Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

    Report Post
    Page 20 of 21 FirstFirst ... 1018192021 LastLast
    Results 381 to 400 of 417
    1. #1
      palalisote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th August 2010
      Location : WA HAPAHAPA
      Posts : 2,064
      Rep Power : 2038
      Likes Received
      929
      Likes Given
      3827

      Default Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge





      UTANGULIZI



      Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha Maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, Maoni ya Kambi yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

      Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa “kuidhalilisha” Mahakama na/au “kuwadhalilisha majaji” (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); “kuwavunjia heshima majaji” (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); “kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji” (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); “kufedhehesha Mahakama na majaji” (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

      Aidha, Msemaji wa Kambi alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na “kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote” (Mangungu). Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba “... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na hii Tume ya Uajiri wa Mahakama.” Zaidi ya hayo, “... labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna… hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii.”

      Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba. Msemaji wa Kambi alikataa kufuta kauli hiyo ambako Mwenyekiti wa Kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi. Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hili muhimu. Maelezo haya yana lengo la kutoa ufafanuzi huo.

      Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya BUnge, Lissu alisema, “Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana ‘uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa Madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.”

      TATIZO LA MUDA MREFU

      Kuna ushahidi mkubwa kuthibitisha kwamba kuna watu wameteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu “... wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma (na) wanapewa ‘zawadi’ ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni.” Ni muhimu kuweka wazi hapa kwamba utamaduni huu haukuanza baada ya Rais Jakaya Kikwete kuchaguliwa kuwa Rais, bali ni tatizo la muda mrefu. Kwa mfano, marehemu Jaji Kulwa Masaba na Jaji Madina Muro na majaji Stephen Ihema, Juxton Mlay, Augustine Shayo na Vincent Lyimo waliteuliwa majaji wa Mahakama Kuu baada ya utumishi wa muda mrefu kwingineko katika utumishi wa umma.

      Majaji Masaba na Muro waliteuliwa huku wakiwa wagonjwa mahututi na – kwa kadri ninavyofahamu - hawakuwahi kuandika hukumu hata moja kabla ya mauti kuwafika! Jaji Lyimo aliteuliwa Machi 28, 2007 mwaka mmoja kabla ya muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, ilipofika Oktoba 26, 2007 Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo Phillemon Luhanjo alimtaarifu Jaji Mkuu kwamba Rais Kikwete “... ameamua kusogeza mbele muda wa kustaafu wa Mheshimiwa Jaji Vincent Kitubio Damian Lyimo kwa miaka mitatu kuanzia Machi 28, 2008 siku ambayo angestaafu kwa lazima”!

      Kwa upande wao, Majaji Ihema, Mlay na Shayo walijizolea umaarufu kwa kuwa majaji wasioandika hukumu na hivyo kuwa wacheleweshaji wakubwa wa kesi katika Mahakama Kuu. Jaji Ihema alitia fora kwenye jambo hili kiasi kwamba Juni 16, 2003 Mwenyekiti wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Mzee Joram Allute, alilazimika kumwandikia Rais Benjamin Mkapa maombi ya kumwondoa Jaji Ihema kama Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania “kwa uzembe na kukosa maadili.”

      Mzee Allute alikuwa na kesi kwa Jaji Ihema ambapo Jaji huyo ‘alikalia’ uamuzi kwa zaidi ya miaka minne hadi aliponyang’anywa faili la kesi hiyo na kukabidhiwa Jaji mwingine aliyeandika uamuzi ndani ya wiki tatu! Mwezi mmoja kabla ya barua ya Mzee Allute kwa Rais Mkapa, mawakili wake walikuwa wamemwandikia Jaji Mkuu Barnabas Samatta kulalamikia ucheleweshaji wa uamuzi wa kesi hiyo. Mawakili hao walidai: “Hadhi na heshima ya Mahakama inaporomoka vibaya kama inachukua zaidi ya miaka mitatu kwa Jaji kutafakari na kutoa uamuzi kwa jambo jepesi kama maombi ya pingamizi.” Licha ya malalamiko haya dhidi yake, Jaji Ihema alipatiwa mkataba wa ajira wa miaka miwili mara baada ya kustaafu mwaka 2005.

      MAJAJI WA MIKATABA

      Agosti 2, 2005 Jaji Kiongozi Hamisi Msumi alitoa taarifa kwa majaji wote wa Mahakama Kuu kwamba Jaji Ihema alikuwa amepewa mkataba mpya baada ya kustaafu kama Jaji wa Mahakama Kuu. Taarifa hiyo ilimfanya Jaji Bernard Luanda, wakati huo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, kuhoji ‘Uhalali Kikatiba kwa Majaji Kufanya Kazi kwa Mkataba Baada ya Kustaafu.’ Katika taarifa yake kwa Jaji Kiongozi Msumi, Jaji Luanda alisema kwamba “... suala la majaji kupewa mikataba ... linaenda kinyume na Katiba.” Jaji Luanda alifafanua: “Kwa kuwa Jaji amestaafu, basi kiapo chake nacho kimeondoka. Kwa bahati mbaya hawaapishwi ili washike kazi hizo za ujaji.... Ni hoja yangu kwamba Majaji waliostaafu na kupewa mikataba si Majaji kwa mujibu wa Katiba.”

      Msimamo wa Jaji Luanda uliungwa mkono mwaka mmoja baadaye na Jaji wa Rufaa, Augustino Ramadhani wakati huo akiwa Kaimu Jaji Mkuu. Katika ‘Mawazo Kuhusu Vifungu Vinavyohusu Mahakama na Majaji’ aliyomwandikia Jaji Mkuu Samatta na kunakiliwa kwa Majaji wa Rufaa wote, Jaji Ramadhani alisema kwamba “... sio sahihi kwa Jaji Mkuu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huo kupindukia umri wa miaka 65 (ambao ndio umri wa kustaafu kwa lazima kwa Jaji wa Rufaa na Jaji Mkuu).” Baadaye Jaji Luanda aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wakati Jaji Ramadhani alikuja kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

      Kauli ya Kambi kwamba kuna ukiukaji mkubwa wa Katiba kuhusiana na uteuzi wa majaji inaungwa mkono na nyaraka za ndani ya Serikali na hasa Ofisi ya Rais, Ikulu yenyewe. Desemba 6, 2007, mkutano kuhusu ajira ya majaji waliostaafu ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Kiongozi Luhanjo. Wajumbe wengine walikuwa pamoja na Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika na Naibu wake Sazi Salula, Katibu Mkuu Utumishi George Yambesi, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Sophia Wambura na Susan Mlawi wa Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.

      Kwa mujibu wa Kumbukumbu za Mkutano huo, “kwa utaratibu unaotumika sasa, baadhi ya Majaji wanaofikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa Ibara ya 110(1) kwa Majaji wa Mahakama Kuu na Ibara ya 120(1) ya Katiba wanaongezewa muda wa kuendelea na utumishi wao kwa mkataba baada ya wao kuwasilisha maombi rasmi.” Baada ya mjadala juu ya jambo hili, wajumbe wa mkutano walikubaliana kwamba “utaratibu wa kuongeza muda kwa njia ya mkataba unakiuka masharti ya Katiba na kuleta mkanganyiko kama Majaji hao wanastahili kulipwa mshahara au pensheni au vyote kwa pamoja.”

      Matokeo ya mkutano wa Ikulu ilikuwa ni kuundwa kwa ‘Kikundi Kazi kwa Ajili ya Kuchambua na Kushauri Kuhusu Ajira ya Majaji Baada ya Kustaafu’ chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kikundi Kazi kiliwasilisha Taarifa yake Machi 7, 2008. Katika Taarifa yake Kikundi Kazi kinakubaliana na msimamo wa kikatiba kwamba “kwa kuzingatia Ibara za 110 na 120 za Katiba inaonekana wazi kuwa suala la ajira za mikataba kwa Majaji ambao wamekuwa wakifanya kazi za Jaji baada ya kufikia umri wa kustaafu ni kinyume cha Katiba.” Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, hadi mwezi Machi 2008, “... walikuwepo Majaji wawili ... wa Mahakama ya Rufani na Majaji tisa ... wa Mahakama Kuu, ambao wapo katika ajira za mkataba, na Jaji mmoja ... wa Mahakama Kuu aliyeongezewa muda wa ajira kwa mujibu wa masharti ya Katiba....”

      Hii ina maana kwamba, kulikuwa na Majaji kumi na moja ambao walikuwa wanafanya kazi kinyume cha Katiba na – kwa maneno ya Jaji wa Rufaa Luanda – hawakuwa Majaji kwa mujibu wa Katiba! Aidha, kwa mujibu wa ushahidi wa nyaraka hizi, kulikuwa na Jaji mmoja tu ambaye alikuwa ameongezewa muda wa ajira ya ujaji kwa mujibu wa Katiba. Katika mapendekezo yake, Kikundi Kazi hakikumung’unya maneno:

      “Mikataba iliyopo hivi sasa iko kinyume cha Katiba.... Hii ina maana kwamba Majaji hao wanafanya kazi ya Jaji kinyume cha Katiba, hivyo kazi zote ambazo wamezifanya na wanaendelea kuzifanya wakiwa chini ya ajira mpya za mikataba hazina uhalali wowote kisheria. Kazi hizo ni sawa kama vile zimefanywa na mtumishi mwingine yeyote asiye na madaraka ya Jaji. Hivyo basi, Rais ashauriwe kuifuta mikataba hiyo mara moja kwa vile ina madhara makubwa kwa jamii na katika uteuzi wa Majaji wapya kuchukua nafasi zao. Majaji waliofutiwa mikataba waendelee na pensheni zao kama kawaida.”

      Miaka minne imepita tangu Kikundi Kazi kiwasilishe mapendekezo yake Ikulu lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kutekeleza mapendekezo hayo. Aidha, licha ya msimamo wa majaji Luanda na Ramadhani kuwa na umri wa takriban miaka saba, utaratibu wa uteuzi wa majaji wastaafu haujaachwa na mamlaka husika ya uteuzi. Ajira ya sasa ya Jaji Kiongozi Fakih Jundu iko katika kundi hili la watu wasiokuwa Majaji kwa mujibu wa Katiba.

      JAJI KIONGOZI FAKIH JUNDU

      Jaji Kiongozi Fakih Jundu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Rais Mkapa mwaka 2003. Julai 29, 2009, Jaji Jundu wakati huo akiwa Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Iringa, alitoa taarifa ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, mara baada ya kutoa taarifa hiyo, Jaji Jundu siyo tu alipewa mkataba wa ujaji kwa miaka mitatu, bali pia alipandishwa cheo na kufanywa Jaji Kiongozi.

