Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

    Report Post
    Page 1 of 37 12311 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 734
    1. #1
      Return Of Undertaker's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Posts : 659
      Rep Power : 541
      Likes Received
      462
      Likes Given
      0

      Default Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      NA MWANDISHI WETU

      CCM imesema imesikitishwa na iliouita usanii mkubwa unaofanywa na Chadema, kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la kuhalalisha mabilioni ya chama hicho yanayodaiwa kutolewa na wafadhali kutoka mataifa tajiri duniani.

      Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyasema hayo leo, Agosti 12, 2012, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijijni Dar es salaam.

      “Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo walifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni." alisema Nape.

      Alisema ,umekuwa ni utamaduni wa Chadema kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za kisanii kina wanapokuwa wameshapewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe kuwa fedha wanazotumia zimetokana na michango ya watanzania wakati si kweli.

      Nape alisisitiza kuwa CCM wanao ushahidi kuhusu zinakotoka fedha na mikataba wanayoingia Chadema na wafadhili hao na kudai kuwa kama hawatasema wenyewe basi yeye (Nape) ipo siku atawasaidia kwa kutaja wafadhili hao na kuanika hadarani mikataba hiyo.

      “Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya, wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama”, Alisema Nape

      Nape alidai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho.

      "Kwanini mabilioni hayo yanatolewa kwa Chadema wakati huu ambapo sasa Tanzania imo katika kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo gesi na mafuta? Na Je ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache hata ndani ya chama chenyewe?", Nape alihoji.

      Alisema, hatua hiyo ya Chadema itaitumbukiza Tanzania katika machafuko yasiyoisha, kama ambavyo inashuhudiwa katika baadhi ya nchi zenye rasilimali kama madini ambako nchi zenye utajiri wa fedha zilijipenyeza kupitia walioitwa wapambanaji wa uhuru na haki katika nchi hizo na hadi sasa hakuna amani.

      "Migogoro mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa.” Alisema Nape.

      Nape alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni muhimu macho na ulaghai huo wa Chadema na wafadhili wao na kukitaka chama hicho na wafadhili wao kama kweli wana nia njema na Tanzania, waweke wazi mashariti ya ufadhili huo wa mabilioni ya fedha ili Watanzania wote wajue kama yana manufaa kwao au la hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya siasa hapa nchini vinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi, hivyo Watanzania wana haki ya kujua.

      Pamoja na kuwataka kuweka wazi mashariti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo, na kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri kutoka nje.

      “ Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasidia kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa.” Nape alisema.

      Nape akawaasa wanasiasa, kuendesha siasa za nchi kwa kuzingatia uzalendo na kukwepa kudumbukia kwenye tamaa za madaraka kujisahau na kuwa tayari hata kuweka nchi rehani, hasa kipindi hichi ambapo ugunduzi wa rasilimali mbali mbali hasa madini, gesi na mafuta vikiwa vinashika kasi nchini na kwamba ugunduzi huo uwe baraka kwa nchi badala ya laana na kuwa chanzo cha kuiuza nchi.
      Quote By John Mnyika
      Katika mitandao ya kijamii kumesambazwa habari zikimnukuu msemaji wa CCM kutoa madai mbalimbali ya uzushi katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu CHADEMA baada ya CHADEMA kuendelea kutekeleza mikakati na mipango yake ya kuwaunganisha watanzania kupitia falsafa ya ‘nguvu ya umma’ katika kuchangia vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika maeneo mbalimbali nchini.

      Nitatoa tamko kamili na kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa iliyotolewa kwa ukamilifu, hata hivyo kuhusu madai yaliyokwisha sambazwa kwenye mitandao ya kijamii na CCM nachukua fursa hii kutoa kauli ya awali kama ifuatavyo:

      Kuibuka huku kwa CCM na kufanya propaganda chafu ni ishara ya kwamba CCM inaumizwa na namna ambavyo watanzania wanajitokeza kuunga mkono CHADEMA kwa hali na mali hivyo CCM sasa inatapatapa kujaribu kudhibiti wimbi la mabadiliko kwa kutumia siasa chafu. Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anapaswa kueleza watanzania iwapo mikakati hiyo michafu ina baraka zake na za serikali anayoiongoza kwa kurejea pia madai yaliyotolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wassira kuwa CHADEMA itasambaratishwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa mbinu mbalimbali.

