Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

    Report Post
    Page 5 of 11 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 201
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,162
      Rep Power : 3546
      Likes Received
      3038
      Likes Given
      460

      Default Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...


      Tuesday, 18 September 2012 19:54





      Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,Othman Rashid

      NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI, MKURUGENZI AMTAKA IGP KUCHUKUA HATUA, MTUHUMIWA AJITETEA

      Waandishi Wetu

      SAKATA la mke wa kigogo wa polisi kudaiwa kuwatapeli vijana 120 kwa kuwachangisha zaidi ya Sh100 milioni ili awatafutie kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru limechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid kuwataka polisi wamkamate na kumchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo.
      Utapeli huo wa aina yake, unadaiwa kufanywa na mama huyo kwa kushirikiana na mwanaye (majina tunayo). Pia yumo kijana anayejulikana zaidi kwa jina moja la Baraka ambaye kwenye mpango huo, anajitambulisha kuwa anafanya kazi Ikulu.

      Akizungumza na mwandishi wetu Dar es Salaam juzi, Rashid alisema tayari amewasiliana na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kuhusu tuhuma hizo ili kujua hatua zilizochukuliwa dhidi yake.

      “Nimewasiliana na IGP Mwema ili aweze kunipa ufafanuzi kuhusu mke wa kigogo huyo, lakini nashukuru amenipa ushirikiano na kuniambia kuwa suala hilo wanalishughulikia kisheria zaidi. Watanipa taarifa pindi watakapokuwa wamekamilisha,” alisema Rashid.

      Alisema huo ni mfano tu wa baadhi ya watu wanaotumia jina la Usalama wa Taifa kufanya utapeli na kwamba tabia hiyo tayari imewaingiza baadhi ya watu matatani baada ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na wengine bado wanatafutwa.

      Alisema sheria ni msumeno, hivyo ikibainika mwanamke huyo alijihusisha kutapeli kwa kutimia jina la Usalama wa Taifa, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanatumia majina ya waume zao kutapeli watu.

      Rashid alisema bado ana imani kwamba polisi itamchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo ikiwa itathibitika kwamba amejihusisha na utapeli kwa kuwa jeshi hilo lipo kulinda usalama wa raia na mali zao.

      Azungumzia tuhuma
      Akizungumzia madai hayo jana kigogo huyo wa polisi ambaye mkewe ndiye anayetuhumiwa (jina tunalihifadhi), alisema tangu mwanzo
      alielewa kwamba anayezungumziwa ni mkewe, lakini akakanusha kuhusika katika utapeli huo.

      Alisema kutokana na taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa katika gazeti hili na kumtaja Baraka, vijana wengi waliotapeliwa kutoka mikoa mbalimbali walifunguka akili zao na kubaini kuwa aliyetajwa katika habari ndiye aliyekuwa akichukua fedha kwao.

      “Jambo linalonisikitisha ni kwamba, aliyewaletea taarifa hizo za uongo zinazomhusisha mke wangu na utapeli huu ndiye tapeli aliyekuwa akizunguka mikoa mingi nchini kutapeli watu. Hata mke wangu ni mmoja wa waliotapeliwa. Alikusudia kuwapeleka wanafamilia watatu akiwemo mtoto wake, mke wa kaka yake na wifi yake ambaye tunamlea,” alisema.

      Alisema mkewe alitoa fedha taslimu zisizopungua Sh1.5 milioni, mbali na gharama za kununua bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanafamilia hao wangetakiwa kwenda navyo mafunzoni.

      Alisema walishtuka kuwapo dalili za utapeli baada ya watu waliokuwa wakidai kushughulikia ‘mipango’ hiyo kuanza kutoa ahadi zisizotekelezwa, huku wakati mwingine simu zao zikipatikana kwa nadra.

      Alipotakiwa kuwataja kwa majina waliokuwa wakishughulikia mipango, ambao walichukua fedha kutoka kwa mkewe kigogo huyo alisema hakumbuki vizuri majina yao. Hata hivyo, alisema mmoja wao anaitwa Baraka.

