Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tundu Lissu yuko sahihi: Majaji wengi hawajahitimu vyuo na elimu zao ni za mitandaoni

    Report Post
    Page 8 of 9 FirstFirst ... 6789 LastLast
    Results 141 to 160 of 166
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 660
      Rep Power : 542
      Likes Received
      462
      Likes Given
      0

      Default Tundu Lissu yuko sahihi: Majaji wengi hawajahitimu vyuo na elimu zao ni za mitandaoni

      Source Gazeti la Fahamu

      Ule usemi wa Mbunge wa Singida Mashariki kuwa ujaji wa kuteuliwa na rais ni wa kirafiki zaidi na kujuana una ukweli ndani yake, na ulikuwa mwiba kwa serikali na mwanasheria mkuu wa serikali kuwa na ukweli kwamba majaji wengi hawana sifa za kuwa majaji na wengi wao elimi zao ni za kuungaunga. Ikitolewa mfano ya wa jaji ambaye kwa miaka minne kashindwa kuandika hukumu kumfatilia hana elimu ya degree na kwa muda huu anafanya degree ya kwanza online.

      Narudia kusema Tundu Lissu yuko sahihi
      Mkandara, Ogah, Pasco and 4 others like this.

    2. Miaka 50

    3. #141
      SoNotorious's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th September 2011
      Posts : 765
      Rep Power : 510
      Likes Received
      185
      Likes Given
      248

      Default

      Quote By Karikenye
      Pasco tangu UHURU bunge la Tanzania halijawahi kutunga sheria!!!!!! Lenyewe linajadili na kupitisha sheria zilizotungwa na serikali!!!!!
      ni kweli

    4. #142
      dudus's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,302
      Rep Power : 1007
      Likes Received
      1291
      Likes Given
      522

      Default Re: Tundu Lisu - Hapa kuhusu majaji umechemka

      Quote By MAMMAMIA
      Maneno yaliyomfukuzisha Ibilisi peponi ni pale alipotamka neno Mimi umniumba kwa Moto (Naar) badala ya neno Mwangaza (Nur). Nina-refer Kitabu cha Koran, Sura ya 7:11-13.

      Pia yamerudiwa maneno hayo katika Sura 38: 76

      Asante sana Mkuu kwa mistari murua. Hata hivyo japo ni nje kidogo ya mada, naomba kuuliza: hivi Ibilisi angetamka vinginevyo, yaani Nur badala ya Naar, unadhani angesalimika? Kwa mistari uliyo-refer inaonekana kilichomtimua Ibilisi ni ile kujiona bora kuliko Adam aliyeumbwa kwa udongo regardless yeye (Ibilisi) aliumbwa kwa nini.

      Katika Biblia kuna kisa, japo tofauti na hicho, lakini ndicho kilichomwondoa Ibilisi Mbinguni:


      "Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka Mbinguni,
      Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;
      Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano,
      Katika pande za mwisho za kaskazini
      ", Isa 14:13

      "Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
      Nitafanana na Yeye aliye juu
      ", Isa 14:14

      Mistari hiyo na hasa huo nilio-underline ndio ulimtoa Ibilisi almaarufu kama Lusifa au Shetani au Mkuu wa Mapepo na Majini au Baba wa Uovu kutoka Mbinguni.

      Eid Mubarak.

    5. #143
      asungwilemwaifunga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2012
      Posts : 346
      Rep Power : 502
      Likes Received
      119
      Likes Given
      35

