Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

    Report Post
    Page 8 of 8 FirstFirst ... 678
    Results 141 to 154 of 154
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6152
      Likes Given
      22273

      Default PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Wanabodi,

      Kila nipatapo fursa, sipendi kabisa kukosa kipindi cha Maswali na Majibu ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza, Peter Pinda, ile leo nilikikosa kipindi hiki.

      Lakini kupitia taarifa za habari, nimemsikia Mhe. Pinda, akisema kuwa ni jukumu la wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili CCM iendelee kutawala milele!.

      Naombeni wajuzi wa masuala ya utawala, mnirekebishe if I'm wrong!, Kuanzia kwa rais JK na wanasiasa wengine wote ambao japo wamechaguliwa kwa tiketi za vyama, ukishakuwa mtumishi wa umma, paid by taxpayers money, jukumu lako kuu sasa ni kuutumikia umma na sio chama chako!.

      Hii inamaanisha rais JK, japo ameshinda kwa tiketi ya CCM, na anaongoza serikali ya Tanzania, na wakati huo huo yeye ndiye Mwenyekiti wa CCM, amechaguliwa kuiongoza Tanzania na Watanzania na sio na wana CCM, hivyo anaongoza serikali ya Tanzania kwa niaba ya Watanzania na kwa manufaa ya Watanzania wote, na sio kwa manufaa ya wana CCM!. (Of the people, by the people and for the people).

      JK ndiye rais wa Chadema, ndiye rais wa CUF na ndiye rais wa wasio na vyama kama sisi!. Yeye ndiye rais wa Dr. Slaa, yeye ndiye rais wa Prof. Lipumba, yeye ndiye rais wetu sisi wote kama Watanzania, ni rais wa waliomchagua na pia rais wa wasiomchagua, anatakiwa kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya chama chake cha CCM!.

      Kauli ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda bungeni leo kuwa Wakuu wa wilaya na mikoa, wako pale kuhakikishe CCM inashinda chaguzi zote ili itawale milele, haiwezi kupita bila kupingwa!. Hi inamaanisha kuwa viongozi hawa, wako kwa ajili ya kuilinda na kuitetea status quo ya CCM ili iendelee kutawala milele!. This is very wrong kwa tafsiri sahihi ya Public Servants!. Kwa kauli hii ya Pinda, it goes without saying kuwa wakuu wa majeshi yetu, Polisi wetu, mahakama zetu na wakuu na vyombo vya dola, na vyombo vya kiserikali, wanateuliwa ili wahakikishe CCM haishindwi na inaendelea kutawala milele!.

      Public Servant, ni mtumishi wa umma, ma RC na ma DC ni viongozi wa serikali, kwa maana hiyo ni viongozi wa umma, na watatimiza majukumu yao kwa maslahi ya umma na sio kwa maslahi ya CCM. Ndio maana Mhe. Tundu lissu aliwakataa hawa wasihusishwe ile tume ya katiba na juzi akasisitizwa hawapaswi kuwamo bungeni!.

      Hata wabunge wa kuchaguliwa, ni watumishi wa umma, japo wanateuliwa kwa tiketi za vyama vya siasa, wanachaguliwa na wananchi na sio na vyama vyao, hivyo wakishashinda ubunge, wanakuwa ni watumishi wa watu na sio watumishi wa vyama vyao, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao ya kibunge kwa maslahi ya wananchi na sio kwa maslahi ya vyama vyao!. Kama ni kweli, majukumu ya ma RC na ma DC ni kuhakikisha CCM haishindwi, hii ina maana kubwa zaidi katika mustakabali wa mabadiliko halali ya serikali!.

      Binafsi yangu, nimesikitishwa na kauli hiyo, and to be honest, nilikuwa na very high hopes kuhusu Pinda, lakini sasa nimeamini, he is good for nothing!, a very disapointing PM!. Kwa vile CCM ni chama tawala, hivyo public servants wana jukumu la kuhakikisha CCM inashinda na kutawala milele!.

