JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

  Report Post
  Page 28 of 61 FirstFirst ... 182627282930 38 ... LastLast
  Results 541 to 560 of 1210
  1. #1
   n00b's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th April 2008
   Posts : 928
   Rep Power : 28531
   Likes Received
   2090
   Likes Given
   229

   Default PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   Wana JF,

   Naomba mniruhusu niweke picha zenye sura za walioshiriki kitendo hiki cha kihuni ambacho ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama kamera yangu ilivyokinasa.

   Nina picha ambazo zimechukuliwa zinazoonyesha walioshiriki na jinsi walivyoshiriki. Hata RPC alikuwepo eneo la tukio.

   Mods, naomba msiunganishe thread yangu plz.

   Picha nyingine nimezituma kwa watetezi wa haki za binadamu na video nimeziweka YouTube (sitatoa link kwa sasa).

   Wanahabari, ni wakati wa kuonyesha umoja wetu dhidi ya udhalimu huu.

   -----

   Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.   Pembeni ni shangingi la RPC, askari huyu naye kashuhudia kitendo hiki cha kikatili. Wanahabari tushirikiane kupiga kelele. Hapa walikuwa wamemaliza unyama wao wakimwondoa mwenzao aliyeumia eneo la tukio

   Maiti ilisambaratishwa kabisa utumbo, si uungwana kuweka picha kama hizo hapa.

   Kama ni kesi, askari huyu anaweza kuhojiwa. Nimekata picha kusitiri mwili wa marehemu.

   Marehemu kafa akipigania haki za wanahabari, ni wakati wa wanahabari kushirikiana vinginevyo wanasiasa wataendelea kutumia vibaya vyombo vya dola dhidi yetu.
   Last edited by n00b; 3rd September 2012 at 02:59.

  2. BHULULU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th June 2012
   Posts : 4,821
   Rep Power : 30917
   Likes Received
   1538
   Likes Given
   1254

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Hii habari imenisiktisha sana,R.I.P Mwandishi,Policcm mjue kabisa haya yana mwisho

  3. #542
   gody's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th April 2010
   Posts : 1,189
   Rep Power : 85901693
   Likes Received
   296
   Likes Given
   130

   Default

   Quote By Habarisha View Post
   Hakuwa hata na silaha ya jadi lakini ametendewa ukatili uliowahi kutokea Rwanda, Burundi na nchi ambazo damu ilimwagika.

   Hivi mnataka wafe watu wangapi ili tuseme Tanzania siyo nchi ya amani?

   Kitendo kilichofanywa na polisi Iringa kinazidi kuongeza chuki ya wananchi dhidi ya polisi.

   yaani wameshazoea kuua na wanatuona tuko kimya
   so wanafanya hivo wanajua kwani tutawafanya nini!!!!

  4. Kimbweka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th July 2009
   Posts : 8,577
   Rep Power : 7511
   Likes Received
   1574
   Likes Given
   137

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Click image for larger version. 

Name:	Daud Mwangosi kulia enzi za uhai wake.JPG 
Views:	211 
Size:	81.2 KB 
ID:	63664

   Enzi za UHAI wake akiwa kazini....
   Very sad sijui wauaji wanajisikiaje....?
   "Life comes once only: No retake/replay/rewind/once-more. One should enjoy it, be happy & keep happy others too."

  5. Mimibaba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st July 2009
   Posts : 4,579
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1267
   Likes Given
   1397

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   Quote By Pasco View Post
   Speechless!

   RIP Daudi Mwangosi!.
   Pasco pole sana la sasa utambue chama unachokitetea sana ama kimeshindwa kutawala (sikuongoza) au kinafanya matendo ambayo wengi wetu tulishayaona maika mingi kuwa si ya kiutawala au kiuongozi

  6. OLESAIDIMU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd December 2011
   Location : As per Assignment
   Posts : 19,178
   Rep Power : 429500773
   Likes Received
   9118
   Likes Given
   5643

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Quote By Kimbweka View Post
   sweetlady amekuja kanielewasha vizuri nimemuelewa....
   Wala sihitaji mabishano.....

