Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

    Report Post
    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 104
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,174
      Rep Power : 3548
      Likes Received
      3044
      Likes Given
      460

      Default Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      JUMAMOSI, SEPTEMBA 22, 2012 08:48 NA ELIZABETH MJATTA

      KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ameibuka na kusema hawezi kujiuzulu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Daud Mwangosi, aliyeuawa hivi karibuni mkoani Iringa.

      Kamanda Kamuhanda alitoa msimamo huo jana alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Radio One wakati wa kipindi cha Kumepambazuka.

      “Ninachofahamu mimi ni kwamba, kesi ya msingi iko mahakamani na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ameshaunda kamati ambayo inachunguza mwenendo mzima wa tukio hili na baadaye itatoa taarifa.

      “Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Kamuhanda.

      Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.

      “Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika, haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.

      “Sisi tunapokuwa kazini, tunalinda raia na mali zao na ndiyo tulilofanya na mara zote tunasisitiza utii wa sheria bila kushurutishwa.

      “Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea,” alisema.

      Septemba 2 mwaka huu, Mwangosi aliuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu alipokuwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

      Baada ya kulipuliwa na kitu hicho, mwili wake ulisambaratika vipande vipande ingawa pia askari mmoja aliyekuwa jirani naye, pia alijeruhiwa mguu.

      Baada ya tukio hilo, waandishi wa habari, wanaharakati na watu mbalimbali, walilaani tukio hilo na kutoa matamko yao wakitaka Kamanda Kamuhanda ajiuzulu, kutokana na mauaji hayo.

      Septemba 12 mwaka huu, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mwenye namba G2573, Pasificus Simon, alipandikizwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Iringa, kwa kosa mauaji ya marehemu Mwangosi.

      Mtuhumiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo, hakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa linalomkabili haliwezi kusikilizwa katika mahakama hiyo. Hadi sasa mshitakiwa yuko mahabusu.

      Pasco likes this.

    2. FemaTV & Radio

    3. #41
      obwato's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2012
      Posts : 733
      Rep Power : 545
      Likes Received
      170
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By jmushi1
      Mauwaji aliyoyafanya ni ya kisiasa,na kwahiyo majibu yake pia ni ya kisiasa.

      Hata asipojiuzulu,kuna wakati atajibu tuhuma hizi za mauwaji.Nchi za wenzetu kashfa kama hii wala asingethubutu kupanua mdomo,maana angekuwa keshajiuzulu na angeogopa maneno yake yasitumike dhidi yake wakati wa mashtaka.Kwa mfano kauli kuwa watu wakikusanyika kufunguwa tawi basi wauwawe kwasababu wamevunja sheria.Kauli kwamba walifanya maandamano ni ya kisiasa,kwasababu mwanzoni alisema ni mikutano haitakiwi kwasababu ya sensa,lakini cha ajabu ccm ilikuwa na mikutano,na pia kulikuwepo na fiesta.

      Only in Tanzania haya ndo yanaonekana kuwa ni ya kawaida.
      Huyu jamaa uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana,yaani pamoja na kusimamia mauwaji ya kizembe yanayolalamikiwa na ulimwengu mzima bado haoneshi ata chembe ya kujutia. Kama wasiotii sheria bila shuruti hukumu yao ni kuuawa mbona hawakuua walioandamana bila kibali kushinikiza kuachiwa waliogomea sensa au waliokata uzio uliowekwa na polisi pale kidongo chekundu? Kama polisi walikuwa wanatekeleza majukumu yao halali kwa nini mtuhumiwa amepelekwa mahakamani? Sishangai sana lkn maana ata raisi wetu ana fikra kama za Kamuhanda ndio maana akuona umuhimu wa kutoa japo pole ya mdomo tu kwa wafiwa.
      Kolero likes this.

    4. #42
      eucalyptos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd January 2010
      Posts : 307
      Rep Power : 535
      Likes Received
      79
      Likes Given
      43

      Default

      Quote By Excellent
      huyu elimu yake itakuwa kiwango gani?
      Hata " VIDUDU ATAKUWA HAJASOMA".
      Excellent likes this.

    5. #43
      Emeka Anyaoku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Posts : 430
      Rep Power : 442
      Likes Received
      134
      Likes Given
      0

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Ningekuwa mimi Jk kwa kauli ya kujiamini ya huyu KANDANDA namfuta kazi.
      Kolero likes this.