      Kama hiyo haitoshi, inasemekana sasa kwamba Jaji Kiongozi Jundu ameongezewa mkataba mwingine tena wa miaka miwili kuendelea kuwa Jaji Kiongozi kuanzia Julai 29, 2012! Huu ni ukiukaji wa Katiba. Kwanza, kwa mujibu wa Taarifa ya Kikundi Kazi, “... umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi ni miaka sitini.... Hivyo, iwapo Rais atamuongezea Jaji Kiongozi muda wa kufanya kazi, hatamuongezea kama Jaji Kiongozi.”

      Kwa maana nyingine, kama ilikuwa makosa kikatiba kumpa Jaji Jundu mkataba wa ajira kama Jaji wa kawaida, ilikuwa makosa makubwa zaidi kikatiba kumpandisha cheo na kumfanya Jaji Kiongozi wakati alikwishafikisha umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi! Pili, kwa utamaduni uliozoeleka Tanzania, majaji wamekuwa wanaongezewa kipindi kimoja cha miaka miwili ili wamalizie kesi walizokuwa nazo hadi muda wao wa kustaafu unawadia. Kwa msimamo wa kikatiba ulioelezwa na Jaji wa Rufaa Luanda, Jaji Mkuu Ramadhani na Kikundi Kazi, siyo sahihi kwa Jaji Kiongozi Jundu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huo kupindukia muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba!

      Nyongeza hii ya pili ya mkataba wa Jaji Kiongozi Jundu imewafanya watu wanaojiita ‘Watumishi wa Mhimili wa Mahakama’ kumwandikia Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kulalamikia jambo hilo. Kwa mujibu wa barua yao, ambayo pia ilinakiliwa kwa Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu, watu hao wamesema yafuatayo kuhusu Jaji Kiongozi Jundu: “Sisi watumishi wa Mahakama tunafahamu udhaifu mkubwa kiutendaji alionao Jaji Kiongozi wetu wa sasa. Kimsingi hamudu madaraka haya. Ipo mifano mingi ya udhaifu wa Jaji Jundu. Mfano alimhamisha hakimu kutoka kituo chake cha kazi kama adhabu kwa vile hakimu huyo alitoa maamuzi ambayo yeye hakuyafurahiya kwenye ile kesi maarufu ya kibaragashia. Ni busara za Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, ndizo zilizomsaidia hakimu huyo.”

      JAJI THOMAS MIHAYO

      Thomas Bashite Mihayo aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Oktoba 8, 2003. Januari 16, 2006 Jaji Mihayo alitoa notisi ya kustaafu kwa mujibu wa Katiba kuanzia Juni 8, 2006 atakapokuwa ametimiza umri wa miaka sitini. Hata hivyo, Machi 8 ya mwaka huo, Jaji Mihayo alitaarifiwa na Jaji Mkuu kwamba Rais Kikwete alikuwa amempa “... mkataba wa miaka miwili kuanzia Juni 9, 2006.” Mkataba huo ulifikia mwisho wake Juni 8, 2008. Hata hivyo, Jaji Mihayo alipatiwa mkataba mwingine tena wa mwaka mmoja ulioanzia Juni 9, 2008 hadi Juni 8, 2009 na baada ya hapo hakupatiwa mkataba mwingine.

      Inaelekea Jaji Mkuu Ramadhani alisahau msimamo wake wa awali kuhusu ajira za mikataba kwani ndiye aliyependekeza Jaji Mihayo “... apewe mkataba mwingine wa mwaka mmoja...” Na wala si Jaji Mihayo pekee aliyepatiwa au kuongozewa mkataba katika mazingira tatanishi kama haya. Kwa mujibu wa nyaraka za Idara Kuu ya Utumishi, Jaji Donasian Mwita alipatiwa mkataba wa ujaji Juni 28, 2004. Mkataba huo wa miaka miwili ulianza kutumika Julai 1, 2004. Vile vile, Jaji Joseph Masanche alisaini mkataba wa aina hiyo hiyo na Idara Kuu ya Utumishi ulioanza kutumika kuanzia Machi 7, 2006.

      MAADILI YENYE SHAKA

      Msemaji wa Kambi hakuzungumzia masuala yanayohusu maadili ya majaji. Hata hivyo, kutokana na mjadala uliojitokeza ndani na nje ya Bunge kutokana na hotuba yake, ushahidi umepatikana unaoonyesha kwamba baadhi ya majaji wameteuliwa bila ya kwanza kuwafanyia uchunguzi juu ya maadili yao.

      MAJAJI KASSIM NYANGARIKA NA ZAINAB G. MURUKE

      Kassim Nyangarika alikuwa wakili wa kujitegemea na wakili mwenza wa Jaji Kiongozi Jundu kabla ya uteuzi wake kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2003. Kama wakili, Bwana Nyangarika aliwahi kumwakilisha mlalamikaji katika kesi ya Peter Muti dhidi ya CIELMAC Ltd., Kesi ya Madai Na. 314 ya 2003 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Katika kesi hiyo mteja wa wakili Nyangarika alishinda.

      Hata hivyo, kufuatia rufaa dhidi ya uamuzi huo, Mahakama Kuu ilifutilia mbali mwenendo wa kesi hiyo baada ya kugundua kwamba Wakili Nyangarika alikuwa amefanya vitendo vyenye kuashiria uvunjifu mkubwa wa maadili. Kwa mfano, Mahakama Kuu iligundua kuwa Wakili Nyangarika alimwelekeza hakimu – kwa kutumia ‘kipande cha karatasi cha rafu na kilichoandikwa kirafiki’ - namna ya kuendesha kesi hiyo. Mahakama Kuu iligundua makosa makubwa zaidi ya hilo. Kwa mujibu wa Jaji Kalegeya, “... kulikuwa na mawasiliano yasiyokuwa rasmi kati ya Mahakama na Wakili.” Jaji Kalegeya alikuta ushahidi wa uwezekano mkubwa kwamba Wakili Nyangarika ndiye aliyeandaa uamuzi wa Mahakama katika kesi hiyo. Aidha, Mahakama Kuu iligundua kwamba Wakili Nyangarika “... aliielekeza Mahakama kutokutoa uamuzi kwa tarehe iliyopangwa badala yake aliielekeza itoe uamuzi huo tarehe nyingine.”

      Kwa mujibu wa Jaji Kalegeya, kama kilichoonyeshwa katika mawasiliano ya Wakili Nyangarika na Mahakama ya Wilaya kilikuwa cha kweli basi “... utoaji haki katika Mahakama hiyo uko katika hatari kubwa kama sio jina la Mahakama yote, kitu kinachohitaji marekebisho ya haraka.” Kwa sababu hiyo, Jaji Kalegeya alielekeza kwamba “mamlaka husika zichukue hatua za kufichua ukweli kuhusu barua ya Wakili Nyangarika ya tarehe 18/03/2004.” Hukumu na maelekezo ya Jaji Kalegeya yalitolewa tarehe 22 Julai, 2005. Miezi saba baadaye, Wakili Nyangarika aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania!

      Wakili mwingine mwenye maadili ya mashaka yanayofanana na ya Jaji Nyangarika ambaye pia ameteuliwa Jaji Mahakama Kuu ni Zainab Muruke. Kama wakili, Zainab Muruke alimwakilisha Stephen Hill Forwood ambaye alikuwa amepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili bila faini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu. Baadaye kampuni ya mawakili ya Z.G. Muruke & Co. Advocates iliwasilisha Hati ya Mapitio (Memorandum of Review) katika Mahakama hiyo hiyo ikiomba Bwana Forwood abadilishiwe hukumu.

      Ombi hilo lilikubaliwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Kabuta na tarehe 26 Julai, 2004, Bwana Forwood akabadilishiwa adhabu kuwa faini ya shilingi 20,000 au kifungo cha miaka miwili. Jambo hili liliripotiwa kwa Jaji Kiongozi ambaye aliamuru uchunguzi ufanywe uliopelekea kushushwa cheo cha Hakimu Mkazi Kabuta. Jaji Kiongozi pia aliamuru Wakili Muruke atoe maelekezo ya ushiriki wake katika sakata hilo. Hiyo ilikuwa tarehe 14 Desemba, 2004. Mwaka mmoja na miezi miwili baadaye, Zainab Muruke aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

      MAJAJI PELAGIA B. KHADAY NA PATRICIA FIKIRINI

      Bi. Pelagia B. Khaday ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliyeteuliwa mwaka 2009. Kabla ya uteuzi huo Bi. Khaday alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kabla ya hapo alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu na Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Agosti 12, 2004, alipewa taarifa ya kusimamishwa kazi kama Msajili wa Wilaya na kuhamishiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na ‘uzito wa shutuma’ zilizotolewa dhidi yake kwa Jaji Mkuu.

      Taarifa hiyo iliandikwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Edward Rutakangwa, kwa maelekezo ya Jaji Mkuu na ilieleza kwamba Bi. Khaday alikuwa anatuhumiwa kwa “kuwashinikiza au kuwashawishi baadhi ya mahakimu mkoani Arusha kushughulikia au kuamua kwa upendeleo mashauri yaliyowahusu ... jamaa au rafiki zake”; na “kuwaandalia sababu za rufaa baadhi ya washitakiwa waliotiwa hatiani na mahakama za mahakimu hapa mkoani.”

      Kabla ya kumsimamisha Bi. Khaday kazi, Jaji Mfawidhi Rutakangwa alikuwa amemteua Mheshimiwa Jacob Somi, wakati huo akiwa Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, kuwa Afisa Uchunguzi (Enquiry Officer) ili kuchunguza tuhuma dhidi ya Bi. Khaday. Taarifa ya Uchunguzi wa Awali ya Afisa Uchunguzi Somi inasema kwamba Bi. Khaday alikuwa amelalamikiwa na mahakimu kwa kuwashinikiza ili watoe maamuzi ya kesi zilizokuwa zinawakabili jamaa au marafiki zake.

      Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Hakimu Mkazi Elvin Mugeta “alikiri kuwa-approached na Bi. Khaday ili atoe hukumu ya upendeleo kwa mshtakiwa Richard Bareto ambaye inasadikiwa kuwa ni jamaa wa rafiki yake wa karibu.” Ijapokuwa Bi. Khaday alikanusha kufanya hivyo, Afisa wa Uchunguzi Somi aliridhika kwamba “Bi. Khaday alikuwa amejiwekea utaratibu, kama alivyodai mwenyewe, wa kuwasiliana na Mahakimu kwa lengo la kuwafahamisha pamoja na mambo mengine malalamiko yaliyokuwa yakimfikia dhidi yao ili kuwanusuru wasiharibikiwe.”

