Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

    Report Post
    Page 6 of 6 FirstFirst ... 456
    Results 101 to 118 of 118
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,614
      Rep Power : 46736
      Likes Received
      16716
      Likes Given
      8547

      Default Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Kwa maoni yangu ni kejeli kubwa na ni tusi kwa kudai kuwa tatizo letu la mikataba ni tatizo la watu kukosa elimu. Hivi tunaweza kusema tatizo la sekta ya afya ni watu kukosa elimu ya udaktari? au tatizo la elimu watu kukosa elimu ya ualimu? Tanzania imekuwa na wanasheria mahiri wengi tu napo wengi tu ambao wamespecialize katika international contracts na sheria hizi za mikataba. Ni kweli Tanzania haina watu wenye elimu hiyo?

      Au wanaposema tatizo ni elimu wana maana kuwa wasomi wetu (wanasheria na wengine) wanapokaa na hawa wageni kwenye meza moja wasomi wetu hawana upeo au uwezo wa kujadiliana kisomi? Kama hili ni kweli kundi lililopelekwa kujadiliana na wa Malawi lenye kuhusisha wasomi lina matumaini gani? Hivi juzi MWakyembe na wataalamu toka Wizarani wameenda Ujerumani na huko wana/wamekutana na wadau mbalimbali wa sekta ya anga na usafirishaji. Sasa waje kuingia mkataba halafu baadaye tuseme hatuna wataalamu wenye ujuzi wa mambo ya anga na usafirishaji?

      It is fallacious kudai kuwa tatizo letu la mikataba ni tatizo linalotokana na elimu? Kivipi.. hatuna wasomi, vyuo vyetu havijui kufundisha mambo ya mikataba? wanafunzi wetu ni wagumu kuelewa? au ni nini hasa? Maana hata Kikwete aliwahi kusema alipokuwa Sweden?? kuwa tatizo la nchi kuingia mikataba mibovu ni kwa sababu wanasheria wetu hawana ujuzi sana! Na hakuna aliyebisha na hivyo kufanya iaminike kuwa tatizo ni elimu.

      Sasa kama tatizo ni elimu na kuwa hatuna wasomi wa kuingia mikataba mizuri hiki kimbelembele cha kuendelea kuingia mikataba mingine kinatoka wapi? Kama kweli hatuna wasomi wenye kuweza kutuletea deals nzuri kwenye mikataba ni kitu gani kinatufanya tukubali kuingia mikataba mingine tukitarajia kuwa itakuwa tofauti? Si imewahi kusemwa kuwa the classical definition of insanity is doing the same thing, the same way, every time expecting different results? Kila ukipanda michongoma unakaa pembeni na kuombea mpunga uote? na ukiota mchongoma unalaumu udongo?
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    2. Ame is offline
      Ame
      #101
      Ame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Location : Global Citizen
      Posts : 1,516
      Rep Power : 1189
      Likes Received
      651
      Likes Given
      2615

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Elizabeth Dominic View Post
      Pasi shaka mabwana hawa wamefanikiwa systematically kuweka akili zetu bado kuwa dependant na za kitumwa. Mimi bado najaribu kuona exactly how do they do it? wanakuwaje wakati wakijadili hii mikataba, wanaweka nini mezani wenzao wakiweka maslahi yao mezani..............ni kama mazombie tu wanakubali tu pale inaposemwa tutachukua 80% na nyie 20% na vipi hawa wanaokuja bila hata mtaji na kutumia rasilimali zetu kama collateral..........hapa tamaa na maslahi binafsi yanahusika..........mbali ya kusema akili zetu ndogo zinaongoza akili kubwa. Kweli hatuna hata chembe utashi wa kawaida wa binadamu mbali ya kuweka kisomo?
      wanakuja na valid arguments na watu wetu kwakua hawana incentive hawajisumbui inabidi wakubali kwani nao wanajua what they are told is the fact.....Wanaonyeshwa jinsi walivyo culculate risks zao wanaonyeshwa jinsi kulivyo na berokrasia katika kutoa vibali na rushwa inayo ambatana navyo mpaka investment kufanyika..Mengine hawaambiwi ila kwakutumia akili hao watanzania wanaelewa tu hawana la kufanya bali ku-dance in the tune ya walioshika makali.....Wafanyeje? Wakati mwingine ni informal contracts kati ya investors na familia husika huku wataalamu wakiwa hao watoto wa mafisadi..and a lot of issues in it investors wafanyeje? Ndiyo maana wanarudi tena publicly kupiga kelele na kuwatolea report ya human rights violation, coruptions etc

