Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 40 of 40
    1. #1
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      "Salaam kwa mkt wa CHADEMA MKOA WA MOROGORO.

      Dada yangu habari za jumapili, kwanza nikukumbushe kwamba leo ni siku ya ibada kwa kuwa natumai wewe ni mkristo, tufanye siasa, lakini daima mungu mbele.

      Nasikitika kutuma salamu hizi kwako, ambazo ni aibu kwako wewe kama mwenyekiti na pia chama chako kwa ujumla,

      Ndg mwenyekiti, makada wa chama chako ndg Juma Tembo na mwanasheria asiyejitambua ndg Tarimo wakiwaongoza vijana wengine katika siku ya juz, majira ya mchana, mtaa wa mkwajuni, kata ya kichangani, wilaya ya moro mjini, makada hawa walileta vurugu za hatari na zisizo na msingi wowote MSIBANI kwa kugombea mwili wa marehemu Amina Juma ambaye mama yake mzazi bi Annastazia ni kada wa chama cha mapinduzi CCM.

      Mmoja kati ya makada niliowataja hapo juu ambaye inasemekana ana mahusiano ya karibu na ya undani na bi Mchilo ambaye ni mama mdogo wa marehemu ndiye aliyekuwa kichochez kikubwa katika vurugu hizo za kijinga, ndg huyo kwakuwa alitoa hela ya mchele na nyama kwa ajili ya shughuli za mazishi, akichanganya na mahusiano yake ya karibu na familia ya marehemu alitumia nafasi hiyo kutaka kuugeuza msiba huo kama jukwaa la kisiasa na eneo la kisiasa la kufanya kampeni za CHADEMA.

      Juma tembo na tarimo waliagiza magari meupe Pick up nne zilizoandikwa M4C, ambazo kwa wakati wote zilikuwa zikirandaranda msibani, kilichotokea...

      1 wakati wa chakula makada hao waliwapanga vijana wa chadema kugawa chakula huku wakimuuliza kila anayekuja kuchukua chakula ajitambulishe kwamba yeye ni wa chama gani? Na akisema yeye ni wa CCM ananyimwa chakula, akisema chadema anapewa chakula kingi. Na akisema hana chama basi anaambiwa kuanzia leo ajiunge na CHADEMA.

      2 matusi na kashfa nzito zilitolewa na makada wa chadema hadharani huku watu wakiwasikiliza, matusi na kashfa hizo ziliekezwa kwa diwan wa kata hiyo komandoo John Waziri(ccm) Mhe Aziz Abood mbunge wa kudumu milele jimbo la morogoro mjini(ccm) viongoz mbali mbali wa ccm, na serikali ngaz ya wilaya mkoa mpaka taifa.

      3 makada wako walishinikiza, waligombea, walitukana na kulazimisha mwili wa mtoto huyo upandishwe kwenye moja ya magari yaliyoandikwa M4C.

      Chama cha mapinduz ccm kilipata mafanikio makubwa katika msiba huo kwa kuweza kuzidhibiti vurugu hizo za chadema kikiongozwa na katibu wa ccm wa kata hiyo bi subira mashaka, vijana wa uvccm wakiongozwa na kamanda wa kata hiyo ndg Hamis Zikatimu, ambao kwa kiasi kikubwa walihakikisha mwili wa mtoto wa kada wa ccm bi Annastazia unapandishwa kwenye gari la ccm. Kama mwenyewe alivyotaka na kusema huku akilia kwamba "nataka maiti ya mwanangu ipandishwe kwenye gari la ccm)

      Viongoz wa ccm wa kata hiyo walichukua hatua hiyo ya kuleta gari la ccm MAHINDRA kutoka ccm wilaya, baada ya kuona mlolongo wa magari ya chadema yakiwa yanazunguka hovyo hovyo msibani kinyume cha taratibu.

      Hekima na busara za vijana wa ccm ndizo zilizo sababisha kutokumwagika damu msibani hapo kwani wananchi wengi walikuwa wameshachukizwa na vurugu hizo za Chadema. Tuliwasihi greengard wetu wawe wapole na watumie hekima zaid ili watofautiane kimaadili mbele ya jamii na vijana wa chadema. Vijana wa ccm walifanikiwa kwa hilo.

