Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
Nimeamua kuiweka hii kwenye separate thread kwa sababu nimeona ina extra concept kulingana na ile ya jana.
Wakati nanunua gazeti nilitumaini kabisa Membe atakuwa na hoja ya ku-convice kwani humu JF mnaongea tu kama mimi. Kwa wale waliosoma RAIA MWEMA wafungua attached paper kwenye ukurasa wa iv. Ndipo anaeleza msimamo wa Serikali kuhusu mpaka wa Ziwa Malawi.
Nakiri kwamba hata wakati naleta thread ile ya kwanza, nilitumaini Bernard Membe atakuwa ameongelea findings ambazo zingetushawishi na mimi nisingesita kuungana kwenye nia ya kukidhi madai haya ya Lake Malawi.
Lakini baada ya kusoma speech ya Membe basi matumaini yote ya kulipata Lake Malawi yamenitoka. Narudia sipingi Tanzania kupata sehemu ndogo ya Lake Malawi kama baadhi mnavyoropoka. Na hata mnavyoropoa wengine hainipi matumani ya kulipata hilo Ziwa. Lakini aliyenisikitisha zaidi ni Waziri Membe na sasa kwangu ni dhahiri kwamba tusahau kabisa kulipata Ziwa hili.
Siku moja nilifanya hesabu ubaoni nikapata jibu na baadaye nikaongeza madoido mwalimu akanikata maksi akasema "Kujitawaza kwingi mwisho unashika kinyesi". Naona ndugu yetu Waziri Membe kaingia katika mtego huu. Kwa nini nasema hivi? Ninanukuu majibu yake kama ifuatavyo:
**** Mheshimiwa Spika,
Lipo tatizo la muda mrefu kati yetu na nchi jirani ya Malawi linalohusiana na mpaka kwenye Ziwa Nyasa. Tatizo lenyewe ni kwamba Malawi wanadai kwamba ziwa lote kaskazini ya Msumbiji kuelekea Ruvuma na Mbeya ni mali yao kwa mujibu wa Mkataba wa Heligoland uliowekwa mwaka 1890.
Mheshimiwa Spika,
Tanzania kwa upande wetu tunasema kuw ampaka wa kweli kati yetu na malawi unapita katikati ya ziwa hivyo kufanya eneo lote la Kaskazini Mashariki ya Ziwa kati Latitude digrii 9 na digrii 11 kuwa mali ya Tanzania kwa mujibu wa mkata huouo wa Heligoland wa mwaka 1890 ambao ulikubali kuwa kwa vile kuna maeneo ya mpaka ambayo hayana mantiki, pande zinazohusiana zikutane na kurekebisha. Aidha tunazo ramani ambazo waingereza wenyewe walipitisha mpaka katikati kama ulivyo mpaka kati ya Msumbiji na Malawi.
****
Nimemalizia hapa kwa sababu mengine yanayofuata ni diplomatic process. Sasa hapa tuchambue hotuba hii ya Membe. Binafsi nimeusoma mkataba wote wa Heligoland na wala si alichokisema Membe. Kama membe anataka kuikomboa Tanzania walau tupate sehemu ya Ziwa basi washauri wake wamempotosha kutumia mkataba ule ambao hautetei hoja yake hata kidogo.
Lakini pia Membe ni mmoja wa wanaodhani watanzania wa sasa hawajui kufukua mambo na ndiyo maana kwenye thread yangu nimesema tutumie usomi wetu. Membe ametaja kwamba sehemu ya ziwa kati ya Latitude digrii 9 na digrii 11 ni mali ya Tanzania.
Hapa ndipo Membe ameumbuka umbuko ambalo hatalisahau. Kwa nini nasema kaumbuka. Kaumbuka kwa sababu geography ya Tanzania wote tunaijua. Ncha ya juu kabisa ya Lake Malawi iko kwenye coordinate { S9.49214 E34.03563} ambapo ni only 7.0km kutoka kijiji kiitwcho Matema kilichopo kwenye coordinate { S9.49601 E33.97215}.
Ukiangalia coordinate hizi maana yake ni kwamba Ziwa Malawi linaishia kwenye Latitude 9.49214. Sasa hapa Membe anasema eti ni kuanzia Latitude 9. Kwa maana hii ya Membe kama Ziwa ni letu kuanzia latitude 9 maana yake ni kwambaMmembe kafanya makosa kwa kulirefusha ziwa hili kwa umbali wa 54.4km kuelekea kaskazini!
Watu mnaotoka kusini hasa Mbeya mnafahamu sehemu iitwayo Matamba. Hapa coordinate zake ni { S9.01171 E34.09959}. Kwa mujibu wa Membe, hii Matamba ingekuwa imeguswa na Ziwa hili!
Hakika waliomletea Membe hizi data wamemvuruga kuliko kulietengeneza suala hili. Ziwa Malawi au Nyasa linaishia kwenye Latitude 9.49214 kama nilivyosema hapo juu. Hapa membe kadanganya Bunge na kadanganya watanzania kasi kwamba sijui sasa ni nani mwenye nguvu ya kulitetea hili.
