Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: JF Focus: Interview with Maxence Melo

    Report Post
    Page 4 of 7 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 140
    1. #1
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,473
      Rep Power : 35629
      Likes Received
      5028
      Likes Given
      5752

      Exclamation JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Salam kwa members wote.

      It has been six years now since Jamii Forums was launched, and since its very inception it has been a controversial forum. There were numerous rumors as to who were behind its creation and the intentions of its founders vis a vis the Tanzanian politics.

      Today JamiiForums is believed to be the largest East African Forum, with more than 87,000 members (and counting) and its growth in Tanzania is faster than international social media like facebook or twitter. We can see members interacting under different type of membership, we read articles from Fikra Pevu, we have seen a Kenyan Forum and all these indicate a new direction for Jamii forums.

      Given the alleged influence it had on the 2010 elections and the role it is currently playing in shaping he public opinion, several questions come to some of us: Who is Maxence Melo? who else could be behind Jamii Forums? What was the idea behind the creation of Jamii Forums? How is Jamii Forums positioning itself in the Tanzanian Political, economic and social sphere etc.

      On Friday the 17th, at 11:00 AM east African Time (Saa tano asubuhi kamili saa za Africa Mashariki) we invite Jamii Forum Founder and owner, Maxence Melo, to respond to some of these questions. The interview will be conducted by King'asti, a long time JF member whom we believe has the necessary impartiality and perspicacity to ask Maxence pertinent questions that will enlighten our lanterns.

      We welcome all questions from members and with Maxence permission we also welcome some suggestions on how to improve on Jamii Forum presence in the Tanzanian, Kenyan and eventually East African Community Political life.


      We hope to have all Jamii Forums members online that day.


      Karibuni

      Roulette

      Updates:
      • As we ask questions, please let's make sure that we do not repeat questions he answered during his interview with Bongo Celebrity (the interview can be found here)
      • As per Maxence, King'asti and some JF members request, the interview is rescheduled to Saturday the 18th, same place (Great thinkers forum) same time (11:00 AM, EAT)
      • Due to reasons beyond his control, Maxence has requested that the interview starts at 12:00 EAT.
      Last edited by Roulette; 18th August 2012 at 11:23. Reason: Update on the interview time
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    2. Miaka 50

    3. #61
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,248
      Rep Power : 31390
      Likes Received
      9620
      Likes Given
      684

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Mimi ningependa kujua haya mawili:
      1) Farida yuko wapi siku hizi?
      2) Ni vigezo gani vinatumiwa kuchagua mods?
      Manyanza and Freema Agyeman like this.
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    4. #62
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,473
      Rep Power : 35629
      Likes Received
      5028
      Likes Given
      5752

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Quote By Nyani Ngabu
      I take it you meant to say "inception", right?
      Thanks for the correction. Inception makes a clearer sense.
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    5. #63
      Dark City's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2008
      Location : Roaming
      Posts : 11,568
      Rep Power : 23554
      Likes Received
      6987
      Likes Given
      11340

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Quote By Nyani Ngabu
      Mimi ningependa kujua haya mawili:
      1) Farida yuko wapi siku hizi?
      2) Ni vigezo gani vinatumiwa kuchagua mods?
      Upo kaka NN??


      (sorry huku tuko kwenye jukwaa la politiki....)!!!
      "WE ALWAYS DON'T CHANGE UNTIL THE COST OF STAYING THE SAME EXCEEDS THE COST OF CHANGE....LOOKING BEYOND THE 31 OKTOBA 2010 LANDMARK"

      Retired Maj Gen DC (1947)...[email protected]

    6. #64
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,473
      Rep Power : 35629
      Likes Received
      5028
      Likes Given
      5752

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Quote By Nyani Ngabu
      Mimi ningependa kujua haya mawili:
      1) Farida yuko wapi siku hizi?
      2) Ni vigezo gani vinatumiwa kuchagua mods?
      Asante sana. Hilo la mwisho limerudi mata tatu, hivo naamini lina chances nyingi sana kuorodheshwa katika zile kumi zitakazo ulizwa live. hilo lapili analiona na nadhani litajibiwa hata in the side comments.
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    7. #65
      zubedayo_mchuzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2011
      Posts : 3,355
      Rep Power : 1061
      Likes Received
      590
      Likes Given
      43

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Mnapango wa kuwa na jamiiforumsTV hapo baadae..?

    8. RukaaJuu Final

    9. #66
      njiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Location : ax^2+bx+c=0
      Posts : 4,955
      Rep Power : 2369
      Likes Received
      959
      Likes Given
      172

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Roulette Maxence Melo, Mike McKee, Invisible mnazungumzia vipi ile allegation aliyotoa Le mutuz "willy malecela " kuhusu umilikiwa JF , je ni nini kimetokea, Je mmeshamfuta humu kama alivyoomba ..? naomba ulizungumzie hili maana tumepata one side of story ...

