Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

    Report Post
    Page 2 of 11 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 201
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,204
      Rep Power : 3555
      Likes Received
      3055
      Likes Given
      462

      Default Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...


      Tuesday, 18 September 2012 19:54





      Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,Othman Rashid

      NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI, MKURUGENZI AMTAKA IGP KUCHUKUA HATUA, MTUHUMIWA AJITETEA

      Waandishi Wetu

      SAKATA la mke wa kigogo wa polisi kudaiwa kuwatapeli vijana 120 kwa kuwachangisha zaidi ya Sh100 milioni ili awatafutie kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru limechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid kuwataka polisi wamkamate na kumchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo.
      Utapeli huo wa aina yake, unadaiwa kufanywa na mama huyo kwa kushirikiana na mwanaye (majina tunayo). Pia yumo kijana anayejulikana zaidi kwa jina moja la Baraka ambaye kwenye mpango huo, anajitambulisha kuwa anafanya kazi Ikulu.

      Akizungumza na mwandishi wetu Dar es Salaam juzi, Rashid alisema tayari amewasiliana na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kuhusu tuhuma hizo ili kujua hatua zilizochukuliwa dhidi yake.

      “Nimewasiliana na IGP Mwema ili aweze kunipa ufafanuzi kuhusu mke wa kigogo huyo, lakini nashukuru amenipa ushirikiano na kuniambia kuwa suala hilo wanalishughulikia kisheria zaidi. Watanipa taarifa pindi watakapokuwa wamekamilisha,” alisema Rashid.

      Alisema huo ni mfano tu wa baadhi ya watu wanaotumia jina la Usalama wa Taifa kufanya utapeli na kwamba tabia hiyo tayari imewaingiza baadhi ya watu matatani baada ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na wengine bado wanatafutwa.

      Alisema sheria ni msumeno, hivyo ikibainika mwanamke huyo alijihusisha kutapeli kwa kutimia jina la Usalama wa Taifa, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanatumia majina ya waume zao kutapeli watu.

      Rashid alisema bado ana imani kwamba polisi itamchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo ikiwa itathibitika kwamba amejihusisha na utapeli kwa kuwa jeshi hilo lipo kulinda usalama wa raia na mali zao.

      Azungumzia tuhuma
      Akizungumzia madai hayo jana kigogo huyo wa polisi ambaye mkewe ndiye anayetuhumiwa (jina tunalihifadhi), alisema tangu mwanzo
      alielewa kwamba anayezungumziwa ni mkewe, lakini akakanusha kuhusika katika utapeli huo.

      Alisema kutokana na taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa katika gazeti hili na kumtaja Baraka, vijana wengi waliotapeliwa kutoka mikoa mbalimbali walifunguka akili zao na kubaini kuwa aliyetajwa katika habari ndiye aliyekuwa akichukua fedha kwao.

      “Jambo linalonisikitisha ni kwamba, aliyewaletea taarifa hizo za uongo zinazomhusisha mke wangu na utapeli huu ndiye tapeli aliyekuwa akizunguka mikoa mingi nchini kutapeli watu. Hata mke wangu ni mmoja wa waliotapeliwa. Alikusudia kuwapeleka wanafamilia watatu akiwemo mtoto wake, mke wa kaka yake na wifi yake ambaye tunamlea,” alisema.

      Alisema mkewe alitoa fedha taslimu zisizopungua Sh1.5 milioni, mbali na gharama za kununua bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanafamilia hao wangetakiwa kwenda navyo mafunzoni.

      Alisema walishtuka kuwapo dalili za utapeli baada ya watu waliokuwa wakidai kushughulikia ‘mipango’ hiyo kuanza kutoa ahadi zisizotekelezwa, huku wakati mwingine simu zao zikipatikana kwa nadra.

      Alipotakiwa kuwataja kwa majina waliokuwa wakishughulikia mipango, ambao walichukua fedha kutoka kwa mkewe kigogo huyo alisema hakumbuki vizuri majina yao. Hata hivyo, alisema mmoja wao anaitwa Baraka.

