Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

    Report Post
    Page 13 of 13 FirstFirst ... 3111213
    Results 241 to 252 of 252
    1. #1
      Mwana Mpotevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2011
      Posts : 1,987
      Rep Power : 863
      Likes Received
      920
      Likes Given
      880

      Default Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Nimeipenda sana kauli hii ya Lowasa katika gazeti la Mwananchi la Leo Jumatano;

      Reginald Simon na Daniel Mjema, Dodoma | Mwananchi | Agosti 08, 2012



      KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imesema Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.

      Akizungumza mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa alisema kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

      “Tumepewa maelezo na jeshi letu na tumeridhika kuwa ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na limejipanga vizuri sana kwa uhakika, kiakili na kivifaa,” alisema Lowassa.

      Kabla ya Lowassa kuzungumza na waandishi wa habari, alifanya kikao cha faragha kilichohusisha pia wajumbe wa kamati hiyo na makamanda wa JWTZ walipofika bungeni kutoa taarifa kwa kamati hiyo.

      Hata hivyo, katika tamko hilo Lowassa alisema Tanzania inatarajia mgogoro huo utamalizika kwa njia za kidiplomasia kwa sababu Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa muda mrefu.

      “Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWTZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo,” alisema Lowassa na kuongeza:

      “Tunategemea hatutafika huko, lakini kwa heshima ya nchi yetu kama ikibidi kufika huko (vitani) tutafika kulinda mipaka yetu”.

      Mwenyekiti huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema kama Tanzania itafikishwa mahali itabidi damu ya Watanzania imwagike, nchi iko tayari kulinda mipaka yake kwa nguvu.

      Alisema kama itabidi kuingia vitani, itatumia umoja na mshikamano wa Watanzania wa mwaka 1978 wakati wa Vita na Uganda kulinda mipaka ili kulinda heshima ya nchi.

      Alisema mwaka 1978 wakati Rais wa Uganda, Idd Amin na majeshi yake walipochukua sehemu ya Tanzania na kujitangazia ni mali yake, ilichukua hatua kumfukuza Amin.

      “Alijitangazia sehemu ile ni mali ya Uganda hutegemei nchi ikae kimya, hutegemei Watanzania wanyamaze wakati nchi yao imetekwa, tulichukua hatua tukamfukuza hadi nchini kwake.”

      Lowassa alisema Kamati ya Bunge inajua madhara ya kiuchumi yaliyotokana na Vita ya Idd Amin na kwamba vita yoyote ikipiganwa lazima kunakuwa na madhara ya kiuchumi.

      Hata hivyo, alisema anaamini mgogoro huo hautafika huko na kusisitiza kuwa, lakini ikibidi JWTZ ni moja kati ya majeshi bora duniani na ni jeshi lililojiandaa vizuri kwa lolote.

      “Wako tayari sisi ni moja kati ya jeshi lililojiandaa vizuri na jeshi bora duniani na la kujivunia. Tuko imara kiakili na kivifaa tena vya kisasa,” alisema Lowassa.

      Alisema kamati yake inaunga mkono msimamo ulitolewa bungeni juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusu mgogoro huo na kwamba ndiyo kauli rasmi ya Serikali.

      Juzi, Waziri Membe alizionya kampuni za kigeni za Malawi zilizoingia katika ardhi ya Tanzania eneo la Ziwa Nyasa kutafiti mafuta na gesi kusitisha mara moja.


      Hapo ndipo huwa namkubali Lowassa kuliko wengine wote ndani ya CCM walau kwa kauli na matendo ya namna hii ukiondoa yale mengine ya ufisadi

      ======
      UPDATE
      ======
      Quote By Tina View Post
      Kwanza nawaomba waheshimiwa wana JF katika kipindi hiki cha mgogoro kati ya Tanzania na Malawi tulete thread na kuchangia kwa kuzingatia maslahi ya Taifa. Tuache SIASA na maslahi.

      Pili naomba michango yenu kwa kuzingatia maslahi ya Taifa, ni nani anayestahili kutangaza kwa mara ya kwanza uwezo na nguvu yetu ya kijeshi? Membe alizungumza na kuionya Malawi baadae akaja Lowassa akasema tuko imara na tayari kwa vita! Sasa suala la nani atangaze ni nyeti sana na lina sababau nyingi na athari zake kitaalamu.
      Nsabhi and Njauledi like this.


    2. #241
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,507
      Rep Power : 21688
      Likes Received
      13812
      Likes Given
      18061

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By Pasco View Post
      Mwana Mpotevu, huu mjadala sio kiboko, hizi ndizo opportunities za kuelimishana ili tuelekee kwenye ukombozi wa kifikra utakaoleta ukombozi wa pili wa Mtanzania.
      sorry out of topic
      naomba ile list please pm
      Pasco likes this.
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    3. #242
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,911
      Rep Power : 1169
      Likes Received
      1056
      Likes Given
      804

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By Howdesi View Post
      Jamani, huyu Lowassa ameingia madarakani akiwa tajiri tu!!!!!!!!!Kama kaongezea mali basi kaongeza ila hakuwa masikini.