Tuje sasa kwa upade wa kusini yaani unaotambuliwa na membe kama sehemu yaetu ya Ziwa. Membe anasema sisi mali yetu ni mpaka kwenye latitude 11. Sijui wangapi mmeona kosa hili la mwaka. Unaposema kwamba unaishia hapa kwenye Latitude 11, je mnaotetea hoja hii mnaelewa madhara yake? Kama hamyajui basi mimi nayasema hapa.
Kama Membe kasema Bungeni kwamba tunaishia kwenye Latitude 11 basi maana yake pale ni kaskazini ya sehemu iitwayo Liuli ambayo iko { S11.05023 E34.63908}. Kumbe, Mwanakijiji wa Liuli haruhusiwi kuvua samaki kwenye ziwa lile kwa sababu ni sehemu ya Malawi, kwa mujibu wa Waziri Bernard Membe!
Yaani mwanakijiji huyu wa Liuli, anakuwa amekiuka mpaka kwa kilomita 6.6 kwa mujibu wa Serikali anayoshiriki membe wala si kwa mujibu wa Serikali ya Malawi!
Nimeanza na mfano huo wa Liuli ambao najua wengine hampaju ahapo. Sasa tuje kwenye mfano ambao wengi mnaujua na mmeutumia kunipinga humu na kuniita mimi ni mmalawi.
Mfano wenyewe ni wa Mbamba Bay. Ndiyo maana nimesema kajipangeni hii kesi tutajikuta tunasambaratika tukidhani tunatetea huku tunajiangamiza. Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.
Hii maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Mbamba Bay haiko katika eneo linalotambuliwa na Waziri Membe kwa latitude degree 0.30519!
Uki-convert hizi latitude kwenda kwenye kilomita basi maana yake Membe haitambui Mbamba Bay kwani iko 33.7km nje ya eneo ambalo Tanzania tunamiliki ziwa!
Waziri membe pia inaelekea kuwa hajui mpaka unavyopita pale Msumbiji. yeye anasema kule ni nunu kwa nusu lakini wote fungueni ramani muone kama hilo nalo lina ukweli. Mpaka wa Msumbiji ni nusu kwa nusu kuanzia kwenye latitude 11 had 13 lakini kuanzia hapo kueleka kule chini kusini ziwa lote liko sehemu ya Malawi na linaishia kwenye coordinate {S14.44635 E35.23539} ambako ni latitude 14.44635.
Hivyo, tujenge hoja zinazojikita kwenye ukweli na tusishabikie mambo kama vile Simba na Yanga. Hapa hatufanyi ushabiki. Hapa tunasaidia kujenga na kupima hoja kama kweli tunaweza kuisaidia nchi yetu kupata sehemu ya ziwa hili.
Ninasubiri kwa hamu kuona mtakuja na hoja gani kuhusu hizi findings zinazochambua hotuba ya Membe na matokeo yake niliyoeleza humu.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By Nali
Pamoja na hoja zako nzuri/mbaya/ulaghai au vyovyote unavyajaribu iwe, Bado wewe sio mzalendo kabisa kabisa na nina chelea kusema hakika ww sio Mtanzania! Pamoja na kuisoma hiyo treaty neno kwa neno na kuielewa wewe wewe unakua wa kwnza kutaja neno "Ziwa Malawi" tena kwa kurudia rudia!! Hii imenipa mashaka makubwa sana!
Hukuanza hili leo toka juzi nafuatilia threads zako zote katika sakata hili ww ni ziwa malawi tu! Na kama ww ni mtz kweli mbona katk kuusoma hotuba ya membe na kugundua mapungufu na upotoshaji, mbona hukuonyesha ukweli upo wapi? Au njia nyyingine mbadala? Kazi yako toka juzi ni kuponda na kutaja "ziwa Malawi! Shame upon you shalow boy!! Natamani nikuone nikunase kibao!!!
kinachonifanya nimshtukie huyu mleta mada, kila mtu anayetoa hoja kutetea upande wa malawi yeye anagonga <like> tu, nikagundua jamaa ndo wale mashushu wa nchi ya malawi waliopo tz. halafu inaonekana ana id kadhaa za kutetea ujinga wake, na kwakweli kafanikiwa kuwateka watanzania kadhaa walioamua kutoshirikisha akili zao kuhusu mtu huyu wakidhani ni mtz mwenzao kisa anaandika kiswahili sanifu.
all in all ziwa nyasa lipo mpakani hatuwezi kunyimwa kulitumia sababu ya mikataba ya wakoloni mpaka utakuwa katikati ta ziwa hawataki tutawatwanga na kulichukua lote kabisa!
wewe nawe ukiwatwanga unapata faida gani hata mafuta yakipatikana hutofaidi japo buku zote watakula mafisadi utapata nn tumia kichwa chako vizuri
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By Nikupateje
Watanzania ndugu zangu. kwa ushauri wangu naomba kama hamjui basi acheni kabisa kutaja haya mambo ya latitude kama hayakuwanata kichwani tangu darasa la sita.
Sijui kimekuingia nini kichwani hadi ushindwe kujua hata kwa kuangalia tu kwamba latitude 33 ni chini kabisa umeshaivuka hata Tropic of Capricon na unakaribia kuimaliza Republic Of South Africa!!!!! Mji wa Portville wa South Africa uko kwenye latitude hii!!!!
