Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Uasi wanukia CCM

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 36 of 36
    1. BAK
      #1
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,535
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8279
      Likes Given
      8280

      Default Uasi wanukia CCM

      Uasi wanukia CCM
      • Vigogo watishana waziwazi

      na Waandishi wetu
      Tanzania Daima
      HALI ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imevurugika, ikiwa zimebaki siku mbili tu kabla ya kuanza kwa vikao vya Halmashauri Kuu (NEC), hapo Septemba 24, kwa ajili ya kuteua majina rasmi ya watakaowania nafasi za uongozi wa juu wa chama hicho.

      Habari za kuaminika zimebainisha kuwa, uhasama mkubwa umezikumba kambi mbili kubwa za wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, wale wa mtandao unaoaminika kukubalika na mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho, na ule unaojinasibu kuwa ni wapambanaji wa ufisadi.

      Uchunguzi wa Tanzania Daima kwa wiki nzima, umebaini kuwepo kwa vikao vingi vya siri baina ya makundi hayo, huku kundi moja likiwa limejizatiti kuhakikisha kuwa majina ya wagombea kutoka kundi jingine hayapitishwi.

      Hata hivyo, katika hatua inayoonesha hali mbaya ya mahusiano baina ya wajumbe wanaounda uongozi wa juu wa CCM ngazi ya taifa, mmoja wa wajumbe ambao wameomba tena kuwania nafasi ya NEC na ambaye anashikilia nyadhifa kadhaa za chama na serikali, alimtolea maneno makali katibu wa CCM wa mkoa mmoja (jina linahifadhiwa) baada ya kukutana uso kwa uso katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam juzi majira ya jioni.

      Kigogo huyo alisikika akimwonya katibu huyo kukaa mbali naye na kumwagiza akawaambie waliomtuma kufuta mara moja mbinu chafu walizoziandaa dhidi yake, la sivyo angelazimika kuanika kile alichokiita uchafu wote anaoujua dhidi yao kwa Watanzania.

      Kadhalika kiongozi huyo alikaririwa akisema kuwa haoni hasara tena ya kuendelea kuwa ndani ya chama kinachoongoza kwa majungu, fitina na chuki, huku akificha siri nyingi za uongo wa viongozi wengi.
      “Kawaambie, tena nakutuma ukawaambie hao waliokutuma, sitaki kufuatwa. Iwe mwanzo na mwisho, vinginevyo nitawaanika kwa Watanzania, ingawa najua mwenyekiti atasikitika.

      “Msione nimenyamaza, mkadhani sijui kile mnachokifanya dhidi yangu. Jaribuni kufuta jina langu, muone kama nanyi sitawaanika kwa Watanzania, wawajue mlivyo wachafu na sijui mtaweka wapi nyuso zenu,” alisikika akisema kabla hajapanda gari lake na kuondoka.

      Wakati hayo yakijiri, kauli iliyotolewa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, mapema wiki hii kwamba hatakubali jina lake likatwe bila maelezo, imekikoroga vibaya chama hicho, na kuna taarifa kwamba kundi kubwa la viongozi kutoka mkoani Mara, linajiandaa kuchukua maamuzi magumu, ikiwa kikao cha Halmashauri Kuu kitabariki kuondolewa kwa jina lake.

      Habari kutoka mjini Musoma, zimedai kuwa hatua yoyote ya kukatwa kwa jina la mbunge huyo na mwanasheria maarufu hapa nchini, itakuwa mwanzo wa anguko kubwa la CCM mkoani humo hata kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

      Mkono hata hivyo, hakuwa tayari kuzungumzia jambo hilo alipotakiwa kufanya hivyo na gazeti hili, wala kukiri ama kukana kujua juu ya kuwepo kwa kundi la viongozi wanaomshabikia, waliojiandaa kuchukua maamuzi magumu ikiwa jina lake halitapitishwa.

      Mbunge huyo alikaririwa akieleza kushangazwa kwake na kukatwa kwa jina lake katika ngazi ya mkoa, na kudai kwamba hatakuwa tayari kukubali kirahisi hali hiyo, bila kuambiwa kosa lake katika ulingo wa siasa ndani ya chama hicho lililosababisha hali hiyo.

