BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kutokana na serikali kutupilia mbali ombi la kunzisha Mahakama ya Kadhi, Waislamu hawataipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Katika taarifa yake, Bakwata ilifikia hatua ya kusema Waislamu wasimchague Rais Jakaya Kikwete iwapo atasimamishwa na CCM kugombea urais, ikiwa ni pamoja na wabunge na madiwani watakaosimamishwa na chama hicho tawala kutokana na kitendo cha serikali kutupilia mbali hoja ya Mahakama ya Kadhi.
Kauli hiyo imetolewa jana wakati Mufti Issa bin Shaaban Simba alipokuwa akitoa tamko kupinga uamuzi wa serikali kutaka kutumia sheria za dini ya Kiislamu katika mahakama za kawaida badala ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi, kitu ambacho alisema anaamini kitawanyima haki Waislamu.
Alisema serikali imedhihirisha kuwa inaendeshwa na Wakristo na si kweli kama serikali haina dini na akamtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kubatilisha kauli hiyo kwa kuwa inamchafua Rais Jakaya Kikwete mbele ya umma wa Waislamu.
Waziri ametuthibitishia kama Rais Kikwete alikuwa akitulaghai ili tumpigie kura kwa kigezo kuwa suala hilo litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na sio kuchanganywa kama ilivyokuwa mwaka 1970 katika Sheria ya Ndoa na kuwanyima haki Waislamu,alisema.
Alisema kwa muda mrefu sana Waislamu wamekuwa kimya wakitumia hekima na busara kudai haki zao, lakini katika hatua hii ambayo serikali imefikia hawapo tayari kuendelea kudhalilishwa na kuwa kitendo hicho ni dhalimu.
Mufti alisema wamekuwa wakiiomba Mahakama ya Kadhi kwa zaidi ya miaka 20 na hivyo hawezi kuendelea kuwa kimya na kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuwa mahakama hiyo ni haki yao.
Alisema kauli ya Waziri Chikawe imedhihirisha kuwa serikali ina wenyewe na Waislamu wamewekwa katika tabaka la pili pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuwatuliza kwa ahadi kuwa watalipatia ufumbuzi suala hilo.
Natoa wito kwa Masheikh wote nchini na Waislamu wa madhehebu yote kupinga vikali kauli iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na kwamba Waislamu waige mfano wa Waislamu wa Afrika Kusini,alisema Mufti na kuhoji:
Kwa nini iwe Afrika ya Kusini na isiwe Zanzibar, Uganda na Kenya ambazo zipo ndani ya Afrika Mashariki? Kwa niaba ya Waislamu nasema serikali haikututendea haki na imetuchukiza sana,alisema.
Alisema lengo la kuomba mahakama hiyo ni kuhakikisha Waislamu wanashughulikia masuala yao ya ndoa na mirathi na si vinginevyo, hivyo waziri asipotoshe jamii kwa kutumia mifano ambayo haiko sahihi.
Mahakama hii haitawakata wezi mikono kwa kuwa nchi hii ina katiba na sheria na sisi tutazirudisha kesi zote za jinai mikononi mwa serikali. Sifahamu hiyo kamati ambayo waziri alisema alikuwa amekaa na kutoa tamko hilo ilikuwa na watu gani,alihoji.
Aliongeza kuwa kutokana na mapungufu hayo waziri arudi tena na kukutana na masheikh ili apate muongozo wa nini Waislamu wanahitaji na sio kuzungumza bila kuwa na usahihi wa kile anachosema.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya tamko la Bakwata, masheikh walikuwa na mitazamo tofauti. Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum Mussa alisema wapo baadhi ya Waislamu ambao watakubali kutokana na ufinyu wao wa elimu ya dini.
Mussa alisema haoni sababu ya serikali kufanya njia ya mkato katika suala hilo kwani Waislamu wanahitaji Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kwa wafanyabiashara ambao wana mahakama yao.