      Hata hivyo, Afisa Uchunguzi Somi aliridhika kwamba “utaratibu huu ulikuwa kero kwa mahakimu pale alipoutumia kwa kushinikizwa na jamaa zake na/au rafiki zake kwa lengo la kupata maamuzi ya upendeleo. Kitendo cha kumtoa mahakamani Hakimu kwa lengo la kutaka kujua hatima ya mshtakiwa Bareto aliyekuwa asomewe hukumu siku hiyo, ni mfano wa matumizi mabaya ya utaratibu huo.”

      Afisa Uchunguzi Somi hakupata uthibitisho wa madai ya Bi. Khaday kuwaandalia sababu za rufaa washtakiwa waliotiwa hatiani. Hata hivyo, kwa mujibu wa Taarifa yake, “... sikuridhishwa na utaratibu wake wa kupeleka nakala ya hukumu kwa Bi. Mushi na kumtaka aisome ili kuona kama kuna uwezekano wa mshtakiwa Hussein Ramadhani Kitema kukata rufaa Mahakama Kuu baada ya kufungwa jela na Bw. Mugeta.” Afisa Uchunguzi Somi alipendekeza kwamba Bi. Khaday – “ambaye ni mtumishi wa Mahakama kwa kipindi kisichopungua miaka 20...” - apewe nafasi ya kujirekebisha.

      Baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi, Jaji Mfawidhi Rutakangwa alimteua Mh. Samuel Karua, Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, kuwa Investigation Officer. Tarehe 23 Februari 2007, Investigation Officer Karua aliwasilisha Taarifa ya Uchunguzi wake kwa Jaji Mkuu. Taarifa ya Investigation Officer Karua ilimkosha Bi. Khaday kwa tuhuma zote dhidi yake.

      Hata hivyo, Taarifa ya Investigation Officer Karua ina maeneo mengi yanayoleta mashaka. Kwanza, kama Investigation Officer Karua mwenyewe alivyosema, shahidi muhimu katika uchunguzi wake alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mushi. Vile vile, shahidi huyu alikuwa ‘star witness’ katika uchunguzi wa awali mbele ya Afisa Uchunguzi Somi na ndiye aliyetoa ushahidi wa yeye na mahakimu wengine kuingiliwa katika kazi zao na Bi. Khaday.

      Hata hivyo, mbele ya Investigation Officer Karua, shahidi huyu muhimu alikana kila kitu alichokisema mbele ya Afisa Uchunguzi Somi. Kwa kiasi kikubwa, Investigation Officer Karua aliitumia about turn hii kumkosha Bi. Khaday dhidi ya tuhuma zote zilizokuwa zinamkabili. Cha kushangaza ni kwamba Investigation Officer Karua hakujiuliza na hakumuuliza shahidi huyu sababu za kukana ushahidi wote alioutoa mbele ya Afisa Uchunguzi Somi.

      Je, alirubuniwa au kutishwa ili amsaidie Hakimu na mtumishi mwenzake katika Mahakama ya Tanzania asifukuzwe kazi? Kama sio hivyo, je, ni sababu zipi zilizomfanya shahidi huyu muhimu kubadili ushahidi wake kwa kiasi hicho? Je, ushahidi alioutoa shahidi huyu mbele ya Afisa Uchunguzi Somi ulikuwa wa uongo? Na kama ulikuwa wa uongo, ushahidi wake wa pili kwa Investigation Officer Karua ni wa kweli kiasi gani mpaka kumfanya Investigation Officer Karua kutamka kuwa shahidi huyu ‘anaweza ... kuwa anasema ukweli.’

      Inaelekea Investigation Officer Karua, Hakimu Mkuu Mkazi mwenye uzoefu wa miaka mingi katika Mahakama, alifanya kazi yake kwa mtazamo wa kimahakama zaidi badala ya kutumia mtazamo wa kiupelelezi na/au kiuchunguzi ambayo hasa ndiyo ilikuwa kazi yake katika uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Bi. Khaday. Kwa mtazamo wa kimahakama, ukweli kwamba shahidi muhimu kama Hakimu Mkazi Mfawidhi Mushi alikana ushahidi wake wa awali mbele ya Afisa Uchunguzi Somi ilikuwa inatosha kumfutia Bi. Khaday hatia yote. Kwa mtazamo wa kiupelelezi/kiuchunguzi, about turn ya shahidi huyu ingemfanya Investigation Officer Karua kuchunguza zaidi sababu za kigeugeu hicho.

      Pili, Investigation Officer Karua hakuipa uzito wa kutosha Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi. Kwa mfano, Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi – yenye kurasa 14 zilizochapwa - imeelezewa katika Taarifa ya Investigation Officer Karua kwa aya moja tu! Kwa sababu hiyo, ni vigumu kukubaliana na Investigation Officer Karua kwamba Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi ‘ilikuwa muhimu sana’ wakati umuhimu huo haujafafanuliwa wala kuelezewa hata kidogo katika Taarifa yake.

      Aidha, Investigation Officer Karua alitakiwa kueleza sababu za kutofautiana na Afisa Uchunguzi Somi kwamba Bi. Khaday alikuwa anakera mahakimu kwa kuwasiliana nao baada ya kushinikizwa na ndugu au rafiki zake ili wapatiwe upendeleo katika kesi zilizokuwa zinawakabili. Investigation Officer Karua hakufanya hivyo. Vile vile, Investigation Officer Karua hakuona ajabu wala kujiuliza kama ilikuwa ni kitu cha kawaida kwa Bi. Khaday kumleta Richard Bareto – mshtakiwa aliyehusishwa na shinikizo la Bi. Khaday kwa Hakimu Mkazi Mugeta – kama shahidi wake wa utetezi.

      Tatu, Investigation Officer Karua hakutoa sababu za maana za kutochukua ushahidi wa mahakimu wengine waliodaiwa kushinikizwa na Bi. Khaday. Katika aya moja tu iliyowahusu mahakimu hao, Investigation Officer Karua alisema kwamba siku ya kutoa ushahidi wao kwake, watu hao “... walishikilia msimamo wa kauli walizotoa mbele ya Bwana Somi ... na baada ya tafakuri ya muda ... mashahidi hawa waliachiwa.”

      Mbele ya Afisa Uchunguzi Somi, mashahidi hawa wawili, Hakimu Mkazi Msumi na Hakimu Mkuu wa Wilaya Mlay, walikuwa wamesema kwamba “... huko nyuma (Bwana Msumi) aliwahi kuitwa na mlalamikiwa baada ya wadhamini walioshindwa kukidhi masharti ya dhamana ... kumpelekea malalamiko ya kukataliwa dhamana, maelezo ambayo hayakuwa na ukweli wowote.” Aidha, kwa mujibu wa Afisa Uchunguzi Somi, “... katika hali isiyokuwa ya kawaida Bw. Mlay, PDM hakuwa tayari kueleza kilichomsibu hadi kujiengua katika usikilizaji wa kesi ambayo Bi. Mushi alidai ilikuwa inamkabili rafiki yake wa karibu na Bi. Khaday.” Investigation Officer Karua hakuona sababu yoyote ya kufuatilia ushahidi wa mahakimu hawa wawili!

      Nne, Investigation Officer Karua anakubali kwamba hali ilikuwa tete katika Kituo cha Arusha: “Inaelekea mtuhumiwa alikuwa na mahusiano mabaya na baadhi ya mahakimu.” Kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, Investigation Officer Karua alikuwa na wajibu wa kuchunguza chanzo cha mahusiano hayo mabaya, hasa kwa vile kulikuwa sio tu na tuhuma bali pia ushahidi wa mahakimu husika kwamba Bi. Khaday alikuwa anawaingilia mahakimu katika kazi zao. Hakufanya hivyo. Badala yake Taarifa ya Investigation Officer Karua inaonekana kama jitihada za kumkosha Bi. Khaday dhidi ya tuhuma nzito za ukosefu wa maadili ya kimahakama. Jitihada hizi zilifanikiwa kwani miaka miwili baada ya Taarifa ya Investigation Officer Karua, Bi. Khaday aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

      Na wala siyo Bi. Khaday pekee aliyeneemeka na taarifa hiyo. Bi. Patricia Fikirini, ambaye Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi inamwelezea kama mmoja wa mahakimu waliosikiliza kesi ya mfanyabiashara maarufu wa Arusha, Justin Nyari iliyokuwa chanzo cha tuhuma dhidi ya Bi. Khaday – alihusishwa na tuhuma dhidi ya Bi. Khaday kwa maneno yafuatayo: “... Kama mtawala ... (Bi. Khaday) ... alisema aliwahi, tena kwa nia njema, kumweleza Bi. Fikirini ... kuhusu uvumi kwamba mume wake alikwenda gerezani na kuchukua mamilioni ya fedha kwa Bw. Nyari na hivyo kumshauri awe mwangalifu zaidi”! Katika uteuzi wa majaji uliofanywa na Rais Kikwete mwezi Juni mwaka huu, Bi. Patricia Fikirini naye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

      Wapo wanaoweza kusema kwamba Bi. Khaday hakupatikana na hatia yoyote na kwa hiyo haikuwa makosa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Aidha, inaweza kudaiwa kwamba Bi. Fikirini hajawahi kutuhumiwa kwa kosa lolote la maadili na kwamba ‘uvumi’ pekee hautoshi kumnyima mtu mwenye sifa haki ya kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kwa wenye hoja za aina hii jibu langu ni kwamba kiwango cha ‘sifa maalum’ kinachotakiwa na Katiba kwa mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ni mtu ambaye “... kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu....” Kiwango hiki ni cha juu kiasi kwamba kutokuwa na hatia pekee haitoshi kumfanya mhusika kuwa ‘kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.’ Kwa maoni yangu, mtu aliyeundiwa uchunguzi wa kimaadili au ambaye kuna uvumi unaomhusisha na rushwa ‘hafai kwa kila hali’ kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu. Majaji Khaday na Fikirini wapo kwenye kundi hili.

      JAJI ALOYSIUS MUJULIZI

      Jaji Aloysius Mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishirini walioteuliwa Majaji wa Mahakama Kuu mwezi Februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili ya Ishengoma, Masha, Magai & Mujulizi Advocates (IMMMA) ya Dar es Salaam. Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. mnamo tarehe 18 Machi 2004. IMMMA Advocates vile vile walikuwa mawakili wa Tangold Ltd.

      Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishia mabilioni ya fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2005 na 2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 10, 2005 kampuni ya Deep Green Finance ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania. Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya Tangold Ltd. ililipwa dola za Marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya EPA. Nyaraka zilizowasilishwa BRELA na mawakili wa IMMMA Advocates na kusainiwa na Gavana wa Benki Kuu wa wakati huo Daudi Ballali tarehe 20 Mei 2005 zinaonyesha kwamba Tangold Limited ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka Jamhuri ya Mauritius. Haya yote yalitokea wakati Jaji Mujulizi akiwa wakili mwenza wa IMMMA Advocates.

      ‘SIFA MAALUM’ ZENYE SHAKA

      JAJI WA RUFAA MBAROUK SALIM MBAROUK

      Mbarouk Salim Mbarouk aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo Jaji Mbarouk alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya Katiba: “Majaji ... wa Rufani watateuliwa na Rais, kwa kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ... zilizoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano.”

      Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984, “mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahkama ya Rufaa kutoka Mahkama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba.” Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama inavyotakiwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba. Jaji huyu ana stashahada ya juu ya sheria (Post Graduate Diploma in Law) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha nchini Uingereza.

      Uteuzi wa Jaji Mbarouk kuwa Jaji wa Rufaa ulileta minong’ono mingi katika taaluma ya sheria kiasi kwamba marehemu Wakili Leopold Kalunga anasemekana kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka uteuzi huo utenguliwe. Hata hivyo, Wakili Kalunga alifariki kabla ya shauri lake kusikilizwa na kwa hiyo liliondolewa mahakamani. Aidha, monong’ono hiyo ilimfanya Jaji wa Rufaa Mbarouk kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambako bado ni mwanafunzi hadi ninapoandika Addendum hii.

      MAJAJI ‘WALIOTOLEWA MITAANI’

      Katika Maoni ya Kambi tulidai kwamba “... sasa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na - kwa sababu hiyo - hawajafanyiwa vetting yoyote na mamlaka hiyo ya kikatiba....” Ukiacha uteuzi wa Jaji wa Rufaa Mbarouk ambao haubanwi na masharti ya Ibara ya 109(1) na 113(1)(a) ya Katiba, majaji wengine waliotajwa kwenye Addendum hii hawakupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Majaji wengine ambao pia hawajawahi kupendekezwa na Tume hiyo ni pamoja Fatuma Massengi, Mary Sumari, Imani Mkwawa-Aboud na Sekela Mushi.

      Last edited by palalisote; 18th August 2012 at 13:56.
      Ogah, JokaKuu, Richard and 116 others like this.

    2. Miaka 50

    3. #381
      Jangakuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2012
      Posts : 351
      Rep Power : 427
      Likes Received
      127
      Likes Given
      238

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Pamoja sana T L. Huwez kumfananisha Nnauye

    4. #382
      Bijou's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2011
      Posts : 382
      Rep Power : 567
      Likes Received
      65
      Likes Given
      126

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Uadilifu: "MY WIFE OUGHT NOT EVEN TO BE UNDER SUSPICION" aka MKE WANGU HAPASWI HATA KUTUHUMIWA JULIUS CEASER ,


      Kwa taarifa hii, TAFAKARI!!!!!!!!!!!

    5. #383
      SUMLEY's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th March 2011
      Posts : 13
      Rep Power : 417
      Likes Received
      1
      Likes Given
      2

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Kinachosikitisha haya yote yanatokea sehemu ambayo ilitakiwa ndo ipelekewe matatizo hayo ili iyaamue! Jaji Agustino Ramadhani alikua katika nafasi nzuri ya kulimaliza tatizo hilo sasa sijui na yeye nini kilimkuta!

    6. #384
      Dina's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th September 2008
      Location : Ulimwenguni
      Posts : 1,124
      Rep Power : 768
      Likes Received
      296
      Likes Given
      174

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Mimi nafikiri umefika wakati wa sisi kuiga jirani zetu Wakenya kuwaamuru hawa waheshimiwa kutetea nafasi zao tena, atakayeonekana hamne hamne na aachane na kazi ya sheria. Na hizo interview tuzione live TBC!

    7. #385
      MpendaTz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th May 2009
      Posts : 1,073
      Rep Power : 724
      Likes Received
      146
      Likes Given
      537

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Quote By Dina
      Mimi nafikiri umefika wakati wa sisi kuiga jirani zetu Wakenya kuwaamuru hawa waheshimiwa kutetea nafasi zao tena, atakayeonekana hamne hamne na aachane na kazi ya sheria. Na hizo interview tuzione live TBC!
      Wenzetu wako mbali sana. Hayo yaliwezekana baada ya paosition ya CJ kutangazwa wazi na watu wakaapeleka maombi na kufanyika public vetting! Sisi bado sheria na hukumu nyingi zinatokea kwenye corridor za Ikulu. Na ndio madhara yake hayo. Jaji Warioba na timu yake washauriwe wakatembelee wenzetu kabla hata ya kusema wamemaliza kazi. Na wasije na uwongo wa kutuambia eti wamelinganisha wakaona mfumo wetu ni bora. Wananchi watawazomea!

    8. FemaTV & Radio

    9. #386
      NdasheneMbandu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd January 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 0
      Likes Received
      294
      Likes Given
      8

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Nilijua tu kwamba mpiganaji Tundu hawezi kubwatuka kama akina lusinde na mwigulu. Nilijua anaongea mambo yenye supporting data. Zaidi ya yote nilijua nyuma yake wapo majaji na wanasheria wasomi wanaokereheka na teuzi zinazotolewa kama muuza njugu anavyowaonjesha wateja wake. Sasa kwa data hizi bunge la magamba na serikali yake watasema nini!!! Hakika wataumbuka.

      Mwisho naomba niseme waziwazi bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno ni kwamba alichofanya rais wa sasa ni kuwajaza waumini wenzie bila kujali uwezo na matokeo yake ameumbuka. Tafakari.

    10. #387
      BelindaJacob's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2008
      Location : Санкт-Петербург
      Posts : 5,251
      Rep Power : 4146
      Likes Received
      1822
      Likes Given
      1289

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      mwenye macho kweli haambiwi tazama!!
      Bésame Mucho...!!!

    11. #388
      Mbwa Mpole's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th July 2012
      Posts : 11
      Rep Power : 346
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Lisu kazi nzuri sana, tafadhari ripoti hii ichapishwe kwenye gazeti zinalouzwa sana ili wananchi wengi waelewe hali ilivyo mbaya, maana tatizo kubwa la maendeleo nchi hii saa ni mfumo mbaya wa uteuzi wa viongozi wa serikali.

    12. #389
      Irizar's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th October 2009
      Posts : 187
      Rep Power : 527
      Likes Received
      11
      Likes Given
      0

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Asante sana Tundu Lissu kwa kutufundishaa na kuzidi kutuonyesha hiyo miozo ya CCM...

      Aibu yao, aibu yaoooooo....

    13. #390
      George Jinasa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2010
      Posts : 339
      Rep Power : 508
      Likes Received
      29
      Likes Given
      5

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Quote By Irizar
      Asante sana Tundu Lissu kwa kutufundishaa na kuzidi kutuonyesha hiyo miozo ya CCM...

      Aibu yao, aibu yaoooooo....
      RIPOTI MAALUMU YA TUNDU LISU: MATUMIZI YA BUNGE KUDHALILISHAMAHAKAMA NA MAJAJI WAKE?

      Na George Jinasa



      Kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 (“Katiba”) Bungelinayo mamlaka ya kuisimamia na kuishauri Serikali. Mamlaka haya hutumiwa naBunge katika vikao vyake mbalimbali kwa kujadili bajeti na taarifa mbalimbaliza Wizara na inapobidi kutunga sheria zinazolenga katika kurekebisha kasorokatika mwenendo wa Serikali. Kwa mujibu wa ibara ya 107 A, mamlaka ya kufasiri sheria nakutoa haki yako mikononi mwa Mahakama. Hakuna hata sehemu moja katika Katiba ambapo Bunge limepewa mamlakayoyote ya kuisimamia na kuishauri Mahakama. Nafasi ya Bunge kuirekebishaMahakama katika mfumo wa “checks and balance”, ni kwa njia ya kutunga sheria. Na hilo limefanyika maranyingi japo mara nyingine limetumika vibaya kama pale Mahakama Kuuilivyobatilisha kifungu katika Sheria ya Uchaguzi kilichokuwa kinazuia mgombeabinafsi na Bunge likajibu kwa kurekebisha Katiba na kuliingiza sharti hilokatika Katiba. Kwa kufanya hivyo, suala la mgombea binafsi lilifanywa kuwa lakikatiba badala ya sheria ya Bunge kama ilivyokuwa mwanzo. Madhara ya uamuzi huo wa Bunge yalionekana katika rangi yakesawia katika kesi maarufu ya MwanasheriaMkuu wa Serikali dhidi ya Mtikila ambapo Mahakama ya Rufaa ilijiona hainamamlaka ya kubatilisha kifungu cha mgombea binafsi katika Katiba kwa misingikwamba Katiba ipo juu ya Mahakama.

      Kuna maswali mengi ya kifalsafa yanayozuka kutokana na kesi hiyo bali kwa minajili ya makala yangu hii nisingependakujielekeza kwayo. Katika nchi zinazooongozwa na utawala wa sheria kama Tanzania,mamlaka ya kusikiliza tuhuma dhidi ya watu na kutolea maamuzi ni ya Mahakama.Bunge halina mamlaka hayo isipokuwa tu katika maeneo machache ya kiutawalaambapo mamlaka ya Mahakama yamekasimiwa kwa njia ya Sheria. Ni mhimu pia kugusia kwamba kwa mujibu wa ibara ya 13 (6) (a) yaKatiba, maamuzi yoyote yanayoathiri haki au wajibu wa mtu hayawezi kufanyika bila ya yeyekusikilizwa.Hvi karibuni imekuwa kawaida kusikia masuala mbalimbaliyanayowahusu watu binafsi yakijadiliwa Bungeni na hatimaye wahusika kudhalilikana kuhukumika na ile hali hamna utaratibu wowowte wa kisheria unaowaruhusu waokwenda Bungeni na kukanusha tuhuma dhidi yao kwa ushahidi. Ipo mifano mingi yakuthibitisha kauli yangu lakini kwa minajili ya andiko hili ninapenda kujikitakwenye taarifa iliyoripotiwa na gazeti la Jamhuri la toleo ya August 14-20yenye kichwa cha nabari “Majaji ‘vihiyo’ watajwa”. Ndani ya taarifa hiyoiliyorejewa kama “Ripoti Maalumu” pamoja na mambo mengine, majina ya baadhi yamajaji yalitajwa na kuhusishwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo za rushwa,upendeleo, kutokuwa na sifa ya ujaji na ukiukwaji wa sheria. Taarifa hizo,mwandishi anasema, amezinukuu neno kwa neno kutoka katika utetezi wa mheshimiwa Tundu Lisu (Mbunge) aliouwasilishakatika Tume ya Maadili ya Bunge.

