Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imetoa taarifa kuwa JK atasafirir kesho kuelekea Ghana akiungana na wageni maarufu 16 akiwemo Hilary Clinton kuhudhuria Mazishi ya aliyekuwa raisi wa nchi hiyo John Mills yatakayofanyika kesho.
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imetoa taarifa kuwa JK atasafirir kesho kuelekea Ghana akiungana na wageni maarufu 16 akiwemo Hilary Clinton kuhudhuria Mazishi ya aliyekuwa raisi wa nchi hiyo John Mills yatakayofanyika kesho.
Akistaafu apewe ubalozi wa umoja wa mataifa wa kuzikana!!itamfaa sana jamani duuu....jana ametoka kuzika msata,leo ghana..
Yule anaehesabu safari za mkulu atujuze ni ya ngapi hii.
Akitoka Ghana anapitiliza Ethiopia kuzika pia!!!
Kikwete atajifunza na kuacha kuzurura lini?
Ingawa ni haki yake kwenda anapotaka kwa mujibu wa sheria, rais wa Tanzania Jakaya Kikwete hana huruma na walipa kodi wake. Pia hana muda wa kushughulikia masuala muhimu ya kitaifa zaidi ya kupenda kuzurura. Inafikia mahali watu wanajenga dhana kuwa anakwepa majukumu yake. Pia inaanza kujengeka dhana kuwa rais Kikwete haoni wala hana haja ya kuwa na makamu wa rais ambaye kisheria anapaswa kuwa msaidizi wake. Juzi alikuwa Kampala kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Rais Mwai Kibaki mchumi asiyependa makuu alimtuma makamu wake, Stephen Kalonzo Musyoka. Kikwete alirejea jana na leo tunaambiwa yuko kiguu na njia na ujumbe wa maswahiba wake wasio hata na umuhimu katika ziara yake kuelekea Ghana eti kwa ajili ya mazishi ya rais wa nchi hiyo. Je kuzika ni bora kuliko masuala nyeti kama tishio la mgomo wa walimu au ule wa madaktari ambao bado unasuasua? Ni juzi juzi karejea toka Brazil kwenye mkutano ambao haukuwa na maana sana. Kama kawaida, Kibaki alimtuma waziri wake mkuu kumwakilisha. Kikwete, kama kawaida yake, aling'ang'ania yeye na mke wake kwenda kule kiasi cha kueleweka alikuwa akikwepa mgomo wa madaktari. Misiba imekuwa sehemu ya Kikwete kukimbilia majukumu na matatizo mazito. Walipoanza mgomo madaktari alitumia msiba wa msanii wa filamu kujificha kabla ya kuondoka zake Brazil. Kesho likizuka tatizo jingine utamsikia huyo katimkia Afrika Kusini kujaribu kujadili tatizo la mpaka na Malawi. Kinachokera ni ile tabia ya Kikwete kuandamana na msafara mkubwa watu ambao hata si muhimu wala lazima. Kila siku ni kiguu na njia hadi watu wanamwita Vasco da Gama.
Je Kikwete ni mgumu wa kujifunza au ni kiburi na kupenda raha na kuzurura? Je atajifunza lini kuwa safari zake ni mzigo kwa taifa na chanzo kizuri cha utoro na matumizi mabaya yanayoongeza uzito kwa maisha ya malipa kodi maskini?
Huyu si wa kujifunza. Ana ka ugonjwa ka kupenda kurukaruka na kuahirisha matatizo kijana wangu huyu. Hilo jina baba. Kweli unajua kupayuka mwanangu.
mpayukaji
Wivu utakukondesha mkuu, huyo ni kiongozi wa nchi. Usifikiri anajiondokea tu na kusafiri. Mwambie Mjomba wako SLAA ajitahidi kupiga propaganda manake sera zimewaishia na sasa wanawategemea watu kama nyinyi kupiga majungu na watanzania wasio na upeo wa kuelewa wakaamini yeye ndo anafaa wakati hata Mwanamke amemshinda ndani ya nyumba, jambo ambalo sasa hata CDM wanaona ni mzigo kwa chama.
Nona mnamezea mate suti ya JK, acheni hizo, Rais wa watu huyo. Binafsi nam-admire rais wangu kwa jinsi ambavyo anawapotezea na majungu yenu. Jk bwana sidhani kama tutakaa tupate rais kama huyu, mtu wa vitendo tu majungu maabdaye. Hivi takribani magonjwa yote sugu yatatibiwa hapa nchini, Vyandarua vya kumwaga kwa kila kaya, bara bara za lami nchi nzima. Mnataka nini? ZITTO anawaambia kwa njia ya picha kua SLAA na MBOWE hoi bin taaban ninyi mmeng'ang'ania. Kama ni mimi mwaka 2015 rais anatoka CCM waziri mkuu ZITTO nukta.
Akirudi tuu anateua VIONGOZI
afadhali umelijua hilo kuwa wewe ni mvivu wa kufikiri. Siwezi kukujibu zaidi ha hapo kwa vile najua niliyosema ni ya kweli na yamekuchoma kweli. Najua uko kazini mkuu, komaa usije ukakosa kwenda chooni. SLAA hivi ssa yeye anapumzika na mama yenu mshumbuzi baada ya kutumbua fedha za chama siku nzima, wewe unakomaza misuli kutetea ujinga.
america at work. Hiki kifo cha Mills nimehsi ki2
Duh! JK huwakilishwi? Lakini acha uende japo safari ili upatekupumzika maana Umelikoroga unashindwa kunywa. Nenda baba usije ukadondoka puuuuu!!!!!!!!!!!
Ni uamuzi mzuri kabisa wa Mhe JK kushiriki katika maziko ya Hayati Mills (RIP) - anatuwakilisha sote. Ombi letu ni moja tu - basi angaa ajifanye kuweka sura ya huzuni katika uso wake ili Waghana wasije wakafikiri utamaduni wa kuomboleza kwa Wabongo ni kuweka tabasamu usoni au kucheka.
Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!
R.I.P John Mills
huyu wa kwetu mwacheni yuko kuitafuta rasi ya tumaini jema.
SIYO WOTE WANAOTANGATANGA WAMEPOTEA
Follow Us Here