    6. #44
      MPIGA ZEZE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th May 2011
      Posts : 575
      Rep Power : 520
      Likes Received
      202
      Likes Given
      199

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Mimi nilifikiri siku ile ya tukio alikuwa amelewa ulanzi kwa jinsi alivyokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kabla ya mauaji yenyewe, kumbe ndivyo alivyo muda wote!!!! Ninakubaliana na wadau walaiotangulia kwamba huyu ni mshitakiwa namba moja. Ndiyo, hatafikishwa mahakamani leo lakini iko siku atakabiliana uso kwa uso na Pilato kama si Dar basi ni the Hague! Hana hata ubinadamu wa kusema kwamba ile ilikuwa ni bahati mbaya.

    7. #45
      genekai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2010
      Location : Loitering!
      Posts : 7,497
      Rep Power : 2078
      Likes Received
      1061
      Likes Given
      1568

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Ndo madhara ya kuwa na dead conscience (dhamiri ilokufa)
      The future of this country is being jeopardized by the intellectual slavery of our top leaders

    8. Study Abroad

    9. #46
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Quote By nngu007
      JUMAMOSI, SEPTEMBA 22, 2012 08:48 NA ELIZABETH MJATTA

      KAMANDA wa Polisi, Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ameibuka na kusema hawezi kujiuzulu kutokana na kifo cha aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Daud Mwangosi, aliyeuawa hivi karibuni mkoani Iringa.

      Kamanda Kamuhanda alitoa msimamo huo jana alipokuwa akihojiwa na Kituo cha Radio cha Radio One wakati wa kipindi cha Kumepambazuka.

      “Ninachofahamu mimi ni kwamba, kesi ya msingi iko mahakamani na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ameshaunda kamati ambayo inachunguza mwenendo mzima wa tukio hili na baadaye itatoa taarifa.

      “Kwa hiyo, siwezi kujiuzulu kwa sababu tukio hilo la kifo lilitokea wakati wa kutimiza wajibu wa kutii sheria bila shuruti,” alisema Kamanda Kamuhanda.

      Alipoulizwa kuhusiana na kuwajibika kutokana na mauaji hayo alisema, hawezi kuwajibika kwa sababu hana makosa.

      “Niwajibike kwa kosa lipi?, kuna kosa mtu anaweza akawajibika, lakini kama huna kosa huwezi kuwajibika, haiwezekani watu waliofanya makosa wenyewe kwa kuandamana bila uhalali wasiwajibike halafu mimi niwajibike, haiwezekani.

      “Sisi tunapokuwa kazini, tunalinda raia na mali zao na ndiyo tulilofanya na mara zote tunasisitiza utii wa sheria bila kushurutishwa.

      “Kwa hiyo, hicho ndicho kilichokuwa kinafanyika, kilichofanyika ndiyo utii wa sheria bila shuruti, wangetii sheria bila shuruti yote yasingetokea,” alisema.

      Septemba 2 mwaka huu, Mwangosi aliuawa kwa kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu alipokuwa kazini katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa.

      Baada ya kulipuliwa na kitu hicho, mwili wake ulisambaratika vipande vipande ingawa pia askari mmoja aliyekuwa jirani naye, pia alijeruhiwa mguu.

      Baada ya tukio hilo, waandishi wa habari, wanaharakati na watu mbalimbali, walilaani tukio hilo na kutoa matamko yao wakitaka Kamanda Kamuhanda ajiuzulu, kutokana na mauaji hayo.

      Septemba 12 mwaka huu, askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mwenye namba G2573, Pasificus Simon,
      alipandikizwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Iringa, kwa kosa mauaji ya marehemu Mwangosi.

      Mtuhumiwa huyo alipofikishwa mahakamani hapo, hakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa linalomkabili haliwezi kusikilizwa katika mahakama hiyo. Hadi sasa mshitakiwa yuko mahabusu.

      Viwanda vya uongo utavijuwa tu.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    10. #47
      SUPERXAVERY's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th September 2012
      Posts : 80
      Rep Power : 353
      Likes Received
      6
      Likes Given
      8

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      acheni kelele, kamanda kesha ongea, andamaneni tena tuwatwale mitwe.
      Afterall mna uhakika gani kuwa bomu lililomuua mwangosi limetoka kwenye bunduki ya yule dogo. Inawezekana walikuja nalo ili wawalipue polisi kwa jazba na kumbe wameua mwandishi.

