Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza; Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

    Report Post
    Page 3 of 3 FirstFirst 123
    Results 41 to 48 of 48
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,691
      Rep Power : 3657
      Likes Received
      3210
      Likes Given
      473

      Default Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza; Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      18 SEPTEMBER 2012

      Na Mwandishi Wetu, Ludewa

      VITA ya ubunge Jimbo la Ludewa, mkoani Njombe, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao 2015, imeanza kujionesha wazi baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Pindi Chana, kudaiwa kufanya jitihada za kumpigia debe mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UWT, wilayani humo.


      Baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM jimboni humo, wanadai jitihada za Bw. Chana kumpigia debe mgombea huyo ni maandalizi ya kunyakua jimbo hilo ambalo hivi sasa lipo chini ya mbunge wake Bw. Deo Filikunjombe.

      Hata hivyo, mgombea aliyekuwa akipigiwa debe na Bw. Chana, alianguka vibaya katika uchaguzi huo na yule aliyekuwa akiungwa mkono na Bw. Filikunjombe, alipata ushindi wa kishindo.

      Chanzo chetu cha habari kimelidokeza gazeti hili kuwa, kutokana na sakata hilo, viongozi wa juu wa CCM Mkoa wa Njombe na Iringa, walilazimika kufika wilayani Ludewa ili kusimamia uchaguzi huo badaa ya kubaini ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu.

      Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa ambaye pia anashikilia Mkoa wa Njombe, Bw. Deo Sanga, alithibitisha kutokea kwa tafrani ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi huo na kudai kuwa, wao kama viongozi wa chama walisimama kidete kuhakikisha misingi na taratibu za chama zinafuatwa.

      Inaelezwa kuwa, chanzo cha mgogoro huo ni Bw. Chana kufanya kampeni ya kuhakikisha mgombea wake Bi. Anna Mlowe, anashinda nafasi hiyo Bi. Mary Mapunda, ambaye alikuwa akiungwa mkono na Bw. Filikunjombe, anaanguka.

      Hata hivyo, katika uchaguzi huo Bi. Mapunda aliibuka kidedea kwa kupata kura 274, wakati Bi. Mlowe akipata 108 na mshindi wa tatu alikuwa Bi. Selina Haule ambaye aliambulia kura 14.

      “Sisi viongozi tunajua wazi kwamba Bw. Chana ana mpango wa kutaka kugombea jimbo hili lakini bado anakabiliwa na upinzani mkali na Bw. Filikunjombe ambaye anakubalika sana.

      “Kiini cha mvutano uliojitokeza juzi katika uchaguzi huu ni baada ya Bw. Chana kutaka kupanga watu wake ili wajijengee mazingira mazuri ya ushindi kkatika Uchaguzi Mkuu ujao.

      “Kama unavyojua mwandishi viongozi wa jumuiya za chama kama UVCCM (Umoja wa Vijana wa CCM), UWT na Jumuiya ya Wazazi wakiwa upande wako ni rahisi kushinda,” kilisema chanzo hicho.

      Chanzo hicho kiliongeza kuwa, mgogoro mkubwa ulizuka baada ya jina la Bi. Mapunda, kutoonekana katika fomu ya kupigia kura huku wakati jina la Bi. Mlowe likiwepo.

      “Tulishangaa kuona jina la mgombea wetu (Mapunda) halipo lakini la (Mlowe), lipo pamoja na wagombea wengine, kutokana na utata huu, Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Njombe, iliamua kuwatuma viongozi wake akiwemo Bw. Sanga na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Njombe, Bw. Hoseah Mpagike kwenda Ludewa kuhakiki mwenendo wa uchaguzi huo.

      “Viongozi hawa walipofika walibaini kuwepo kasoro katika ujazaji fomu za muhtasari kwa wagombea hivyo waliagiza marekebisho yafanywe na majina ya wagombea kutathminiwa upya na ndipo uchaguzi ufanyike ambapo Bi. Mapunda aliibuka kidedea,” alisema.

      Akizungumzia suala hilo, mshindi wa nafasi hiyo Bi. Mapunda, alidai Bw. Chana amemdhalilisha kwa kumtolea lugha ya matusi.

