Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

    Report Post
    Page 6 of 6 FirstFirst ... 456
    Results 101 to 107 of 107
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,498
      Rep Power : 46709
      Likes Received
      16345
      Likes Given
      8417

      Default Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi



      Daraja ya Kagera (Kyaka) lililobomolewa na Idi Amin na vikosi vyake pamoja na majengo yaliyobomolewa nakubakia majeraha ya vita.


      • Wanasiasa wanaotoa lugha ya vita hawana hekima na ni hatari
      • Wengine wanatafuta ujiko wa kisiasa
      • Tusizungumzie vita kama hatuko tayari kupigana
      • Vita si lelemama


      Na. M. M. Mwanakijiji

      Sikutegemea kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje Bw. Lowassa kutoa kauli ambayo ikiunganishwa na ile ya Sitta na ya Membe inazidi kuchochea hali ya kutotafuta suluhu. Wote hawa watatu bila ya shaka wanasema kutokana na nafasi zao lakini pia yawezekana wanasema kwa sababu wote watatu wanatajwa vile vile kama wagombea watarajiwa wa urais mwaka 2015. Hata hivyo nazipima kauli hizi kwa jambo la kwanza na si kwa hilo la pili.

      Vita si jambo dogo na si jambo la mzaha kama watu wengine wanavyochukulia. Nimeona tangu Wamalawi walipozungumza suala la kudai "ziwa zima" la Nyassa kuwa ni lao baadhi ya watu wetu mwitikio wao wa kwanza umekuwa ni "tupeleke majeshi" au "tupeleke vijana wetu" na sasa leo Lowassa ananukuliwa na vyombo vya habari mbalimbali kuwa JWTZ liko tayari kwenda vitani na Malawi kuhusu suala hili. Hili ni jambo la kusikitisha na kushangaza.

      Kufikiria vita siyo jambo dogo na wala si jambo la kutafuta ujiko au siasa. Ni sawa na kuamua kushika bunduki na kumuelekezea mtu. Polisi huwa wanaambiwa kuwa usielekeze Bunduki kama hauko tayari kuitumia. Wale ambao wanabeba silaha (nao ni raia) wanajua kabisa kuwa hutoi silaha kibindoni kama hauko tayari ku-pull the trigger. Maana ya yote haya ni kuwa kutoa silaha na kuishika mkononi siyo suala la ubishoo, urembo au kujionesha kuwa unaweza.

      Tusipokemea hili la wanasiasa mwisho tutaona watu wanaanza mazoezi ya kutuonesha vifaa vya kivita ili kuwapiga mkwara wa Malawi. Na kweli wapo ambao wanatamani kuona "vijana wetu" wanaanza kuelekea mpakani au kwenye ukingo wa Ziwa Nyassa ili kutuma ujumbe kuwa tuko tayari. Sasa hili ni zuri na linasisimua akili na hisia za "kizalendo". Lakini tusije kuwa ni mambo ya Wag the Dog ambapo ili kushinda uchaguzi timu ya wanamkakati wa kampeni waliamua kutengeneza 'vita isiyokuwepo' ili kupoteza mawazo ya wapiga kura.

      Ninachoogopa zaidi ni kuwa wakati watawala wetu tumewabana kuhusu uongovi wao mbovu, sera zao zilizoshindwa na ukosefu wa maono usiokoma suala la mgogoro wa Ziwa Nyassa limewapa 'gia' ya kutokea na sasa hata watu waliokaa kimya wakati wananchi wetu wanauawa nakudhalilishwa na vyombo vya usalama wanasimama pasi ya kuomba radhi na kutaka tusimame nyuma yao. Nimeshangaa kuona Lowassa leo ameweza kukutana na vyombo vya usalama na kupewa taarifa zinazohusu vita lakini huyu huyu hajakutana na vyombo hivi wakati maisha ya wananchi wetu yanahatarishwa na vyombo hivi. Alikuwa wapi kwenye matukio ya Arusha, Mbeya (Tukuyu), Tarime na Songea? Kote huku hakuonesha kujali sana lakini leo ameibuka na kuonesha kuwa ana uwezo wa kufuatilia vyombo vya usalama?

