Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

    Report Post
    Page 10 of 11 FirstFirst ... 891011 LastLast
    Results 181 to 200 of 201
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,704
      Rep Power : 3659
      Likes Received
      3220
      Likes Given
      473

      Default Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...


      Tuesday, 18 September 2012 19:54





      Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,Othman Rashid

      NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI, MKURUGENZI AMTAKA IGP KUCHUKUA HATUA, MTUHUMIWA AJITETEA

      Waandishi Wetu

      SAKATA la mke wa kigogo wa polisi kudaiwa kuwatapeli vijana 120 kwa kuwachangisha zaidi ya Sh100 milioni ili awatafutie kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru limechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid kuwataka polisi wamkamate na kumchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo.
      Utapeli huo wa aina yake, unadaiwa kufanywa na mama huyo kwa kushirikiana na mwanaye (majina tunayo). Pia yumo kijana anayejulikana zaidi kwa jina moja la Baraka ambaye kwenye mpango huo, anajitambulisha kuwa anafanya kazi Ikulu.

      Akizungumza na mwandishi wetu Dar es Salaam juzi, Rashid alisema tayari amewasiliana na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema kuhusu tuhuma hizo ili kujua hatua zilizochukuliwa dhidi yake.

      “Nimewasiliana na IGP Mwema ili aweze kunipa ufafanuzi kuhusu mke wa kigogo huyo, lakini nashukuru amenipa ushirikiano na kuniambia kuwa suala hilo wanalishughulikia kisheria zaidi. Watanipa taarifa pindi watakapokuwa wamekamilisha,” alisema Rashid.

      Alisema huo ni mfano tu wa baadhi ya watu wanaotumia jina la Usalama wa Taifa kufanya utapeli na kwamba tabia hiyo tayari imewaingiza baadhi ya watu matatani baada ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria na wengine bado wanatafutwa.

      Alisema sheria ni msumeno, hivyo ikibainika mwanamke huyo alijihusisha kutapeli kwa kutimia jina la Usalama wa Taifa, hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ili iwe fundisho kwa wengine ambao wanatumia majina ya waume zao kutapeli watu.

      Rashid alisema bado ana imani kwamba polisi itamchukulia hatua za kisheria mwanamke huyo ikiwa itathibitika kwamba amejihusisha na utapeli kwa kuwa jeshi hilo lipo kulinda usalama wa raia na mali zao.

      Azungumzia tuhuma
      Akizungumzia madai hayo jana kigogo huyo wa polisi ambaye mkewe ndiye anayetuhumiwa (jina tunalihifadhi), alisema tangu mwanzo
      alielewa kwamba anayezungumziwa ni mkewe, lakini akakanusha kuhusika katika utapeli huo.

      Alisema kutokana na taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa katika gazeti hili na kumtaja Baraka, vijana wengi waliotapeliwa kutoka mikoa mbalimbali walifunguka akili zao na kubaini kuwa aliyetajwa katika habari ndiye aliyekuwa akichukua fedha kwao.

      “Jambo linalonisikitisha ni kwamba, aliyewaletea taarifa hizo za uongo zinazomhusisha mke wangu na utapeli huu ndiye tapeli aliyekuwa akizunguka mikoa mingi nchini kutapeli watu. Hata mke wangu ni mmoja wa waliotapeliwa. Alikusudia kuwapeleka wanafamilia watatu akiwemo mtoto wake, mke wa kaka yake na wifi yake ambaye tunamlea,” alisema.

      Alisema mkewe alitoa fedha taslimu zisizopungua Sh1.5 milioni, mbali na gharama za kununua bidhaa na vifaa mbalimbali ambavyo wanafamilia hao wangetakiwa kwenda navyo mafunzoni.

      Alisema walishtuka kuwapo dalili za utapeli baada ya watu waliokuwa wakidai kushughulikia ‘mipango’ hiyo kuanza kutoa ahadi zisizotekelezwa, huku wakati mwingine simu zao zikipatikana kwa nadra.