      Hii inamaanisha hata kama 2015, Watanzania wataamua kuivote out CCM kupitia njia halali ya ballot box, hao public servanys wenye jukumu la kuitumia serikali mpya ya chama kitakachoshinda, wako kwenye mind set ya kuhakikisha lazima CCM inashinda, na jee ikitokea CCM ikashindwa, jee watakabidhi madaraka kwa mshindi halali?!, jee majukumu yao yatabadilika or what does Pinda exactly meant?!.

      Kusema ukweli, civic education kuhusu multipartism, inatakiwa kuanzia juu ndipo ishuke chini kwa wananchi wa kawaida!.

      Sasa ndio nimeanza kuelewa, no wonder kwa nini jina la Pinda, halitajwi kabisa kabisa katika presidential materials!. Maliza tuu term yako kwa amani, ukaiendeleza ile kampuni yako ya P & P, nami nitakutangazia sana ile asali yako, ila nakuomba Tanzania yetu utuachie kwa amani, hii sio Tanzania ya CCM, CHADEMA au CUF!. Tanzania ni ya Watanzania wote.

      Kiukweli, mabadiliko yakija, hizi nafasi za ma DC na ma RC ndizo ziwe za kwanza kufutiliwa mbali!.

      Very Disapointed!.

      Pasco.

      NB. Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mshabiki wa Utanzania kwa maslahi ya Taifa mbele!.

      Last edited by Pasco; 17th August 2012 at 12:17.

    2. Miaka 50

    3. #141
      jmushi1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2007
      Posts : 14,376
      Rep Power : 16492
      Likes Received
      4299
      Likes Given
      5491

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Mnazungusha maneno tu...jukumu la kwanza la mwanaccm ni nini? Soma ibara ya 15:1 ya katiba ya katiba ya CCM kuweza kupata majibu.
      Hivi jukumu kwanza la mwana ccm ni kulinda maslahi ya Taifa?this stuff is abit confusing to me.Hivi tuna uhakika kuwa maslahi ya ccm haya "trump" ama kuwa juu ya maslahi ya taifa?

      What's the distinction kati ya maslahi ya ccm vs yale ya taifa?

      Kwaninavyofahamu,maslahi ya taifa yanasimamiwa na chama kilichoshinda uchaguzi kwa mujibu wa katiba.Lakini hatuna mechanism ya check and balances kuhakikisha kuwa democracy haiwi jeopordized.Na kwamba constitution of the land is been upheld.Katiba yetu haiendani na mfumo tulionao.So this is one of the issue to give it a look while preping for the new constitution.

      Kinachotakiwa kuwahakikishia viongozi wa ccm kurudi madarakani ni utumishi wao kwa wananchi na kama wanatimiza ahadi wanazozitoa.Pinda alitakiwa kusema accomplishments zao ndizo zitakazowahakikishia kurudishwa madarakani na wananchi na si kuwatumia viongozi hao kuwagawa wananchi ili tu ccm ishinde.Ni kinyume cha katiba kupanda chuki zenye kuhatarisha usalama wa wananchi na taifa.Ni kinyume cha katiba ya nchi kuwakandamiza na kuwanyanyasa wananchi kwasababu ya tofauti za kiitikadi.Ndo maana chama kikiondoka madarakani bado kinaweza kuburuzwa kwenye mkono wa sheria na wananchi kama waliona wameimissuse katiba ya nchi na kuyatumia madaraka na dhamana waliyopewa kinyume na katiba ya nchi,haitajalisha katiba ya ccm inasema nini,its time we become a nation of "constitutional law".
      "One of the penalties for refusing to participate in politics is that you end up being governed by your inferiors"-Plato

    4. #142
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Hao wananchi atawatumikia kwa sera za chama kipi?
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    5. #143
      makundi4619's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2012
      Posts : 485
      Rep Power : 442
      Likes Received
      135
      Likes Given
      388

      Angry Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Mungu anawaanika wana CCM mchana kweupe. Wamelewa madaraka hata haelewi alama za nyakati na kubadilika. Kuropoka kwao kunazidi kuwadhalilisha bila wao kujijua. Kauli kama hizi zinatia wananchi hasira sana. Sasa mwisho wake ni nini? Such statements will only insight anger and raise awesome awareness of the oppressed thus developing efective strategies on how to deal with CCM during the coming elections. The ballot box will speak siyo hawa watu wa hila na ghiliba!!!!