      Mtifuano mwingine uko katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu ambako mahasimu wakubwa wawili wanachuana.
      Mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni inadaiwa anafanyiwa njama za kuenguliwa jina lake ikidaiwa kuwa ni kutokana na uhasama mkubwa alionao dhidi ya mbunge wa sasa, Dk. Titus Kamani.
      Wawili hawa wameshitakiana mahakamani kwa tuhuma za kutaka kuuana, zinazomkabili Dk. Kamani. Hali hiyo inakuja huku jina la Dk. Chegeni likidaiwa kukatwa na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

      Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Busega, Samuel Ngofilo, alikiri kuwepo kwa njama hizo alizoziita chafu zinazolenga kumchafua Dk. Chegeni ili asipitishwe na NEC kugombea wilayani humo.
      Dk. Chegeni pamoja na wagombea wengine watatu, ambao ni Kashen Fanuel, Miknes Mahela na Amos Onesmo, ndio wanawania u-NEC kupitia Wilaya ya Busega, katika Mkoa mpya wa Simiyu.

      “Kuna njama chafu zimeanza kufanywa kwa lengo la kumchafua Dk. Chegeni ili asipitishwe kugombea NEC katika wilaya yetu ya Busega. Kauli ya vijana Busega tunaka NEC itende haki. Dk. Chegeni ni mchapa kazi hodari na CCM wanalijua hili.
      “Kwa kutambua uchapakazi, ushawishi na uhodari wa kujenga na kutetea hoja kwa maslahi ya chama na jamii alionao Chegeni, ndiyo kilichotusukuma tumchukulie fomu ya kugombea NEC. Sasa kama NEC watakata jina lake, tuko tayari kuchukua maamuzi magumu. Hatuwezi kusema kama tutaenda Peoples au la, maana bado mapema mno,” alisema.

      Aidha, Ngofilo alimtuhumu Dk. Kamani kwa madai ya kuandika barua kwenda kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, akiomba jina la Dk. Chegeni lisipitishwe kwenda ngazi ya taifa.
      “Siasa za namna hii sisi vijana wa Busega hatuzitaki. Tunachotaka ni kujenga chama chetu kwa kuwa na viongozi makini, hodari na imara katika kupigania maendeleo ya chama na Watanzania. Tunaisihi sana NEC ipuuze uzushi wa aina yoyote ile, na ituletee majina ya watu wanaokubalika kijamii,” alisema Ngofilo.

      Alipopigiwa simu yake ya kiganjani juzi ili atoe ufafanuzi juu ya tuhuma hizo, Dk. Kamani alipokea simu na kusema kwa kifupi: “Baadaye” kisha akakata simu.
      Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms), akiombwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, alikaa kimya hadi tunakwenda mitamboni.

      Kwa upande wake, Dk. Chegeni alipotafutwa kwa simu yake ya kiganjani ili azungumzie suala hilo la kuundiwa njama chafu kwa lengo la kumchafua, hakuweza kupatikana ambapo baadaye taarifa zilidai kwamba yuko safarini nchini Colombia.
      Kutoka mjini Kahama, habari zinasema kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), jana waliungana na kushiriki katika hafla ya kuaga wanafunzi wa darasa la saba katika shule binafsi ya Kwema Modern.

      Sitta ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, inaelezwa kuwa alialikwa ikiwa ni moja ya mikakati ya pamoja na Lembeli, huku kukiwa na taarifa kwamba majina ya wawili hao ni miongoni mwa yale yatakayofyekwa kuwania nafasi ya ujumbe wa NEC.

      Duru za kisiasa zimebainisha kuwa wawili hao sasa wameamua kushikamana kwa dhati dhidi ya hila zinazoonekana kufanywa na viongozi wenzao ndani ya CCM, ambazo inadaiwa zimechangiwa na kile kinachoelezwa kauli zao tata ambazo zimekuwa mtaji kwa vyama vya upinzani.