      Shukran

      JF DAIMA!
      Pure Matrimony >> Purity starts here (Quran 24:26)
      My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective" Njiwa"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯


    10. #67
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,434
      Rep Power : 2886
      Likes Received
      4794
      Likes Given
      2857

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Hongera JF

      Hoja:
      Kwa kawaida ili 'Brand' iendelee kuwa brand ni lazima kuwepo na ubunifu kila mara.
      Jf kama brand ni lazima iwe tayari kukabiliana na ushindani au wizi wa brand unaoweza kufanyiwa maboresho na kuipiku.
      Yahoo ilidumaa na kubweteka leo Google inaongoza. Pamoja na Google kuongoza haijawahi kusimama au kubweteka katika ubunifu.

      Swali:
      a)Baada ya kufanikiwa katika internet,kuwa na wafuasi katika majukwaa na vionjo tofuati, je, JF inampango gani wa kuendelea katika eneo la Audio (mathalani FM station, au Internet radio) au kushirikiana na wadau wengine waliotanuka na kupata access za visual za vitu kama 'streamline' za michezo na habari japo kwa muda mfupi kwa kuanzia.

      b)Kutokana na A hapo juu, je, jf haioni kuwa huwa ndio mwanzo wa kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kuwa chanzo kizuri cha mapato katika muundo wa biashara.

      Ahsante

    11. #68
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,473
      Rep Power : 35629
      Likes Received
      5028
      Likes Given
      5752

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Quote By zubedayo_mchuzi
      Mnapango wa kuwa na jamiiforumsTV hapo baadae..?
      Quote By njiwa
      Roulette Maxence Melo, Mike McKee, Invisible mnazungumzia vipi ile allegation aliyotoa Le mutuz "willy malecela " kuhusu umilikiwa JF , je ni nini kimetokea, Je mmeshamfuta humu kama alivyoomba ..? naomba ulizungumzie hili maana tumepata one side of story ...

      Shukran

      JF DAIMA!
      Quote By Nguruvi3
      Hongera JF

      Hoja:
      Kwa kawaida ili 'Brand' iendelee kuwa brand ni lazima kuwepo na ubunifu kila mara.
      Jf kama brand ni lazima iwe tayari kukabiliana na ushindani au wizi wa brand unaoweza kufanyiwa maboresho na kuipiku.
      Yahoo ilidumaa na kubweteka leo Google inaongoza. Pamoja na Google kuongoza haijawahi kusimama au kubweteka katika ubunifu.

      Swali:
      a)Baada ya kufanikiwa katika internet,kuwa na wafuasi katika majukwaa na vionjo tofuati, je, JF inampango gani wa kuendelea katika eneo la Audio (mathalani FM station, au Internet radio) au kushirikiana na wadau wengine waliotanuka na kupata access za visual za vitu kama 'streamline' za michezo na habari japo kwa muda mfupi kwa kuanzia.

      b)Kutokana na A hapo juu, je, jf haioni kuwa huwa ndio mwanzo wa kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kuwa chanzo kizuri cha mapato katika muundo wa biashara.

      Ahsante
      Masuali yenu yamepokelewa, asanteni sana kwa ushiriki.
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    12. #69
      Roulette's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 15th December 2010
      Posts : 5,473
      Rep Power : 35629
      Likes Received
      5028
      Likes Given
      5752

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Kuna interview ya mkuu Maxence inayo patikana hapa, hivo ningependa masuali yasijirudie:



      Tukiamua kubishana,tunaweza kufanya hivyo. Lakini endapo mwisho wa ubishi huo tutaamua kukubaliana,basi sina shaka kwamba sote tutakubaliana kwamba; miongoni mwa mitandao inayotembelewa na yenye ushawishi mkubwa na wa aina yake miongoni mwa watanzania wengi,mtandao wa Jamii Forums au kwa kifupi JF hauwezi kukosa katika orodha hiyo.

      Lakini tofauti na mitandao mingine ambayo kimsingi imekuwa ikiendeshwa na mtu au watu wachache tu, JF ni mtandao unaondeshwa na watu wengi.Wengi wakiwa watanzania wenyewe. Pengine hiki ndicho kinachoufanya mtandao wa Jamii Forums kuwa na “upekee” kama nilivyogusia hapo juu.Uendeshwaji huu wa jumla unafanyika kwa uhuru wa kila mtu kujiunga na kuanzisha mjadala,kuchangia au kuupanua zaidi. Kimsingi,hivyo ndivyo mtandao wa Jamii Forums unavyochanja mbuga hivi leo.

      Wewe na mimi sote tunaweza kujiunga na kuendeleza mijadala. Ndani ya Jamii Forums kuna watu wa kila aina.Kuna watanzania.Kuna viongozi/wanasiasa,wanataaluma mbalimbali na pia kuna wenzangu na mie,watu wa kawaida wenye mapenzi na tekinolojia,habari,maarifa na wenye kutafuta mahali pa kutolea maoni yao huku wakiwa na imani kubwa kwamba kuna mtu atasoma ,kusikia na kuyafanyia kazi.