      Mke wa kigogo huyo alikataa kuzungumzia tuhuma hizo akisema: “Hayo yote yapo kwa wakubwa, mimi siwezi kuongelea kitu kilicho ngazi za juu yangu.”

      Alipoambiwa kuwa mwandishi wetu amezungumza na mumewe ambaye ameeleza kuwa mama huyo naye ni miongoni mwa waathirika katika utapeli huo, hivyo atoe ufafanuzi alikataa pia kuzungumzia hilo na kukata simu.

      Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo alisema: “Kwa sasa niko huku Maputo (Msumbiji), siwezi kuzungumzia suala hilo lakini nikirudi nitafutane nitatoa ufafanuzi.”

      Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Polisi (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia tuhuma hizo akielekeza atafutwe msemaji wa polisi ambaye simu yake haikupatikana kutwa nzima jana.

      Ilivyokuwa
      Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti habari kuhusu mke wa kigogo kuwatapeli vijana 120 kwa ahadi ya kuwapa ajira katika Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru.

      Kati ya Agosti 5 na 7, mwaka huu vijana hao 120 kwa nyakati tofauti walipata taarifa kwamba kuna nafasi za kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru na kwamba nafasi hizo zinapatikana kupitia kwa vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

      Kwa kupitia kwa mtoto wa mwanamke huyo na kupewa taarifa na rafiki zao, inadaiwa kwamba watu hao ambao wengi wao ni wenye elimu ya chuo kikuu walielezwa kwamba ili kupata kazi hizo ni lazima watoe fedha kati ya Sh700,000 hadi Sh1 milioni.

      Walielezwa kuwa mafunzo ya kazi hizo yatatolewa kwa miezi minne katika vyuo vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), vilivyopo eneo la Mbweni (Dar es Salaam), Zanzibar na Monduli (Arusha).

      Siku ya kwanza ambayo waliambiwa kukutana katika viwanja vinavyozunguka uwanja wa zamani wa Taifa, karibu na Ofisi za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ili wapelekwe Mbweni kwa ajili ya kupangiwa vituo vyao vya kazi walielezwa kwamba baadhi yao majina yao yalikuwa hayajaingizwa katika mfumo. Baada ya wiki moja walitakiwa kukutana tena eneo hilo ili kupelekwa, lakini walielezwa kuwa wangepelekwa Septemba 2, mwaka huu kwa kuwa baadhi yao hawakuwa na namba.

      Ilipofika Septemba 2, vijana hao wakati wakielekea Mbweni, walielezwa kuwa muda umekwenda na hawataweza kupokewa katika kambi hiyo hivyo kupangishiwa nyumba za kulala wageni zilizopo Tegeta.

      Hadi walipofika katika Ofisi za Mwananchi, Ijumaa wiki iliyopita, bado baadhi yao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo na wengine kupewa nauli ili warudi katika mikoa waliyotoka kwa maelezo kuwa nafasi zitatangazwa gazetini Oktoba 3, mwaka huu.

      Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa polisi imefungua jalada kuhusu tuhuma hizo na tayari limewahoji watu kadhaa Dar es Salaam na mikoani, lakini mke wa kigogo huyo hajahojiwa.



      MIRIJA IKATWE likes this.

    2. Miaka 50

    3. #81
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,664
      Rep Power : 974
      Likes Received
      578
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By Njaare
      Mh! Japo TAKUKURU imeonyesha udhaifu katika kutokomeza rushwa, sitaki kuamini kuwa imefikia hatua ya kuajiri watoa rushwa ili wakapambane na rushwa.

      Iwe ni utapeli au la, vijana waliotoa rushwa wanatakiwa kukamatwa na kushtakiwa kwani kutoa rushwa ni kosa la rushwa
      .
      Ajira ya TAKUKURU inatangazwa kwa uwazi na ni wenye sifa na vigezo wanaajiriwa!