Hukumu inayotolewa katika Mahakama ya Kadhi ni ibada kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) hivyo ni lazima kwa atakayetoa hukumu hiyo awe Muislamu na si vinginevyo,alisema.
Namshanga waziri anapotaka sheria hizi zitumiwe katika mahakama za kawaida. Aliona wapi John akawa imamu,alihoji sheikh huyo wa mkoa wa Dar es Salaam.
Naye katibu wa Bakwata wilayani Ilala, Sheikh Issa Ausi alisema historia iko wazi. Waasisi na wanaharakati ambao waliitoa Tanganyika mikononi mwa wakoloni walikuwa Waislamu, na akahoji sababu za serikali kuwa mstari wa mbele kuwafunga midomo leo.
Bakwata imezinduka sasa Waislamu wote tumeungana katika kupigania haki zetu na kutetea maslahi yetu na serikali itambue kuwa Bakwata iko hai hao Wakristo walikuwa wapi wakati sisi tukipigania uhuru,alihoji.
Wakati huohuo, Sheikh Salum Rwambo alisema anawashangaa wabunge Waislamu ambao baadhi ni mahajat na malhaj wanakaa kimya na kushindwa kutetea hoja za msingi na kudai kuwa huo sasa ndio mwisho wao wa kuwaita masheikh na kutaka waombewe dua ili wasipate wepesi katika kampeni zao.
Sheikh Rwambo pia alimsifia mbunge wa Nzega Lucas Selelii kwamba ni miongoni mwa wabunge katika Bunge hilo wanaozungumza ukweli na kwa kujiamini tofauti na wengine ambao wanaenda kukaa bila kufanya kazi zilizowapeleka.
Source: Mwananchi
CCM watajuta kuweka swala la Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani yao uchaguzi ya 2005.
Katiba ya nchi ni kanuni ambazo jamii imejiwekea ili zifuatwe katika maisha yao ya kila siku. Kama suala ni kuingizwa kwenye katiba sioni ubaya ili mradi iwekwe wazi kuwa halazimishi mtu kwenye hilo. Mbona Hiyo BAKWATA Ilipoanzishwa wakati wa Nyerere maaskaofu hawakupinga?.
Halafu kama issue ni kuingizwa kwenye katiba, huoni kuwa kwa sheria hizohizo kuingizwa kwenye mahakama za kawaida zinakuwa tayari zimeingizwa kwenye katiba ( Sheria mama?). hoja yako bado imeelemea upande mmoja. Ndoa imefungishwa na Sheikh kwa sheria za dini yao ya kiislamu wewe hakimu Brown Christian unatumia sheria za dini isiyokuhusu kuhukumu wapi na wapi?. Huku ndiyo mwanzo wa kutafuta patashika. Kwa hili serikali imekosea inabidi watu waache idiology zao na kufanya kazi ya nchi sio maaskofu.
Hoftsede;
a. Je Mahakama ya Kadhi ni sehemu ya ibada ya Waislamu kama inavyodaiwa?
b. Je, Katiba imetoa uhuru wa kuabudu.
c. Kama a na b ni kweli, kwanini Waislamu wasitekeleza ibada yao kwa uhuru wao kama dini inavyosema bila kutaka wakristu na wasio wakristu waingilie kati ibada hiyo?
Mkandara kasema kitu kimoja muhimu sana. Sisi kama taifa tunatakiwa kujifunza na kuchukua yaliyo mema katika tamaduni mbalimbali. Tayari tunafanya hivyo. Sheria zetu zinaakisi tamaduni za jadi, dini ya kikristu na kiislamu. Ukisoma Sheria ya Ndoa ya mwaka 71 utaona kwa hata kadhi anatajwa. Hivyo, kuchukua yaliyo mema kwenye dini fulani na kuyaweka kwenye sheria zetu si jambo la ajabu. Ni kitu kinachoitwa secularization.