    3. #102
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Elizabeth Dominic View Post
      Pasi shaka mabwana hawa wamefanikiwa systematically kuweka akili zetu bado kuwa dependant na za kitumwa. Mimi bado najaribu kuona exactly how do they do it? wanakuwaje wakati wakijadili hii mikataba, wanaweka nini mezani wenzao wakiweka maslahi yao mezani..............ni kama mazombie tu wanakubali tu pale inaposemwa tutachukua 80% na nyie 20% na vipi hawa wanaokuja bila hata mtaji na kutumia rasilimali zetu kama collateral..........hapa tamaa na maslahi binafsi yanahusika..........mbali ya kusema akili zetu ndogo zinaongoza akili kubwa. Kweli hatuna hata chembe utashi wa kawaida wa binadamu mbali ya kuweka kisomo?
      Shukran sana ktk hili maana tunaenda mahala ktk kujitambua. Pengine wakati najaribu kuijibu hoja ya Mwanakijiji inabidi kwanza tufikirie kwamba maadui wetu ni UMASKINI na UJINGA. Na Tunaposema Maadui ina maana hawa ndio wanaotuweka chini hivyo haiwezekani moja kuwa suluhu la jingine. Pengine kuna tumaini fulani la Mtanzania kwamba tukipata kuelimika kwanza basi tumekabidhiwa silaha ya kuondoa Umaskini wakati haipaswi kabisa kufikiria hivyo isipokuwa Umaskini wenyewe utaondolewa vipi..

      Kwa hiyo tumejifunza nini ktk elimu tulopewa!.. maana ifike mahala tujitazame wenyewe na kuutambua kwamba wasomi wetu wameondokana tu na adui mmoja hivyo wanapopewa dhamana ya kuongoza hujifikiria kuondokana na Umaskini maana tumewakabidhi silaha ya kupambana na Umaskini. Na haingekuwa mbaya kama fikra hizi zingewalenga kuwaokoa Watanzania wote. Elimu ikatumika kama fundisho la mwokozi iwe zimamoto au lifeguard... Lakini laa haswa elimu tulofundishwa ni ile inayoendana na mazingira ya Ulaya ambako kila mmoja wao husoma kwa kumwendeleza yeye na ktk hesabu ya wengi walosoma hivyo ujumla wao utaiwezesha nchi kuendelea zaidi. Dada Mazingira yetu tofauti, leo hii ukipata ajali watu hawaji kukuokoa ila huja kukuvua mkufu, simu, laptop, viatu na hata suruali maana mtaji wa maskini ni maskini mwenzake.

      Hivyo maadam leo hii vyama vyetu vya siasa pamoja na wasomi wetu hawalengi kumwokoa Mtanzania mwingine toka ktk umaskini na Ujinga isipokuwa ni mfumo wa biashara baina yetu.. Tunategemea vipi wakili alosoma ktk elimu ya biashara kuitetea Tanzania iweze kupata pango zuri ilihali mazingira yenyewe hayakuandaliwa hivyo wala yeye hakusomeshwa ili kuwakomboa Watanzania wenzake bali kuuziana maana soko lipo nyumbani. Hata tunaposema Uzalendo lazima tuupime mfumo umelenga uzalendo huo kwa nani?.

      Nakumbuka wakati wa Nyerere tulisoma tukijua wazi tunaelimika ili kujikomboa toka ktk Ujinga, sera na mfumo wa kiutawala ulilenga kukomboana na sii mtaji wa maisha au soko la biashara lakini hili limebadilika toka mwaka 1992 ambapo elimu imewekwa sokoni. Na ndio maana Madaktari wamegoma kwa sababu wanaitazama profession yao kama professional nyinginezo ktk lindi la Biashara. They have a point kama hawa wanasheria na wasomi wengine tunao washangaa. Maana kwa kila msomi elimu yake ni silaha ya kumuondoa ktk Umaskini badala ya nyenzo ya upembuzi, hivyo kina Chenge, Mkono na wanasheria wengine wote tumewakabidhi silaha au mtaji wa biashara na sio nyenzo ya kuwakomboa Watanzania...
      Last edited by Mkandara; 21st September 2012 at 17:15.
      August, Pasco, Narubongo and 1 others like this.
      Exploration of reality

    4. #103
      Wamunzengo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd August 2012
      Posts : 500
      Rep Power : 446
      Likes Received
      126
      Likes Given
      4

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Capital View Post
      Kasome na wewe. problem kubwa ni kuwa wasomi wengi wamekuwa sidelined katika organs za kutoa maamuzi na badala yake mediocres au junks ndo wamejaa huko.

      Kwa Tanzania, wajinga ndo viongozi wa welevu, ajabu sana. mchango wa wasomi haupo kwani wana kilio cha kusaga meno, wanasiasa ambao wengi hardly wana kashahada kamoja kama siyo vyeti vya kuungaunga ndo thinkers and decision makers.

      Changamoto kwa wasomi ni kuwa mpaka lini vilaza wataendelea kutushika masikio? kwa hali ilivyo wasomi wanapata ulaji toka kwa watu wasiosoma kwa hiyo ni ngumu kufikiria na kutenda zaidi ya kilaza aliyekupa ulaji.

      Wasomi tuwe na courage na intent tuwaambie vilaza kwanza wakasome, watuachie nchi, miaka 10, tz itakaribiana na S.Afr.

      Cha kushangaza, vilaza wana mikakati ya kuwabana wasomi na wasomi hawana mkakati wa kuwabana vilaza. sijui ni laana ama nini.
      Duh!!! mkubwa umenishika ile kisawasawa, you have real made my day. umenisaidia sana kuunganisha dots fulani nilizokuwa nazo kichwani.