      Kama nilivyosema hapo juu vita si lelemama kama baadhi ya watu wanafikiria. Najua wapo ambao wanafikiria kuwa vita dhidi ya Uganda ilikuwa ni uamuzi wa haraka na papara. Wengi (labda vijana zaidi) wanakumbuka tu maneno ya "nia tunayo na sababu tunayo" lakini ni wachache (hata wazee yumkini) wanaokumbuka kuwa kabla ya kufikia maneno hayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alielezea juhudi mbalimbali za kutatua mgogoro wetu na Uganda licha ya "chokochoko" zilizoanza miaka karibu mitano nyuma. Kwa Tanzania kwenda vitani ilikuwa ni uamuzi wa mwisho pale ambapo njia zote za amani na kidiplomasia ziliposhindwa.

      Leo viongozi wetu tena wakubwa na wenye dhamana nzito zaidi wanazungumza kana kwamba tumeshindwa kabisa kutafuta njia za amani na za demokrasia na sasa wanataka kuifanya Malawi kama wanavyofanyia wananchi wetu. Wananchi wakiandamana wanapigwa virungu na kuuawa na wakigoma wananyamazishwa kwa ghafla. Na hata mazungumzo wanataka yawe kwa masharti yao. Matokeo yake wamejenga fikra wanaweza kum-bully mtu yeyote, vyovyote, na kwa lolote kiasi kwamba wanataka kuanza kuibully Malawi. Hili linafanywa kwa sababu moja tu kuwa Tanzania ni kubwa kuliko Malawi na inawezekana ina uwezo mkubwa wa kuishinda Malawi.

      Wanaozungumza hivi wanafikiria vita inapigwana na wingi wa watu tu na vitu. Vita ni mikakati na mbinu lakini vile vile vita ni kujitoa muhanga. Tunapozungumzia lugha ya vita sijui kama tunafikiria viongozi wetu wanaweza kuhamasisha taifa kama ilivyokuwa miaka ya 1970 ambapo watu walichangia kuku, mbuzi na ng'ombe. Wangapi kati yetu leo watakuwa tayari kutoa magari na mabasi yao kwenda vitani? Wangapi wataamua kwa hiari yao kwenda kupigana chini ya viongozi hawa hawa? Itakuwaje kama watu wakiwa vitani kashfa kubwa ya ufisadi nyumbani inanguruma tena (mafisadi kwa asili hawabadiliki).

      Tunapozungumzia vita tunazungumzia maisha ya watu kuuawa. Watu wasifikiri kuwa tukienda vitani na Malawi au nchi nyingine yoyote jirani basi tutakuwa kama tunamsukuma mlevi. Ni wangapi wanafikiria kulipuliwa kwa miji yetu inayozunguka ziwa Nyassa? Mbamba Bay, Kyela, Tukuyu, Rungwe, Mbeya, hata Songea? Kweli kina Lowassa wanapozungumza lugha ya vita wanafikiria kabisa kuwa tumesahau jinsi Amin alivyolipua Mwanza? au ndio viongozi wetu hata historia tena wamesahau? Au watu wamesahau jinsi tulivyolazimika kuchimba mahandaki na kufanya mazoezi ya kujihami hadi kuwa na kuku ndani kwa ajili ya kukimbia nao kwenye mahandaki? Au watu wameshasahau jinsi Idi Amin alivyoweza kuua mamia ya watu wetu pale vikosi vyake vilipovuka Mutukula na kuingia Kagera?

      Ninachosema ni kuwa ipo haja ya haraka ya viongozi wetu kuonesha hekima ya kukwepa lugha ya vita. Si kwa sababu hatuna uwezo wa kupigana na Malawi (naamini tunao tena mkubwa na naamini tunaweza kushinda) lakini bado hatujawa na sababu ya kufanya hivyo. Watu kudai "ziwa zima" wakati sisi tumejenga bandari na watu wetu wanavua na kuishi kwenye ziwa hilo na tuna meli miaka nenda rudi na Wamalawi hawajarusha hata baruti ni jambo la kutufanya tufikiri. Kama kweli Wamalawi wangekuwa wanataka vita au ugomvi mbona wao sababu "wanayo" kuwa tumeingilia Ziwa lao na tunafanya vitu kinyume cha sheria?