      Alipotakiwa kuwataja kwa majina waliokuwa wakishughulikia mipango, ambao walichukua fedha kutoka kwa mkewe kigogo huyo alisema hakumbuki vizuri majina yao. Hata hivyo, alisema mmoja wao anaitwa Baraka.

      Mke wa kigogo huyo alikataa kuzungumzia tuhuma hizo akisema: “Hayo yote yapo kwa wakubwa, mimi siwezi kuongelea kitu kilicho ngazi za juu yangu.”

      Alipoambiwa kuwa mwandishi wetu amezungumza na mumewe ambaye ameeleza kuwa mama huyo naye ni miongoni mwa waathirika katika utapeli huo, hivyo atoe ufafanuzi alikataa pia kuzungumzia hilo na kukata simu.

      Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo alisema: “Kwa sasa niko huku Maputo (Msumbiji), siwezi kuzungumzia suala hilo lakini nikirudi nitafutane nitatoa ufafanuzi.”

      Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Polisi (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia tuhuma hizo akielekeza atafutwe msemaji wa polisi ambaye simu yake haikupatikana kutwa nzima jana.

      Ilivyokuwa
      Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti habari kuhusu mke wa kigogo kuwatapeli vijana 120 kwa ahadi ya kuwapa ajira katika Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru.

      Kati ya Agosti 5 na 7, mwaka huu vijana hao 120 kwa nyakati tofauti walipata taarifa kwamba kuna nafasi za kazi Idara ya Usalama wa Taifa na Takukuru na kwamba nafasi hizo zinapatikana kupitia kwa vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

      Kwa kupitia kwa mtoto wa mwanamke huyo na kupewa taarifa na rafiki zao, inadaiwa kwamba watu hao ambao wengi wao ni wenye elimu ya chuo kikuu walielezwa kwamba ili kupata kazi hizo ni lazima watoe fedha kati ya Sh700,000 hadi Sh1 milioni.

      Walielezwa kuwa mafunzo ya kazi hizo yatatolewa kwa miezi minne katika vyuo vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), vilivyopo eneo la Mbweni (Dar es Salaam), Zanzibar na Monduli (Arusha).

      Siku ya kwanza ambayo waliambiwa kukutana katika viwanja vinavyozunguka uwanja wa zamani wa Taifa, karibu na Ofisi za Baraza la Michezo Tanzania (BMT), ili wapelekwe Mbweni kwa ajili ya kupangiwa vituo vyao vya kazi walielezwa kwamba baadhi yao majina yao yalikuwa hayajaingizwa katika mfumo. Baada ya wiki moja walitakiwa kukutana tena eneo hilo ili kupelekwa, lakini walielezwa kuwa wangepelekwa Septemba 2, mwaka huu kwa kuwa baadhi yao hawakuwa na namba.

      Ilipofika Septemba 2, vijana hao wakati wakielekea Mbweni, walielezwa kuwa muda umekwenda na hawataweza kupokewa katika kambi hiyo hivyo kupangishiwa nyumba za kulala wageni zilizopo Tegeta.

      Hadi walipofika katika Ofisi za Mwananchi, Ijumaa wiki iliyopita, bado baadhi yao walikuwa wanaishi katika nyumba hizo na wengine kupewa nauli ili warudi katika mikoa waliyotoka kwa maelezo kuwa nafasi zitatangazwa gazetini Oktoba 3, mwaka huu.

      Habari zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa polisi imefungua jalada kuhusu tuhuma hizo na tayari limewahoji watu kadhaa Dar es Salaam na mikoani, lakini mke wa kigogo huyo hajahojiwa.



      MIRIJA IKATWE likes this.


    2. #181
      sawabho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2011
      Location : Miyakojima
      Posts : 1,835
      Rep Power : 788
      Likes Received
      430
      Likes Given
      121

      Default Re: Revealed: Mke wa Chagonja ndie aliyetapeli watu, lakini kibao chageuzwa eti katapeliwa.......