      Suala la kujiuliza kwanza ni kama Kamati ya Maadili ya Bungeinauwezo wa kuamua kama tuhuma hizo zimethibitika au la? Kama nilivyoeleza hapo mwanzo jibu ni hapana.Bunge, achilia mbali kamati zake, halina mamlaka yoyote ya kikatiba yakuichunguza Mahakama wala majaji wa Mahakama Kuu. Tume ya Maadili ya Bunge ni chombo nusumahakama (Quasi-Judicial Board) kilichokasimiwa mamlaka ya kimahakama yakusikiliza mashauri ya kinidhamu yanayowahusu wabunge. Hakina mamlaka yoyote yakuthibitisha tuhuma dhidi ya majai wa mahakama kuu au maofisa wowowte wamahakama. Tuhuma hizo nzito dhidi ya majaji wa Mahakama Kuu japo inadaiwakwamba zimepelekwa katika Kamati ya Madili ya Bunge kama utetezi wa Mbunge,zimeshasambazwa kwa umma hata kabla hazijajadiliwa na Kamati hiyo. Kwa kufanyahivyo ni wazi kwamba majaji waliotajwa pamoja na idara nzima ya Mahakamawamehukumiwa hata kabla tuhuma hizo hazijathibitika. Ni wazi kabisa kwambaimani ya watu katika chombo hiki mhimu cha kutoa haki itashuka.

      Ni mhimu kusema hapakwamba tuhuma alizotakiwa kuthibitisha katika Kamati ya Maadili ya Bunge ni juuya uwepo wa majaji wanaoteuliwa na Raisi bila kupitia Tume ya Utumishi wa Mahakama. Badala yakujikita katika kuthibitisha madai hayo mheshimiwa Tundu Lisu aliamua kutoatuhuma nzito mpya dhidi ya baadhi ya majaji wa Mahakama Kuu.

      TUHUMA ZENYEWE

      1. MAJAJI KUONGEZEWA MKATABA WA AJIRA KINYUMECHA KATIBA


      Madai ya mheshimiwa Tundu Lisu katika nukta tajwa hapo juu nikwamba majaji wanaoongezewa muda wao baada ya kufikia muda wa kustaafu kwalazima (yaani miaka 60 kwa Mahakama Kuu na 65 kwa Mahakama ya Rufaa) si majajikwa mujibu wa ibara 110 na 120 ya Katiba maana jaji anapostaafu kiapo cha ujajikinaisha na kuufanya ujaji wa mkataba kuwa nje ya kiapo.

      Kwa mujibu wa taarifahiyo, hoja ya mh. Tundu Lisu katika nukata hii pia inaungwa mkono na tamkolililowahi kutolewa na mh. Jaji Luanda (kabla hawaja Jaji wa Mahakama ya Rufaa)na mheshimiwa Jaji Mkuu Staafu Ramadhani (kabla hajawa Jaji Mkuu). Ibara ya 110 (3) ya Katiba inasema kwamba “Iwapo Raisi ataona kuwakwa ajili ya manufaa ya umma inafaa Jaji alietimiza umri wa miaka sitiniaendelee kufanya kazi, na huyo Jaji mwenyewe anakubali kwa maandishi kuendeleakufanya kazi, basi Raisi aweza kuagiza kuwa Jaji huyo aendelee kufanya kazi kwamuda wowowte atakaotaja Raisi”. Kifungu cha 120 (3) kina maneno kama hayokuhusiana na Majaji wa Mahakama ya Rufaa ila tu muda wao wa kustaafu kwa lazimani miaka sitini na tano. Maneno yaliyomo katika ibara hizo mbili kama yalivyo, yanaruhusuJaji aliyefikia miaka 60 kuendelea kuwa jaji kwa kipindi Raisi atakachoongezaili mradi tu iwe ni kwa maslahi ya umma na jaji mhusika aridhie. Kwa maoniyangu, sioni tatizo lolote kwa jaji kuongezewa muda wa ujaji baada ya kufikiamuda wa kustaafu ili mradi masharti ya ibara ya 110 (3) na 120 (3) ya Katibayanazingatiwa. Ibara za 110 (3) na 120 (3) hakijaweka ukomo wa muda ambao Raisianaweza kumuongezea Jaji aliyestaafu na wala havijaweka tafsiri ya neno “maslahi ya umma”.

      Hiyo inamaana kwamba suala la kuamua kama kuna maslahi yaumma au la katika kuongeza muda lipo katika “discretion) ya Raisi. Maoni ya mh Tundu Lisu na watu wengine wanayomuunga mkono katikasuala hili ni maoni ya kifalsafa zaidi ambapo wasomi wa fani ya sheria wanawezakuwa na maono tofauti. Na wala maoni ya jaji mkuu mstaafu na jaji wa mahakamaya Rufaa hayakutolewa kama sehemu ya uamuzi, bali ni maoni kama maoni ya raiayeyote. Ndio maana mheshimiwa Ramadhani anakiri uwezekano wa hoja zakekuathiriwa na chimbuko lake la kijeshi. Lakini Katiba kama ilivyo inahalalishanyongeza ya muda wa ujaji kwa maslahi ya umma kwa kadili Raisi anavyoonainafaa.

      Maamuzi ya kuongeza muda, kwa kadili nijuavyo, hufanywa kabla muda wakustaafu haujafika. Na hivyo Jaji anapoongezewa muda wa ujaji anakuwa badondani ya kiapo kile kile. Isitoshe, ya Jaji Ramadhani na wenzake, kama yalivyonukuliwakatika gazei la Jamhuri la tarehe la August 21-27/2012, kwenye makala yenye kichwa cha habari “RIPOTI MAALUMU MAJAJI MAJI SHINGONI”, hayapingi jaji kuongezewa muda baada ya kufikia umri wakustaafu, bali yanapinga kuwepo ajira ya mkataba baada ya jaji kustaafu kwa misingikwamba ajira ya Mkataba inamuondolea jaji kinga ya ajira “security of tenure” nakuiweka ajira yake chini ya sheria za kawaida za Mkataba.

      Ni hoja yao pia kwamba ajira hiyo inahesabika kama ajira mpya maana jaji anakuwa ameshapewa marupurupu yake baada ya kustaafu. Kwamaneno yake mwenyewe, mheshimiwa Jaji Mstaafu Ramadhani amenukuliwa naaliejiita “mwandishi wetu” katika ukulasa wa 3 wa gazei la Jamhuri akisemakama ifuatavyo:-‘ Tafsiri yangu hapa ni kuwa, Raisi anasemaJaji “XYZ” badala ya kustaafu akitimiza umri wa miaka 65 na kuongezea miaka ABCuendelee kufanya kazi na utastaafu umri wa miaka OPQ. Hii haina maana kuwa jajiwa Rufaa anaehusika atastafu baada ya kutimiza miaka 65 na kupata marupurupuyake halafu aajiriwe kwa Mkataba. Tafsiri yangu kuwa aendelee na kazi mfululizona aje kustaafu baada ya kicho kipindi cha ziada alichopewa. Akistaafu nakupata haki yake haendelei na kazi bali anaanza ajira mpya ya mkataba.” Kutokana na taarifa kutoka katika vyanzo vya kuamika, majajiwanaoendelea kufanya kazi baada ya muda wa kustaafu, huongezewa muda na Raisikabla ya muda wa kustaafu na sio kusaini Mkataba baada ya kustaafu. Kwa mfano,muda wa nyongeza wa mheshimiwa Jaji Kiongozi unaolalamikiwa, ulitolewa kwabarua ya tarehe 13.06.2012 yenye kumbu kumbu namba SAB289/482/01/120 wakatimuda wake wa kustaafu ulikuwa uwe tarehe 20/07/2012, takribani mwezi mmojakabla hajapewa barua ya kuongezewa muda. Hamna Mkataba wowote aliousaaini walaRipoti ya mheshimiwa Tundu Lisu haijaonyesha mkatba huo.Ni mhimu pia kusisitiza kwamba hata Ripoti ya “Kikundi Kazi”kama ilivyonukuliwa na gazeti tajwa hapo juu, hamna sehemu yoyote ambaponyongeza ya muda wa ujaji imepingwa.

      Kinachopingwa katika Ripoti hiyo ni uwepowa ajira ya mkataba kwa jaji baada ya kustaafu. Inashangaza hata hivyo kuona kuwajapo katika Ripoti hiyo inadaiwa kwamba mheshimiwa Jaji Lyimo baada ya kustaafualiingia ajira ya Mkataba, kielelezo kilichoambatanishwa sio Mkataba bali nibarua ya nyongeza ya muda wa ajira kitu ambacho kwa mujibu wa Jaji Ramadhani naRipoti ya Kikundi Kazi, hakina matatizo ya kisheria. Katika hali ya kushangaza kidogo, suala la kuongezewa muda waujaji linahusishwa na malalamiko ya wale wanaojiita “wanamhimili wa Mahakama”kwamba Jaji Kiongozi ameshindwa kumudu mamlaka yake kwa kutishia kumhamishahakimu mmoja alietoa maamuzi ambayo hakuridhika nayo. Katika Ripoti hiyo hiyo,uamuzi wa Jaji Kiongozi kumhamisha hakimu kwa maamuzi asiokubaliana nayounakubaliwa na kutumika kumhukumu wakili aliehusika katika kesi hiyo kuwaamekiuka maadili na hakustahili kuwa Jaji.

      Katika Ripoti yakemheshimiwa Tundu Lisu hakutoa uthibitisho wowote kwamba kuhamishwa kwa hakimuhuyo ilikuwa ni adhabu. Nijuavyo mimi, uhamisho kwa mahakimu na majaji niutaratibu wa kawaida wa kazi na wala hamna hakimu yoyote mwenye hati miliki yakuwa Dar es Salaam. Wala mahakimu walioko mikoani hawako huko kwa sababu yaadhabu na walipo Dar es Salaam hawako Dar es Salaam kwa sababu ni weledi zaidiya walio mikoani.Ripoti yake inaonesha kwamba maamuzi ambayo Jaji kiongozihakukubaliana nayo, yanahusu kesi aliyoiita maarufu ya “kibaghalashia”.Kumbukumb u zangu zinaonesha kwamba kesi hiyo iliwahi kuripotiwa kwa mshangaokatika magazei kadhaa.

