Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

    Report Post
    Page 4 of 27 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 529
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22277

      Default Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Wanabodi, Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is nothing to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...
      1. Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
      2. Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama vile ni mbali, unless wamsimamishe their one and only jewel!.
      3. Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakiichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu!.
      4. Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu, sasa wameichoka, hivyo uchaguzi wa 2015, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
      5. Hakuna ubishi kuwa Chadema, ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kuliko CCM, hivyo ule mtaji mkubwa wa CCM iliyoutegemea kwa miaka nenda miaka rudi, sasa umehamia Chadema!.
      6. Kama ambavyo CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea tuu, na sasa CCM imechokwa, vivyo hivyo kwa sasa Chadema haina lolote la kukifanya kipendwe, bali kinapendwa kwa sababu "watu" wameichoka CCM!.
      7. Kama uchaguzi utaitishwa leo, Chadema itashinda kwa kishindo kikubwa cha ajabu, lakini ukiwauliza hao watakaokipa Chadema ushindi, ni sababu zipi za kuichagua Chadema, hawatakupa sababu yoyote zaidi ya kuichagua Chadema kwa sababu wameichoka CCM!.
      8. ili Chadema iweze kupata ushindi wa Tsunami kwa uchaguzi wa 2015, lazima Chadema ikubali kubadilika, isiendelee kuutegemea huu umaarufu wa muda kwa kushangiliwa na umati wa watu walioichoka CCM, bali Chadema sasa lazima iwape Watanzania sababu za kuichagua Chadema!.
      9. So far so good, Chadema is doing a good job chini ya Uongozi Shupavu wa Kamanda Mbowe na kinara wa M4C, Dr. Wibroad Slaa, Chadema is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
      10. Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kuzifanyia kazi hizi hoja na tatu mkubali kubadilika!.

      Naomba kumalizia kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanachama wetu humu jf.
      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Nitasema jambo moja zito- labda mbeleni nitaliangalia zaidi - ni wagumu sana kushaurika. Wametengeneza cocoon ya kujilinda kiasi kwamba ni vigumu sana kuweza kutoka ndani. Na kama kuna kitu kitakachosababisha waendelee kuwa wapinzani wa kudumu siyo kukosa ushauri au mawazo mapya bali kutokukubali kubadilika.
      Kwa wale wapenzi wa Chadema, for sure, Uchaguzi wa 2015, Chadema inaweza kabisa Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If "Itabadilika" and provided that CCM haitamsimamisha yule mgombea wangu!. Japo ni vema kuwa na great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best na kama Chadema haitabadilika, you better get prepared for the worst kwa sababu 2015 itakuwa ni CCM Tena!.NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.Naomba kuwasilisha.Pasco.
      UP DATE 1.Kufuatia maswali mengi kuhusu Chadema wabadilike nini, naomba kumnukuu mmoja wa great thinkers wetu humu jukwaani
      Quote By Mchambuzi
      ‘The Country is Suffering From CCM Fatigue’. Kuna tofauti kubwa baina ya “Doing the Right Things” na “Doing things Right”, na ili ufanikiwe, nilazima kufanya yote mawili. Chadema has been doing the right things ambayo ni kutumia kikamilifu mapungufu ya CCM kujijenga kisiasa. Lakini tatizo linakuja kwenye “doing things right” Mbinu za upinzani zinazotumiwa na Chadema Hazipo Consistent na CoherentKwanza Chadema wanastahili pongezi kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kuwa politically active majira yote. Lakini pamoja na mafanikio haya, bado Chadema kinaonyesha udhaifu mkubwa kwenye mbinu inazotumia kuendesha siasa za upinzani. Mbinu za Chadema kwa kiasi kikubwa hazina consistency (uthabiti) na coherence kwani zinabadilika mara kwa mara. Hili ni tatizo, hasa pale chama kinapokuwa hakina mvuto unaotokana na itikadi bali masuala ya mpito Upinzani dhidi ya Itikadi ya CCM, lakini bila ya kutoa dira na itikadi mbadala iliyo practical – Chadema wamekuwa wanapinga sera nyingi za CCM bila ya kutoa itikadi na dira mbadala Ni muhimu nisisitize kwamba tatizo sio mbinu hizi za upinzani bali the inconsistency na incoherence katika hilo.