      Sitaki kuamini. Yaani Mke wa Kamishna wa Operation na Mafunzo wa Jeshi la Polisi atoe rushwa ili Mwanaye Mpendwa apate nafasi ya kuingia TAKUKURU AU TISS !!!!!!! Nchi imekwisha !!! Hapa ukweli kama unapindishwa vile.
      Ndukidi likes this.
      INAWEZEKANA, TIMIZA WAJIBU WAKO

    3. #182
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,863
      Rep Power : 7377
      Likes Received
      6196
      Likes Given
      22555

      Default

      Quote By Tbag Hatari View Post
      Ninamshaka na kwenye Blu hapo lakini kwengine kote..well said! hua napenda ufafanuzi wako hasa linapokuja swala la wanahabari na sheria nkama ulivomchambua G'Hando!!! Big up brother Pasco
      Mkuu TB-Hatari, kila kosa la jinai huwa linawekewa defence mechanisim ili kupunguza makali ya adhabu.

      Ndio maana mtu anaweza kabisa kudhamiria kutenda jinai ya mauaji na hatimaye akaitimiza kwa kuua kiukweli. Kesi yake inapaswa iwe "cold blooded murder" na adhabu yake ni kifo!. Lakini kwa vile murder nazo zinazo defence zake , mojawapo ni "insanity" na kudai wakati ukitenda kile kitendo cha mauji ulirukwa na akili hivyo hukujua utendalo, nyingine ni "provocative" hii ni kudai marehemu alifanja jambo la maudhi mpaka ukapandisha hasira ukaua kwa bahati mbaya!. Kesi inageuzwa from murder to manslaughter yaani toka kesi ya mauaji hadi mauaji bila kukusudia na mshtakiwa anaweza kuachiwa huru!.

      Hivyo hata kama ni kweli Chagonja alimpa mkewe pesa na alijua ni za kutolea rushwa, sheria yetu ya makasa ya jinai inatoa kinga kwa mke dhidi ya mumewe au mume ndidi ya mkewe hivyo kisheria Changonja hana kosa lolote ila kinidhamu "morals" za kiongozi wa polisi kumpa mkewe pesa za rushwa ndiko kunakoweza kumcost kigogo!.
      P.
      Adrian Stepp likes this.

    4. #183
      Ndukidi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 374
      Rep Power : 579
      Likes Received
      141
      Likes Given
      352

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Tiba View Post
      Mkuu MMJ,

      Sio watanzania wote wanaojua ni jinsi gani ajira za usalama wa taifa zinapatikana, lakini ninashangaa ilikuwaje huyo kigogo wa Polisi alimuacha mke wake akatoa Tshs. 1.5 ili ndugu zake wapate ajira. Ina maana yeye hajui ni jinsi gani ajira za UWT zinapatikana vipi? Nafikiri kuna ukweli kwamba huyo mke wa kigogo alikuwa anahusika kwenye huo utapeli na sasa wanatafuta jinsi ya kujinasua.

      By the way, anayejua jina la huyo kigogo wa polisi ni nani amwage jina lake hapa. Hatuwezi kuendelea kuzungumza kwa mafumbo na hapa JF ni sehemu tunayosema "where we dare to talk openly"

      Leta majina hapa!!!!!!!! Kwa nini jina la Baraka litajwe na mengine yafichwe?

      Tiba
      Kuna thread mbona imeshaweka wazi kuwa ni mke wa Chagonja sijui..

    5. #184
      masopakyindi's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 5th July 2011
      Posts : 3,882
      Rep Power : 4228
      Likes Received
      1049
      Likes Given
      429

      Default Re: Revealed: Mke wa Chagonja ndie aliyetapeli watu, lakini kibao chageuzwa eti katapeliwa.......

