Serikali 3 ni bora sana kwa sababu zifuatazo:
(i) Ni muarobaini wa malalamiko ya kuonewa au kumezwa;
(ii) Ni balance nzuri ya uwiano serikalini - 50 kwa 50 katika uwakilishi na gharama;
(iii) Hujuma za kuingiliana ktk chaguzi na kulazimisha chama kimoja kiongoze pande zote mbili zitadhibitiwa kirahisi;
(iv) Hoja ya muunda wa serikali kuwa sera za vyama tutakuwa tumeimaliza;
(v) Gharama za uendeshaji zitapungua kwa zaidi ya 50%. Mfano mmoja, serikali ya Muungano (serikali 2) kwa sasa (siyo SMZ) inalipa wabunge zaidi ya 80 wa Zanzibar (yenye wapigakura pungufu ya laki 4 na 50 na ukubwa sawa na wilaya ya Sengerema). Kila mbunge akilipwa milioni 11 kwa mwezi (11x80) sawasawa na milioni mia 8 na 80. Muundo wa serikali 3 tutakuwa na wabunge 30 au 40 (15 au 20 toka kila upande kufanya kazi za muungano wakigharamiwa na pande zote 2) na wabunge Serikali ya Tanganyika wapatao 150. Huu ni mzigo mwepesi kwa walipa kodi wote. SERIKALI MBILI NI MZIGO!!!!!

Reply With Quote


Follow Us Here