Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Barazani Kwa Ahmed Rajab: Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

    Report Post
    Page 2 of 9 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 174
    1. #1
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Barazani Kwa Ahmed Rajab: Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      ............
      Tangu mchakato huu wa kulipatia Taifa Katiba mpya uanze suala la Muungano limekuwa ndilo suala kuu linalotawala usanifu wa kisiasa wa Visiwani. Kweli tangu Muungano uasisiwe Aprili mwaka 1964 umekuwa ukizungumzwa na kujadiliwa sana na Wazanzibari pengine kushinda suala lolote jingine la kisiasa lakini safari hii hili ndilo suala kuu linalowashughulisha Wazanzibari.

      Inavyoonyesha ni kwamba suala hili haliwashughulishi hivyo wenzetu wa Bara. Si kwamba hawalitii maanani lakini hawalipi kipaumbele kama ndugu zao(1) wa Visiwani.

      Inayumkinika kwamba hili zoezi la kukusanya na kuyaratibu maoni ya wananchi litahitimishwa katika muda wa miezi sita ijayo. Litapomalizika sitostaajabu nikiwaona baadhi ya watu wakitahayari na kujaribu kuziziba nyuso zao. Hawa ni wale wasioamini kwamba Tume itayawakilisha vilivyo maoni inayoyakusanya Zanzibar(2).

      Wana msimamo huo kwa sababu hadi sasa maoni hayo yamekuwa ni ya kutoa mapendekezo yenye kutaka pawepo mageuzi ya kimsingi hasa kuhusu muundo wa Muungano(3) na wana wasiwasi kwamba Tume ya Katiba haitokuwa na ujasiri wa kuyawakilisha kidhati maoni hayo.

      Kwa hakika kwa hali ya mambo inavyoendelea nina hakika kwamba idadi kubwa zaidi ya wananchi wa Zanzibar wataendelea kuiambia Tume itapoanza tena shughuli zake Zanzibar kwamba wanataka pawepo na Muungano wa(4) nchi mbili lakini uwe Muungano wa Mkataba na si wa Katiba(5).

      Haiwezi kuwa vingine kwani pendekezo hilo linazidi kuungwa mkono Visiwani ingawa wapo wenye kulipinga na wenye kushikilia kwamba muundo wa sasa wa Muungano usalie ulivyo. Huu wa sasa pia ni Muungano wa nchi mbili lakini ni wa Katiba.
      Hivi karibuni wasomaji kadhaa wa Raia Mwema, wote wakisema wametoka Bara, wameniandikia wakinitaka nielezee zaidi juu ya Muungano wa Mkataba.

      Mmoja ameandika kwamba wananchi wengi hasa Watanganyika hawaelewi nini maana ya Muungano wa Mkataba na kwamba huu ni wakati muafaka kama watapata fursa ya kuuelewa huu Muungano wa Mkataba kwa sababu wakiuelewa nao pia wataupendekeza(6) wakati wa kutoa maoni na hivyo kuongeza uzito badala ya kuwaachia Wazanzibari peke yao.

      Msomaji huyo ameendelea kuandika kwamba kwa hali ilivyo sasa hatima ya Muungano, uwepo au usiwepo, na aina gani ya Muungano kama utakuwepo, itaamuliwa na Wazanzibari “kwa sababu Watanganyika wengi wanaona vyote sawa isipokuwa viongozi…”
      Kwa hakika si jambo la kushangaza kuona kwamba hisia kuhusu Muungano ni kali mno Visiwani kushinda Bara kwa sababu Wazanzibari ndio wenye kudai kwamba muundo uliopo sasa wa mahusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar hauna manufaa kwao.(7)

      Hivyo wanahisi kwamba ni chaguo lililo wazi kwao iwapo wanataka kuendelea na umbile la sasa la Muungo lenye muundo wa Kikatiba au pawepo na umbile mbadala la Muungano utaojengeka juu ya misingi ya Mkataba(8).

      Nini tofauti ya aina hizo mbili za Muungano? Lile umbile la Muungano wa Katiba linakuwa na dola moja yenye kuhodhi mamlaka yote ya ndani na ya nje ya nchi na linaiwezesha Tanganyika kuyasimamia kwa ukamilifu yale yanayoitwa ‘Mambo ya Muungano.’
      Wakati huohuo, Zanzibar inapoteza mamlaka yake kamili na uhuru wake wa kujiamulia itakavyo mambo yake ya ndani na ya nje na inakuwa na jukumu tegemezi ndani ya Muungano wake na Tanganyika.

      Lile umbile la pili, la mbadala, ni la Muungano wa nchi zilizo huru na kila moja ikiwa na mamlaka kamili na uhuru wa kujiamulia mambo yake ya ndani na ya nje. Nchi hizo zitaunganishwa kwa Mkataba(9).

      Muungano utaojengwa kwa Mkataba utairejeshea Tanganyika na pia Zanzibar mamlaka yao kamili ya kidola na utawezesha kuwapo utaratibu wa ushirikiano kati ya nchi mbili zilizo sawa(10) na zilizo huru na zenye mamlaka kamili ya kidola.

      Mkataba, utaokuwa msingi wa Muungano huo, utaeleza wazi nchi hizo zitashirikiana juu ya mambo gani na namna ushirikiano huo utavyokuwa(11).

      Jambo jingine la kuvutia katika Muungano wa Mkataba ni kwamba kila nchi itayotia saini mkataba wa muungano huo itakuwa na nguvu ya kutumia kura ya ‘turufu’ (veto). Hivyo hata katika jambo lililokwishakubaliwa kuwa la Muungano nchi fulani inaweza kuitumia nguvu yake ya turufu na kupinga pale itapohisi kwamba utekelezaji wa sera kuhusu jambo hilo unaihatarisha hiyo nchi au unakwenda kinyume cha maslahi yake.