Nitakuambia binafsi ni sheria gani za Kiislamu ningependa ziingizwe kwenye sheria zetu na kuwa sehemu ya sheria zetu; ni zile zinazohusiana na masuala ya fedha na biashara. Wenzetu wana sheria na taratibu nzuri ambazo kuzifuata zingepunguza sana madeni yasiyo na lazima.
Sasa, kama binafsi ningependa kushawishiwa ni mambo gani yaliyo katika sheria ya Kiislamu ambayo yanaweza kumfaa kila Mtanzania hata asiye na dini? Tukiiyapata hayo tuone ni jinsi gani tutayasecularize ili yatumike kama secular laws na hivyo ni binding?
__________________ Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Mwanakijiji,
Mkuu nitaendelea kukujibu kwa sababu bado kabisa majibu yako ni ndani ya kabati hilo ulojifungia... hutaki wala husikii sauti nje ya kabati hilo..
Mkuu binafsi sikubaliani na swala la mahakama ya kadhi kwa sababu za msingi ambazo hazihusiani kabisa na dini zetu.. Ni mahakama yenyewe ya kadhi nikitazama WATU na MAZINGIRA tunayoishi ndipo nakuja na hoja zangu..lakini wewe umeshikilia Udini tuuuu kiasi kwamba maswali yako ni ya kidini tupu... ukiwaona wao ni waislaam na wewe Mkristu.. mambo ya CCM na Chadema..kwa ufinyu huo ndio maana Pinda kajibu ujenzi wa barabara Kigoma umefanywa na chama chake - CCM..
Hivi nikuulize mambo ya wanawake mathaln UWT mbona huulizi nani alaipia gharama zake. kwa nini usiwaambie wanawake wachukue dhamana ya matumizi ya chombo hicho badala ya taifa zima kulipa hali sisi sii wote wanawake..Watoto Yatima, vilema, budget ya mikoa, wilaya kwa nini tunahusishwa sote wakati wengine haituhusu!..Haya ndio mawazo yako mkuu wangu unajaribu kutuvisha lakini huyo huyo Mwanakijiji inapofikia siasa huichambua CCM kama vile yeye sii mkristu anayepinga mambo mengine..
Mkuu, unapofikiria tu kuwa waislaam ni WAO, wale, na kadhalika tayari wewe umeshaweka utengano, yaani hao wana mabaya fulani ambayo wewe hutaki kuhusishwa, hivyo hoja yako haiwezi kujenga Umoja unataka kuutangaza hapa.bali kujitenga kama unavyojitenga na Ufisadi.
Wewe unajua fika kwamba Magistrate Court Act yetu ina restrict matumizi ya Islamic law ktk maswala yote ya personal matters ya waislaam ambao Kikatiba wanaruhusiwa kufanya ibada hizo..Sasa jiulize inakuwaje unamruhusu mtu kufanya ibada zake lakini inapofikia matatizo settlement ya dispute baina ya wahusika haifanyiki kufuata misingi ya dini..
Toka wakoloni Tanzania tulikuwa na mahakama za kadhi, toka Mreno, Mjarumani, Muingereza na hata baada ya Uhuru sheria nyingi za kiisilaam ziliendelea kutumika ktk legal framework..
Nitarudia kusema, kuwa mimi binafsi natazama nje ya box na nafanya hivyo sii kwa sababu ni Muislaam isipokuwa natazama wahusika na mustakabali wa nchi nzima kwa ujumla wake kwani binafsi sina mke zaidi ya mmoja, mirathi yangu ipo ktk will na kadhalika. Binafsi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuweka vitu vyangu kulingana na mazingira ya hapa, nchi ambayo haitambui Uislaam zaidi ya dini ya Waarabu (Axis of evil)..kwangu poa vile vile lakini sii nyumbani ambaklo tunadai ati sisi ni nchi isiyokuwa na dini wakati tunatoa maamuzi mengi kufuata mfumo wa dini moja..