      Kwamba hakimu mmoja amemhukumu mtu kwenda jela kwa kuvaakibaghalashia Mahakamani. Kwa nchi kama Tanzania ambako vazi la kibaghalashia ni vazirasmi katika baadhi ya dini, haikutegemewa kwa hakimu huru na mwenye busara kumfunga mtu kwa kuvaakibaghalashia Mahakamani. Kwa namna suala hilo lilivyovuta hisia za watu wengihapa nchini na mbaya zaidi hisia za kidini, nisingeshangaa hata kidogo kamahakimu huyo angechukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu achilia mbali kuhamishwa.Mahaka kama chombo cha kutoa haki kinapaswa kujiweka katika hali ambayo kilamtu atakiona kama chombo huru kisichokuwa na muegemeo wowowote wa kisiasa,kidini au kikabila. Maamuzi mabovu kama hayo hayakupaswa kutolewa na chombo cha Mahakama.

      2. MAJAJI KUTOKUWA NA MAADILI

      Katika nukta tajwa hapa juu, Tundu Lisu ametoa mfano wa majajiwanne ambao nitawazungumzia bila kutaja majina yao.Jaji mmoja analaumiwa kwa sababu kampuni ya uwakili aliokuwaakifanyia kazi kabla hajakuwa Jaji ilikuwa ni mawakili wa kampuni inayotuhumiwakujihusisha na ufisadi. Tuhuma hizi zinashangaza sana maana katika maadili yakazi za uwakili wakili hazuiwi kumtetea mtu anaetuhumiwa kuwa mhalifu. Na kwa mujibu wa sheria za nchi, mtuhumiwa yoyote wa makosamakubwa kama mauaji na uhaini hata kama hana uwezo, ana haki ya kutetewa. Kwa hiloserikali hutenga mamilioni ya pesa kuwalipa mawakili kwaajili ya kuteteawatuhumiwa wa mauwaji. Kama hoja za mh. Tundu Lisu itakuwa sawa, ina maanakwamba mawakili wote waliowahi kuwatetea wauwaji na mwishowe wakaonekana nahatia, hawatakuwa na sifa ya kuwa majaji.

      Haki ya kupata uwakilishi wa kisheriaanaizungumziaje mheshimiwa Tundu Lisu? Ina maana watu wenye hatia hawana hakiya kutetewa na kupata huduma za kisheria? Nijuavyo mimi hata mhalifu anahaki yakuhukumiwa kwa mujibu wa sheria na kazi ya wakili inaweza kuwa kuhakikishamhalifu haonewi kwa kupewa adhabu kubwa zaidi ya anayostahili kwa mujibu washeria. Nilitegemea kuona katika Ripiti ya mh. Tundu Lisu sehemu yoyoteinayoonesha namna mheshimiwa huyo alivyohusika yeye mwenyewe binafsi na tuhumahizo wakati bado anafanya kazi ya uwakili katika kampuni husika. Au japokuwaangeonyesha namna kampuni yake ya zamani ya uwakili ilivyohusika na uhalifu nakama mheshimiwa pia alikuwa na habari kuhusiana na uhalifu huo.

      Vinginenvyosioni kama mheshimiwa Tundu Lisu alikuwa na uhalali wowote wa kuliingiza jinala wakili huyo katika utetezi wake.Jaji mwingine ametuhumiwa kwa kupinga amri ya mahakama kwa njiaya mapitio (Review). Kama anavyoeleza kwenye Ripoti yake, Jaji husika enzi zilealipokuwa bado wakili aliwahi kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama na kuupingakwa njia ya mapitio na hatimaye mahakama ikabatilisha uamuzi wake wa kumfungamshitakiwa bila faini na badala yake kuamua kwamba atumikie kifungo au atoefaini. Mh. Tundu Lisu hasemi kama kifungu cha sheria kilichotumika kumhukumshitakiwa hakikuwa na “options” hizo. Sasa sioni kwa nini suala hili limechukuwa sura ya kimaadilibadala ya taratibu za kawaida za kutetea wateja. Kama suala ni kukoseakiutaratibu katika kupinga uamuzi huo, hayo ni masuala ya kawaida maana jaji auwakili si Mungu ajue kila kitu. Ndio maana mara nyingi hukumu za majaji waMahakama Kuu huwa zinapingwa Mahakama ya Rufaa kwa kujenga hoja kwamba Jajimhusika alikosea ima kisheria au kimantiki. Hujawahi kusikia jaji yoyote anahukumiwakutokuwa na maadili au kutokuwa na uwezo kwa sababu maamuzi yake yalitenguliwa namahakama ya juu kwa sababu ya kuwa na makosa. Maamuzi ya Mahakama Kuu baada yakulifanyia marejeo jalada hilo hayaoneshi hata kidogo kama jaji anaetuhumiwaalifanya jambo lolote la kukiuka maadili ya uwakili. Zaidi ya hapo, kumbukumbukatika jalada zinaonesha kwamba hata mtu aliewasilisha hoja za mapititio mbeleya mheshimiwa hakimu wa wilaya alikuwa ni wakili mwingine aliebeba mikoba yajaji anaetuhumiwa.

      Jaji mwingine ametuhumiwa kuwahi kuhusika katika kumwandikiahakimu hukumu enzi za uwakili wake. Hamna ushahidi wowote uliotolewakuthibitisha tuhuma hizo na wala Jaji katika hukumu husika hakumuona Jaji huyokuwa na hatia yoyote. Ni vizuri pia kuzingatia hapa kwamba sifa maalumu za jajikwa mujibu wa ibara ya 109 (8) ya Katiba ni sifa zilizotajwa katika Sheria yaMawakili. Kwa mana hiyo kama tuhuma dhidi ya Jaji huyo zingesimama,angeondolewa uwakili kabla hajawa Jaji. Ni jambo la mhimu kuzingatia hapakwamba kutuhumiwa kosa sio kutenda kosa. Kwa kulilinda hilo,Katiba katika ibara ya 13 inaweka dhana ya mtu kutokuwa na hatia hadi Mahakamaimithibitishe kuwa hivyo. Ndio maana hamna mtu anaeweza kusema kwa sasa kwambaTundu Lisu ni mtovu wa nidhamu ya ubunge mpaka Kamati ya Maadili ya Bungeitakapomuona ana hatia. Ni maneno hayo hayo naweza kusema kuhusiana na Majajiwaliotuhumiwa kutokuwa na sifa kwa sababu waliwahi kuundiwa tume ya kuchunguzaukiukwaji wa maadili. Utetezi wa Tundu Lisu unaonesha kwamba walishinda katikatuhuma zao na kuonekana hawana hatia. Katika kazi ya ujaji na uhakimu ni marangapi watu wanaopoteza kesi kuwazushia majaji tuhuma ili mradi wafanikiwekatika kesi zao? Mara ngapi majaji wanaombwa kujitoa katika kesi kwa sababu yamigogoro ya kimaslahi na wkati tuhuma hizo ni za kisanii tu.

      3. JAJI KUAJIRIWA BILA KUWA NA SIFA KITAALUMA

      Jaji anaelalamikiwa kuhusina na tuhuma tajwa hapo juu inadaiwakwamba kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Jaji wa MahakamaKuu ya Zanzibar. Mh Tundu Lisu anakiri kwamba sifa za kitaaluma za mtu kuwaJaji Tanzania Zanzibar ni sawa na za Tanzania bara. Ibara ya 118 (3) ya Katibainabainisha wazi kwamba Raisi kwa kushirikiana na Jaji Mkuu anaweza kumteuwamtu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa yule ambaye anasifa ya kuteuliwa kuwa Jajiwa Mahakama Kuu ya Tanzania au Mahakama Kuu ya Zanzibar. Jaji mhusika wakatianateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa alishakuwa Jaji wa Mahakama Kuu yaZanzibar. Mh. Raisi na Jaji Mkuu hawakuwa na sababu yoyote ya maana kutiliashaka uteuzi wake kuwa Jaji wa MahakamaKuu ya Zanzibar.

      4. MAJAJI WA MITAANI


      Katika utetezi wake mheshimiwa Tundu Lisu ametaja baadi yamajaji kuwa waliajiriwa bila majina yao kupitia Tume ya Utumishi wa Mahakamakwaajili ya uchunguzi. Bahati mbaya chanzo cha taarifa hiyo hakijaonyeshwa. Uchunguziwangu nilioufanya unaonyesha kwamba majaji wote wane wanaotuhumiwa sio majajiwa mitaani na uteuzi wao ulipata Baraka za Tume ya Utumishi wa Mahakama. Wakatikwa mara ya kwanza tuhuma hiyo inatolewa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambayeni mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo alikanusha. Wajumbe wengine katika Tume hiyo ni pamoja na Jaji Mkuu na Jaji Kiongoziambao kwa namna yoyote wasingekubali mtu ateuliwe Jaji bila kupitia katika Tumeyao. Hatuoni ni kwanini mhesimiwa Tundu Lisu kabla hajatoa tuhuma nzito kamahizo hakuona umhimu wa kuonana na makamishina wa Tume hiyo na kupata taarifasahihi.Kumbu kumbu zinaonesha kwamba mmoja kati ya majaji wanaotuhimiwakuwa wa mitaani, kabla ya kuteuliwa kuwa jaji alikuwa ni Mkurugenzi Msaadizikatika ofisi za Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania. Alipohitimi shahada ya sheriaajira yake ya kwanza ilikuwa ni mwanasheria wa serikali na alipanda kidogokidogo hadi akafikia cheo cha mkurugenzi msaidizi katika ofisi nyeti katikamasuala ya sheria ya DPP. Ni jambo la mzaha mtu kama huyo kuitwa “jaji wamitaani”Jaji wa pili anaetuhumiwa alianza kazi kama mwanasheria waserikali mwaka 1993 baada ya kuhitimu shahada ya sheria. Mpaka anateuliwa kuwajaji wa Mahakama Kuu alikuwa ni Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Sera wa Utumishi.Pamoja na kazi kubwa alizozifanya kulitumikia taifa katika nafasi mbalimbalianaishia kuitwa jaji wa mitaani.Jaji wa tatu anaetuhuumiwa kwa hili alianza kazi katika Idara yaMahakama mwaka 1974 kama Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo. Mda mchache kablahajateuliwa kuwa Jaji alishapanda hadi kufikia ngazi ya Ukurugenzi wa Mahakamaza Mwanzo Tanzania, nafasi aliteuliwa namheshimiwa Jaji Mkuu wa wakati huo Samata baada ya kuridhika na uadilifu wakena uwezo wake wa kazi. Mtu kama huyu kuna uhalali gani wa kumwita jaji wamitaani?Wa mwisho katika tuhuma hii mpaka anateuliwa kuwa jaji waMahakama Kuu mwaka 2009 alikuwa Mkurugenzi wa Mahakama za Wilaya mpaka Mahakamaya Rufaa Tanzania. Na katika maisha yake yote ya ajira za umma amekuwa akifanyakazi kwa uaminifu mkubwa katika Idara ya Mahakama. Ni bahati mbaya sanawanasiasa wameamua kumpa jina la jaji wa mitaani.

