Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

    Report Post
    Results 1 to 13 of 13
    1. #1
      ndamo emmanuel's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th September 2012
      Posts : 31
      Rep Power : 347
      Likes Received
      7
      Likes Given
      1

      Post Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Ilikuwa Jumapili ya tarehe 9 Dec 2011 saa kumi na mbili asubuhi, nilikuwa nikitembelea bustani iliyoko nyuma ya Nyumba yangu. Miguu yangu ilipata mshituko wa ghafula niliposhuhudia jambo hili lililonikosesha amani, hadi nikaamua kuomba maoni kwa wasomaji wenzangu ili kupata nini hasa maana ya nilichokiona. Nilisikia mshindo mkubwa uliotokana na mwanguko wa kitu fulani kutoka katika mti mkubwa wa Mzambazau uliokuwa karibu yangu! Nilipotazama mbele yangu, nilimwona kinyonga aliyepasuka tumbo huku mayai yakitapakaa mahali pale, na alikuwa katika hatua za mwisho wa uhai wake. Mengi ya mayai hayo, yalikuwa yamepasuka yakiwa na mchanganyiko wa chembe za damu na ute mweupe kama wa yai la kuku lililoanza kutunga kifaranga! Wazo liliniijia kichwani niangalie kwa umakini zaidi,kwa maana niliwahi kusimuliwa na babu yangu kuwa kinyonga jike akipata mimba na mimba ile ikikua na kufikia muda wa kuzaa, kinyonga huyo hupanda mtini, juu kabisa ya matawi akaangalia chini na kulenga palipo na jiwe kubwa, au sehemu iliyo ngumu na akajiachia kutoka kwenye matawi ya mti huo. ili aangukiapo mwamba huo, tumbo lipasuke ili mayai yaliyokomaa tumboni mwake yapasuke vilevile ili watoke watoto walio hai baada ya yeye kufa, maana tumbo lipasukapo na uhai wake hufikia mwisho! Baada ya uchunguzi uliodumu kwa zaidi ya nusu hivi, ndipo nilipogundua yafuatayo: 1.Mzoga wa Kinyonga yule ulikuwa na mchanganyiko wa rangi ya KIJANI na MANJANO! 2. Kinyonga Yule mayai yake yalikuwa hayana dalili yoyote ya kukomaa, hivyo kupoteza matumaini na bahati nadra ya kushuhudia tukio la mwanzo wa maisha ya Vinyonga wengi watoto, walio matokeo ya mwisho wa maisha ya kinyonga jike mama yao! 3.Kifo cha kinyonga yule kilitokana na ajali baada ya kukatika tawi la mti lililoonekana pembeni kidogo ya mzoga ule! Nilikumbuka siku ya mdahalo ulioandaliwa na kituo cha katiba UDSM, mwezi mmoja kabla ya Rais kuridhia uandikwaji wa Katiba Mpya, Mchangiaji wa mwisho kabisa katika mdahalo huo Uliorushwa na kituo cha I.T.V, alikuwa mzee niliyemkadiria umri wa miaka 80 hivi, Na alisema yafuatayo………''Ili kinyoga aweze kuzaa na kuendeleza kizazi, lazima afe kabla ya watoto wake kuanza maisha.'' Akamaliza kwa kusema ‘’SITAKUFA HADI NITAKAPOSHUHUDIA KIFO CHA C.C.M’’ Niliondoka kwa huzuni bustanini, huku nikibaki na maswali mengi kadhaa yasiyo na majibu! Baadhi ya maswali yaliyokuwa yakipita kichwani mwangu ni kama yafuatayo! Nilijiuliza kuwa, Ikiwa kupasuka kwa tumbo la kinyonga yule yalikuwa ni maono juu ya kufa kwa C.C.M, Je mbona nisione mayai yakitoa watoto wa kinyonga kama ilivyo ada? Nini kitatokea ikiwa C.C.M itakufa na Isipate mrithi wa kuendeleza kizazi? Na ikiwa Mama atakufa na watoto tumboni, Nini Itakuwa Mustakabali wa kizazi kijacho kama sio GIZA? IKIWA MSOMAJI MWENZANGU UTAFIKIRIA MAONO JUU YA MAANA HALISI YA KIFO NA MATOKEO YA KINYONGA HUYU ‘’WA KIJANI NA MANJANO’’ KWA MUKTADHA WA KISIASA NCHINI TANZANIA, NISAIDIE KUBORESHA TAFSIRI YA MAONO HAYA. NOTE: NO PART OF THIS ARTICLE SHOULD BE REPRINTED NOR REPRODUCED FOR BUSINESS USES OTHER THAN IN JAMII FORUM WITHOUT PRIOR CONSENT OF THE AUTHOR. THANK U 0759-069406
      daniel don likes this.