    11. #48
      Naytsory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 721
      Rep Power : 759
      Likes Received
      127
      Likes Given
      2

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Atuambie Marehemu Mwangosi alivunja sheria ipi hata astahili adhabu ya kifo? Hakuwa hata na jiwe mkononi zaidi ya kamera yake tena chini ya polisi wasiopungua 8 wenye silaha. Hilo kosa hata Shetani atamhukumu.

    12. #49
      Naytsory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 721
      Rep Power : 759
      Likes Received
      127
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By SUPERXAVERY
      acheni kelele, kamanda kesha ongea, andamaneni tena tuwatwale mitwe.
      Afterall mna uhakika gani kuwa bomu lililomuua mwangosi limetoka kwenye bunduki ya yule dogo. Inawezekana walikuja nalo ili wawalipue polisi kwa jazba na kumbe wameua mwandishi.
      Sidhani kama uko salama.

    13. #50
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,527
      Rep Power : 3319
      Likes Received
      1206
      Likes Given
      457

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      hajakurupuka serikali ndio inampa jeuri,viongozi wengi serikalini hawapendi chadema kiendelee kuwa hewani. Hivyo yoyote anaekihujumu chadema yupo upanda wao.!!

    14. #51
      SUPERXAVERY's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th September 2012
      Posts : 80
      Rep Power : 353
      Likes Received
      6
      Likes Given
      8

      Default

      Quote By Naytsory
      Sidhani kama uko salama.
      Niko salama kabis, members wa cdm wengi wao ni wenye hulka ya hasira,jaziba na wasiokubali kuwa hata wasio kubaliana nao mawazo yao yanaweza kuwa sahihi.
      Ni rahisi m2 wa aina hii kubeba bomu hata la tnt kwa madhumuni ya kuwaripua polisi ambao kwa cdm kwao ni kikwazo.

    15. #52
      Naytsory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 721
      Rep Power : 759
      Likes Received
      127
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By SUPERXAVERY
      Niko salama kabis, members wa cdm wengi wao ni wenye hulka ya hasira,jaziba na wasiokubali kuwa hata wasio kubaliana nao mawazo yao yanaweza kuwa sahihi.
      Ni rahisi m2 wa aina hii kubeba bomu hata la tnt kwa madhumuni ya kuwaripua polisi ambao kwa cdm kwao ni kikwazo.
      Unaweza kuthibitisha hilo kuwa Mwangosi alikuwa na Bomu na je alipewa na nani? Mazingira na kauli ya Kamuhanda yanathibitisha polisi ndiyo waliomwua Mwangosi sasa sielewi kwanini unapinga kitu chenye ushahidi uliojitosheleza. Hata ubinadamu huna mkuu?
      SUPERXAVERY likes this.

    16. #53
      Manyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Posts : 1,701
      Rep Power : 716
      Likes Received
      288
      Likes Given
      258

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Anatia kichefuchefu sana huyu! Yani usipotii sheria bila shuruti adhabau yake ndo kifo? Halafu hawa waandishi wetu wa habari nae, utafikiri kama hawajui kuuliza maswali bana!

    17. #54
      Manyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Posts : 1,701
      Rep Power : 716
      Likes Received
      288
      Likes Given
      258

      Default

      Quote By SUPERXAVERY
      Niko salama kabis, members wa cdm wengi wao ni wenye hulka ya hasira,jaziba na wasiokubali kuwa hata wasio kubaliana nao mawazo yao yanaweza kuwa sahihi.
      Ni rahisi m2 wa aina hii kubeba bomu hata la tnt kwa madhumuni ya kuwaripua polisi ambao kwa cdm kwao ni kikwazo.
      Kama hufikirii kwa kutumia masaburi, basi unatamani sana leo kutukanwa!

    18. #55
      Foum Jnr's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th July 2012
      Location : UK
      Posts : 157
      Rep Power : 374
      Likes Received
      76
      Likes Given
      76

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Mwandishi wa IPP! unategemea nini hapo zaidi ya white wash? Huyu kamanda ni ignorant good for nothing, nasijui hata kama ana elimu, mwenye cv yake na aiweke tumjadili zaidi inawezekana kabisa katika kupekua madaftari akajakukutwa na maradhi ya akili.