    4. #82
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Game Reserve
      Posts : 7,927
      Rep Power : 11997
      Likes Received
      5248
      Likes Given
      5097

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Huu ndio ujinga wa gazeti la mwananchi, kwanini wanaficha jina la mke wa kigogo lakini baraka anatajwa?
      Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa gazeti la mwanahalisi, wangeshamwaga mchele siku nyingi.
      Dark City likes this.
      Honesty is a very expensive GIFT. Do not expect it from cheap people.

    5. #83
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Micha
      Alisema mkewe alitoa fedha taslimu zisizopungua Sh1.5 milioni, mbali na gharama za kununua bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanafamilia hao wangetakiwa kwenda navyo mafunzoni.

      Kwahiyo huyu anachotaka kutuambia ni kwamba alimruhusu mkewe akatoe rushwa ili wanafamilia wake wapate kazi?


      Chagonja kwa madaraka yake alikuwa na nafasi ya kujua au kuwasiliana na jamaa wa Idara ya Usalama wa Taifa kwa nini mkewe anafanya vitu ambavyo kimsingi vinachafua Idara ya Usalama wa Taifa?

    6. #84
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Ajira za vyombo vya ujasusi ni ya siri duniani kote lakini usiri huo si wa kutumia njia za panya kama za mke na mtoto wa kigogo huyo.

    7. #85
      LINCOLINMTZA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th March 2011
      Location : Opposite The JF Web Page
      Posts : 1,357
      Rep Power : 694
      Likes Received
      349
      Likes Given
      216

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By nngu007

      Miaka iliyopita USALAMA wa TAIFA ndio waliokuwa WANAKUFUATA na Kukueleza kuwa WAMEKUANGALIA MWENENDO WAKO KWA MUDA MREFU

      Unafaa kufanya KAZI USALAMA WA TAIFA; Walikuwa hawaajiri kama MAKAMPUNI MENGINE; Leo hii pamekuwa OFISI ZA AJIRA ? NDIO Maana hao

      Waliompiga ULIMBOKA waliacha a lot of criminal items... NAONA WALISOMBWA na kumwagwa USALAMA wa TAIFA...
      Mambo yamebadilika sana siku hizi, Hata Nchi zilizoendelea zinatangaza ajira hizi ila usaili wake ndo unapata watu wanaofaa. Kwa hiyo ni vizuri wakazitangaza kwani watapata watu ambao wanaipenda hii kazi kwani si kila mtu anaipenda ingawa njaa inaweza kushawishi watu.
      Ame likes this.
      Love everybody, trust no body. If you can not convince them, confuse them. If you can not teach them, cheat them.

    8. FemaTV & Radio

    9. #86
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,664
      Rep Power : 974
      Likes Received
      578
      Likes Given
      10

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Nje ya mada.. ningetarajia TISS iwabane wakuu wa Polisi kwa mauaji ya Iringa. Siamini kwamba vyombo vya usalama kufanya kazi kiraia. Kwanini Kamuhanda hajakamatwa? Kwanini hawajashauri Chagonja akae pembeni wakati uchunguzi ukiendelea?

    10. #87
      Jodoki Kalimilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2012
      Location : Ihayabuyaga
      Posts : 2,244
      Rep Power : 885
      Likes Received
      759
      Likes Given
      1431

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By kande kavu
      Kwa hiyo huyo mheshimiwa sana Kamanda wa Polisi alijua mchezo mzima wa hao kina Baraka,ikiwamo kuomba rushwa wafanikishe vijana kuajiriwa,lakini bado alitoa ruhusa kwa mkewe kuendelea na huo mpango?