      Wamalawi walipozungumza kwa lugha ya Vita mara moja walitambua kuwa hakuna sababu ya ku-escalate tension kwenye eneo hilo hasa kwa vile tayari tumeshawahi kuwa na tension sana. Ndio maana Waziri wa Mambo ya Nje aliamua kupunguza makali ya lugha ya vita. NI wakati kwa viongozi wa TAnzania nao kupunguza ukali usio wa lazima na kuchochea lugha ya vita. Na sisi wananchi tusiuziwe kirahisi vita kwani ina gharama kuliko watu tunavyoweza kufikiria. Ikumbukwe vita ya Uganda iliigharimu Tanzania kuliko watu wengi wanavyojua na imeacha mojawapo ya majeraha makubwa katika mwelekeo wa uchumi wetu ambayo hadi leo tunasikia maumivu yake. Sijui kama tunataka vita nyingine hasa kwa sababu ambazo ni za kidiplomasia na kisiasa.

      Hekima itusukume kufikiria mara mbili. Tutoe nafasi kwa diplomasia na mazungumzo ya amani na nina uhakika wa Malawi kama ni watu wa amani watanyosha mkono wa amani. Njia mojawapo kama tukitaka na sisi kutumia mbinu za diplomasia ni hilo nililosema kwenye mada nyingine badala ya kupeleka vifaru na askari wetu karibu na Ziwa Nyassa na sisi tuanze utafiti kwenye eneo tunaloamini ni letu na kuwaacha Wamalawi wafanye kwenye eneo lao. Kama wanafanya hivyo kwenye sehemu ya eneo letu basi tuna sababu ya kuhakikisha hizo 'incursions' hazitokei na hapo ikibidana kuweka boti zenye silaha kuhakikisha hayo hayatokei.

      Endapo juhudi hizi za kuonesha sisi ni watu wa amani hazitapokelewa na kama juhudi za kidiplomasia zitashindwa na Wamalawi watapuuzia kabisa madai yetu na kuanza kutenda kanakwamba hatuna la kusema basi ni wakati huo Watanzania waandaliwe kwa kitu ambacho kinaweza kutokea - vita. Na hili lisizungumzwe na kila "dick, tom and harry" kwa sababu wanavaa suti za vyeo mbalimbali. Mtu pekee wa kuweza kulizungumzia hili kama uwezekano ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

      Endapo tutaacha wanasiasa ambao wanatafuta ujiko kwenye macho ya wananchi walizungumzia na kututia hamasa wakati wao wenyewe hawatoenda vitani na yawezekana hawana mtoto au ndugu hata mmoja JWTZ basi tutajikuta tunapelekwa vitani kisiasa na siyo kwa sababu tunatishiwa au tunajihami. Ni matumaini yangu viongozi wa upinzani (CHADEMA) hawatoingia mtego huu wa kuzungumza lugha ya vita. Hili waachiwe CCM na mashabiki wake mpaka pale ambapo juhudi zao za kisiasa zitakpokuwa zimeshindwa basi waseme tunaenda vitani na hapo viongozi wa upinzani watolee maoni na msimamo wao. Wapinzani wasizungumze lugha ya vita bali ya amani.

      Ndio maana kwa upande wangu ninaangalia sana watu wanaotaka kuwa ma-amiri jeshi wakuu, tusipoweza kuwaangalia wanavyoweza kutumia hekima watu hawa watakuja kutupeleka vitani na tukajikuta tunapigana na tukiulizwa tunapigania nini hatujui kumbe watu walitukaniana mama zao na taifa likaingizwa vitani. Na matumaini yangu JWTZ halitaingia kwenye hili suala la kisiasa na kidiplomasia. Tunataka JWTZ letu litakapozungumza iwe ni baada ya tangazo rasmi la vita nje ya hapo JWTZ iwaache wanasiasa wafanya mambo yao.

      Siasa na Diplomasia vikishindwa tujiandae kwa ushindi wa Kivita. Hapo ndio tutoe silaha zetu kibindoni na kuzielekeza kwani tutakuwa tayari kuzitumia.