Kingine naelewa fika kwamba Tanzania ni Democratic secular State, imetoa ruksa kwetu sote yaani kila dini kuendesha shughuli zetu tofauti ktk maswala ndoa, Talaka, guardianship, Urithi na kadhalika lakini serikali hiyo hiyo inakataa (restrict)kutambua sheria za dini moja ktk maswala ambayo imeruhusu..Sasa jiulize kweli unawapa uhuru waislaam kuabudu au unawakaanga kwa mafuta yao wenyewe.
.
Hii ndio point ya hao Masheikh kutaka mahakama ya kadhi na kama utatumia sabnbabu zako mkuu unazidi kujenga hoja zao vizuri kwani unaonekana wewe ni Mdini..
Kinachotakiwa ni empirical and objective information. Tuwapingew kwa hoja nzito ambazo zinahusu wananchi wenyewe wanaotakiwa kupewa suluhu. mahakama ya kadhi haifungi mtu, ni mahala pa kutoa suluhu, Upatanisho kulingana na dini na wanachokiomba wao ni kutambuliwa kisheria kwa mahakama hizi ili maamuzi yao yaweze kutumika hata High Court itakapo bidi..kinyume chas kutambulika mtu anaweza kupuuza mahakama na hapo ndipo tutakapo anza kuuana ovyo..
Hivyo kabla ya kutoa suluhu Liwali anatakiwa kuzijua sheria za dini zinasema nini ktk swala husika, sio kuvuta sheria za kikristu ktk personal matters za Waislaam..tunakuwa hatujengi demokrasia ila tutagawanyika. Haya mmefikia hadi kusema waislaam wapewe kisha wagharamie, mbona leo hii tunahukumiwa kikristu na sisi waislaam tunagharamia..Hizo Biblia zilizoko Kortini, maofisi, magereza na kwingineko mnalipia nyie pekee yenu..
Wakuu sii swala la gharama tujenge hoja tuombe serikali ichukue baadhi ya sheria kuziweka ktk vipengele kwa maamuzi.. kipengele kisomeke ikiwa mhusika ni Muislaam solution ya tatizo hilo inatakiwa kuwa hivi au vile..hatuwezi sote kukumbatia culture yanu mkwa sababu tu imeletwa na Muingereza au Nyerere..Changes ni mwanzo wa kwenda mbele tusipokubali hili ni sawa na CCM anayefikiria kwamba atatawala milele..
Na believe me, huko CCM wanakuona wewe mchawi tu pamoja na kwamba unaangusha vigongo kisawasawa..Sababu kubwa, CCM nao wamejifunguia katika kabati lao (kisiasa) vile vile.
__________________
Exploration of reality
Last edited by Mkandara; 4th July 2009 at 12:46 AM..
umesema kitu ambacho kinaitwa "bottom line". Suala la kadhi ni suala la fedha. Nani afadhili na kugharimia mahakama hizo? Uongozi wa Waislamu wanasema serikali! lakini at the same time hawataki serikali kuingilia kati!? So hilo litawezekana vipi?
Baniani mbaya kiatu chake dawa!
__________________ Nobody can give you freedom. Nobody can give you equality or justice or anything. If you're a man, you take it.
Madrasa si kaazi bwana, nafikri developing countries kazi kwelikweli.... Kua mkweli haya ni matokeo ya be developing country , kwani asikudanganye mtu bwana hamna anae weza toa maamuzi yoyote juu ya nchi yake ikiwa kuna pressure za dunia ya kwanza.
Katiba ya nchi ni kanuni ambazo jamii imejiwekea ili zifuatwe katika maisha yao ya kila siku. Kama suala ni kuingizwa kwenye katiba sioni ubaya ili mradi iwekwe wazi kuwa halazimishi mtu kwenye hilo. Mbona Hiyo BAKWATA Ilipoanzishwa wakati wa Nyerere maaskaofu hawakupinga?.