      Wakati Sitta akikwaruzana na wenzake ndani ya CCM, Lembeli amekuwa na ‘ugomvi’ wa muda mrefu na Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Hamis Mngeja.
      Imeelezwa kuwa wawili hao, wanawania uenyekiti wa chama hicho mkoa.
      Jijini Dar es Salaam, kumezuka tafrani kutoka kwa baadhi ya wagombea wanaodai kuwa majina yao yalienguliwa na kuwekwa mengine kwa maslahi binafsi ya makundi katika chama hicho.

      Katika uchaguzi uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii, kulizuka purukushani kubwa zilizotaka kusababisha kuchapana makonde kutokana na kuwepo kwa mizengwe katika uteuzi wa nafasi za uongozi.
      “Jina la kada aliyewahi kuwa Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na aliyewahi kuwa diwani katika Kata ya Ubungo liliondolewa kutokana na kushinikiza arudishwe Diwani wa Makurumla, Rajab Hassan,” kilisema chanzo chetu.

      Kwa maelezo ya chanzo hicho, katika vikao vyote vya mkoa, sekretarieti, kamati ya maadili ya mkoa na kamati ya siasa ilimpendekeza kada huyo aliyeondolewa kwa kuwa ana sifa zote, lakini Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, John Guninita, alishinikiza jina la kada huyo kukatwa kwa maslahi binafsi ya makundi Mkoa wa Dar es Salaam.
      Chanzo hicho kiliongeza kuwa, hata katika nafasi ya mkutano mkuu wa taifa, kulikuwa na matatizo kwa kuwa baadhi ya wajumbe walikuwa na maslahi yao binafsi.

      Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abilahi Mihewa, alisema kuwa anadhani kuwa wale wanaolalamika hawajui utaratibu wa vikao vya chini kuwa vinashughulika na matengenezo.
      Mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ametishia kuwazuia waandishi wa habari watakaotangaza habari ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa juu, kuingia ndani ya viwanja vya makao makuu ya chama hicho.
      Nape akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa wamewaelekeza walinzi wao kutoruhusu waandishi wa chombo kilichoandika habari za barabarani kuingia ndani ya jengo hilo.

      Alisema kwa muda wa siku tatu wamekuwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ambapo kazi yake kubwa ni kupokea taarifa ya mapendekezo kutoka wilayani na mikoani na kuziunganisha pamoja na kuziboresha.

      Alisema nafasi ambazo ziliombwa na zitajadiliwa na vikao hivyo ni wajumbe wa NEC kupitia wilaya na wale wa Zanzibar na Tanzania Bara, nafasi ya uenyekiti, katibu uenezi na uchumi wa mkoa na wagombea kutoka jumuiya mbalimbali za chama hicho.
      we gule likes this.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    2. Study Abroad

    3. #21
      KV LONDON's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2012
      Posts : 260
      Rep Power : 396
      Likes Received
      21
      Likes Given
      220

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      CCM kuna viongoz wa ajabu sana, kwenye uchaguzi mkuu huwa wanaungana wote kuchakachua kura za wapinzani ila kwenye chaguzi za ndani ya chama huwa hawaangaliani usoni kabisa kila mtu na nafasi yake' utaskia huyu katishia huku, huyu kabeba bastola anataka kumuua mwenzake mara huyu kahama chama au anataka kuanzisha chama chake baada ya kuchezewa mchezo mchafu, wao huwa wanadai ni upepo tu utapita.
      we gule likes this.

    4. #22
      we gule's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 124
      Rep Power : 371
      Likes Received
      10
      Likes Given
      65

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Bado sijaona mpamabanaji wa UFISADI wa ukweli ndani ya CCM, walio wengi ni wanafiki baada ya kukosa aina ya maslahi wanayoyata basi huhamia kupiga vita wenzao kwa njia ya kudai wanatetea wananchi .WOTE NI WEZI,WAONGO ,WANAFIKI .