      5. TUEPUKE KUELEKEZA SIASA KATIKA IDARA YA MAHAKAMA


      Moyo wa nchi yoyote inayotawaliwa na utawala wa sheria ni mahakama. Mahakama ni kimbilio la wote na ni mlinzi na mtoaji mkuu wa haki.Hili linafanikiwa pale mahakama inapoheshimiwa na kuaminiwa kama chombo huru kisichofungamana na makundi yoyoteya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Kwa kuzingatia umhimu wa hilo, Katiba imekataza bayana kwamaofisa wa mahakama kuwa na uhusiano na vyama vya kisiasa. Kiapo cha ujaji nauhakimu kinawataka majaji katika kufamya kazi zao kuwa huru na kutoa maamuzibila kuathiriwa na upendeleo wa aina yoyote. Zaidi ya hilo, Katiba imewekaibara zinazolinda uhuru wa Mahakama na kuondoa uwezekano wowote wa kuingiliwana vyombo vyenye nguvu sana kama serikali na Bunge. Hata pesa zinazotumikakulipa mishahara ya majaji na mahakimu hazipaswi kuwa pesa za bajeti ya kawaidazinazojadiliwa na kupitishwa na Bunge. Dhamira ya sheria hapa ni kuzuiauwezekano wa Bunge kuingilia uhuru wa Mahakama kwa sababu wana uwezo wa kuamuajuu ya mishahara na marupurupu ya majaji.Pamoja na uhuru mkubwa mahakama iliyopewa kwaajili ya kufanyamaamuzi yake yawe ya haki, Mahakama haijawekwa kuwa juu ya sheria. Maamuzi yaoyanapaswa kuwa kwa mujibu wa sheria na pale jaji anapokosea kuna utaratibumaalumu wa kumrekebisha na hata kumvua kofia ya ujaji.

      Kama jaji anaonekanakuteuliwa kinyume cha sheria, Katiba na sheria mbalimbali za nchi zimewekautaratibu ambao kwao maamuzi ya uteuzi wa jaji yanaweza kubatilishwa. Hamna uhalaliwowote kwa wanasiasa kutumia Bunge na vyombo vya habari kuichafua Mahakama namaofisa wa Mahakama. Ni vizuri watanzania tukajihadhari na kuiingiza siasa katikaMahakama. Tuache mahakama ziendelee kuwa huru maana ni kimbilio letu sote. Kamakuna mapungufu katika Idara ya Mahakama (na of course hayawezi kukosekana)tutumie taratibu zinazokubalika kisheria kuyarekebisha.

      Kulya likes this.

    14. #391
      Chakunyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Location : Masasi
      Posts : 751
      Rep Power : 561
      Likes Received
      134
      Likes Given
      283

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Yaani inauma sana kuona uozo wa wazi halafu mtu anaamua kubisha tu ili kulinda kazi na nafasi yake! tunaliangamiza taifa kwa kutokuwa wazalendo.

    15. #392
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,744
      Rep Power : 1317
      Likes Received
      720
      Likes Given
      147

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Tunamshukuru Tundu Lissu kwa kutusanuwa kujua ukweli wa Mahakama ilivyoingiliwa na wanasiasa na serikali huyo anayebisha abishe lakini wananchi tumejua ukweli ni taabu kubwa nchi hii kupata haki yako ,nchi ya dhuluma,unyonyaji,ukatili na wizi uliokithiri,ufujaji wa mali za umma na upuuzaji wa wananchi

    16. #393
      Nsabhi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd February 2011
      Posts : 630
      Rep Power : 543
      Likes Received
      69
      Likes Given
      123

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Hapa Jk na serikali yake hawatoki!
      Paw likes this.

    17. #394
      Dr-of-three-Phd's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th October 2010
      Posts : 180
      Rep Power : 471
      Likes Received
      19
      Likes Given
      397

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Hii kitu imeenda shule.... lazima wajiulize.....
      "A nation or civilization that continues to produce soft-minded men purchases its own spiritual death on the installment plan" Martin Luther King, Jr.

    18. #395
      George Jinasa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th September 2010
      Posts : 339
      Rep Power : 508
      Likes Received
      29
      Likes Given
      5

      Default

      Quote By Chakunyuma
      Yaani inauma sana kuona uozo wa wazi halafu mtu anaamua kubisha tu ili kulinda kazi na nafasi yake! tunaliangamiza taifa kwa kutokuwa wazalendo.
      Nudge yangu hapa tunabadilishana mawazo. Mh lissu ametoa maoni yake hamna hata sehemu moja nimeyarejea Kwa maneno ya kejeli. Nilitajia ungeonesha udhaifu na mapungufu katika ripoti yangu kama mimi nilivyoonyesha katika ripoti ya kaka yangu lisu. Badala yake unaniuzia kesi ya kwamba natetea kazi yangu. Bila kuitaja.

      Kwa msingu watanzania tutafika kweli? Mabadiko ya kukubaliana na kila anachokisema mh lisu kwa vile ni mbunge wa upinzani hayana tofauti na enzi ya zidumu fikra za kwenye kiti. Kila mtu anapas

    19. #396
      gogomoka's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2008
      Posts : 69
      Rep Power : 571
      Likes Received
      49
      Likes Given
      240

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      George Jinasa,

      Hebu labda tumsome another Learned friend - Fatma Karume (mmoja wa beneficiary wa system yetu). Sijui na yeye amefuata fikra za mwenyekiti?

      If judges` appointment remains shrouded in secrecy, Lissu will be believed
      By Fatma a. Karume
      10th September 2012EmailPrintComments
      MP Tundu LissuIt has been a woeful few weeks for the Judiciary in Tanzania. Transparency International named it as the 2nd most corrupt institution in Tanzania; a member of Parliament accused it of comprising of legally and intellectually incompetent judges; Tugendhat J, a judge of the High Court of England, Queen’s Bench Division in Reginald Mengi v. Sarah Hermitage, ordered Mengi to pay into court a sum in excess of USD 3 million in order to secure Hermitage’s legal costs on the ground that the Courts in Tanzania are so riddled with corruption that he would not subject a British citizen sued in England by a Tanzanian without assets in England, to the unnecessary risk of enforcing an English judgment in courts known for their corruption.

      No doubt, the rest of the commonwealth will soon be relying on the same judgment to exact exorbitant security for costs from any Tanzanian intending to make a claim in their courts against their citizens. So essentially, we will be shut out of functioning judicial systems because the international community considers our system too corrupt to wilfully expose their citizens to.

      During the Parliamentary session of 13 August 2012, Tundu Lissu an Advocate and opposition MP dared to state publicly without fear that there are judges in this country who are being appointed to the bench contrary to the requirements set out in the Constitution. For his bravado, a number of MPs from the ruling party and the Attorney General accused Tundu Lissu of bringing the judiciary into disrepute, an accusation that is premised on the assumption that our judiciary is reputable. Tundu Lissu managed to wind up his colleagues in the house to such an extent that he was promptly sent by the prefect to explain himself to the Ethics Committee.

      The general public waited with bated breath for Tundu Lissu’s explanation; some members of the bar happily assisted Lissu to collect information to prove his case and others dropped their foreheads into their hands and groaned in disbelief at the trap which members of the ruling party had unknowingly sprung on the Government at the expense of the Judiciary, for everyone save for the Attorney General and the MPs calling for Lissu’s blood knew giving Lissu the stage to prove his point would only end badly.

      The report which Lissu presented to the Ethics Committee was naturally leaked verbatim to the press and printed in a little known Swahili weekly tabloid called Jamhuri, in its August 14-20 Edition. I am told that the newspaper was in such demand that they had to reprint to satisfy the public’s curiosity. If this were a tennis match the score at this point would be 15 Lissu : Love the Judiciary.

      Being a consummate politician, Lissu made political mileage out of the report and unilaterally expanded the terms of reference by stating that he would not only provide evidence to prove that there are judges of the High Court who have been appointed unconstitutionally but in addition he would also provide evidence to prove that there are judges of the High Court who have neither the ability nor the skills necessary for such an appointment and who are not worthy to be appointed as judges of the High Court. 30 Lissu : Love the Judiciary.

      The Constitution sets 60 and 65 years as the retirement age for judges of the High Court and judges of the Court of Appeal respectively. In practice, it is quite common for presidents to extend the shelf life of judicial appointments by awarding retired judges contracts to continue serving as judges for specific time periods.

      These contracts have created a number of high profile debates and discussions within the legal fraternity. In his report, Lissu suggests that these contracts are by their very nature unconstitutional and he cites Mr. Luanda JA, presently serving as a judge of the Court of Appeal and the retired Ramadhani CJ, who have both publicly argued against extending judicial service beyond retirement age by way of contract, as authorities to strengthen his argument. On an artificial level Lissu’s argument appears to be very sound indeed, particularly to those who do not have access to the Constitution. However, it is incorrect and misleading.

      Articles 110(3) and 112(3) of the Constitution are categorical in providing provisos to the compulsory retirement age of judges of the High Court and judges of the Court of Appeal respectively. In both cases, where the President considers it to be in the public interest that a judge who has attained his retirement age continues in office, subject to the agreement of the judge in question, may direct that he remain in office for any period, which the President may specify.

      The debate concerning the contractual appointment of judges post retirement, was to my understanding, never about the Constitutionality of the act but rather about the effect that these appointments have on judicial independence, which is founded upon the doctrine of security of tenure.

      Judicial independence is the cornerstone of a democratic society and in order to ensure the existence of this independence, security of tenure must be assured so that a judge’s appointment and continued employment is not subjected to the whims of a politician.