      Quote By Ndyali View Post
      Mkuu masopakyindi, unaanza kufunguliwa taratibu, maana siku zote nilikuweka kwenye kundi la misukule ya serikali ya matapeli inayoongozwa na Rais Dhaifu chini ya chama cha hovyohovyo chenye wabunge wenye Phd lakini wanatumia akili ya watoto wa chekechea. NDAGA FIJO MALAFYALE.
      Ndugu yangu mimi CCM damu damu na ni CCM orijino!
      Kwamba jamaa wanafanya makosa haina maana chama hakina sera, maadili na miiko.

      History itawahukumu wanalipeleka gari la CCM mtoni kwa kasi ya ajabu.
      Na nakumbuka mzee Moses Nnauye aliwahi kusema , "kikombe kikiingiwa na nzi na kuchafua kinywaji, hutupi kikombe bali unamwaga kinywaji na kukitumia kikombe wakati mwingine."

      Kikombe hakina kosa , kinywaji kimechafuka.
      Pasco and Ame like this.
      "If you don't know where you are going, any road will get you there-nowhere”

    6. #185
      Mtanzania1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2010
      Location : Kalenga, Liringa
      Posts : 992
      Rep Power : 627
      Likes Received
      125
      Likes Given
      94

      Default

      Quote By controler View Post
      Spot on! Umegonga pale pale. Mgao tu haukwenda sawa. Ni njia ya kawaida kabisa. Hata mm ndo nliyotumia.
      kwa nini ulitumia?? haukuwa na vigezo??? ufanisi wako ni ukoje kwa sasa? umeipenda kazi yako?? maana kuna kuipenda kazi na kupenda mshahara.......


    7. #186
      Jagarld's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2011
      Posts : 794
      Rep Power : 573
      Likes Received
      193
      Likes Given
      140

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Nilitegemea kusikia wanaoshitakiwa ni zaidi ya watu 120,matapeli pamoja na waliotapeliwa na hapa maelezo ya waliotapeliwa waliyoyatoa mbele ya polisi ni ushaidi tosha,wakati wanatoa pesa kama kulikua na utaratibu uliowataka wafanye hivo?,walipewa risti kwa ajili ya malipo kama ni halali? Tofauti na hivo wote ni matapeli na wala rushwa ambao ni hatari kwa taifa,wasipochukuliwa hatua na takukuru hawa vijana nadhani rushwa ni halali kabisa uli upate huduma yoyote ile,je,ambao hatuma pesa tutaishi sayari gani! TAFAKARI.

    8. #187
      Mtanzania1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2010
      Location : Kalenga, Liringa
      Posts : 992
      Rep Power : 627
      Likes Received
      125
      Likes Given
      94

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      hapa mashtaka nadhani ni wizi wa kuaminiwa kwa kina baraka.....na hao 120 washtakiwe kwa kosa la kutoa rushwa....ushahidi upo....TAKUKURU MKO WAPI??

    9. #188
      Narubongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 1,886
      Rep Power : 815
      Likes Received
      854
      Likes Given
      680

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      -"..SAKATA la mke wa kigogo wa polisi kudaiwa kuwatapeli vijana 120 kwa kuwachangisha zaidi ya Sh 100 milioni ili awatafutie kazi.." (mwananchi)

      -"...Mbali na kumtapeli Happyphania Paul Chagonja pia washtakiwa hao wanadaiwa kumtapeli Issa Mohamed Chikundi Sh22,250,000, Issa Hussein Rutemba Sh13,450,000, Daud Mgonja Sh3,700,000, Calota Philemon Ngowi Sh2,342,000 na Emmanuel Chagonja Sh11, 400,000...