      Ame likes this.

    5. #104
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,752
      Rep Power : 1168
      Likes Received
      253
      Likes Given
      2541

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Zitto View Post
      Nitakupa mfano wa wasomi walioshindwa kutumia elimu zao na hivi sasa wanaonekana kama tumaini kwa serikali ya CCM. Prof. Muhongo - alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO mwaka 2005. Aliruhusu Kiwira kuuzwa kwa Mkapa, Yona na wenzake. Alikuwa mshauri mtaalamu kwa kampuni ya Sutton Resources ilipokuwa inauza mgodi wa Bulyanhulu kwa Barrick. Alikuwa kwenye timu iliyoandika sera ya madini ya mwaka 1997 na sheria ya madini ya mwaka 1998 ambayo ndio chanzo cha mikataba ya sasa ya madini ambayo imeligharimu sana Taifa.
      Huyu ni msomi lakini at the hour of need hakusaidia jamii yake. Hata tulipokuwa tunahangaika (ukiwemo wewe MwanaKijiji) kuleta mabadiliko katika sekta ya madini hakupaza sauti yake. Hawa ndio wasomi wetu.

      Ninapingana na hitimisho lako ambalo ndio ulianza nalo kwenye kichwa, mikataba mibovu inatokana na elimu mbovu. Elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi badala ya maslahi ya Umma.
      i salute you kwa kuelezea upande wa pili wa Prof wetu (tumaini lililopotea) lakini hiyo ya chini "kwamba mikataba mibovu ina tokana na elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi" mimi kwa muono wangu mikataba mibovu inatokana na ubinafsi au lack of committment. Maana ka suala la usomi, kuna Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, licha ya kutokusoma kwake lakini kuna vitu vingi tu vya busara alifanya kwa maslahi ya Zanzibar, hata Iddi Amin kwa mfano kununua ofisi za ubalozi za Uganda wakati ule. hata mimina wewe leo hii tukiangukia huko sio kwa sababu hatuelewi,bali ni kutokanana kuweka maslahi binafsi mbele kuliko ya Taifa, sema sasa inaweza kutokea tatizo jingine kutokana na mahitaji binafsi ya binadamu nalo ni kipato/mshahara na assurance kwa watendaji wetu zinaangaliwaje? na jinsi nionavyo mimi kuna level ambayo maslahi hayo yanaangaliwa kuanzia wakurugenzi, makamishina, makatibu wakuu, mawaziri, PM na Raisi lakini bado tu tunaangukia kwenye matatizohayo hayo. Kulikoni? tumekuwa wa rahisi saana kununuliwa au kuangalia ufalme wetu?
      Ame likes this.

    6. Ame is offline
      Ame
      #105
      Ame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Location : Global Citizen
      Posts : 1,516
      Rep Power : 1189
      Likes Received
      651
      Likes Given
      2615

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By August View Post
      i salute you kwa kuelezea upande wa pili wa Prof wetu (tumaini lililopotea) lakini hiyo ya chini "kwamba mikataba mibovu ina tokana na elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi" mimi kwa muono wangu mikataba mibovu inatokana na ubinafsi au lack of committment. Maana ka suala la usomi, kuna Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, licha ya kutokusoma kwake lakini kuna vitu vingi tu vya busara alifanya kwa maslahi ya Zanzibar, hata Iddi Amin kwa mfano kununua ofisi za ubalozi za Uganda wakati ule. hata mimina wewe leo hii tukiangukia huko sio kwa sababu hatuelewi,bali ni kutokanana kuweka maslahi binafsi mbele kuliko ya Taifa, sema sasa inaweza kutokea tatizo jingine kutokana na mahitaji binafsi ya binadamu nalo ni kipato/mshahara na assurance kwa watendaji wetu zinaangaliwaje? na jinsi nionavyo mimi kuna level ambayo maslahi hayo yanaangaliwa kuanzia wakurugenzi, makamishina, makatibu wakuu, mawaziri, PM na Raisi lakini bado tu tunaangukia kwenye matatizohayo hayo. Kulikoni? tumekuwa wa rahisi saana kununuliwa au kuangalia ufalme wetu?
      August,

      Kuna mchangiaji mmoja kasema wasomi tumekubali kushikwa masikio na mediocres na pia elimu Tanzania imegeuka kuwa prestige na siyo nyenzo ya kuondoa matatizo yetu I mean solving our development and social problems. Hapa nitatoa mfano wa head of the state hivi anaelewa nini maana ya yeye kukubali kuitwa Dr. wakati hiyo ni honored degree? Najaribu kuangali kwanini Nyerere haku wahi kutumia hiyo title wakati ameandika scholarly articles kibao na kuwa reference hata kwenye concept ya ujamaa na kujitegemea?