      Ulianzaje? Nini malengo yake?Ni kweli kwamba mtandao huu unamilikiwa na chama fulani cha kisiasa? Mtandao huu una malengo gani?Ili kupata majibu kwa maswali lukuki niliyokuwa nayo(na bila shaka uliyonayo wewe msomaji) nilimtafuta Maxence Melo Mubyazi(pichani), ambaye ni mwanzilishi-mwenza wa Jamii Forums na mtu ambaye mpaka hivi leo anabakia kuwa mhimili wa Jamii Forums ili kupata baadhi ya majibu kwa maswali yangu.
      Haya hapa ni mahojiano yangu naye;


      BC: Kawaida mtu anapoanzisha kitu cha mtandaoni huwa ana malengo fulani ingawa inaweza ikatokea kwamba hapo baadae malengo yakabadilika au kujinyambulisha kidogo ili kwenda na wakati na hali halisi. Kwa upande wenu, mlikuwa na malengo gani kimsingi mlipoanzisha Jamii Forums? Je, bado malengo ni yale yale au yamebadilika?

      MM: Malengo yetu tangu mwanzo ni yale yale na hayajabadilika na wala hatudhanii yatabadilika karibuni; kutoa uhuru wa kujieleza kwa njia mbadala. Ni wazi kuwa hili linaendelea japo linakuwa ndani ya sheria (http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ums-rules.html ) tulizojiwekea tangu mapema 2006.

      BC: Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama wa Jamii Forums kwamba nyie Moderators wakati mwingine mmekuwa mkionyesha utashi binafsi. Mmewahi kulalamikiwa kwamba huwa mnatoa thread fulani kwa sababu zenu binafsi. Unasemaje kuhusu tuhuma kama hizi na labda unaweza kutusaidia kuelewa ni kitu au sababu gani zinaweza kusababisha “thread” fulani kuondolewa?

      MM:
      Kama nilivyotangulia kusema tangu mwanzo; moderators wa JF wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria za uendeshaji JF; ufafanuzi juu ya thread (topic) gani huondolewa na kwa vigezo gani upo wazi http://www.jamiiforums.com/habari-na...kabisa-jf.html na tuliutoa baada ya malalamiko ya wengi. Kila kitu kiko wazi, wengi wa wanaolalamika huwa hawapendi kuumiza vichwa, wale wanaowasiliana nasi huwa tunawapa ufafanuzi.
      Kuna kipindi tuliweka ‘automated notifications’ pindi thread inapohamishwa au kufutwa, tulichoambulia ilikuwa ni kazi bure, watu hawasomi hizo notifications!
      Kila binadamu ana mapungufu, lakini hatuwezi kusema kuwa tutafanya kazi kwa hisia tu. Kuna moderation tools, moderator akifanya makosa yanaonekana kwa wote kuwa aliyefanya kosa ni moderator gani hivyo wote tunawajibika kurekebisha kosa la mmoja. Nyakati nyingine huwa tunalazimika kuomba radhi kutokana na makosa yanayoweza kutokea tokana na utendaji wa mmoja wetu.
      Tuseme ukweli, uhuru bila mipaka wakati mwingine ni fujo. Huwezi kuruhusu mijadala ambayo inachochea umwagikaji damu, inachochea vurugu ama inajenga utengano miongoni mwa watanzania bila kufikiria athari za mbeleni kwa taifa letu.
      Tunaijua hulka ya mwanadamu; wakati mwingine akishaweka kitu flani kichwani mwake basi kukibadili inakuwa kazi kubwa. Mtu anayeanzisha mjadala wa uchokonozi wa kidini ama kikabila ama kuanzisha mjadala ambao hana ushahidi ili mradi anataka kuchangamsha jamvi tu anakuwa anajua wazi anachofanya si kizuri lakini anafanya hivyo akiwa kajiandaa kuwashambulia viranja wa jukwaa (moderators).

      BC: Bila shaka hili ntakalokuuliza na nyie wenyewe mmeshalisikia sana. Inasemekana kwamba Jamii Forums ni kama vile mkono wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) cha mtandaoni. Mnazungumziaje tuhuma kama hizi ?Ukweli uko wapi?

      MM:
      Tuhuma hizi zilikuwepo kuelekea uchaguzi 2010; well, mara zote huwezi kukwepa tuhuma maana tuhuma ni tuhuma na anayetuhumu mara nyingine hana sababu za kutuhumu.
      Ukweli ni kuwa hata hao CHADEMA wanatulalamikia kuwa tunatumiwa na CCM; lakini cha kujiuliza, ni kweli tuhuma hizi wanapozitoa wanakuwa na ushahidi wa wazi?CCM:Baada ya uchaguzi walitoa tuhuma zinazoelekeana na hili, tulitoa ufafanuzi (Political Paranoia? Tanzania’s Ruling Party threatens online social media | Fikra Pevu | Kisima cha busara!) na kwa bahati walituelewa na kuongeza jeshi lao ndani ya JF.Siamini kama Mwigulu, Nape, Dr. Kigwangalla, Hussein Bashe n.k ambao ni wanachama hai (achilia mbali Salva Rweyemamu, AG Werema n.k) ndani ya JF ni CHADEMA. Hawa ni wenye uthubutu toka CCM.CHADEMA:Kinachoipa CHADEMA credit kwenye social networks nyingi (si JF pekee) ni uharaka wa wao kujibu hoja wanapoona imelengwa kwao. Wengi wamejisajili kwa majina yao halisi na wanakuwa ‘active’ kwenye ‘hot issues’. Dr. Slaa, Zitto, Mnyika na Dr. Kitila Mkumbo ni baadhi watu toka CHADEMA ambao wako active JF.
      Lakini, kukubali kwao kukosolewa na kujibu pale wanapoweza ndiko kunakowafanya wengi wajikute wanakishabikia chama chao. Nina wasiwasi kuwa hata hao wanaowashabikia hawana kadi za CHADEMA.
      Kifupi:‘Trending’ ya siasa ndani ya Tanzania ndiyo inapelekea mijadala kuonekana kui-favor CHADEMA. Lakini ukiangalia kwa sasa hali inavyoelekea mwaka 2012 CHADEMA inaweza kupita kwenye wakati mgumu kuliko wakati wowote; hata hivyo ni endapo hawataweza kuling’amua hili na kulifanyia kazi.