      CCM kwa kuwa imekuwa na kawaida ya kufanya usanii kuhalalisha fedha haramu kama ilivyofanya kwenye chaguzi zilizopita baada ya viongozi waandamizi wa CCM na makada wake kuchota fedha za chafu kifisadi kama zile za kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na vyanzo vingine vichafu na kuzisafisha kupitia harambee za hadaa zilizofanywa na CCM kwa nyakati mbalimbali; inataka kuichafua CHADEMA inayopata fedha kutoka vyanzo halali kwa njia za wazi ili kukatisha tamaa umma wa watanzania unaochangia vuguvugu la mabadiliko.

      Viongozi wa CCM wameamua kujidanganya, kuidanganya Serikali yao na kujaribu kuwapotosha watanzania lakini CHADEMA inatambua kwamba watu wachache wanaweza kudanganyika kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote; na kwamba watanzania wa leo kwa uwingi wao hawawezi kudanganyika na uzushi wa kijinga wa CCM.

      Ni ukweli ulio wazi kwamba CHADEMA imekuwa ikifanya harambee kwa uwazi kwa nyakati mbalimbali katika kumbi na katika mikutano ya hadhara ikiwemo ya vijijini ambapo michango hutolewa kwa uwazi, aidha michango kwa njia ya simu inaweza kufuatiliwa na kuthibitisha bila shaka yoyote kwamba watanzania wameamua kuchangia mabadiliko ya kweli.

      Madai ya CCM kuwa CHADEMA imepokea au itapokea mabilioni ya shilingi kutoka mataifa ya nje ni ya uzushi na narudia kwa mara nyingine tena kuitaka CCM itaje majina ya serikali, taasisi ama makampuni ya nje ambayo CCM inadai kwamba CHADEMA imepokea mabilioni ya shilingi katika siku za karibuni au inatarajia kupokea.

      Badala ya CCM kuisingizia CHADEMA ilipaswa CCM ieleze watanzania orodha ya vigogo wa Serikali inayoongozwa na wanachama waandamizi wa CCM ambao wanaelezwa kuwa na akaunti nchini Uswisi na nchi zingine wakituhumiwa kupewa fedha za kifisadi kutoka kwa makampuni ya utafutaji wa mafuta, gesi asili pamoja na uchimbaji wa madini.

      CCM ilipaswa ieleze watanzania sababu za kuendelea kusuasua kujivua magamba ya ufisadi kinyume na maazimio ya CCM yaliyofikiwa baada ya msukumo wa CHADEMA kutaja orodha ya mafisadi kwa kuwa kati ya mafisadi hao ni pamoja na viongozi wa CCM walioiingiza nchi katika mikataba mibovu.
      Quote By John Mnyika
      WanaCCM mtanisamehe, lakini imenibidi kutoa kauli hii ya awali kufuatia madai ya uzushi na ya kijinga yaliyotolewa na Msemaji wa CCM dhidi ya CHADEMA

      Madai kama haya yanaendelea kudhihirisha kuwa taifa letu limefika hapa lilipo kwa pamoja na sababu zingine ‘upuuzi wa CCM’. CHADEMA haijawahi kufadhiliwa mabilioni kutoka nje, michango kwenye M4C iwe ni kwenye kumbi za hoteli au vijijini tunapochangiwa na wananchi wenye kutaka mabadiliko ya kweli ni ishara ya imani ambayo watanzania wanayo kwa CHADEMA.

      Badala ya CCM kuisingizia CHADEMA kuwa inafadhaliwa na mataifa ya nje kupora rasilimali za nchi ikiwemo mafuta na gesi yanapaswa kupuuzwa kwa kuwa CCM ndio inao wajibu wa kuwatajia watanzania viongozi wa Serikali na CCM waliongiziwa mabilioni Uswisi kuingia mikataba mibovu ya rasilimali za nchi yetu.