      Ndg mwenyekiti, hivyobasi, naomba umkanye ndugu Juma Tembo ambaye mara zote amekuwa akikichafua chama chenu hapa morogoro kwa siasa zake za vurugu, akiwa mgombea wa ubunge jimbo la morogoro mashariki ambapo alishindwa vibaya na mgombea wa ccm ndg Innocent Kalogerez, Juma Tembo mwaka huo wa 010 alipata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa greengard wa ccm ambapo ghafla akilitumia gari la chadema aliuingilia msafara wa ccm katikati ambao ulikuwa umetoka kwenye kampeni kata ya sultan, nikiwa ndani ya gari la greengard pamoja na katibu wa uvccm w beatrice tuliwaruhusu vijana wamtandike vizuri sana juma tembo, na vijana wakiongozwa na massawe walimpa discpline ya nguvu mpaka kakimbilia polisi ambapo alionekana mjinga kwa kuingilia msafara ambao haumuhusu.

      Mwenyekiti waambie vijana wako kwamba, watambue

      1 msibani sio eneo la kufanya siasa, ni eneo la majonz na linalowakutanisha watu wa iman tofaut, si vyema kugawa watu kwa misingi ya vyama na siasa.

      2 kutukana viongoz wa nchi ni kuvunja sheria za nchi, ni upuuz, ni ushamba wa siasa, ni ujinga uliopitiliza na kutaka kuifanya nchi yetu isitawalike. Hatujengi, tunabomoa

      3 Demokrasia isiyofuata sheria ni janga na maafa kwa taifa, marazote chama chenu kimekuwa ni chanzo cha vurugu, maandamano na mikutano isiyofuata taratibu, matusi na makelele yasiyo na maana, si vyema

      Dada yangu mkt, waelimishe makada wako na umwambie Juma na wakili tarimo, iwe mwanzo na mwisho, wamevumiliwa sana, siku nyingine wakileta vurugu msibani kama vile, hakika vijana wetu watazirejesha nidhamu zao kwa vitendo. Juma anajua vizuri sana

      Jumapili njema..."
      By Mdau - Morogoro.

      Familia zimegawanyika katika mazishi ya mtoto kutokana na itikadi za kisiasa. - YouTube

      My take: Iwapo jitihada hizi zingeelekezwa kwenye upatikanaji wa maji safi au uboreshaji wa shule zetu na huduma za afya pamoja na miundombinu, tungekuwa mbali sana kimaendeleo. Badala yake watu wanashindana kununua chakula misibani na kupeperusha bendera zao kwenye magari ya kubeba jeneza!!!

      Ni wapi tunakwenda?
      Last edited by ZeMarcopolo; 23rd September 2012 at 15:01.
      "To greed, all nature is insufficient"

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      Uwezo Tunao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 6,897
      Rep Power : 2294
      Likes Received
      1154
      Likes Given
      1495

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Mkuu ZeMarcopolo,

      Nimeguswa sana na hii picha hapa chini, je wewe? Unajua wakati mwingine 'what goes around comes around' kama ambavyo wahenga walivyopata kunena. Na ukweli kama huo ndio kama hivi umejidhihirishia hapa chini - ukatili kitu kibaya sana!!!!!!

      Hii picha kidoooogo inanikumbusha unyama wa polisi kumburuta chini na gari umbali wa kilometa moja kijana mwenzetu hadi alipoaga dunia pale Tabora mapema mwaka huu.

      Mwenye taarifa zozote na maendeleo ya ile kesi atujuze humu kilichoendelea zaidi.

    4. #22
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By Uwezo Tunao

      Mimi pia nimeguswa sana na ukatilii huu. Wahusika wote wanastahili kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
      "To greed, all nature is insufficient"

    5. #23
      tenende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 1,086
      Rep Power : 589
      Likes Received
      216
      Likes Given
      492

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By King Kong III
      Hapo nimekupata mkuu,naunga mkono hoja...Kwamba jitihada hizo zingefanywa kwenye maendeleo tungekuwa mbali sana.
      Mkuu umeingizwa mkenge na Ze marcopolo. Yeye yupo pale anatumikia DINI. Anazusha na kurubuni kila mtu amuonaye. Ingekuwa taarifa hii haijulikani angeichafua CDM kwa uzushi wake!. Wao hela walizoendea msibani Ghana, Malawi na Ethiopia kwa nini hawakuzitumia kwa maendeleo hapa nchini?. CDM wakienda msibani nongwa, wasipoenda nongwa!.. Sababu za Udini, Ukabila na ukanda zitatafutwa mpaka zipatikane.
      Last edited by tenende; 24th September 2012 at 07:55.

    6. #24
      jingalao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th October 2011
      Location : kikonga
      Posts : 728
      Rep Power : 530
      Likes Received
      128
      Likes Given
      27

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      jk alivyoenda kwenye msiba wa Kanumba sikusikia hizi chokochoko.

      KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

    7. #25
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By jingalao
      jk alivyoenda kwenye msiba wa Kanumba sikusikia hizi chokochoko.

      KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

      Hakwenda kutundika bendera ya chama cha siasa...

      Kwa hisani ya mtu wa Tanzania, Hahahhahahahahahaha...
      "To greed, all nature is insufficient"

    8. Miaka 50

    9. #26
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By tenende
      Mkuu umeingizwa mkenge na Ze marcopolo. Yeye yupo pale anatumikia DINI. Anazusha na kurubuni kila mtu amuonaye. Ingekuwa taarifa hii haijulikani angeichafua CDM kwa uzushi wake!. Wao hela walizoendea msibani Ghana, Malawi na Ethiopia kwa nini hawakuzitumia kwa maendeleo hapa nchini?. CDM wakienda msibani nongwa, wasipoinda nongwa!.. Sababu za Udini, Ukabila na ukanda zitatafutwa mpaka zipatikane.
      Wewe mbona uko desperate sana. hapa swala la udini, ukabila na ukanda limetoka wapi. Jaribu kutulia chini and take some deep breaths. Take it easy, tunajenga nyumba moja ya nini kugombania fito?
      "To greed, all nature is insufficient"

    10. #27
      tenende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 1,086
      Rep Power : 589
      Likes Received
      216
      Likes Given
      492

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By ZeMarcopolo
      " Hekima na busara za vijana wa ccm ndizo zilizo sababisha kutokumwagika damu msibani hapo kwani wananchi wengi walikuwa wameshachukizwa na vurugu hizo za Chadema. Tuliwasihi greengard wetu wawe wapole na watumie hekima zaid ili watofautiane kimaadili mbele ya jamii na vijana wa chadema. Vijana wa ccm walifanikiwa kwa hilo.

      Ndg mwenyekiti, hivyobasi, naomba umkanye ndugu Juma Tembo ambaye mara zote amekuwa akikichafua chama chenu hapa morogoro kwa siasa zake za vurugu, akiwa mgombea wa ubunge jimbo la morogoro mashariki ambapo alishindwa vibaya na mgombea wa ccm ndg Innocent Kalogerez, Juma Tembo mwaka huo wa 010 alipata mkong'oto wa nguvu kutoka kwa greengard wa ccm ambapo ghafla akilitumia gari la chadema aliuingilia msafara wa ccm katikati ambao ulikuwa umetoka kwenye kampeni kata ya sultan, nikiwa ndani ya gari la greengard pamoja na katibu wa uvccm w beatrice tuliwaruhusu vijana wamtandike vizuri sana juma tembo, na vijana wakiongozwa na massawe walimpa discpline ya nguvu mpaka kakimbilia polisi ambapo alionekana mjinga kwa kuingilia msafara ambao haumuhusu.

      Jumapili njema..."
      By Mdau - Morogoro.

      Familia zimegawanyika katika mazishi ya mtoto kutokana na itikadi za kisiasa. - YouTube

      Ni wapi tunakwenda?
      Kamanda Juma Tembo na Mwenyekiti Suzan kiwanga na wana CDM woote wa mkoa wa MOROGORO mkipigwa na green guard au mwana - CDM akiuawa, watafuteni viongozi wa GREEN GUARD hawa wafuatao: beatrice, Massawe na huyu "ZE MARCOPOLO" mtambueni mapema ili mjue pa kuanzia.

    11. #28
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By tenende
      Kamanda Juma Tembo na Mwenyekiti Suzan kiwanga na wana CDM woote wa mkoa wa MOROGORO mkipigwa na green guard au mwana - CDM akiuawa, watafuteni viongozi wa GREEN GUARD hawa wafuatao: beatrice, Massawe na huyu "ZE MARCOPOLO" mtambueni mapema ili mjue pa kuanzia.
      Kweli kuku mgeni hakosi kamba mguuni...
      "To greed, all nature is insufficient"

    12. #29
      Janjaweed's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2010
      Posts : 3,620
      Rep Power : 1129
      Likes Received
      1391
      Likes Given
      1541

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By dudus

      Haikupatwa kunenwa kwamba akufaaye wakati wa dhiki ndiye rafik wa kweli? Au, mahali pengine haikuandikwa kwamba " ... na jirani yangu ni nani?" CCM bana hata haya hamna?
      mahangaiko tu hayo......... myoyoni hawana raha mkuu, kwani kila wanachoona kinawashangaza walikua wapi kukifanya??
      dudus likes this.
      Kama Vipi nipotezee tu; ntakuboa....

