|
Quote: |
|
 |
|
|
Mambo yote mengine ambayo sisi tunayapigia kelele hayawafanyi wao kuichukia CCM; yaani yote yaliyofanyika dhidi ya nchi yetu na utajiri wetu wao hayawagusi wala kuwataka waumini wao kuyafanya ya kisiasa na kuiadhibu CCM; yaani yote hayo hayajafikia kiwango cha kuwakera.. isipokuwa hili moja tu? |
|
|
|
|
Mwanakijiji wacha hiyo,maana wakijihusisha mtakuja na rangi nyengine hapa ,hawa ni wananchi walioipigia kura CCM na waliipigia kwa kuahidiwa kupatiwa dai hilo wanalolidai ni sawa sawa kabisa na mwanaCCM alieahidiwa kujengewa hospitali,daraja,njia ya lami na mambo kabakaba yakiwemo maisha bora sasa ni wakati wa wale wote walioahidiwa na hadi leo hawajapelekewa hata kokoto au matofali kuanza kubadili muelekeo kama hao Waislamu walioipigia kura CCM hivyo kuanza safari ya kuipeleka CCM kaburini. Hao waislamu walioipigia kura CCM wameanza kuonyesha njia sasa huko kwenye wakiristu walioipigia kura CCM na madai yao hayakutekelezwa nao wapige mbiu ya mgambu ile kufanikisha maziko.
Mambo ya utajiri hayawashughulishi wanaCCM hayo ni ya vyama vya upinzani au hulielewi hilo ? Ila inaonyesha viongozi wa CCM wamewadanganya wenzao waliomo kwenye mrengo wa uislamu, hivyo wanajitayarisha kutoa pigo kwa viongozi wao,sasa tatizo upande wetu wapinzani lipo wapi, hivi ukisikia vita vya panzi furaha ya kunguru unakuwa hufahamu maana ?
Hao sidhani wanazungumza na wanachama wa Chadema CUF au vyama vingine vya kambi ya upinzani ,si waislamu wote waliipigia kura CCM,bali wanazungumza na wanachama wa CCM ambao ni Waislamu kubadili muelekeo wa kuhamisha kura zao na kuzipeleka wanakoona madai yao yatatekelezwa ,hivyo Chama chochote kile kinaweza kuchukua dai hilo na kusema kuwa endapo wao watapewa kura hizo watalitekeleza dai hilo,sioni tatizo la kidini hapa.
Ila ngoma ni nzito sana ukiangalia jamaa alivyopiga mahesabu tokea kudai uhuru.Inaonyesha uvumilivu umeanza kugonga ukomo.