      Anasema askari hawana kosa sasa yule aliepelekwa mahakamani kufanya nini? anasema kazi yao kulinda sheria bila shuruti sasa hajui hata kanuni za polisi zinazohimiza kwa nguvu ya sheria utumiaji wa propotinate force, sasa kama kuuwa sio dispropotinated use of force ni kitu gani? Ubaba wake utakuja kumsuta siku yake itafika, madhali kachangia pakubwa katika dhulma ya roho ya marehem na warithi wake ajue tu dunia hii iko siku itamsuta na atasimama mbele ya sharia kujibu tuhuma.

      Huyu sifikiri kama hata anaelimu ya darasa la saba, mbali ya elimu hana hata akhlaki za kibinaadamu, chuki, jazba na upendeleo ndio uliomuathiri akili akawa ni sawa ni mgonjwa wa akili. Aibu kuwa ndio mkuu wa polisi wa mkoa, kila siku zinavyokwenda ndio kunaniwia vigumu kukitetea chama nilichokiamini. shame on you.

    19. #56
      don-oba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th December 2011
      Posts : 739
      Rep Power : 523
      Likes Received
      256
      Likes Given
      29

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Wanasheria tutakufwata popote pale ulipo, uwe umevaa gwanda uwe umevua gwanda!

    20. #57
      Yaya Toure's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2012
      Posts : 1,190
      Rep Power : 647
      Likes Received
      262
      Likes Given
      117

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Jinga kabisa hili zee..
      Ni hatari sana kwa afya yako kushabikia siasa za Tanzania....

    21. #58
      Kiby's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th November 2009
      Posts : 3,499
      Rep Power : 1187
      Likes Received
      599
      Likes Given
      33

      Default

      Quote By Gwankaja Gwakilingo
      kwa nini waandishi wa habari huwa mnawaauliza hawa mnaowauliza maswali mwongozo? kwa nini usimuulize ni makosa gani ambayo yanapaswa mtu akawajibika kama alivyosema kuna makosa ya kuwajibika?
      .
      Njaa mbaya sana. Waandishi wengi Tanzania wanauliza maswali huku wakiwa wamechora picha ya bahasha ya kaki kichwani.
      .

    22. #59
      Mama Mdogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st November 2007
      Posts : 1,351
      Rep Power : 857
      Likes Received
      669
      Likes Given
      72

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Quote By Jackbauer
      ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia subordinates wake mpaka wakamfyatulia bomu mwangosi at zero distance.pia awajibike kwa mauaji yaliyofanywa na polisi huko sumbawanga.
      Hapo kwenye red, ni Songea siyo Sumbawanga
      Jackbauer likes this.
      Anyone who has never made a mistake has never tried anything new - Albert Einstein
      No problem can be solved from the same level of consciousness that created it
      - Albert Einstein

    23. #60
      Njoka Ereguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 503
      Rep Power : 459
      Likes Received
      167
      Likes Given
      30

      Default Re: Kamanda Kamuhanda: Siwezi kujiuzulu

      Kuna kila sababu kwa viongozi wetu kupatiwa mafunzo ya uwajibikaji. Mara nyingi utawasikia wakisema niwajibike kwa lipi wakati mimi sina kosa. Nijuavyo mimi, wengine watasahihisha kuwajibika siyo lazima ufanye kosa, unaweza kuwajibika kwa kupinga kilichotokea au kukerwa na kilichotokea au kinachoendelea katika utawala wako au uongozi wako. Kwa maana nyingi ni vyema viongozi wetu wakatambua kuwa kiongozi anayefanya makosa yeye hatakiwa kujiuzulu tu bali ni lazima ashitakiwe kwa kosa alilolifanya. Sasa wanaposema hawawezi kujiuzulu kwa kuwa hawana kosa wanashindwa kuelewa kuwa ukifanya kosa na ikabainika ni kosa unatakiwa kushitakiwa na kujibu tuhuma dhidi yako.

      Kujiuzulu unaweza usiwe umefanya kosa lakini kwa kuwa wewe ni kiongozi na umeshindwa kudhibiti makosa chini ya usimamizi wako unashauriwa kujuuluzu ili kuacha hiyo nafasi kwa kuwa imekushinda au haumweshindwa kutimiza masharti ya kazi husika.

      Kashule hako ni muhimi sana kwa viongozi wetu, ni aibu kuona kiongozi mkubwa kama Waziri, Mbuge, RC, RPC N.K anashindwa kutofautisha au kuelewa maana ya kuwajibika kwa kujiuzulu na kuwajibishwa kwa mustakabali wa sheria kutokana na kosa ulilofanya.

      Nawasilisha

    24. Miaka 50
    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...