Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

    Report Post
    Page 3 of 4 FirstFirst 1234 LastLast
    Results 41 to 60 of 75
    1. #1
      Mwana Mpotevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2011
      Posts : 1,972
      Rep Power : 857
      Likes Received
      908
      Likes Given
      878

      Default Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Hapa ndipo unapoona watendaji wa chini wanapokuwa na dharau kwa uongozi wa serikali ya JK

      Naibu waziri wa JK atunishiwa msuli na Mratibu wa Kata

      Atunishiwa msuli na Mratibu Elimu Kata
      *Ni baada ya kumzuia kugombea uongozi CCM

      NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI-Elimu), Kassim Majaliwa, ameonja machungu ya uongozi, baada ya kutunishiwa msuli na Mratibu wa Elimu wa Kata ya Mvumi Mission, Charles Ulanga, kutokana na kuzuiwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo.

      Lakini pamoja na Waziri Majaliwa kutoa kauli hiyo, Mratibu huyo amesema atagombea nafasi hiyo, kwa sababu ni haki yake ya kikatiba.

      Akitoa ufafanuzi kuhusiana na uamuzi wake, Waziri Majaliwa alisema kitendo cha mratibu kugombea nafasi hiyo ni kukiuka sheria.

      Licha ya kauli hiyo, mratibu huyo amechukua fomu kwa mara nyingine kwa ajili ya kutetea nafasi yake hiyo ya uenyekiti.

      Waziri Majaliwa, alisema nafasi ya Uratibu Elimu Kata, ni kazi ya kila siku ambayo haipaswi kuambatana na shughuli za kisiasa.

      “Kitendo cha Mratibu Elimu Kata kugombea nafasi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni kwenda kinyume na kanuni za utumishi.

      “Haiwezekani akaweza kutenda haki kwa watu anaowaongoza na wala hatotenda haki kwa mwajiri wake, kwa kuwa katika harakati za kisiasa ni lazima ataacha nafasi moja na kutumikia zaidi nafasi nyingine,” alisema Majaliwa.

      Alisema Mkurugenzi wa Halmashauri, ana wajibu wa kutoa majibu ya mratibu kuhusu mratibu huyo kutumikia nafasi katika chama, wakati ni muajiriwa wa halmashauri.

      Malalamiko ya kugombea kwa Ulanga katika nafasi hiyo, yalikuja baada ya baadhi ya walimu anaowaongoza kuandika barua kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Chamwino, kupinga jina lake, kupitishwa kwa madai kuwa kiongozi wao huyo hawatendei haki.

      Pamoja na mambo mengine, barua hiyo ilimtaka mratibu huyo kuchagua nafasi moja, kwani kutaka nafasi zote zinapunguza ufanisi wake wa kazi.

      Kwa upande wake mgombea huyo, alisema anayo haki ya kugombea na ana haki pia ya kuchaguliwa kwa ajili ya kuwaongoza, huku akitolea mfano wa Rais kwamba licha ya majukumu mengi, lakini bado ni mwenyekiti wa CCM.

      “Haya ni majungu tu yanayotengenezwa dhidi yangu na mimi nitaendelea kugombea na wanachama ndio wenye haki ya kumchagua mtu au kutokumchagua, lakini suala la kazi haliwezi kunizuia kuendelea na harakati zangu za kisiasa,” alisema.

      SERIKALI YA JK, KAZI IPO
      Don't break the LAW, just Bend It!

    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      nndondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2010
      Posts : 614
      Rep Power : 687
      Likes Received
      145
      Likes Given
      1

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Atamuogopa vipi wakati kaingia kwa mfumo wa kishenzi, mwalimu wa primary sijui mwenye diploma kuwa waziri mdogo wa elimu hivi mmeiona wapi na wale ma profesor wote waliojaa vyuo vyote vikiwemo vya elimu.

      Sababu tu ni mdogo wa Salma Kikwetu na mjomba wa damu wa Ridhiwani, wameichafua kabisa nchi hii halafu wanafungua midomo, huyo katibu kata mtararajiwa anajua kuwa kasoma kihalali kuliko hicho kituko cha wakina salma, hatudanganyiki mtapata tabu sana kutawala, nchi haitawaliki safisheni uchafu wote waje wanaume wenye akili watufundishe ethics,
      Chief likes this.