      Uzuri mwingine wa umbile hilo ni kwamba utaweza pia kuzivutia nchi nyingine zijiunge na Muungano huo kwa vile hakuna nchi itayohisi kwamba itaweza kumezwa na nyingine. Umbile hili la Muungano haliipi nchi yoyote nafasi ya kujitwika dhima ya ‘ukaka’ na kujifanya kuwa ni adhimu kwa sababu ya ukubwa wake uwe wa eneo au mwingineo.

      Nchi zote zilizo ndani ya Muungano aina hiyo wa Mkataba zinakuwa na usawa bila ya kujali ukubwa wao au kima chao cha maendeleo. Sheria ya kimataifa na jumuiya ya kimataifa huziangalia nchi zote hizo kwa jicho moja na huziona kuwa ni sawa mbele ya sheria ilimradi kila moja ya nchi hizo iwe huru na iwe na mamlaka yake kamili ya kidola na ya utawala.

      Mazingira ya kilimwengu katika milenia tuliyo nayo hayashajiishi wala kutia moyo kuwako kwa mahusiano kati ya nchi huru kama yalivyo sasa baina ya Tanganyika na Zanzibar ambamo nchi moja inaonekana ni ‘mshiriki mkuu’ na nyingine ‘mshiriki mdogo’(12)
      Hapo ndipo panapozuka ile dhana ya kwamba mshiriki mdogo ameyahaulisha mamlaka yake ya utawala kwa mshiriki mkuu.
      Mfano mzuri wa Muungano wa Mkataba ni ule Muungano wa Ulaya(13).

      Kutoa mfano wa Muungano huo si kukiri kwamba huo ndio aina ya Muungano uliokamilika. La. Tusemacho ni kwamba ni mfano mzuri wa aina ya Muungano ulio bora kushinda huu tulio nao. Najua kwamba suala la ‘ukaka’ kuna wataoruka na kusema mbona Ujerumani na Ufaransa zinajifanya makaka katika Muungano wa Ulaya? Ni kweli kwamba nchi hizo mbili hujaribu kujitutumua katika masuala ya kiuchumi hasa yale yanayohusika na sarafu ya euro lakini haziwezi kushurutisha lolote kisiasa kwani lazima zifuate mkataba uliopo.
      Mfano mwingine wa Muungano ulio bora kuliko huu tulionao ni ule Muungano wa Senegambia(14)

      ulioziunganisha nchi mbili wanachama wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) yaani Senegal na Gambia toka mwaka 1982 hadi 1989.
      Muungano wao ulikuwa aina ya Muungano wa Mkataba na uliunganisha majeshi ya nchi hizo, pia uliunganisha mambo yao ya uchumi na fedha, uliratibu sera zao za mambo ya nje na mawasiliano na ulianzisha taasisi za Muungano. Urais wa Muungano huo ulikuwa ushikwe na Senegal ambayo pia ilikuwa iwe na thuluthi mbili ya viti vya Bunge la Muungano. Hata hivyo, juu ya kuwapo kwa Muungano huo kila nchi iliendelea kuwa na uhuru wake.

      Mkataba huo wa Muungano ulianza kutekelezwa mwezi Julai mwaka 1982 lakini kwa bahati mbaya Muungano huo ukavunjwa mwaka 1989 kwa sababu Gambia ikilalamika kwamba ikiingiliwa na Senegal katika uhuru wake na mamlaka yake.(15)
      Kama pana nia ya kuwa na Muungano wa dhati utaopelekea kuungana kwa Bara la Afrika basi suluhisho la matatizo yanayoyakabili mahusiano kati ya Tanganyika na Zanzibar lipo katika kuundwa kwa Muungano wa Mkataba. Hiyo si ndoto.

      Jambo linalowahamasisha Wazanzibari watake Muungano wa Mkataba na Tanganyika ni hamu yao ya kutaka kuiendeleza nchi yao kwani wanatambua kwamba Serikali yao ya Umoja wa Kitaifa lazima iweze kutawala na kuendesha shughuli za nchi bila ya kungojea ridhaa kutoka Tanzania Bara hasa ikiwa Zanzibar itakuwa na sarafu yake yenyewe, mfumo wake wa kuendesha biashara pamoja na mfumo wake wa kodi na ushuru na uhuru wa wa kuwa mahusiano na mataifa ya nje.Pia iwe na uwezo wa kutumia mali zake asili bila ya kuwa na ubia na taifa lolote la kigeni.(16)

      Mbali na kuwa suluhisho mujarab kwa matatizo yanayoukumba Muungano wa Tanzania, umbo hilo jipya la Muungano wa Mkataba litahakikisha kuwako kwa Muungano endelevu utaokuwa na uwazi na utaotoa haki sawa kwa nchi zote zitazojiunga nao na utazipa nchi za Tanganyika na Zanzibar mamlaka kamili ya kila nchi kujiamulia mustakbali wake bila ya kuomba ridhaa ya nchi mwenzake(17)

      Tuombe tu kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kuyakusanya na kuyaratibu maoni ya wananchi itakuwa na hadhari itapotoa mapendekezo yake kwenye ripoti yake ya mwisho kwani suala hili ni nyeti.

      Uchambuzi wangu: Chanzo cha taarifa hii ni makala katika gazeti la Raia mwema wiki hii.

      Ili wasomaji waweze kuelewa hoja zangu vema nimeziwekea namba kwa minajili ya kuzjibu bila kupoteza maana. Ahmed Rajab amenishangaza na jinsi anavyobadili misimamo kila uchao 'change his position' kuhusu suala hili.

      Ukisoma namba (1) anasema Tanganyika ni ndugu halafu anawaita nchi ya kigeni (16). Namba (2) anasema tume itakusanya maoni ya wznz kikamilifu hata kama tume hiyo inakusanya pia kutoka Tanganyika. Hapa anaonyesha kuwa wanaolilia hatima ya muungano ni ZNZ na siyo Tanganyika. Kwa mantiki hiyo wangeweza kufanya kura ya maoni wao kuamua hatima yao bila kusubiri tume.