Ndiyo utetezi wenu huu na tunasema tuna haki ya kutoa maoni!!!!!
Nitakupateje hapo umenikosha maana hiyo Geography yako mm sikuisoma na nina uhakika hata Mwl wako alifika Chuo bila kujua k2 ndo maana watoto wetu wanaingia 4m one bila kujua kusoma
Naomba niwafundisheni darasa lenu wote kuwa mstari wa kijiografia haupiti kijiji kimoja, ukiambiwa Greenwich Meridian time 0 degree inapita Acraa Ghana pia unapita London UK sasa mstari unaopita Ziwa Nyasa nimeukadiria kutokana na evidence data unapitia karibu na 33E (taz picha no 1) na hata hivyo mistari yote inashuka na kupanda initwa Latitude (Taz no.2) Halafu hii mada ilishamalizwa hata na magazeti na humu JF sisi tunaikomaliahttp://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ml#post4402118
Mfano wako mwenyewe nimequote kwenye thread wa Mbamba Bay. Ndiyo maana Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By congobe
wewe nawe ukiwatwanga unapata faida gani hata mafuta yakipatikana hutofaidi japo buku zote watakula mafisadi utapata nn tumia kichwa chako vizuri
Mimi sifikirii mafuta nafikiria watanzania wenzetu wanaozunguka ziwa wanajipatia riziki yao kwa uvuvi mdogomdogo na kwa umwagiliaji pia! halafu wewe ndio unaotumia kichwa vibaya kwa kufikiria nchi yetu itatawaliwa na mafisadi milele, funguka angalia mbele ipo cku haipo mbali sana nchi yetu itatawaliwa na sensible leaders!
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
Mimi si mtaaalamu wa coordinates, ila nadhani ulichokibainisha kwenye hoja yako kinamantiki kubwa kuliko kile kilichosemwa kwenye Hotuba ya Waziri Membe. Upo uwezekano kuwa Waziri Membe alipotoshwa kidogo na wataalamu wake wa hotuba. Lakini pamoja na hilo, hoja ya TZ kudai umiliki wa mpaka wake ktk Ziwa Nyasa ina mantiki na haibadilishiki kwa technical errors ktk hotuba ya bajeti ya Waziri Membe. Ninaamini kuwa hata yeye (Waziri Membe) hakukusudia kuupotosha Umma au Bunge. Hivyo, Watanzania tuungane ktk hili tuipiganie ardhi yetu.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By JohnQcarney

Mkuu John,
Narudia kama nilivyoeleza kote ni kwamba jinsi maafisa wa Serikali ya Tanzania wanavyotuletea facts za utetezi wao hadharani ndivyo mtu anayetumia akili ananapata wasiwasi kama kwa utetezi huo usio accurate tunaweza kweli kupata hata tone moja la Ziwa Malawi.
Nilidhani ni kosa ni akina membe tu, lakini hata humu JF tumefika page ya tisa kwa thread hii. Ungedhani JF ni ThinkTank kuisaidi nchi kupata mawazo kujenga hoja tupate hata kipande cha ziwa lile.
Lakini, hebu nipe hata post moja humu inayotia matumaini kwamba kwa msaada wa hiyo post basi tunaweza kupata hata tone moja la Ziwa Malawi.
Ukimaliza kusoma hapa, soma matamko ya maafisa wa Malawi akiewemo Foreign Affairs wao. Ukisikia kauli zao hadi unakata tamaa kwamba tutaibukaje ama kweny emazungumzo ama kwenye arbitration. Na kibaya zaidi Malawi ndiyo wako mbele zaidi kutaka kutushitaki kule International arbitrator.
Sasa, humu JF badala ya kuleta point zitakazosaidia, wanazidi kukoroga na Membe wao hata kwa zile ambazo tulitakiwa tuwe accurate.
hivi unadhani wamalawi hawajui Kiswahili? Hivi unadhani hawajui kupekua Hansard ya Bunge letu. Wakisoma huko wakakuta Membe kachemsha unadhani hawawezi kuchukua ushahidi kama huo kwamba hata mipaka ya ndani ya nchi yetu tu hatujui demarcation yake. Mnaodhani ushahidi wa hansard hauna nguvu basi kumbukeni ndiyo moja ya ushahidi uliotumika kwenye kesi ys Mahalu ambapo kauli ya Kikwete kwenye hansard ndiyo iliyomsafisha Costa Mahalu mahakamani.
Ni juu yetu kuendelea kukejeli au kujenga hoja kuhusu ziwa Malawi.
Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By Ukwaju
Nitakupateje hapo umenikosha maana hiyo Geography yako mm sikuisoma na nina uhakika hata Mwl wako alifika Chuo bila kujua k2 ndo maana watoto wetu wanaingia 4m one bila kujua kusoma
Naomba niwafundisheni darasa lenu wote kuwa mstari wa kijiografia haupiti kijiji kimoja, ukiambiwa Greenwich Meridian time 0 degree inapita Acraa Ghana pia unapita London UK sasa mstari unaopita Ziwa Nyasa nimeukadiria kutokana na evidence data unapitia karibu na 33E (taz picha no 1) na hata hivyo mistari yote inashuka na kupanda initwa Latitude (Taz no.2) Halafu hii mada ilishamalizwa hata na magazeti na humu JF sisi tunaikomaliahttp://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ml#post4402118
Nikupateje pia nimegundua Mwl wenu aliwaelekeza coordinate { S11.30519 E34.80449}. kuwa ni point moja tu ya x wakati kwenye ramani ya kitu bapa inaweza someka mara nyingi hizo coordinate zake hivyo je ? (S11.35 sio Longtude ya kusini toka Ikweta?) inakuja ku-coordinate na (E34.8 sio Latitude ya mashariki?) kwa upande wa Ziwa Nyasa wa kaskazini ambao uko Tanzania kuwa hiyo mistari mnaipima kwa km ndani ya mipaka wakati mm napima juu ya Ardhi ya Dunia iwe ni Conture au Grid reference ndo tulifundishwa STD V wala sio 6 Mfano wako mwenyewe nimequote kwenye thread wa Mbamba Bay. Ndiyo maana Narudia kusema kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Membe ni kwamba umiliki wetu wa Ziwa hili unaishia kwenye latitude 11. Mbamba Bay iko kwenye coordinate { S11.30519 E34.80449}.
Kwa hiyo mm na Membe hatuna makosa tukikaribisha hizo digrii ili muelewe kwani hata Ramani najua inaonyesha kabisa 35 E Degree na kwa vile ni round ww karibisha lakini sio kuniambia mstri wa Latitude 33 umepita Mji wa Portville wa South Africa huko ni ile mstari ya 30 Longtude kwenye Capricon
Hivi toka mwanzo usingetaja latitude 33 na badala yake ukataja 33E kama unavyosema sasa, nani angahangaika na wewe.
Hebu soma ulichoandika mwenywe kwenye post yako namba 121 ambayo bahati nzuri hadi sasa hujai-edit au click hapa au isome hapa chini:
By Ukwaju
Nikupateje umeshaamka lkn kwa taarifa yako wajumbe 10 kutoka Malawi wapo hapa Bungeni wakijadiliana na spika kuhusu sakata hilo la mpaka, na wao ndio watakaotudhibitishia ni nani hasa ana wasiwasi au hofu kuhusu hayo maji ya ziwa katika latitude 33 na huo mpaka ulionyooshwa kwenda nyuzi 230 SSW TUVUTE subira mchana haufiki
Sasa, ndiyo uone ni nani kati ya mimi na wewe anayetakiwa kurudi darasa la sita kujifunza kwamba latitude 33 inapita kule chini kabisa hata South Africa inaigusa kidogo tu huko!!!
Hata hapa ulivyopost bado unazidi kujikanyaga. hebu ona unavyosema:
By Ukwaju
(E34.8 sio Latitude ya mashariki?) kwa upande wa Ziwa Nyasa wa kaskazin
Toka lini kukawa na latitude za mashariki?
Ungerudi darasa la sita kama nilivyokushauri ungetambua kwamba latitude zote ni ama za kaskazini au kusini. Hakuna za mashariki au magharibi.
Mchukue mtoto wa darasa la sita akusaidie hili hata hapo Dodoma maana umeeleza mwenyewe kuwa uko Dodoma Bungeni.
.."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
Hizi ni ramani 2 za Tanzania na Malawi na zinaonyesha mipaka kwa uwazi kabisa. Kwamba Ziwa Nyasa limegawanywa mara 2 kwa upande wa kusini kwa maana ya sehemu moja iko Malawi na sehemu nyingine iko Mozambique. Kwa upande wa Kaskazini wa Ziwa Nyasa mipaka inaonyesha Ziwa lote liko Malawi huku Mpaka wa Tanzania ukiambaa kandokando ya Ziwa.
Kwa Ramani hizi 2 ni dhahiri Ziwa Nyasa haliko Tanzania unless uniambie hii mipaka siyo ile ya Berlin 1884 Treaty ambayo Wakoloni walikaa na kuigawa Afrika kama walivyoona inafaa. Mipaka hii ndiyo imeunda Ramani ya nchi za Kiafrika mpaka leo hii.
Madai ya kuwa mpaka wa Tanzania na Malawi imepita katikati ya Ziwa Nyasa ni madai ya uongo. Kwa Ziwa Tanganyika ni kweli mpaka umepita katikati ya Ziwa lakini siyo Nyasa. Kwa hapa Wamalawi wana madai ya msingi kabisa. Kama Tanzania tunataka mpaka usogezwe katikati ya Ziwa Nyasa that is another story. Itabidi twende UN kupeleka madai hayo na sababu zetu za kutaka kufanya hivyo. Nje ya hapo ni kutangaza vita na Malawi na kuitwaa nusu ya Ziwa Nyasa kwa mabavu kitu ambacho kitakuwa hakina tija wala faida kwa nchi yetu labda kama kweli kuna MAFUTA chini ya Ziwa Nyasa tena yawe kwa upande wetu baada ya kuligawa Ziwa Nyasa katikati.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By makoye2009

Afadhali wewe una ujasiri wa kuusema ukweli huu hapo kwenye RED ambao kama ukifuatwa kidogo unatia matumaini kwama tunaweza kufikiriwa kupata sehemu ya Ziwa Malawi.