   Haha ha ah aha I salute you........karibu kundini and enjoy the ride!!!!!!
   Where political parties exist it is important to asses the degrees in which the parties express the interests of the various classes (Karl Marx)

  7. Mangimeli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th September 2011
   Posts : 677
   Rep Power : 655
   Likes Received
   75
   Likes Given
   18

   Default

   Quote By Candid Scope View Post

   Tukio la Kuuawa Mpiganaja Daud Mwangosi Nyororo - Iringa lilivyotokea

   Tanzania tunakoelekea si kwenyewe, mambo haya sasa lazima kupeleka kwenye vyombo vya usalama na watetezi wa haki za binadamu kimataifa ieleweke hali ya Tanzania ilivyo kuliko tunavyojitokeza kifua mbele kila kukicha kwamba Tanzania tuna amani.
   1. Marehemu Daud Mwangosi anauawa huku ameshikilia video camera na namkoba wake wa vifaa vya kazi ya uanahabari.
   2. Mkuu wa Upelelezi Polisi mwenye shati la light blue na kofia nyeusi kashika pistol akiinyosha hewani.
   3. Kamanda wao mwenye kirungu akiwa katikati akitoa amri ya kuua
   4. Plisi mwenye kofia nyekundu ana pistol
   5. Aliyepewa amri ya kumwua Daud Mwangosi ameshika sila kali ya kivita ya masafa marefu kana kwamba ni kuwindana vita vya msituni.

   Napata picha kwa nini nchi nyingi na hasa zilizoendelea ni marufuku polisi kutumia silaha kali za kivita isipokuwa ni silaha za masafa mafupi ambazo ni pistol. Hapa katika tukio kuna waliokuwa na silaha za masafa mafupi ambazo ni pistol zinaonekana wazi, lakini wakaamua kutumia silaha kali ya kivita ya masafa marefu ile watumiayo vita vya nchi kavu na vya msituni.

   Kadiri ya wazoefu waliopitia hata somo la jiografia kusoma picha unaona wazi marehemu hakuna na chombo cho chote chenye kuleta madhara kwa polisi, bali ni vifaa vyake vya kazi ambavyo amekufa amevishikilia mkononi na begani ambavyo ni video camera na mkoba wa vifaa vya uandishi.

   Kwa tukio hili tunatazamia kusikia utetezi wa jeshi la polisi dhidi ya utumiaji nguvu uliokithiri, kwani morogoro wamechepusha kwa vile tukio halikuwa recorded na vyombo vya habari, lakini hili ni wazi kabisa ambapo taswira zinatoa picha kamili ya kilichojilia.
   mdau nikurkebishe kidogo apo kwenye no 5 amna silaha ya kivita iyo ni bomba la kufyatulia bomu la machozi,na uyo askari hakuwa na nia ya kmfyatulia bomu,huyo mwandishi isipokua tunaweza kusema uyo askari alijisahau akaweka kidole kwenye triger wakati usalama wa silaha ukiwa ON,hivyo basi uyo askari anapaswa kuhadhibiwa kwa kosa la uzembe kazini ndo maana akamjerui ata askari mwnzake,SOS ni mm mwenyewe nlikua eneo la tukio.

  8. neggirl's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th July 2009
   Posts : 4,767
   Rep Power : 11280
   Likes Received
   1945
   Likes Given
   2792

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   Ni nyakati za mwishooo eee Watanzania tumwombe Mungu ....

  9. MIRIJA IKATWE's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 21st October 2011
   Posts : 136
   Rep Power : 542
   Likes Received
   12
   Likes Given
   126

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   Ziweke hzo picha plzzzzzzz

   Hawa wauaji wamezidi

  10. Mu-Israeli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2012
   Location : Jerusalem
   Posts : 2,337
   Rep Power : 21245615
   Likes Received
   857
   Likes Given
   513

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Quote By Kimbweka View Post
   wewe kirundu... umekaa kaa kishabiki, kwani hapo ni vitani?....
   Hujajibu swali kwa nini CDM wanafanya maandamano bila kibali?
   Je wangekuwa na kibali haya yangetokea?
   Tunalalama baada ya kupata matokeo mabaya ya kutofuta taratibu.....Tujifunze na hili pia..... na siyo kuwa mashabiki tu...
   Kwenye red,
   Sababu ni kwamba polisi huwa wanakataa kutoa vibali vya maandamano kwa kisingizio cha kutokuwa na askari wa kutosha kulinda maandamano.

