BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kutokana na serikali kutupilia mbali ombi la kunzisha Mahakama ya Kadhi, Waislamu hawataipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Katika taarifa yake, Bakwata ilifikia hatua ya kusema Waislamu wasimchague Rais Jakaya Kikwete iwapo atasimamishwa na CCM kugombea urais, ikiwa ni pamoja na wabunge na madiwani watakaosimamishwa na chama hicho tawala kutokana na kitendo cha serikali kutupilia mbali hoja ya Mahakama ya Kadhi.
Kauli hiyo imetolewa jana wakati Mufti Issa bin Shaaban Simba alipokuwa akitoa tamko kupinga uamuzi wa serikali kutaka kutumia sheria za dini ya Kiislamu katika mahakama za kawaida badala ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi, kitu ambacho alisema anaamini kitawanyima haki Waislamu.
Alisema serikali imedhihirisha kuwa inaendeshwa na Wakristo na si kweli kama serikali haina dini na akamtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kubatilisha kauli hiyo kwa kuwa inamchafua Rais Jakaya Kikwete mbele ya umma wa Waislamu.
Waziri ametuthibitishia kama Rais Kikwete alikuwa akitulaghai ili tumpigie kura kwa kigezo kuwa suala hilo litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na sio kuchanganywa kama ilivyokuwa mwaka 1970 katika Sheria ya Ndoa na kuwanyima haki Waislamu,alisema.
Alisema kwa muda mrefu sana Waislamu wamekuwa kimya wakitumia hekima na busara kudai haki zao, lakini katika hatua hii ambayo serikali imefikia hawapo tayari kuendelea kudhalilishwa na kuwa kitendo hicho ni dhalimu.
Mufti alisema wamekuwa wakiiomba Mahakama ya Kadhi kwa zaidi ya miaka 20 na hivyo hawezi kuendelea kuwa kimya na kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuwa mahakama hiyo ni haki yao.
Alisema kauli ya Waziri Chikawe imedhihirisha kuwa serikali ina wenyewe na Waislamu wamewekwa katika tabaka la pili pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuwatuliza kwa ahadi kuwa watalipatia ufumbuzi suala hilo.
Natoa wito kwa Masheikh wote nchini na Waislamu wa madhehebu yote kupinga vikali kauli iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na kwamba Waislamu waige mfano wa Waislamu wa Afrika Kusini,alisema Mufti na kuhoji:
Kwa nini iwe Afrika ya Kusini na isiwe Zanzibar, Uganda na Kenya ambazo zipo ndani ya Afrika Mashariki? Kwa niaba ya Waislamu nasema serikali haikututendea haki na imetuchukiza sana,alisema.
Alisema lengo la kuomba mahakama hiyo ni kuhakikisha Waislamu wanashughulikia masuala yao ya ndoa na mirathi na si vinginevyo, hivyo waziri asipotoshe jamii kwa kutumia mifano ambayo haiko sahihi.
Mahakama hii haitawakata wezi mikono kwa kuwa nchi hii ina katiba na sheria na sisi tutazirudisha kesi zote za jinai mikononi mwa serikali. Sifahamu hiyo kamati ambayo waziri alisema alikuwa amekaa na kutoa tamko hilo ilikuwa na watu gani,alihoji.
Aliongeza kuwa kutokana na mapungufu hayo waziri arudi tena na kukutana na masheikh ili apate muongozo wa nini Waislamu wanahitaji na sio kuzungumza bila kuwa na usahihi wa kile anachosema.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya tamko la Bakwata, masheikh walikuwa na mitazamo tofauti. Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum Mussa alisema wapo baadhi ya Waislamu ambao watakubali kutokana na ufinyu wao wa elimu ya dini.
Mussa alisema haoni sababu ya serikali kufanya njia ya mkato katika suala hilo kwani Waislamu wanahitaji Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kwa wafanyabiashara ambao wana mahakama yao.
Hukumu inayotolewa katika Mahakama ya Kadhi ni ibada kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) hivyo ni lazima kwa atakayetoa hukumu hiyo awe Muislamu na si vinginevyo,alisema.
Namshanga waziri anapotaka sheria hizi zitumiwe katika mahakama za kawaida. Aliona wapi John akawa imamu,alihoji sheikh huyo wa mkoa wa Dar es Salaam.
Naye katibu wa Bakwata wilayani Ilala, Sheikh Issa Ausi alisema historia iko wazi. Waasisi na wanaharakati ambao waliitoa Tanganyika mikononi mwa wakoloni walikuwa Waislamu, na akahoji sababu za serikali kuwa mstari wa mbele kuwafunga midomo leo.
Bakwata imezinduka sasa Waislamu wote tumeungana katika kupigania haki zetu na kutetea maslahi yetu na serikali itambue kuwa Bakwata iko hai hao Wakristo walikuwa wapi wakati sisi tukipigania uhuru,alihoji.
Wakati huohuo, Sheikh Salum Rwambo alisema anawashangaa wabunge Waislamu ambao baadhi ni mahajat na malhaj wanakaa kimya na kushindwa kutetea hoja za msingi na kudai kuwa huo sasa ndio mwisho wao wa kuwaita masheikh na kutaka waombewe dua ili wasipate wepesi katika kampeni zao.
Sheikh Rwambo pia alimsifia mbunge wa Nzega Lucas Selelii kwamba ni miongoni mwa wabunge katika Bunge hilo wanaozungumza ukweli na kwa kujiamini tofauti na wengine ambao wanaenda kukaa bila kufanya kazi zilizowapeleka.