Mawazo kama haya ambayo yakifanikiwa yanaleta tija ndiyo mawazo ya kizalendo zaidi kuliko kuropoka bila hoja za msingi.

Mkuu nasubiri kipengele kile kinachosema kwamba UN convection ya 1982 inaaply tu kwenye sehemu ile ambayo haina "treaty"
Hivi toka mwanzo usingetaja latitude 33 na badala yake ukataja 33E Hebu soma ulichoandika mwenywe kwenye post yako namba 121 ambayo bahati nzuri hadi sasa hujai-edit au click hapa au isome hapa chini:
Mchukue mtoto wa darasa la sita akusaidie hili hata hapo Dodoma maana umeeleza mwenyewe kuwa uko Dodoma Bungeni.
bado mm niko na Membe nataka nikubaliane naye, kuwa hajakosea kuwaelewesha watanzania kuwa amekaribisha hizo nyuzi ww (nimeQuote ) Membe ametaja kwamba sehemu ya ziwa kati ya Latitude digrii 9 na digrii 11 ni mali ya Tanzania.
Hapa ndipo Membe ameumbuka umbuko ambalo hatalisahau. Kwa nini nasema kaumbuka. Kaumbuka kwa sababu geography ya Tanzania wote tunaijua. Ncha ya juu kabisa ya Lake Malawi iko kwenye coordinate { S9.49214 E34.03563} ambapo ni only 7.0km kutoka kijiji kiitwcho Matema kilichopo kwenye coordinate { S9.49601 E33.97215}. Basi na mm nasema Coordinate ya juu kabisa ya Ziwa Nyasa ni {Latitude 9.24'34" S }na{Longtude 33.59'19E} ndio maana nikasema hilo ziwa ni round na maji huwa yanaongezeka na kupungua kutokana na mvua sasa kosa la membe silijui hayo makosa ya Longtude na Latitude wengi wameshaelewa km ni erros za 33E nitazisahihisha ila mm sio nipo Bungeni nipo Mji ambao kuna Ukumbi wa bunge maana kuna wengine mnafuatilia hata nukta mtajasema ninalala hapo au mlinzi ila ni STD 6
NIMEWEKA LINK YA FLASH MAP uizoom uangalie nani yuko sahihi mpaka Bunge lidanganywe Flash Earth - Zoom into satellite and aerial imagery of the Earth in Flash
SI @ MTU NI PERFECT na si kweli kuwa kalipotosha labda sisi
Sending by: BlackBerry 8100 Smartphone using JamiiForum
Hizi ni ramani 2 za Tanzania na Malawi na zinaonyesha mipaka kwa uwazi kabisa. Kwamba Ziwa Nyasa limegawanywa mara 2 kwa upande wa kusini kwa maana ya sehemu moja iko Malawi na sehemu nyingine iko Mozambique. Kwa upande wa Kaskazini wa Ziwa Nyasa mipaka inaonyesha Ziwa lote liko Malawi huku Mpaka wa Tanzania ukiambaa kandokando ya Ziwa.
Kwa Ramani hizi 2 ni dhahiri Ziwa Nyasa haliko Tanzania unless uniambie hii mipaka siyo ile ya Berlin 1884 Treaty ambayo Wakoloni walikaa na kuigawa Afrika kama walivyoona inafaa. Mipaka hii ndiyo imeunda Ramani ya nchi za Kiafrika mpaka leo hii.
Madai ya kuwa mpaka wa Tanzania na Malawi imepita katikati ya Ziwa Nyasa ni madai ya uongo. Kwa Ziwa Tanganyika ni kweli mpaka umepita katikati ya Ziwa lakini siyo Nyasa. Kwa hapa Wamalawi wana madai ya msingi kabisa. Kama Tanzania tunataka mpaka usogezwe katikati ya Ziwa Nyasa that is another story. Itabidi twende UN kupeleka madai hayo na sababu zetu za kutaka kufanya hivyo. Nje ya hapo ni kutangaza vita na Malawi na kuitwaa nusu ya Ziwa Nyasa kwa mabavu kitu ambacho kitakuwa hakina tija wala faida kwa nchi yetu labda kama kweli kuna MAFUTA chini ya Ziwa Nyasa tena yawe kwa upande wetu baada ya kuligawa Ziwa Nyasa katikati.