      Aidha, CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kuwataja kwa majina wanaoingia mikataba mibovu ikiwemo kwenye madini, CCM kwa kuwa ilikubali kuwa ina magamba ya ufisadi irejee kwenye orodha ya mafisadi na kuchukua hatua ya kujivua gamba badala ya kufanya siasa chafu dhidi ya CHADEMA.

      Majibu zaidi mnaweza kuyasoma kwenye mnyika.blogspot.com na kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kupitia CHADEMA katika kuwezesha Tanzania kupata uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya taifa letu na watu wake wote bila kujali itikadi. Hakuna Kulala, Mpaka Kieleweke
      Dr. Slaa: Nape kakurupuka!

      *Aponda hoja zake, adai hazina tija
      *Mjumbe NEC naye amshangaa


      KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willbrod Slaa, amesema kamwe hawezi kujibizana na hoja za kukurupuka zilizotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye.

      Kauli ya Dk. Slaa, imekuja siku moja tu baada ya Nape kukituhumu Chadema kuwa kimekuwa kikiendesha harambee za kukusanya fedha, jambo ambalo ni sawa na usanii mtupu.

      Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema Nape si saizi yake kisiasa na wanachokifanya CCM ni kuweweseka na jinsi chama chake, kinavyozidi kukubalika kwa Watanzania.

      Alisema CCM, wamekuwa wakikurupuka kutoa hoja ambazo hazina msingi na badala yake zimekuwa na mrengo wa kuwachanganya Watanzania.

      “Kwanza napenda kusema Nape si saizi yangu … hoja zake zote nazipuuza, zimejaa propaganda na uchochezi kwa Watanzania.

      “Inashangaza kusikia watu hawa wanatuhumu chama chetu, eti kinapokea fedha chafu, inashangaza kuona wao ndio polisi, usalama wa taifa na Benki Kuu (BoT), sasa inakuwaje wanaacha fedha hizi zinaingia nchini?” Alihoji Dk. Slaa.

      Alisema inaonyesha wazi namna ambavyo Nape amekosa hoja za msingi za kuwaambia Watanzania.

      Alisema atafurahi kusikia Nape anataja mataifa ambayo yamekuwa yakitoa fedha kuifadhili Chadema, kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza propaganda.

      Alisema kuna sheria ya kudhibiti fedha chafu ambayo imepitishwa na Bunge, sasa inakuwaje utekelezaji wake unakuwa mgumu.

      “Nawaomba Watanzani watuelewe tunachofanya, kwani kuendelea kuwasikiliza watu hawa tunapotezea mud wetu.

      “Watanzania wanatakiwa kufahamu, kuwa umoja wa utaifa unavurugika kutokana na uchochezi kutoka kwa viongozi au watu waliopewa dhamana ya kusimamia na kulinda amani.

      “Nimechoshwa na kujibu hoja za kitoto na hii itakuwa ni mara ya mwisho kwangu kumjibu Nape, kwa sababu hoja zenyewe hazina mashiko kwa wananchi.

      “Nasema hivyo, kwa sababu watu hawa wanakurupuka kutoa hoja zisizokuwa na mantiki yoyote…hawana hata makabrasha ya ushahidi wa maneno wanayoyasema …sijui ni aina gani ya viongozi?” alihoji Dk. Slaa.

      Juzi Nape alikutana na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam na kudai CCM, imeshtushwa na kasi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuendesha harambee za kukusanya fedha kila kukicha, kitendo ambacho ni sawa na usanii.

      Alisema, CHADEMA kimekuwa kikiendesha usanii huo, licha ya ukweli kuwa, kinapokea mamilioni ya fedha kutoka mataifa ya nje.

      Alisema CCM, imesikitishwa na kushangazwa na usanii unofanywa na CHADEMA, kwa kuwahadaa Watanzania, kwa kufanya harambee ili kuhalalisha uwepo wa mabilioni ya fedha wanazopewa na wafadhili wao nje ya nchi.

      ‘‘Umekuwa utamaduni wa chama hiki kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za kisanii, baada ya kupewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe fedha wanazotumia zimetokana na michango ya Watanzania, wakati si kweli.

      “Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha fedha walizopewa na wafadhili kutoka nje ya nchi, kwa lengo la kuendeleza operesheni mbalimbali nchini. Cha kushangaza, badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania ukweli wa haya, wanaanza kuwahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato haya, mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama.

