Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Lowassa: Mkapa alikuza uchumi, JK punguza matumizi

    Report Post
    Page 2 of 15 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 281
    1. #1
      Zipuwawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2010
      Posts : 2,206
      Rep Power : 875
      Likes Received
      310
      Likes Given
      123

      Default Mh. Edward Lowassa Leo..........

      Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama Mh. Edward Lowassa atazungumzia mgogoro wa Malawi kuhusu ziwa nyasa na pia ugawaji vitalu migodini Katika Kipindi cha SAA 3.00: DAKIKA 45 Kupitia Runinga ya ITV.

      Najiuliza maswali alistaili kuongelea haya? Mbona Bungeni huwa mkimya sana? Je Jimbo lake halina matatizo? Ungependa aulizwe maswali gani?
      Quote By Njoka Ereguu View Post
      21 August 2012 | Gazeti la Mwananchi

      WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ameitaka Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kupunguza matumizi na kufanya uamuzi wa kukuza uchumi kama ilivyokuwa wakati wa mtangulizi wake, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

      Lowassa alisema, Mkapa alifanya uamuzi mgumu kiuchumi uliowezesha nchi kupiga hatua zaidi kimaendeleo ikilinganishwa na sasa ambapo taifa limekumbwa na mfumuko mkubwa wa bei.

      “Serikali ipunguze matumizi ili kupunguza Inflation (mfumuko wa bei) kwani ni tatizo kubwa,” alisema Lowassa katika kipindi cha dakika 45 kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV juzi usiku na kuongeza:

      “Rais Mkapa wakati wake alifanya maamuzi mengi ya uchumi, lakini pamoja na wakati wake watu kuuita ukapa, bado alifanya maamuzi mazuri na uchumi ukaenda juu.”

      Lowassa alimsifu Mkapa akisema, alifanya uamuzi mgumu wenye lengo la kukuza uchumi na kuyasimamia jambo ambalo linapaswa kuwa mfano kwa Serikali zingine.

      “Tusikubali hivyo, tufanye maamuzi ya msingi na tuyaeleze hivyo… Rais Mkapa wakati wake alifanya maamuzi ya kiuchumi akayasimamia, sasa tufanye maamuzi ya namna hiyo na kuyasimamia," alisema Lowassa na kuendelea:

      “Mfumuko (wa bei) umefikia asilimia 17.9. Imekuwa hivyo kwa muda mrefu. Wakati wa Rais Mkapa ulishuka zaidi.”

      Alisema Serikali ya Rais Kikwete imefanya mambo makubwa, lakini inatakiwa kubana matumizi ili ukuaji wa uchumi umnufaishe mwananchi wa kawaida.

      Lowassa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alisema ili ukuaji wa uchumi umnufaishe mwananchi wa kawaida, lazima mambo matano yafanyike. Alitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na usalama wa chakula, upatikanaji wa mafuta na kilimo cha mashamba makubwa.

      “Lakini la muhimu zaidi ni Serikali kupunguza matumizi. Lazima Serikali ipunguze matumizi ili kupunguza ‘inflation’ (mfumuko wa bei) lazima kupunguza matumizi, lazima sana,” alisisitiza Lowassa.

      Kuhusu usalama wa chakula, Lowassa alitaka wakulima waruhusiwe kuuza mazao yao nje ya nchi bila bughudha.

      “Kuna maeneo ambayo nadhani hatujayafanyia kazi, moja ni ‘Food Security’ (usalama wa chakula). Tuangalie uwezekano wa kuongeza hizo barabara zitumike kuwasaidia wakulima,” alisema na kuongeza:

      “Kwa mfano wanalima mazao yao Rukwa, tusiwalazimishe kuyauza Arusha kwa sababu gharama za kuyatoa mahindi kutoka Rukwa hadi Arusha ni kubwa mno…Anayetaka kuuza Kenya auze, anayetaka kwenda Burundi ayapeleke. Wakulima wapate nafasi ya kuuza mazao yao kwa uhuru kwa haraka na kwa bei nzuri, hilo ni muhimu sana,” alisema Lowassa.

      Kuhusu suala la mafuta alisema ,aliishauri Serikali kununua mafuta kwa wingi wakati wa bei ni nzuri.