      Leo hii masuala ya uongozi na siasa yametawaliwa sana na misingi ya Ukanda, Ukabila na Udini. Inawezekana baadhi ya watu wasikubaliane na mimi katika hili, Ni vigumu kwa sasa kubaini masuala la udini, ukabila na ukanda yata ‘play out’ vipi katika siasa za CCM na Chadema 2015. Vinginevyo ni muhimu Chadema ikafanya marekebisho ya maana kwenye itikadi yake, kwani nje ya uchovu wa wananchi na CCM, nje ya agenda ya serikali ya CCM kutokuwa na maamuzi magumu kutatua matatizo ya nchi, na pia nje ya agenda ya ufisadi, Chadema haina ammunition ya kutosha kisera kuitoa CCM magogoni. Hili linahitaji kubadilika na ndio kete kuu ya Chadema 2015 itakayowaletea mafanikio yenye mashiko zaidi mbali ya vita dhidi ya ufisadi ambayo sio mwarobaini (panacea) ya matatizo ya wananchi walio vijijini.

      Ni mambo haya ambayo nadhani yakifanyiwa kazi na Chadema, basi yatazidi kujenga mazingira ya utayari kwa Chadema kushika madaraka ya nchi 2015 – kwani mbali ya “doing the right things”, pia watakuwa wametekeleza dhana ya “doing things right”
      NB. Kwa maswali yoyote kuhusu haya mambo ambayo Chadema inahitaji kubadilika, naomba uyaelekeze moja kwa moja kwenye thread husika hapa.CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015
      UPDATE 2: Input ya Mchambuzi.
      Quote By Mchambuzi

      Ningependa kuchangia kidogo kuhusu suala hili la rushwa, hasa kwa kujaribu kujengea hoja kwanini rushwa ni hoja ya ukombozi. Naungana na wewe kupinga hoja kwamba Ufisadi sio hoja ya kuwakomboa watanzania. As a matter of fact, vita dhidi ya Ufisadi/Rushwa na ile dhidi ya umasikini lazima viende kwa pamoja, vinginevyo kuendeleza vita dhidi ya umaskini huku vita dhidi ya ufisadi vikilega lega, juhudi za kutokomeza umaskini hazitazaa matunda na tutaishia tu kupoteza resources nyingi sana pamoja na muda mwingi bure kwenye vita dhidi ya umaskini ambavyo havitamalizika.

      Mabadiliko yoyote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yenye kulenga kuletea faida wananchi walio wengi hayawezi kufanikiwa bila ya kutokomeza rushwa; Rushwa/Ufisadi ni ‘an infection’ kwenye juhudi za Maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ndio maana hata kwenye kwenye international development community, Suala la Rushwa/Ufisadi limeanza kuchukuliwa kama ‘a development issue’ & ‘a development imperative’;

      Kwanini Rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania?

      Rushwa covers a wide spectrum, kuanzia rushwa ndogo ndogo/petty corruption to large scale/grand corruption. Tukianza na Petty corruption, ili mtanzania aweze pata huduma za msingi kabisa zinazosimamiwa na Bureucrats/Administrators kama vile Uhamiaji, Polisi, Ardhi, Elimu n.k, bila ya kutoa ‘kitu kidogo’, normal bureaucratic procedures can’t be accomplished; Mwalimu Nyerere alipokuja na kauli mbiu ya TANU dhidi ya Rushwa kwamba RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA, aliliona hili kwani MASKINI HAWEZI KUPATA HAKI katika jamii inayoendeshwa kwa rushwa, na maskini tanzania ni zaidi ya 80% na hawa wanasubiria ukombozi kwa miaka 50 sasa;
      Mpaka hapa, hoja kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi?

      Tukiangalia aina nyingine ya rushwa - Large scale/Grand Corruption, hii inatokea pale ambapo a considerable amount of money inatolewa kama hongo ili kuwapatia watu fulani fulani preferential treatment au access kwa Rasilimali za watanzania ambazo walipewa na Mungu. Nyerere alitueleza kwamba ili kufanikiwa katika Maendeleo, moja ya vitu muhimu tunavyohitaji ni ARDHI, vingine vikiwa ni watu, siasa/sera safi, uongozi bora n.k. Tumeshuhudia jinsi gani wageni wanajinyakulia ardhi kwa kutoa rushwa huko kwa watawala; tunazidi kuona jinsi gani wawekezaji wanawawekea watawala mamilioni ya dola kwenye mabenki huko Uswisi na kupewa miradi ya madini, mafuta, gesi….miradi ambayo ina kila sura ya kijambazi na unyang’anyi kwani HAKI YA MUNGU aliyopewa mtanzania (rasilimali) inakuwa HAKI YA MZUNGU.
      Pia kwa mfano mwingine huu mdogo tu, hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania inajishikilia wapi.