      Default Re: Tundu Lisu - Hapa kuhusu majaji umechemka

      Katika macho ya jumuia ya Watanzania walio wengi wanaielewa Mahakama kama chombo cha haki kwa wenye pesa au mamlaka. Wangekuwa na mahali pengine pa kwenda kudai haki zao wangeepuka kabisa mahakama za kitanzania. Mpaka sasa hivi dhana ya watanzania walio wengi mtu akishinda kesi wanaamini amehonga na akishindwa wanaamini hakuwana na hela za kuongea vizuri na hakimu. Shauri likisikilizwa haraka, anazo na kwa asiyenazo asahau. Kwa mtazamo huo ni wazi chombo hiki kimepoteza heshima yake, hakiaminiki na kinadharaulika na jamii. Wazo la kuwa chombo cha kutafsiri sheria na kutoa haki limebakia nadharia ya mdomoni mwa wanasheria tu. Makimu hutoa neno hili wanapotaka kutambuliwa kama watu muhimu, lakini wanapotenda kazi yao ni chombo cha kupindisha na kuinajisi taaluma hii muhimu.
      Usipate taabu kuthibitisha hili, fuatilia majibu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bungeni. Hata kama si mwanasheria utajua kuwa anaibaka sheria. Mtu mwenye cheo kama cha AG hata kama yeye hajiheshimu basi angeheshimu cheo chake, lakini la hasha! Yeye haheshimu vyote. Anatukana Waheshimiwa Bungeni-Mahala patakatifu. Anapendelea upande anaotaka. Picha ikoje kwa wanasheria wengine waliochini yake?
      Mahakama imejishushia hadhi yenyewe kabla ya Tundu Lisu KUANDIKA CHOCHOTE. Tundu Lisu ameshika kamba ya kuteremshia kaburini jeneza la mahama iliyokufa, hajaua imejiua, msisingizie bure

    6. #144
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3257
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default Re: Tundu Lisu - Hapa kuhusu majaji umechemka

      Quote By dudus
      Asante sana Mkuu kwa mistari murua. Hata hivyo japo ni nje kidogo ya mada, naomba kuuliza: hivi Ibilisi angetamka vinginevyo, yaani Nur badala ya Naar, unadhani angesalimika? Kwa mistari uliyo-refer inaonekana kilichomtimua Ibilisi ni ile kujiona bora kuliko Adam aliyeumbwa kwa udongo regardless yeye (Ibilisi) aliumbwa kwa nini.

      Katika Biblia kuna kisa, japo tofauti na hicho, lakini ndicho kilichomwondoa Ibilisi Mbinguni:


      "Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka Mbinguni,
      Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;
      Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano,
      Katika pande za mwisho za kaskazini
      ", Isa 14:13

      "Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
      Nitafanana na Yeye aliye juu
      ", Isa 14:14

      Mistari hiyo na hasa huo nilio-underline ndio ulimtoa Ibilisi almaarufu kama Lusifa au Shetani au Mkuu wa Mapepo na Majini au Baba wa Uovu kutoka Mbinguni.

      Eid Mubarak.
      Asante sana kwa baraka za Eid. Ibilisi angetoka tu mbinguni, hata angesema Nuur bado angekamatwa kwa kiburi chengine, kama hayo maneno katika Isa: 14:4
      Ubarikiwe.
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    7. #145
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Re: Tundu Lisu umechemka kuhusu majaji

      Quote By jogi
      mkuu Pasco, huyu Ana Makinda si alichaguliwa na kuridhiwa na bunge? pamoja na uchafu wa chenge, tumeshuhudia bunge likimpitsha kuwa mwenyekiti wa kamati NYETI ya bunge?!!!! Nikubaalie japo mara hii tu kuwa, tatizo linalotumaliza ni zimwi CCM.

      Veting pamoja na ccm ni sawa kunywa panadol kama tiba ya malaria!!!!!!
      Tuivurumishe ccm, tuwashughulikie akina chenge & co. tutengeneze protocal za haki na wajibu kuwa mzegamzega mmoja, then veting itakuwa na mantiki.
      Mkuu Jogi,

      1. kwanza nakushukuru kutambua kuwa Spika Anna Makinda, alichaguliwa na kuridhiwa na bunge, ila usichojua wewe
      ni alipendekezwa na nani, who was behind Anna Makindas speakership?, hoa ndio who pays the piper, na
      anachofanya Makinda is just to play the tune ambayo imekuwa called by the one who paid for it!.

      2. Mimi ni mtu ninayeamini on "principles of natural justice", kwa vile Chenge, hajashitakiwa popote kwa kosa lolote,
      he is a clean man, na hana uchafu wowote!, so do EL, ndio maana mimi niko wazi katika kumsupport EL!.Kama JK
      alidiriki kupanda jukwaani na kumnadi Basil Mramba mwenye kesi mahakamani, then Chenge na EL ni malaika kabisa
      mbele ya macho ya CCM!.