      Hao viongozi wakuu ni role models so kila action wanayo i-potray iwe social economic ama hata statutory ina high impact kwenye attitudes na behaviour... Implication ya viongozi kupenda kuwa adressed kwa vyeo vya ki-academics wakati wao ni politicians ina negative impact kwenye knowledge na hasa invention and innovation..Maana badala ya watu kupigana kupata title kwa kuvumbua kitu watapigana ile wawe ma-rais na mawaziri, ma-katibu wakuu CEOs etc vyeo ambavyo vinahitaji basics tu katika decisionmaking na wala siyo invention and innovation ambapo science and technology inapoangukia..Usidhani Obama ni mjinga kuacha kujiita Professor kama Rais wa US kama alivyokuwa akiwa chuoni akifundisha..

      Pia how do we compansate our people ina maana salaries..Utaona kwetu ni siasa ndiyo the most paying job na yenye imediate return kiasi cha ku leta high demand unnecesary katika decision making position i.e parliament, administrative kwenye serikali na Jury kwenye Judiciary positions. Kwa hiyo as a result watu wote wanao soma hakuna hata mmoja analenga kuleta invention ama ku boresha existing ideas kwa context ya nchi yetu..Wote mawazo ni wapate vyeti ili wawe wabunge, wakurugenzi, makatibu, wakuu, Rais, mawaziri so you can see the objective of knowledge here is not about bringing solutions to the problems but to get well paid through honored positions and ultimately we reduce knowledge to be a symbol of prestige and not a problem solving tool.

      Kwenye academia hivyo hivyo watu wako busy kufanya lolote wapate u-profesor hata wakati hawa wezi prophesy any thing...Nao hao wanaojipandisha bila ku-reflect wanachoki-claim kuwa nacho wako busy kutengeneza by-laws za kujihakikishia wao tu ndiyo wanakuwa rewarded huku wale wa chini wakipewa rules ngumu ngumu ku-climb the ladder kwakua wanajua wengi wakifuata nyayo zao in not less than 5 years everybody atakuwa profesor so what they do ni ku-kick the ladder maana kwakua hawajafanya impact yoyote kwenye production sector basi serikali haitaweza kuwalipa kwa kiwango kinachotakiwa...

      Hakuna udanganyifu its a rule of thumb you cannot eat what you dont produce..Economy imejengwa katika equlibrium labda tuje na principle za kwetu house holds ni consumers na hao hao ndiyo wanatoa capital kwa producers ili waweze ku-supply!
      Last edited by Ame; 23rd September 2012 at 20:10.
      Mkandara, August and ral like this.

    7. #106
      paulss's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th August 2009
      Posts : 3,636
      Rep Power : 4411
      Likes Received
      1105
      Likes Given
      986

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Binafsi siamini kabisa kama tatizo ni elimu za wasomi wetu hata kama wamesoma ili kupata vyeti tu
      Tatizo ni mifumo mibovu ya kimaadili inayotoa mwanya wa hao wasomi kufanya mambo kwa ubinafsi wao badala ya taifa bila woga wala hofu yoyote pasi na kuulizwa na yeyote

      Nchi hii utawala wa kweli wa sheria ni kizungumkuti kabisa, hivi leo kijana anaajiriwa kutoka chuo kikuu na TRA anafika pale anakuta kuanzia muhudumu hadi kamishna wanacheza deal la kupunguza na misamaha ya kodi, unategemea nini kutoka kwa msomi huyu? unategemea awe na uzalendo gani kwenye mazingira haya? mazingira yanafanya anakuwa wale wale tu na anaona ni sehemu ya maisha ya kawaida kabisa

      Nchi za wenzetu mtu pamoja na uzalendo alio nao lakini sheria zinafanya kazi kweli, ukibainiki kuingia mikataba ya kipuuzi kwa maslahi yako binafsi umekwisha, china unanyongelewa mbali....lakini hapa bongo serikali nzima hadi bungeni wanatumia muda na nguvu nyingi kumkingia mtu kama huyo kifua.

      Ni hulka ya binadamu tu kutaka zaidi kwa maslahi yake na ndio maana tunaongozwa na taratibu zinazo simamiwa na sheria, hakuna utawala wa kuheshimu sheria nchini kabisaa na hatuwezi kuishia kuwalaumu wanasheria tu,
      Kuna wahasibu, wanunuzi nk nk hawa wote ni wasomi kubwa lakini kwakuwa sheria hazitekelezwi basi wanatumia mwanya huo kuendeleza hulka ya ubinaadam kutaka zaidi kwa maslahi yao

      Nchi hii kuwa msomi mkubwa na kupata madaraka makubwa serikalini ndivyo unavyokuwa safe zaidi kwenda kinyume cha taratibu kwa kufisadi zaidi uwezavyo bila bughudha.
      Na unakuwa hatarini zaidi kama utakuwa ngumbaru na kuiba kuku maana utaishia kutiwa kibiriti ukiwa hai
      Last edited by paulss; 24th September 2012 at 09:30.

    8. #107
      nderingosha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th March 2011
      Posts : 863
      Rep Power : 1461
      Likes Received
      450
      Likes Given
      127

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      Kwa maoni yangu ni kejeli kubwa na ni tusi kwa kudai kuwa tatizo letu la mikataba ni tatizo la watu kukosa elimu. Hivi tunaweza kusema tatizo la sekta ya afya ni watu kukosa elimu ya udaktari? au tatizo la elimu watu kukosa elimu ya ualimu? Tanzania imekuwa na wanasheria mahiri wengi tu napo wengi tu ambao wamespecialize katika international contracts na sheria hizi za mikataba. Ni kweli Tanzania haina watu wenye elimu hiyo?