      Kama ni hivyo basi nchi hii itazinduliwa na kiama! Kamanda wa Polisi anashiriki kutoa rushwa,Kamanda wa Polisi haamini katika haki bali pesa mbele,Kamanda wa Polisi hajiongezi na kutaka kufatilia kwa nini ajira kwa pesa,kamanda wa Polisi anakaa kimya ili watu wake wafaidike, kamanda wa Polisi.
      Yaani serikali imepotea njia inatakiwa irudi ilipotoka ili itambue wapi imepotea, hivi kwanini utaratibu wa kufanya selection usifanyike kama zamani mtu anajaza selection form kama akikosa other post kama A level anapelekwa ualimu, police, vyuo vya certificate n.k maana inaepusha hata UNDUGUNIZATION na kuchagua vilaza. KWA KAULI YA HUYO KIONGOZI HAPO MOJA KWA MOJA ANA KESI YA KUJIBU NAYO NI kutoa rushwa tena mtu anaesimamia utekelezaji wa sheria
      Ame likes this.

    11. #88
      Jodoki Kalimilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2012
      Location : Ihayabuyaga
      Posts : 2,244
      Rep Power : 885
      Likes Received
      759
      Likes Given
      1431

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By MAMA POROJO
      Chagonja kwa madaraka yake alikuwa na nafasi ya kujua au kuwasiliana na jamaa wa Idara ya Usalama wa Taifa kwa nini mkewe anafanya vitu ambavyo kimsingi vinachafua Idara ya Usalama wa Taifa?
      Kumbe kigogo ni Chagonja, asurubiwe huyo!!!

    12. #89
      Mimibaba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2009
      Posts : 3,148
      Rep Power : 1527
      Likes Received
      754
      Likes Given
      590

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!
      Walifikiri kwa kiwango cha shule za kata
      Ukweli utakuweka huru daima

    13. #90
      naumbu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Posts : 304
      Rep Power : 494
      Likes Received
      104
      Likes Given
      1

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Na kuna taarifa kuwa huyo Baraka alikamatwa, hao vijana waliotapeliwa waliitwa kituon na wakathibitisha kuwa ni yeye lakin taarifa ya polisi kwa gazet la mwananchi wanasema wanamtafuta huyo tapeli Baraka!!kuna mchezo unachezwa ili waje na sinema zao kama kawaida.
      Unstoppable likes this.

    14. #91
      silao's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st April 2012
      Posts : 24
      Rep Power : 363
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By naumbu
      Na kuna taarifa kuwa huyo Baraka alikamatwa, hao vijana waliotapeliwa waliitwa kituon na wakathibitisha kuwa ni yeye lakin taarifa ya polisi kwa gazet la mwananchi wanasema wanamtafuta huyo tapeli Baraka!!kuna mchezo unachezwa ili waje na sinema zao kama kawaida.
      MBONA KIGOGO HUYO WA POLISI ANAJULIKANA NI CHAGONJA NA MKEWE NDIYE MTUHUMIWA. KUNA UZI ULISHATOLEWA HAPA KWAMBA MKEWE HUYU NI RAIA WA RWANDA NA AMEINGIZA RAIA WENGI WA RWANDA KWENYE JESHI LA POLISI. MMOJAWAPO YUPO KWENYE BAND YA CHUO CHA POLISI MOSHI ANAITWA VERONIKA, WENGINE WAKO MIKOANI WANAFANYA KAZI ZA POLISI TANZANIA. HUYO MWANAMKE NI TAPELI KWELIKWELI HATA POLISI WENYEWE WAMEMGWAYA. KIONGOZI WAO HUYO CHAGOJA AMELIAIBISHA JESHI LA POLISI NA AMEONYESHA NI JINSI GANI HAO ASKARI WALIVYO. KITENDO CHAKE CHA KUDAI KUWA MKEWE NAYE ALITAPELIWA NA AKAKAA KIMYA HADI TUHUMA HIZO ZILIPOIBULIWA NA WENGINE KINAONYESHA NI JINSI GANI ALIVYO NA UPEO MDOGO WA KUFIKIRI HATA KUTOA WASIWASI WA JINSI AMBAVYO ALIPEWA HIYO NAFASI. NIMEAMINI KUWA SERIKALI YETU HII NI DHAIFU. KWA UPANDE MWINGINE NI KUWA KUSEMA KUWA MKEWE PIA KATAPELIWA NI KUTAKA KUMFANYA MKEWE NAYE AWE SHAHID KATIKA HILO SAKATA BADALA YA KUWA MTUHUMIWA HALISI HUO NAONA NI UTOTO NA UFINYU WA KUFIKIRI WA KIGOGO HUYU. UTAKUMBUKA HATA KAULI YAKE SIKU MWANDISHI ALIPOUWAWA KULE IRINGA YEYE AKAKIMBILIA KUTOA TAMKO KUWA ALIRUSHIWA KITU KUTOKA KWENYE KUNDI LA WANANCHI NA ALIKIMBILIA KWA POLISI KOMBA MSAADA. KAULI HIYO NA NYINGINE NYINGI PAMOJA NA HII YA KWAMBA MKEWE KATAPELIWA NI USHAHIDI TOSHA KUWA KIONGOZI HUYU NI DHAIFU NA NDIYE AMBAYE NAHISI ANALIFANYA JESHI LA POLISI LIWA PIA DHAIFU.
      LINCOLINMTZA likes this.