      Mtu anayetoa hoja kwamba rushwa sio hoja ya kumkomboa watanzania ni dhahiri anawatusi mamilioni ya watanzania waliotaka mabadiliko mwaka 1995 wakati wa Augustine Mrema na NCCR Mageuzi kwani nchi ilikuwa inanuka rushwa, jambo ambalo hata Nyerere alilisema sana; Kama tunaamini katika demokrasia, hasa katika dhana ya nguvu ya umma, umma ule kumuunga mkono Mrema kutokana na msimamo wake dhidi ya Rushwa ni maana kwamba Rushwa ni Hoja ya kumkomboa Mtanzania; Vile vile, katika nyakazi hizi, Chadema imejinyakulia umaarufu na kuungwa mkono na watanzania wengi sana (kwa mamilioni) kwani watanzania wengi wanaona hoja ya rushwa ina mashiko;vile vile the fact kwamba CCM inazidi kupoteza mapenzi mioyoni mwa watanzania wengi ni ushahidi tosha kwamba rushwa ni hoja ya kuwakomboa watanzania;

      Nchini Tanzania rushwa imeshaota mizizi, na its ‘negative effects’ imesha – multiply kwenye jamii. Katika Tanzania, Rushwa/Ufisadi umepelekea mamilioni ya watanzania kupoteza matumaini na hali zao za maisha, umezaa cynicism, hali ya kutoaminiana kwani watanzania wengi sasa wanaamini kwamba rushwa/ufisadi is a ‘norm’. Ufisadi/rushwa unazidi ku-undermine our social values kwa sababu watu wengi wanaona ni rahisi na inalipa kujiingiza katika shughuli za ufisadi/rushwa kuliko kutafuta shughuli au ajira halali;

      Rushwa/ufisadi umeshapelekea mmomonyoko wa uhalali wa serikali ya CCM in the eyes ya watanzania wengi kwani mbali na madhara ya Ufisadi ambayo yanawanyang’anya watanzania ile HAKI YA MUNGU na kugeuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU, vile vile petty corruption inapunguza kwa kiasi kikubwa sana ‘effective delivery’ ya huduma za kijamii, na ni ahadi juu ya upatikanaji wa huduma za namna hii ndio ilipelekea watanganyika wengi kuiunga mkono TANU miaka ya 1950s na hatimaye kuisaidia TANU kutekeleza malengo yake ya ukombozi wa nchi;

      Given all this, mtu anaweza vipi kuja na hoja kwamba Rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania? Wakati tunazidi kushuhudia madhara ya rushwa/ufisadi katika upatikanaji wa huduma za kijamii kwa watazania walio wengi? Na pia jinsi gani ufisadi/rushwa unapelekea watanzania kuporwa HAKI YAO KUTOKA KWA MUNGU (Rasilimali) na inageuzwa kuwa HAKI YA MZUNGU?
      Quote By Mchambuzi
      Cha kuzidi kushanganza zaidi ni pale CCM (tofauti na TANU) kinapogeuka kuwa ni chama cha kujiuma uma kuhusu suala la rushwa/ufisadi. Pengine tunapoteza muda kujadili hoja hii kwamba rushwa sio hoja ya kuwakomboa watanzania bila ya kujua kwamba kumbe ina mahusiano na kujiuma uma kwa CCM; I don’t know, Lakini yetu macho na masikio.
      UPDATE 3: CLOSING REMARKS YA MKUU NGURUVI3

      Quote By Nguruvi3
      Mkuu, kama nilivyoahidi nipo. Ingawa mjadala unaonekana kufungwa hakika sitasita kutupa neno moja au mawili hasa kujibu hoja yako ya kuwa inaonekana nakubaliana na Pasco.

      Ni kweli nakubaliana naye kwa asilimia kubwa sana hata kama si mia moja. Na sababu za kufanya hivyo ni:
      1. Kama alivyosema CCM imechokwa, si tu imechokwa bali imechokwa na matendo yake. Chama kilichopo madarakani miaka 50 hakionekani kuwa tumaini kwa Wananchi, badala yake kimegeuka kuwa genge la waporaji na waporaji hao kulindwa kwa kura za wananchi licha ya kuwa uporaji ni wa kodi zao.

      2.Wananchi wametafuta mbadala kwa miaka mingi na hakika 'ndele' ya kupendwa imeangukia Chadema.
      Ndele hiyo inatokana na jitihada hasa zilizofanyika bungeni kuuonyesha umma wapi tatizo lilipo.
      Yule mama aliyehojiwa Iringa yeye alisema 'Anaipenda chadema kwasasababu kama si wao, yeye asingejua uhuni na udhalimu unaoendelea nchi hii'.Hadi hapo Chadema wame win nyoyo za watu kwa kutambua kuwa wapo wanaosimama nao.

      3.Mikutano inayoendelea ya M4C ni jambo sahihi, lakini haitoshi tu kuwa sahihi ni lazima ifanyike kwa usahihi.
      Mfano, je kila baada ya mkutano kuna ufuatiliaji wa kuimarisha chama eneo husika? Au ni kugawa kadi tu na kukusanya watu na kama ni hivyo je huo ni usahihi hata kama jambo lenyewe ni sahihi?