      Aliitaka Serikali kuchukua uamuzi mgumu katika kuimarisha kilimo cha mashamba makubwa na matumizi ya zana za kilimo za kisasa hasa matrekta.

      “Trekta ni muhimu sana… Serikali inajitahidi, imeleta matreka mengi ya kutosha… tuongeze mengine, tuondoke kwenye jembe la mkono,..haliwezi kututoa kwenye umaskini,”alisema Lowassa na kuongeza:

      “Hata wakati wa Nabii Bwana Yesu, watu walishahama kwenye jembe la mkono… unakumbuka ile habari ya mtu aliyealikwa kwenye sherehe akasema ‘mimi nimenunua jozi ya ngombe nakwenda kulijaribu’ walikuwa wameshahama, sisi mpaka leo tuko na jembe la mkono, haiwezekani.”

      Kauli hiyo ya Lowassa imekuja wakati kukiwa na malalamiko kutoka kwa wananchi na wadau wa siasa kuitaka Serikali ipunguze matumizi hasa katika ununuzi wa magari ya kifahari na safari za ndani na nje za viongozi wa Serikali
      Pasco likes this.
      Maisha yetu ni mafupi lazima tuyatete kwa namna yeyote ile!


    2. #21
      ALEYN's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,065
      Rep Power : 597
      Likes Received
      134
      Likes Given
      17

      Default

      Quote By sir.JAPHET View Post
      Nasubiri kumuona,, akiongea pumba naendelea kujiandalizia man untd live van prsie
      msubiri Jk aje kutoa tamko.

    3. #22
      Marire's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 2,370
      Rep Power : 992
      Likes Received
      636
      Likes Given
      0

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Kipindi ni rekoded nikiuliza swali hapa atalijibuje?

      Haya swali,anatoa maoni gani kufiatia taarifa ya watz walioficha fedha uswis?

    4. #23
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Quote By idawa View Post
      hivi hiki kipindi kinakuwaga live au kinakua kimesherodiwa.!
      recorded n edited

    5. #24
      Seif al Islam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2011
      Posts : 1,165
      Rep Power : 560
      Likes Received
      271
      Likes Given
      425

      Default Re: Mh. Edward Lowassa Leo..........

      haya baadaye kidogo atakuja membe hapo kusawazisha

    6. #25
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      ana maoni gani juu ya gharama za UMEME?


    7. #26
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2888
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default Re: Mh. Edward Lowassa Leo..........

      Quote By Seif al Islam View Post
      haya baadaye kidogo atakuja membe hapo kusawazisha
      then KIKWETE kupitia wazee wa MUSOMA

    8. #27
      Kibanga Ampiga Mkoloni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th August 2007
      Location : Here! here!
      Posts : 5,127
      Rep Power : 1785
      Likes Received
      1275
      Likes Given
      1710

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Naona huwa napita humu na kusoma,
      HONGERA LOWASSA KWA KUDESA, Sasa Sijuhi kama ume ACKNOWLEDGE SOURCE:


      MBONA WANAUZA KILA KITU: 4th Tanzania Offshore Licensing Round
      For the Holy Quran says in Sura 42, verse 41: 'All those who fight when oppressed incur no guilt, but Allah shall punish the oppressor, Come the day.

    9. #28
      Lambardi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th February 2008
      Location : KITAANI ZAIDI
      Posts : 4,588
      Rep Power : 1813
      Likes Received
      666
      Likes Given
      0

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Bado hajaanza kuongea

    10. #29
      Hobic11ac's Avatar
      Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 29
      Rep Power : 368
      Likes Received
      7
      Likes Given
      0

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Tatizo litakuwa kwa Semunyu maana EL atamubuliza na siku zote jamaa huwa na atekwa mawazo na wageni wake studio.

      Muda mwingine anakoswa hata swali la maana ama anabaki kurudia rudia yaliyosemwa na mgeni wake;

    11. #30
      chizi1's Avatar
      Member Array
      Join Date : 16th December 2011
      Location : dar es salaam tanzania
      Posts : 78
      Rep Power : 394
      Likes Received
      23
      Likes Given
      1

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      mi naomba ndugu zangu, niko mbali.. mtakao angalia, mtuelezee ni nini ataongelea then ndo nitatoa maoni
      A great person attracts great people and knows how to hold them together.