   Kwenye blue,
   Wangekuwa na kibali haya mauaji bado yangetokea. Kwasababu huyo aliyeuawa sio mwanachama wa chadema, na wala hakuwa anaandamana.
   Angalia vizuri picha utaona mwandishi aliyeuawa na polisi akiwa amezingirwa na polisi saba.
   • Jiulize bila unafiki, hao polisi saba waliomzingira mtu mmoja walishindwa kumkamata? hata wakalazimika kumuua?
   • Jiulize tena bila unafiki, kama polisi huwa wanasema hawana askari wa kutosha kulinda maandamano, hao askari saba dhidi ya mtu mmoja wametoka wapi?

   Kwa kifupi:-
   Mauaji yalipangwa, ili kuchafua jina la Chadema, kama ilivyokuwa Morogoro, na sehemu nyingine nyingi.

   Acha kutetea mauaji haya maana siku nyingine unaweza ukawa wewe au ndugu yako ndio atakaye uawa na polisi hao na polisi watasema "...umeuawa na kitu kizito kilichotupwa na waandamanaji..."
   "Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. " - Yakobo 04:17

  11. mchukiaufisadi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st January 2011
   Posts : 446
   Rep Power : 646
   Likes Received
   135
   Likes Given
   188

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Quote By Mzee Wa Rubisi View Post
   Attachment 63659Attachment 63660 Ushahidi gani waitajika kudhibitisha kuwa Polisi wameua.???//
   MUNGU Tunakuomba ushuke uone watu wako wanavyoangamia. Ulishuka Misri ukawaokoa wana wa Israel, shuka Tanzania utuokoe. Tunauwawa kama mbu mleta malaria anavyouwawa. Damu hii iwe juu yao wote waliohusika akiwemo Kiongozi mkuu wa nchi.

   Mungu shuka utuokoe.

  12. Manyanza's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 4th November 2010
   Location : Look Behind You......
   Posts : 4,446
   Rep Power : 25607
   Likes Received
   1203
   Likes Given
   933

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   mkuu asante kwa picha ingependeza ungezituma mpa BBC, Al Jazeera DW CNN ili waone jinsi polisi wa kitanzania wanavyokandamiza demokrasia

  13. Kulya's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 24th September 2011
   Posts : 337
   Rep Power : 586
   Likes Received
   122
   Likes Given
   90

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Quote By Mangimeli View Post
   mdau nikurkebishe kidogo apo kwenye no 5 amna silaha ya kivita iyo ni bomba la kufyatulia bomu la machozi,na uyo askari hakuwa na nia ya kmfyatulia bomu,huyo mwandishi isipokua tunaweza kusema uyo askari alijisahau akaweka kidole kwenye triger wakati usalama wa silaha ukiwa ON,hivyo basi uyo askari anapaswa kuhadhibiwa kwa kosa la uzembe kazini ndo maana akamjerui ata askari mwnzake,SOS ni mm mwenyewe nlikua eneo la tukio.
   Mkuu, sio kosa la uzembe kazini, thats muerder, uki-point mtu na bunduki, who is unarmed, thats contrary to the rules of engagement! And of course that suffice for Mens Rea for the offence of murder. And the Actus Reus is openly justifiable. Apelekwe Mahakama ya Kawaida na sio Martial Court.

  14. Kimbweka's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th July 2009
   Posts : 8,577
   Rep Power : 7511
   Likes Received
   1574
   Likes Given
   137

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Quote By Mu-Israeli View Post
   Kwenye red,
   Sababu ni kwamba polisi huwa wanakataa kutoa vibali vya maandamano kwa kisingizio cha kutokuwa na askari wa kutosha kulinda maandamano.