      4.Juzi tumeona picha za CDM mji mwema. Tena viongozi wakionekana kuwa makini. Aliyeleta picha ni mkereketwa wa Chadema na haikuwa na maelezo nini kimesemwa. Mkutano ni jambo sahihi, je, wamelifanya kwa usahihi? Jibu ni hapana kwasababu hawajawasiliana na umma kama ilivyokuwa mwazoni.
      Wamekuwa 'out of touch' kwa public kama walivyo kwa JF.
      Tayari wameshau ngazi iliyowapindisha na hiyo tu ni tatizo.

      5.Pasco amesema lazima wawe tayari kukubali ushauri, na ushauri tuliwahi kutoa kwa kitengo cha mawasiliano ya umma 'public relationship' na ni wazi hawajaufanyia kazi. Hapo nakubaliana na Pasco kuhusu hoja hiyo.

      6.Uwajibikaji; Tumeona panga la Arusha na Mwanza kwa madiwani.Uamuzi huo ni sahihi, lakini je wameufanya kwa usahihi? Jibu ni ndiyo na hapana. Ni ndio kwasababu wale wanaoleta vurugu wanapaswa kushughulikiwa.
      Ni hapana kwasababu sheria au taratibu zinapindwa kila mara. Kama CDM ilikuwa tayari kupoteza madiwani wa Arusha na wa Mwanza hadi kufikia kupoteza hatamu za umeya katika grassroot level, imeshindikanaje kwa CDM kukubali kupoteza ubunge kwa utaratibu ule ule wanaoutumia? Mbunge mmoja na madiwani 9 ni nani muhimu katika kuimarisha chama.

      7.Taratibu zinazowaangukia madiwani kwanini zisitumike kutuliza mtafaruku uliopo BAVICHA?
      Ikifika hapo tofauti kati ya CDM na CCM inayowafukuzu makatibu wa matawi na kuwaacha wahalifu NEC na CC haipo.
      Inaonekana kama Chadema wanafanya kazi kwa template ya CCM.
      Kwa staili hiyo wananchi wataonaje tofauti ya vyama hivi katika kusimamia taratibu zao kabla ya kupewa madaraka!

      Hapo ndipo niliposema Chadema lazima iwe na clear demarcation iliwatu waone mbadala walio na matumaini nao.
      Ni lazima kuwe na demarcation katika kutoa misimamo ya mambo ya kitaifa. Chadema kama chama pinzani na tegemo kwa wakati mfupi ujao inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujibu, kupendekeza na kunyumbulisha hoja zinazohusu utaifa.
      Mfano, nini msimamo wa Chadema kuhusu muungano?

      8.Chadema wanapaswa kusimama kama taasisi na si kundi la watu fulani maarufu. Taasisi ina namna ya kupanga na kushughulikia mambo yanayohusiana nayo. Suala la Iringa ni mfano mzuri tu. Imewachukua wiki moja kukabiliana na uharibifu wa taswira ya chama uliohusishwa na tukio. In fact kauli ya Mbowe ilikuwa 'damage control' badala ya statement. Tatizo lisiloonekana kwa wengi ni hili la kutokuwa taasisi kikamilifu na ni ngumu kuliona kirahisi.

      9.Kama Chadema hawatajipambanua kama Chama kinachosimamia na kueleza sera zake basi ipo siku wananchi watasema tofauti iko wapi? Hawa wanatenda wale wanakosoa nini kilitakiwa kifanyike!
      Kwa maneno mengine ukosoaji pekee hautoshi ni lazima kuwepo na makusudi ya kueleza sera zao.

      Chadema isimamie sera zake na kuzieneza na si kubaki katika makabrasha au kukaa kimya zikiporwa.
      Hoja kama ya katiba, utawala wa majimbo wameziacha zimeporwa na sasa kuonekana kama za CCM.
      Kwanini hili linatokea? Hoja ya katiba ilikuwa sahihi, je ilifanywa kwa usahihi?

      Kwa ufupi, Chadema sasa kimekuwa na ni wakati kiongoze. Hoja za kukubaliana na CCM kama ya katiba haionyeshi mbadala. Kwangu mimi CDM walikuwa na hoja na waliwaacha wananchi porini. Nitty gritty!
      Pamoja na ukosaoaji sasa ni wakati waeleze wao wana matarajio gani kwa njia gani, rasilimali gani na kipaumbele gani.

      Vinginevyo wananchi watasema 'better the devil you know than the angel you don't know'.
      The simple way CDM could counter act this arguement is to set a clear goal, and make a clear distinction between the past and the future.