Halafu kama issue ni kuingizwa kwenye katiba, huoni kuwa kwa sheria hizohizo kuingizwa kwenye mahakama za kawaida zinakuwa tayari zimeingizwa kwenye katiba ( Sheria mama?). hoja yako bado imeelemea upande mmoja. Ndoa imefungishwa na Sheikh kwa sheria za dini yao ya kiislamu wewe hakimu Brown Christian unatumia sheria za dini isiyokuhusu kuhukumu wapi na wapi?. Huku ndiyo mwanzo wa kutafuta patashika. Kwa hili serikali imekosea inabidi watu waache idiology zao na kufanya kazi ya nchi sio maaskofu.
Sasa inakuwa vipi kina Brown Christian wanapotakiwa kuchangia (kodi) uendeshwaji wa hiyo mahakama?! Kwa nini kina Alhaji Idd Al-Muslim wasichukue jukumu lote la kuendesha mahakama ikiwa ni pamoja na funding?! This is the main PUZZLE!!!!!! And, only Islams (BAKWATA) can answer it!
__________________ Nobody can give you freedom. Nobody can give you equality or justice or anything. If you're a man, you take it.
Madrasa si kaazi bwana, nafikri developing countries kazi kwelikweli.... Kua mkweli haya ni matokeo ya be developing country , kwani asikudanganye mtu bwana hamna anae weza toa maamuzi yoyote juu ya nchi yake ikiwa kuna pressure za dunia ya kwanza.
Duh! Basi tuna safari ndefu. Kama hata mahakama ya kadhi ni kufanya maamuzi kutokana na pressure ya dunia ya kwanza mh.
__________________ "Ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country"-JFK.
Mwanakijiji,
Mkuu nitaendelea kukujibu kwa sababu bado kabisa majibu yako ni ndani ya kabati hilo ulojifungia... hutaki wala husikii sauti nje ya kabati hilo..
Mkuu binafsi sikubaliani na swala la mahakama ya kadhi kwa sababu za msingi ambazo hazihusiani kabisa na dini zetu.. Ni mahakama yenyewe ya kadhi nikitazama WATU na MAZINGIRA tunayoishi ndipo nakuja na hoja zangu..lakini wewe umeshikilia Udini tuuuu kiasi kwamba maswali yako ni ya kidini tupu... ukiwaona wao ni waislaam na wewe Mkristu.. mambo ya CCM na Chadema..kwa ufinyu huo ndio maana Pinda kajibu ujenzi wa barabara Kigoma umefanywa na chama chake - CCM..
Mkandara, tatizo lako unachodai wengine wanfanya ndicho wewe unafanya. Hoja zako japo ni nzuri lakini haziwezi kusimama hadi umshambulie mtu. Mara kabati, mara droo, mara hili mara lile. Inafanya vigumu kweli kukusoma bila kukerwa na mashambulizi binafsi ya mtu. Uzuri wa hoja na nguvu ya hoja haiji kwa kulazimisha hivyo isipokuwa kwa kuitetea na kuonesha ukweli wake.
Quote:
Hivi nikuulize mambo ya wanawake mathaln UWT mbona huulizi nani alaipia gharama zake.
Sina sababu ya kuuliza kwa sababu UWT ni jumuiya ya wanawake wa CCM. Mimi si mwana CCM na si mwanamke; lakini pia kwa sababu fedha za walipa kodi wa Tanzania kinadharia haziingii kule. Nikiwa mwana CCM nitahoji.
Quote:
kwa nini usiwaambie wanawake wachukue dhamana ya matumizi ya chombo hicho badala ya taifa zima kulipa hali sisi sii wote wanawake..
Ungesema Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto hilo tutalizungumzia; lakini UWT haiendeshwi kwa fedha za serikali. Period.
Quote:
Watoto Yatima, vilema, budget ya mikoa, wilaya kwa nini tunahusishwa sote wakati wengine haituhusu!.
sijui unazungumzia nini hapa. Kama UWT basi haituhusu; kama ni mambo ya serikali yanatuhusu.
