Mtiririko wa matukio kabla polisi hawajautoa uhai wa marehemu Mwangosi (RIP)
Picha zaidi zinakuja (mtandao upo slow)
Wakuu hizi picha mkiangalia kwa makini kuna nyuso zinajitokeza. Katika picha hii ya mwisho kuna shahidi muhimu ambaye amevaa kiraia, amejitokeza kwenye picha ya sita kutoka juu. Huyu haiyumkiniki ameshuhudia mlipuko na msambaratiko wa mwili wa marehemu...
Hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe hadi ukweli uanikwe
Last edited by Msanii; 6th September 2012 at 14:44.
Ningekuwa mshauri wa WAOEM, ningeshauri waachane na mkakati wa kuwazuia CDM kuandamana na kufungua matawi, kwa kuwa kwa kutokujua, wanawaongezea sana umaarufu CDM na hasa wakati huu wa kuelekea 2015! hili liko wazi sana na nahisi CDM wanafurahi sana! huhutaji kuwa na digrii nne kama zangu kuliona hili.
Nawasilisha.
safari hii policeccm wameruka majivu wamekanyaga moto, watakiona cha mtema kuni
Wajanja sana policcm ndio maana wametaka uchunguzi ufanyike ndani ya mwezi mmoja maana ili watu watoe details zote maana wakitoa mapema picha kama hizi zitawaumbua na report yao.
mbona sasa kama idadi ya watu ilikuwa ndogo kiasi hicho kulikuwa na sababu gani za msingi polisi kutumia nguvu kubwa kiasi hicho,,, sina hakika kama hawa polisi walikuwa na akili nzuri... binafsi sioni kama hayo yalikuwa maandamano ama mkusanyiko mkubwa uliohitaji polisi kutoka morogoro, dodoma na mbeya...

Lengo ni kuua!.. Haikutegemewa mambo yatakuwa wazi kiasi hiki.. Polisi tunao mtaani siku zote!.. Wasipothamini maisha yetu, hatutathamini maisha yao!.. Aliyeuawa si CDM hivyo kila mtu yuko hatarini kuuawa!...
Damu za watu siyo mchezo, tusubiri kidogo tu wataanza kuvua nguo hadharani kwa kurukwa na akili!
Kama police wa Afande Shilogile (Morogoro) nao walishiriki kama ilivyofichuka leo, basi haya mauaji yalitegemewa kwa sababu huko Moro walikuwa wameshaonja damu ya mtu. KUMBUKA nukuu za mwalimu: "ukishaonja nyama ya mtu utaendelea kuila" .......mwisho wa kunukuu
Mtiririko wa matukio kabla polisi hawajautoa uhai wa marehemu Mwangosi (RIP)
Picha zaidi zinakuja (mtandao upo slow)
Yaani hao watu wachache ndo policcm waliita mkutano wa hadhara, kweli wana akili za mbwa maana yeye akiambiwa tu kamata anakamata tu hata kama mtu hana kosa maana mbwa hawazi, je, na polisi ni mbwa?
Hakika kusingekuwa na ushahidi wa hizi picha POLICCM wangekuja na longolongo nyingine mara ooh marehemu alipigwa na tofali mara ooh alishambuliwa na wananchi.Lakini MUNGU YU mwema amewaumbua POLICCM na unyama wao na hakika MUNGU ataendelea kuwalaani.Pumzika kwa amani Daud
Hivi wakati haya yanatokea kina Slaa walikuwa wapi? Mbona hakuna picha hata moja wanayoonekana kina Slaa?
Ina maana pamoja na kumwona mkuu wa opereshen M4C Kigaila bado huridhiki ? Slaa unamtakia nini ?Ushabiki mwingine unafaa kupeleka stendi ya bodaboda siyo hapa.
Police wali incite hizo fujo waliwachokoza ili wawadunde vizuri...hakuna sehemu picha zinaonesha dalili zozote za wanachadema waliohudhuria kuanzisha fujo...
Mkuu kuutaratibu nimesikia hawa jamaa hufanya kazi zao kwa kufuata amri waliyopewa... wako kama mashine hivi ambayo inasubiri maelekezo kutoka kwa mtumiaji... sasa hapa cha muhimu si kujua jina lake wala anaishi wapi... cha muhimu ni kujua nani alimpa amri ya kufanya hivyo kama ikidhibitika yalifanywa hivyo.......kinyume cha hayo hatutakuwa tunatatua matatizo tuliyo nayo bali tutaongeza matatizo huko mbeleni.....
Ukifanya jambo la werevu utaitwa mwerevu, ukifanya jambo la kijinga basi utaitwa mjinga pia
safari hii policeccm wameruka majivu wamekanyaga moto, watakiona cha mtema kuni
Kumbukumbu zangu zinaonesha kuwa mara zote hao policcm wanapofanya mauwaji huwa wanakuwa 'rewarded' kuliko kuwa 'purnished' kwa hiyo tutarajie watu kupandishwa vyeo kwa sababu lengo la kuwadhibiti waandishi wa habari pamoja na wapinzani litafikiwa tu kwa kuwahujumu kama hivo.
Hakika kusingekuwa na ushahidi wa hizi picha POLICCM wangekuja na longolongo nyingine mara ooh marehemu alipigwa na tofali mara ooh alishambuliwa na wananchi.Lakini MUNGU YU mwema amewaumbua POLICCM na unyama wao na hakika MUNGU ataendelea kuwalaani.Pumzika kwa amani Daud
Mkuu Nsabhi umemaliza kila kitu....huyu Mungu tunaemlilia hatatuacha kamwe.
Ina maana pamoja na kumwona mkuu wa opereshen M4C Kigaila bado huridhiki ? Slaa unamtakia nini ?Ushabiki mwingine unafaa kupeleka stendi ya bodaboda siyo hapa.
Swali ni Slaa alikuwa wapi? Yeye ndio kiongozi wa¨msafara. Linapotokea lolote kama kiongozi wa msafara anawajibika kuwepo katika jitihada za kuweka mambo sawa. Hii tabia ya Slaa kuingia mitini na kuacha wanachama wake wakivunja sheria inabidi ijadiliwe.
wakuu hizi picha mkiangalia kwa makini kuna nyuso zinajitokeza.
Katika picha hii ya mwisho kuna shahidi muhimu ambaye amevaa kiraia, amejitokeza kwenye picha ya sita kutoka juu. Huyu haiyumkiniki ameshuhudia mlipuko na msambaratiko wa mwili wa marehemu...
Hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe hadi ukweli uanikwe
huyo aliyevaa kiraia amejitokeza mara mbili akiwa na askari mmoja kwenye gari karibu na ofisi ya chadema na pale eneo la tukio! Huyu anajua kabisa huo mlipuko ulitokeaje!
Follow Us Here