      CLOSING REMARKS.
      Wababodi, baada ya 25 pages each with twenty posts, with a total 500 Posts Plus, imethibitika pasi shaka kuwa uchaguzi wa 2015, Ikulu ni ya Chadema, hivyo sasa kuelekea 2015, kila dalili zinaelekeza Chadema kuchukua nchi, ila kwa maoni ya wengi serious waliochangia thread hii (ukiondoa wale wa ushabiki), wengi wamekubali Chadema iko on the right track, ila ili kutimiza lengo hilo la kubisha hodi ikulu, na kukubaliwa kuwa mpangaji rasmi wa jengo lile, lazima Chadema ikubali kubadilika, apart from doing the right thing kama inavyofanya sasa, it got to do things right!.

      Baada ya maneno haya, sasa kwa heshima na taadhima naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa hawa wafuatao.
      1. Mkuu Mkandara, topic yako ya ndio was the inspiration ilionifanya kuanzisha hii thread na niliepuka kukutaja wala kukuquote popote kwa sababu maalum. Asante kwa kujitanabaisha kama mwana Chadema ambaye uko tayari kusimama na ukweli, "no matter what"
      2. Mzee Mwanakijiji , ile quote yako niliyoitumia humu, imekuwa kama ndio "colabo" ya hit single kwa mwanamuziki mchanga, kumshirikisha "star mkubwa" ili atoke!, ndivyo ilivyokuwa hii thread, imefikisha record hits kwa mada yangu yoyote kufikisha posts 500 in two days, hii ndio mara yangu ya kwanza, na naamini kuna wachangiaji walichangia thread hii kwa ajili ya quotation yako. Ingawa wewe binafsi hukuchangia kwa sababu ambazo ninazifahamu fika, thanks for being you, who you are!.
      3. Mkuu Mchambuzi, ule uzi wako wa ndio the subject matter ya hii mada, kwa jinsi ninavyokusoma humu, naamini wewe ni genius kwenye politics zetu, kama Chadema wanakusoma na kuzifanyia kazi hoja zako, 2015, hatuzungumzii ushindi wa Chadema, bali how big the margin is, kati ya mshindi na mshindwa!.
      4. Mkuu Nguruvu3, wewe ni other political genius wetu humu, nilikufahamu kupitia theory yako ya "demage control" na kuendelea kukufuatilia kule kwenye Jukwaa lako, hii closing remarks yako, ni faraja kubwa kwangu, kuendelea kuibua topic ambazo sio popular kwa wana jf wengi, ila huu ndio ukweli halisi ambapo siku zote, kweli itasimama.
      5. Na mwisho, napenda kuwashukuru, wachangiaji wote mlioungana nami katika mada hii, ni vigumu kumtaja kila mtu, lakini shukrani za pekee ziende kwa wachangiaji changamoto akiwemo Mag3, J Mushi, Nicholas, na wengine wengi ambao japo hatukubaliani, lakini tumeishia kukubali kutokubaliana na hii ni healthy kwenye mjadala wowote. Mimi pia ni binadamu kama binadamu wengine, huwa nakwazika na kuwakwaza wengine, na especial kwenye mada yoyote inayomhusu "yule mgombea wangu"! tusameheane na tuzidi kusonga mbele kwa maslahi ya taifa.


      Nakufikia hapa, naomba sasa ku declare rasmi, mjadala huu, umefungwa rasmi!
      this Topic is officially Closed by the thread starter!!
      Last edited by Pasco; 20th January 2013 at 14:00.

    2. RukaaJuu Final

    3. #61
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,019
      Rep Power : 637
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1269

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By JUST
      huu wimbo wa kidini utakusaidia nini wakati hauuziki? usingetawaliwa na wazungu na waarabu leo kauli yako ungesemaje?
      Utaujua hiyo 2015 kama umeuzika au umedoda ... suiri uone, tuombe uhai na uzima mkuu,
      Pasco likes this.
      "If the Virgin Mary appears wearing a Veil on all her pictures, how can you ask me to sign on a HIJAB BAN law ?" -Roberto Maroni, Italian Minister.