      Namba(3)na (8) anasema maamuzi kuhusu muundo wa muungano. Hapa anaikana hoja yake ya siku nyingi ya kutaka ZNZ ijitenge ili iwe kama Malyasia au Mauritius kama alivyowahi kuandika. Sasa anakiri kuwa WZN wanahitaji muungano. Wale wanaomfuata wamebaki njia panda kama alivyowaacha katika suala la serikali 3.

      Namba (4) anashadidia hoja kuwa WZNZ wanataka muungano. Anamkana hata Maalim anayetaka ZNZ ijitenge. Tena anarudia hoja ya mkataba

      Namba(6) anawatukana Watanganyika kuwa hawaelewi maana ya mkataba. Kwamba Watanganyika ni sawa na WZN wanaomwitikia hata pale anapoandika upuuzi. Kama anadhani hatuelewi mktaba angalia hoja zake zote ametaja mkataba bila kutuambia ni wa kitu gani(11). Huyu msomi wa ZNZ anataka tukubaliane na mawazo yake hata kama yana mapungufu, hayafai au ni ya elimu ya chini sana.

      Namba (7)anasema muungano hauna manufaa ZNZ wakati huo huo anataka muungano (3)(4)(8)

      Namba (9) anasema nchi zitaunganishwa kwa mkataba. Hajasema wa mambo gani. Namba (10)Anasema utaratibu wa ushirikiano wa nchi mbili zilzio sawa. Kwasahivi hakuna usawa kwasababu nchi moja inajiona mshiriki mkuu(12) Hasemi kuwa ushiriki mkuu unatokana na ukweli kuwa Tanganyika inatoa 100% na ZNZ 0%. wakati huo huo anataka kuwe na usawa(12) kwamba mmoja atoe sana na mwingine apokee huo ndio usawa anaouongelea.

      Namba (11) anataja mkataba na ushiriki wa mambo, asichojaribu kukiandika ni kuwa mkataba wa ushiriki wa mambo gani. Hilo hajaweza kulisema wakati huo huo anatukana Watanganyika kuwa hawajui mkataba maana yake nini. Laiti angelijua maana ya mkataba asingekuwa anahangaika kila siku kuandika kitu asichokijua

      Namba(13)anatolea mfano mzuri wa EU. Huyu mwandishi ni waajabu sana, alianza na kuvunja muungano ZNZ iwe kama Malaysia, akabadili kuwa na serikali 3, akaja mkataba sasa anatupeleka EU. Maana ya kuwa na EU ni ili WZN wafaidike na rasilimali za Tanganyika bila Watanganyika kufaidi rasilimali zao kama alivyoonyesha namba(16)(17)

      Namba (14)Anashauri tuwe na muungano kama wa Senegambia wakati huo huo anasema ule ulishindwa (15). Ahmed anataka tuige uchafu ili mradi tu tuwe na mkataba anaotaka yeye. Anaandika jambo na kulikanausha hapo hapo, ushahidi wa kiwango dhaifu sana cha uandishi.

      Namba(16)kama hataki ZNZ iingiliwe katika mambo yake basi ashauri muungano uvunjwe. Kwanini anatapa tapa na serikali 3, mkataba au mfumo wa EU. Kitendo cha kuwa na mkataba tayari ZNZ inapoteza uhuru sasa sijui anataka mamlaka kamili yapi. Mwandishi Ahmed anajichanganya na sina uhakika anajua anaandika nini.

      Namba(17)Huko nyuma amesema mkataba utakuwa na kura ya turufu, hapa anasema kila nchi itakuwa na uhuru bila kuomba ridhaa ya nchi nyingine. Too low Ahmed

      Watanganyika, hapa tulipo hatuna sababu ya kuwa na ushirikiano na ZNZ kwasababu ZNZ haina kitu cha maana cha kutoa. Wao wanataka kuwe na ushirikiano kama wa EU ili waendelee kuinyonya Tanganyika.

      Ukweli ni kuwa yale madai kuwa Tanganyika inaizuia ZNZ sasa ni wazi ni uongo uliotukuka. Zanzibar haina ujanja inataka muungano kwa hiari au kwa lazima. Hizi habari za serikali 3, mkataba wa EU, wa Uswiss ni kutapa tapa kwa kutambua kuwa nje ya muungano atakayepigika na kuumia ni ZNZ.

      Ahmed Rajab aache kututukana kuwa hatujui mkataba, yeye ndiye hajui kwasababu hajataja jambo hata moja. Ukweli ni kuwa anataka ushirikiano ili Tanganyika itoe rasilimali zake kama alivyosema katika ulinzi na usalama ambapo ZNZ haina bajeti, elimu ya juu ZNZ haina bajeti, soko la ajira ambalo ZNZ haina, soko la Biashara ambalo ZNZ haina, Ardhi ambayo ZNZ haina n.k. Hicho ndicho anataka katika hoja ya mkataba.

      Tayari tuna EAC, SADC na UA, tukutane huko kama nchi huru. Upuuzi wa kusema eti tutawavutia wengine ni umahaluni wa hali ya juu. Tuwavutie kwanini wakati tayari tuna ushirikiano. Hatunatutakachopata kwa ushirikiano wowote ule, sisi tutakuwa losers na hapa ni wakati tuwaambie kuwa Wanatuhitaji na wafunge midomo, kinyume chake LET ZNZ GO!

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By FJM
      Hii article ya Ahmed Rajab ni kizunguzungu tupu! Maalim Seif anazunguka dunia sasa akishawishi wakubwa ili Zanzibar iwe na kiti chake UN. Kwa maneno mengine Maalim Seif anataka Zanzibar iwe dola kamili. Sasa kama anataka dola kamili hatua sahihi za kuchukua ni zipi, kupeleka muswada BLW au kwenda Marekani na UK kupiga porojo?

