Mkuu Nguruvi3
Hii tuhuma imetolewa sana na Wazenj kuwa Tanganyika imejigeuza jina tu na kujiita Tanganyika. Leo umelithibitisha hilo.
Kama ni kweli hili ulisemalo basi yapasa tuwaombe radhi wazenj kwa kuwafanyia hadaa.
Halafu inakuwaje tena, tutake serikali moja?
Kama Tanganyika ilijibadilisha jina tu basi mkuu Nguruvi3 hata kama na mimi ningekuwa Mzanzibari basi nisingejiita mtanzania.
Kwa maneno uliyoyaandika hapa, mtanzania ni mtanganyika.
Mkuu leo umethibitisha ukiini macho wa Muungano.
Yaani Tanganyika haijafa wala serikali ya Tanganyika haijafa. Hili nalo neno!!!
Haya wamekusikia?
Mkuu unajua maana ya ulaghai? hadaa? Vipi utafanya biashara kihadaa hadaa halafu useme unapata hasara?
Leo, mkuu naona umeamua kuimwaga siri hadharani.
Tanganyika haikufa wala serikali ya Tanganyika haikufa!!!??? Ila ilibadili jina tu. Duhhh!!! Hii kiboko, kwa hiyo kwa miaka 48 ni usanii tu na mazingaombwe. Sasa napata idea kwa nini UAMSHO na wazanzibari wanapiga kelele siku zote.
Kama ni hivyo, maana yake hakuna Muungano au haujawahi kuwepo muungano. Ni usanii kwenda mbele na mazingaombwe tu.
Pasco alipokuja na mada yake ya ratification naona aliekewa mkwara wa nguvu.
Kuna la ziada Mkuu Nguruvi3 ambalo unataka kulisema kutuelimisha zaidi? Masikio yetu yako tayari kupokea darsa. Funguka mkuu.
Follow Us Here