Sikia mr makoye2009, usikubali wamalawi wakufanye mjinga. Mie naomba nikuhakikishie kwamba sie tuna eneo katika ziwa nyasa tena mpaka uko katikati: Katika mkutano wa Berlin hakukuwa na mipaka ya uhakika iliyooneshwa hasa ktk maeneo ya maji kama maziwa mito mikubwa maana sehemu hizo ilikubaliwa kuwa ziwe free trade zone. Hata Wamalawi hawasemi kabisa habari ya berlin conference wanajua hakuna haki waliyopewa kupitia berlin conference, wao wameegemea Heligoland treaty. Na kipengele walichokishikilia naomba nikikopi na kukipesti
"To the south by the line that starts on the coast of the northern border of Mozambique Province and follows the course of the Rovuma River to the point where the Messinge flows into the Rovuma. From here the line runs westward on the parallel of latitude to the shore of Lake Nyasa. Turning north, it continues along the eastern, northern, and western shores of the lake until it reaches the northern bank of the mouth of the Songwe River"
Lakini mie nimesoma mkataba wa Heligoland kifungu kwa kifungu hakuna mahali paliposema kuwa Ziwa lote liko malawi na wala hapajasemwa kuwa mpaka wa malawi uko ktk ufukwe wa mashariki wa ziwa nyasa. Lakini kuna baadhi ya documents zinaonesha Mpaka wa malawi nao ulikuwa unaambaa ktk pwani ya magharibi ya ziwa nyasa; Mwaka 1902 miaka 12 baada ya Helgoland treaty Mfalme wa Uingereza alipotakiwa kutaja mipaka ya himaya yake kwa upande wa eneo aliloliita British central Africa alisema mpaka upande wa himaya yake uko magharibi mwa ziwa nyasa na wala hakusema uko kwenye ufukwe wa mashariki. Haya aliyatoa kwa maandishi na nakala ikachapishwa ktk gazeti la London Gazette la tarehe 15 August 1902, nimekopi na kupesti kama ifuatavyo:
"At the Court at Buckingham Palace^ the llth
day of August^ 1902.
PRESENT,
The KING'S Most Excellent Majesty
in Council.
WHEREAS the territories of Africa situate
within the limits of this Order are under
the protection of His Majesty the King, and are
known as the British Central Africa Protectorate
:
And whereas by Treaty, grant, usage, sufferance,
and other lawful means, His Majesty has
power and jurisdiction within the said territories :
Now, therefore, His Majesty, by virtue and in
exercise of the powers on this behalf by the
•Foreign Jurisdiction Act, 1890, or otherwise, in
His Majesty vested, is pleased, by and with the
advice of his Privy Council, to order, and'it is
hereby ordered, as follows :—
Preliminary.
1. This Order may be cited as " the British
Central Africa Order in Council, 1902."
The limits of this Order are the territories of
Africa situate to the west and south of Lake
Nyassa, and bounded by North-Eastern Rhodesia,
German blast Afri a, and the Portuguese territories.
The said territories are in this Order referred,
to as •' British Central Africa " and " the Protectorate."
Ukisoma vizuri tamko hilo la mfalme wa uingereza utagundua kuwa hata yeye ana taja mipaka iliyowekwa mwaka 1890 ambayo ni Heligoland treaty kwahiyo anathibitisha kuwa hata mpaka wa malawi ulikuwa unaambaa ktk ufukwe wa magharibi hivyo ziwa nyasa haliko upande wowote.
Baada ya vita vya kwanza vya dunia waingereza wakapewa uangalizi wa Tanganyika; mwanzoni waingereza wakaamua kutoa ramani zilizoonesha mpaka uko katikati ya ziwa nyasa lakini baadae ktk miaka ya mwanzo ya 1930 wakati madai ya Hitler kuwa ujerumani irudishiwe makoloni yake ndio wakabadili tena wakatoa ramani zinazoonesha mpaka umepita mashariki mwa ziwa lakini ukumbuke kuwa haya yalifanywa na peke yao kwa hisia zao.
Ndio maana Tanzania inasema mpaka wanaoudai wamalawi ni illogical. Na kwa misingi hiyo common international law ndiyo inatakiwa kufuatwa ambayo inasema maeneo yoyote ya maji yanayopakana na nchi zaidi ya moja mpaka utakuwa katikati ya maji.
Hizo ramani za google zisiwapumbaze watanzania maana wameadopt makosa ya waingereza na ndi maana ramani hizi zimesababisha migogoro kadhaa ya mipaka duniani. Na si kila kitu kilicho kwenye google kinaweza kutumika kama references zingine ni just unpublished information ambazo zinaweza zisiwe na ukweli.
Kuhusu utata kwenye coordinates alizozitaja membe; hilo sio tatizo na haliwezi kuondoa ukweli wa madai ya Tanzania kwasababu hata ktk serious documents kuna errors kama hizo, chukua doc yoyote hata inayotoka kwenye international court usishangae kukutana na errors kama hizo. Hata nilipokuwa nasoma Heligoland treaty nimekutana na typing errors mbili ktk mkataba huo.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By Zanta
Mkuu nasubiri kipengele kile kinachosema kwamba UN convection ya 1982 inaaply tu kwenye sehemu ile ambayo haina "treaty"
Kikamilifu inaitwa United Nations Convention on the Law of the Sea (UNCLOS), au Law of the Sea Convention au the Law of the Sea treaty.