   Kwenye blue,
   Wangekuwa na kibali haya mauaji bado yangetokea. Kwasababu huyo aliyeuawa sio mwanachama wa chadema, na wala hakuwa anaandamana.
   Angalia vizuri picha utaona mwandishi aliyeuawa na polisi akiwa amezingirwa na polisi saba.
   • Jiulize bila unafiki, hao polisi saba waliomzingira mtu mmoja walishindwa kumkamata? hata wakalazimika kumuua?
   • Jiulize tena bila unafiki, kama polisi huwa wanasema hawana askari wa kutosha kulinda maandamano, hao askari saba dhidi ya mtu mmoja wametoka wapi?

   Kwa kifupi:-
   Mauaji yalipangwa, ili kuchafua jina la Chadema, kama ilivyokuwa Morogoro, na sehemu nyingine nyingi.

   Acha kutetea mauaji haya maana siku nyingine unaweza ukawa wewe au ndugu yako ndio atakaye uawa na polisi hao na polisi watasema "...umeuawa na kitu kizito kilichotupwa na waandamanaji..."
   Habari yako inakasoro soma hapa chini

   *Polisi walimpiga bomu na kumsambaratisha
   *Utumbo wazagaa, wananchi wataharuki
   *Vilio kila kona, simanzi yatawala Iringa
   MWANDISHI wa habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi, ameuawa kwa bomu. Taarifa zilizopatikana kutoka Mjini Iringa zinasema kuwa, Mwangosi aliuawa alipokuwa akipiga picha za polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mjini Mufindi jana jioni.
   Taarifa hizo zinasema kuwa, baada ya kudaiwa kupigwa bomu hilo, Mwangosi alisambaratishwa na mwili wake kuwa vipande vipande huku utumbo ukizagaa eneo la tukio. Kutokana na tukio hilo, taarifa zinasema kuwa, wananchi waliokuwa eneo la tukio walitaharuki na kuanza kulia, baada ya kutoridhishwa na jinsi alivyouawa mwandishi huyo wa habari.
   Pamoja na hayo, taarifa hizo zinasema kuwa, jana asubuhi, kabla ya polisi kuanza kudhibiti maandamano hayo, Mwangosi alikwenda kufanya mahojiano na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, ili kupata uhakika wa maandamano ya Chadema yaliyopangwa kufanyika Mjini Mufindi jana hiyo hiyo.

   Wakati akiwa katika mahojiano hayo, inasemekana kamanda huyo wa polisi alikasirika na kumtaka aeleze anauliza maswali hayo kama nani, jambo ambalo lilimfanya mwandishi huyo wa habari kuondoka ofisini kwa ofisa huyo wa polisi bila majibu ya uwepo wa mkutano huo.

   Kwa mujibu wa taarifa hizo, wakati Mwangosi akizungumza na Kamanda Kamuhanda, alikuwa na ratiba ya mikutano ya chama hicho ingawa kulikuwa na taarifa kwamba, polisi wamezuia mikutano yoyote hadi Sensa ya Watu na Makazi itakapokamilika.

   Kamanda Kamuhanda alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.

   Kuuawa kwa mwandishi huyo, ni mwendelezo wa vifo ambavyo vimekuwa vikidaiwa kusababishwa na askari polisi pindi wanapokuwa wakizuia maandamano ya wafuasi wa CHADEMA.

   Wiki iliyopita, askari polisi waliua mwananchi mmoja mkazi wa Morogoro wakati walipokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa chama hicho, waliokuwa wakitaka kuandamana.

   Pamoja na polisi kutanda kila kona ya Mji wa Morogoro, wananchi hao waliandamana hadi Viwanja vya Uwanja wa Ndege ambako viongozi wa CHADEMA walihutubia mkutano wa hadhara.

   Mwanzoni mwa mwaka jana, polisi walidaiwa kuua wananchi watatu Mjini Arusha wakati walipokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa chama hicho.