    2. #2
      The Hunter's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th December 2010
      Location : Lubumbashi
      Posts : 910
      Rep Power : 612
      Likes Received
      233
      Likes Given
      128

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Jameni hata kama tunaichukia ccm lakini hatuna budi ku stick kwenye mipango, masimulizi na strategy zenye kuzalisha fikra chanya, hizi simulizi nadharia tuwaachie sekondari, jiulize wewe mwenyewe baada ya kumshuhudia kinyonga mfu, hukuona cha mtoto wala watoto wakitokea kwenye huo mzoga

    3. #3
      Swts's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2012
      Location : Atlanta Georgia
      Posts : 1,766
      Rep Power : 725
      Likes Received
      575
      Likes Given
      293

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Nmependa simulizi ya kinadharia. Hao watoto sasa..hmm na iv knyonga hazai bata..hatuna budi kuwaangamiza vinyonga watoto..

    4. #4
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,863
      Rep Power : 7377
      Likes Received
      6196
      Likes Given
      22555

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Maadam kinyonga huyo alikufa kwa ajali ndio maana hukuona watoto!. Kinyonga halisi ni reptilia kwanza huyaga mayai, kisha huyameza for gestation period yote na hali kitu na mayai hayo huangulia tumboni akiwa bado hai na yakishaangua ndipo hujitupa tumbo kupasuka na watoto kusambaa!.

      Huyu kinyonga halisi aliyepo hafi kwa sababu hata hayo mayai ya kumeza hayapo!. 2015 ataendelea kudunda only if watamsimamisha mgombea wangu fulani! hivyo ulichoshuhudia ni ajali tuu ya masikini kinyonga na wala sio maono yoyote!.

    5. #5
      Raia Fulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2009
      Posts : 9,339
      Rep Power : 2643
      Likes Received
      1305
      Likes Given
      846

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Ni coincidence tu hiyo, ila hata kama usingemwona huyo kinyonga ni wazi kuwa ccm kwa heri

    6. #6
      Goodrich's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2012
      Posts : 612
      Rep Power : 625
      Likes Received
      217
      Likes Given
      29

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Huyo kinyonga wa kijani na manjano atakufa na mayai yake

    7. #7
      dotto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2010
      Posts : 1,475
      Rep Power : 738
      Likes Received
      169
      Likes Given
      30

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      HAta kama vinyonga wengine wadogo wanegetokea kungekuwa na mwewe wa kuvimeza vizionekane tena. Ni hatari kuwa na vinyonga wa rangi hiyo.

    8. #8
      Mentor's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 14th October 2008
      Location : On my way to Heaven!
      Posts : 6,128
      Rep Power : 5304
      Likes Received
      3590
      Likes Given
      9842

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Quote By Pasco View Post
      Maadam kinyonga huyo alikufa kwa ajali ndio maana hukuona watoto!. Kinyonga halisi ni reptilia kwanza huyaga mayai, kisha huyameza for gestation period yote na hali kitu na mayai hayo huangulia tumboni akiwa bado hai na yakishaangua ndipo hujitupa tumbo kupasuka na watoto kusambaa!.

      Huyu kinyonga halisi aliyepo hafi kwa sababu hata hayo mayai ya kumeza hayapo!. 2015 ataendelea kudunda only if watamsimamisha mgombea wangu fulani! hivyo ulichoshuhudia ni ajali tuu ya masikini kinyonga na wala sio maono yoyote!.
      Hahahah...leo nimeujua msimamo wako!
      "Be an example.." 1 Timothy 4:12
      Irere lya Isembo ni ndeu - Benki ya mjinga ni tumbo lake.
      Mndu Kangikunda naware rero Lyako..John 14:23
      NACHO CHA RUWA
      !

