Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

    Report Post
    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast
    Results 101 to 120 of 154
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22277

      Default PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Wanabodi,

      Kila nipatapo fursa, sipendi kabisa kukosa kipindi cha Maswali na Majibu ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza, Peter Pinda, ile leo nilikikosa kipindi hiki.

      Lakini kupitia taarifa za habari, nimemsikia Mhe. Pinda, akisema kuwa ni jukumu la wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili CCM iendelee kutawala milele!.

      Naombeni wajuzi wa masuala ya utawala, mnirekebishe if I'm wrong!, Kuanzia kwa rais JK na wanasiasa wengine wote ambao japo wamechaguliwa kwa tiketi za vyama, ukishakuwa mtumishi wa umma, paid by taxpayers money, jukumu lako kuu sasa ni kuutumikia umma na sio chama chako!.

      Hii inamaanisha rais JK, japo ameshinda kwa tiketi ya CCM, na anaongoza serikali ya Tanzania, na wakati huo huo yeye ndiye Mwenyekiti wa CCM, amechaguliwa kuiongoza Tanzania na Watanzania na sio na wana CCM, hivyo anaongoza serikali ya Tanzania kwa niaba ya Watanzania na kwa manufaa ya Watanzania wote, na sio kwa manufaa ya wana CCM!. (Of the people, by the people and for the people).

      JK ndiye rais wa Chadema, ndiye rais wa CUF na ndiye rais wa wasio na vyama kama sisi!. Yeye ndiye rais wa Dr. Slaa, yeye ndiye rais wa Prof. Lipumba, yeye ndiye rais wetu sisi wote kama Watanzania, ni rais wa waliomchagua na pia rais wa wasiomchagua, anatakiwa kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya chama chake cha CCM!.

      Kauli ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda bungeni leo kuwa Wakuu wa wilaya na mikoa, wako pale kuhakikishe CCM inashinda chaguzi zote ili itawale milele, haiwezi kupita bila kupingwa!. Hi inamaanisha kuwa viongozi hawa, wako kwa ajili ya kuilinda na kuitetea status quo ya CCM ili iendelee kutawala milele!. This is very wrong kwa tafsiri sahihi ya Public Servants!. Kwa kauli hii ya Pinda, it goes without saying kuwa wakuu wa majeshi yetu, Polisi wetu, mahakama zetu na wakuu na vyombo vya dola, na vyombo vya kiserikali, wanateuliwa ili wahakikishe CCM haishindwi na inaendelea kutawala milele!.

      Public Servant, ni mtumishi wa umma, ma RC na ma DC ni viongozi wa serikali, kwa maana hiyo ni viongozi wa umma, na watatimiza majukumu yao kwa maslahi ya umma na sio kwa maslahi ya CCM. Ndio maana Mhe. Tundu lissu aliwakataa hawa wasihusishwe ile tume ya katiba na juzi akasisitizwa hawapaswi kuwamo bungeni!.

      Hata wabunge wa kuchaguliwa, ni watumishi wa umma, japo wanateuliwa kwa tiketi za vyama vya siasa, wanachaguliwa na wananchi na sio na vyama vyao, hivyo wakishashinda ubunge, wanakuwa ni watumishi wa watu na sio watumishi wa vyama vyao, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao ya kibunge kwa maslahi ya wananchi na sio kwa maslahi ya vyama vyao!. Kama ni kweli, majukumu ya ma RC na ma DC ni kuhakikisha CCM haishindwi, hii ina maana kubwa zaidi katika mustakabali wa mabadiliko halali ya serikali!.

      Binafsi yangu, nimesikitishwa na kauli hiyo, and to be honest, nilikuwa na very high hopes kuhusu Pinda, lakini sasa nimeamini, he is good for nothing!, a very disapointing PM!. Kwa vile CCM ni chama tawala, hivyo public servants wana jukumu la kuhakikisha CCM inashinda na kutawala milele!.

      Hii inamaanisha hata kama 2015, Watanzania wataamua kuivote out CCM kupitia njia halali ya ballot box, hao public servanys wenye jukumu la kuitumia serikali mpya ya chama kitakachoshinda, wako kwenye mind set ya kuhakikisha lazima CCM inashinda, na jee ikitokea CCM ikashindwa, jee watakabidhi madaraka kwa mshindi halali?!, jee majukumu yao yatabadilika or what does Pinda exactly meant?!.