    4. #62
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By MKALIKENYA
      MPANDA KATI,NYAMAGANA,BIHALAMULO,MBOZ I,SINGIDA,MASWA,MBEYA MJINI kote uko wamejaa WACHAGA wewe kweli ni PUMBA POINT.
      Huko baaasi, umemaliza? Uzini vipi?
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    5. #63
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By BashaDido
      Hivi huko ccm hakuna wachagga? na je Mwanza na Mbeya wakazi wake wote ni wachagga?
      Msafara wa mamba kenge hakosekani.
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    6. #64
      Fidel80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 19,067
      Rep Power : 9501
      Likes Received
      3186
      Likes Given
      1237

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Mkuu Pasco kwa muktadha huu tuhesabu Lowasa kesha dondokea pua?
      Dah na zile 10m anazotoa bora asitishe tu aendelee kula na wajukuu.
      Pasco likes this.
      **^^+..Ukiuza Utumbo usiogope nzi..+^^**
      Chuda Raha
      Email: [email protected]

    7. #65
      IBRAAH's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd August 2012
      Posts : 127
      Rep Power : 368
      Likes Received
      43
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By mkomatembo
      Chadema sio rahisi kushinda, kwa sababu imeonesha dhahiri kuwa ni chama cha kanisa, sisi waislamu hatuwapi kura zetu , hilo lazima walijue, sasa watashinda kwa kura za kina nani?
      Usiseme sisis waislam.kwanza faham waislam wengi tupo CDM na tunamapenz nacho sasa we utanikataza mim nisipigie kura? kwanza we sio muislam dini yenyew inakataza wiz mbona ssm wanatuibia halaf nijiunge na wez? sitothubutu kuwa CCM au mwana CCM emungu nisaidie.
      Pasco and nsanu like this.

    8. Miaka 50

    9. #66
      Mbalinga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2010
      Posts : 654
      Rep Power : 594
      Likes Received
      130
      Likes Given
      0

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By Pasco
      Wanabodi,
      Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!

      Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...

      1. Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
      2. Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama ni mbali sana!.
      3. Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakuichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu!.
      4. Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa kuwa wakiichagua CCM kwa mazoea, sasa wameichoka, hivyo 2015, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
      5. Hakuna ubishi kuwa Chadema, ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kuliko CCM, hivyo ule mtaji mkubwa wa CCM iliyoutegemea kwa miaka nenda miaka rudi, sasa umehamia Chadema!.
      6. Kama ambavyo CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea tuu, na sasa CCM imechokwa, vivyo hivyo kwa sasa Chadema haina lolote la kukifanya kipendwe, bali kinapendwa kwa sababu "watu" wameichoka CCM!.
      7. Kama utaguzi utaitishwa leo, Chadema itashinda kwa kishindo kikubwa cha ajabu, lakini ukiwauliza hao watakaokipa Chadema ushindi, ni sababu zipi za kuichagua Chadema, hawatakupa sababu yoyote zaidi ya kuichagua Chadema kwa sababu wameichoka CCM!.
      8. ili Chadema iweze kupata ushindi wa Tsunami kwa uchaguzi wa 2015, lazima Chadema ikubali kubadilika, isiendelee kuutegemea huu umaarufu wa muda kwa kushangiliwa na umati wa watu walioichoka CCM, bali Chadema sasa lazima iwape Watanzania sababu za kuichagua Chadema.
      9. So far so good, Chadema is doing a good job kwa sababu M4C is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
      10. Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kubadilika kwa kuzikiliza hoja zinazotolewa kuhusu Chadema na kuzifanyia kazi!.


      Naomba kumalizia kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanachama wetu humu jf.



      Kwa wale wapenzi wa Chadema, ni vema kuwa great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best and get prepared for the worst kama Chadema haitabadilika na 2015 itakuwa ni CCM Tena!.

      NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.

      Naomba kuwasilisha.

      Pasco.



      Uko sahihi kiasi fulani lakini tathmini yako imekosa nyama za kutosha. Katika mfumo mgumu kama wetu, mfumo ulioegemea chama kimoja kwa miongo mingi huja muda kikachokwa. Lakini sikubaliani nawe kuwa wapiga kura watakaokichagua CDM hawatakuwa na sababu ya kukichagua. Wanakichagua kwa kuwa CCM imeshindwa kukidhi matarajio yao, na hapa kuna chama mbadala kinacholeta matumaini mapya. Je hiyo siyo sababu kubwa? Ndiyo vyama viko vingi na vyema sera nzuri tu, lakini watu wamekichagua CDM kuongoza ukombozi wa nchi hii, si kwa kubahatisha la hasha, isipokuwa kwa kuwa uongozi umeonyesha dira, kule ambapo watanzania wanatamni tuwe.

      Unaposema CDM kibadilike unatakiwa usifiche kitu, ama usituache hewani, kama kweli wewe ni mwenzetu sema unachoona kina shida ili kibadilishwe sio kuweka mafumbo mafumbo na kutuacha sisi tukibashiri
      Pasco and nsanu like this.