    5. #23
      Mercyless's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 449
      Rep Power : 448
      Likes Received
      90
      Likes Given
      575

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Quote By Precise pangolin
      Mpambanaji mwenyewe ni sita eti!
      Huyu naye (Sitta) anatia kichefuchefu. Kila kukicha anajidai anapambana na ufisadi, ni ufisadi upi anaopingana nao? Ajipime kama anaweza kupambana na chama kizima cha magamba ilhali akiwa ndani ya hicho hicho chama anachopingana nacho. Aache kutuona watanzania kuwa ni majuha. Kama ana nia ya dhati ahame chama akapambane nje ya ccm tutamwelewa. La sivyo akae kimya tutamwelewa zaidi.
      Precise pangolin likes this.

    6. #24
      Bubona's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st August 2011
      Posts : 278
      Rep Power : 445
      Likes Received
      53
      Likes Given
      11

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Tatizo wanafanya uchaguzi wakiwa wamegandamizwa na jinamizi la uchaguzi 2015!!

    7. #25
      kibogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Location : MBEYA
      Posts : 1,677
      Rep Power : 692
      Likes Received
      418
      Likes Given
      312

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Quote By chama
      Ndoto za alinacha hiki ni chama cha mapinduzi; waliondoka kina Mrema hapo mwendo mdundo asiyekubali maamuzi sahihi ya chama na aanze!

      Chama
      Gongo la mboto DSM
      Hayo ni maneno ya kujifaliji, uliza kenya wapi KANU siku hizi
      ''IT'S BETTER TO HAVE HIV IN BLOOD THAN HAVING CCM IDEAS IN BRAIN''

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Mwanaweja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 3,446
      Rep Power : 1108
      Likes Received
      457
      Likes Given
      923

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      ccm ndio mwisho wake wake huu sina imani kama watanusuka kwenye kiama hiki laana za watanzania lazima zionekane hapa hapa dunia wala si CDM/CUF bali wao kwa wao

    10. Ame
      #27
      Ame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Location : Global Citizen
      Posts : 1,513
      Rep Power : 1183
      Likes Received
      650
      Likes Given
      2615

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Siyo tu CCM itasambaratika bali hata Engine yao inayoongoza nchi itawaka moto hewani na mara wote mtashangaa how come! Butwaa yaja sooner than I anticipated duuh!..Hollygost over to you am tired of my country being led by witches in their coven.

      I set ablaze all the altars raised to baal the godes of Pharaoh by fire by force in the name of the most high Jesus Christ of Nazareth!

      In Jesus name I claim back my country and its people.....Father from now on expose all who by their doings are against your good will of prosperity to the people of Tanzania. I command all the fisad to start eating their flesh and drink from their own blood...Angels of God do your work from east, west, south and north gather them all; bind them and burn them to the ashes like you did in the days of Lutu and Abraham in the Cities of Sodoma and Gomora. God as you are the same yesterday today and forever; let your Glory prevail in Tanzania. Amen!

      Am in the Race to destiny - YouTube

    11. BAK
      #28
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,535
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8279
      Likes Given
      8280

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Wameyataka wenyewe ya kumkabidhi chama DHAIFU sasa chama kinasambaratika na nchi inazidi kudidimia kiuchumi. Halafu cha ajabu hakuna hata anayemkemea kwa UDHAIFU wake. Bora kizikwe rasmi tu na 2015 tupate utawala mpya nchini.

      Quote By Mwanaweja
      ccm ndio mwisho wake wake huu sina imani kama watanusuka kwenye kiama hiki laana za watanzania lazima zionekane hapa hapa dunia wala si CDM/CUF bali wao kwa wao
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    12. #29
      Daudi Mchambuzi's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 25th November 2010
      Posts : 6,175
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2994
      Likes Given
      13624

      Default Uasi wanukia CCM

      Wacha wafu wazike wafu wao.

      Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

    13. #30
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,692
      Rep Power : 903
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      ngoja nisubiri nione mie,baada ya 24,teh teh

    14. #31
      Mzalendo JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2012
      Posts : 900
      Rep Power : 530
      Likes Received
      274
      Likes Given
      212

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Fear of the unknown
      "Happiness is what you think, what you say, and what you do are in harmony"

    15. #32
      Curriculum Specialist's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2007
      Posts : 1,887
      Rep Power : 1597
      Likes Received
      557
      Likes Given
      183

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      Quote By Precise pangolin
      Mpambanaji mwenyewe ni sita eti!
      Kumbe walikuwa wanajiita wabambanaji tu, siyo wambanaji wa kweli! ha ha haaaa

    16. #33
      pilau's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th August 2012
      Posts : 1,035
      Rep Power : 547
      Likes Received
      223
      Likes Given
      74

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      ............. Kiongozi tangu miaka 40 iliyopita ..... tatizo ni kwamba wanaendelea kung'ang'ania madaraka wanajua hakuna kujiuzuru hata kama wakifanya madudu katika uongozi huku wakijisahau kwamba kuna mwisho wa uongozi, pamoja na wizi walioufanya bila kufikishwa mahakamani ndani ya miaka 60 bado wanataka kukaa humo humo.... mwisho ndio huu

    17. #34
      Manyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Posts : 1,700
      Rep Power : 716
      Likes Received
      287
      Likes Given
      258

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      “Msione nimenyamaza, mkadhani sijui kile mnachokifanya dhidi yangu. Jaribuni kufuta jina langu, muone kama nanyi sitawaanika kwa Watanzania, wawajue mlivyo wachafu na sijui mtaweka wapi nyuso zenu,” alisikika akisema kabla hajapanda gari lake na kuondoka.

      Hivi hawa ndiyo viongozi tunaowategemea, kwa hiyo anajua mauozo ya CCM lakini kwa kuwa ana cheo ndo hataki kusema huo uozo mpaka atoswe? Hii ni aibu kubwa sana kwa chama cha ki-ukoo!

    18. #35
      Elli's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Kijito-Upele
      Posts : 8,513
      Rep Power : 0
      Likes Received
      2102
      Likes Given
      1839

    19. BAK
      #36
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,535
      Rep Power : 44951
      Likes Received
      8279
      Likes Given
      8280

      Default Re: Uasi wanukia CCM

      CCM yawasuta Sitta, Lembeli
      • Nape asema kauli zao haziwezi kusikilizwa kwani hawajiamini

      na Waandishi wetu
      Tanzania Daima
      CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitishwi na baadhi ya viongozi wake ambao wamekuwa wakitoa kauli zao barabarani kwa ajili ya kulalamika na kukikosoa chama badala ya kupeleka malalamiko yao katika vikao husika.

      Kitendo cha viongozi hao kuendelea kutoa taarifa zao za malalamiko barabarani ni dalili za kutojiamini na kuonyesha udhaifu wa kuhimili mikiki ya uchaguzi ndani ya chama hicho na inawezekana wana agenda zao za siri.
      Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya chama hicho, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya vikao vya chama ambavyo vinaendelea mjini hapa.

      Licha ya Nape kutowataja vigogo hao kwa majina, lakini ni wazi kuwa walengwa ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye kwa siku za karibuni amenukuliwa akilalamikia vitendo vya ufisadi kwenye mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM na hivyo kuibua mjadala mzito kwa baadhi ya makada akiwemo Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, wakimtaka awataje kwa majina anaowatuhumu.

      Wengine waliosikika hivi karibuni wakilalamikia mchakato huo wa uchaguzi unaoendelea ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Nimrod Mkono wa Musoma Vijijini ambao inasemekena majina yao yamekatwa kwenye orodha ya wagombea, huku wakisema hapatatosha iwapo wataenguliwa kweli kimizengwe.

      Nape alisema kuwa CCM inashangazwa na baadhi ya wanachama wake ambao wanaonyesha woga wa kushindwa kuhimili mikiki ndani ya chama, hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi na badala yake wamekuwa wakitishia kujitoa kama majina yao hayatarudishwa kwa ajili ya kuchaguliwa katika nafasi zao walizoomba.