      Kusema ukweli, civic education kuhusu multipartism, inatakiwa kuanzia juu ndipo ishuke chini kwa wananchi wa kawaida!.

      Sasa ndio nimeanza kuelewa, no wonder kwa nini jina la Pinda, halitajwi kabisa kabisa katika presidential materials!. Maliza tuu term yako kwa amani, ukaiendeleza ile kampuni yako ya P & P, nami nitakutangazia sana ile asali yako, ila nakuomba Tanzania yetu utuachie kwa amani, hii sio Tanzania ya CCM, CHADEMA au CUF!. Tanzania ni ya Watanzania wote.

      Kiukweli, mabadiliko yakija, hizi nafasi za ma DC na ma RC ndizo ziwe za kwanza kufutiliwa mbali!.

      Very Disapointed!.

      Pasco.

      NB. Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mshabiki wa Utanzania kwa maslahi ya Taifa mbele!.

      Last edited by Pasco; 17th August 2012 at 12:17.

    2. RukaaJuu Final

    3. #101
      Nyunyu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 9th March 2009
      Location : Here.
      Posts : 3,349
      Rep Power : 2044
      Likes Received
      465
      Likes Given
      2749

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Hivi kweli pasco unataka kuniambia ulikuwa unategemea nini toka kwa mtoto wa mkulima!

      Kwa maono yangu ni waziri mkuu bomu we have ever had!
      There is no such a thing as part freedom- Nelson Mandela

      e-mail: [email protected]

    4. #102
      WildCard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 6,455
      Rep Power : 1980
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      59

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By REMSA
      Miaka ya nyuma nilikuwa nawaza kuwa Pinda ni mmoja wa viongozi makini,lakini kadiri miaka
      ilivyoendelea kwenda nimeona ni kiongozi asiyefaa kabisa,kwani hana hekima hata kidogo
      ya kumfanya kuwa waziri mkuu,kama anayo ni kidogo ya kuongoza familia yake tu"maana ni
      mropokaji wa pointless kuliko Nape."
      Kumbuka maneno ya JK baada ya uteuzi wa Pinda kuwa Waziri Mkuu. Alisema Lowasa, mtangulizi wa huyu Pinda, alikumbwa na AJALI ya KISIASA tu. Kwa maana hiyo Pinda aliupata UwaziriMkuu kiajali tu. Hakuwahi na hajawahi kuonyesha UONGOZI kokote kule. UKRISTO na UTIIFU wake wa kiseminari ulimsaidia pia.
      Mikael P Aweda likes this.

    5. #103
      Ndoa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2011
      Posts : 630
      Rep Power : 504
      Likes Received
      120
      Likes Given
      46

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Inachukiza sana. Uwaziri mkuu wenyewe wa kubahatisha.

    6. #104
      lukindo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th March 2010
      Posts : 1,575
      Rep Power : 781
      Likes Received
      415
      Likes Given
      481

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By REMSA
      Miaka ya nyuma nilikuwa nawaza kuwa Pinda ni mmoja wa viongozi makini,lakini kadiri miakailivyoendelea kwenda nimeona ni kiongozi asiyefaa kabisa,kwani hana hekima hata kidogo
      ya kumfanya kuwa waziri mkuu,kama anayo ni kidogo ya kuongoza familia yake tu"maana ni
      mropokaji wa pointless kuliko Nape."
      na hii iwe reminder kuwa hata huko walikoendelea hakuna viongozi wazuri wala wabaya bali wamezifanya sheria kuwa kama nyenzo za kuwabana hawa wajamaa!
      Kwa mfano, unadhani ni mawaziri wangapi wamepita Uingereza mpaka leo lakini wanamkumbuka Churchill waliobakia wanaongozwa na sheria tu. Hili ndilo lilitupotosha kudhani kuwa rais daima angekuwa kama Mwl. Nyerere, PM kama Kawawa na hatukuona haja ya kuweka vipengele vya katiba sasa acha tuyaone. Niambie ni kiongozi gani ambaye alikuwa mzuri kabla na kuingia kwenye 'system' akaendelea hivyo (Magufuli, Tibaijuka, Mwakyembe)????
      Bahati mbaya sana ni kuwa hata hiyo Katiba Mpya iko mashakani maana MaDC na RC ndeio wanasaidia kukusanya watoa maoni na ni maoni gani watoe (nafikiri umemsikia Mzee Warioba). Kwa maana hiyo huenda nayo ikaja ileile, hapa ni wewe na mimi kuziacha 'keyboards' na kufanya linalowezekana!