      BC: JF as JF haitozuia mjadala endapo ya CUF yatawakuta CHADEMA, ndo uhuru wa kujieleza huo, na kama nimewahi kuongea nao kuhusu au kuiongelea Jamii Forums nikiwa nao,wamekuwa wakihoji kuhusu chanzo cha habari zenu. Ninavyojua mimi ni kwamba chanzo chenu kikubwa ni wanachama wenyewe (JF Members). Ninachotaka kuhoji mimi ni jinsi au utaratibu mnaoutumia katika kuhakiki authenticity au ukweli wa habari zinazochapwa au kutokea katika Jamii Forums. Mnafanyaje?
      MM:
      Well,Maswali ya ‘Chanzo chenu cha habari’ huwa tunakumbana nayo sana. Lakini ni pale mtu anaposhindwa kuelewa JF ni nini. JF si gazeti, si redio na wala kituo cha televisheni. JF ni social network; moderators wapo kusimamia sheria za kujadiliana bila kuziathiri, pale inapokuja habari ambayo mwanzishaji tunamtilia walakini huwa tunajitahidi kuwasiliana na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo tuna ushirikiano nao na pengine kutuma waandishi wetu kuweza kutafiti ukweli wa habari husika. Mara nyingi zinakuwa si habari bali ni ‘news tips’.
      Kwa kutambua hilo, tuliamua kuwa na kitengo maalumu kinacho-deal na habari ambapo habari zilizohaririwa toka kwetu zinapatikana www.FikraPevu.com hapa ukituuliza chanzo cha habari tutakupatia kila aina ya ushahidi na waandishi wetu wapo makini wanapofuatilia jambo flani.Kuwazuia watu ati wanapoandika JF kwanza kila ‘comment’ au hoja mama (thread) ithibitishwe kabla ya kwenda hewani itakuwa ni ukiritimba ambao utapelekea mambo mengine kuwa magumu kufanyika. Wanachama wa JF wengi ni waungwana (japo si wote), wanatambua umuhimu wa jukwaa lao na wanahakikisha wanalilinda. Vifaa (tools) kwa ajili ya kuwasaidia moderators kujua kuwa kuna kitu hakipo sawa vimewekwa (Report Abuse) na wanachama wetu huvitumia kutujulisha pindi panapokuwa na kitu ambacho si cha kawaida ili kiweze kuwa ‘reviewed’ haraka kabla hakijasababisha madhara kwa Jamii yetu.

      BC: Baadhi ya habari zinazoandikwa kwenye Jamii Forums (hususani zile za kimataifa) huonekana kama zimenyofolewa kutoka katika vyombo vya habari vya nchi za nje. Hii huwa na picha na maelezo wakati mwingine. Hamuoni kama kwa kufanya hivyo na hususani pale source ya habari hizo inapokuwa haijawekwa wazi ni ukiukwaji wa masuala ya hakimiliki? Mnakabiliana vipi na changamoto hizo?

      MM: Kama nilivyoongea hapo awali; wanachama wa JF wapo makini; mtu anapoanzisha mjadala ambao unaonekana wazi si wake ameunyofoa sehemu basi humlazimisha aweke chanzo cha habari. Mara nyingi mataifa ya nje wako makini kwenye hili, wanapogundua unatumia habari zao bila ku-credit source (kuonyesha chanzo) basi hukupiga DMCA. Moderators wa JF wanajitahidi kufuatilia endapo mtu anaweka habari bila kuweka chanzo kuhakikisha inaonyeshwa wazi kuwa habari hii ina chanzo na chanzo chake ni kipi.Hili hufanyika kwa vyanzo vyote; iwe ni online au offline (radio, magazeti au televisheni); mhusika LAZIMA awafahamishe wasomaji chanzo cha habari yake; kama ni hoja yake ni wachache watakaomhoji juu ya chanzo cha habari husika

      .
      BC: Baadhi ya wanasiasa wenye majina makubwa nchini, aidha wakitumia majina yao halisi au wakitumia majina ya kujipandikizia, wamekuwa wakitumia mtandao wenu katika kujadili hoja mbalimbali na wengine hata kuelezea sera zao. Una ushauri gani?