Quote:
.Haya ndio mawazo yako mkuu wangu unajaribu kutuvisha lakini huyo huyo Mwanakijiji inapofikia siasa huichambua CCM kama vile yeye sii mkristu anayepinga mambo mengine..
sijakuelewa.
Quote:
Mkuu, unapofikiria tu kuwa waislaam ni WAO, wale, na kadhalika tayari wewe umeshaweka utengano, yaani hao wana mabaya fulani ambayo wewe hutaki kuhusishwa, hivyo hoja yako haiwezi kujenga Umoja unataka kuutangaza hapa.bali kujitenga kama unavyojitenga na Ufisadi.
wewe unaona "wakristu" na "waislamu" mimi naona Watanzania. Mambo ya Waislamu hayanihusu. Bahati mbaya wao wanayafanya ya Watanzania wote.
Quote:
Wewe unajua fika kwamba Magistrate Court Act yetu ina restrict matumizi ya Islamic law ktk maswala yote ya personal matters ya waislaam ambao Kikatiba wanaruhusiwa kufanya ibada hizo.
.
sasa kama ni suala la ibada, kwani wamekatazwa na nani kuitekeleza? Hivi kuna Muislamu aliyeenda kwa Shehe na kutaka jambo lake liamuliwe kidni akakataliwa?
Quote:
Sasa jiulize inakuwaje unamruhusu mtu kufanya ibada zake lakini inapofikia matatizo settlement ya dispute baina ya wahusika haifanyiki kufuata misingi ya dini..
sasa hilo ni swali la kidini siyo la serikali. Kwanini Waislamu kwa mambo ambayo yako katika dini yao hawafanyi kile dini yao inataka hususan masuala haya ya kisheria?
Quote:
Toka wakoloni Tanzania tulikuwa na mahakama za kadhi, toka Mreno, Mjarumani, Muingereza na hata baada ya Uhuru sheria nyingi za kiisilaam ziliendelea kutumika ktk legal framework..
hili mbona halina utata. Lakini wakati wa Mkoloni tulikuwa na mambo mengi ambayo leo hatuendelei nayo. Sasa kama wakoloni walikuwa wanafanya basi na sisi tufanye? Hii hoja haina nguvu, kuna sheria ambazo tulizirithi toka kwa wakoloni na tumeeendelea kuzifuta kila inapobidi. Suala la Mahakama ya Kadhi liangaliwe kwa mwanga wa leo na mahitaji ya taifa zima.
ndiyo maana sina tatizo la mahakama za kadhikuwepo au sheria za Kiislamu ambazo zinatufaa Watanzania wote kuingizwa kwenye sheria zetu. Lakini sheria za kikundikimoja tu cha dini kuingizwa kwenye sheria zetu ili zifae kikundi hiko kimoja cha dini hilo nalikataa kwani zinafunza non-discrimination clause ya Katiba yetu.
Quote:
Nitarudia kusema, kuwa mimi binafsi natazama nje ya box na nafanya hivyo sii kwa sababu ni Muislaam isipokuwa natazama wahusika na mustakabali wa nchi nzima kwa ujumla wake kwani binafsi sina mke zaidi ya mmoja, mirathi yangu ipo ktk will na kadhalika.
Sijui kama ni kweli unataza nje ya box. Kauli zako zimejaa mashambulizi ya kidini,kejeli za kidini na kudhalilishana kidini kwa sababu tu wewe si mtu wa dini hiyo.
Quote:
Binafsi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuweka vitu vyangu kulingana na mazingira ya hapa, nchi ambayo haitambui Uislaam zaidi ya dini ya Waarabu (Axis of evil)..kwangu poa vile vile lakini sii nyumbani ambaklo tunadai ati sisi ni nchi isiyokuwa na dini wakati tunatoa maamuzi mengi kufuata mfumo wa dini moja..
nakusikia.
