Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

    Report Post
    Page 16 of 17 FirstFirst ... 614151617 LastLast
    Results 301 to 320 of 322
    1. #1
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,921
      Rep Power : 1171
      Likes Received
      1058
      Likes Given
      804

      Default Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, ameibuka toka mafichoni na kuwaambia Watanzania kwamba anayejua mpango mzima wa kumteka, kumtesa na kumpiga ni yeye pekee.

      Dk. Ulimboka ambaye juzi alikuwa mafichoni, alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusiana na tukio zima la kutekwa, matibabu yake nchini Afrika Kusini na mambo mengine yaliyojiri wakati akiwa nje.

      Huku akiwa makini kuchagua maneno, Dk. Ulimboka alisema waandishi wa habari wasiihoji familia yake wala mtu mwingine yeyote, kwani ukweli wa tukio lake anaujua yeye mwenyewe.

      Dk. Ulimboka ambaye tangu arejee amekuwa akiishi kwa kujificha, amewataka Watanzania kuvuta subira kwani anajipa muda wa kueleza ukweli wa tukio la kutekwa kwake.

      “Najua waandishi wa habari na Watanzania wengi wanataka kujua ukweli ambao ninao mwenyewe, lakini hakuna sababu ya kuwa na haraka, wakati ukifika nitazungumza yaliyonisibu,” alisema.

      Hata hivyo, Dk. Ulimboka ambaye alikuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari uliolitikisa taifa hivi karibuni, hivi sasa anaishi kwa hofu na kujificha huku akichagua marafiki wa kukutana na kuzungumza nao. Kiongozi huyo, yuko makini pia katika kuzungumza na simu, na amekuwa akipokea zile za watu anaowajua tu.

      Alipobanwa ili azungumze kwa ufupi juu ya wanaohusika na kutekwa kwake, Dk. Ulimboka alisisitiza kuwa hayuko tayari kueleza ukweli huo kwa sasa na kuongeza kuwa muda ukifika ataeleza kila kitu.

      Polisi wapanga kumhoji

      Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Suleiman Kova ametoa kauli inaonesha kwamba vyombo vya usalama vitamuhoji Dk. Ulimboka.

      Kova ambaye alikuwa akizungumza na gazeti hili, lililotaka kujua msimamo wa vyombo vya usalama katika kulishughulikia suala la Ulimboka, hasa baada ya kurejea kutoka kwenye matibabu nchini Afrika Kusini, alisema kwamba taratibu za kipelelezi zitafuatwa.

      Wakati Kova akizungumza hayo, chanzo kimoja cha habari toka kwa maofisa wa ngazi za juu wa polisi kilidokeza kuwa endapo Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika uchunguzi wake atabaini kuwa kuna shahidi muhimu anahitajika, atahojiwa.

      Hata hivyo Kova alisisitiza kuwa; “watu wakipeleleza hawasemi ila tambua tu kwamba taratibu za upelelezi zitafuatwa.”

      Tayari taarifa na mwenendo wa tukio zima zinaonesha pasipo shaka kuwa, Jeshi la Polisi katika taratibu zake sasa linafikiria kumuita na kumuhoji Dk. Ulimboka ili liweze kuondoa maneno ya kusikia sikia.

      Kuhusu kutajwa tajwa kwa mtu anayedaiwa kuwa ni ofisa wa Usalama wa Taifa wa Ikulu, Ramadhan Ingondhur kuwa alihusika na njama za kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka, Kova aliahidi kulizungumzia hilo siku ya Ijumaa.

      Mbali na gazeti la MwanaHalisi kumtaja Ramadhan kuwa ndiye mhusika mkubwa wa kutekwa kwa Dk. Ulimboka, mwingine aliyeungana na msimamo huo ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa ambaye aliitaka Idara ya Usalama wa Taifa pamoja na serikali ithibitishe hadharani juu ya mtu anayetajwa kuhusika na tukio hilo.

      Dk. Slaa alisema chama chake kitaanzisha harakati za kutaka kujua ukweli wa nani anahusika kumteka Dk. Ulimboka. Mwanzoni mwa wiki, Dk. Ulimboka alirejea kwa kishindo nchini kutoka Afrika Kusini alikokuwa anatibiwa, na kusema yupo tayari kuendeleza mapambano na kazi baada ya kupona kabisa. Dk. Ulimboka alikwenda Afrika Kusini Juni 30 mwaka huu kwa ajili ya matibabu baada ya kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Juni 27, 2012.

      Aliondoka nchini akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa kwa vile alikuwa kwenye hali mbaya kiafya, lakini alirejea akitembea kwa miguu na kuonekana mwenye afya njema.