    13. #30
      tenende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 1,086
      Rep Power : 589
      Likes Received
      216
      Likes Given
      492

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By ZeMarcopolo
      Wewe mbona uko desperate sana. hapa swala la udini, ukabila na ukanda limetoka wapi. Jaribu kutulia chini and take some deep breaths. Take it easy, tunajenga nyumba moja ya nini kugombania fito?

      Ze Marcopolo, ungekuwa unazungumza haya maneno kutoka moyoni mwako, usingeingiza uzushi hatari kwa amani ya nchi yetu!. Hata kama unatafuta watu waichukie CDM huwezi kuzusha kuwa waligawa chakula kwa kuwauliza wewe ni chama gani!. Ukileta propaganda za kijinga tutakujibu sawa sawa na ujinga wako. UDINI, UKANDA na UKABILA niliozungumzia najua wote mnajua ni propaganda hatari mnayoitumia kudhoofisha vyama vya siasa. Najua kama mgekuwa serious kutafuta umoja na mshikamano hizi propaganda msingezileta.

    14. #31
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By tenende
      Ze Marcopolo, ungekuwa unazungumza haya maneno kutoka moyoni mwako, usingeingiza uzushi hatari kwa amani ya nchi yetu!. Hata kama unatafuta watu waichukie CDM huwezi kuzusha kuwa waligawa chakula kwa kuwauliza wewe ni chama gani!. Ukileta propaganda za kijinga tutakujibu sawa sawa na ujinga wako. UDINI, UKANDA na UKABILA niliozungumzia najua wote mnajua ni propaganda hatari mnayoitumia kudhoofisha vyama vya siasa. Najua kama mgekuwa serious kutafuta umoja na mshikamano hizi propaganda msingezileta.
      Mkuu, soma vizuri habari and mind the punctuation. Hayo unayonilaumu siyo maneno yangu. Wapi nimesema kuna mtu aligawa chakula kwa kuuliza affiliation ya chama?
      Again, swala la udini, ukabila na ukanda limetoka wapi?
      "To greed, all nature is insufficient"

    15. #32
      Janjaweed's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2010
      Posts : 3,620
      Rep Power : 1129
      Likes Received
      1391
      Likes Given
      1541

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By ZeMarcopolo
      Wewe mbona uko desperate sana. hapa swala la udini, ukabila na ukanda limetoka wapi. Jaribu kutulia chini and take some deep breaths. Take it easy, tunajenga nyumba moja ya nini kugombania fito?
      tangu lini mnajenga nyumba moja??

      umesahau wewe unajenga nyumba yako na mkeo wakati wengine wanajenga taifa??

      dont push for credits that you havent earned buddy!
      tenende likes this.
      Kama Vipi nipotezee tu; ntakuboa....

    16. #33
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By Janjaweed
      tangu lini mnajenga nyumba moja??

      umesahau wewe unajenga nyumba yako na mkeo wakati wengine wanajenga taifa??

      dont push for credits that you havent earned buddy!
      Sawa mkuu nimekusoma. Tuko pamoja...
      Janjaweed likes this.
      "To greed, all nature is insufficient"

    17. #34
      tenende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 1,086
      Rep Power : 589
      Likes Received
      216
      Likes Given
      492

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Mie si mgeni na utaratibu huo na tena nimefanya mara nyingi sana. Ukiweza fuatilia. Hata hivyo msimamo uliouweka hauna tofauti na maneno ya huyo uliyemtambulisha kuwa mdau!. Pili, Source ni mdau? Huyo mdau yeye haijui jamii forum mpaka umletee post ya kishabiki namna hii? Post hii ulipokuwa unaileta mbona hujaonesha msimamo wako kuhusu mambo machafu kama Green Guard kupiga watu? Kweli nia yetu iwe kuchochea watu wapigwe? Ndugu yangu, WEWE NI MTANZANIA MWENZANGU - NAKUHESHIMU, ila mawazo yako ya leo siyakubali!.

      Quote By ZeMarcopolo
      tenende umeshindwa kuelewa.
      Nilichofanya mimi ni kuleta habari. Mimi sio mwandishi wa habari husika.
      Kuleta habari JF kutoka vyanzo mbalimbali ni jambo la kawaida hapa JF, wewe inawezekana hujui hilo kutokana na ugeni wako.
      Ukitaka kusoma maoni yangu angali kwenye "my take".