   Wakati hayo yakiendelea, jana awali Jeshi la Polisi, Mkoa wa Iringa, lilipiga marufuku mikutano ya CHADEMA, kupitia Oparesheni yao ya M4C, ili kupisha Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kukamilika Septemba 8 mwaka huu.

   Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alisema zuio hilo la mikutano ya CHADEMA, litaendelea mpaka watakapotoa maagizo mengine juu ya mikutano hiyo.

   “Ni kweli jana saa mbili tuliwapa barua ya kuruhusu shughuli zao ila baada ya kuongezwa kwa kazi ya Sensa ya Watu na Makazi nimepokea agizo la kusitisha mikutano hii.

   “Mimi ninakaribia kustaafu na kazi yangu ninaipenda, hivyo siwezi kuruhusu suala la maandamano kinyume na maagizo yaliyopo,” alisema Kamanda Kamuhanda.

   Wakati Kamanda Kamuhanda akisema hayo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Willbrod Slaa, alisema msisimko wa mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea hivi sasa nchini, hayataweza kusimamishwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi, hata kama wataamua kuwaua viongozi wote wa chama hicho.

   Dk. Slaa aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya Jeshi la Polisi kuzuia mikutano yao, huku jeshi hilo likiapa kuzuia mikutano hiyo kwa gharama yoyote.

   Katibu Mkuu huyo alisema, chama chake kilipata taarifa za kusitisha mikutano jana ambapo alilazimika kuwasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP ), Said Mwema, ili kupata ufafanuzi kutokana na kukiukwa kwa makubaliano ya awali, ambayo yaliwataka kusitisha mikutano yao kwa siku tano kisha waendelee na ratiba yao.

   “Kwa nia njema nilimpigia IGP Mwema ili kuweza kujadiliana juu ya jambo hili, lakini hakupokea simu mpaka nilipomtumia ujumbe mkali akaniambia, angepiga saa mbili usiku pia hakufanya hivyo na nilipomtafuta, alisema zuio linaendelea.

   “Nikamuuliza kama Watanzania wameelekezwa wawatafute waandikishaji wa Sensa kwa namba za simu wawe sababu ya kuzuia shughuli zetu halali, Mwema hakuwa na jibu,” alisema Dk. Slaa.

   Alisisitiza kuwa, hata baada ya kushindwa kutolea maelezo ya hoja hiyo, IGP Mwema alisema hilo ni agizo na ni lazima, litekelezwe kwa sababu ni amri iliyotolewa kisheria.

   Dk. Slaa alisema, hata alipomuuliza Mkuu huyo wa Polisi nchini ni sheria gani inayozuia hali hiyo, hakuweza kumjibu huku akisisitiza amri yake ifuatwe.

   “Sisi hatuna bunduki, hatuna mabomu wala majeshi, lakini Serikali ya CCM na Polisi wanapaswa kutambua haya tunayoyafanya ni sawa na gharika kuyazuia ni ngumu hata kama watatuuwa viongozi wote watambue mioyo ya Watanzania, itaendelea kulilia mabadiliko haya,” alisema Dk. Slaa.

   Alisema sheria ya Sensa inabainisha wazi kuwa, kama kutakuwa na zuio lolote juu ya shughuli hiyo, mhusika atahesabika kuwa ni mhalifu kazi ambayo mahakama imeshafanya kwa kuwahukumu baadhi ya watu waliochana karatasi za dodoso.

   Wakati huo huo, Mkuu wa Operesheni ya M4C Benson Kigaila alieleza kuwa, mikakati hiyo ya kuzuia mikutano ya CHADEMA ni mipango ya CCM kutokana na baadhi ya wabunge wao kuomba hilo katika Bunge lililopita.

   Alisema kwamba, Agosti 4 mwaka huu walipokuwa wakijiandaa kufanya mikutano yao katika Mkoa wa Morogoro, Jeshi la Polisi lilizusha sababu mbalimbali alizoeleza hazikuwa na msingi na kwamba, hata walipotumia busara ya kukubaliana bado waliendelea kubuni hila chafu za kuzuia.

