Wakuu nimekuwa na maswali mengi sana juu ya polisi kupiga mabomu ya machozi mpaka ndani ya ofisi kule nyololo Iringa.
1:je lengo lilikuwa kwa waliokuwemo ndani ya ofisi?
2:nini kilikusudiwa watoke ndani wakimbie?
3:nini maana yakutawanya watu,walio nje au walio ndani ya ofisi?
4:je ni agizo la RPC Kamuhanda kuwa wafanye hivyo,maana alikuwepo eneo la tukio akitoa amri.
Na maswali mengine mengi ambayo unaweza kuyaongezea.Wakuu haya ndiyo mafunzo ya jeshi letu la polisi juu ya kutawanya watu.Hata kama wametawanyika ni halali kupiga bomu la machozi ndani ya nyumba walizokimbilia? Kama hii si haki kwanini viongozi wa juu wa jeshi la polisi wasichukuliwe hatua?
Nawasilisha.

Reply With Quote


Follow Us Here