    6. #144
      TEMILUGODA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2012
      Posts : 954
      Rep Power : 557
      Likes Received
      134
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By chama
      Pasco, Kizotaka;
      Nimesema kauli ina unatata hapo inamaanisha sikubaliani moja kwa moja na kauli ya waziri mkuu; nimeongezea serikali ni ya CCM sera zinazofanya kazi ni za CCM; sasa tatizo lipo wapi au ni kitu gani ambacho hakieleweki? mkuu Pasco tuwekee hiyo hotuba nzima kwa sababu siku kuna matatizo ya kunukuu nina uhakika maneno ya waziri ya waziri mkuu hayakuishia hapo tuwekee clip nzima tuisikilize hapo ndipo tutakuwa na mjadala mzuri; inawezekana umenukuu kile unachotaka tusikie, hoja kimarekani sio nyepesi wateule wa raisi wanatekeleza sera za raisi aliyewateua na raisi anatelekeza sera za chama chake; sasa itakuwa ajabu sana kwa wakuu wa wilaya kutekeleza sera za chadema; si unakumbuka yule mkuu wa wilaya Mbeya kama sikosei alikuwa Rungwe alijaribu kuleta sera za Chadema wakati ni mteule wa CCM matokeo yake alijichanganya mwenyewe.

      Chama
      Gongo la mboto DSM- in vacation Puerto Vallarta
      Sina mengi ya kuongeza,ila nasema hivi kati ya ma PM tuliowahi kuwapata MKPP NI BOGUS KULIKO.

    7. #145
      Raia Fulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2009
      Posts : 9,252
      Rep Power : 2622
      Likes Received
      1291
      Likes Given
      834

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Hata mi ile kauli ilinichefua. Katika bunge hili nimemwona huyu mzee akiwa na hasira zaidi na wapinzani kuliko wanaochafua nchi kwa ufisadi. Ni wazi kuwa ccm hawana tena nia nzuri na ustawi wa nchi hii kwa kuwa wako radhi kwa lolote litakalowaahidi kushika Dola. Ni macho na masikio yetu tu hapo 2015

    8. FemaTV & Radio

    9. #146
      vipik2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2011
      Posts : 368
      Rep Power : 451
      Likes Received
      80
      Likes Given
      74

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By Raia Fulani
      Hata mi ile kauli ilinichefua. Katika bunge hili nimemwona huyu mzee akiwa na hasira zaidi na wapinzani kuliko wanaochafua nchi kwa ufisadi. Ni wazi kuwa ccm hawana tena nia nzuri na ustawi wa nchi hii kwa kuwa wako radhi kwa lolote litakalowaahidi kushika Dola. Ni macho na masikio yetu tu hapo 2015
      Nani anaamini kuwa CCM itaachia madaraka pale itakaposhindwa uchaguzi? Kauli hiyo ya pinda inatoa ujumbe mahususi kuwa tujipange kiaina kuweza kuwatoa madarakani na sio kutegemea sanduku la kura, Hivi kitendo walichomfanyia
      Dr Ulimboka mnafikiri kilikuwa bahati mbaya au hakina uhusiano na long plan zao za kutawala milele? Chadema inavyozunguka inchi nzima mnafikiri CCM inapenda? Rejea kauli ya Nape kuhusu michango ya hisani toka kwa mzee Sabodo au kauli ya Nape huyo huyo juzi alipotamka kuwa Chadema inapata michango toka kwa wahisani nje ya inchi, Hawa CCM sasa wamechanganyikiwa vibaya na wakati huo huo wanaona dalili zote za kuporomoka