   “Hawakutosheka na zuio la Agosti 4, wakaja na zengwe la Agosti 27 kuwa barabara ni ndogo na kwamba siku hiyo ni ya kazi, baada ya hapo wakaja na sensa, tumewasikiliza leo tena wanatuambia bado kuna zuio hili haliwezekani,” alisema Kigaila.

   Mkuu huyo wa Oparesheni alisema chama chao kilitii matakwa ya Jeshi la Polisi, kwa lengo la kuuonyesha umma ni namna gani jeshi hilo linatumika na kwamba sasa wamefika mwisho wa kusikiliza matakwa ya jeshi hilo yasiyo katika sheria.

   CHANZO: www.mtanzania.co.tz
   "Life comes once only: No retake/replay/rewind/once-more. One should enjoy it, be happy & keep happy others too."

  15. saragossa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd January 2011
   Location : Mkunazini
   Posts : 2,038
   Rep Power : 963
   Likes Received
   628
   Likes Given
   1030

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   RIP Mpiganaji.

   Najiuliza tu, ni silaha kiasi gani zinazomilikiwa na raia wa tanzania? lile zoezi la kuzisajili, kuzigonga namba na kuziingiza kwenye computer database limetoa data gani kwa jeshi la polisi? idadi? aina? hivi na raia wakiamua kutumia silaha zao kimya kimya na kusulubu askari wanaoishi uraiani, patatosha kweli?

  16. Zogwale's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th July 2008
   Posts : 10,954
   Rep Power : 201427448
   Likes Received
   3114
   Likes Given
   1323

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   Kifo hiki kina ushahidi wa kila namna kupitia still and moving pictures (video) sasa polisi watasingizia ni nani ameua? Hivi mtuhumiwa ambaye ni mwandishi wa habari anayeruhusiwa kuchukua matukio yote alikosa nini? Walimwona kabisa na camera na bag lake na baadhi ya askari watakuwa wanamfahamu sasa ilikuwaje wamuue? Ukishamkamata mhalifu kama wao polisi walimwona ni mhalifu si wangemfikisha katika vyombo vya sheria? Je mpaka wamuue kwa unyama kiasi kile huyo alikuwa na grenade la kujitetea ndipo wakaona wamuue kabla hajalilipua? So sad maana mwandishi huyu hakuwa na silaha zaidi ya vifaa vyake vya kutendea kazi. Machozi yananitoka jinsi ambavyo awamu ya nne imepoteza ile amani hayati Baba wa Taifa alituwekea kwa miaka mingi. Nchi imekuwa ya mauaji ya raia wasiokuwa na hatia kila eneo ukianzia kwenye migodi, siasa, na kila kona. Kweli majambazi watuue tena huwa wakishaiba usipowaletea vurungu wanakuacha but polisi walinzi wa raia na mali zao wanaua. CCM = Chama Cha Mauji.
   "Kama unaingia Ikulu kwa njia ya rushwa, je ni biashara gani iko huko ya kuwezesha kulipa fadhila ya rushwa hiyo???"

  17. Mu-Israeli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2012
   Location : Jerusalem
   Posts : 2,337
   Rep Power : 21245615
   Likes Received
   857
   Likes Given
   513

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Quote By Mangimeli View Post
   mdau nikurkebishe kidogo apo kwenye no 5 amna silaha ya kivita iyo ni bomba la kufyatulia bomu la machozi,na uyo askari hakuwa na nia ya kmfyatulia bomu,huyo mwandishi isipokua tunaweza kusema uyo askari alijisahau akaweka kidole kwenye triger wakati usalama wa silaha ukiwa ON,hivyo basi uyo askari anapaswa kuhadhibiwa kwa kosa la uzembe kazini ndo maana akamjerui ata askari mwnzake,SOS ni mm mwenyewe nlikua eneo la tukio.

   Hapo kwenye red,
   Unaandika kama vile wewe ndio huyo askari mwenyewe aliyefyatua bomu la kumuua mwandishi, maana kama vile ulikuwa 'live' ndani ya mawazo na akili za huyo askari wakati wa tukio lenyewe !!!