      Mke wa kigogo huyo alikataa kuzungumzia tuhuma hizo akisema: “Hayo yote yapo kwa wakubwa, mimi siwezi kuongelea kitu kilicho ngazi za juu yangu.”

      Alipoambiwa kuwa mwandishi wetu amezungumza na mumewe ambaye ameeleza kuwa mama huyo naye ni miongoni mwa waathirika katika utapeli huo, hivyo atoe ufafanuzi alikataa pia kuzungumzia hilo na kukata simu.

      Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo alisema: “Kwa sasa niko huku Maputo (Msumbiji), siwezi kuzungumzia suala hilo lakini nikirudi nitafutane nitatoa ufafanuzi.”

      Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Polisi (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia tuhuma hizo akielekeza atafutwe msemaji wa polisi ambaye simu yake haikupatikana kutwa nzima jana.

      Ilivyokuwa
      Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti habari kuhusu mke wa kigogo kuwatapeli vijana 120 kwa ahadi ya kuwapa ajira katika Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru.

      Kati ya Agosti 5 na 7, mwaka huu vijana hao 120 kwa nyakati tofauti walipata taarifa kwamba kuna nafasi za kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru na kwamba nafasi hizo zinapatikana kupitia kwa vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

      Kwa kupitia kwa mtoto wa mwanamke huyo na kupewa taarifa na rafiki zao, inadaiwa kwamba watu hao ambao wengi wao ni wenye elimu ya chuo kikuu walielezwa kwamba ili kupata kazi hizo ni lazima watoe fedha kati ya Sh700,000 hadi Sh1 milioni.

      Walielezwa kuwa mafunzo ya kazi hizo yatatolewa kwa miezi minne katika vyuo vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), vilivyopo eneo la Mbweni (Dar es Salaam), Zanzibar na Monduli (Arusha).

      Siku ya kwanza ambayo waliambiwa kukutana katika viwanja vinavyozunguka uwanja wa zamani wa Taifa, karibu na Ofisi za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ili wapelekwe Mbweni kwa ajili ya kupangiwa vituo vyao vya kazi walielezwa kwamba baadhi yao majina yao yalikuwa hayajaingizwa katika mfumo. Baada ya wiki moja walitakiwa kukutana tena eneo hilo ili kupelekwa, lakini walielezwa kuwa wangepelekwa Septemba 2, mwaka huu kwa kuwa baadhi yao hawakuwa na namba.

      Ilipofika Septemba 2, vijana hao wakati wakielekea Mbweni, walielezwa kuwa muda umekwenda na hawataweza kupokewa katika kambi hiyo hivyo kupangishiwa nyumba za kulala wageni zilizopo Tegeta.

      Hadi walipofika katika Ofisi za Mwananchi, Ijumaa wiki iliyopita, bado baadhi yao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo na wengine kupewa nauli ili warudi katika mikoa waliyotoka kwa maelezo kuwa nafasi zitatangazwa gazetini Oktoba 3, mwaka huu.

      Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa polisi imefungua jalada kuhusu tuhuma hizo na tayari limewahoji watu kadhaa Dar es Salaam na mikoani, lakini mke wa kigogo huyo hajahojiwa.



      MIRIJA IKATWE likes this.

    2. Miaka 50

    3. #21
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Mke wa polisi kutoa rushwa kwa baraka ili kuwezesha wanafamilia wake kupata kazi Usalama wa Taifa ni kosa la kutoa rushwa.

      Hii ni sura ingine namna Idara ya Usalama wa Taifa inavyopakwa matopa kwa mambo ambayo hayatokani na majukumu yake kwa Taifa.

      kundi hili linastahiri adhabu.

    4. #22
      MwanaCBE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd September 2009
      Posts : 491
      Rep Power : 589
      Likes Received
      34
      Likes Given
      241

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By idawa
      Kigogo,mke wa kigogo,mtoto wa kigogo ndio nini.?? Ina maana hata mahakamani watapelekwa kwa majina hayohayo.!!
      Ndo maana naimis sana MwanaHalisi
      BabaDesi likes this.