      MMM
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. Miaka 50

    3. #101
      Nsabhi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd February 2011
      Posts : 629
      Rep Power : 542
      Likes Received
      69
      Likes Given
      121

      Default Re: Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

      [QUOTE=Mzee Mwanakijiji;4393018]huwezi kujua how correct uko kwenye hili. Msidhani wao watapigana hivyo vita shauri Mzee Mwanakijiji mimi nakubaliana kabisa na mawazo yako umeeleza vizuri sana kuwa vita si lelema lakini katika hali iliyofikiwa kuwa Mawalawi walikuwa tayari wamegawa blocks " vitalu"katika eneo lote la ziwa wakati wakijua wazi mazungumzo yalikuwa yanaendelea ni uchokozi ni tangazo la vita.Hivi unapovamia mipaka ya nchi nyingine unategemea nini kwa viongozi walie wanune au wacheke? Wamalawi walionesha kuyapuuza mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea. Hi sawa na jamaa kukuchukulia mke wako na kwenda naye huku wewe ukiendelea kumchekea kuwa atamrudisha tu hapo baada au utazungumza nae ile hapa baadaye aache hilo halikubalini.Unapochokozwa si lazima wakati mwingine ujiandae unaweza kutumia nguvu uliyonayo kupambana na huyo mchokozi hata kama anakuzidi nguvu.Mimi naungana na Sitta, Membe na Lowasa katika kukemea hili.Uoga wetu utakuja kuuza nchi./QUOTE]

    4. #102
      Nicholas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 4,933
      Rep Power : 3603
      Likes Received
      1256
      Likes Given
      2116

      Default Re: Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

      Quote By Ronal Reagan
      Sharti mojawapo ni lazima hawa watatu watoe watoto wao wa kiume kuwa mstari wa mbele ktk vikosi ikiwa tutaingia vitani. Vita si mchezo!
      ha ha..Ningependa niwaone wale watoto wanajiita wenyewe kuwa ni watoto wa vigogo na wamekuwa na tabia ya kuchomoa ha hata kupiga risasi katika matukio ya sehemu za starehe wakigombea mademu.nadhani hiki ndicho kipindi chao cha kuonyesha si kwa mademu zao tuu bali kwa watanzania hamu yao ya kutumua bastola na kubwa zake.
      SIMPLY THE RADICAL: I can`t wait to see the criminalization of CCM,UWT,Bunch of Policemen/women,and all wanafiki na wachumia tumbo.

    5. #103
      Kingcobra's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th January 2011
      Posts : 713
      Rep Power : 563
      Likes Received
      128
      Likes Given
      14

      Default Re: Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

      Siungi mkono vita na siungi mkono nchi yetu kudharauliwa na taifa jingine kwa namna yoyote ile. Kauli za lowassa na sitta zinaweza kuonekana ni za kichochezi lakini zinatoa assurence kwamba usalama wetu na uhuru wetu unaweza kulindwa hata ikiwezekana kwa mtutu wa bunduki. Tukiongelea diplomacy tu, wamalawi watavimba vichwa na kuendelea kutuchokonoa usoni.
      Nicholas likes this.

    6. #104
      Nicholas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 4,933
      Rep Power : 3603
      Likes Received
      1256
      Likes Given
      2116

      Default Re: Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

      Right combination ya threat na diplomacy inaweza saidiana kuwa divide enemies.Wapo watu waliwahi survive majambazi(wakiwa na mapanga) katika mazingira ya kuogofya . I have a guy aliyekutwa na dhoruba la majambazi akiwa hata hana silaha na lipohisi kuwa walikuwa wakitaka kumua anyway hata kito auhsirikiano.Alichofanya ni kusoma mood ya lile kundi na kufahamu mwenye comand na aka predict results ya atakachofanya.Kwa mjumuiko wa hofu na kusema liwalo na liwe alipandisha sauti na kumpiga kiongozi kwa haraka na kwa nguvu zote, haakumini jinis alivyoweza lichukua lile panga na kunfanya aonekane kama katoto .Coincidence ni kwamba wale jamaa wengine walikuwa wakiamini kuwa kiongozi wao ni shupavu sana kiasi ,kwamba hata wote kwa pamoja hawawezi mshinda katika mpambano, na hivyo walichokiona kiliwafanya waone kuwa yule jamaa ni mara nyingi ya kiongzoi wao.So game liliisha kabla ya kuanza kwani wengine walikuwa kona, akabaki kiongozi wao pekee huku silaha yake ikiwa kwa adui.So jamaa kwa huruma alimwachia aondoke , huku akiwa nahofu kuu pengine akijiapiza kuwa akifika huko gheto jamaa zake walitosa watamkoma.