Quote:
Kingine naelewa fika kwamba Tanzania ni Democratic secular State, imetoa ruksa kwetu sote yaani kila dini kuendesha shughuli zetu tofauti ktk maswala ndoa, Talaka, guardianship, Urithi na kadhalika lakini serikali hiyo hiyo inakataa (restrict)kutambua sheria za dini moja ktk maswala ambayo imeruhusu..Sasa jiulize kweli unawapa uhuru waislaam kuabudu au unawakaanga kwa mafuta yao wenyewe.
hili si kweli. Hivi ni muislamu gani aliyetaka mirathi yake iendeshwe kwa minajili ya dini ya kiislamu akakataliwa? Ni nani aliyetaka talaka au kutoa talaka kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu akakataliwa au talaka yake kutotambuliwa?
je, Muislamu akitoa talaka kama inavyosemwa katika Uislamu, talaka yake serikali yetu haiitambui? Kama inaitambua je siyo huko kutambua sharia za kiislamu?
.
Quote:
Hii ndio point ya hao Masheikh kutaka mahakama ya kadhi na kama utatumia sabnbabu zako mkuu unazidi kujenga hoja zao vizuri kwani unaonekana wewe ni Mdini..
well inamhitaji mtu mmoja mdini kumjua mwingine.
Quote:
Kinachotakiwa ni empirical and objective information.
sidhani kamahili linawezekana kwa mtindo huu wa kuongozwa na dini.
__________________ Nchi hii imewahi kung' oa masultani wa kila aina. Tukianza kuvumilia masultani wakuchaguliwa tutapanda mbegu ya masultani wa kuzaliwa. - Nyerere katika "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania"
Tatizo hapa nimekuta wengi wa wanao chambua kadhia hii wapo nje ya nchi halafu wanataka waonekane wanajua sana masuala ya nchi vilivyo.Hivi nyie mnao jadiliana hapa mnajua kesi ngapi za mirathi zipo mahakamani zinazo husu Waislam na familia zao?Kwa mujibu wa sheria za kiislaam mtoto wa nje ya ndoa harithi lakini kuna kesi nyingi zimefunguliwa na hao waliozaliwa nje ya ndoa kudai mirathi kutoka kwa baba wa kiislaam ambao mahakama zetu zinachukua muda kutoa maamuzi ?Kuna akina mama waliozaa na akina baba wa kiislaam nao wanafungua kesi wapate mirathi !Kuna kesi za uongozi wa nyumba za ibada na wakfu zipo mahakamani yanatakiwa yahakumiwe kwa mujibu sheria za kiislaam,Kuna kipindi nilikuwa Iringa kulikuwa na mgogoro wa uongozi msikiti mmoja wakapeleka mahakama kuu iliyopo Iringa Jaji katika kutoa maamuzi aliwaeleza "sijaona sheria za nchi zitakazo niwezesha kutoa hukumu ya kesi yenu nawashauri mjaribu kuwatumia Masheikh wenu kutatua suala lenu".Kesi hiyo ilikuwa ya muda mrefu sana mahakamani.
Kuna kesi nyingi zinazo husu kadhia za waislam ambazo zinahitaji sheria za kiislaam kuzitatua zimechukua miaka kuamuliwa na mahakama zetu .Ndipo hapo Waislaam wanapodai mahakama za kadhi kutokana na hayo matatizo wanayo kabiliana nazo.Takriban kila familia ya kiislaam wameshaguswa na matatizo hayo yanayohusiana mirathi ,ndoa nk na matatizo ya uongozi kwenye taasisi mbali mbali za kiislaam.
Mia nipo mitaani nimetembea mitaa na maeneo mengi ya Dar es salaam .Tanga na Pwani nk nimeongea na Waislaam wengi hili suala lina wagusa sana.
Naami naawambia msiwabeze viongozi wa kiislaam wa tasisi mbali mbali hapa nchini ndiye wanao tuliza amani siku wakiwaambia waumini wao wafyatuke hapatakalika .Nyie mliopo kwenye deskptop ku type na kukujeli waislaam tutakuja kukumbushana hapa siku moja hayo mnae yakejeli.
Mungu Ibariki Tanzania