kata ya Lwamugasa walivuna wanachama 200, jana hiyo hiyo jioni katika maeneo ya Kilombero moja walivuna wanachama 78 na Kilombero mbili walivuna wanachama 110.
Leo mashambulizi yata endelea katika kata ya Bulela. Hivyo kwa uhalisia tu M4C wiki hii imevuna jumla ya wanachama wapatao 738. Haya ni maeneo ya vijijini ndani kabisa ambapo ccm chini propaganda za Nape wamekuwa wakijidai kuwa ni mtaji kwao. Je kwa mrejesho huu bado ccm ina mtaji vijijini? Zaidi tuta endelea kujuzana kuhusu harakati hizi. Naomba kuwasilisha.

Reply With Quote



Follow Us Here