    9. #9
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 7,281
      Rep Power : 0
      Likes Received
      239
      Likes Given
      1

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Quote By ndamo emmanuel View Post
      Ilikuwa Jumapili ya tarehe 9 Dec 2011 saa kumi na mbili asubuhi, nilikuwa nikitembelea bustani iliyoko nyuma ya Nyumba yangu. Miguu yangu ilipata mshituko wa ghafula niliposhuhudia jambo hili lililonikosesha amani, hadi nikaamua kuomba maoni kwa wasomaji wenzangu ili kupata nini hasa maana ya nilichokiona. Nilisikia mshindo mkubwa uliotokana na mwanguko wa kitu fulani kutoka katika mti mkubwa wa Mzambazau uliokuwa karibu yangu! Nilipotazama mbele yangu, nilimwona kinyonga aliyepasuka tumbo huku mayai yakitapakaa mahali pale, na alikuwa katika hatua za mwisho wa uhai wake. Mengi ya mayai hayo, yalikuwa yamepasuka yakiwa na mchanganyiko wa chembe za damu na ute mweupe kama wa yai la kuku lililoanza kutunga kifaranga! Wazo liliniijia kichwani niangalie kwa umakini zaidi,kwa maana niliwahi kusimuliwa na babu yangu kuwa kinyonga jike akipata mimba na mimba ile ikikua na kufikia muda wa kuzaa, kinyonga huyo hupanda mtini, juu kabisa ya matawi akaangalia chini na kulenga palipo na jiwe kubwa, au sehemu iliyo ngumu na akajiachia kutoka kwenye matawi ya mti huo. ili aangukiapo mwamba huo, tumbo lipasuke ili mayai yaliyokomaa tumboni mwake yapasuke vilevile ili watoke watoto walio hai baada ya yeye kufa, maana tumbo lipasukapo na uhai wake hufikia mwisho! Baada ya uchunguzi uliodumu kwa zaidi ya nusu hivi, ndipo nilipogundua yafuatayo: 1.Mzoga wa Kinyonga yule ulikuwa na mchanganyiko wa rangi ya KIJANI na MANJANO! 2. Kinyonga Yule mayai yake yalikuwa hayana dalili yoyote ya kukomaa, hivyo kupoteza matumaini na bahati nadra ya kushuhudia tukio la mwanzo wa maisha ya Vinyonga wengi watoto, walio matokeo ya mwisho wa maisha ya kinyonga jike mama yao! 3.Kifo cha kinyonga yule kilitokana na ajali baada ya kukatika tawi la mti lililoonekana pembeni kidogo ya mzoga ule! Nilikumbuka siku ya mdahalo ulioandaliwa na kituo cha katiba UDSM, mwezi mmoja kabla ya Rais kuridhia uandikwaji wa Katiba Mpya, Mchangiaji wa mwisho kabisa katika mdahalo huo Uliorushwa na kituo cha I.T.V, alikuwa mzee niliyemkadiria umri wa miaka 80 hivi, Na alisema yafuatayo………''Ili kinyoga aweze kuzaa na kuendeleza kizazi, lazima afe kabla ya watoto wake kuanza maisha.'' Akamaliza kwa kusema ‘’SITAKUFA HADI NITAKAPOSHUHUDIA KIFO CHA C.C.M’’ Niliondoka kwa huzuni bustanini, huku nikibaki na maswali mengi kadhaa yasiyo na majibu! Baadhi ya maswali yaliyokuwa yakipita kichwani mwangu ni kama yafuatayo! Nilijiuliza kuwa, Ikiwa kupasuka kwa tumbo la kinyonga yule yalikuwa ni maono juu ya kufa kwa C.C.M, Je mbona nisione mayai yakitoa watoto wa kinyonga kama ilivyo ada? Nini kitatokea ikiwa C.C.M itakufa na Isipate mrithi wa kuendeleza kizazi? Na ikiwa Mama atakufa na watoto tumboni, Nini Itakuwa Mustakabali wa kizazi kijacho kama sio GIZA? IKIWA MSOMAJI MWENZANGU UTAFIKIRIA MAONO JUU YA MAANA HALISI YA KIFO NA MATOKEO YA KINYONGA HUYU ‘’WA KIJANI NA MANJANO’’ KWA MUKTADHA WA KISIASA NCHINI TANZANIA, NISAIDIE KUBORESHA TAFSIRI YA MAONO HAYA. NOTE: NO PART OF THIS ARTICLE SHOULD BE REPRINTED NOR REPRODUCED FOR BUSINESS USES OTHER THAN IN JAMII FORUM WITHOUT PRIOR CONSENT OF THE AUTHOR. THANK U 0759-069406
      Haya kapitie posho yako pale KINONDONI MTAA WA UFIPA sisi tunasonga mbele na ujenzi wa taifa letu.