    10. #67
      JUST's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th December 2010
      Posts : 377
      Rep Power : 504
      Likes Received
      149
      Likes Given
      31

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      [QUOTE=mzeelapa;4621682]Napata tatizo moja, TANU na baadae CCM wametawala tangu 1961 kufikia mwaka 1995 alipong'atuka Nyerere. Wakati huo hawakuwepo mafisadi, wala rushwa,sijui wauwaji, mikataba mibovu and so and so....na nchi haikuendelea na tumeendelea kuwa masikini. CDM wanachoongelea ni matatizo hayo hapo juu kama kwamba yakiondolewa na umaskini utakwisha. Kwa vile siamini hilo, naomba nifahamishwe CDM itafanya nini cha ajabu hapo 2015 kama wataingia madarakani? Naona sasa haziongelewi sera bali kuondoa mambo yanayotokana na matukio yanayojitokeza...! Nipeni ushawishi niichague CDM hapo 2015. (ila sasa hivi siandamani ng'o niko kwenye kujitafutia riziki

      Watanzania tunahitaji kuelimika na sio vyeti sasa mbona majibu unayo hapo juu kwenye maandishi mekundu tena sababu nzuri kabisa
      Pasco likes this.

    11. #68
      Topical's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 1232
      Likes Received
      853
      Likes Given
      707

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Chadema ikichukua nchi nahama Tanzania naenda "Malawi"

      Subiri 2015 kilio cha mamba, wanahangaika ili wapate ku-negoatiate na ccm kabla ya 2015 maana wanajua ndio kifo chao..

      Wanataka kupata deal kama la CUF zanzibar mapema ndio maana maandamano usiku na mchana..bureeeeeeeee.
      Pasco likes this.
      "Mbowe for Presidency 2015""

    12. #69
      Ngongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th September 2008
      Location : Mlima Meru
      Posts : 4,877
      Rep Power : 1978
      Likes Received
      2357
      Likes Given
      3047

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Mwaka 2005 walikuwa wachache mwaka 2010 wakaongezeka mwaka 2015 unatarajia nini ?.

      Quote By zomba
      Kwani hao walikuwa wapi mwaka 2005 na 2010? mbona Mbowe aligaragazwa vibaya sana, uchaguzi uliofatia akaona huyu Jakaya Mrisho Kikwete si size yake akamuomba Slaa amsaidie, nae akagaragazwa vibaya sana na hao vibaraka wenu si walikuwepo au umesahau?
      Pasco likes this.

    13. #70
      Steven Robert Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2009
      Location : majita makojo
      Posts : 645
      Rep Power : 628
      Likes Received
      175
      Likes Given
      281

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      mkuu Pasco

      nimekuelewa hivi "" wanachadema pamoja na viongozi wao huu ndo wakati wa kumwaga sera za chama na kuzinadi kwa sana kadiri ya uwezo wao ili wananchi waelewe ni kwa nini muda ukifika wa uchaguzi wataamua kuichagua chadema.""" inadidi hili vuguvugu la mabadiliko liendane na kuitofautisha CCM na CHADEMA kisela na kiutendaji ili baadaye wapiga kura wote wawe wanajua kwa nini wataichagua chadema. BRAVO BRO,PASCO MKANDARA NA WENGINEO WOTE AMBAO MNAENDELEA KUFICHUA MAPUNGUFU ILI YAFANYIWE MAREKEBISHO NA HUU NDO MUDA MUAFAKA.



      SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM
      Mkandara and Pasco like this.

    14. #71
      Omuregi Wasu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st May 2009
      Posts : 527
      Rep Power : 552
      Likes Received
      63
      Likes Given
      47

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Nasikitika kuona umetumia muda wako mwingi kuandika hivi. Binafsi nimehudhuria mikutano ya Chadema. Wanaeleza sera zao na watu wanajua kwanini waichague CDM na si CCM. Binafsi najua sijui mwenzangu umeandika tu bila utafiti?
      Pasco likes this.
      Jesus is my Lord, the provider of my needs; He provides sufficient for me.

    15. #72
      Topical's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 1232
      Likes Received
      853
      Likes Given
      707

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By Ngongo
      Mwaka 2005 walikuwa wachache mwaka 2010 wakaongezeka mwaka 2015 unatarajia nini ?.
      Aisee 2015 watadondoka kwa pua..
      Pasco likes this.
      "Mbowe for Presidency 2015""

    16. #73
      Steven Robert Masatu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th August 2009
      Location : majita makojo
      Posts : 645
      Rep Power : 628
      Likes Received
      175
      Likes Given
      281

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By zomba
      Kwani hao walikuwa wapi mwaka 2005 na 2010? mbona Mbowe aligaragazwa vibaya sana, uchaguzi uliofatia akaona huyu Jakaya Mrisho Kikwete si size yake akamuomba Slaa amsaidie, nae akagaragazwa vibaya sana na hao vibaraka wenu si walikuwepo au umesahau?

      zomba, ule sio ushindi ambao jk anaweza kujivunia 60% ya kuchakachua then linganisha na idadi ya waliojiandikisha na waliopiga kura alafu angalia na population ya watanzania wote. BE ANALYTICAL!!!!!
      Pasco likes this.