      3. Umeniomba "Nikubaalie japo mara hii tu kuwa, tatizo linalotumaliza ni zimwi CCM". Samahani sana, sikukubalii,
      tatizo sio CCM, CCM is just the vehicle, haikujiweka hapo ilipo, imewekwa, hivyo tatizo sio CCM iliyowekwa, bali
      tatizo ni walioiweka CCM hapo ilipo!. That simply means, tatizo ni sisi Watanzania tulioiweka CCM madarakani and it
      plays games on us again and again na sisi tukiendelea kuiweka madarakani again and again na sitashangaa kama
      hata 2015, tukairudisha tena!.

      4. Hii dhana ya kudhania adui mkubwa wa Tanzania ni CCM, is a wrong concerpt, na ndilo kosa kubwa la wapinzani,
      katika chaguzi zote za nyuma kuelekeza mashambulizi yote CCM wakijihesabu ndie adui yao mkubwa, hivyo ku miss
      the target ya adui halisi ni nani!.

      5. CUF baada ya kujaribu mara 3 ikashindwa, ikaamua kutumia principle ya "if you can't beat them, join them", kwa
      mara ya 4 katika uchaguzi wa 2010, ikakubali yaishe, ikawajoin ndani ya SUK katika ndoa ya kukubali kutekeleza
      ilani ya uchaguzi ya CCM, at the same time, its fighting from within, and is hitting them very hard kwa mtindo wa
      "kikulacho" na kikundi cha "uamsho" ni matokeo chanya ya kipigo from within, hivyo kwa 2015 upande wa Zanzibar
      CUF ni njia nyeupe!.

      6. Naishukuru Chadema, kupitia M4C, imeshagundua adui halisi anayewakosesha ushindi, na sasa imejielekeza kwa
      wananchi. Mara baada ya uchaguzi wa 2010 na mafanikio makubwa upande wa Chadema, niliwaeleza kuwa bado
      hawajipanga mkao wa kushika dola, kwa sasa kupitia M4C, wanaonyesha wanajipanga, ila udhaifu mwingine mkubwa
      wa chadema niliousemea ni ule "umimi" kujiamini kupita kiasi kuwa peke yao wataweza!, nilisema peke yao
      hawawezi, na leo nasema te na na tena, "Chadema peke yao hawawezi!", lazima wa join forces kutafuta how they
      work together hata na watu wasiokubaliana nao!.

      7. Japo CUF ni mke wa CCM kwa upande wa Zanzibar, hiyo ni "marriage of convinience", hivyo inavunjika wakati
      wowote "conveniences" zikimalizika, hivyo Chadema inacho kibarua kigumu cha kumtongoza huyu mke wa mtu
      kumhakikishia akikubali kutoka nje ya ndoa, yeye sasa hatakuwa mke tena, bali atageuka mume na 2015 ni yeye
      sasa ndie atageuka kidume na kumuoa huyo mume aliyenae sasa kwa sababu mume huyo ategeuzwa mke!.

      8. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya CUF kule Zanzibar na Chadema itake isitake, ipende isipende, ili kujihakikishia njia
      nyeupe ya kuwa mpangaji wa magogoni kwa 2015, ni lazima ikubali kuisupport ya CUF kwa upande Zanzibar ili CUF
      nao wakubali kuisupport Chadema huku bara!. Chadema wakae chini na CUF, waainishe maeneo ya strong holds za
      kila mmoja na kuachiana maeneo hayo ili 2015, kuepuka kumfaidisha kunguru kwa vita vya panzi!.

      Wasalaam.

      Pasco.

    8. FemaTV & Radio

    9. #146
      Mimibaba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2009
      Posts : 3,171
      Rep Power : 1533
      Likes Received
      761
      Likes Given
      592

      Default Re: Tundu Lisu umechemka kuhusu majaji

      Quote By Pasco
      Mkuu Jogi, 7. Japo CUF ni mke wa CCM kwa upande wa Zanzibar, hiyo ni "marriage of convinience", hivyo inavunjika wakati wowote "conveniences" zikimalizika, hivyo Chadema inacho kibarua kigumu cha kumtongoza huyu mke wa mtu kumhakikishia akikubali kutoka nje ya ndoa, yeye sasa hatakuwa mke tena, bali atageuka mume na 2015 ni yeye sasa ndie atageuka kidume na kumuoa huyo mume aliyenae sasa kwa sababu mume huyo ategeuzwa mke!.