    18. #35
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By tenende
      Mie si mgeni na utaratibu huo na tena nimefanya mara nyingi sana. Ukiweza fuatilia. Hata hivyo msimamo uliouweka hauna tofauti na maneno ya huyo uliyemtambulisha kuwa mdau!. Pili, Source ni mdau? Huyo mdau yeye haijui jamii forum mpaka umletee post ya kishabiki namna hii? Post hii ulipokuwa unaileta mbona hujaonesha msimamo wako kuhusu mambo machafu kama Green Guard kupiga watu? Kweli nia yetu iwe kuchochea watu wapigwe? Ndugu yangu, WEWE NI MTANZANIA MWENZANGU - NAKUHESHIMU, ila mawazo yako ya leo siyakubali!.

      Tenende, its ok kutokukubaliana na mawazo yangu ya leo. Ni vizuri kujadili tofauti zilizopo katika fikra zetu ili tuweze kuzitambua tofauti hizo na kujifunza kuziheshimu pale inaposhindikana kubadilishana...
      "To greed, all nature is insufficient"

    19. #36
      tenende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 1,086
      Rep Power : 589
      Likes Received
      216
      Likes Given
      492

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Bado hata haya utayakana kuwa si maneno yako? Unadhani CDM wao wajinga wajipeleke msiba usiowahusu? U - CCM - wa mama wa marehemu hauifanyi CDM kuwa chama kinachovamia misiba. Fuatilia ujue CDM walimfuata nani, usilete ushabiki!

      Quote By ZeMarcopolo
      Hakwenda kutundika bendera ya chama cha siasa...

      Kwa hisani ya mtu wa Tanzania, Hahahhahahahahahaha...
      Last edited by tenende; 23rd September 2012 at 23:33.

    20. #37
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By tenende
      Bado hata haya utayakana kuwa si maneno yako? Uandhani CDM wao wajinga wajipeleke msiba usiowahusu? UCCM - wa mama wa marehemu hauifanyi CDM kuwa chama kinachovamia misiba.
      Tenende, unadhani ni jambo sahihi kwa washabiki wa chadema kwenda kupeperusha bendera za chama msibani?
      "To greed, all nature is insufficient"

    21. #38
      tenende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 1,086
      Rep Power : 589
      Likes Received
      216
      Likes Given
      492

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By ZeMarcopolo
      Tenende, unadhani ni jambo sahihi kwa washabiki wa chadema kwenda kupeperusha bendera za chama msibani?
      NI SAHIHI kabisa!.. kwanza asante kwa maoni yako!, bendera za chama zinaweza kutumika pale ambapo aliyefariki au mzazi wake ni mwanachama wa chama husika. Hata kitaifa, aliyekuwa kiongozi wa kitaifa, au mwakilishi wa taifa, bendera ya taifa hutumika. Morogoro marehemu alikuwa mtoto, na pande mbili za wazazi ni CCM na CDM. Msiba huu haukuwa wa kugombea bendera wala mavazi ya ushabiki wa vyama bali mgogoro huo uliibuka kutokana na vyama viwili kupingana. Huu si msiba wa kwanza kwa vyama vyote viwili kuwa na magari na mavazi ya vyama na tena utaratibu huu utaendelea kuwepo!. Hili linakuwa kosa iwapo mtu atapeleka bendera za chama msiba usiomhusu, LAKINI HUU wa MOROGORO ASIDANGANYE MTU kuwa CCM pekee walikuwa na haki!. CCM walikuwa na haki kwenda kumfariji yule mama, lakini si sawa KUGOMBEA ukuu wa MSIBA!

    22. #39
      tenende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 1,086
      Rep Power : 589
      Likes Received
      216
      Likes Given
      492

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Any way! Ze marcopolo huu si ugomvi wala kazi ya kutafuta mshindi!. Mimi sioni shida mtu akiishambulia CCM, CDM, au CUF, kwa udhaifu wake lakini si uzushi. Nashukuru kwa mchango wako.

    23. #40
      Janjaweed's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2010
      Posts : 3,620
      Rep Power : 1129
      Likes Received
      1391
      Likes Given
      1541

      Default Re: Misiba yawa mtaji wa kisiasa...

      Quote By ZeMarcopolo
      Sawa mkuu nimekusoma. Tuko pamoja...
      Thanks, at least we are agreeing on one thing

      that is why i ma not a politician, coz my family comes first, i hate politicians who pretend to put country first and support the oppressors with all their ability, and yet they think their conscious is clear
      Kama Vipi nipotezee tu; ntakuboa....

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...