    15. #92
      Remote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th May 2011
      Posts : 4,246
      Rep Power : 1356
      Likes Received
      941
      Likes Given
      182

      Default

      Mkuu siku hizi ni mipango tu huku nyumbani mimi kuna jamaa zangu walitumia njia hiyo lkn wao walifankiwa hawakutapeliwa
      Quote By Mzee Mwanakijiji
      sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!
      Ame likes this.

    16. #93
      kibol's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2012
      Location : dar es salaam
      Posts : 1,086
      Rep Power : 573
      Likes Received
      285
      Likes Given
      59

      Default

      Quote By KIM KARDASH
      Halafu mbaya zaidi ni vijana wenye elimu ya vyuo vikuu vyetu!
      hapo ndipo mahali ata mimi niliposhika kichwa,kama mtu wa chuo kikuu anafanyiwa hivyo how about others???
      Ame likes this.

    17. Ame
      #94
      Ame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Location : Global Citizen
      Posts : 1,513
      Rep Power : 1183
      Likes Received
      650
      Likes Given
      2615

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Entrepreneur
      Kila siku nawaona humu jf, wakidanganyana watapata vipi hizo ajira ... Usijekuta mambo haya yanaanzia kwenye PM, kwan utapeli wa namna hii unahitaji kuwakuta watu wenye nia na kazi hizo na wako desperate pia
      Attitude za vijana wetu zimeharibiwa na ufisadi....Wengi wanadanganyana ukipata kazi huko usalama wa Taifa basi ndo ujue umasikini umeshausahau.....Bora kama wangekuwa wanawaza impact yao katika kazi ya kutetea maslahi ya taifa lakini utashangaa kinacho wafanya kukimbilia ni pesa za bure na siyo out put yao ambayo italeta significant change katika economy nzima ya nchi....So sad...

      Kuna haja ya kuwaonyesha watu jinsi ya kutengeneza welfare kupitia talents zao na pesa kuwa ni media of exchange tu lakini ideas ndizo zinazo leta pesa na welfare and not vice versa....

      Hii ndiyo shida inayotokea hata kwenye siasa. Wengi wanakimbilia siyo kwasababu wanapenda siasa ila kwasababu hawana vision wala mission katika maisha yao na hivyo kwakua wachache through ufisadi na monopoly iliyotengenezwa na wanasiasa kupitia sheria zinazowapa wao uhalali wa kupewa malipo makubwa bila responsibility yoyote na kuacha wengine katika umasikini na shida basi watu wanatoana roho ili kupata hizo nafasi 300 za kisiasa...

      Serikali inayokuja lazima ivitafakari hivi vitu kwa kina...Nakuruhusu wenye uwezo kuweka sawa general equilibrium ya uchumi wa nchi vizuri.