Kuna article 15 ya Convention hiyo inasema hivi:
{Where the coasts of two States are opposite or adjacent to each other, neither of the two States is entitled, failing agreement between them to the contrary, to extend its territorial sea beyond the median line every point of which is equidistant from the nearest points on the baselines from which the breadth of the territorial seas of each of the two States is measured. The above provision does not apply, however, where it is necessary by reason of historic title or other special circumstances to delimit the territorial seas of the two States in a way which is at variance therewith.}
Article 16(1) inasema hivi:
{1. The baselines for measuring the breadth of the territorial sea determined in accordance with articles 7, 9 and 10, or the limits derived therefrom, and the lines of delimitation drawn in accordance with articles 12 and 15 shall be shown on charts of a scale or scales adequate for ascertaining their position. Alternatively, a list of geographical coordinates of points, specifying the geodetic datum, may be substituted.}
Article 16(2) inasema hivi:
{The coastal State shall give due publicity to such charts or lists of geographical coordinates and shall deposit a copy of each such chart or list with the Secretary-General of the United Nations.}
Sasa, wale wasiojua usahihi wa coordinate hapo kwenye RED sijui watasemaje. Lakini kifungu hiki 16(2) kinaonyesha wazi kuwa kopi ya hii ramani yako ikibidi na coordinate zako unatakiwa kuwa umezipeleka United Nations.
Sasa, muulizeni Rose Migiro kule UN tulipeleka ramani inayoonekana vipi. maana hapo ndio mwisho wa kila kitu na atakayeonekana mvamizi kwa mujibu wa ramani iliyoko UN basi UN ina haki y akumfanya kama inavyowafanya wavamizi wengi tena walidhani wameshindikana humu duniani.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By Kibona
Sikia mr makoye2009, usikubali wamalawi wakufanye mjinga. Mie naomba nikuhakikishie kwamba sie tuna eneo katika ziwa nyasa tena mpaka uko katikati:
Kibona,
Kwanza nikupongeze kwa sababu ya ufuatiliaji lakini hoja zako nazijibu kama ifuatavyo
By Kibona
Katika mkutano wa Berlin hakukuwa na mipaka ya uhakika iliyooneshwa hasa ktk maeneo ya maji kama maziwa mito mikubwa maana sehemu hizo ilikubaliwa kuwa ziwe free trade zone. Hata Wamalawi hawasemi kabisa habari ya berlin conference wanajua hakuna haki waliyopewa kupitia berlin conference, wao wameegemea Heligoland treaty
Heligoland treaty ilikuja miaka mitano baada ya Berlin Conference. Heligoland Treaty ni matokeo ya kuhakikisha kwamba Berlin Conference haikutosheleza kila kitu hivyo treatise kama hizo zilitakiwa kuhitimisha ugomvi.
By Kibona
Lakini kuna baadhi ya documents zinaonesha Mpaka wa malawi nao ulikuwa unaambaa ktk pwani ya magharibi ya ziwa nyasa;
Kibona,
Suala la kuwepo document si tatizo. Je, document hizo zinaonyesha kwamba kuna makubaliano mapya au ni muono wa mtengeneza document.
By Kibona
Mwaka 1902 miaka 12 baada ya Helgoland treaty Mfalme wa Uingereza alipotakiwa kutaja mipaka ya himaya yake kwa upande wa eneo aliloliita British central Africa alisema mpaka upande wa himaya yake uko magharibi mwa ziwa nyasa na wala hakusema uko kwenye ufukwe wa mashariki.
Kumbuka history inasema kwamba Uingereza ilipoanza kukamata koloni lolote mengi haikuanza kuyatawala kutokea Uingereza. Ilituma mashirika yanayofanya administration kul. Kumbuka hata kule India ilikuwa hivi na hata ile Indian Mutiny ni kwa sababu India (Bengal) ilikuwa bado iko chini ya makapuni haya kama lie la British East Indian. Kusini mwa Africa kulikuwa na shirika liitwalo British South Africa na nadhani hapa utasikia sana jina Cecile Rhodes kuliko hata mfalme. Kumbuka cartoon ya punch iliwahi kumchora Rhodes amekanya Tunisia na Cape Twon wakati mmoja!
Baada ya makampuni kujenga ukoloni huo ndipo nchi yakawa yanakabidhi eneo kwa mfalme au malkia wa Uingereza. Eneo linapokabidhiwa hivi huitw Crowny Colony.
Kwani nchi nyingi za Africa hakukuwa na ule ukoloni wa settlers kuja na ilikuwa ni hali ya protectorate. Hivyo, Mfalme wa Uingereza alikabidhiwa eneo la Malawi mwaka 1907 yaani miaka mitano zaidi ya uliotaja hapo juu. Hivyo, huo mwaka 1902, alikuwa na haki ya kujibu kwamba hana uhakika na mipaka ya eneo la Malawi ya sasa.
Vilevile mwaka huo 1902 kulikuwa na vuguvugu la kulazimisha kuwe na Federation of South Africa na baadaye Federation of Rhodesia bila kusahahu upinzani wa akina Robengula.
Hivyo, majibu haya ya Sovereign wa UK si ya kutumainiwa sana.
By Kibona
Baada ya vita vya kwanza vya dunia waingereza wakapewa uangalizi wa Tanganyika; mwanzoni waingereza wakaamua kutoa ramani zilizoonesha mpaka uko katikati ya ziwa nyasa lakini baadae ktk miaka ya mwanzo ya 1930 wakati madai ya Hitler kuwa ujerumani irudishiwe makoloni yake ndio wakabadili tena wakatoa ramani zinazoonesha mpaka umepita mashariki mwa ziwa lakini ukumbuke kuwa haya yalifanywa na peke yao kwa hisia zao.