      Mambo ambayo ningeta kumuuliza Rajab:
      1. AG anataka muungano unaofanana na Switzerland - (kwa vipi, Swiss wameungana kivipi?)
      2. Rajab alikuwa anaongelea serikali 3, kabali mwelekeo lini na kwa nini?
      3. Sasa hivi Rajab anataka muungano wa mkataba. What excatly anataka kiwe kwenye mkataba, na Zanzibar wanaweka nini mezani?
      4. Kama nia ku-copy & paste EU, kwanini tusikutane Addis - AU? au Arusha - EAC?
      FJM, Ahmed alianza na kutaka muungano uvunjwe ili ZNZ iwe kama Malaysia au Mauritius. Wenzake wakamwambia watu laki 350 wakirudi ZNZ soko la ajira na biashara litatoka wapi? Wakamshauri afikirie njia nyingine.

      Akaja na serikali 3, tukamkomalia hapa aeleze hiyo ya tatu itakuwa na mamlaka gani wakati ZNZ inataka kiti UN na EAC, FIFA, International Netball Org n.k Tukamtonya kuwa Tanganyika ikirudi haitakubali upuuzi wa kutoa ajira wakati wananchi wake wanatengwa, upuuzi wa kugawa ardhi wakati wananchi wake hawana haki hiyo, haitakubali kusomesha watoto wa nchi jirani bure, wala kugawa umeme wa bure watu wakicheza bao n.k.
      Wiki mbili zilizopita akasema WZNZ hawataki serikali 3 zimepitwa na wakati.

      Akaja na Mkataba, tukamuuliza lini alicha kudai mkataba wa mwaka 1964? Na je anataka mkataba wa mambo gani.
      Hajaweza kufungua kinywa kusema neno hata moja linalohusu mkataba. Akaona hapo ni pagumu

      Sasa amehamia muungano wa EU, tukwamwambia EU si muungano ni jumuiya kama EAC na kama hicho ndicho anataka basi twende EU tukiwa nchi tofauti. Anasema hapana tutengeneze mkataba wetu ''wa mmoja kutoa na mwingine kukinga mkono'' ili tuwavutie Kenya, Uganda n.k. Tukamuuliza tuwavutie kwa lipi wakati tuna EAC inayotakiwa iivutie ZNZ?

      Amebadili anasema tuwe na Mkataba wa Senegambia, hapo hapo anasema huo ulishindwa, yaani tuige upuuuzi hata kama ulishindwa kisa WZNZ wanataka kubebwa mgongoni.
      Hili tunasema hakuna ni ima watulie ndani ya mbeleko na kama hawataki wateremeke na kutembea wenyewe.

      Maalimu yupo huko akitaka kiti UN, kitu kinachopingana na sera ya CUF.
      Huyu bwana ni mjanja sana baada ya kuchochea UAMSHO sasa amekwenda kusafisha jina kama alivyokuwa anawachochea CUF na kukimbilia Ulaya. Hakuwahi kushiriki maandamano yoyote.

      Mkataba wanaotaka kama umesoma makala ya Ahmed ni kuhusu
      1. Ulinzi na usalama ambao hawana bajeti hata senti tano.
      2. Kuendelea kusomesha watoto bureee kwa kodi za Mtanganyika
      3. Kupata soko la ajira maana wakirudi kwao wote watauana tu, ajira itoke wapi?
      4. Soko la biashara, asilimia 97 ya biashara yao inategemea soko la bara wakirudi kwao watafanya na nani
      5. Supplies, wanategemea sana bara kama kununua viazi, ndizi mkono, kisamvu, mhogo, nyama n.k kwa bei ya madafu nje ya hapo ni dollar
      5. Mkataba wa ardhi kwasababu sultani atakaporudi kabwela itabidi aondoke alipo. Kisiwa kitanunuliwa kwa bei poa.
      6. Achilia mbali pesa za bure za bajeti, bilioni 32 zisizo na kazi n.k

      Ndiyo maana hata siku moja hutasikia wanadai passport, wanajua wakiwa na passport iliyo na rangi tofauti na kijani ulaji, bwerere, halua, starehe, taa za bure na kila aina ya starehe mwisho Chumbe! Hawadai hata kwa bahati mbaya

      Nadhani umesoma makala na kuona alivyojivuruga na kujichafua. Sasa hivi kule Mzalendo wanasema mkataba ndio jambo bora na wanahofu kama nini, Zanzinet kule ni kwa sultan wao wanasema wanataka uhuru.

      LET ZNZ GO!
      JokaKuu, Ngongo, FJM and 1 others like this.

    4. #22
      takashi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2009
      Posts : 787
      Rep Power : 674
      Likes Received
      139
      Likes Given
      780

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By Nguruvi3
      Mzee Mwanakijiji, yaani naona wewe kama una moyo zaidi maana hata kuwapa nafasi ya pili ni moyo.
      Mimi naona tuwaunge mkono waondoke katika muungano huu usio na faida kwao kabisa, wakishajifunza watarudi kuomba mkataba wakiwa na adabu.
      Ndio maana kila siku tunasema LET ZNZ GO
      Hamna lolote ...nyinyi kazi yenu porojo tu. Kama kweli mnasema LET ZNZ GO! Iweje mnaleta hela ili watu wakubali Muungano kama ulivyo. Iweje kila unapofanyika uchaguzi ZNZ mulete mamulki ili wapige kura ku-support pro Tanganyika . Kama nyinyi ni wakweli , mngeanza kuzuwia watanganyika wasije kupiga kura hapa ZNZ. Vile vile wakatazeni hao wanaoleta hela hapa kurubuni waZNZ.

      Kazi kuongea porojo na unafiki LET ZNZ GO! LET ZNZ GO! Kumbe kuachia hamuwezi. Mwabieni Nape , asijipendekeze ZNZ , mfumo wake Kristo awapelekee wakulima wa milimani sio hapa. ZNZ sio mali ya CCM.
      HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE...MPAKA KIELEWEKE.