      MM: Mazingira ya nchi yetu ndiyo yanapelekea watu kutumia majina ya bandia. Wanaotumia majina yao halisi ni wengi kwa sasa, lakini kuna hoja inawawia vigumu kushiriki pale wanapohitaji kufanya hivyo.JamiiForums ni mkusanyiko wa mijadala mbalimbali (zaidi ya siasa); ni vigumu kwa Zitto/Slaa/Kigwangalla kuingia Jukwaa la Mapenzi na kushiriki mjadala flani ambao huenda angetamani kushiriki.
      Kuna perception flani ilishajengeka juu yake, kwa mantiki hii anaweza kujikuta analazimika kutumia jina la kivuli kuweza kuwasilisha hoja na kutoa maoni yake kama mwananchi.
      Mara zote tunawasisitiza watu ‘kuwa wao’ (to be genuine) na kuepuka kuandika uzushi, hii inasaidia watu kuweza kushiriki mijadala bila kuingiza chumvi sana au kuandika bila kufikiria (japo si wote). Watu wa propaganda huwezi kuwazuia, haswa wanapoingia Jukwaa la Siasa!Kifupi; muhimu kwetu ni hoja ya mtu na si jina la mtu
      .
      Bahati mbaya sana sheria za JF hazijui cheo cha mtu wala jina lake; anapovuka mipaka bila kujali yeye ni nani atafungiwa kwa muda na endapo ataendelea kukiuka sheria atafungiwa moja kwa moja!Lakini, kwa kutambua kuwa wengine wanahitaji kushiriki mijadala isiyokaa kishabiki; ndani ya JF kuna Jukwaa maalum kwa wale wanaojadili hoja tu bila kuingiza vioja. Jukwaa hili tumeliita ‘Great Thinkers’. Jukwaa hili halina moderator, wanaojadili huko wanajadili ‘issues’ zaidi na tunajitahidi kabla ya kumpa mtu fursa ya kuwa mdau huko kuzipitia baadhi ya jumbe alizokwisha weka ndani ya JF, kama ni mwanasiasa mwenye jina na ndio kwanza kajisajili, tunawasiliana naye na akitaka msaada tupo tayari kumfuata kumwelekeza namna ya kutumia jukwaa hili. Kimsingi, ukilitembelea utathibitisha kuwa wanaojadili issues huko ni kweli ni ‘Great Thinkers’.

      BC: Ni kiasi gani cha muda ambao mnautumia kwa siku katika kuhakikisha kwamba JF inakwenda katika mtiririko mnaoutaka. Hapa nazungumzia mambo kama kuhakikisha ipo hewani, ku-approve members wapya, kuhakiki kinachoandikwa au kuwekwa mtandaoni na mambo mengine kwa ujumla?

      MM: Mpaka sasa tuna moderators 22, wapo maeneo tofauti ya Dunia na hivyo JF inakuwa monitored masaa 24. Labda niseme MIMI huwa natumia masaa takribani 18-20 kwa siku nikiwa online.

      BC: Kumekuwa na changamoto kwamba vyombo vingi vya habari vya mtandaoni kama vile JF na hata hii bongocelebrity.com ni vyombo vya kimjini mjini…hususani Dar-es-salaam yaani tunawafikia zaidi watu waliopo mjini ambao kimsingi ndio wenye uelewa zaidi na uwezo wa kuingia mtandaoni kwa maana ya kuwa na access na mtandao. Mnaziongelea vipi changamoto hizi na mipango ikoje kuwafikia wengi na wengi zaidi?

      MM: JF imeenda step kubwa zaidi, si ya ki-mjini mjini tena. Kama utakumbuka, mwanzoni (2006-2008) JF ilikuwa na wachangiaji wengi toka ng’ambo. Kwa kifupi asilimia kama 75 hivi ya waliokuwa wanatembelea JF (enzi hizo JamboForums.com) ilikuwa ni toka ng’ambo.Maisha yamebadilika Tanzania, kwa leo hii zaidi ya 70% ya wanaotembelea JamiiForums ni toka Tanzania! JamiiForums kwa kutambua umuhimu wa kuwawezesha walio vijijini kuipata, tuliweka ‘mobile detection tools’ ili mtu anapoitembelea kwa simu ya mkononi (hata ya kichina) yenye uwezo wa kutumia mtandao aipate ndani ya sekunde 3. Kwa survey tuliyoifanya, watumiaji wa simu za mikononi kwenye mitandao wameongezeka na inaelekea kufikia 2014 asilimia hamsini (50%) ya watumiaji wa mtandao inaweza kuwa ni kutoka simu za mikononi.Kuna changamoto, lakini hii haikwepeki kuwa ukuaji wa teknolojia utasaidia watanzania wa vijijini kuzipata tovuti nyingi toka simu za mikononi. Kumbuka, karibia 50% ya watanzania wana simu za mikononi (kwa mujibu wa TCRA).

      BC: Kama moderator,mwanzilishi na mmiliki wa JF nina uhakika kwamba unaona na kusikia mengi ambayo yanaakisi kwa kiasi kikubwa, fikra za wananchi, maoni, mwelekeo na utashi wao kwa vyama vya kisiasa na siasa zenyewe. Kwa kutumia mwangaza huo huo, unadhani ni mambo gani matano ambayo yanawakera zaidi wananchi na ambayo ni rahisi tu kupatiwa ufumbuzi lakini kwa makusudi tu yanapewa nafasi ya nyuma?