      “Hebu tujiulize, kwa nini mabilioni haya yanayotolewa kwa Chadema wakati huu, ambao nchi yetu inaendelea kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali, zikiwamo mafuta na gesi? Je, ufadhili huu licha ya kufichwa sana na kufanywa kwa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu?” alihoji Nape.

      “Ni muhimu Watanzania tukawa macho na ulaghai huu na tunawataka wafadhili wao kama kweli wana nia njema na nchi yetu, waweke wazi masharti ili Watanzania watambue fedha hizi zina manufaa au la,” alisema Nape.

      MJUMBE WA NEC

      Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema anashangazwa na kauli za Nape.

      “Nimeshangazwa mno na kauli hii, nimeshtushwa kusikia eti kuna mataifa ya nje yanayotoa fedha nje kwa ajili ya kuisaidia Chadema…kumbuka Serikali yetu zaidi ya asilimia 30 tunapewa na wafadhili.

      “Naamini kusaidiwa na mataifa si ajabu, kwa sasa hata sisi CCM tunasaidiwa na mataifa ya nje ambayo ni rafiki zetu kifedha na kiutawala.

      “Naamini Nape ni kiongozi mkubwa ndani ya chama, hii mikataba anayosema angeitaja ningefurahi sana… huu ni udhaifu mkubwa kwa kiongozi wangu, huu ni mwendelezo wa kujenga majungu na fitina,

      …hoja yake ya kusema atawataja ni miujizi, kwa sababu hii si mara ya kwanza kwake, kuibuka na maneno ya aina hii… nadhani kiongozi katika chama kikubwa na tawala wanapaswa kukaa chini na kutafakari kabla ya kuongea,” alisema mjumbe huyo.


      CHANZO: Mtanzania - Agosti 14, 2012

    2. Miaka 50

    3. #2
      sabasita's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2009
      Location : HOLLYWOOD
      Posts : 956
      Rep Power : 677
      Likes Received
      145
      Likes Given
      135

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      boooooo..kwenda aaaaa zako huko

    4. #3
      mdizi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th January 2011
      Posts : 1,106
      Rep Power : 798
      Likes Received
      309
      Likes Given
      66

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Thanks god ... CHADEMA is the most famous chorus in this country

      Nape is dancing it now and always will
      alex50, Remmy, mpenda and 5 others like this.

    5. #4
      Ni Mimi Msiogope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 284
      Rep Power : 408
      Likes Received
      152
      Likes Given
      31

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      "Kazi ya upande wa mashtaka ni kuthibitisha mashtaka na si kazi ya mshtakiwa" Nape ni mwepesi sana!.. Anataka CHADEMA wataje nini? Kama yeye anadai kuwa anayo 'mikataba' kwanini asiitoe?
      Ujinga ni kumtangazia adui yako "Nimekuzunguka pande zote" ili anyooshe mikono juu!.. Ajipange upya.
      alex50, mvingira, gmosha48 and 3 others like this.

    6. #5
      Yaya Toure's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2012
      Posts : 1,214
      Rep Power : 651
      Likes Received
      266
      Likes Given
      117

      Default

      Daaah nape bwana..

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Sometimes's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th December 2010
      Posts : 1,365
      Rep Power : 760
      Likes Received
      230
      Likes Given
      39

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Nimeipenda hii sentensi"wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho".Hii ina maana zile pesa tulizoambiwa zimewekwa Uswisi kwenye akaunti za watu binafsi na makampuni ya gesi na petroli yanayofanya utafiti ni shukrani kwa CDM!

    9. #7
      Salary Slip's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 1,338
      Rep Power : 690
      Likes Received
      648
      Likes Given
      380

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Mfa maji haachi kutapatapa.Wewe na chama chako ndio mnauza nchi yetu kila kukicha.Hizo ni propaganda zenu kama zile za udini na ukanda.Baada ya hizo kuwashinda sasa mnakuja na propaganda mpya.Tumewachoka na hata nchi wafadhili ni wazi hawana imani na nyinyi lakini unalolisema hawawezi kilifanya kwa lengo hilo.
      alex50, TAYADI and FreedomTZ like this.