Kwa namna moja umesaidia kusema kwamba kilichofanyika baada ya Heligoland Treaty mwaka 1890 kilifanyika si kwa level ya mkataba bali kwa matakwa binafsi ya aliyekuwa anatawala eneo la Tanganyika.
.."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
By Nikupateje
Ninasubiri kwa hamu kuona mtakuja na hoja gani kuhusu hizi findings zinazochambua hotuba ya Membe na matokeo yake niliyoeleza humu.
Sijui unaposema "mtakuja na hoja gani" walengwa ni nani hasa? Watanzania? Na wewe uko kundi gani? Nikupateje, sijui una umri gani lakini naomba nikutoe hofu kidogo. Sisi wazee tuliosoma wakati wa mkoloni, kufaulu mtihani wa kumaliza Primary School (darasa la kwanza hadi nne) na kuingia Middle School (darasa la tano hadi nane) tayari tulikuwa tunaweza kuichora ramani ya Tanganyika na kuigawanya katika majimbo yote manane. Mpaka wa Tanganyika tuliousoma, tulioujua na tuliokuwa tukiuchora (kabla ya uhuru 1961) ulikuwa unapita katikati ya Ziwa Nyasa. Hadi naingia sekondari ungeweza kuniamsha hata usiku wa manane nikakuchorea ramani ya dunia kutoka kichwani (sina hakika kama siku hizi mwanafunzi anayemaliza darasa la saba anaweza akafanya hilo!)
The true sign of intelligence is not knowledge but imagination.
Education is what remains after one has forgotten what one has learned in School
-Albert Einstein.
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
Huyu Mmalawi aliyeleta mada anatumia nguvu nyingi kuhalalisha hoja yake ambayo haina tija kabisa. Hivi kweli hotuba ya waziri ndio itatumika kugawa mipaka? Waziri Tibaijuka alivyoenda UN kudai eneo la bahari kule visiwani, alijiendea na hotuba yake peke yake au aliambatana na timu ya wataalamu? Hivi rais akihutubia taifa na kusema Tanzania ina watu milioni 44, figure hiyo haitoshi kwa uwasilishaji wa taarifa, eti hadi ataje idadi kamili? Kuna watu humu hawana kazi za kufanya.
Endelea na coordinate zako, sisi tunataka maeneo yote yenye vizazi vya watanzania yabaki Tanzania, na mpaka wa ziwa upite katikati ya ziwa kuanzia ncha ya juu hadi pale unapokutana na mpaka wa Msumbiji ulipoweka right angle. Ukimaliza coordinates, utuambie figure kamili ya population ya watanzania
Kibona,
Kwanza nikupongeze kwa sababu ya ufuatiliaji lakini hoja zako nazijibu kama ifuatavyo
Heligoland treaty ilikuja miaka mitano baada ya Berlin Conference. Heligoland Treaty ni matokeo ya kuhakikisha kwamba Berlin Conference haikutosheleza kila kitu hivyo treatise kama hizo zilitakiwa kuhitimisha ugomvi.
Heligoland treaty kama jina linavyojieleza ni treaty ya kisiwa cha Heligoland kipo Ujerumani. Hiki kisiwa kilikaliwa na Uingereza. Waingereza walikipata toka kwa Wadenmark mwaka 1807.
Ujerumani ilikuwa inataka ikikomboe hicho kisiwa hivyo wakaamua wamalizane huku Afrika. Ujerumani ikaamua imkatie Mwingereza baadhi ya maeneo ya himaya yake hapa Tanganyika/ East Africa ili Mwingereza arudishe kile kisiwa kwa Wajerumani
Si sawa kusema Heligoland treaty ilikuwa ina lengo la kukidhi mapungufu ya Berlin conference
Re: Waziri Bernard Membe kalipotosha Bunge kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa
In brief tanzania position yake ni mstari wa mpaka upite katikati ya ziwa mpaka usawa wa mto ruvuma na position ya malawi mpaka wote ni wao kwa mujibu wa article I of heligoland treaty. Sisi pia tunaitumia hiyo treaty kupitia Article VI. Sasa issues nyingine oh tulikuwa wapi siku zote ni irrelevant. Kwa sababunissue hii was raised by Tanzania in 1967 wakati ilipowasiliana na serikali ya malawi lakii wao hawakuwa na interest ya kuzungumza. Kumbukeni sula la mpaka lina dhana ya historia, jiograia, sovereingty na sheria! It is also where internal affairs end and foreign affairs begin.
100% upo sahihi lakini kufuatana na heligoland treaty ya mwaka 1890 mkataba uliowekwa na wajerumani na waingereza.....lakini mwaka 1982
UN Convention on Law of the Sea that stipulates that in case nations are bordered by a water body (sea or lake), the border of the two nations will always be on the middle of the water body." ambayo ndiyo sahihi kwa sasa kwani malawi na tanzania ni wanachama wa umoja wa mataifa na sio makoloni ya uingereza na ujerumani......kwa hiyo Waziri membe yupo sahihi.....tusipotoshe jamiii kwenye hili
Kwani hiyo treaty si ni ya miaka ya karibuni?Does it apply retrospectively kwa kitu ambacho cha zamani kama heligoland ya 1890? Na pia does a later treaty of general application alter a former treaty of a specific application(eg.heligoland)?
Follow Us Here