      “Kwa kweli amenitukana sana na pale kulikuwa na watu wa rika zote kuanzia wakina mama, watoto na wanaume, sijajua kwanini aliamua kufanya vile wakati yeye ni kiongozi anayeheshimika.

      “Binafsi nilishiriki kumpigia kura nikiwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Wilaya,” alisema Mapunda.

      Kutokana na sakata hilo, gazeti hili lilimtafuta Bw. Chana, ambaye alikiri kutokea kwa vuta nikuvute katika uchaguzi huo lakini alikataa kulizungumza kwa undani na kudai linafanyiwa kazi na chama.

      “Hivi sasa nipo kikaoni lakini naweza kukupigia nitakapokuwa katika nafasi nzuri ya kulielezea kwa kina,” alidai Bw. Chana lakini hadi jana hakuweza kupiga simu kulizungumzia suala hilo.

      Kwa upande wake, Bw. Filikunjombe alikiri kuwepo kwa taflani hiyo na kudai kuwa, haukuwa mgogoro kati yake na Bw. Chana bali ulihusisha kwa kiasi kikubwa wagombea wa kiti hicho.

      “Si kwamba tulizozana ana kwa ana na Bw. Chana hapana, Kilichotokea ni kwamba mwenzangu alikuwa na mgombea anayemuunga mkono na akina mama wa Ludewa walikuwa na mgombea wao.

      “Yeye alitaka kutumia nguvu kama Mjumbe wa Kamati Kuu kupindisha sheria ili mgombea wake ashinde, lakini sisi tulisimama kidete kuhakikisha kanuni za chama zinazingatiwa kumpata mshindi halali.

      “Kwa mfano, alama alizowekewa Bi. Mlowe hakuna kikao chochote kuanzia Kamati ya Utekelezaji ya Wanawake Wilaya, Baraza la Wanawake Wilaya na Kamati ya Siasa Wilaya waliohusika kuziweka, Bw. Chana alitaka haya yote yapuuzwe na viongozi walipomweleza yeye akaleta ubabe,” alisema Bw. Filikunjombe.

      Kwa upande wake Bw. Sanga, alisema suala hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya kurekebishwa kasoro zilizojitokeza.

      “Sisi tulikwenda kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa kufuata misingi na taratibu za chama chetu baada ya Halmashauri ya Mkoa kutuagiza twende kulishughulikia kutokana na utata uliokuwepo.

      “Hapa ninapozungumza na wewe uchaguzi umeshafanyika na mshindi halali Bi. Mapunda,” alisema Bw. Sanga.



      kibananhukhu likes this.


    2. #41
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,862
      Rep Power : 7377
      Likes Received
      6195
      Likes Given
      22551

      Default

      Quote By ludewa View Post
      unataka ushahidi wa kuwa pindi ni mgawaji? au unataka kumtetea tu?
      Mkuu Ludewa, uadilifu wa Mhe. Pindi Chana, ni wa integrity unauona machoni with naked eyes, hauhitaji ushahidi wowote kumdhibitisha ni mgawaji!. Kuna watu huku wanaamini kila mwanamke mzuri wa level ya Pindi Chana ambaye ana madaraka, lazima atakuwa kayapata kwa kubebwa!. No wanawake wengine ni shoka na wamefika hapo walipofika kwa kujibeba wenyewe!.

      Ila pia wajameni tusijisahau sana, tukumbuke pia kuwa Mungu yupo!. Kumsingizia uchafu a born again Christian sio tuu ni kosa kimaadili, bali pia ni dhambi!.

      Amini nawaambieni malipo ni hapa hapa duniani, jiepushe usihukumu ukaja kuhukumiwa!. Inaweza kujikuta unaandamwa na mabalaa hujui chanzo, kumbe ndio "pay back" ya kuwasingizia mabaya wengine!.

      Mwenye masikio na asikie!.
      Pasco.
      Ame likes this.