    12. #31
      Kongosho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Location : Location loading...
      Posts : 26,173
      Rep Power : 25450
      Likes Received
      14879
      Likes Given
      15834

      Default Lowasa ITV

      Hebu tizameni ITV sasa Lowasa anahojiwa.

      Kasema afya yake iko safi kabisa ila watu wanatunga habari, anachoumwa yeye ni jicho.

      Pia kaongelea kuhusu kauli ya kutangaza vita, kakana kasema wamamnukuu si sawa.

      Sasa anaongelea mgogoro na Malawi kwa ujumla.

    13. #32
      Ally Kanah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Posts : 816
      Rep Power : 570
      Likes Received
      40
      Likes Given
      37

      Default Lowasa ITV

      Tupe update mkuu... Huyo ndio Rais wetu mtarajiwa
      WEKENI AKIBA YA MANENO by ZZK

    14. #33
      Emeka Anyaoku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Posts : 436
      Rep Power : 448
      Likes Received
      134
      Likes Given
      0

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Mi cpo mbali na tv ila cmuhitaji mtu huyu 4ril

    15. #34
      Ally Kanah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Posts : 816
      Rep Power : 570
      Likes Received
      40
      Likes Given
      37

      Default Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Quote By usungilo View Post
      zimerudi thread za huyu jamaa. Urais unatafutwa hata kwa damu.
      Huyo ndiyo Rais wetu na Inshaalah Allah atamuongoza vyema kuwa Rais wa JMT
      WEKENI AKIBA YA MANENO by ZZK

    16. JBK is offline
      JBK
      #35
      JBK's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th August 2012
      Posts : 44
      Rep Power : 352
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default lowasa awashangaa waandishi wa habari

      awashangaa kwa kupotosha ukweli hakana si kweli alitangaza vita bali kama mwenyekiti wa kamati aliunga mkono mapendekezo ya selikari

    17. #36
      Zogwale's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 10th July 2008
      Posts : 6,133
      Rep Power : 6511
      Likes Received
      1253
      Likes Given
      538

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Du sijafika home. Nasikitika kuikosa hii Tanziwood movie!!!
      "Kama unaingia Ikulu kwa njia ya rushwa, je ni biashara gani iko huko ya kuwezesha kulipa fadhila ya rushwa hiyo???"

    18. #37
      kingxvi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2011
      Posts : 883
      Rep Power : 599
      Likes Received
      134
      Likes Given
      1

      Default Re: lowasa awashangaa waandishi wa habari

      mwandishi kasoma chuo cha kimjini mjini unategemea nini

    19. #38
      Ally Kanah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th June 2011
      Posts : 816
      Rep Power : 570
      Likes Received
      40
      Likes Given
      37

      Default Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Quote By Bajabiri View Post
      then KIKWETE kupitia wazee wa MUSOMA
      Baadae sana Slaa kupitia Wazee wa Kanisa
      WEKENI AKIBA YA MANENO by ZZK

    20. #39
      OTIS's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2011
      Posts : 1,918
      Rep Power : 777
      Likes Received
      477
      Likes Given
      202

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      lowassa anapapatika tu.naona lile tamko lake la vita linamuandama na limemkalia vibaya.
      Jitihada za kujisafisha naona zimegonga mwamba.
      Mbaya zaidi hali ya afya bado inatia shaka.

    21. #40
      platozoom's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 4,088
      Rep Power : 8295
      Likes Received
      2775
      Likes Given
      3797

      Default Re: Lowassa ndani ya dakika 45 za ITV

      Anaunga mkono kauli ya serikali kuhusu suala la Malawi na kwamba magazeti yalipotosha kwamba yeye ametoa kauli kama amiri jeshi mkuu

      Amezungumzia pia afya yake na kusema yuko fiti kwa hali yeyote ile na kwamba ni upotoshaji kusema ana stroke...kwamba hizo ni siasa za watu na malengo yao
      "Education is something that remain in your head after forgeting what you learn at school"

    Page 2 of 15 FirstFirst 123412 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...