    10. #8
      Ndyali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2011
      Posts : 549
      Rep Power : 487
      Likes Received
      140
      Likes Given
      3

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Quote By Ni Mimi Msiogope
      "Kazi ya upande wa mashtaka ni kuthibitisha mashtaka na si kazi ya mshtakiwa" Nape ni mwepesi sana!.. Anataka CHADEMA wataje nini? Kama yeye anadai kuwa anayo 'mikataba' kwanini asiitoe?
      Ujinga ni kumtangazia adui yako "Nimekuzunguka pande zote" ili anyooshe mikono juu!.. Ajipange upya.
      Huyu dogo amepandikizwa roho ya uchawi kwenye nafsi ya hajitambui msameheni !!!!
      Endangered likes this.

    11. #9
      Sungurampole's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 17th November 2007
      Posts : 704
      Rep Power : 728
      Likes Received
      121
      Likes Given
      555

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Quote By Return Of Undertaker
      ..... huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa.” Alisema Nape.....
      Hapa nafikiri Nape alipitiwa alikuwa anaongelea DRC labda, kwa Tanzania hizo rasilimali zinachotwa mchana kweupe, AMANI tele haisubiri machafuko wala migogoro.
      There is a higher court than courts of justice and that is court of conscience.

      It supersedes all other courts.
      Mohandas Gandhi

    12. #10
      adolay's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th December 2011
      Posts : 1,646
      Rep Power : 773
      Likes Received
      493
      Likes Given
      501

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Bandubandu humaliza gogo, inawezekana chama cha msim kuihenyesha ccm? Nape tena!

      Nitarudi baadae ngoja niangalie kwanza chesea na man city.
      mvingira and TAYADI like this.

    13. #11
      yaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2011
      Posts : 676
      Rep Power : 535
      Likes Received
      210
      Likes Given
      67

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Inasikitisha sana kwa mtu wa cheo chake kusema vitu kama hivyo.
      Nilidhani yeye mwenye nyumba angekuwa wa kwanza kumtaja mkaazi anayetaka kuichoma nyumba yake kwa kushirikiana na mtu wa nje kuliko kumtaka mchomaji huyo awaambie wakaazi wengine wa nyumba hiyo ni nani anayeshirikiana naye katika njama mbaya hiyo.

      Eti wasipowaeleza wa-Tz ukweli yeye atasema. Ni nini kinachomzuia kusema sasa? Anasubiri mpaka moshi uanze kufuka ndipo aseme jamani nyumba yangu inaungua na mchomaji ninamjua lakini sikutaka kumsema!!?? Wenye akili watamshangaa sana, ndivyo ilivyo kwa kauli hii ya kwake Mhe. Nape.

      Mimi ninadhani kwa ushindani uliopo kwa sasa TZ, yeye angebuni njia rahisi zaidi ya ile ya CDM ili kuhuisha chama chake CCM, kuliko kutoa kauli zenye utata kama hizi ambazo zinazidi kukidhoofisha.
      PENDING'ULA and TAYADI like this.

    14. #12
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,421
      Rep Power : 10874
      Likes Received
      3799
      Likes Given
      426

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Ooh boy! Mropokaji at work
      mtozwaushuru likes this.

    15. #13
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 4,157
      Rep Power : 1846
      Likes Received
      1431
      Likes Given
      1539

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Huyu jamaa nashindwa nim-define vipi....Kauli kuwa kuna watu wanavizia utajiri wetu ni ujinga na upumbavu...Ni kweli kuwa huyu Nape Nnauye hajui kuwa kuna wawekezaji wanachimba madini utadhani ni ya kwao kipindi hiki kwa mikataba mibovu iliyofikiwa na chama chake na serikali yake? Ni kweli kwa akili zake anaamini chama chake na serikali yake wamelinda mali ya umma kwa kiwango cha kuridhisha hasa madini na wanyama pori? Ni kweli huyu Nape anaamini kuwa CCM haipokei pesa toka kwa mafisadi na wezi? Ni kweli huyu Nape anaamini kuwa serikali yake haipokei misaada toka kwa hao anaowaita ni maadui wa Tanzania?