      MM:
      Well, mimi si mmiliki; ni mwanzilishi tu. Wamiliki ni watanzania wanaoitumia JF.
      Kujibu swali lako kwa uzuri nitoe ufafanuzi (mfupi nikiwa limited kwa mambo matano tu) ifuatavyo:


      1. Watanzania wenye kuwa na uanachama wa vyama vya siasa ni wachache; vyama vinatakiwa kuelewa kuwa watanzania shida yao kubwa si siasa, maisha mazuri ndicho kilio chao. Maisha ya watanzania wengi ni duni, wanaishi bila kujua kesho itakuwaje! Pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho linazidi kuwa kubwa, ni hatari tunakoelekea.
      2. Miundombinu iboreshwe, ukitembelea vijiji vingi hawana hata maji walau ya visima na vyanzo vya maji vimeharibiwa (achilia mbali mijini); jitihada za serikali kwenye kuboresha barabara zinaonekana lakini haziendani na kasi ya ongezeko la idadi ya watanzania.
      3. Siasa za majitaka watanzania kwa sasa hawazioni za maana, bado zinatumiwa na vyama vyote na kwa mtizamo wangu zitavimaliza vyama vyenyewe! Kuna Tanzania zaidi ya vyama tunavyoviona sasa.
      4. Mfumo wa elimu uangaliwe upya; wanaohitimu serikali iangalie wapo wapi na wanafanya nini. Iweke namna ambayo kila chuo kitaweza ku-track wahitimu wake na kujua wafanyalo; tunakoelekea bomu la watanzania kukosa ajira litakuwa kubwa. Kuna baadhi ya wanasiasa wameanza ku-capitalize kwenye hili kuelekea uchaguzi 2015!
      5. Kuna umuhimu wa kuwa na wawekezaji lakini wengi wa wanaokuja Tanzania ni wakwapuaji. Wapinzani hata kama wamelipigia kelele hili bado hawajafanya vile walivyotarajiwa! Tanzania imekuwa shamba la bibi na kwa sasa wageni wanazidi kujazana na inaelekea ni wazi tunakoelekea hili litakuwa tatizo kubwa.



      BC: Mbali na tovuti au blogs, watanzania wengi siku hizi wanatumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter katika kupashana habari nk. Pamoja na hayo, wataalamu mbalimbali wa mawasiliano ya kimtandao wanasema Tanzania tupo nyuma katika kuitumia mitandao hiyo katika kupashana habari na kupeana ujuzi ambao/ambazo zinaweza kusaidia katika kuleta maendeleo au mabadiliko ya kijamii. Tunaambiwa sisi tumebakia “kupiga umbea” tu katika mitandao hiyo badala ya kuitumia kama ambavyo wenzetu wa nchi mbalimbali ulimwenguni wanavyoitumia. Nini maoni yako na ushauri katika hili?

      MM:
      Kifupi: Ni vigumu njia inayotumiwa na Congo/Kenya kuwasiliana kufanya kazi Tanzania. Namaanisha kuwa, si kama mitandao ya FaceBook au Twitter ni mibaya kwa watanzania, tunachogundua kwa sasa ni kuwa wasomi wa Tanzania wengi ni waoga na wabinafsi; tusitarajie wale tunaowaona wakipongezana, wakisifiana Facebook na twitter siku moja waamue kuanza kukosoana kirahisi.
      Isipokuwa twitter au facebook au JamiiForums vitakavyoleta mabadiliko muhimu, bado watanzania watakuja na namna mbadala; mitandao hii itatumika kupashana habari na huenda ikachukua hatamu baada ya wananchi ‘wa kawaida’ kuja na namna mbadala.Tumetoka mbali, taratibu tutafika. Kusema watanzania ‘wanapiga umbea’ kwenye twitter ni kuwaonea, ikiwa ni facebook hapo naweza kukubaliana na wanachosema. Aidha, sidhani kama malengo ya mitandao hii ni kuleta ukombozi/mapinduzi bali upashanaji habari. Hili linaelekea kufanikiwa kwa Tanzania, tutaulizana miaka 5 ijayo juu ya kauli yangu hii.

      BC: Kuna tofauti gani kubwa kati ya mtandao wa Jamii Forums na mitandao mingine mingi hapa nchini au hata nje ya nchi ambayo inaandika au kudurusu habari na matukio kutoka Tanzania?


      MM:
      JF unaweza kuitofautisha na mitandao kulingana na mtandao unaoilinganisha nao. Tofauti sidhani kama ni kubwa bali kinachoitofautisha JF na kwingineko ni kuwa hoja/mijadala inakuwa monitored na kumfanya mwingine adhanie huenda ni chombo cha habari!
      Zaidi, JF ni tovuti ya kwanza kwa Tanzania kuwa na mobile apps zake; tunazo apps kwa ajili ya watumiaji wa iPad/iPhone, BlackBerry na Android.

      BC: Kama nilivyogusia huko juu, kupitia JF unaona, unasikia mengi nk. Una ushauri gani kwa vijana wa kitanzania ambao ndio watakaoshika dola miaka ijayo?

