Re: Nimrod Mkono aitisha CCM

By
Kimbunga
Mkuu
Mchambuzi nashukuru kwa hoja mujarabu. Nilijua tu nitapata kitu toka kwako. Umenena vyema kuhusu matycoon wa CCM ambao inaonekana ndio wanakivuruga chama. Lakini nakumbuka kwamba matycoon walikuwepo tangia enzi za TANU wakichangia Chama lakini hawakuwa wakikemea na kuvuruga chama. Hivi watu kama akina Rupia enzi hizo si walikuwa matycoon ambao walifikia hata kumapatia mwalimu nauli ya kwenda UNO pamoja na kumpangia nyumba ya kuishi jijini lakini hawakuwa na makeke kama haya? Akina Al nuur Kasum vipi wao hawakuwa wachangiaji wa chama kweli?
Haya tukija miaka ya tisini ndipo hapo nakumbuka wale pace makers nao waliamua kuingia kwenye chungu kuona kuna nini humo. Kumbuka yule pace maker wa Ifakara akiitwa Abbas Gulamali na akina Biku mbona wao hawakuwa kama hawa wa sasa? Nadhani kuna shida nyingine kubwa zaidi ya huu utycoon. Hivi tunaweza kusema kwamba CCM ina mkemeaji ambaye anaweza kusimama na kukemea na watu wakamsikia siyo kwa ukali wa sauti yake bali kwa historia na usafi wake?
Mkuu Kimbunga,
Ni kweli CCM ilikuwa na wachangiaji watanzania (WEUSI) huko nyuma lakini pia wenye asili ya kiasia; Lakini uchangiaji ule ulikuwa zaidi katika hatua za mapambano dhidi ya ukoloni ambapo watanganyika walihitaji kujitolea kwa hali na mali kufanikisha project ya independence; pia miaka y amwanzo ya uhuru, kulikuwa na wachangiaji wa namna nyingi (weusi, lakini hasa wahindi) katika hatua za mwanzo za TANU kuzidi kujiimarisha na baada ya kushika hatamu, hasa katika kipindi cha Ujamaa hadi miaka ya mwanzo ya tisini, CCM iliweza kujiendesha kupitia njia nyingine mbalimbali, lakini hasa kwa kutegemea fedha kutoka serikalini na pia kutoka kwa marafiki wa Ujamaa waliokuwa nje ya Tanzania;
Suala la Abbas Gulamali na wengine, uwepo wa Nyerere in my view ulisaidia sana kupunguza vituko tunavyoviona sasa, kwani Nyerere alikuwepo na alikemea sana mienendo ya ajabu ajabu iliyokuwa inakivuruga chama, kila ilipokuwa inajitokeza;
Kuhusu CCM kuwa na kiongozi mwenye moral authority, ni dhahiri mtu wa namna hiyo hatunae tena baada ya Nyerere kuondoka; kiongozi kuwa na moral authority maana yake ni kwamba kauli au tamko lake juu ya masuala ya maadili na uadilifu kuhusu mwenendo wa siasa za nchi, ina mamlaka ambayo yanatambulika na kukubalika na wananchi wengi, hasa katika mtazamo wa masuala yaliyo over and above politics; kiongozi wa namna hiyo ni lazima akubalike na makundi yote ya jamii bila ya kujali tofauti za kidini, kabila, jinsia, kipato,au political orientation; mtu wa namna hiyo lazima aheshimike, na aungwe mkono na walio wengi kwa mtazamo wa kitaifa zaidi kuliko kitu kingine chochote; baada ya kuondoka Nyerere, hata moral authority ya CCM kitaasisi imemomonyoka; haya hasa ni matokeo ya chama kuchafuka kwa rushwa/ufisadi, lakini muhimu zaidi chama ku-betray historia yake yenyewe; Hivi sasa ni vigumu kwa mtu kupinga hoja kwamba CCM imepoteza both Moral authority na Political legitimacy;
CCM is a cookie that crumbles; Chama hakiwezi tena kujinasua kutoka kwenye maporomoko ya sasa katika anga za siasa; kinachoiweka CCM madarakani sasahivi ni RULE BY LAW (sio RULE OF LAW) na pia vyama vya upinzani (hasa Chadema), kutokuwa na dira mbadala ya taifa inayo inspire watanzania walio wengi, hasa vijijini; Kitendo cha CCM kupita kwenye kampeni na kutamka majukwaani itajenga barabara na Chadema kufuata muda mchache baadae na kusema itatoa elimu bure msingi hadi chuo kikuu haitoshi;
"In the future, it is possible that a Second Party will grow in Tanganyika, but in one sense such a growth would represent a failure by TANU."
J.K Nyerere, 1968.
Follow Us Here