    5. #23
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By takashi

      Sheikh anayedai serikali 3, mkataba, EU, Uswiss, Vanuata na Fiji, Senegambia, California na Mayote n.k. ni nani?

      Si umeona Mwalimu wenu Ahmed Rajab Msomi anavyovurugwa hapa na hoja zake kuonekana kana insha ya mtoto wa Form II C.

      Kuleni pesa, kateni muungano! lakini kama mnalilia lia na mkataba na serikali 3 hamna hoja nyie, tulieni kimya mgongoni.
      Ala! Mumebebwa halafu manataka kucheza msewe mgongoni! ohoo!

      LET THEM GO! LET ZNZ GO!

    6. #24
      takashi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2009
      Posts : 787
      Rep Power : 674
      Likes Received
      139
      Likes Given
      780

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By Nguruvi3
      Sheikh anayedai serikali 3, mkataba, EU, Uswiss, Vanuata na Fiji, Senegambia, California na Mayote n.k. ni nani?

      Si umeona Mwalimu wenu Ahmed Rajab Msomi anavyovurugwa hapa na hoja zake kuonekana kana insha ya mtoto wa Form II C.

      Kuleni pesa, kateni muungano! lakini kama mnalilia lia na mkataba na serikali 3 hamna hoja nyie, tulieni kimya mgongoni.
      Ala! Mumebebwa halafu manataka kucheza msewe mgongoni! ohoo!

      LET THEM GO! LET ZNZ GO!
      Ahmed Rajab na wengine wanahaki ya kuwa na maoni huru...Mimi siungi mkono makataba wala serikali 3...Mimi nataka nyinyi muendelee na Tanganyika yenu na sisi mtuachie tupumue. Lakini hamuwezi , yule mtakatifu wenu aliwadanganya, kawambia ZNZ ni sehemu ya Tanganyika ndio maana hamuwezi kwenda kinyume na yule mnae muabudu.

      Lakini tunaapa kwa jina la ALLAH iko siku mtajuta kulazimisha Muungano... Tumechoka .
      HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE...MPAKA KIELEWEKE.

    7. #25
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,745
      Rep Power : 1163
      Likes Received
      251
      Likes Given
      2515

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      una jua hawa jamaa wajinga saana, muungano wa namna hiyo ni kwamba wakiona hawawezi kuishi wenye ndio wanataka muungano, wakiona wanaweza pata bwana mwingine hawa utaki muungano

    8. Miaka 50

    9. #26
      takashi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2009
      Posts : 787
      Rep Power : 674
      Likes Received
      139
      Likes Given
      780

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By August
      una jua hawa jamaa wajinga saana, muungano wa namna hiyo ni kwamba wakiona hawawezi kuishi wenye ndio wanataka muungano, wakiona wanaweza pata bwana mwingine hawa utaki muungano
      Umelewa pombe au umevuta unga au umechanganya?
      HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE...MPAKA KIELEWEKE.

    10. FJM
      #27
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,182
      Rep Power : 2570
      Likes Received
      5331
      Likes Given
      4587

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By takashi
      Ahmed Rajab na wengine wanahaki ya kuwa na maoni huru...Mimi siungi mkono makataba wala serikali 3...Mimi nataka nyinyi muendelee na Tanganyika yenu na sisi mtuachie tupumue. Lakini hamuwezi , yule mtakatifu wenu aliwadanganya, kawambia ZNZ ni sehemu ya Tanganyika ndio maana hamuwezi kwenda kinyume na yule mnae muabudu.

      Lakini tunaapa kwa jina la ALLAH iko siku mtajuta kulazimisha Muungano... Tumechoka .
      takashi, Zanzibar ina rais wake, bendera, wimbo wake wa Taifa, na katiba yake. Yote haya yamefanyika na Tanganyika hawakuzuia. Sasa kama kweli manata 'muachwe mpumue' kwanini msitangaze muungano finito? Ni kitu gani kimewashinda kupeleka muswada BLW ili mpate kupumua kimoja? Hii tabia ya kunata nata kama binti wa darasa la tano itaisha lini?

      Rajab na wengine wangine wanazunguka mbuyu as if hawajui ni kitu gani cha kufanya. Mara Marekani, mara Uingereza, mara makala, lakini mambo yako wazi:

      1. Kataeni kuwa hamtambui Makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano na mumuite nyumbani Dr Bilal
      2. Watumieni ticket za boti mawaziri, naibu mawaziri toka Zanzibar warudi nyumbani
      3. Pigeni marufuku wabunge toka Zanzibar kwenda Dodoma kushiriki bunge la muungano
      4. Tangazenu uhuru kamili.

      LET ZANZIBAR GO!!!
      Nguruvi3 likes this.

    11. #28
      takashi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2009
      Posts : 787
      Rep Power : 674
      Likes Received
      139
      Likes Given
      780

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By FJM
      takashi, Zanzibar ina rais wake, bendera, wimbo wake wa Taifa, na katiba yake. Yote haya yamefanyika na Tanganyika hawakuzuia. Sasa kama kweli manata 'muachwe mpumue' kwanini msitangaze muungano finito? Ni kitu gani kimewashinda kupeleka muswada BLW ili mpate kupumua kimoja? Hii tabia ya kunata nata kama binti wa darasa la tano itaisha lini?

      Rajab na wengine wangine wanazunguka mbuyu as if hawajui ni kitu gani cha kufanya. Mara Marekani, mara Uingereza, mara makala, lakini mambo yako wazi:

      1. Kataeni kuwa hamtambui Makamu wa rais wa Jamhuri ya muungano na mumuite nyumbani Dr Bilal
      2. Watumieni ticket za boti mawaziri, naibu mawaziri toka Zanzibar warudi nyumbani
      3. Pigeni marufuku wabunge toka Zanzibar kwenda Dodoma kushiriki bunge la muungano
      4. Tangazenu uhuru kamili.