      MM: Wasome!Mtu anayejisomea vitabu vingi (si vya udaku tu) ana hazina kubwa kichwani. Kwa vijana ambao wanaitembelea JF, nashauri kwa umakini mkubwa wawe wasomaji zaidi, wajaribu kuuliza ili waeleweshwe juu ya jambo flani. JF inaweza kuwa hazina kubwa kwao endapo watafuatilia mijadala inayoendelea na iliyopita. Jukwaa la Great Thinkers ndani ya JF lina mijadala ambayo inamfanya mtu atumie bongo zake anapochangia (Great Thinkers )Wajibidishe na washirikiane; kufanya mambo kivyakovyako ina gharama kubwa. Tukiungana ni rahisi kufanikiwa hata bila kuwezeshwa na serikali ama wahisani.Wajiamini!Vijana tunaweza, tusisubiri kuwezeshwa. Mtaji wa kwanza kwetu ni akili kichwani; pesa ni ziada tu!

      BC: Asante sana Max kwa muda wako. Kila la kheri katika kazi zako
      MM: Asante Jeff.Kazi njema na wewe pia.

      Read more: “WAMILIKI WA JAMII FORUMS NI WATANZANIA WANAOITUMIA”-MAXENCE MELO (MAHOJIANO MAALUM) - BongoCelebrity

      popiexo, bayonamperembi and cement like this.
      Information is not knowledge

      Albert Einstein

    13. #70
      Richard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2006
      Location : LANGLEY
      Posts : 2,277
      Rep Power : 1099
      Likes Received
      492
      Likes Given
      1683

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Hio ni good idea.

      Mimi pia napenda kumpongeza Max na mwenzio Mike kwa ushujaa wenu hasa pale mlipokabiliwa na matatizo mbalimbali ya wasioitakia mema JF.

      Max na Mike mmepita kwenye kipindi kigumu sana na hapo mlipofikia si padogo, ni mahali pa kujivuia sana.

      JF itakuwa imara na hata kule kwenye Fikra Pevu ulikokuanzisha ni wazo zuri na litalipa na pia nasikia sasa JF inakwenda Kenya ni jambo la kujivunia sana.

      Mimi nilikuwa na swali linalohusu uchaguzi mkuu mwaka 2015 lakini naona mwenzangu mmoja amekwishauliza.

      Mwisho mimi nikiwa ni mmoja wa wanachama wa muda mrefu tena pengine mmoja wa wale wa kwanza kusajili jina langu bila kufahamu madhara na matokeo yake, nawapongeza Mods wote na kuwahamasisha wajitahidi kufanya kazi yao ya kuhakiki bila woga wala upendeleo au ushabiki.

      Inapotokea kwamba "Thread" inahamishwa au kuondolewa kwa sababu zozote zile Mods wana budi kumjulisha mwanachama ili awe na taarifa mapema na si kuanza kutafuta "Thread" yake kila mahala.

      Viva Max na Mike,

      Viva JF na Mods,

      Viva members wote.

      Richard.
      Fang likes this.
      When thinking about my risk assessment, I always remember:
      HAZARD and the RISK .

    14. #71
      Duduwasha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 2,620
      Rep Power : 6249
      Likes Received
      523
      Likes Given
      418

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Safi Sana Ila Wakuu kuna kitu nimekuwa kila nikiuliza sijibiwi ni Kuhusu livechat zamani ilipokuwa jamboforums kulikuwa na vivutio vingi sana kama music haswa zilipendwa,livechat,games,Radi o n.k sasa hii Jamii forums imeondoa vyote sijaelewa imeenda mbele au imerudi nyuma!!

      sometime unapokuwa umekuwa bored na forum ukizungukia kwenye vivutio vingine ndani ya jf inaweka akili sawa kabla hujarejea kwenye mdahalo...

      Ila nawapongeza sana Wadau wote wa JF....

      La Mwisho Matangazo ya Pombe hata Ndani ya Mwezi Mtukufu kiasi yanawaletea Wadau wengine Shida kuchangia...
      Kina Faizafoxy angefunguliwa kwani huleta changamoto sana

    15. #72
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,200
      Rep Power : 28906
      Likes Received
      11685
      Likes Given
      4819

      Default

      Mkuu, hujaweka swali lako. Kumbuka maswali yataangaliwa kwa uzito wake na kisha kuchaguliwa maswali kumi tu ambayo mods hawataweza kujibu kwa niaba ya maxence.

      Kama una swali kuhusu madame itakuwa vyema kumfuata kwenye pm. This interview will be focused on Maxence Melo and the jf dream peke yake.
      Quote By KakaKiiza
      Dah ninamaswali mengi sana ila na wewe Madame ya kupasa uwe kwa pembeni kwani nauhakika watu watataka kujua zaidi juu yako japo naona maswali yatakuwa kwenye chekecho hivyo itakuwa nikazi kubwa kumaliza kihu ya wachangiaji!!Kwa yote mimi naanzia hapa kumpa shukurani za dhati kwakuweza kuanzisha chombo hiki!!mbali na hiyo kuweza kusimamia mawazo yake!niwengi wanaanzisha lakini kwakosa kusimamia mawazo yao wameshindwa kufika mbali!!

    16. #73
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,200
      Rep Power : 28906
      Likes Received
      11685
      Likes Given
      4819

      Default

      Asante mkuu.