      Huyu mzee Pinda kama Pinda achaneni nae na tuendelee kuufumua utawala dhalimu kwa mbinu zozote zile tunazoona zinafaa, Pinda tayari Mungu anampa dozi ndogondogo kama tulivyosikia fuso lilivyowanyonga ndugu zake huko Rukwa
      Tunasikitika kutangaza kifo cha ndugu CCM, Mazishi yatakuwa 2015 na habari ziwafikie ndugu wote mafisadi na shost wake CUF

    10. #147
      Same ORG's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 10th June 2012
      Location : Dubai
      Posts : 323
      Rep Power : 0
      Likes Received
      19
      Likes Given
      2

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Nakumbuka "Zanzibar si nchi" alipotamka hili waznz waliumia sana na mpk leo kidonda hiki hakijapoa, ulikua ndio mwanzo wa kuamshwa waznz. Ila tumpongeze huyu PM kwa kusema ukweli ambao na sasa unawaamsha hata watanganyika walokua hawajui siasa. Kutamka wakuu wa mikoa/wilaya wanafanya kazi za chama ni sahihi kabila na wala hajababaika kama mkuu wa nchi alozoea kuwatia watu changa la macho.. Hapa sasa ndio na nyinyi watanganyika munaamshwa mumezoe kulala baa sana hamjui mnalolifanya.

    11. #148
      mwangalizi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th April 2012
      Posts : 87
      Rep Power : 374
      Likes Received
      10
      Likes Given
      4

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      So what??!!

    12. #149
      manucho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Posts : 561
      Rep Power : 469
      Likes Received
      79
      Likes Given
      0

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Kama alivyo J.K hata Pinda ni chaguo la Mungu. Uzao wa 4 ni wa mabadiliko.

      Hawa watu wawili na viongozi wengine ktk chama chao wanaleta mabadiliko makubwa sana. Pinda anaongea ukweli mtupu ila hajijui wala hajitambui na wengine wanaongea tena lugha moja lkn hawaelewani

    13. #150
      kdany's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th July 2012
      Posts : 90
      Rep Power : 362
      Likes Received
      6
      Likes Given
      1

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Liwalo na liwe!

    14. #151
      manucho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Posts : 561
      Rep Power : 469
      Likes Received
      79
      Likes Given
      0

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Kama alivyo J.K hata Pinda ni chaguo la Mungu. Uzao wa 4 ni wa mabadiliko.

      Hawa watu wawili na viongozi wengine ktk chama chao wanaleta mabadiliko makubwa sana. Pinda anaongea ukweli mtupu ila hajijui wala hajitambui na wengine wanaongea tena lugha moja lkn hawaelewani.

      Yote haya ni makusudi ya Mungu. Mungu amewachagua hawa watu ili yote yaliyokusudiwa YATIMIE.

    15. #152
      mwinukai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2011
      Posts : 656
      Rep Power : 539
      Likes Received
      134
      Likes Given
      51

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Kifupi kama majibu ndio yale hatutarajii mapya, lakini kasema ukweli anapaswa kupongezwa kwani huo ndio ukweli sikuzote .

    16. #153
      congobe's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st May 2012
      Posts : 123
      Rep Power : 375
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      nasikitika wewe unae endelea kumwita mhe wakati huo huo unasema hafai ,mwite jina lake yeye kama yeye

    17. #154
      HUGO CHAVES's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th March 2011
      Posts : 666
      Rep Power : 546
      Likes Received
      95
      Likes Given
      13

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      sijuin ni vigezo gani vilitumika kumpata waziri mkuu wa aina hii .tunahitaji mtu anayejali utaifa kwanza .ameonyesha kuanguka ingekuwa pale london ni kura nje hufai ,bahati umezaliwa tanzania

    Page 8 of 8 FirstFirst ... 678

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...