    3. #42
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,887
      Rep Power : 946
      Likes Received
      471
      Likes Given
      440

      Default Re: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza; Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      pindi chana ni mwanamke,viti maalum!ila kiukweli hamuwezi filikunjombe hata chembe

    4. #43
      IPECACUANHA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th February 2011
      Posts : 1,114
      Rep Power : 644
      Likes Received
      229
      Likes Given
      51

      Default Re: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza *Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      Quote By Pasco View Post
      Mkuu Concrete, my opinion its the other way round!.
      1. Kwa uzuri wa kutizamika, huyu mama amejaaliwa kila idara, kuanzia rangi, nywele, umbo, shape, leggyline, macho, etc,etc, hivyo angekuwa ni mtu wa kujiachia, wazee wangeshakula fadhila na kumuingiza cabinet zamani, haswa ukizingatia udhaifu wa ile top layer yetu!.
      2. Zaidi ya uzuri, huyu mama ni holder wa LL.B na LL.M, hivyo ni msomi wa hali ya juu na ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba. Kwa sifa hizo, angekuwa anatoa, angesha paishwa zamani!.
      3. Kuna watu nawafahamu, hawana hata nusu ya uwezo wake, wako juu kwa sababu wametoa!, naamini kuna wazee wanaomba, wananyimwa na ili kumkomoa ndio maana amebaki hapo hapo alipo!.
      4. Kama unajicho zuri la kutazama, wabunge waachiaji utawajua juu kwa macho, na wale ombao ni "women of substance" and "integrity", utawajua tuu, huyu mama ni "of sustance na integrity"!.
      5. Mimi nimeshakaa nae mahali for dinner, qualifications zake sio paper, but she is ok upstairs, na ndio maana kaamua kama kukwaa ulaji ni mpaka mtu ujirahisi, then tu hell with uwaziri, na ndio amebaki alivyo!

      Pasco.
      You are wrong brother..her area commisioner husband knows also that you are wrong. Anyway utakua umepitiwa na ule usemi "kitu usichokijua ni sawa na usiku wa giza"
      Nicholas likes this.

    5. #44
      neva cin neva bin's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Posts : 49
      Rep Power : 368
      Likes Received
      6
      Likes Given
      17

      Default Re: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza; Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      kwa tetes za huku mjin iringa ni kwamba mumewe alipewa u-DC baada ya kugundua mzigo wake unaliwa na baba ri.z

    6. #45
      Nicholas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 6,409
      Rep Power : 3903
      Likes Received
      1512
      Likes Given
      2661

      Default Re: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza *Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      Quote By Mulama View Post
      Kwani mgobea wa CDM hayupo katika jimbo hilo mpaka hawa wapange mikakati ya kutoana ngeu hivo?!
      Huwa wanachelewa sana kutabua kuwa CCM haina tena ile probability ya kushinda,kwa hiyo bado wataimbiana mipasho hadi watakapofika ktk mziki wa CDM halafu wanaanza kilio ,wanaanza kuwaomba polisi na wakuu wa wilaya wafanye kazi ya ziada.
      SIMPLY THE RADICAL: I can`t wait to see the criminalization of CCM,UWT,Bunch of Policemen/women,and all wanafiki na wachumia tumbo.


    7. #46
      Nicholas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 6,409
      Rep Power : 3903
      Likes Received
      1512
      Likes Given
      2661

      Default Re: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza *Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      Quote By Pasco View Post
      Mkuu Concrete, my opinion its the other way round!.
      1. Kwa uzuri wa kutizamika, huyu mama amejaaliwa kila idara, kuanzia rangi, nywele, umbo, shape, leggyline, macho, etc,etc, hivyo angekuwa ni mtu wa kujiachia, wazee wangeshakula fadhila na kumuingiza cabinet zamani, haswa ukizingatia udhaifu wa ile top layer yetu!.
      2. Zaidi ya uzuri, huyu mama ni holder wa LL.B na LL.M, hivyo ni msomi wa hali ya juu na ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba. Kwa sifa hizo, angekuwa anatoa, angesha paishwa zamani!.
      3. Kuna watu nawafahamu, hawana hata nusu ya uwezo wake, wako juu kwa sababu wametoa!, naamini kuna wazee wanaomba, wananyimwa na ili kumkomoa ndio maana amebaki hapo hapo alipo!.
      4. Kama unajicho zuri la kutazama, wabunge waachiaji utawajua juu kwa macho, na wale ombao ni "women of substance" and "integrity", utawajua tuu, huyu mama ni "of sustance na integrity"!.
      5. Mimi nimeshakaa nae mahali for dinner, qualifications zake sio paper, but she is ok upstairs, na ndio maana kaamua kama kukwaa ulaji ni mpaka mtu ujirahisi, then tu hell with uwaziri, na ndio amebaki alivyo!

