Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

    Report Post
    Results 1 to 7 of 7
    1. #1
      sir.JAPHET's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Posts : 611
      Rep Power : 479
      Likes Received
      90
      Likes Given
      45

      Default Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

      Monday, 27 August 2012 | Ibrahim Yamola

      SERIKALI inazifanyika kazi tuhuma 175 za kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zinazowahusu baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo na Wizara ya Nishati na Madini.

      Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema juzi Dar es Salaam kwamba tuhuma hizo ni zile zilizotolewa katika mkutano wa viongozi wa wizara hiyo na wafanyakazi wa Tanesco Mei 19, mwaka huu.

      Maswi alisema katika tuhuma hizo zipo ambazo ni za ndani hivyo zinafanyiwa uchunguzi wa kina kabla ya kuchukua hatua.

      “Watu wasiwe na wasiwasi juu ya kinachoendelea, lakini tunawaahidi kuwa watulie na kuna mambo mazuri yanakuja baada ya kumaliza kuzifanyia kazi,” alisema Maswi na kuongeza: “Kuna vitu ambavyo vinaendelea ndani ya Tanesco ambavyo vinatakiwa kufanywa kwa uangalifu ili kuhakikisha hadhi ya shirika hilo inarejea.”

      Katika mkutano huo wa Mei, wafanyakazi wa Tanesco walimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo majina ya vigogo wa wizara yake wanaodaiwa kulihujumu shirika hilo.

      Tukio hilo lilitokea wakati waziri huyo akiwa na manaibu wake, George Simbachawene na Steven Masele pamoja na Maswi, walipozungumza na wafanyakazi wa Tanesco Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

      Agizo la kukusanya majina hayo lilitolewa na Maswi muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya Shirika hilo, Abdul Mkama kutoa taarifa kwa niaba ya wafanyakazi iliyoeleza kuwa kuna vigogo katika wizara hiyo na wafanyakazi wengine wa Tanesco, wanaojihusisha na vitendo vya hujuma.

      Katika mkutano huo, Mkama alisema Kamati yake ya Majadiliano inawafahamu kwa majina vigogo wa wizara hiyo wanaojihusisha na njama za kulihujumu shirika hilo kwa lengo la kuingiza wawekezaji wanaowataka katika sekta hiyo.

      Miezi miwili baada ya tuhuma hizo, Bodi ya Tanesco ilimsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi William Mhando pamoja na watendaji wakuu wengine wa Tanesco ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

      Nafasi ya Mhando imechukuliwa na Felchem Mramba ambaye alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko na Usambazaji wa Tanesco.

      Viongozi wengine wa Tanesco waliosimamishwa kazi ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma za Shirika, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi, Harun Mattambo.


    2. #2
      Kagalala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Posts : 1,321
      Rep Power : 702
      Likes Received
      398
      Likes Given
      157

      Default re: Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

      Tunasubili matokeo ndo muhimu zaidi
      Our biggest Enemy is not to try what others have done.

    3. #3
      congobe's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st May 2012
      Posts : 126
      Rep Power : 380
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default re: Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

      hakuna lolote zaidi ya siasa tu hapa

    4. #4
      Tutafika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2009
      Posts : 756
      Rep Power : 641
      Likes Received
      234
      Likes Given
      175

      Default Re: Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

      Katibu mkuu anatakiwa kuchapa kazi sio kuchapa domo! kazi hiyo amwachie Nape na Mnyika.

    5. #5
      CHOMA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd August 2012
      Posts : 108
      Rep Power : 754
      Likes Received
      9
      Likes Given
      3

      Default Re: Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

      Ni mapema mno kusema lolote.Kuchunguza tuhuma na kuzithibitisha kisha kuzifanyia kazi ni mazoezi yanayohitaji umakini mkubwa.Tunasubiri tuone kitakachoendelea.


    6. #6
      babykailama's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th March 2012
      Posts : 226
      Rep Power : 413
      Likes Received
      227
      Likes Given
      77

      Default Re: Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

      Wahusika wafikishwe mara moja kwenye vyombo vya sheria bila kuoneana aibu.
      Pa shoka hapaingii kisu

    7. #7
      Mzee wa Usafi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th April 2008
      Posts : 248
      Rep Power : 620
      Likes Received
      53
      Likes Given
      0

      Default Re: Serikali yachunguza tuhuma 175 TANESCO

      Nadhani sasa Maswi amekutana na Prof.Muhongo, wote ni wapenda misifa bila kutumia busara. Si Prof.Muhongo (a.k.a Mzee wa Gondwana) sio mchapa kazi la hasha bali ni kile kielement cha kupenda sifa ndo huwa kina mharibia....Sasa Maswi naye achape kazi kama mtendaji wa serikali na kufuata kanuni, taratibu na sheria za kazi kwa watumishi wa umma.

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...