      Skype, Losomich and Adharusi like this.
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!


    2. #301
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,103
      Rep Power : 1445
      Likes Received
      485
      Likes Given
      72

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Quote By Ritz View Post
      Dr Ulimboka, kaishasema muacheni apumzike ukweli anaujuwa yeye mwenyewe ikifika muda nitayasema yote yalionitokea na kwa utaratibu maalumu si kama hivi mnavyotaka nyie, kila mtu ananiuliza halafu mnakwenda kuandika ya kwenu, naona imekuwa biashara...haya maneneo ya Dr Ulimboka, anaendelea kufunguka anasema anavilaumu baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari ambazo si za kweli kuhusu suala la kutekwa na kwake anasema wamekuwa wakipotosha ukweli...hapa analielezea gazeti la udaku la Mwanahalisi...R.I.P
      Quote By Ritz View Post
      Cha kushangaza kuna kundi la Pro-Chadema linalazimisha Dr Ulimboka afuate maelezo ya gazeti la Mwanahalisi kama ushahidi kinyume na hapo wanasema eti kanunuliwa...yeye ndio katekwa, kateswa, kapigwa kafanyiwa, na ndio anajua uchungu aliyofanyiwa, halafu wanakuja wana siasa wakiongozwa na Saidi Kubenea, wanajifanya wao ndio wasemaji wa Dr Ulimboka, Kubenea, ulivyomwagiwa tindikali nani alikuwa msemaji wako...msitake kumtumia Dr Ulimboka, maslahi yenu.
      Quote By Ritz View Post
      Mtu yupo mahututi hospital anapumulia mashine, anakuja mtu ambaye hata hawajuani anajifanya anamjua sana Dr Ulimboka nakuanza kuandika waliomteka Dr Ulimboka ni hawa hapo majina yao ni haya pamoja na namba za simu hizi hapa zingine zilishiwa salio saa usiku...unakwenda kwenye TV unazidi kuropoka, bahati Mungu kamjalia Dr Ulimboka kapona karudi salama yeye ndio atatueleza ukweli.
      Quote By Ritz View Post
      Hawa ndio katika lile kundi la Mwahalisi wanalazimisha Dr Ulimboka aseme wanavyotaka wao.
      Quote By Ritz View Post
      Sasa mbona Mwanahalisi imetoa mpaka picha za watu na kusema hawa ndio waliomteka Dr Ulimboka.
      Quote By Ritz View Post
      Sijui kwa nini hata jana bungeni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe analalamika kwa nini Mwanahalisi limefungiwa.
      Ritz inaelekea hii thread inakunyima usingizi kabisa. Naona kila page ina michango yako kati ya nne na sita. Tafuta walau muda wako binafsi wa kupumzika badala ya kupata pressure humu JF. Kama humpendi Ulimboka si ungesema wazi na yale ya moyoni unayomuombea badala ya kujifanya unamtetea wakati tunajua uliyosema alipotoka mstu wa pande mzima.
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)

    3. #302
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Quote By Uliza_Bei View Post
      Dr Ulimboka tayari kasha tishiwa anyamaze la sivyo?!!...... utaona hii kesi ndiyo imeisha hakuna maswali!
      Katishiwa au kala kichapo, umeshasahau mara hii?
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    4. #303
      Queen Esther's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 164
      Rep Power : 396
      Likes Received
      84
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By Elungata View Post
      WEWE MUNGU NA HARDSHIP ALLOWANCE WAPI NA WAPI?..unatumia mistari ya mungu kuhalalisha mauaji ya wagonjwa wasio na hatia?
      Hardship allowance tena ndugu mbona sijaongea Hilo? Mama au mwanamke yo yote anapoona mwanae ameumia anasikia uchungu. Nilidhani umenielewa Kumbe umehamia kwingine. Anyway jambo hili litamalizwa na maombi kwa wote wenye kuitakia mema Tanzania. Mungu ni mwema atatusaidia na kuzidi kuwapaka mafuta viongozi wetu tunawaombea usije na mchana. Hata sasa EBENEZA.

    5. #304
      mooduke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Posts : 360
      Rep Power : 511
      Likes Received
      40
      Likes Given
      758

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Da Radhia labda wewe uko kwenye Tanzania yao sie tulioko Tanzania jua kali tunapambana kujiepusha na hawa baladhuli wanaojifanya viongozi wetu kumbe ni vibaraka wa mabwenyenye na huyu ni mpiganaji shupavu tuko nyuma yake na tutapambana mpaka tone la mwisho kwa hakuna sababu ya kuogopa we cheated death.