      8. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya CUF kule Zanzibar na Chadema itake isitake, ipende isipende, ili kujihakikishia njia
      nyeupe ya kuwa mpangaji wa magogoni kwa 2015, ni lazima ikubali kuisupport ya CUF kwa upande Zanzibar ili CUF
      nao wakubali kuisupport Chadema huku bara!. Chadema wakae chini na CUF, waainishe maeneo ya strong holds za
      kila mmoja na kuachiana maeneo hayo ili 2015, kuepuka kumfaidisha kunguru kwa vita vya panzi!.

      Wasalaam.

      Pasco.
      Pasco again

      Tafadhali sahau kuwa CDM inaweza kushauriwa kwenye hili. Sababu moja kubwa "never give ccm a lease of life". Hoja zako zina hofu ya mazoea kuwa haiwezekani ukaamka kuikuta CCM haipo madarakani; fine lakini mwenye kauli ya mwisho ni mpiga kura siyo magumashi na matumizi mabaya ya madaraka ili kubaki madarakani.

      Naomba utafakari je agenda za CUF ndizo agenda za CDM AU CCM? Mimi kama mpiga kura agenda yangu ya kwanza CCM itoke madarakani nina uwezo nalo hata kama kura yangu itachakachuliwa. Pamoja na hilo; asilani ushrika na CUF ni na CC pekee si na CDM, ushahidi wa uzandiki wa CUF upokia mahali. Pili nikiwa nje ya utawala wa CCM nitachangia kwa uwezo wangu wote kusimika mfumo rafiki kwa manufaa ya taifa kama ambavyo TL anavyo onyesa kwa vitendo uozo kwenye mfumo wa uteuzi wa nyadhifa za mahakama.

      Naheshimu sana mawazo yako lakini pamoja na yote hayo tafadhali usiwapotoshe watu kwa dhana ya kuinusuru CCM. CCM will go if not now later with no regret.
      Pasco likes this.
      Ukweli utakuweka huru daima

    10. #147
      kuku dume's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2012
      Location : School of Medicine
      Posts : 335
      Rep Power : 424
      Likes Received
      47
      Likes Given
      12

      Default Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Kuna taarifa kwamba pamoja na mambo mengine mahakama inatoa ushirikiano kwa Lissu ili kufichua urojo wa mkuu.
      Serikali yatuma watu wake kununua nakala za JAMHURI katika mitaa ya Posta.
      Watu wapiga photocopy nakala ya JAMHURI ili kuutafuta ukweli.

    11. #148
      Raia Fulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2009
      Posts : 9,256
      Rep Power : 2623
      Likes Received
      1292
      Likes Given
      834

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Ungetuwekea kidogo content ya hicho usemacho

    12. #149
      Mapujds's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th May 2011
      Location : Dar es salaam
      Posts : 1,282
      Rep Power : 666
      Likes Received
      118
      Likes Given
      6

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Sikuelewi,fafanua zaidi

    13. #150
      Father of All's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 3,093
      Rep Power : 1044
      Likes Received
      1829
      Likes Given
      3343

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Nadhani majaji wote walioteuliwa na Jakaya ni feki ima wameteuliwa kwa kufuata ushikaji udini ushirika na upuuzi mwingine. Msishangae yule mwizi wa EPA Mwanaidi Majaar siku moja akazawadiwa ujaji baada ya kuuchoka ubalozi au kustukiwa na nchi anakowakilisha maslahi ya bosi wake. Sitashangaa siku moja Andrew Chenge au Chikawe kuzawadia ujaji. Siku hizi ujaji ni si big deal anymore, ni ukuadi wa kawaida wa kuuza na kudhalilisha haki. Nani mara hii kasahau majaji kama Augustine Shangwa aliyeteuliwa baada ya kunyonga kesi ya Mrema iliyodai Mkapa alihongwa shilingi 500,000,000? Hao ndiyo majaji wetu wa vodafaster.

    14. #151
      mmbangifingi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2011
      Posts : 2,569
      Rep Power : 858
      Likes Received
      452
      Likes Given
      2908

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Hili Jamhuri miliki ya nani? kama vile linakuja vzuri kwenye utoaji habari fikirishi,na nn hatma ya mwanahalisi?karidhika na kifungo?namiss ile gazeti
      Who Jah bless, No one Curse!