      Alisema kuwa chama hakiwezi kuwasikiliza viongozi ambao wamekuwa na tabia ya kutoa matamshi yao barabarani na kwamba kama wanataka kutoa kauli hizo, watumie fursa ya kuwasilisha hoja zao katika vikao.
      “Chama hakiwezi kusikiliza kauli za barabarani ambazo zinatolewa na viongozi hao, kama wana hoja wazilete katika vikao kwa maana nao ni viongozi, wasipofanya hivyo basi huenda wana agenda zao za siri, ambazo wanazijua wao,” alisema.

      Kuhusu baadhi ya wagombea ambao walisikika wakidai kuwa majina yao yasiporudishwa patachimbika, alisema kuwa inaonyesha ni jinsi gani hawajiamini kwani kiongozi ni lazima awe mvumilivu na mwenye kuhimili mikiki ya siasa za sasa ambazo zina ushindani mkubwa.
      “Kama kiongozi anaanza kusikia tetesi kuwa jina lake halitarudishwa halafu anaanza kusimama barabarani na kudai kuwa hapatatosha, ni wazi kuwa ni mwoga wa kuhimili ushindani, lakini nataka kusema kuwa haki itatendeka na busara zitatumika.
      “Hakuna mtu ambaye jina lake litakatwa kwa ajili ya mizengwe, bali vigezo vitazingatiwa ili kila mmoja apate haki yake, na lazima wagombea watambue kuwa kwa vyovyote vile lazima apatikane kiongozi ambaye ataweza kuongoza jumuiya husika,” alisisitiza Nape.

      Aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa wingi wa wagombea katika nafasi mbalimbali, kuna uwezekano wa kutokea msuguano mkubwa kwa wanachama kutokana na kila mmoja kutamani kushika nafasi aliyoiomba.
      “Kimsingi wanachama waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ni wengi zaidi ya mahitaji, hii ni ishara kuwa chama bado kinapendwa… kunawezekana kukatokea msuguano wa ndani kutokana na wingi wa wagombea, lakini chama kina utaratibu wa kumaliza mambo kama hayo,” alisema.

      Kuhusu vikao kwenda kinyume na ratiba, Nape alisema kuwa kutokana na wingi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, imelazimika sekretalieti kukaa siku tatu badala ya moja na kamati ya maadili ilitakiwa ikae siku moja, lakini imekaa mbili tofauti na matarajio.

      Nape alisema kutokana na wingi wa wagombea, imewalazimu vikao kuchukua muda mwingi kujadili kwa makini ili kuhakikisha haki inatendeka na kuongeza kuwa, kwa nafasi ya wenyeviti wa mikoa zinazotakiwa ni nafasi 31 ila walioomba ni 187, katibu siasa na uenezi mkoa zinatakiwa nafsi 31 walioomba pia ni 187.

      Alisema kuwa makatibu wa uchumi/fedha wa mkoa nafasi zinazohitajika ni 31 ila walioomba ni 170, wenyeviti wa wilaya nafasi ni 31 walioomba 148, wenyeviti wa wilaya wanahitajika 161 walioomba ni 965, wajumbe wa NEC taifa wanahitajika 221, lakini walioomba ni 1,380 na wajumbe wa NEC taifa wanahitajika 20 bali walioomba ni 89.

      Nape alisema kuwa nafasi nyingine ni wenyeviti wa Jumuiya Taifa ya UVCCM ambayo inahitajika nafasi moja ila imeombwa na wagombea 47, UWT nafasi moja nayo inagombewa na watu 9, Jumuiya ya Wazazi nafasi moja imeombwa na watu 22 na makamu mwenyekiti UVCCM inahitajika nafasi moja, lakini walioomba ni 27, UWT nafasi ya makamu imeombwa na watu watatu huku ile ya wazazi ikiombwa na watu 10.

      Hata hivyo, Nape alisema kuwa hatua ya mwisho ya kupitisha majina ya wagombea hao ni NEC na kwamba vikao vingine vinapitisha na kutoa alama za sifa ya wagombea.