      LET ZANZIBAR GO!!!
      Sisi "tuachiwe tupumue" temekua tukidai kura ya maoni kuhusu Muungano. CCM na vibaraka wao hawataki suala la kura ya maoni kwasababu wanajua matokeo yake ni nini... CCM ndio imeshikilia mpini Tanganyka na ZNZ, nadhani unaona madhila yanayowakuta CHADEMA. Lakini tanasema mwanzo wa mwisho umeanza.

      Kundi la vibaraka lililo vishwa vilemba vya ukoka bado wamo katika ndoto za mchana. Ukombozi unakuja kwa njia moja au nyengine. Tumechoka na Muungano aka mfumo kristo.
      HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE...MPAKA KIELEWEKE.

    12. #29
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By takashi
      Sisi "tuachiwe tupumue" temekua tukidai kura ya maoni kuhusu Muungano. CCM na vibaraka wao hawataki suala la kura ya maoni kwasababu wanajua matokeo yake ni nini... CCM ndio imeshikilia mpini Tanganyka na ZNZ, nadhani unaona madhila yanayowakuta CHADEMA. Lakini tanasema mwanzo wa mwisho umeanza.

      Kundi la vibaraka lililo vishwa vilemba vya ukoka bado wamo katika ndoto za mchana. Ukombozi unakuja kwa njia moja au nyengine. Tumechoka na Muungano aka mfumo kristo.
      Mumeshawahi kupeleka mswada? Nani katika ninyi ametoa japo maoni ya kuvunja muungano? Mnataka mkataba wa nini?mnataka serikali 3 za nini?
      Mnatafuta mahali pa kusingizia, hangaikeni muikomboe ZNZ vinginevyo mtulie mle malezi
      JokaKuu likes this.

    13. #30
      takashi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2009
      Posts : 787
      Rep Power : 674
      Likes Received
      139
      Likes Given
      780

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By Nguruvi3
      Mumeshawahi kupeleka mswada? Nani katika ninyi ametoa japo maoni ya kuvunja muungano? Mnataka mkataba wa nini?mnataka serikali 3 za nini?
      Mnatafuta mahali pa kusingizia, hangaikeni muikomboe ZNZ vinginevyo mtulie mle malezi
      Bw Nguruvi3,

      Sisi "tuachiwe tupumue" tulishakusanya saini za watu ambao hawataki Muungano. Chaajabu hapa hapa JF ,mlisema kama sisi tunajiingiza kwenye siasa wakati sio chama cha siasa. Tumekwenda hadi Baraza la Wawakilishi kumuona muwakilishi wa jimbo la Kikwajuni kumkabidhi maoni yetu ya kutaka aitishe hoja maalumu. Katibu wa Baraza alituitia POLISI eti tumekusanyika kinyume cha sheria.

      Hatimae jubu tulilopewa na katibu kwa niaba ya Spika Kificho, eti tupeleke maoni yetu kwenye tume ya katiba mpya. Baraza kwa sasahivi haliwezi kujadili hoja ya yeyote juu ya kuvunja Muungano. Hizo ni miongoni mwa harakati ambazo tumezifaya. Wewe kama mmoja wa wapiga debe LET ZNZ GO ! Umefanya nini zaidi ya porojo hapa? Umeandika makala yeyote kuhoji kwa nini watanganyika wanapelekwa ZNZ kupiga kura kwa PRO-MUUMGANO? Umeandika makala yeyote kuhoji kwa nini Tanganyika wapeleke hela ZNZ kuwagaia watakao kubali Muungano uendelee kama ulivyo?

      Sisi tunasema tunataka nchi yetu, ikiwa kwa amani au kwa shari lakini hilo mlielewe kama harakati hizi mwisho wake ni ushindi hapana njia nyengine, iwe leo au baada ya miaka kadhaa lakini ushindi lazima.
      Last edited by takashi; 18th September 2012 at 12:02.
      HIZI SIO ZAMA ZA NYERERE...MPAKA KIELEWEKE.

    14. #31
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Nguruvi3
      Ukisoma namba (1) anasema Tanganyika ni ndugu halafu anawaita nchi ya kigeni (16)
      Hivi wewe unaishi dunia ipi? huna ndugu ambae si Mtanganyika? uko so "confined" kwenye dunia yako ya pekee.

      Watanzania au in this case Watanganyika kwa mamilioni wenye undugu na wasio Watanganyika wala Watanzania tena kwa damu kabisa na si undugu wa Nyerere.

      Mtu ambae unajigamba kuwa utachambuwa bila kupoteza maana, huo ndio uchambuzi wenyewe? Amma kweli Tanzania tuna safari ndefu sana.
      takashi likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    15. #32
      Takalani Sesame's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2008
      Location : Mobile
      Posts : 548
      Rep Power : 666
      Likes Received
      139
      Likes Given
      99

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Hivi ni nini kinachowazuia Wazanzibar kujitoa kwenye Muungano?!! Tumechoshwa na kelele zenu. Khah!! Mshapewa hadi desa la jinsi ya kujitoa lakini bado tu mnaendelea kutupigia kelele na kutudhalilisha watu wa Tanzania bara. Kama mmeuchoka Muungano mshaambiwa pelekeni muswada BLW na mpitishe kujitoa. Hizi kelele za bata hazisaidii kitu hapa!
      JokaKuu likes this.
      Usually when people are sad they don't do anything. They just cry over their condition. But when they get angry they bring about a change. Malcolm X

    16. #33
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By zomba
      Hivi wewe unaishi dunia ipi? huna ndugu ambae si Mtanganyika? uko so "confined" kwenye dunia yako ya pekee.

      Watanzania au in this case Watanganyika kwa mamilioni wenye undugu na wasio Watanganyika wala Watanzania tena kwa damu kabisa na si undugu wa Nyerere.