    15. #152
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1826
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      watasema gazeti la jamhuri ni la CHADEMA.

    16. #153
      Don Draper's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 138
      Rep Power : 379
      Likes Received
      62
      Likes Given
      25

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      mimi nasubiri kuona hayo majina na kisha tutajua wengi wao ni dini gani?

    17. #154
      Duble Chris's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2011
      Posts : 2,340
      Rep Power : 872
      Likes Received
      382
      Likes Given
      304

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Ingekuwa bora ungeliweka hapa maana kwa sasa tunajadili nadharia tu.
      frustration is given by expectationdivide by
      outcome
      ie
      frustration = expectation/outcome


    18. #155
      simplemind's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2009
      Posts : 2,848
      Rep Power : 1155
      Likes Received
      509
      Likes Given
      0

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Kuepusha haya tunahitaji Kitu hiki katiba mpya The Judicial Service Commission :: Republic of Kenya - The Judiciary

    19. #156
      Mromboo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Posts : 232
      Rep Power : 416
      Likes Received
      89
      Likes Given
      80

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Pls kaka tuwekee gazeti huku Rombo halifik leo

    20. #157
      CHUAKACHARA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd June 2011
      Posts : 3,022
      Rep Power : 7642
      Likes Received
      990
      Likes Given
      752

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Quote By Father of All
      Nadhani majaji wote walioteuliwa na Jakaya ni feki ima wameteuliwa kwa kufuata ushikaji udini ushirika na upuuzi mwingine. Msishangae yule mwizi wa EPA Mwanaidi Majaar siku moja akazawadiwa ujaji baada ya kuuchoka ubalozi au kustukiwa na nchi anakowakilisha maslahi ya bosi wake. Sitashangaa siku moja Andrew Chenge au Chikawe kuzawadia ujaji. Siku hizi ujaji ni si big deal anymore, ni ukuadi wa kawaida wa kuuza na kudhalilisha haki. Nani mara hii kasahau majaji kama Augustine Shangwa aliyeteuliwa baada ya kunyonga kesi ya Mrema iliyodai Mkapa alihongwa shilingi 500,000,000? Hao ndiyo majaji wetu wa vodafaster.

      Shangwa ni jaji fake na janga la haki Tanzania
      . Nitapost some of his judgements mzione kuthibitissha aliyoyasema Lisu kuwa hawawezi kuandika hukumu.
      Father of All likes this.

    21. #158
      Teroburu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th August 2009
      Posts : 39
      Rep Power : 506
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Quote By kuku dume
      kuna taarifa kwamba pamoja na mambo mengine mahakama inatoa ushirikiano kwa lissu ili kufichua urojo wa mkuu.
      Serikali yatuma watu wake kununua nakala za jamhuri katika mitaa ya posta.
      Watu wapiga photocopy nakala ya jamhuri ili kuutafuta ukweli.

      mahakama ya tanzania iko imara na haitikisiki
      watanzania amkeni, sio porojo zote zinazoandikwa magazetini bila kufuata maadili ni ukweli. Tujaribu kujitafutia taarifa sisi wenyewe bila kuwategemea wale wanaotoa tafsiri zao za sheria. Tujisomee hukumu sisi wenyewe na tusisubiri wanasiasa watutafsirie hukumu za mahakama kisiasa na na maslahi ya kisiasa.

      Mahakama ni muhimili uliyo imara na haungiliki kama baadhi ya wanasiasa wanavyodai.

    22. #159
      New2JF's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th October 2011
      Posts : 123
      Rep Power : 407
      Likes Received
      26
      Likes Given
      32

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      Wanaanza kugeukana na kuvuana nguo sasa. Jamhuri gazeti alilolianzisha Lowassa!!!!
      "Some people are alive only because it's illegal to kill them." (Unknown)

    23. #160
      fimboyaasali's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 148
      Rep Power : 452
      Likes Received
      20
      Likes Given
      0

      Default Re: Gazeti jamhuri na orodha ya majaji feki; serikali yatikisika.

      jamhuri ni gazeti la lowassa,nadhani inatosha kueleza nini kinaendelea,pia tuwe makini juu ya suala la kuwaponda ama kutowaponda majaji wetu

    Page 8 of 9 FirstFirst ... 6789 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...