   Hapo kwenye blue,
   Haraka sana, wewe umeshafanya uchunguzi, umeshapata majibu ya uchunguzi kuwa askari aliua kwa bahati mbaya, na wewe huyo huyo, umeshatua mapendekezo ya hukumu na adhabu inayofaa kupewa muuaji huyo !!!

   Kazi tunayo !!!
   "Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. " - Yakobo 04:17

  18. mchukiaufisadi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st January 2011
   Posts : 446
   Rep Power : 646
   Likes Received
   135
   Likes Given
   188

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Mlioko Iringa, tuwekeeni picha ya huyu muuaji, jina lake, na lolote mnalolifahamu ili tuliweke mbele za Mungu ili Mungu amuhukumu ndani 24 hours kama Haman.

  19. kaangwa's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 30th January 2011
   Posts : 647
   Rep Power : 681
   Likes Received
   181
   Likes Given
   90

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   Quote By kichwat View Post
   wapi picha sasa?
   kama hujaona picha basi macho yako yana walakini,kwa ushauri uende ccbrt ufanyiwe uchunguzi wa akili na macho.

  20. Mu-Israeli's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2012
   Location : Jerusalem
   Posts : 2,337
   Rep Power : 21245615
   Likes Received
   857
   Likes Given
   513

   Default Re: Kuuawa Mwangosi Nyororo Iringa, polisi watakwepaje ushahidi huu?

   Quote By Kimbweka View Post
   Habari yako inakasoro soma hapa chini

   *Polisi walimpiga bomu na kumsambaratisha
   *Utumbo wazagaa, wananchi wataharuki
   *Vilio kila kona, simanzi yatawala Iringa
   MWANDISHI wa habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi, ameuawa kwa bomu. Taarifa zilizopatikana kutoka Mjini Iringa zinasema kuwa, Mwangosi aliuawa alipokuwa akipiga picha za polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano ya wafuasi wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mjini Mufindi jana jioni.
   .
   .
   .
   Wakati hayo yakiendelea, jana awali Jeshi la Polisi, Mkoa wa Iringa, lilipiga marufuku mikutano ya CHADEMA, kupitia Oparesheni yao ya M4C, ili kupisha Sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kukamilika Septemba 8 mwaka huu.

   Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, alisema zuio hilo la mikutano ya CHADEMA, litaendelea mpaka watakapotoa maagizo mengine juu ya mikutano hiyo.

   “Ni kweli jana saa mbili tuliwapa barua ya kuruhusu shughuli zao ila baada ya kuongezwa kwa kazi ya Sensa ya Watu na Makazi nimepokea agizo la kusitisha mikutano hii.

   Mimi ninakaribia kustaafu na kazi yangu ninaipenda, hivyo siwezi kuruhusu suala la maandamano kinyume na maagizo yaliyopo,” alisema Kamanda Kamuhanda.
   .
   .
   CHANZO: www.mtanzania.co.tz
   Hapo kwenye red,
   Bado tu hupati picha ??
   Mikutano iliyozuiliwa ni ya Chadema tu !! Upo hapo ?? au na wewe umenukuu habari hii kwa makosa ??
   Jamaa karibu anastaafu, hawezi kuruhusu maandamano kinyume cha "maagizo" yaliyopo !! Maagizo gani ?? Au sensa inawagusa Chadema peke yao ??
   Upo hapo ???
   "Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi. " - Yakobo 04:17

  21. Professa's Avatar
   Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Posts : 14
   Rep Power : 493
   Likes Received
   2
   Likes Given
   34

   Default re: PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

   Kwa matendo yao machafu, Serikali imelifungia mwanahalisi. Bahati mbaya imesahau kuna jamii forums. RIP kamanda Mwangosi, ndugu zake poleni sana.

  Page 28 of 61 FirstFirst ... 182627282930 38 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Waziri wa CUF Zanzibar abariki upigwaji mwandishi wa Channel ten
   By muhogomchungu in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 20
   Last Post: 28th January 2011, 13:13

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...