      Mtu ambae unajigamba kuwa utachambuwa bila kupoteza maana, huo ndio uchambuzi wenyewe? Amma kweli Tanzania tuna safari ndefu sana.
      Jibu hoja kwasababu mimi nimejibu hoja.
      Insha ya Mwalimu wenu imewaudhi sana ilipogeuzwa ze comedy.
      Ukweli ni huo kuwa Ahmed anawayumbisha left right upside down.
      Sasa ni yeye peke yake ndiye ajuaye ZNZ wanataka nini ninyi wengine mnaimba tu.

      Nimeuliza maswali hamtaki kujibu mumejawa na hasira kwasababu makala ya Ahmed imedhihirika kuwa na kiwango hafifu sana huku Tanganyika ingawa inaweza kuwa excellent kwa ZNZ kutokana na viwango tofauti vya mitizamo na uelewa.
      Tunamwambia uzuri wa makala zake Chumbe!

      Jibuni hoja, mnataka mkataba wa nini?
      Kwanini hamtaki kuvunja muungano mumebaki mnahangaika hangaika na muungano wa EU, Uswiss, Vanuata,
      Comoro na Mexico.
      Mmepeleka mswada barazani?
      Mmewaita 350,000 warudi nyumbani?
      Mumewaita akina Mwinyi, Nahodha na Bilal watoke katika serikali ya muungano.
      Je mlishawaambia wanafunzi wenu wanaosoma kwa social welfare warudi wakasome Tunguu?

      Zomba na Takashi, muda wa matusi umekwisha sasa ni hoja, kama hamna nendeni kwa Mwalimu Ahmed awapige darsa feki kama la serikali 3, EU, uswiss, muungano wa Somalia na Ghana n.k.
      JokaKuu likes this.

    17. #34
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By Nguruvi3
      Jibu hoja kwasababu mimi nimejibu hoja.
      Insha ya Mwalimu wenu imewaudhi sana ilipogeuzwa ze comedy.
      Ukweli ni huo kuwa Ahmed anawayumbisha left right upside down.
      Sasa ni yeye peke yake ndiye ajuaye ZNZ wanataka nini ninyi wengine mnaimba tu.

      Nimeuliza maswali hamtaki kujibu mumejawa na hasira kwasababu makala ya Ahmed imedhihirika kuwa na kiwango hafifu sana huku Tanganyika ingawa inaweza kuwa excellent kwa ZNZ kutokana na viwango tofauti vya mitizamo na uelewa.
      Tunamwambia uzuri wa makala zake Chumbe!

      Jibuni hoja, mnataka mkataba wa nini?
      Kwanini hamtaki kuvunja muungano mumebaki mnahangaika hangaika na muungano wa EU, Uswiss, Vanuata,
      Comoro na Mexico.
      Mmepeleka mswada barazani?
      Mmewaita 350,000 warudi nyumbani?
      Mumewaita akina Mwinyi, Nahodha na Bilal watoke katika serikali ya muungano.
      Je mlishawaambia wanafunzi wenu wanaosoma kwa social welfare warudi wakasome Tunguu?

      Zomba na Takashi, muda wa matusi umekwisha sasa ni hoja, kama hamna nendeni kwa Mwalimu Ahmed awapige darsa feki kama la serikali 3, EU, uswiss, muungano wa Somalia na Ghana n.k.
      Hilo la kwanza tu huwezi lijibu na unajuwa kuwa umekosea sana tena sena, kutufanya Watanzania kuwa hatuna ndugu wasio Watanganyika au Watanzania. Bado tu? unataka mengine? moja hili hujalimaliza na unaona haya kusema kuwa hapo ulichanganya madawa.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    18. #35
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By zomba
      Hilo la kwanza tu huwezi lijibu na unajuwa kuwa umekosea sana tena sena, kutufanya Watanzania kuwa hatuna ndugu wasio Watanganyika au Watanzania. Bado tu? unataka mengine? moja hili hujalimaliza na unaona haya kusema kuwa hapo ulichanganya madawa.
      Kwanza nashukuru sana kwamba umekubaliana na yote isipokuwa hilo moja tu. Pili, ni kawaida ya Ahmed kutumia neno ndugu zetu pale anapotaka hoja yake ikubaliwe na Watanganyika.

      Katika mazingira tuliyo nayo ambayo ni nchi ya Tanzania yenye kiti kimoja UN, EAC, SADC, FIFA n.k ni jambo la kusikitisha kusikia kuwa hao anaowaita ndugu zake inapofika mahali pa kuongelea rasilimali anasema ni Wageni.
      Ungeliangalia hilo kwa mtazamo mpana lisingekusumbua.

      Zomba, hoja kubwa ni hizi;
      Kwanini ZNZ inataka mkataba
      Kwanini ZNZ imegoma kuondoka katika muungano, kama alivyosema Ahmed
      Kwanini ZNZ haijafanya jitihada za kisheria na kijamii kutaka kuvunja muungano

      Ukishafikiri hayo jiulize haya
      Hivi kuna muungano wa EU?
      Kwanini tuamini kuwa muungano wa Sengambia ambao Ahmed ameuleza kuwa ni mzuri na kisha kujisuta kuwa umekufa unadhani unafaa kwa mintaarafu ya kiongozi wako Ahmed

      Jiulize kwanini Ahmed, ameacha hoja ya kuvunja muungano, kuwa na serikali 3, mkataba na sasa anataka EU ambayo kimsingi si muungano labda kwa mtazamo wa kiunguja.
      JokaKuu and Ngongo like this.

    19. #36
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By Nguruvi3
      Kwanza nashukuru sana kwamba umekubaliana na yote isipokuwa hilo moja tu. Pili, ni kawaida ya Ahmed kutumia neno ndugu zetu pale anapotaka hoja yake ikubaliwe na Watanganyika.

      Katika mazingira tuliyo nayo ambayo ni nchi ya Tanzania yenye kiti kimoja UN, EAC, SADC, FIFA n.k ni jambo la kusikitisha kusikia kuwa hao anaowaita ndugu zake inapofika mahali pa kuongelea rasilimali anasema ni Wageni.
      Ungeliangalia hilo kwa mtazamo mpana lisingekusumbua.