      Quote By Radhia Sweety View Post
      Huyu naye angetulia zake tu huko aliko ili asilianzishe lingine litakalowaudhi watesi wake.

      Kwa sasa anachoweza kufanya cha busara ni kumshukuru Mungu tu kwa kumponya na kifo ambacho kilikuwa dhahiri.

      Unless ana hamu ya kumalizwa moja kwa moja, jambo la muhimu kwake kwa sasa ni kukaa kimya na kuendelea na mambo mengine.

    6. #305
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 19,230
      Rep Power : 12775
      Likes Received
      6452
      Likes Given
      999

      Default

      Quote By Mr. Zero View Post
      Ritz inaelekea hii thread inakunyima usingizi kabisa. Naona kila page ina michango yako kati ya nne na sita. Tafuta walau muda wako binafsi wa kupumzika badala ya kupata pressure humu JF. Kama humpendi Ulimboka si ungesema wazi na yale ya moyoni unayomuombea badala ya kujifanya unamtetea wakati tunajua uliyosema alipotoka mstu wa pande mzima.
      Mr. Zero,
      Naona comment zangu zimekuchoma sana naona unaangaika ku-copy...mkuu hujue JF kuna hansard ebu weka maneno yangu yeyote ambayo nimefurahi Dr Ulimboka kutekwa ukiweka mie na najitoa JF na usipoweka nakuweka kwenye kundi la Vapour...na nitakutuku PhD ya Umbeya.


    7. #306
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,752
      Rep Power : 1168
      Likes Received
      253
      Likes Given
      2541

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      hili jambo lina mambo mengi, moja niwatu kupelekwa ICC, kutokupata matibabu hospitali za nje kwani MaDr wengi wanalielewa rejea british medical journal, kuna UN na diplomasia yao ya kutokupiga kelele, kuna hisia za muathirika wa jambo hili na hatima yake ya baadae, je auze issue au asiuze, majadiliano bado yanaendelea. chochote kile kinaweza kutokea, plus or minus, au plus plus, sasa sitaki kumwaga kuku kwenye mtama kidogo, watapigana

    8. #307
      Determine's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th April 2012
      Posts : 238
      Rep Power : 407
      Likes Received
      76
      Likes Given
      96

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Quote By Ritz View Post
      Mr. Zero,
      Naona comment zangu zimekuchoma sana naona unaangaika ku-copy...mkuu hujue JF kuna hansard ebu weka maneno yangu yeyote ambayo nimefurahi Dr Ulimboka kutekwa ukiweka mie na najitoa JF na usipoweka nakuweka kwenye kundi la Vapour...na nitakutuku PhD ya Umbeya.
      hapo kwenye red ulimanisha nini???
      Kikwete ni Jasiri Sana

    9. #308
      Mia Mia's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 17th August 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      1

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Tujikumbushe ya Dr Mwakyembe alivyorudi na kusema kuwa anajua ukweli na angesema.... Wazee wakatuliza na wamempa wizara, wametupiga chenga mbili tatu kutusahaulisha... Hamna mtu aliyemtaka tena Mwakyembe aeleze ukweli wa ugonjwa wake... Hii ya Dr Ulimboka is just the same story in different scenario.. Statement yake tu tayari ipo kisiasa "NINAEJUA UKWELI NI MIMI" Kuna nini tena hapo???

    10. #309
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 19,230
      Rep Power : 12775
      Likes Received
      6452
      Likes Given
      999

      Default

      Quote By Determine View Post
      hapo kwenye red ulimanisha nini???
      Nitakutunuku...
      Determine likes this.

    11. #310
      Mwlmgomaji's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd August 2012
      Posts : 32
      Rep Power : 352
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Bado tanzania hatuna uhuru wa kuongea. Hatuna uhuru kabisaa. Nchi ni kulindana sana. Huyo kala fedha, katulizwa kelele zote zimeisha. Ukweli unajulikana Ikulu hapo hapo maifa salama ndo wamehusika. Anajua yeye wapi, kuna ma intelligencia wa ukweli Tanzania. Jamaa atakuwa katishiwa maisha na familia yake, ndo maana kawa mpole sio hivi. Wana JF, hivi kama ungekuwa wewe umepigwa mpaka hoi bin taaban, ukapelekwa nje kutibiwa, ukirudi na vitisho juu. Utafurah kusema ukweli waki uko hatarini. Chadema wamepeleza na hawawez kulipuka. Na Kova nae kala kona kumzungumzia Huyo Ramadhan. Mwanahalisi chake nae kule. Hali mbaya jaman

    12. #311
      Indume Yene's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2008
      Location : Chumbani
      Posts : 2,169
      Rep Power : 4961
      Likes Received
      340
      Likes Given
      324