    7. #105
      Waridi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th March 2008
      Posts : 854
      Rep Power : 739
      Likes Received
      88
      Likes Given
      84

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By Nyakageni
      Pinda kachemsha, nasubiria kauli toka CDM, CUF, NCCR, LHRC, wanaharakati. So pathetic. Upuuzi huu. Wanahabari wamuhoji mama Anna Kilango a.k.a mama Willy@kumkoma nyani, kuhusu kuwatetea ma RC na DC katika uandaaji wa katiba na kauli ya kilaza Pindwa
      Mkuu,
      Chama cha NCCR-Mageuzi, tulikwishawaambia watanzania kuhusu tatizo hili. Matharani, katika ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2010, kuna maelezo yauatayo:

      4.1.3 MUAFAKA WA KITAIFA

      Ili kuleta maelewano, kudumisha amani, na kuleta utawala bora, chama cha NCCR-Mageuzi kitaanzisha mchakato wa kupata kwanza muafaka wa kitaifa. Muafaka wa kitaifa unajumuisha maridhiano kuhusu maadili ya kitaifa, na makubaliano katika mambo ya msingi yenye maslahi kwa taifa. Aidha katika hoja hii wana NCCR-Mageuzi tunapendekeza taifa letu liwe na muafaka kuhusu misingi mikuu ya utaifa wetu. Misingi hiyo itatokana na mambo ambayo yatakuwa yamekubaliwa na jamii bila kujali chama, dini, kabila, nasaba au jinsia.

      Muafaka wa kitaifa utatusaidia kupanua wigo wa fikra zetu kuhusu maadili ya viongozi na ya wananchi. Hivi sasa mjadala kuhusu maadili ya taifa umejali tu suala la ufisadi, lakini hoja hii ni pana kuliko ufisadi. Lazima tuzungumzie malezi ya taifa, misingi na maadili ya malezi hayo, uzalendo wetu na masuala mengineyo.

      Vilevile, muafaka wa kitaifa utatuwezesha kuondokana na mfumo wa utawala wa chama dola. Kwa sasa chama kilichopo madarakani ni chama dola kinachotawala kijeshi kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama tangia ngazi ya wilaya hadi taifa. Kwa mfano, bado wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa ni wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama zinazojumuisha wakuu wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama kama vile Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Usalama wa Taifa na Jeshi la Mgambo. Wakuu haohao wa Mikoa na Wilaya ni makada wa chama tawala na wakuu wa kamati za siasa za chama tawala katika ngazi zao.

      Mfano mwingine ulio hai ni jinsi Tume ya Uchaguzi ya Taifa ilivyofumbikwa na mfumo wa chama kimoja, hali ambayo inaifanya tume isiwe huru. Licha ya kuwa wajumbe wa tume hii walio wengi ni wanachama wa chama kilichoko madarakani kwa sasa, watumishi wa tume ni watendaji wa Wizara ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI). Hawa wanawajibika kwa wakuu wao na wala si kwa Tume ya Uchaguzi. Muafaka wa kitaifa utatuletea Tume huru ya Uchaguzi.

      Hatuna budi kuafikiana (kuwa na muafaka) kwamba licha ya tofauti zetu za kiitikadi yapo musuada ambayo chama chochote kitakachoshika madaraka lazima kiyaheshimu maana hayo ni yetu sote kama taifa.

      Soma ilani nzima ukitaka hapa:
      NCCR-MAGEUZI BLOG: PAMOJA TUTASHINDA!: Ilani za Uchaguzi
      Last edited by Waridi; 17th August 2012 at 15:08.