    5. #23
      Shadow's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th May 2008
      Posts : 2,003
      Rep Power : 962
      Likes Received
      147
      Likes Given
      102

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!
      Mzee Mwanakijiji: si unajua baadhi ya vijana sikuhizi wanapenda kupigiwa 'krosi', wavivu kufikiri na kujituma!
      MAMA POROJO likes this.
      Hasta ala victoria, siempré

      "Forever, Until Victory"

    6. #24
      masopakyindi's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 5th July 2011
      Posts : 3,723
      Rep Power : 4192
      Likes Received
      999
      Likes Given
      415

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!
      Mkuu nafikiri tatizo hapa ni kubwa kuliko tunavyolifikiria.
      The National Security Codes of conduct and operations inaelekea ziko in tatters!

      wanaofanya utapeli huo si ajabu walikwisha fanikiwa katika mipango ya awali.
      Siku hizi utakuta vijana wakijitapa wako TISS kiwazi wazi, exposing themselves to obvious dangers and blowing their cover.
      Tuliosoma miaka mingi iliyopita na kupitia JKT tunajua jinsi new recruits wa Idara hii walivyokuwa wanachujwa.

      Chombo kama TISS inabidi kibadilike kiutendaji kulingana na mabadiliko ya muelekeo wa nchi kisiasa.
      Na hapo ndio wajanja wachache wametumia mwanya huo wa "grey area" kuingiza utapeli wao kwa vile wanajua hakuna vetting ya aina yoyote.


      Kwa kifupi sioni kama utapeli uliofanywa na "vigogo" au "mke wa kigogo" kuwa ni bahati mbaya, yamekuwapo hayo kwa muda mrefu tu.
      "If you don't know where you are going, any road will get you there-nowhere”

    7. #25
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 11,924
      Rep Power : 24139
      Likes Received
      4646
      Likes Given
      2631

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Mke wa kigogo huyo alikataa kuzungumzia tuhuma hizo akisema: “Hayo yote yapo kwa wakubwa, mimi siwezi kuongelea kitu kilicho ngazi za juu yangu.”

      Kwa hiyo huyu mama nae ni Polisi au UwT?
      Kassim Awadh likes this.

      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te


    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By idawa
      Kigogo,mke wa kigogo,mtoto wa kigogo ndio nini.?? Ina maana hata mahakamani watapelekwa kwa majina hayohayo.!!
      Polisi wawe wazi zaidi kutaja watuhumiwa itaondoa mashaka ya kulindana....

    10. #27
      MtamaMchungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 1,539
      Rep Power : 806
      Likes Received
      710
      Likes Given
      64

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Hapa ndio utajua uongo wa huyu jamaa.Pamoja na cheo chake na umri wake bado anatapeliwa!!

    11. #28
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By kande kavu
      Kwa hiyo huyo mheshimiwa sana Kamanda wa Polisi alijua mchezo mzima wa hao kina Baraka,ikiwamo kuomba rushwa wafanikishe vijana kuajiriwa,lakini bado alitoa ruhusa kwa mkewe kuendelea na huo mpango?

      Kama ni hivyo basi nchi hii itazinduliwa na kiama! Kamanda wa Polisi anashiriki kutoa rushwa,Kamanda wa Polisi haamini katika haki bali pesa mbele,Kamanda wa Polisi hajiongezi na kutaka kufatilia kwa nini ajira kwa pesa,kamanda wa Polisi anakaa kimya ili watu wake wafaidike, kamanda wa Polisi.
      well said,

      Bila kujali kwamba kitendo cha mke wake kitaichafua Idara ya usalama wa Taifa..... ni hatari kwa Taifa. utetezi ambao hauna mshiko na ambao hautarajiwi kutoka kwa kiongozi anayesimamia sheria za nchi (polisi)