      Ukweli ni kuwa CCM na serikali yake wamekuwa na kuweweseka sana wanapoisikia CHADEMA, na hii ni dalili njema kwa CHADEMA, na huyu kilaza Nape anapaswa kufahamu kuwa, hata kama kuna ukweli kuwa CHADEMA inapokea hiyo misaada kwani kuna kosa? Mbona hii ni kawaida kabisa, Mbona wao CCM wanamahusiano ana vyama vingine, na kuna siku Katibu mkuu wa CCM alipokea wageni toka nchi moja(jina limenitoka) wakiwa ni wafanyabiashara wakubwa toka chama kinachotawala kwenye hiyo nchi? Kwanini CCM wanapenda kuleta propaganda za kijinga na kishenzi kwa kila chama wanachodhani kuwa ni kikwazo kwao? Huu ni upuuzi wa Nape na chama chake pamoja na serikali yake.

      Go to hell CCM.
      "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"
      "Matatizo hayawezi kutatuliwa na uwezo ule ule mdogo wa watawala wa CCM walioyasababisha"




    16. #14
      Shardcole's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,393
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1032
      Likes Given
      4

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Lissu aliwataja wabunge wa CCM wenye maslahi binafsi na tanesco, wakaja hivi hivi kubwabwaja bila nao kutaja basi hao wapinzani wanaowatuhumu, Nape mbona anamake cheap propaganda na kudhani hivi zama za 1940, anatakiwa ajue kwamba hiki si kizazi cha wajinga kwani yeye kashindwa kuisamimia serkal yake na mikataba mibovu.
      Pia ni vyema angezungumzia pia na swala la DEO FILIKUNJOMBE on M4C.
      mtozwaushuru and TAYADI like this.

    17. #15
      tedo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 17th August 2011
      Location : uchochoroni
      Posts : 5,479
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1259
      Likes Given
      880

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Nape, Dr. Ulimboka amesharudi. Tunasubiri kauli yako kuhusu kurejea kwake.
      Watanzania tunasubiri kauli yako kwa hamu..
      mvingira and TAYADI like this.

    18. #16
      ukwelikitugani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th October 2010
      Posts : 659
      Rep Power : 568
      Likes Received
      294
      Likes Given
      855

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      Kuna muungwana aliwahi kuleta thread ndani humu '" Chunga Ccm inapoanza kulia rafu"..! hawajamaa ukweli wameshikwa PABAYA. Na bado bwana nape,utavua hadi nguo ya mwisho muziki ukikolea sawasawa. Go Chadema, go!
      Utii bila Uhuru ni Utumwa,
      Uhuru bila Utii ni Wendawazimu.. by Julius K. Nyerere

    19. #17
      Godwinnko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Location : Moshi
      Posts : 484
      Rep Power : 669
      Likes Received
      111
      Likes Given
      64

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!

      carolite at work
      TAYADI likes this.

    20. #18
      Shardcole's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,393
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1032
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By Molemo
      Ooh boy! Mropokaji at work
      thanks kamanda for your realization on it cheap petty propaganda.

    21. #19
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,606
      Rep Power : 15261
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2866

      Default re: Nape azungumzia Harambee ya CHADEMA, wamjibu na kusema kakurupuka!



      Dalili za mtu mzima kuchanganyikiwa si lazima aokote makopo. Haya mambo ya Chadema kutoka Chama cha Msimu na kuwa chama cha Uwajibikaji kinaichanganya kabisa CCM.

      CCM ikipata nafasi ya kuvuna mapesa ni haki yako, vyama vingine ni makosa, acheni usanii huu akina Nape. Ipo siku Nape utavua Gamba na kuvaa gwanda, na ulivyo kinyonga sitashagaa.
      KANIALE likes this.

    22. #20
      KISUNGURA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Posts : 31
      Rep Power : 427
      Likes Received
      5
      Likes Given
      7

      Default

      Nape na chama chake amechanganyikiwa. Yeye anafikiri watanzania wa leo ni kama wa enzi zile ya 'zidumu fikra za mwenyekiti' watu wana uelewa kwa saaaana kuliko yeye na chama chake.


      Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
      TAYADI likes this.

    Page 1 of 37 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...