    8. Miaka 50

    9. #106
      artorius's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 524
      Rep Power : 477
      Likes Received
      100
      Likes Given
      0

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Kwa kweli nimesikitishwa na kauli yake,waziri mkuu asiye na busara,ndo maana hawezi kutatua migogoro kwenye jamii,hawezi hata kuchagua maneno ya kuongea kama ''LIWALO NA LIWE'',mwisho 2015 aondoke kwa amani hata akitoka kabla ya hapo itakuwa vizuri sana

    10. #107
      Kindimbajuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th July 2009
      Posts : 686
      Rep Power : 1045
      Likes Received
      207
      Likes Given
      168

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By Pasco
      Wanabodi,

      Kila nipatapo fursa, sipendi kabisa kukosa kipindi cha Maswali na Majibu ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza, Peter Pinda, ile leo nilikikosa kipindi hiki.

      Lakini kupitia taarifa za habari, nimemsikia Mhe. Pinda, akisema kuwa ni jukumu la wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili CCM iendelee kutawala milele!.

      Naombeni wajuzi wa masuala ya utawala, mnirekebishe if I'm wrong!, Kuanzia kwa rais JK na wanasiasa wengine wote ambao japo wamechaguliwa kwa tiketi za vyama, ukishakuwa mtumishi wa umma, paid by taxpayers money, jukumu lako kuu sasa ni kuutumikia umma na sio chama chako!.

      Hii inamaanisha rais JK, japo ameshinda kwa tiketi ya CCM, na anaongoza serikali ya Tanzania, na wakati huo huo yeye ndiye Mwenyekiti wa CCM, amechaguliwa kuiongoza Tanzania na Watanzania na sio na wana CCM, hivyo anaongoza serikali ya Tanzania kwa niaba ya Watanzania na kwa manufaa ya Watanzania wote, na sio kwa manufaa ya wana CCM!. (Of the people, by the people and for the people).

      JK ndiye rais wa Chadema, ndiye rais wa CUF na ndiye rais wa wasio na vyama kama sisi!. Yeye ndiye rais wa Dr. Slaa, yeye ndiye rais wa Prof. Lipumba, yeye ndiye rais wetu sisi wote kama Watanzania, ni rais wa waliomchagua na pia rais wa wasiomchagua, anatakiwa kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya chama chake cha CCM!.

      Kauli ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda bungeni leo kuwa Wakuu wa wilaya na mikoa, wako pale kuhakikishe CCM inashinda chaguzi zote ili itawale milele, haiwezi kupita bila kupingwa!. Hi inamaanisha kuwa viongozi hawa, wako kwa ajili ya kuilinda na kuitetea status quo ya CCM ili iendelee kutawala milele!. This is very wrong kwa tafsiri sahihi ya Public Servants!. Kwa kauli hii ya Pinda, it goes without saying kuwa wakuu wa majeshi yetu, Polisi wetu, mahakama zetu na wakuu na vyombo vya dola, na vyombo vya kiserikali, wanateuliwa ili wahakikishe CCM haishindwi na inaendelea kutawala milele!.

      Public Servant, ni mtumishi wa umma, ma RC na ma DC ni viongozi wa serikali, kwa maana hiyo ni viongozi wa umma, na watatimiza majukumu yao kwa maslahi ya umma na sio kwa maslahi ya CCM. Ndio maana Mhe. Tundu lissu aliwakataa hawa wasihusishwe ile tume ya katiba na juzi akasisitizwa hawapaswi kuwamo bungeni!.

      Hata wabunge wa kuchaguliwa, ni watumishi wa umma, japo wanateuliwa kwa tiketi za vyama vya siasa, wanachaguliwa na wananchi na sio na vyama vyao, hivyo wakishashinda ubunge, wanakuwa ni watumishi wa watu na sio watumishi wa vyama vyao, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao ya kibunge kwa maslahi ya wananchi na sio kwa maslahi ya vyama vyao!. Kama ni kweli, majukumu ya ma RC na ma DC ni kuhakikisha CCM haishindwi, hii ina maana kubwa zaidi katika mustakabali wa mabadiliko halali ya serikali!.

      Binafsi yangu, nimesikitishwa na kauli hiyo, and to be honest, nilikuwa na very high hopes kuhusu Pinda, lakini sasa nimeamini, he is good for nothing!, a very disapointing PM!. Kwa vile CCM ni chama tawala, hivyo public servants wana jukumu la kuhakikisha CCM inashinda na kutawala milele!.