    12. #29
      sembuli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Posts : 599
      Rep Power : 487
      Likes Received
      243
      Likes Given
      167

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      huyo mke wa kigogo itakuwa kaingiza wengi usalama wa taifa kwa njia hiyo kabla ya dili kushtukiwa! hata RAMA wa dr ulimboka huwenda ni product yake!
      There are two ways to slide easily through life; to believe everything OR to doubt everything; Both ways save us from thinking- Alfred korzybski

    13. #30
      bizzare's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th August 2012
      Posts : 60
      Rep Power : 351
      Likes Received
      11
      Likes Given
      22

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Deo wa tabata

    14. #31
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Na wewe ni mtoa rushwa kama mzalendo wa kweli kajisalimishe ushitakiwe.

    15. #32
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,582
      Rep Power : 16765
      Likes Received
      2481
      Likes Given
      1846

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Mpaka sasa hakuna aliyewataja hao watuhumiwa kwa majina yao halisi imebaki tu ni mke wa kigogo, anayejua majina ayataje hapa ili watu wawe makini nao.

    16. #33
      Katavi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 31st August 2009
      Location : Lyamba Lya Mfipa
      Posts : 19,582
      Rep Power : 16765
      Likes Received
      2481
      Likes Given
      1846

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Wewe ungeweza?

    17. #34
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Nimeipenda hii.

    18. #35
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Mwandishi anaficha nini???

      Mbona nasikia ni mke wa Chagonja ( i stand to be corrected)
      Kassim Awadh likes this.

    19. #36
      Mkwe21's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 912
      Rep Power : 759
      Likes Received
      212
      Likes Given
      165

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Kunakofukuta moshi ujue Moto upo nyuma yake!! Nawaomba kwanza usalama wa Taifa Wajichunguze kwanza!! Utakuta watu wenye Ajira sampuli hii ni Nusu ya Kombania yao!! Ndio Maana Hata huyo Kamanda Hakushtuka kwani alijua ni kama ilivyo desturi ya Majeshi Yote!! Ajira Kwa Kununua!!

    20. #37
      Tram Almasi's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 26th February 2009
      Location : Marsabit
      Posts : 753
      Rep Power : 671
      Likes Received
      217
      Likes Given
      92

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By nngu007
      NDIO USIRI WA SERIKALI YETU... atakayekwenda Mahakamani atakuwa ni kigogo Mshona VIATU na sio KIGOGO MKE WA TAPELI.

      Tunaficha Majina ya WEZI!
      Kaaazi kweli kweli. Mpaka tutakapojirekebisha juu ya hili wabadhilifu wataendelea kupeta.
      "YouR MoST UNhaPPy CuSToMers ArE YoUr GREateST SOurCE Of LEarNInG"- BiLL GaTEs

    21. #38
      Kassim Awadh's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Posts : 587
      Rep Power : 480
      Likes Received
      108
      Likes Given
      785

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!
      Hapo ndo unaona bora wamelizwa! vjana hawa wasomi wa leo wamekuwa wavivu mno kujifikirisha,haiwezekani mtu from no where akwambie kazi ya usalama inauzwa laki 7,akukutanishe uwanja wa taifa na akulaze guest tegeta we umo tu!

    22. #39
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,580
      Rep Power : 3330
      Likes Received
      1219
      Likes Given
      458

      Default

      Quote By harakat
      Mi mwenyewe nilipigwa 20000/=tu nyingine niliwaambia kwamba mpaka nione wamefikia wapi ikawa sanaa na mimi hela ya kuunga unga mpaka leo naona sanaa tu kumbe tuko wengi tuanzishe chama cha waliotapeliwa
      hiyo 20000/= ulimpa nani.? Wewe unawafahamu waliokutapeli kwa nini hutaki kuwamwaga hapa kwa faida ya wengi..au umeona ni haki yako kuibiwa.??

    23. #40
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      590
      Likes Given
      413

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Kama ndivyo atasema yote kizimbani kwa nini tuishi kwa hisia?

    Page 2 of 11 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...