    10. #10
      Ginner's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th May 2011
      Posts : 630
      Rep Power : 537
      Likes Received
      125
      Likes Given
      7

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      kutokana na uelewa wangu mdogo, nimeelewa ya kwamba....kinyonga wa kijani na njano alianguka toka juu ya mti na kufa (ni kwa ajali ya kuvunjika ka tawi la mti na sio kuwa wakati wake muafaka wa kuzaa watoto kuwa umefika)

      baada ya mama kupoteza uhai, mayai yaliopasuka yenye chembe za damu yalitapakaa kila mahali katika eneo lile...( kwa mtizamo wangu ni utitiri wa vyama vya siasa vilivyopo ambavyo vingine ni vichanga vinavyokusudiwa kuwa mrithi wa mama na kuendelea na maisha ya kila siku)

      "lakini baada ya uchunguzi wa kina wa muda zaidi ya nusu saa , ikagundulika kuwa yale mayai hayakuwa yamekomaa kuweza kufanya vile vichanga kuendelea kuishi baada ya kifo cha mama yao (hapa nimeelewa kwamba...kwa mtu atakae tumia muda mwingi kutafakari, kufanya uchambuzi yakinifu, na utafiti wa kutosha.. haita mchukua zaidi ya nusu saa kwa yeye kutambua kwamba vyama vilivyopo bado havina uwezo wa kendeleza gurudumu hili la maisha kwa vile havijakomaa bado na wakati wake haujafika kwa wao kujitegemea na kuitegemeza nchi kwa ujumla)

      hiyo ni tafakari yangu ndogo tu na sio ya mleta mada. kwa maana na mimi nimeaminishwa kuwa maana ya neno ipo kwa mpokeaji wa neno na sio mtamkaji.

    11. #11
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 890
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Natafakari kwa kina

    12. #12
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,931
      Rep Power : 16839
      Likes Received
      2650
      Likes Given
      2034

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Quote By Pasco View Post
      Maadam kinyonga huyo alikufa kwa ajali ndio maana hukuona watoto!. Kinyonga halisi ni reptilia kwanza huyaga mayai, kisha huyameza for gestation period yote na hali kitu na mayai hayo huangulia tumboni akiwa bado hai na yakishaangua ndipo hujitupa tumbo kupasuka na watoto kusambaa!.

      Huyu kinyonga halisi aliyepo hafi kwa sababu hata hayo mayai ya kumeza hayapo!. 2015 ataendelea kudunda only if watamsimamisha mgombea wangu fulani! hivyo ulichoshuhudia ni ajali tuu ya masikini kinyonga na wala sio maono yoyote!.
      Nani huyo??

    13. #13
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3261
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default Re: Baada ya kifo cha kinyonga huyu wa ''kijani na manjano'' unaona nini mbele?

      Quote By ndamo emmanuel View Post
      Ilikuwa Jumapili ya tarehe 9 Dec 2011 saa kumi na mbili asubuhi, nilikuwa nikitembelea bustani iliyoko nyuma ya Nyumba yangu. Miguu yangu ilipata mshituko wa ghafula niliposhuhudia jambo hili lililonikosesha amani, hadi nikaamua kuomba maoni kwa wasomaji wenzangu ili kupata nini hasa maana ya nilichokiona. Nilisikia mshindo mkubwa uliotokana na mwanguko wa kitu fulani kutoka katika mti mkubwa wa Mzambazau uliokuwa karibu yangu! Nilipotazama mbele yangu, nilimwona kinyonga aliyepasuka tumbo huku mayai yakitapakaa mahali pale, na alikuwa katika hatua za mwisho wa uhai wake. Mengi ya mayai hayo, yalikuwa yamepasuka yakiwa na mchanganyiko wa chembe za damu na ute mweupe kama wa yai la kuku lililoanza kutunga kifaranga!