      Hii inamaanisha hata kama 2015, Watanzania wataamua kuivote out CCM kupitia njia halali ya ballot box, hao public servanys wenye jukumu la kuitumia serikali mpya ya chama kitakachoshinda, wako kwenye mind set ya kuhakikisha lazima CCM inashinda, na jee ikitokea CCM ikashindwa, jee watakabidhi madaraka kwa mshindi halali?!, jee majukumu yao yatabadilika or what does Pinda exactly meant?!.

      Kusema ukweli, civic education kuhusu multipartism, inatakiwa kuanzia juu ndipo ishuke chini kwa wananchi wa kawaida!.

      Sasa ndio nimeanza kuelewa, no wonder kwa nini jina la Pinda, halitajwi kabisa kabisa katika presidential materials!. Maliza tuu term yako kwa amani, ukaiendeleza ile kampuni yako ya P & P, nami nitakutangazia sana ile asali yako, ila nakuomba Tanzania yetu utuachie kwa amani, hii sio Tanzania ya CCM, CHADEMA au CUF!. Tanzania ni ya Watanzania wote.

      Kiukweli, mabadiliko yakija, hizi nafasi za ma DC na ma RC ndizo ziwe za kwanza kufutiliwa mbali!.

      Very Disapointed!.

      Pasco.

      NB. Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mshabiki wa Utanzania kwa maslahi ya Taifa mbele!.

      Pasco hapo ndo kazi ilipo. maana hata waziri mkuu hataki kujishughulisha na elimu ya uraia. akina mimi tutakuwa wapi sasa?. likini maoni yangu ni kuwa hii inatokana na kuwa tuna viongozi wasiojua wanawajibika kwa nani. PM kama angefahamu anawajibika kwa nani asingezungumza maneno rahisi na potoshi kama yale. chukua mfano 2015 chama Y ambacho si CCM either kinashindwa kwa wazi au kwa kuonewa, vurugu inazuka, tunauana tunafikishwa kule kwa mahakama ya wale jamaa, unadhani Pinda kwa maneno kama haya atawekwa nje ya kapu kweli?. kwa maana haya maeno ni makali haya

    11. #108
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      jamani msifanye nianze kuamini vingine...Yaani hadi leo hamfahamu kwamba Mnatawaliwa?..Mlinatak kweli Pinda aseme RC na DC hawahusiki na uchaguzi ama ushindi wa CCM nmiaka yote ya nyuma? aseme kwamba Polisi hawahusiki na ushindi wa CCM miaka ya nyuma?. Amekosea amekosea kakosea kufuata kiapo au mlivyotegemea nyie watawaliwa?

      Pinda kakosea - Pinda kakosea, jamani mwee, mlokosea ni nyie ambao mnashindwa kabisa kuchanganua hali halisi viwanjani na mambo yaliyoandikwa kwenye vitabu wakati katiba ya chama inamlazimisha kukitumikia chama. Mliona wapi, fisadi anakamatwa kahujumu uchumi wa nchi anaombwa kujiuzuru kustaafu mapema mchezo umekwisha! Toka kina EL, Jeetu Patel, Mkapa na hata Chenge alosema anavijisenti tu account za nje na akaua watu akiendesha gari amelewa leo bado ni mbunge. Ni fisadi gani la juu alokwisha kamatwa na kufungwa kama kweli kuna sheria?.

      Jamani muonyeshwe nini zaidi ujeuri wa wabunge wenu, viongozi wenu hata kina Nape wana jeuri ya kutukana watu siku hizi..Hili li Nchi limeshaoza zamani na mtaendelea kutawaliwa maana umuhmu wa Utawala wowote ni hawa kina kaizali wakuu wa Mikoa na wilaya. Bila kuwatumia hawa kina Kaizali na majeshi, utawala wa Roma ungesimama vipi Ulaya nzima hadi guba ya Urabuni?. Pinda kasema ukweli mtupu na nampongeza kwa kauli hiyo mkae mkijua wazi kwamba Ma RC ma Ma DC watafanya kila mbinu CCM ishinde uchaguzi ujao kama zilizopita - Hamtaki Mnahama!
      Last edited by Mkandara; 17th August 2012 at 15:39.
      omujubi likes this.
      Exploration of reality