      Au wanaposema tatizo ni elimu wana maana kuwa wasomi wetu (wanasheria na wengine) wanapokaa na hawa wageni kwenye meza moja wasomi wetu hawana upeo au uwezo wa kujadiliana kisomi? Kama hili ni kweli kundi lililopelekwa kujadiliana na wa Malawi lenye kuhusisha wasomi lina matumaini gani? Hivi juzi MWakyembe na wataalamu toka Wizarani wameenda Ujerumani na huko wana/wamekutana na wadau mbalimbali wa sekta ya anga na usafirishaji. Sasa waje kuingia mkataba halafu baadaye tuseme hatuna wataalamu wenye ujuzi wa mambo ya anga na usafirishaji?

      It is fallacious kudai kuwa tatizo letu la mikataba ni tatizo linalotokana na elimu? Kivipi.. hatuna wasomi, vyuo vyetu havijui kufundisha mambo ya mikataba? wanafunzi wetu ni wagumu kuelewa? au ni nini hasa? Maana hata Kikwete aliwahi kusema alipokuwa Sweden?? kuwa tatizo la nchi kuingia mikataba mibovu ni kwa sababu wanasheria wetu hawana ujuzi sana! Na hakuna aliyebisha na hivyo kufanya iaminike kuwa tatizo ni elimu.

      Sasa kama tatizo ni elimu na kuwa hatuna wasomi wa kuingia mikataba mizuri hiki kimbelembele cha kuendelea kuingia mikataba mingine kinatoka wapi? Kama kweli hatuna wasomi wenye kuweza kutuletea deals nzuri kwenye mikataba ni kitu gani kinatufanya tukubali kuingia mikataba mingine tukitarajia kuwa itakuwa tofauti? Si imewahi kusemwa kuwa the classical definition of insanity is doing the same thing, the same way, every time expecting different results? Kila ukipanda michongoma unakaa pembeni na kuombea mpunga uote? na ukiota mchongoma unalaumu udongo?
      si chanzo cha mikataba mibovu tu..bali chanzo cha matatizo yoote ya watanzania ni watanzania wenyewe.....hapa swala si kuwa au kutokuwa na elimu.....la hasha...hata kama nchi hii ingekuwa imejaa wasomi bado tungekuwa na matatizo tuliyonayo......By the way....kama swala ni ukosefu wa elimu ya mikataba.......bado kama watu(watanzania)wangetaka tuwe na mikataba mizuri tungekuwa nayo tu.....kwani kuna consultants au exparts ambao wako kwenye kila field kwa ajili ya mambo haya......hapa issue ni ukosefu wa uzalendo kwa watu wa tanzania.....haijalishi wamesoma au hawajasoma....mbona vi nchi kama Botswana na Namibia wanafaidi raslimali zao?????wakati hawana wasomi kama tulionao!!!!mbona nchi kama Rwanda tunaona wanasonga mbele??wakati ni juzi tu walikuwa wanakatana mapanga!!!!hata Msumbiji wanatushinda kwa kasi ya maendeleo!!!why????....kwasaba bu watu wa Tanzania wana tatizo kubwa la msingi la kukosa uzalendo(patriotism)...hata ukizungumza na watanzania(wasomi na wasio wasomi)utagundua tofauti kubwa sana kimantiki juu ya misimamo yao kama watanzania....haswa ukiwalinganisha na raia wa nchi nilizotaja juu(mfano)......hata mwanakijiji mlugaluga asiye na chembe ya elimu toka tz ana tofauti kubwa sana ukimlinganisha na mwenzake toka nchi nilizotaja......vile vile msomi wa tz......Nakushauir ufanye utafiti wa haya nayosema alafu utapata jibu la swali lako....Adui wa mtanzania ni mtanzania mwenyewe.....na hili limeanzia ngazi ya famlia zetu.....toka wazazi wanapowapeleka watoto wao shule mpaka wanapopata ajira....watu wanaopenda short cuts kwenye maisha utawategemea vipi wawe wajenga nchi???hao ndo watanzania.....
      ....real change begins with PEOPLE.......