      Wazo liliniijia kichwani niangalie kwa umakini zaidi,kwa maana niliwahi kusimuliwa na babu yangu kuwa kinyonga jike akipata mimba na mimba ile ikikua na kufikia muda wa kuzaa, kinyonga huyo hupanda mtini, juu kabisa ya matawi akaangalia chini na kulenga palipo na jiwe kubwa, au sehemu iliyo ngumu na akajiachia kutoka kwenye matawi ya mti huo. ili aangukiapo mwamba huo, tumbo lipasuke ili mayai yaliyokomaa tumboni mwake yapasuke vilevile ili watoke watoto walio hai baada ya yeye kufa, maana tumbo lipasukapo na uhai wake hufikia mwisho! Baada ya uchunguzi uliodumu kwa zaidi ya nusu hivi, ndipo nilipogundua yafuatayo:

      1. Mzoga wa Kinyonga yule ulikuwa na mchanganyiko wa rangi ya KIJANI na MANJANO!
      2. Kinyonga Yule mayai yake yalikuwa hayana dalili yoyote ya kukomaa, hivyo kupoteza matumaini na bahati nadra ya kushuhudia tukio la mwanzo wa maisha ya Vinyonga wengi watoto, walio matokeo ya mwisho wa maisha ya kinyonga jike mama yao!
      3. Kifo cha kinyonga yule kilitokana na ajali baada ya kukatika tawi la mti lililoonekana pembeni kidogo ya mzoga ule!

      Nilikumbuka siku ya mdahalo ulioandaliwa na kituo cha katiba UDSM, mwezi mmoja kabla ya Rais kuridhia uandikwaji wa Katiba Mpya, Mchangiaji wa mwisho kabisa katika mdahalo huo Uliorushwa na kituo cha I.T.V, alikuwa mzee niliyemkadiria umri wa miaka 80 hivi, Na alisema yafuatayo………''Ili kinyoga aweze kuzaa na kuendeleza kizazi, lazima afe kabla ya watoto wake kuanza maisha.'' Akamaliza kwa kusema ‘’SITAKUFA HADI NITAKAPOSHUHUDIA KIFO CHA C.C.M’’

      Niliondoka kwa huzuni bustanini, huku nikibaki na maswali mengi kadhaa yasiyo na majibu! Baadhi ya maswali yaliyokuwa yakipita kichwani mwangu ni kama yafuatayo! Nilijiuliza kuwa, Ikiwa kupasuka kwa tumbo la kinyonga yule yalikuwa ni maono juu ya kufa kwa C.C.M, Je mbona nisione mayai yakitoa watoto wa kinyonga kama ilivyo ada? Nini kitatokea ikiwa C.C.M itakufa na Isipate mrithi wa kuendeleza kizazi? Na ikiwa Mama atakufa na watoto tumboni, Nini Itakuwa Mustakabali wa kizazi kijacho kama sio GIZA?

      IKIWA MSOMAJI MWENZANGU UTAFIKIRIA MAONO JUU YA MAANA HALISI YA KIFO NA MATOKEO YA KINYONGA HUYU ‘’WA KIJANI NA MANJANO’’ KWA MUKTADHA WA KISIASA NCHINI TANZANIA, NISAIDIE KUBORESHA TAFSIRI YA MAONO HAYA.

      NOTE: NO PART OF THIS ARTICLE SHOULD BE REPRINTED NOR REPRODUCED FOR BUSINESS USES OTHER THAN IN JAMII FORUM WITHOUT PRIOR CONSENT OF THE AUTHOR. THANK U 0759-069406
      Hadithi nzuri sana, lakini siku nyengine jaribu kutenganisha aya katka maandishi yako ili iwe rahisi kwa wasomaji, vyengine mtu analazimika kurejea mstari huo huo mara tatu.

      Hapo nyekundu, hicho kishindo kikubwa kilitokana na uzito wa kinyonga au na mpasuko wake?

      Na blue je, mbona ghafla umetuwekea Kidhungudhungu?
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...