    12. BAK
      #109
      BAK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2007
      Location : Mfaranyaki
      Posts : 26,633
      Rep Power : 44971
      Likes Received
      8385
      Likes Given
      8363

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Hehehehe nimeipenda hii...Inaonyesha ni jinsi gani JF ilivyo kuwa kiboko kwa kuweza kumbadilisha Pasco alias.....mpenda magamba na manukato yanayoweza kumrukia pindi Fisadi Lowassa akiweza kuchakachua uchaguzi 2015 na hadi kufikia kutoa kauli kwamba si mfuasi wa chama chochote bali mpenda maslahi ya Watanzania. Sasa ngoja tuingie kazini na M4C ili tukupe kadi rasmi. Hongera sana na natumai micango yako itabadilika na hivyo kuonyesha kipaumbele cha maslahi ya Watanzania badala yale ya magamba

      Weekend njema.

      Quote By Pasco
      Wanabodi,

      NB. Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mshabiki wa Utanzania kwa maslahi ya Taifa mbele!.

      Let your graceful words fly out into the World, carried on winds of courage, imagination and joy. Let them inspire others to step into action

    13. #110
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,370
      Rep Power : 1212
      Likes Received
      1214
      Likes Given
      1591

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Mi sioni tatizo la kauli hiyo, sababu hata asingesema adharani wangeendelea kuwatumia gizani bila sisi kujua, uzuri ni kwamba hao wakuu wa wilaya sio pekee wanaopiga kura.

    14. #111
      kbosho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th June 2012
      Location : dar es saalam
      Posts : 1,581
      Rep Power : 667
      Likes Received
      200
      Likes Given
      33

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      mi naona 2liarakisha kuingia kwenye mfumo wa vyama vng..bado sana kwa tz..bado hata viongoz wa juu awajui nn maana ya demokrasia na nn maana ya mfumo wa vyama vng

    15. #112
      TOWNSEND's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th May 2011
      Location : kwa ngulelo
      Posts : 1,117
      Rep Power : 630
      Likes Received
      196
      Likes Given
      31

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Hakuna laa maana ndani ya bunge hili ila ni laana tu itawapata ...hawakujadili chochote kusaidia wale walio na shida hasa vijijini hakuna dawa wala bara bara .wamevuta posho tu na kukandamiza opposition muda mwingi walijadili cdm kuliko inssues.
      hata wao wenyewe kupitia spika amesema wataangalia namna ya kupitisha budget ...walipitisha budget kuu kabla halafu ndio wakaja kupitisha za wizara utaona ni jinsi gani walivyokuwa wanafanya mchezo wa kuigiza
      For tommorow belonging to those people who prepared fo it

    16. #113
      armanisankara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2011
      Posts : 273
      Rep Power : 677
      Likes Received
      43
      Likes Given
      108

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By Papizo
      Huyu mzee sijui hata kwa nini alipewaa uwaziri maana saa zingine namuona kama hajui nini anafanya maana mambo yake tu anaoneken mfata upepo kutoka mjengoni....
      hakuna rais ambaye anataka kua na waziri mkuu mchapa kazi ili wasigombane. marais wetu wanataka waziri mkuu mpole na awe anakubali kila kitu yaani YES MEN. kipindi cha mwinyi alibadilisha mawaziri wakuu watatu [ warioba, malecela na msuya] sababu alikua anapingana nao. yeye ni mzee wa ruksa wakati waziri mkuu walikua sio wazee wa ruksa..

    17. #114
      nyabhingi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th October 2010
      Posts : 3,242
      Rep Power : 1295
      Likes Received
      1374
      Likes Given
      2668

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      mkoa ninaofanyia kazi nilishuhudia RC akimshinikiza RAS(KATIBU TAWLA WA MKOA)kwa kumuandikia dokezo la kulipia vyakula na vinywaji kwa ajili ya kikao cha ccm yeye akiwa kama mwenyekiti,..siku hiyo jengo zima lilitapakaa hii mijamaa na minguo yao ya kijani na njano..anger boiled my blood and pathetically there was nothing i could do...
      Every nation in every region now has a decision to make: Either you are with us, or you are with the terrorists.George W. Bush