      Personally naona kama serikali itajibahave kama grown up group of leaders, hakutakuwa na vita wala mgogoro na jumuia za kimataifa.Tunahitaji tumia parmaters nyingi kuwabana wamalawi.Lazima tu instigate fear kwa raia na viongozi wao tukiwa nyuma ya mlango, na diplomacy tukiwa hadharani.Lazima Pia tuwaweke mataifa muhimu katika state ya kuona bright future kuwa rafiki nasi pia kuwashindanisha kutugombea.Pia ni lazima tuwekeze kuwa na mamluki kwa kila level ndani ya malawi ili wawe koloni letu la kudumu.Bahati yao akina mangi wa rombo na Kibosho hawaongei lugha za huko?Tungewapa tender za kuenda nzisha bar za kila aina, ili no.1 wazinywe wenyewe hadi wapunguze nguvu na uzalendo wao.
      SIMPLY THE RADICAL: I can`t wait to see the criminalization of CCM,UWT,Bunch of Policemen/women,and all wanafiki na wachumia tumbo.

    7. #105
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,498
      Rep Power : 46709
      Likes Received
      16345
      Likes Given
      8417

      Default

      Quote By Ben Saanane
      Kinachofanyika ni kitu cha kawaida kabisa kwenye medani za siasa za kimataifa.Kauli kama hizi zina detterence effect.
      Pia hii ni siasa ya kimataifa na tunakosea sana pale tunapoamini kwamba diplomasia inaweza kufanikiwa bila shinikizo.Suala la kuweka majeshi chini au kutoongelea millitary strength pia tutakosea na watu hawaelewi kwamba hata wakati wa vita Diplomasia bado inafanyika
      Kutatua migogoro kwa njia ya kidiplomasia kuna:
      -Kushawishi kabla ya kufikia hatua ya kutishana
      -Kukirimu/kuhonga kwa ushawishi wa raslimali au mamlaka
      -Lobbying ya kutafuta sapoti kwa jumuiya ya kimataifa
      -Shinikizo la kijeshi au shinikizo la vikwazo vya kiuchumi(coercion)
      -Ama vyote kwa pamoja

      Pia kinachofanyika ni kuondoa sasa hofu wananchi na kuongeza ari ya jeshi na kama nilivyosema kuleta detterence effect kwa nchi hasimu.Hii ni propaganda ya kidiplomasia na haiepukiki
      Malawi imeanza lini kuwa nchi hasimu hadi kuzungumza hii lugha ya vita?

    8. FemaTV & Radio

    9. #106
      Ben Saanane's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2007
      Posts : 6,717
      Rep Power : 32784
      Likes Received
      4988
      Likes Given
      6451

      Default Re: Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Malawi imeanza lini kuwa nchi hasimu hadi kuzungumza hii lugha ya vita?
      Pande mbiliz zinazovutana kugombania maslahi yake ni hasimu.Mgogoro huzaa hasimu.Lugha ya vita ni diploamacy at the extreme position,Lugha ya vita ni diplomasia
      Wametuonyesha Jeuri ya ukaburu,tuwaonyeshe jeuri ya Umkhontho we sizwe kupitia Red Brigade.Tukiwaonyesha woga wetu, itakua silaha imara zaidi kwao kutumaliza-Ben Saanane

    10. #107
      obasa's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 26th April 2012
      Posts : 3
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

      Quote By Magesi
      Fisadi amepata pakutokea anaropoka 2 anfikiria vita ni sawa na ufisad wanaoufanya
      mtu kama LE na mafisadi wenzake wanafikiria tender za ku-supply vifaru,AK 47,mabomu na silaha zingine bei na mauaji kama richmond

    Page 6 of 6 FirstFirst ... 456

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...