    9. #108
      Tausi Mzalendo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd May 2010
      Location : Solomon Island
      Posts : 1,457
      Rep Power : 891
      Likes Received
      681
      Likes Given
      865

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Tanzania bana ni nchi ya aina yake.
      Matatizo hatujayaona bado.Fikirieni haya:
      1. Sekta ya sheria ime"ingiliwa" - kumbukeni aliyoyasema Tundu Lissu. Uteuzi wa watendaji - majaji. Huko nyuma wananchi tuliamini kuwa kadiri unavyoenda ngazi za juu katika mfumo wa mahakama, ndivyo uwezekano wa kupata haki uliongezeka. Sasa hawa majaji wenye "walakini" wanaoteuliwa kila siku, na wengine wanajulikana wana chamber zao zilizo active, tutegemee nini? Kesi ya nyani inapomfikia ngedere itakuwaje?
      2. Mtihani wa kuchagua jibu ni A, B, C au D - MULTIPLE CHOICE hatima yake itakuwa nini?
      Kwa kifupi sana, unapokuwa na mifumo mibovu ya kila kitu kuanzia elimu hadi uteuzi wa watendaji usitegemee miujiza.Mikataba mibovu haina uhusioano na elimu ya wanaoijadili.Unapokuwa na watendaji waliosoma vizuri lakini wakateuliwa na kupewa kazi kwa masharti ya kufikia lengo fulani, usitegemee waonyeshe umahiri na weledi kiutendaji.

      Hicho MM unachokisema hapa ni kizungumkuti! Ushaona utando wa buibui ulivyo? Basi tafuta kianzio cha kutandua.
      Mzee Mwanakijiji and August like this.
      "You were born an original. Don't die a copy." —John Mason

    10. #109
      omujubi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Location : Bumbire Island
      Posts : 1,716
      Rep Power : 724
      Likes Received
      690
      Likes Given
      1774

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Elizabeth Dominic View Post
      Pasi shaka mabwana hawa wamefanikiwa systematically kuweka akili zetu bado kuwa dependant na za kitumwa. Mimi bado najaribu kuona exactly how do they do it? wanakuwaje wakati wakijadili hii mikataba, wanaweka nini mezani wenzao wakiweka maslahi yao mezani..............ni kama mazombie tu wanakubali tu pale inaposemwa tutachukua 80% na nyie 20% na vipi hawa wanaokuja bila hata mtaji na kutumia rasilimali zetu kama collateral..........hapa tamaa na maslahi binafsi yanahusika..........mbali ya kusema akili zetu ndogo zinaongoza akili kubwa. Kweli hatuna hata chembe utashi wa kawaida wa binadamu mbali ya kuweka kisomo?
      hii post yako Elizabeth Dominic imenigusa sana na nimetumia muda wangu tangia nilivyoiona kufikiria sana juu ya hili.
      Unajua ni kama vile tunazumguka mbuyu lakini hapa ndipo chanzo cha tatizo. Wewe hebu fikiria, pamoja na resources zote zilizopo sasa hivi kumpatia taarifa Mtanzania lakini bado tumebakia kuwa 'manunda' tu na hatutaki kubadilika bali tunabakia fitina na unafiki tu!!!
      Mwishowe nakasoma kwenye gazeti la Mwananchi la jana Jumapili wakikumbushia story ya yule mlemavu wa Kisarawe Mohamed Kondo aliyependekeza kwenye mkutano wa kutoa maoni ya katiba kuwa Wimbo wa Taifa ufutwe. Ni kweli baada ya kuulizwa kwa nini akasema hawa wote walioko juu ni wezi lakini tunalazimika kila siku kumuomba Mungu awabariki kupitia wimbo wetu wa taifa!!
      Ukichukulia ile sheria ya Kimungu kuwa "Kila aombaye hupewa" kwa maana hiyo hawa jamaa na madudu yao huenda wakendelea kufaidi maana sisi ndio tunaowaombea, wimbo hauna maaudhui ya 'kuwaombea wananchi wa kawaida'.
      Tunajiroga wenyewe.

      August and ral like this.
      “those who are so ready to take what is not theirs must be ready to loose what is theirs”

    11. #110
      Stephen Buloya's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st August 2007
      Posts : 29
      Rep Power : 612
      Likes Received
      11
      Likes Given
      365

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Pasco View Post
      Wapinzani wakuu Chadema wanaendelea kufanya kazi kibunge, kusubiri kwanza mawaziri kamili kuleta sera zao kisha wao mawaziri vivuli watoe sera mbadala!.

      Kwa maoni yangu, kama ni kweli Chadema mnataka kujipambanua kuwa sasa mmeisha wiva vya kutosha na mko tayari kukabidhiwa nchi mwaka 2015, lazima mmbadilike, msiisubiri CCM iendelee to lead the way, you must come forward and show the way, the right way ili CCM nao wakija ama wafuate njia ya kweli au wawe forced to show the wrong way na wananchi wawe na options ya choice wachague nini na chochote watakacho chagua iwe wamekichagua for justified reasons kuwa kitatutoa hapa tulipo na kutufikisha pale!.

      Zitto, kwenye suala hili la mafuta na gesi, kwa vile hatuna sera, this is an opportunity kwa Chadema to come with the best ever policy ahead of policy ya serikali na serikali will be left with no options lazima kuna vitu wataviiga watake wasitake na hii sasa ndio plus for Chadema na justified reasons to vote out CCM come 2015 besides kuichoka!, na iwe ndio justified reasons to vote in Chadema besides kuipenda. Chadema ijenge reasons to be votted in!.