      Pasco.
      Duh..pasco unavyotoa sifa ni wazi yupo katik fikra na hisia zako.Hw come unamfagilia hivyo?Na hako ka dinner kalikuzengua haswa ukabaki kukagua mpaka etc...sijui kama upsatir ulipaona sana kihivyo kwa muda mfupi na jinsi hisia zilivyozidi akili.

      Ila jua kitu kimoja. Hakuna demu anakwenda dinnner kachukiza?kama una mpango wa kumwacha demu mwache ktk lunch.katika dinner wanajipara,wanavaa kwa kujiachia,wanapiga mchuchumio, wanakuwa wapo tayari kwa mengi kisaikolojia, na zile "Putty" wazipigazo zinakuwa complimented na taa hafifu.Usijikute ulikuwa mazingira hayo..?Sishangaihayo bongo kwani ,wapiga debe,vijana poa wapo wengi sana kwa ajili ya akina mama na mara nyingine ni madereza wa kipindi cha privacy

      Kiufupi unathibitisha unachokikataa.Au ndio wivu akili haitakia kubali kuna mwingine?
      Last edited by Nicholas; 20th September 2012 at 22:50.
      SIMPLY THE RADICAL: I can`t wait to see the criminalization of CCM,UWT,Bunch of Policemen/women,and all wanafiki na wachumia tumbo.

    8. #47
      kibananhukhu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th July 2009
      Posts : 234
      Rep Power : 553
      Likes Received
      68
      Likes Given
      72

      Default Re: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza; Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      Nimefuatilia siasa za Ludewa, Bi Pindi chana ni Mbunge viti maalum kwa vipindi viwili kama sijakosea na anatoka Iringa Mjini. Alilipenda jimbo la Ludewa wakati wa Prof. Raphael Mwalyosi ana Aliwahi kuwa na Makubaliano na Prof kuwa, Yeye Pindi chana ndiye atakayemrithi baada ya miaka 10.

      Kwa makubaliano hayo, Bi. Pindi aliacha kugombea Ubunge awamu iliyopita ili Amwachie Prof na yeye amalize vipindi viwili viti maalum.

      Pindi chana alifanya kosa kudhani Ubunge ni wa watu Fulani. Deo, aliibuka kwa mara ya pili ili kugombea na akaweza kumdondosha Prof Kwa kazi kubwa sana. Kundi la Prof Lilihamaki na kutaharuki na kuamua kuhamia kwa Pindi, na sasa bado linagawika kwani kuna vijana wameamua kumuunga mkono deo.

      Si vibaya Pindi kuonesha nia ya kulitaka jimbo la Ludewa na Kumvua Ubunge Deo Filikunjombe, Mie ninachokiona tatizo litakuwa uamuzi wa kupambana na Fili Ambaye kazi zake zimemfanya hata majimbo mengine yamuombe akagombee kwao na vyama vingine vya siasa kumhusudu.

      Ningelimshauri Pindi atafakari tena, Naona kama deo ana uwezo mkubwa na Jimbo analimudu sijui Pindi atakuwa na sababu zipi za kumtaka deo amuachie kijiti. Nadhani Pindi kumtoa deo ni sawa na kuhamisha milima ya Livingstone kuipeleka malawi, kama ana sababu nzuri basi itamuwia rahisi. Nawatakia kila la kheri.

    9. #48
      hacena's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 396
      Rep Power : 520
      Likes Received
      93
      Likes Given
      11

      Default Re: Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza *Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

      ni bi pindi chana, rafiki wa beatrice shelukindo wapendwa (walokole) pindi ni mbunge viti maalumu, na mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria lowassa camp huku mjengoni tunamjua sana

    Page 3 of 3 FirstFirst 123

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...