    4. #42
      chuwaalbert's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th September 2010
      Posts : 295
      Rep Power : 499
      Likes Received
      52
      Likes Given
      129

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Mbona Mraia Nagu, na wengine wanagombea UNEC na nafasi nyingine za kisiasa huko CCM? Tungependa wawazuie na hao!

    5. #43
      mtumishidc's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th March 2012
      Posts : 190
      Rep Power : 402
      Likes Received
      67
      Likes Given
      131

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By chigwiye
      Namfahamu Mr Ulanga,huwezi mtenganisha na siasa,iko damuni.Hata pale Kigwe alikuwa akifanya siasa na uratibu at a time.Lakini kama asemavyo ni haki yake kikatiba
      vipi kama angekuwa anafanya uratibu huku anafanya siasa akiwa CDM, bado angekuwa ana kazi ya uratibu au tungeshamsahau kwenye utumishi serikalini?
      SG8 likes this.
      "matukio hutupa UFAHAMU zaidi"

    6. #44
      Mwana Mpotevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2011
      Posts : 1,972
      Rep Power : 857
      Likes Received
      908
      Likes Given
      878

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By mtumishidc
      vipi kama angekuwa anafanya uratibu huku anafanya siasa akiwa CDM, bado angekuwa ana kazi ya uratibu au tungeshamsahau kwenye utumishi serikalini?
      swali zuri
      Don't break the LAW, just Bend It!

    7. SG8
      #45
      SG8's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Location : DSM
      Posts : 2,557
      Rep Power : 4177
      Likes Received
      771
      Likes Given
      730

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By mtumishidc
      vipi kama angekuwa anafanya uratibu huku anafanya siasa akiwa CDM, bado angekuwa ana kazi ya uratibu au tungeshamsahau kwenye utumishi serikalini?
      Angekuwa ameshatimuliwa zamani, tena bila kufuata taratibu
      "Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete,Uzembe wa Bunge na Upuuzi wa CCM"

    8. Miaka 50

    9. #46
      Foum Jnr's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th July 2012
      Location : UK
      Posts : 157
      Rep Power : 374
      Likes Received
      76
      Likes Given
      76

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Concept nzuri, utawezaje kuwa mhudumu wa kata isio na itikadi ya chama chochote huku ukiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho. Niko kwa upande wa waziri kwa hili.

    10. #47
      andishile's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2012
      Posts : 604
      Rep Power : 480
      Likes Received
      150
      Likes Given
      304

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By nndondo
      atamuogopa vipi wakati kaingia kwa mfumo wa kishenzi, mwalimu wa primary sijui mwenye diploma kuwa waziri mdogo wa elimu hivi mmeiona wapi na wale ma profesor wote waliojaa vyuo vyote vikiwemo vya elimu, sababu tu ni mdogo wa Salma Kikwetu na mjomba wa damu wa Ridhani, wameichafua kabisa nchi hii halafu wanafungua midogom, huyo katibu kata mtararajiwa anajua kkuwa kasoma kihalali kuliko hicho kituko cha wakina salma, hatudanganyiki mtapata tabu sana kutawala, nchi haitawaliki safisheni uchafu wote waje wanaume wenye akili watufundishe ethics,
      una hakika na maneno yako au unabahatisha?sasa kama hujui ngoja nikuambie kuwa mheshimiwa ana degree ya UDSM! na alishakuwa katibu wa chama cha walimu ngazi ya wilaya,ikiwemo singida!JF tujifunze kuongea na kuandika ukweli!
      Chief likes this.

    11. #48
      Same ORG's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 10th June 2012
      Location : Dubai
      Posts : 323
      Rep Power : 0
      Likes Received
      19
      Likes Given
      2

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Wabunge na mkuu wa mkoa je?

    12. #49
      JERUSALEMU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th September 2012
      Posts : 793
      Rep Power : 494
      Likes Received
      231
      Likes Given
      153

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By Mwana Mpotevu
      ni dalili pia ya kupotea kwa heshima ya watendaji wadogo kwa mabosi wao wateule wa JK
      ofisi nyingi za serikali huwezi kujua nani bosi na nani ni mhudumu.madhara ya kukulia katika siasa za ujamaa.kwakuwa anagombea uongozi ccm basi anaona hawezi kufanywa chochote.KAZI KWA MKURUGENZI WAKE,FUKUZA KAZI TU NO MORE.