      Pia wapo, Dunstan Eliapenda Mkwizu Sh1,420,000, Yudas Simon Mkelane Sh2,200,000, Ibrahim Hashim Sh10,500,000 na Lauriana Joseph Sh 29,200, 000 na kufanya jumla ya fedha hizo kufikia Sh102,862,000." Wakili wa Serikali, Sakina Sinda
      - wengi walisema wanasheria wa tanesco walipeleka ushahidi dhaifu ili tanesco ishindwe kesi dhidi ya dowans
      - DC wa korogwe alimwambia mwanasheria ana degree ya chupi
      - waandishi wa habari wa tanzania si watu wa kuamini

      mwananchi --> X1 + X2 +.... + X120 = Tsh 100, 000,000/=

      mashtaka --> Happyphania Paul Chagonja (5,000,000) + Issa Mohamed Chikundi (Sh22,250,000) + Issa Hussein Rutemba (Sh13,450,000) + Daud Mgonja (Sh3,700,000) Calota Philemon Ngowi (Sh2,342,000) + Emmanuel Chagonja (Sh11, 400,000) + Dunstan Eliapenda Mkwizu (Sh1,420,000) + Yudas Simon Mkelane (Sh2,200,000)+ Ibrahim Hashim (Sh10,500,000) + Lauriana Joseph (Sh29,200, 000) = Sh102,862,000/=

      Huyu anasema wametapeliwa 120, huyu anasema 10 na wote hawaaminiki lakini wote wanafanana kwenye amount (100m/=)
      Pasco likes this.
      "Chadema kinatumia alama ya vidole viwili kama manati, manati kamwe haiwezi kuua tembo" Livingstone Lusinde (2012)

    10. #189
      Tiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2008
      Posts : 1,758
      Rep Power : 909
      Likes Received
      439
      Likes Given
      520

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Ndukidi View Post
      Kuna thread mbona imeshaweka wazi kuwa ni mke wa Chagonja sijui..
      Mkuu hiyo thread bahati mbaya sikuiona lakini na wewe inaelekea huna uhakika na unachosema maana umemalizia sentensi kwa kutamka neno "sijui"

      Kama kweli ni mke wa Chagonja, hiyo itakuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu kwani huyu jamaa anajiona kama Mungu Mtu kwa siku za hivi karibuni.

      Tiba

    11. #190
      Twasila's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th May 2011
      Posts : 442
      Rep Power : 498
      Likes Received
      61
      Likes Given
      0

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Huyu mke wa Changonja amekiri kwamba naye alitoa fedha ( kwa lugha yake alitapeliwa), hivi Polisi wanahitaji ushahidi gani zaidi ya huu kuwa alishiriki katika utapeli huu.
      Kitendo tu cha kutoa fedha ili Usalama wa Taifa wakahongwe ni ushiriki tosha. Ila kwa sababu ni mke wa Kamishna wa Polisi wanasema yeye ni shahidi badala ya mshitakiwa. SERIKALI ISIPOINGILIA NA KUHAKIKISHA MAMA HUYU ANAFIKISHWA MAHAKAMANI ITAKUWA NI USHAIDI TOSHA WA UDHAIFU WA JK.
      Pasco likes this.

    12. #191
      KipimaPembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th August 2007
      Posts : 785
      Rep Power : 768
      Likes Received
      347
      Likes Given
      131

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Tanzania rushwa ni ujanja na haionekani kuwa kosa la kimaadili kwa sababu wote waliopo madarakani wameshiriki na wanaendelea kushiriki katika vitendo vya rushwa moja kwa moja au kupitia kwa watu wengine. Ndo maana hakuna mwenye mamlaka ya kimaadili ya kumkemea mwenzie. kadri ukubwa unavyoongezeka ndo na ushiriki katika makosa ya kimaadili kama rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu wa mali za umma, n.k. yanavyokuwa mengi. Kuna watu kila siku anashiriki katika kosa moja au jingine moja kwa moja au "indirectly" kiasi kwamba hayo mambo ni ya kawaida sana.

      Ajira na vyeo kwa kununua ni jambo lililozoeleka hasa kwa wakubwa huko serikalini. Sisi watazamaji tulioko nje ndo tunafikiria kuwa kazi za ajira serikalini zinapatikana kwa njia ya kawaida ndo maana tunapiga makelele. Wanaojua mambo yanavyoenda hawashangai hata kidogo. Ndo maana mtu mkubwa kama huyo atuhumiwe kutoa mamilioni ili mwanaye apate ajira tena serikalini ambako yeye ni mkubwa. Tunaoamini kuwa bado kuna mfumo na mambo yanakwenda kimfumo tunajidanganya tu.