      Hilo la matangazo ungeliongelea mapema kabla mfungo haujasogea ingekuwa vyema zaidi. Haina neno, tutakubaliana kwa ajili ya siku za usoni.
      Quote By Duduwasha
      Safi Sana Ila Wakuu kuna kitu nimekuwa kila nikiuliza sijibiwi ni Kuhusu livechat zamani ilipokuwa jamboforums kulikuwa na vivutio vingi sana kama music haswa zilipendwa,livechat,games,Radi o n.k sasa hii Jamii forums imeondoa vyote sijaelewa imeenda mbele au imerudi nyuma!!

      sometime unapokuwa umekuwa bored na forum ukizungukia kwenye vivutio vingine ndani ya jf inaweka akili sawa kabla hujarejea kwenye mdahalo...

      Ila nawapongeza sana Wadau wote wa JF....

      La Mwisho Matangazo ya Pombe hata Ndani ya Mwezi Mtukufu kiasi yanawaletea Wadau wengine Shida kuchangia...
      Kina Faizafoxy angefunguliwa kwani huleta changamoto sana
      Duduwasha likes this.

    17. #74
      FirstLady1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th July 2009
      Location : Mama Mwenye Nyumba
      Posts : 14,973
      Rep Power : 3703
      Likes Received
      3580
      Likes Given
      5769

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Pamoja sana wakuu
      No one is in charge of your happiness except you...
      God time is the best..

    18. #75
      Freema Agyeman's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2011
      Posts : 1,705
      Rep Power : 4179
      Likes Received
      1074
      Likes Given
      892

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Quote By Nyani Ngabu
      Mimi ningependa kujua haya mawili:
      1) Farida yuko wapi siku hizi?
      2) Ni vigezo gani vinatumiwa kuchagua mods?
      Painkiller nae yupo wapi siku hizi.
      Fang likes this.
      "The louder the protester, the more there is in their closet"

    19. #76
      Kashaijabutege's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 20th October 2010
      Location : Kabuteigi
      Posts : 1,918
      Rep Power : 823
      Likes Received
      371
      Likes Given
      241

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      SWALI: Je inawezekana mtu aliyetumia jina la "kificho" kujibadili na kutumia jina lake halisi hapo baadaye, iwapo atataka kufanya hivyo?
      NAKUSHUKURU MUNGU KWA KUIADHIBU CCM MCHANA KWEUPE, BABA NINAKUOMBA UZIDI KUWAUMBUA, KWA KUYAWEKA WAZI MCHANA WANAYOYAFANYA USIKU. OMBI KWA MUNGU: MUNGU WEWE NI MWEZA WA YOTE, NA SIKU ZOTE UNAYASIKILIZA MAOMBI YA WAKUCHAO, NAKUOMBA UKAFUNGE NGUVU ZA GIZA ZINAZOINYEMELEA M4C; NA UVUNJE MIPANGO YOTE YA MASHETANI WALIOPO NDANI YA CHADEMA. AMINA

    20. #77
      MTAZAMO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 4,235
      Rep Power : 2204
      Likes Received
      1818
      Likes Given
      2476

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Maxence Melo Changamoto gani kubwa unayokutana nayo kulinda hadhi ya JF against members wa JF ambao ni 'wazito' kwa nafasi zao na pengine wanamchango mkubwa wa hali na mali hapa JF (mfano wanasiasa ) pale wanapotaka favour au uvunje ka utaratibu fulani ka hapa JF kwa faida yao? hapa naigusa na serikali pale inapotaka u edit habari au iondolewe kwa shinikizo kwa kisingizio cha usalama wa taifa?

      Max nini kinachokuongoza kuweza kusimamia chombo hiki kwa haki bila upendeleo na unafikiri una misingi inayoweza kufanya team yako yote isimame pale unapoamini bila kuyumbisha lengo na msimamo wa JF?

    21. #78
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 11,989
      Rep Power : 24152
      Likes Received
      4705
      Likes Given
      2647

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Quote By Roulette

      On Fridaythe 17th, at 11:00 AM east African Time (Saa tano asubuhi kamili saa za Africa Mashariki) we invite Jamii Forum Founder and owner, Maxence Melo, to respond to some of these questions. The interview will be conducted by a long time JF member, whom we believe has the necessary impartiality and perspicacity to ask Maxence pertinent questions that will enlighten our lanterns.

      Update: As we ask questions, please let's make sure that we do not repeat questions he answered during his interview with Bongo Celebrity (the interview can be found here)
      May we be informed who this member is?.......thanks

      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te


    22. #79
      Mpita Njia's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 6,703
      Rep Power : 3255
      Likes Received
      984
      Likes Given
      754

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      Quote By Roulette
      Hakuna suali loa moja kwa moja mkuu, unaweza kuweka suali lako hapa na masuali kumi "most pertinent" yatachaguliwa.
      Our membership is 87,000 (and still counting). Where do we go from here? What should we expect?
      I assume full responsibility for my actions, except the ones that are someone else's fault.

    23. #80
      gfsonwin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 12th April 2012
      Posts : 10,729
      Rep Power : 27101
      Likes Received
      10088
      Likes Given
      14003

      Default Re: JF Focus: Interview with Maxence Melo

      thanks @roullete, tutakuwa pamoja.
      "thought takes man out of servitude into freedom"
      'daima tudumu katika upendo'

    Page 4 of 7 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...