    18. Ame
      #95
      Ame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th March 2011
      Location : Global Citizen
      Posts : 1,513
      Rep Power : 1183
      Likes Received
      650
      Likes Given
      2615

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By kibol
      hapo ndipo mahali ata mimi niliposhika kichwa,kama mtu wa chuo kikuu anafanyiwa hivyo how about others???
      Hao vijana ungejua psychology zao ungetoa machozi...Innocent youths ambao hawana training na governance nzuri ku-wapa assurance ya good future through their education...Who is to be blamed? Hawa vijana ni reflection ya poor governance inayosababishwa na bad policies so vijana hawapashwi kubebeshwa lawama zote. Wako katika active age ambapo akili yao inawaruhusu kuchukua risk kubwa kwa wale walio na IQ kubwa kuweza ku-excel!

    19. #96
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,465
      Rep Power : 19740
      Likes Received
      5425
      Likes Given
      3612

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By MAMA POROJO
      Ajira za vyombo vya ujasusi ni ya siri duniani kote lakini usiri huo si wa kutumia njia za panya kama za mke na mtoto wa kigogo huyo.
      Mwongo mkubwa wewe....


      CIA Home > Careers and Internships > Application Process

      Application Process

      Because of the classified nature of our work at the Central Intelligence Agency, the application process is a lengthy one. Depending on your specific circumstances, the process may take as little as two months or more than a year.
      To start the application process you should visit the View All Career Opportunities page or explore each occupation under our career paths:




      Each section tells you general information about the career path and features position openings. If you don't see the right jobs for you now, check back again soon. Our needs change frequently.
      Once you've determined the position(s) you’d like to apply for, visit the Application Instructions page for guidance about completing the online application form.
      Here are a few things you'll need to know before starting the application process.


    20. #97
      Somoche's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th October 2010
      Posts : 1,861
      Rep Power : 813
      Likes Received
      345
      Likes Given
      338

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Polisi alitoa rushwa na ameshakiri alitoa hilonalo ni kosa kwa hiyo nae akamatwe, na mkewe wote, tatizo hii nchi Mwizi ni mwizi na mfukuza mwizi nae mwizi halafu wanaitwa Vigogo!!!
      Unstoppable and Ame like this.

    21. #98
      Fidel80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 18,931
      Rep Power : 9474
      Likes Received
      3052
      Likes Given
      1192

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Uchunguzi bado unaendelea mpaka kipindi cha uchaguzi
      **^^+..Ukiuza Utumbo usiogope nzi..+^^**
      Chuda Raha
      Email: [email protected]

    22. #99
      Turbulence's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th April 2012
      Posts : 81
      Rep Power : 372
      Likes Received
      10
      Likes Given
      12

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Mwananchi mnaboa, why hamuwataji majina wahusika wakati mmeshawahoji? Mke wa kigogo hana jina? Kigogo wa polisi haa jina? Msituletee habari robo. Wasomaji tunajiuliza maswali mengi e.g. mmepewa ela msitaje majina etc.

    23. #100
      Concrete's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 1,741
      Rep Power : 983
      Likes Received
      461
      Likes Given
      0

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Sasa tumeshajulishwa huyo mwalifu ni MKE WA PAULO CHAGONJA, MFANYAKAZI WA NBC(UDSM BRANCH), NI MAMA MWENYE TAMAA YA PESA NA VITISHO VYA KUTUMIA MADARAKA, hivyo basi mtu yoyote mwenye kujua jina lake kamili na wasifu wake zaidi atutajie hapa na pia huyo mtoto wake pia tutajiwe hapa.

      Tuko serious na nchi yetu, watawala na dola wako kulindana tu, sasa ni wakati wa kutumia akili na nafasi tulizonazo kumwaga mboga na Ugali vikiwa bado jikoni vinapikwa.
      Matola and LINCOLINMTZA like this.

    24. Study Abroad
    Page 5 of 11 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...