      Kama sera ya madini ya CCM mrahaba ulikuwa asilimia 03% na kwa sheria mpya ni asilimia 04% ambayo makampuni ya madini yameigomea kwa kisingizio cha kuheshimu mikataba ya zamani ya kinyonyaji, Chadema inapaswa ije na sera mbadala ikionyesha what is the best deal ili wananchi waweze kutofautisha CCM na Chadema na kuelewa kuendelea kuichugua CCM ni kuendelea kuwa masikini na kuichagua Chadema ni kuchagua ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.
      Pasco.
      Kama nilimuelewa Zitto kwenye post yake kuhusu sekta ya gesi, suluhisho la kudumu ni uwazi kwenye mikataba. Whatever alternative policy that may be put forward. When it comes to exploiting natural resources, anything less than full transparency in contracts will be meaningless. Hakuna nchi ilioendelea duniani kwa kuingia mikataba na multinational enterprises kwenye uwekezaji katika strategic sectors za uchumi bila mikataba hiyo kupitia na bunge au mikataba kuwa wazi. USA. Canada na hata Australia zote zina hazina kubwa ya natural resources, all of them are leading capitalist nations and yet contracts to invest in natural resources are transparent.

      When there is transparency, mapungufu yote yanakuwa wazi na mianya ya kufanya ujanja ujanja unazibwa. Tatizo la elimu ubinafsi e.t.c. litatoweka. Having said that I am looking forward to policy alternatives from Chadema.
      Last edited by Stephen Buloya; 25th September 2012 at 17:35.
      August and Pasco like this.

    12. #111
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Narudia kusema hivi maadam gatuna sheria ya madini, hatuna msimamo wa imfumo kuhusu Taxation kama wenzetu hizi ELIMU pasipo tunazosoma pasipo mwongozo ni sawa kabisa na Zitto alivyosema kuwa "kwamba mikataba mibovu ina tokana na elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi" maana utawezaje kusema maslahi ya taifa ikiwa hatuna mwongozo wa mapato hivyo unatetea kisheria kitu ambacho kimepitishwa halafu watu mkapata kupima na kuzijadili wapi tumekosea. Tazama wenzetu Botswana Bofya
      Exploration of reality

    13. #112
      paulss's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th August 2009
      Posts : 3,636
      Rep Power : 4411
      Likes Received
      1105
      Likes Given
      986

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By Mkandara View Post
      Narudia kusema hivi maadam gatuna sheria ya madini, hatuna msimamo wa imfumo kuhusu Taxation kama wenzetu hizi ELIMU pasipo tunazosoma pasipo mwongozo ni sawa kabisa na Zitto alivyosema kuwa "kwamba mikataba mibovu ina tokana na elimu ambayo inaangalia maslahi binafsi" maana utawezaje kusema maslahi ya taifa ikiwa hatuna mwongozo wa mapato hivyo unatetea kisheria kitu ambacho kimepitishwa halafu watu mkapata kupima na kuzijadili wapi tumekosea. Tazama wenzetu Botswana Bofya
      Mkuu Mkandara kimsingi nakubaliana na hoja zako kuwa kutokuwa na sheria za madini na mifumo ya kodi inaweza kuwa tatizo lakini ukiangalia kwa makini utaona hawa wasomi hawafanyi tu mikataba hii kwa makosa ya kutofahamu vizuri sheria.........
      Kunakitu zaidi mkuu, hawa wasomi wako free kufanya watavyo kwa maslahi yao binafsi na pengine kwa maelekezo ya viongozi wakubwa wao, hawabanwi na yeyote
      Mkandara likes this.
      Independent thinker
      Humu jf baadhi yetu wametengeneza haki miliki ya they way they think, you have to think like them and have drawn a line of where one has to belong, you are either "with us" or "against us", if you don't sail the same boat then you are an enemy!. -Pasco wa JF

    14. #113
      wa hapahapa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd August 2012
      Posts : 210
      Rep Power : 385
      Likes Received
      21
      Likes Given
      35

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      tatizo
      1. ni kucopy na kupaste mikataba pasipo kusoma ndani
      2. wawakilishi kwa niaba ya wananchi wanatanguliza maslahi yao mbele pasipo kujari
      maslahi ya Taifa
      3. wawekezaji ni wajanja sana wanaweza ku rob akili ya mwakilishi wa wananchi na kujikuta anapata mgao wake mapema

    15. #114
      wa hapahapa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd August 2012
      Posts : 210
      Rep Power : 385
      Likes Received
      21
      Likes Given
      35

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      tatizo
      1. ni kucopy na kupaste mikataba pasipo kusoma ndani au kupuuza Contents mmmbovu... za mkataba makusudi
      2. wawakilishi kwa niaba ya wananchi wanatanguliza maslahi yao mbele pasipo kujari
      maslahi ya Taifa
      3. wawekezaji ni wajanja sana wanaweza ku rob akili ya mwakilishi wa wananchi na kujikuta anapata mgao wake mapema

    16. #115
      wa hapahapa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd August 2012
      Posts : 210
      Rep Power : 385
      Likes Received
      21
      Likes Given
      35