      Kinana ang’atuka
      Mwanasiasa nguli na kada maarufu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ametangaza kung’atuka kuwania nafasi yoyote ndani ya chama hicho tawala.
      Kinana ambaye amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) kwa miaka 25 sasa, ametoa kauli hiyo jana alipoulizwa sababu za kutogombea nafasi yoyote ya uongozi katika uchaguzi unaoendelea ndani ya CCM.

      Kada huyo maarufu ambaye amepata kuwa Meneja Kampeni wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete, alisema miaka 25 ya kushiriki katika vikao vya juu inatosha na ni vizuri kung’atuka.

      “Naamini kuna wana-CCM wengi wazuri wenye sifa na uwezo wa kuongoza chama. Uongozi ni kupokezana vijiti na ni wakati wangu kukabidhi wengine kijiti hiki,” alisema Kinana.
      Hata hivyo hakuwa tayari kueleza kama mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete atamteua kuwa mjumbe wa NEC atakubali au la.

      Kinana amekuwa kada anayeheshimika sana ndani ya CCM, mwenye ushawishi mkubwa hasa wakati wa vikao vya juu vya chama.
      Wakati Kinana aking’atuka, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kada huyo amekuwa msaada mkubwa kwa chama.

      Hata hivyo alisema licha ya kung’atuka, Rais Kikwete anaweza kumteua akitaka kupitia nafasi kumi alizonazo kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
      “Kinana ameng’atuka wakati bado chama kinahitaji mchango wake. Hata hivyo mwenyekiti wetu wa taifa, Rais Kikwete hazuiwi akitaka kumteua,” alisema Nape.

      Katika hatua nyingine, Nape amesema kuwa yeye hajagombea nafasi yoyote ya uongozi ili kujipa nafasi ya kusimamia vizuri uchaguzi huo.
      “CCM ina watu wengi sana wenye sifa na uchaguzi umekuwa na changamoto kubwa. Hivyo nimejipa nafasi kuweza kusimamia uchaguzi huo kwa karibu zaidi,” alisema Nape.

      Katika hatua nyingine, kikao cha Kamati Kuu (CC), kilichotarajiwa kuanza jana na kumalizika leo, huenda kikamalizika kesho baada ya kuchelewa kuanza.
      Kikao hicho chini ya Rais Kikwete, kilitarajiwa kuanza jana saa tatu asubuhi, lakini kilikwama na kuanza saa 11 jioni.

      Habari kutoka ndani ya CCM zilisema kuwa hali hiyo ilitokana na kikao cha Kamati ya Maadili kuchelewa kumalizika kutokana na mvutano mkubwa wa kupitia majina ya wagombea.

      Wazee wamvaa Sitta
      Wazee wa CCM mkoani Shinyanga, wametishia kufanya maandamano ya amani kuhusiana na kauli tata zinazoendelea kutolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

      Katika tamko lao, wazee hao walisema wakati umefika sasa Sitta awaeleze Watanzania juu ya kauli zake hizo, ikiwemo ile ya kuwepo kwa mafisadi ndani ya chama na aliyoitoa hivi karibuni akiwa Karagwe, ya maisha bora kwa kila Mtanzania hayatawezekana.

      Kwa niaba yao, Shomvi Ibrahimu Saidi, alisema kuwa waziri huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC na mbunge wa Urambo Mashariki, amekuwa akikaririwa akitoa tuhuma nzito ndani ya serikali na chama, hivyo ni vema akaweka wazi majina ya watuhumiwa wa ufisadi.

      Pia walikumbushia jinsi kiongozi huyo alivyowahi kuitolea maneno makali Kamati Kuu ya CCM katika kipindi cha ‘Dakika 45’ kinachurushwa na Televisheni ya ITV, akisema kwamba ilihongwa na mafisadi ikabadili utaratibu wa kuchagua Spika wa Bunge.

      Wazee hao wamemuomba Waziri Sitta kama hana ushahidi wa kutosha wa kuupeleka kwenye vikao vya chama na vyombo vya dola kama TAKUKURU, polisi na mahakama, ni afadhali akae kimya kuliko kuendelea kuwachanganya watu.
      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    20. Miaka 50
    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...