Source: Mwananchi
CCM watajuta kuweka swala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani yao uchaguzi ya 2005.
Bakwata hawana ubavu huo wanabwaka tu, wao wenyewe credibility yao ni questionable wasafishe nyumba yao kwanza.
Hawana jipya zaidi ya kutafuta njia ya kutokea na kuficha madudu yao. Ni ukweli usio na shaka uislam haupo kitaasisi kama ukristo na madhehebu yake catholics, Lutheran, Anglican nk. Bakwata ni kikundi cha wajanja wachache wasio na mandate yeyote kwa waislam ndio maana no body is taking them serious.
Masatu.. nakuunga mkono 100% kuhusu credibility ya BAKWATA kwenye safu za waislamu.
Ila ni ukweli usiopingika kuwa at least kwa hili they have said some thing.... yaani kwa maneno mengine ile kauli ya enough is enough wameithibitisha. Nadhani tuwapongeze.
Unajuwa sikutegemea kusikia kauli hii kutoka BAKWATA. Maana hawakuwa na kuumauma maneno..they went very straight to the pint na kuita nyeupe ni white.
Kwa ufupi CCM inaendelea kushikwa pabaya maana kila wanapojaribu kuziba kunatoboka na kuvuja kwengine.
Inaelekea wanapoteza wapiga kura kwenye mambo yahusuyo Muungano,Ufisadi na sasa waiislamu wenye siasa kali bado wakiristu wenye siasa kali naona wao bado wanajikurubisha kwa kila hali ,wakiristu amkeni wacheni kuikumbatia CCM ,vyama mbadala vimejaa tele ahadi za CCM zitawatoa vibega.
__________________
Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.
Na wasiislaam wasiokuwemo Bakwata, kama Answari Sunaah, (Mtaniwia radhi kama nimekosea spelling) nao itabidi waanzishe mahakama ya kadhi yao na ilipiwe na serikali hihi hihi bila kuleta vumbi?
Bakwata hawana ubavu huo wanabwaka tu, wao wenyewe credibility yao ni questionable wasafishe nyumba yao kwanza.
Hawana jipya zaidi ya kutafuta njia ya kutokea na kuficha madudu yao. Ni ukweli usio na shaka uislam haupo kitaasisi kama ukristo na madhehebu yake catholics, Lutheran, Anglican nk. Bakwata ni kikundi cha wajanja wachache wasio na mandate yeyote kwa waislam ndio maana no body is taking them serious.
Masatu,
Nakubaliana na uliyoyaeleza isipokuwa niliyo bold. Tatizo la Waislam Tz ni dogo. Serikali haijawaruhusu wajipange waweke viongozi wenye muono kwenye hiyo Bakwata. Na hilo waislam wanaweza kulifanya kama hawataingiliwa katika mambo yao na Serikali. Hakuna uchaguzi mkuu wa Bakwata utafanyika bila kuingiliwa na serikali. Hata TEC au CCT zikiweka na bogus leaders hakuna cha maana wanachoweza kufanya.
Bahati mbaya ni kuwa serikali inafurahi kuwa na dudu bovu kama Bakwata kisha inalipa nguvu nyingi. Na hapo ndipo watu wanapata fursa ya kuwatukana Waislam.
Waislam wanaweza. Mfano mdogo ambao wewe unaufahamu, tazama tofauti ya shule za Bakwata na zilizoanzishwa na vitaasisi vidogo tu vya Kiislam tena karibuni. Waislam wasipoingiliwa katika masuala yao wanaweza kufanya zaidi ya hapo.
Mambo yote mengine ambayo sisi tunayapigia kelele hayawafanyi wao kuichukia CCM; yaani yote yaliyofanyika dhidi ya nchi yetu na utajiri wetu wao hayawagusi wala kuwataka waumini wao kuyafanya ya kisiasa na kuiadhibu CCM; yaani yote hayo hayajafikia kiwango cha kuwakera.. isipokuwa hili moja tu?
Nachelea kusema huu ni ubinafsi, kwani hii nchi imeraluliwa na hawa manyang'au wa CCM. Sasa kusema wanakataa CCM kwa sababu tu ya kukatiliwa kwa mahakama ya kadhi ambayo ni sehemu yao ya ibada haingii akili na naweza kusema ni uamuzi wa kukurupuka.
Naikataa CCM kwa sababu kuu, imeifilisi nchi hii na hakuna matumaini kwa waTZ.
Mi nafikiri tuaiche Tz kama secular nation. Tusiingize halafu ya kidini ili kuwe na fair play kwa dini na imani zote. Wahubiriane misikitini na makanisani na watu wawe converted kwa kutafuta pepo na si maslahi ya kiuchumi, vyeo serkalini n.k
There are two things in our job. Criticism i accept with respect. Disrespect i dont accept and dont respect" - Arsene Wenger.
Let us discuss the issue with clear mind. As far as I am concerned there is nothing wrong with having " mahakama ya Kadhi". The sticking point is to make it a constitutional affair. Its establishment does not need a government hand, it should be internally handled by the Muslim community itself. We all know the legality and acceptability of BAKWATA, an institution established with a government hand, among the Muslim community is not at 100% with alot of discenting voices. Some going as far as calling it a govern;ent tool used to deter development of the concerned community. The isue was a non starter in the parliament. Here again we see how politician can exploit and distabilise a country by giving false or hard to implement promises, just to have your vote.
Muslims, if they will heed to the call, they will be doing all of us a favor to vote CCM out,but will they still have the Kadhi demand?