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Quote By ureni View Post
      Kitu kilichotokea Dr.Ullimboka maadui zake sasa hivi wako kwenye mazungumzo nae ndio maana analeta siasa hataki kueleza kilichomtokea usishangae asieleze kabisa au akaeleza story tofauti na ile ya mwanahalisi.Manake maadui zake wanaweza kumweleza bwana samehe yale yalikuwa ni matatizo ya kiufundi wakampa shavu akatulia zake kimya.Ndio maana ameanza kuleta porojo.
      Manake hili neno:Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi... limepigwa kiufundi sio ajabu ameambiwa aliseme ili kunarrow ushaidi.
      Mmmh huko ni kutokota sasa na si kuchemsha. Sasa kama akipewa shavu akatulia ....what about the money ambayo madaktari wenzake walichanga Tanzania nzima kuhakikisha anapata matibabu na kurudi salama?? What about risk iliyochukuliwa na madaktari wenzake kuji-expose kwenye issue yake? Huo utakuwa ni ubinafsi na siamini mwanamageuzi kama Ulimboka anaweza kukubali hilo shavu. Kama akilikubali hilo shavu basi hana umaana wowote kwa jamii, angebaki huko huko Mwabepande.....sorry that is the truth (That's what we call "USALITI")

    13. #312
      Jayfour_King's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th November 2009
      Location : Tanzania
      Posts : 1,150
      Rep Power : 718
      Likes Received
      84
      Likes Given
      186

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Subira yavuta heri.
      Wrong is a mirror for the rights

    14. #313
      Mwiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Posts : 4,594
      Rep Power : 2089
      Likes Received
      223
      Likes Given
      19

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Huyu Uli nae anazidisha kiza ,si ajabu yakaishia kwenye horizon na kutoweka kwenye thin air !
      Light travels faster than sound. This is why some people appear bright until you hear them speak.

    15. #314
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,545
      Rep Power : 6186
      Likes Received
      3112
      Likes Given
      1025

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Atasema na wala hatasema kwa kuwa kesi iko mahakamani haisemwi!

    16. #315
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,545
      Rep Power : 6186
      Likes Received
      3112
      Likes Given
      1025

      Default

      Quote By Mwiba View Post
      Huyu Uli nae anazidisha kiza ,si ajabu yakaishia kwenye horizon na kutoweka kwenye thin air !
      Tutaishia kusema atasema ila hatasema! Horizon itachukua nafasi yake na habari kupotea bila Khabari. Jambo lolote linakuwa na raha likiwa la motomoto sasa hii habari ni nitasema ukifika wakati muafaka inakuwa kama habari ya kuku na vifaranga kuhusu kunyonya; utanyonya kesho na kesho huwa haipo. Naona kama muda muafaka nao haupo.

    17. #316
      MNYISANZU's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 6,311
      Rep Power : 0
      Likes Received
      593
      Likes Given
      76

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Dr Ulimboka, strike the iron while is still hot!

    18. #317
      mtoto wa mama's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th January 2011
      Posts : 93
      Rep Power : 446
      Likes Received
      6
      Likes Given
      32

      Default

      Quote By 1800 View Post
      Hakuna wa kuogopwa zaidi ya Mungu,nidhamu ya uoga na kumsujudia mwanadamu mwenzako ni mbaya na dhambi mbele ya Mungu,walishashindwa kumuangamiza mara ya kwanza sasa ni zamu yao kupata pigo takatifu ambalo familia zao hawataka kuja kusahau

      We unacheza na kung'olewa kucha.., lazima atulie sasa... Chezea usalama wewe

    19. #318
      Uliza_Bei's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2011
      Posts : 796
      Rep Power : 581
      Likes Received
      112
      Likes Given
      46

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Quote By zomba View Post
      Katishiwa au kala kichapo, umeshasahau mara hii?
      Yep...alikula kichapo ila aliporudi toka SA nadhani alitishiwa
      ukipenda asali usiogope ukali wa nyuki

    20. #319
      CHOMA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd August 2012
      Posts : 108
      Rep Power : 754
      Likes Received
      9
      Likes Given
      3

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Hiyo movie ya Dr.Ulimboka STAR wake amezimia.Tusubiri akizinduka tutajua la kumhoji mpaka kieleweke.

    21. #320
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Dk. Ulimboka: Ninayejua ukweli ni mimi...

      Quote By Uliza_Bei View Post
      Yep...alikula kichapo ila aliporudi toka SA nadhani alitishiwa
      Kichapo ndio kimefanya kazi, aliyempa kichapo anastahili sifa.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    Page 16 of 17 FirstFirst ... 614151617 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...