John John Mnyika umeonyesha umahiri mkubwa katika kuchangia mijadala na kutoa hoja binafsi bungeni, na hasa katika kikao hiki kinachokaribia kwisha. Sikushangaa kwamba michango hiyo na hoja hizo hazikuwalenga watu wako wa Ubungo maana katika kipindi chote cha kuelekea katika mkutano huu, hukuwahi kuzunguka jimboni na kufanya mikutano na wapiga kura wako ili kubaini kero na matatizo yao na kuona namna bora ya kuyawasilisha. Muda mwingi ulikuwa na operesheni sangara, ukikosoa hali mbaya ya uongozi na uduni wa maisha ya watanzania wa majimbo mengine.
Kwa vile sasa unarudi Dar es Salaam (nikiamini hupitilizi kwenda Kinondoni - CDM Makao Makuu), njoo uone yale yale uliyoyatumia kukufikisha hapo ulipo yakiwa hayajaguswa. Kero zenyewe naweza kukumbusha kwamba:
Ukosefu wa maji japo wizara ya maji na bomba kubwa linapita ubungo;
Makorongo kwenye barabara zetu zinazoingia ndani kutoka barabara kuu ya Morogoro;
Ukosefu wa vituo vya kutosha vya afya, polisi;
Uhaba wa vyumba vya madarasa katika mashule yetu;
Ukosefu wa umeme katika maeneo ya pembezoni kama vile mbezi msumi, makabe na mbopo n.k.
Usidanganywe na watu watakaokutaka uende kwenye ziara M4C ukajikuta unang'olewa, 2015 ni keshokutwa tu!
Tafakari, chukua hatua.

Reply With Quote

Follow Us Here