    13. #50
      Mwana Mpotevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2011
      Posts : 1,972
      Rep Power : 857
      Likes Received
      908
      Likes Given
      878

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By JERUSALEMU
      ofisi nyingi za serikali huwezi kujua nani bosi na nani ni mhudumu.madhara ya kukulia katika siasa za ujamaa.kwakuwa anagombea uongozi ccm basi anaona hawezi kufanywa chochote.KAZI KWA MKURUGENZI WAKE,FUKUZA KAZI TU NO MORE.
      ni kama nyumba ya kambare, kila mmoja ana sharubu kuanzia baba, mama hadi mtoto
      Don't break the LAW, just Bend It!

    14. #51
      Gaza and Israel's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd January 2012
      Location : The West Bank
      Posts : 602
      Rep Power : 493
      Likes Received
      114
      Likes Given
      54

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Mtumishi wa umma huruhusiwi kugombea ya nafasi ya kisiasa ambayo ni ya ofisini lakini ni haki ya kila mtumishi wa umma kugombea nafasi kama za ujumbe katika chama anachokipenda. Mfano mzuri ni Mkumbo pamoja na Ballegu enzi za UDSM.
      "Tanzania has every Thing in Nature, Except Valid Technology and Politics"

    15. #52
      Gwandalized's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th January 2012
      Posts : 208
      Rep Power : 412
      Likes Received
      34
      Likes Given
      10

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Sioni kosa la mratibu hapo.
      'watanzania hawakukosea kumchagua Rais Jakaya Kikwete...walijua ana busara...' -Tundu Lissu


    16. #53
      MtamaMchungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 1,540
      Rep Power : 807
      Likes Received
      710
      Likes Given
      64

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By Mwana Mpotevu
      mkuu, kwahiyo mratibu yuko sahihi kulazimisha kugombea?
      Jamaa amewapa changamoto ya ukweli ambao uko wazi lakini wao hawataki kuuona. Watu kila siku wanapiga kelele kuhusu mlundikano wa vyeo vingi kwa mtu mmoja, tukianzia na mr President mwenyewe. Kama wanaona mratibu wa elimu hawezi kugombea nafasi ya chama kwenye kata, kwanini hawafikiri vivyo hivyo kwa mr President?? Je rais ameweza kumudu urais na uenyekiti kwa wakati mmoja? Kama ameweza, huyu mratibu atashindwaje, kama ameshindwa, mbona hawamyang'anyi kimoja?

      His argument makes perfect sense, that's all I was saying.
      No one wants to die. Even people who want to go to heaven don't want to die to get there - Steve Jobs

    17. #54
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,672
      Rep Power : 977
      Likes Received
      584
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By MtamaMchungu
      Jamaa amewapa changamoto ya ukweli ambao uko wazi lakini wao hawataki kuuona. Watu kila siku wanapiga kelele kuhusu mlundikano wa vyeo vingi kwa mtu mmoja, tukianzia na mr President mwenyewe. Kama wanaona mratibu wa elimu hawezi kugombea nafasi ya chama kwenye kata, kwanini hawafikiri vivyo hivyo kwa mr President?? Je rais ameweza kumudu urais na uenyekiti kwa wakati mmoja? Kama ameweza, huyu mratibu atashindwaje, kama ameshindwa, mbona hawamyang'anyi kimoja?

      His argument makes perfect sense, that's all I was saying.
      Mkuu kama ungepitia posts zote hapo juu usingeandika hivi. Hakuna changamoto hapo,huyo mratibu ni mbumbumbu wa sheria za utumishi wa umma! Kikwete alikua mwajiriwa wa JWTZ,baada ya Vyama vingi ilibidi achague kuwa aidha mwanasiasa ama abakie mtumishi wa umma jeshini,alichagua kuwa mwanasiasa!