      Zomba, hoja kubwa ni hizi;
      Kwanini ZNZ inataka mkataba
      Kwanini ZNZ imegoma kuondoka katika muungano, kama alivyosema Ahmed
      Kwanini ZNZ haijafanya jitihada za kisheria na kijamii kutaka kuvunja muungano

      Ukishafikiri hayo jiulize haya
      Hivi kuna muungano wa EU?
      Kwanini tuamini kuwa muungano wa Sengambia ambao Ahmed ameuleza kuwa ni mzuri na kisha kujisuta kuwa umekufa unadhani unafaa kwa mintaarafu ya kiongozi wako Ahmed

      Jiulize kwanini Ahmed, ameacha hoja ya kuvunja muungano, kuwa na serikali 3, mkataba na sasa anataka EU ambayo kimsingi si muungano labda kwa mtazamo wa kiunguja.
      Hivi wewe ndugu yako uliyezaliwa nae kwa damu mnaachiana mali zenu? account yako ya benki ndio yake? nyumba zako ndio zake? mali zake ndio zako? Hebu kuwa mkweli kidogo. Ndugu mnaweza kusaidiana ikibidi lakini mali kila mtu na yake, hata iwe ya kurithi kila mtu ana chake. Kwa mawazo kama yako mwisho utasema mkeo ni mke wa nduguyo.

      Huna hoja wala sikukusoma zaidi ya hiyo sentensi moja, mpaka urekebishe hiyo kwanza. Utetezi wako wote mpaka sasa kuhusu undugu hauna msingi.
      takashi likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    20. #37
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,745
      Rep Power : 1920
      Likes Received
      1180
      Likes Given
      972

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Tatizo moja nililogundua hususan katika mada hizi za Muungano ni kuona waTanganyika wamekuwa
      1. waoga sana kutaka kuvunja muungano
      2. Wanajiona kuwa ni dhaifu sana katika huo muungano kiasi cha kuwa waoga kutoa maamuzi
      3. maamuzi yote wamepewa waZnz ambao wao hawana nguvu za Doula. lakin ndio wasemaji na wakosoaji wa waziwazi kuhusu huo muungao.

      Nawapa pole watanganyika.
      zomba and takashi like this.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    21. #38
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,848
      Rep Power : 2972
      Likes Received
      2455
      Likes Given
      3538

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Nguruvi3,

      ..mpotezee tu huyo.

      ..nia yake ni utoke kwenye msingi wa hoja zako, uanze kujadili vitu trivial.
      Nguruvi3 and FJM like this.

    22. #39
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By Barubaru
      Tatizo moja nililogundua hususan katika mada hizi za Muungano ni kuona waTanganyika wamekuwa
      1. waoga sana kutaka kuvunja muungano
      2. Wanajiona kuwa ni dhaifu sana katika huo muungano kiasi cha kuwa waoga kutoa maamuzi
      3. maamuzi yote wamepewa waZnz ambao wao hawana nguvu za Doula. lakin ndio wasemaji na wakosoaji wa waziwazi kuhusu huo muungao.Nawapa pole watanganyika.
      Baru baru Watanganyika ni waoga kwa lipi? Ukisoma makala ya Ahmed Rajab hakuna mahali ametaja kuvunja muungano badala yake amerudia mara 3 kuhusu kubadili muundo wa muungano.

      Ukisoma zaidi amesema Watanganyika hawajishughulishi na suala la muungano kama Zanzibar hapa maana yake ni kuwa Watanganyika hawana cha kupoteza.

      Heu jiulize nani ameshikia bango suala la serikali 3, mkataba, muungano wa EU, muungano wa Uswiss, muungano wa SeneGambia n.k? Kwanini ZNZ wanao ona wanaonewa wasiamue hatima yao kwa kauli moja wamebaki kuzunguka mbuyu na kuimba vibwagizo vya nyimbo wasizoweza kuzitetea?

      Takalani Sesame na FJM wamesema kuwa licha ya ZNZ kupewa mbinu zote(desa) za kujitoa nakuwa dola huru mbona hakuna uthubutu wa kufanya japo kimoja?

      Mbona hatusikii tena zile kauli za kuvunja muungano? badala yake tunasikia kubadili muundo, mkataba n.k.
      Labda Baru baru unifahamishe, kwani mkataba mnaosema utahusu nini?
      JokaKuu and Ngongo like this.

    23. FJM
      #40
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,182
      Rep Power : 2570
      Likes Received
      5331
      Likes Given
      4587

      Default Re: BARAZANI KWA AHMED RAJAB Muungano wa Mkataba utaleta Umoja wa Afrika

      Quote By Barubaru
      Tatizo moja nililogundua hususan katika mada hizi za Muungano ni kuona waTanganyika wamekuwa
      1. waoga sana kutaka kuvunja muungano
      2. Wanajiona kuwa ni dhaifu sana katika huo muungano kiasi cha kuwa waoga kutoa maamuzi
      3. maamuzi yote wamepewa waZnz ambao wao hawana nguvu za Doula. lakin ndio wasemaji na wakosoaji wa waziwazi kuhusu huo muungao.

      Nawapa pole watanganyika.
      Tanganyika hawaogopi kuvunja muungano Barubaru, as a matter of fact, mjadala ya muungano haujageuzwa kuwa three course meal kama ilivyo kwa Zanzibar. Kinacholeta shida hapa ni hizi kelele za 'dovorce' lakini hakuna mtu anajaza fomu za talaka - for years! Mtu unasema unataka talaka lakini wakati huo huo unamtayarishia maji ya kuoga na chakula mezani kawa kawaida - hivi hapo unadai talaka au unataka kujua kama una bei?

      Taratibu za kuachana na ndoa zinajulikana, hizi geresha za nini? Au mnatishia ili bill ya umeme mlipiwe tena?
      Nguruvi3 likes this.

    Page 2 of 9 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...