      The problem with contractual extension of judicial service is that it subjects judges to presidential whims and accordingly impacts their independence. If a judge wants to remain serving in the judiciary post retirement, there is a risk that he will feel a need to serve the President rather than the Judiciary, thus compromising his independence.

      The use of contracts to extend judicial appointments post retirement age is not unconstitutional as declared by Lissu. The question that we as a society have to ask and answer is whether the power that the President has been given under the Constitution to extend judicial appointments post retirement age undermines judicial independence and if so, then we must take advantage of the present constitutional reform process and do away with it. 30 Lissu : 15 the Judiciary.

      Lissu’s report commences by providing evidence to prove that incompetent people have consistently been appointed to the bench. He makes his argument succinctly and very simply indeed by naming a number of judges who have failed to write judgements or have taken a considerable amount of time to write a few judgments.

      Other than corruption, one of the most common complaints about the Judiciary in Tanzania is that the courts take an inordinate amount of time to dispose of cases.

      Therefore, to everyone who has had contact with the Judiciary and its slow pace, Lissu’s evidence attributing the dilatory nature of the judicial process to the incompetence of judges themselves, seems perfectly reasonable. 40 Lissu : 15 the Judiciary.

      The question of ethics amongst members of the judiciary is also addressed in Lissu’s report. He names 4 serving members of the bench and suggests that they have questionable professional ethics.

      According to Lissu’s report only one of the named judge’s conduct has been found wanting by an independent third party; one judge was cleared of misconduct after an internal judicial investigation; and two other judges were never charged nor investigated for Lissu’s alleged acts of misconduct.

      There is no doubt that we must expect high ethical standards from our judges and people of debatable moral and/or ethical standing should not be permitted to serve on the bench.

      This does not mean though that we should deteriorate into a nation of witch hunters, destroying people’s reputations on the basis of unproven rumours and punishing those who have been found innocent. 40 Lissu : 30 the Judiciary

      Finally, in order to support his claim that judges have been appointed unconstitutionally, Lissu makes 2 major allegations: (1) The Constitution requires that a judge should have a first degree in law and there is presently serving on the Court of Appeal bench a judge who does not have a first degree in law; and (2) The Constitution requires the President to appoint judges from those persons who have been vetted and recommended to him by the Judicial Service Commission, and there are numerous judges presently serving on the High Court bench who have not been vetted or recommended by the Judicial Service Commission.

      The Judicial Service Commission is a body that has been set up by the Constitution and comprises of 6 members; the Chief Justice, the Attorney General, a Judge of the Court of Appeal, the Principal Judge of the High Court and two additional members appointed by the President.

      The Constitution requires the President to appoint judges of the High Court after consultation with the Judicial Service Commission, and pursuant to the Judiciary Administration Act of 2011 one of the functions of the Judicial Service Commission is to advise the President in respect of inter alia the appointment of judges of the High Court and the Court of Appeal.

      The Judiciary Administration Act of 2011 and its predecessor, the Judicial Service Act of 2005, fail to set out the criteria upon which judicial appointments are made and the process, which the Judicial Service Commission is required to apply in vetting judicial candidates.

      Other than members of the Judicial Service Commission, and probably the President, we do not know when posts on the High Court bench fall open; how names for prospective judges are proposed; how they are vetted; whether prospective judges are interviewed; what criteria are used to short list names proposed to the President; any tests which prospective judges are expected to take; the names of the persons short listed for recommendation to the President; the policy which is applied when appointing judges. It is surprising in the modern era that such highly specialised, professional and important appointments are made by so few individuals and in a cloud of mystery and secrecy.

      Unfortunately this lack of transparency undermines the credibility of the appointment process itself, particularly when for over a decade, the Judiciary in Tanzania has had the consistent dubious reputation of being second only to the Police in various reports on corruption. It has to be said that the manner of appointing members of the bench has a direct and inevitable impact on the quality of the bench.

      Our neighbour, Kenya has recognised this fact and amended its Constitution and in so doing relegated the role of the President in appointing judges to a ceremonial one only.

      The role of the Judicial Service Commission of Kenya has been enhanced and it now consists of 11 members, including one male and one female from the Kenyan bar and two members of the general public appointed by the President and approved by the National Assembly. Article 172(2)(a) of the 2010 Kenyan Constitution requires the Judicial Service Commission of Kenya to be guided by “competitiveness and transparent processes of appointment of judicial officers and other staff of the judiciary;”.

      On the other hand, the Judicial Appointments Commission for England and Wales has 15 Commissioners, amongst whom 5 are members of the judiciary, 2 from either the bar or the law society, and 5 lay members. The Chairperson of the Commission must always be a lay member. 12 Commissioners including the Chairman, are appointed through open competition.

      The Judicial Appointments Commission for England and Wales advertises all judicial posts including posts for judges of the High Court. Interested persons are expected to apply and those who are shortlisted proceed to undergo a vigorous interview process including interview panels, role-playing and situational questioning.

      The JAC’s key statutory responsibilities are “to select candidates solely on merit; to select only people of good character; to have regard to the need to encourage diversity in the range of persons available for selection to appointments.”

      The key to a successful judiciary is diversity and appointment by merit. This can only be achieved through transparency and competitiveness. Quietly spoken recommendations amongst a select few men, followed by taps on the shoulders to those lucky enough or influential enough to be considered by a few to be worthy of joining the judicial club, has resulted in a judiciary with an unenviable reputation. Gentlemen, after years implementing a weak judicial appointments policy, the chickens have come home to roost. I am afraid to say that so long as the process of appointing judges remains shrouded in secrecy, uncompetitive and jealously guarded by the few, Lissu will be believed. Game Lissu.

      Ms. Karume was called to the Bar in the Middle Temple and is an advocate of the High Courts of Tanzania and Zanzibar. She is presently Litigation Partner with IMMMA Advocates in Dar es Salaam. Email: [email protected]

      SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY
      Maundumula likes this.

    20. #397
      SoNotorious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th September 2011
      Posts : 750
      Rep Power : 507
      Likes Received
      184
      Likes Given
      241

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      hii article ya mtoto wa karume ni next level, sina cha kumzawadia zaidi ya kumuoa kama bado yuko single.
      Maundumula likes this.

    21. #398
      mpigauzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th July 2012
      Posts : 276
      Rep Power : 400
      Likes Received
      70
      Likes Given
      174

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      Quote By MTAZAMO
      Haya Wanasheria ongezeni nondo hapa tuzidi kuwaumbua hawa wanaonajisi taaluma yenu!
      Wanasheria wenyewe hawawezi hata kuongea.

    22. #399
      mbish's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th October 2011
      Posts : 45
      Rep Power : 391
      Likes Received
      19
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By NdasheneMbandu
      Nilijua tu kwamba mpiganaji Tundu hawezi kubwatuka kama akina lusinde na mwigulu. Nilijua anaongea mambo yenye supporting data. Zaidi ya yote nilijua nyuma yake wapo majaji na wanasheria wasomi wanaokereheka na teuzi zinazotolewa kama muuza njugu anavyowaonjesha wateja wake. Sasa kwa data hizi bunge la magamba na serikali yake watasema nini!!! Hakika wataumbuka.

      Mwisho naomba niseme waziwazi bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno ni kwamba alichofanya rais wa sasa ni kuwajaza waumini wenzie bila kujali uwezo na matokeo yake ameumbuka. Tafakari.
      umeanza vizuri umeharibu mwishoni, hapo kwenye "waumini wenzie" hao kina sekela ni waumini wenzie?, acha nadharia potofu ww

    23. #400
      Kulya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2011
      Posts : 263
      Rep Power : 439
      Likes Received
      89
      Likes Given
      55

      Default Re: Ripoti Maalum: Utetezi wa Tundu Lissu (MB) mbele ya kamati ya Haki na Maadili ya bunge

      The Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 ( As amended)

      110.-(1) Every Judge of the High Court shall vacate his office on

      attaining the age of sixty years, but the provisions of this subarticle shall apply
      subject to the subsequent provisions of this Article.


      (2) Any Judge of the High Court may retire from office in the service of
      the United Republic at any time on attaining the age of fifty five years, except
      where the President directs that he should not retire from office, and if the
      President so directs, then the Judge to whom the directions of the President relate
      shall not retire from office until the expiry of the period specified by the President
      for that purpose.

      (3) In the event that the President considers it to be in the public interest
      that a Judge who has attained sixty years of age continue in office, and the Judge
      agrees in writing to continue in office, then the President may direct that the judge
      continue in office for any period which may be specified by the President.

      (4) Notwithstanding that a Judge has attained the age at which he is
      required by the provisions of this Article to vacate office, a person who was
      holding the office of Judge of the High Court may continue to perform the
      functions of that office after attaining that age until he completes the preparation
      and delivery of the decision or until he completes any other business in connection
      with matters which he had started hearing before attaining that age.

      I shall direct my self only on the issue of tenure of the Judges of the High Court and the Powers of the President on such.

      The Constitution of the URT, under the provisions of the aforementioned article herein above, gives the President of the URT undoubted powers to extend the tenure of a Judge, if he, on his own counsel and reasoning as he sees fit to do so.

      Make reference to sub-art 3 herein-above, "If the President sees it is of the public interest, after 60 years of a particular Judge service, he may extend his tenure, after such a Judge consents.

      For the purpose of the above para, "Public Interest" has the meaning, by the Court of Appeal of Tanzania construe in the case of
      Attorney General vs. Sisi Enterprises LTD
      Public purpose or public interest must include a purpose, that is to say an aim or object in which the general interest of the community is concerned or involved, as opposed to the particular interest of individuals or institutions.
      Emphasis supplied.

      The power of extending the tenure of a Judge by the President does not involve any person, neither legal nor natural for consultation, its only if he so directs, upon his wish.

      In accordance with the Constitution of URT, the extension of the tenure of the Judges of the High Court is very Constitutional!

      The remaining question unanswered rests on the phrase Public Interest, does the extension benefits the whole of Tanzanians? Or is for the purpose of serving the best interests of the few...?! In my opinion and the way it is used, it is for the benefit of the few.

      Since this issue is so provided by our Constitution, "Katiba Mpya" shall perpendicularly deal with it, but I am afraid the so called "Katiba Mpya" is already drafted awaiting promulgation.

      Unless otherwise, this issue of Judges Tenure and the Powers of the President on such be petitioned to the Constitutional Court for determination.

    Page 20 of 21 FirstFirst ... 1018192021 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...