    18. #115
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th November 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 7,243
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1087
      Likes Given
      7

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Pinda ni mlevi wa madaraka

    19. #116
      chiborie's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th September 2011
      Posts : 173
      Rep Power : 421
      Likes Received
      26
      Likes Given
      51

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Quote By bullet
      Hivi hawa ma RC na DC si ndio Anna Kilalgo aliwatetea kuwa wawemo katika uratibu wa katiba mpya? Fikiria sasa ni upendeleo kiasi gani kwa CCM watakao uonyesha! Vyeo hivi vifutwe kabisa ndani ya katiba
      Hawa watavuruga mchakato wa katiba mpya kwa kutaka kuingiza interests za CCM. Pinda is always a disappointing PM. Wanaothani kwamba huyu mzee ana busara wanajidanganya wenyewe.
      bullet likes this.

    20. #117
      we gule's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Posts : 124
      Rep Power : 371
      Likes Received
      10
      Likes Given
      65

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Pasco
      Mawazo yako ni sahihi kabisa, hata ambaye hajaenda shule unaona kabisa ambavyo nchi inapelekwa kwa miaka 50 iliyopita kwa Viongozi waliokaribu na wanachi waliotakiwa kuelewa matatizo yao,kuratibu ,kufuatilia na kulinda maslahi ya nchi yetu badala yake wametoa kipaumbele kulinda maslahi ya Chama, dhahabu ziende bila kujali idadi yake sawa,Twiga waende wakiwa hai au wamekufa sawa ,wanafunzi wakae chini sawa,Zahanati kila kijiji zisizo na dawa wala wataalamu sawa .Ilimradi RC,DC,A/TARAFA ,M/KATA Wanachojua kimoja tu Chama kiendele kutawala milele, na utendaji wao utauona chaguzi zinapo karibia.Kama kwa mawazo hayo ya Kiongozi Mkubwa anatoa majibu hayo tutegemee nini miaka 50 ijayo?

    21. #118
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 4,157
      Rep Power : 1847
      Likes Received
      1431
      Likes Given
      1539

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Leo umefunguka mkuu.
      "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"
      "Matatizo hayawezi kutatuliwa na uwezo ule ule mdogo wa watawala wa CCM walioyasababisha"

    22. #119
      Bahati Risiki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th June 2012
      Posts : 535
      Rep Power : 593
      Likes Received
      87
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By Pasco
      Wanabodi,

      Kila nipatapo fursa, sipendi kabisa kukosa kipindi cha Maswali na Majibu ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza, Peter Pinda, ile leo nilikikosa kipindi hiki.

      Lakini kupitia taarifa za habari, nimemsikia Mhe. Pinda, akisema kuwa ni jukumu la wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili CCM iendelee kutawala milele!.

      Naombeni wajuzi wa masuala ya utawala, mnirekebishe if I'm wrong!, Kuanzia kwa rais JK na wanasiasa wengine wote ambao japo wamechaguliwa kwa tiketi za vyama, ukishakuwa mtumishi wa umma, paid by taxpayers money, jukumu lako kuu sasa ni kuutumikia umma na sio chama chako!.

      Hii inamaanisha rais JK, japo ameshinda kwa tiketi ya CCM, na anaongoza serikali ya Tanzania, na wakati huo huo yeye ndiye Mwenyekiti wa CCM, amechaguliwa kuiongoza Tanzania na Watanzania na sio na wana CCM, hivyo anaongoza serikali ya Tanzania kwa niaba ya Watanzania na kwa manufaa ya Watanzania wote, na sio kwa manufaa ya wana CCM!. (Of the people, by the people and for the people).

      JK ndiye rais wa Chadema, ndiye rais wa CUF na ndiye rais wa wasio na vyama kama sisi!. Yeye ndiye rais wa Dr. Slaa, yeye ndiye rais wa Prof. Lipumba, yeye ndiye rais wetu sisi wote kama Watanzania, ni rais wa waliomchagua na pia rais wa wasiomchagua, anatakiwa kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele na sio maslahi ya chama chake cha CCM!.