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      tatizo
      1. ni kucopy na kupaste mikataba pasipo kusoma ndani au kupuuza Contents mmmbovu... za mkataba kwa makusudi
      2. wawakilishi kwa niaba ya wananchi wanatanguliza maslahi yao mbele pasipo kujari
      maslahi ya Taifa
      3. wawekezaji ni wajanja sana wanaweza ku rob akili ya mwakilishi wa wananchi na kujikuta anapata mgao wake mapema

    17. #116
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,911
      Rep Power : 1169
      Likes Received
      1056
      Likes Given
      804

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      kuna mtu anaitwa Msema aliwahi kutaja vigogo kadhaa wa kisiasa wakiwa na vyeti feki, hakuna hatua iliyochukuliwa hatua, wapo wanadunda wala hawakuchunguzwa, juzijuzi professor mmoja sikumbuki vizuri kama wa UD au wapi alipoint out kuwa 80% ya degree za Tanzania zina walakini au watu wamefanyiwa tafiti au walikopi tafiti za wengine hakuna aliyefuatilia so kuna possibility kubwa wanaoshiriki kwenye mikatabahiyo ni wa aina ya Msemakweli aliotaja au ni miongoni mwa hao 80% alio point professor!
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    18. #117
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4930
      Likes Given
      4509

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Quote By paulss View Post
      Mkuu Mkandara kimsingi nakubaliana na hoja zako kuwa kutokuwa na sheria za madini na mifumo ya kodi inaweza kuwa tatizo lakini ukiangalia kwa makini utaona hawa wasomi hawafanyi tu mikataba hii kwa makosa ya kutofahamu vizuri sheria.........
      Kunakitu zaidi mkuu, hawa wasomi wako free kufanya watavyo kwa maslahi yao binafsi na pengine kwa maelekezo ya viongozi wakubwa wao, hawabanwi na yeyote
      Mkuu wangu hicho kitu cha ziada kimetokea kwa sababu hakuna cha kwanza. Hata mimi nikiwekwa ktk nafasi hizo na nikakuta hakuna sheria inayonikwaza isipokuwa ni muafaka baina yetu, nitazidiwa karata na mwekezaji kwa sababu yeye atakuja na sheria zilizomfunga yeye...Na kwa kuitafuta faida zaidi ataendelea kunibana kama Machinga anapokuuzia kitu barabani maana hakuna sheria. Zaidi ya hapo 10% inatokana na kutokuwa na sheria vile vile maana wapo radhi kuitoa kiasi hicho wakijua hawabanwi na sheria. Kama sheria ipo mwekezaji hana sababu ya kutoa 10% maana sheria inasema kadhaa wa kadhaa sasa akupe wewe 10% kwa sababu gani?.
      paulss likes this.
      Exploration of reality

    19. #118
      omujubi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Location : Bumbire Island
      Posts : 1,716
      Rep Power : 724
      Likes Received
      690
      Likes Given
      1774

      Default Re: Kudai kuwa chanzo cha mikataba mibovu ni kukosa elimu ni tusi na kejeli kwa wengi nchini!

      Mkuu nazidi kuwa na wasiwasi na vichwa vya Watanzania na kukumbuka kauli moja iliyowahi kutolewa siku za nyuma Bungeni Dodoma kuwa huenda vizazi vijavyo vikafukua mafuvu yetu kujua kama tulikuwa binadamu wa kawaida au aina nyingine katika hii sayari ya dunia! By then vyuo vilikuwa vichache na tungesingizia elimu lakini sasa vyuo vimejaa kila kona na magraduates kutoka hata nje ya nchi.
      Naenda nje kidogo ya mada ili kuhalalisha mawazo yangu maana watu wanasema ni serikalini tu lakini hata taasisi zetu zinazoundwa na 'watu huru' wanafanya mambo ya ajabu kupita kiasi, hebu tafakari na hili:
      Hivi inawezekanaje timu masiki ya Tanzania ambayo hata akaunti yake ya benki haina pesa kumkodisha kocha kutoka nje alafu baada ya siku 70 anadai Million mia mbili (200,000,000/-)???!!!!!

      Soma hapa oune: Saintfiet, Yanga see amicable end to contact

      By Majuto Omary
      The Citizen Reporter
      Dar es Salaam. Contrary to what some people had expected, compensation for sacked Young Africans head coach Tom Saintfiet has settled nobly and amicably.

      Saintfiet confirmed yesterday that Yanga leadership has paid him the money he deserves in compensation for terminating his contract.
      “We have settled the matter amicably. As of now, they owe me nothing, I expect to return to Belgium on October 10,” the Serbian said.

      There were worries among some soccer fans that there could be more twists and turns before the “divorce” finalised by the two parties.
      But Saintfiet, whose fairytale “marriage” with the Kagame Cup champions came to an abrupt end on Friday, declined to reveal more details on the package he got in compensation, saying it was confidential.

      However, reports had it that the Belgian tactician would earn at least Sh200 million. The 39-year-old also hinted that he may return to Tanzania in the future, despite the fact that a number of clubs (outside Tanzania) have shown interest in hiring him.
      “those who are so ready to take what is not theirs must be ready to loose what is theirs”

    Page 6 of 6 FirstFirst ... 456

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...