    18. SG8
      #55
      SG8's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Location : DSM
      Posts : 2,557
      Rep Power : 4177
      Likes Received
      771
      Likes Given
      730

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By Gwandalized
      Sioni kosa la mratibu hapo.
      Huoni kosa kwa sababu hata sheria na kanuni za Utumishi wa Umma huzijui. Kasome extract ya standing orders nimeweka kwenye post hapo juu
      "Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete,Uzembe wa Bunge na Upuuzi wa CCM"

    19. #56
      MtamaMchungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 1,540
      Rep Power : 807
      Likes Received
      710
      Likes Given
      64

      Default

      Quote By timbilimu
      Mkuu kama ungepitia posts zote hapo juu usingeandika hivi. Hakuna changamoto hapo,huyo mratibu ni mbumbumbu wa sheria za utumishi wa umma! Kikwete alikua mwajiriwa wa JWTZ,baada ya Vyama vingi ilibidi achague kuwa aidha mwanasiasa ama abakie mtumishi wa umma jeshini,alichagua kuwa mwanasiasa!
      Sasa mjadala wote ni wa nini? Kama sheria zinamkataza, wamwache afanye then sheria zichukue mkondo wake.
      SG8 likes this.

    20. #57
      KOMBAJR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th November 2011
      Posts : 3,872
      Rep Power : 5953
      Likes Received
      803
      Likes Given
      229

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Dhaifu @ work
      Face Reality As it Is, Not As it Was or As You Wish It To Be.

    21. #58
      T2015CCM's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 13th September 2012
      Posts : 3,673
      Rep Power : 0
      Likes Received
      38
      Likes Given
      14

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Kichwa cha habari hakiendani kabisa na content

    22. #59
      Kifarutz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2012
      Posts : 1,155
      Rep Power : 573
      Likes Received
      171
      Likes Given
      4

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By Gerrard
      Kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali kwenye Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na Standing Orders for Public Service ya mwaka 2009 Mtumishi wa Umma haruhusiwi kushika nafasi yoyote ya Kisiasa ama kwa kuchaguliwa kuteuliwa lakini anaruhusiwa kushiriki shughuli za vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na mikutano. Kwa mara ya kwanza nampongeza Majaliwa kwa kusimamia ukweli hasa kwa kuwa hiyo nafasi ya Kata haina athari yoyote kwa Majaliwa. Wana JF tujifunze kusoma sheria za nchi badala ya kushabikia vitu ambavyo ukweli uko wazi. Hii ndio iliyomtoa Prof Baregu pale Mlimani na wengi humu tulilalamika kwamba ameonewa, sasa huyu ni Mwana CCM tumpongeze Waziri na Tumwambie aendelee kuwaondoa wana CCM wote waliopo kwenye Utumishi wa Umma na wana madaraka kwenye Chama. Wote tunakumbuka kwamba alipoteuliwa kugombea Uenyekiti wa UVCCM Masauni Hamad Masauni alilazimika kuacha kazi Wizara ya nishati na madini na hata yule Kashindye wa Chadema Igunga aliacha kazi tyake ya Afisa Elimu (W). Huyo Mratibu kama mnampenda mwambienni atapaoteza kazi na maslahi yake kijinga kazi ya kujifanya kushinda na sheria
      Kaka funguka zaidi kuhusu JK kuwa rais huku ni mwenyekiti wa chama

    23. SG8
      #60
      SG8's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Location : DSM
      Posts : 2,557
      Rep Power : 4177
      Likes Received
      771
      Likes Given
      730

      Default Re: Waziri wa JK ahenyeshwa na Mratibu wa Kata

      Quote By Kifarutz
      Kaka funguka zaidi kuhusu JK kuwa rais huku ni mwenyekiti wa chama
      Hizo zote ni Political Posts, hakuna aliyoajiriwa kama Mtumishi wa Umma (kwa maana ya kufuata mchakato wa ajira kama ilivyo kwa huyo MEK ambaye ni Mwalimu huku anataka siasa. Suala la JK nadhani litatatuliwa kikatiba zaidi...Jitahidi upeleke maoni kwenye Tume ya Warioba kwamba Katiba ijayo itenganishe Urais na Uenyekiti wa Chama, Ubunge na Uwaziri, Uspika na Ujumbe wa CC, n.k
      "Tumefika hapa kutokana na udhaifu wa Rais Kikwete,Uzembe wa Bunge na Upuuzi wa CCM"
      Reply With Quote

    Page 3 of 4 FirstFirst 1234 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...