      Kwa kuwa wanaohusika ni wengi, mara nyingi mambo haya hufumka pale kunapokuwa na kutapeliana kati ya wale waliotakiwa kupata mgao huu. Na mara nyingi kutapeliana hutokea tu, isipokuwa mara nyingi waliotapeliwa hushitukia wakati wameshachelewa. Ndo maana haiwezekani mfumo uendelee kufanya kazi namna hiyo kwa muda mrefu. Hufikia huku kuumbuana kukageuka sasa kuwa mapambano ya kibinafsi. Hapa huyu mkuu, kuna watu lazima nayeye atawageuzia kibao katika madili yao mengine. Mambo huendelea hivi hadi hapo unapoona mambo yanalipuka na ghafla huna nchi, bali una magenge ya mibabe ya kivita.

      Hutaona hata siku moja mkubwa akiguswa katika michaka michaka hii ya kuelekea kwenye "failed state"

    13. #192
      Ndukidi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 374
      Rep Power : 579
      Likes Received
      141
      Likes Given
      352

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Tiba View Post
      Mkuu hiyo thread bahati mbaya sikuiona lakini na wewe inaelekea huna uhakika na unachosema maana umemalizia sentensi kwa kutamka neno "sijui"

      Kama kweli ni mke wa Chagonja, hiyo itakuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu kwani huyu jamaa anajiona kama Mungu Mtu kwa siku za hivi karibuni.

      Tiba
      Tiba, humu utakuta mambo yote http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...-kutapeli.html

    14. #193
      Heri's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th August 2007
      Posts : 201
      Rep Power : 644
      Likes Received
      19
      Likes Given
      31

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Whatever the case is, Chagonja inabidi a step down kurudisha imani ya wananchi kwa polisi (hata kama ni kweli mke wake ni victim wa hii scam). Kwangu mimi charge sheet imetengenezwa kumuokoa mke wake Chagonja.
      Tutafurahi kujua mtoto wake Neema ana play role gani kwenye hii scam.

    15. #194
      Tuliwonda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 103
      Rep Power : 371
      Likes Received
      24
      Likes Given
      24

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Yaani ndo maana mm nimejiamulia kulima na kuwa chinga tu! maana unaweza kumaliza soli za viatu, ukauza na kale kabanda ka urithi mwisho wakakupa na gonjwa kutaka ajira wakati huna godfather wa uhakika! mweh hii inji hii kweli ina wenyewe.... nashangaaga kukutana na wenzangu niliosoma nao mara mwingine yuko nbc, mara bot, mara un! maskini ya mungu mieeee...

    16. #195
      Tuliwonda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 29th June 2012
      Posts : 103
      Rep Power : 371
      Likes Received
      24
      Likes Given
      24

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Yaani ndo maana mm nimejiamulia kulima na kuwa chinga tu! maana unaweza kumaliza soli za viatu, ukauza na kale kabanda ka urithi mwisho wakakupa na gonjwa kutaka ajira wakati huna godfather wa uhakika! mweh hii inji hii kweli ina wenyewe.... nashangaaga kukutana na wenzangu niliosoma nao mara mwingine yuko nbc, mara bot, mara un! maskini ya mungu mieeee...

    17. #196
      mpigauzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 276
      Rep Power : 404
      Likes Received
      70
      Likes Given
      174

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By harakat View Post
      Mi mwenyewe nilipigwa 20000/=tu nyingine niliwaambia kwamba mpaka nione wamefikia wapi ikawa sanaa na mimi hela ya kuunga unga mpaka leo naona sanaa tu kumbe tuko wengi tuanzishe chama cha waliotapeliwa
      Nani alikuchangisha mkuu. Tuambie na huyo kigogo ni nani

    18. #197
      Mag3's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 3,581
      Rep Power : 1817
      Likes Received
      2521
      Likes Given
      2549

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...