      Kauli ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda bungeni leo kuwa Wakuu wa wilaya na mikoa, wako pale kuhakikishe CCM inashinda chaguzi zote ili itawale milele, haiwezi kupita bila kupingwa!. Hi inamaanisha kuwa viongozi hawa, wako kwa ajili ya kuilinda na kuitetea status quo ya CCM ili iendelee kutawala milele!. This is very wrong kwa tafsiri sahihi ya Public Servants!. Kwa kauli hii ya Pinda, it goes without saying kuwa wakuu wa majeshi yetu, Polisi wetu, mahakama zetu na wakuu na vyombo vya dola, na vyombo vya kiserikali, wanateuliwa ili wahakikishe CCM haishindwi na inaendelea kutawala milele!.

      Public Servant, ni mtumishi wa umma, ma RC na ma DC ni viongozi wa serikali, kwa maana hiyo ni viongozi wa umma, na watatimiza majukumu yao kwa maslahi ya umma na sio kwa maslahi ya CCM. Ndio maana Mhe. Tundu lissu aliwakataa hawa wasihusishwe ile tume ya katiba na juzi akasisitizwa hawapaswi kuwamo bungeni!.

      Hata wabunge wa kuchaguliwa, ni watumishi wa umma, japo wanateuliwa kwa tiketi za vyama vya siasa, wanachaguliwa na wananchi na sio na vyama vyao, hivyo wakishashinda ubunge, wanakuwa ni watumishi wa watu na sio watumishi wa vyama vyao, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao ya kibunge kwa maslahi ya wananchi na sio kwa maslahi ya vyama vyao!. Kama ni kweli, majukumu ya ma RC na ma DC ni kuhakikisha CCM haishindwi, hii ina maana kubwa zaidi katika mustakabali wa mabadiliko halali ya serikali!.

      Binafsi yangu, nimesikitishwa na kauli hiyo, and to be honest, nilikuwa na very high hopes kuhusu Pinda, lakini sasa nimeamini, he is good for nothing!, a very disapointing PM!. Kwa vile CCM ni chama tawala, hivyo public servants wana jukumu la kuhakikisha CCM inashinda na kutawala milele!.

      Hii inamaanisha hata kama 2015, Watanzania wataamua kuivote out CCM kupitia njia halali ya ballot box, hao public servanys wenye jukumu la kuitumia serikali mpya ya chama kitakachoshinda, wako kwenye mind set ya kuhakikisha lazima CCM inashinda, na jee ikitokea CCM ikashindwa, jee watakabidhi madaraka kwa mshindi halali?!, jee majukumu yao yatabadilika or what does Pinda exactly meant?!.

      Kusema ukweli, civic education kuhusu multipartism, inatakiwa kuanzia juu ndipo ishuke chini kwa wananchi wa kawaida!.

      Sasa ndio nimeanza kuelewa, no wonder kwa nini jina la Pinda, halitajwi kabisa kabisa katika presidential materials!. Maliza tuu term yako kwa amani, ukaiendeleza ile kampuni yako ya P & P, nami nitakutangazia sana ile asali yako, ila nakuomba Tanzania yetu utuachie kwa amani, hii sio Tanzania ya CCM, CHADEMA au CUF!. Tanzania ni ya Watanzania wote.

      Kiukweli, mabadiliko yakija, hizi nafasi za ma DC na ma RC ndizo ziwe za kwanza kufutiliwa mbali!.

      Very Disapointed!.

      Pasco.

      NB. Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida ambaye sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mshabiki wa Utanzania kwa maslahi ya Taifa mbele!.

      Sasa wewe angalia hata majina. Sii pinda, sii kiwete, sii dhaifu. Unategemea kitu hapa? Hii nchi inaelekea pabaya ni vizuri kuwa huyo pinda anaendelea kujifunika kwenye blnketi la ccm. Siku yaja na haiko mbali, pinda ataita ccm na mizimu labda ndiyo itakayoitikia. Watanzania wa kweli watakuwa walishaondoka zamani!

    23. #120
      TIQO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2011
      Posts : 4,616
      Rep Power : 6856
      Likes Received
      1040
      Likes Given
      131

      Default Re: PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

      Wasome alama za nyakati sio kuitumbukiza nchi kwenye machafuko.
      Mwisho wa Ubaya Aibu.

    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...