    17. #74
      Shardcole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,402
      Rep Power : 1286
      Likes Received
      1032
      Likes Given
      4

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Tujirekebishe kwa nini? Hizi ni thread za kijuha na kizuzu kweli.
      Pasco likes this.

    18. #75
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,019
      Rep Power : 637
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1269

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By IBRAAH
      Usiseme sisis waislam.kwanza faham waislam wengi tupo CDM na tunamapenz nacho sasa we utanikataza mim nisipigie kura? kwanza we sio muislam dini yenyew inakataza wiz mbona ssm wanatuibia halaf nijiunge na wez? sitothubutu kuwa CCM au mwana CCM emungu nisaidie.
      Ha ha ha unanifanya nicheke, nadhani unajifurahisha sana!
      Pasco likes this.
      "If the Virgin Mary appears wearing a Veil on all her pictures, how can you ask me to sign on a HIJAB BAN law ?" -Roberto Maroni, Italian Minister.

    19. #76
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,019
      Rep Power : 637
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1269

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By Shardcole
      Tujirekebishe kwa nini? Hizi ni thread za kijuha na kizuzu kweli.
      Nimegundua humu jamvini chadema mipewa ushauri mnakuja juu, hata kama una manufaa na chama chenu kwanini? nashindwa kuelewa! ni mtu gani asotaka kushauri? hii ni ishara ya chama kibaya, mnataka kujifanya nyie kama nyerere alokataa ushauri na kujifanya kutawala kwa akili zake yeye tu ! hivi mtafika kweli?
      Pasco likes this.
      "If the Virgin Mary appears wearing a Veil on all her pictures, how can you ask me to sign on a HIJAB BAN law ?" -Roberto Maroni, Italian Minister.

    20. #77
      IBRAAH's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd August 2012
      Posts : 127
      Rep Power : 368
      Likes Received
      43
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By zomba
      Kwani hao walikuwa wapi mwaka 2005 na 2010? mbona Mbowe aligaragazwa vibaya sana, uchaguzi uliofatia akaona huyu Jakaya Mrisho Kikwete si size yake akamuomba Slaa amsaidie, nae akagaragazwa vibaya sana na hao vibaraka wenu si walikuwepo au umesahau?
      nani asie fahamu kama slaa alishinda uchaguz wa mwaka2010,ila magamba mliiba kura. kiti ni chakupokezana unataka twende kama CUF ambapo kila uchaguz lipumba na wameshamjua kama anatafuta RUZUku& kumgawia mme wake kura.
      Pasco likes this.

    21. #78
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,019
      Rep Power : 637
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1269

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By IBRAAH
      nani asie fahamu kama slaa alishinda uchaguz wa mwaka2010,ila magamba mliiba kura. kiti ni chakupokezana unataka twende kama CUF ambapo kila uchaguz lipumba na wameshamjua kama anatafuta RUZUku& kumgawia mme wake kura.
      Aaaaah! wewe umepata wapi hiyo? slaa ashinde? na ndio maana amehalalisha ndoa kujua atagombea 2015 na kwamba mnajidanganya mtashinda? ha ha ha ha mnachekesha kweli !
      Pasco likes this.
      "If the Virgin Mary appears wearing a Veil on all her pictures, how can you ask me to sign on a HIJAB BAN law ?" -Roberto Maroni, Italian Minister.

    22. #79
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,516
      Rep Power : 19751
      Likes Received
      5449
      Likes Given
      3641

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Moderators pamoja na kwamba Zomba ni Comedian wetu hapa JF kwa kutuchekesha chekesha, lakini hizi Regional & tribe hatred alizonazo nyinyi mnazifurahia? I value to differ lakini si chuki dhidi ya makabila mengine, au hapa kabila la Wakwere peke yake ndilo linalindwa?

      Nakala kwa Invisible Paw Roulette Cookie
      Pasco, Bigirita, Cookie and 2 others like this.
      Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.

    23. #80
      Topical's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2010
      Posts : 5,050
      Rep Power : 1232
      Likes Received
      853
      Likes Given
      707

      Default Re: Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

      Quote By Shardcole
      pumpikin head! Una uwezo wa kuhamia nchi gani watakayokupokea juha kama wewe mwenye mawazo ya kipunguani ya namna hii!
      Nitaenda hata somalia kusiko na serikali kama 2015 chadema watashinda?
      Pasco likes this.
      "Mbowe for Presidency 2015""

    Page 4 of 27 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...