      Paul Chagonja, Commissioner of Operations in the Tanzania Police Force.



      IGP Mwema akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri, Meena. Katikati ni Kamishna wa Operesheni wa jeshi la Polisi, Paul Chagonja.


      Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dr Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, wakati wa kuitangaza kamati ya kuchunguza kifo cha mwandishi wa habari wa mkoa wa Iringa, Daudi Mwangosi. Kushoto ni kamishna wa Oparesheni wa Polisi, Paul Chagonja na kamishna wa utawala wa Rasilimali wa jeshi hilo, Clodwin Mtweve. Picha na Michael Jamson.

      The true sign of intelligence is not knowledge but imagination.
      Education is what remains after one has forgotten what one has learned in School
      -Albert Einstein.


    19. #198
      Sophist's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th March 2009
      Posts : 444
      Rep Power : 609
      Likes Received
      42
      Likes Given
      0

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
      sasa hao vijana nao duh... hawakuchukua hata muda kidogo kujifunza ajira za usalama wa taifa zinapatikana vipi? kadizooo!!!
      ... Vijana hao wanaelewa; hivi ndivyo ambavyo ajira za usalama wa taifa zimekuwa zikipatikana. Vija walikuwa sahihi. Gazeti la Mwananchi limewatibulia mambo. Polisi, mkewe, Baraka na wanamtandao wengine ndani ya UWT na Takukuru (sema Ikulu) lao moja. Kuuza ajira.

    20. #199
      obwato's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2012
      Posts : 789
      Rep Power : 560
      Likes Received
      189
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By Jagarld View Post
      Nilitegemea kusikia wanaoshitakiwa ni zaidi ya watu 120,matapeli pamoja na waliotapeliwa na hapa maelezo ya waliotapeliwa waliyoyatoa mbele ya polisi ni ushaidi tosha,wakati wanatoa pesa kama kulikua na utaratibu uliowataka wafanye hivo?,walipewa risti kwa ajili ya malipo kama ni halali? Tofauti na hivo wote ni matapeli na wala rushwa ambao ni hatari kwa taifa,wasipochukuliwa hatua na takukuru hawa vijana nadhani rushwa ni halali kabisa uli upate huduma yoyote ile,je,ambao hatuma pesa tutaishi sayari gani! TAFAKARI.
      Ni kweli mkuu,mwl Nyerere alisema anayetoa na anayetoa rushwa wazanaki wanasema wote mankanjanja,japo sielewi lugha hiyo lkn ni wazi alimaanisha wote ni wavunja sheria tandika viboko 10 na viwili siku ya kuingia na 10 na viwili siku ya kutoka akaoneshe mkewe, kwa sasa hakuna kiongozi mwenye usafi wa kukemea hayo,kama baba una tabia ya kumpa bintiyo vimemo apeleke kwa hawala zako wa nje siku ukimkuta gesti na bwana utaanzia wapi kumkemea?,ajira na vyeo vya bongo ni kujuana tu ndio maana familia hizohizo ndio zinatawala na kupita bila kupingwa kila sehemu. bongo huulizwi una nini bali una nani

    21. #200
      MKALIMOTTO's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 136
      Rep Power : 390
      Likes Received
      9
      Likes Given
      8

      Default Re: Usalama wa Taifa waibana polisi; NI KUHUSU TUHUMA ZA MKE WA KIGOGO KUTAPELI...

      big up othman kula nao hao wamezoea kuichafua idara nyeti inayoheshimika na wananchi. usiishie hapo uanze kudeal na vijana wa hosea-PCCB nao mtaani wanawatisha watu kwa kutumia jina la TISS. PCCB wanajitambulisha kwa watu kuwa ni maafisa usalama wa taifa na wanakula rushwa ni balaaaaaaaa!

    Page 10 of 11 FirstFirst ... 891011 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...