      Ila tuseme ukweli tuweke itikadi zetu na vyama vyetu pembeni. Jamani Lowasa ni JEMBE! N i kiongozi ambaye ni tallented, nakumbuka alipokuwa waziri mkuu, alikuwa akienda mahali ziara, watendaji huko wanaharisha, maana waliozembea alikuwa anawaachisha kazi on spot! Nani anaweza haya kwa SIRIKALI yetu hii DHAIFU?? kAMA SIO WAPINZANI BASI NI LOWASSA ingawaje wapo kina Mwakyembe, lakini kwa wanaoonyesha nia yakugombea, kweli Lowassa for Presidency!
      Mbona hajaeleza kwa dhati na moyo safi kilichotokea kwenye sakata la Richmond na kumsababisha kujiuzulu kabla hajatimuliwa na bunge?? amebaki kulalamika! hata kama ni mchapa kazi lakini tayari jamii ina shaka nae,.halafu alitajirika kutokana na nini? ni mfanya biashara?? wakati akiwa waziri wa ardhi ndipo alipotajirika huku utajiri wake ukianza alipokuwa mkurugenzi wa AICC ukitaka data za ufisadi wake utapewa,. Majembe safi yasiyo na shaka au doa yapo mengi sana tukiacha ushabiki wa vyama tukatuliza akili tunaweza kupata rais safi na jembe la kweli!
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    4. #243
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,862
      Rep Power : 7377
      Likes Received
      6195
      Likes Given
      22550

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By The Boss View Post
      sorry out of topic
      naomba ile list please pm
      The Boss, sorry we have the obligation to maintain "the right to privacy" za watu kama wanafanya mambo yao in private, ila wanaokuwa exposed ni wale tuu wanaofanya privacy zao in public kama wale wanaojianika!. Kwa vile hao wengine nao wanafanya biashara in private tena wengine ni kwa "corporate clients" mpaka mpangaji wa ile nyumba nyeupe!, sio vizuri kuwa expose hata in pm, ili nisiingilie uhuru wa watu na starehe zao!. Hivi hujiulizi kwa nini wengi wa kundi lile wako single na wengine kwa kuwaona tuu kwa macho, utawajua tuu jinsi walivyo macho juu!.

    5. #244
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,507
      Rep Power : 21688
      Likes Received
      13812
      Likes Given
      18061

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By Pasco View Post
      The Boss, sorry we have the obligation to maintain "the right to privacy" za watu kama wanafanya mambo yao in private, ila wanaokuwa exposed ni wale tuu wanaofanya privacy zao in public kama wale wanaojianika!. Kwa vile hao wengine nao wanafanya biashara in private tena wengine ni kwa "corporate clients" mpaka mpangaji wa ile nyumba nyeupe!, sio vizuri kuwa expose hata in pm, ili nisiingilie uhuru wa watu na starehe zao!. Hivi hujiulizi kwa nini wengi wa kundi lile wako single na wengine kwa kuwaona tuu kwa macho, utawajua tuu jinsi walivyo macho juu!.
      kuna siku ulisema utaweka a thread humu
      so hunitendei haki ukininyima
      hutavunja haki yao ya privacy ukitumia pm
      labda na mimi nina clients wa biashara zao?lol who knows?
      Pasco likes this.
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    6. #245
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,862
      Rep Power : 7377
      Likes Received
      6195
      Likes Given
      22550

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By The Boss View Post
      kuna siku ulisema utaweka a thread humu
      so hunitendei haki ukininyima
      hutavunja haki yao ya privacy ukitumia pm
      labda na mimi nina clients wa biashara zao?lol who knows?
      Sorry Boss ila nikupm nitajisikia guilt. Ukija pale eneo, njoo tuu kwenye vile viwanja, utawaona tuu kwa mivao yao, mitembeo yao, mikorogo yao na over make -ups zao huku wakibirigisha mi seductive eyes zao, please just come!.

      Hata nanii si alisema hawajui wamiliki wa Richmonduli, au hajui kwa nini Tanzania ni masikini!, na mimi naomba kusema siwajui, ile kutishia kuwataja ilikuwa ni danganya toto!.
      The Boss likes this.


    7. #246
      Sabayi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th December 2010
      Posts : 1,526
      Rep Power : 738
      Likes Received
      479
      Likes Given
      960

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      duuu kweli Serikali ya JEIKEI ni noma hata hii ishu ya walawi nadhani alijisemea ni upepo tu na naona unapita kweli,hakuna cha vita wala nini wajeda wetu walioletwa mpakani warudi tu kula iddi na familia zao,ila usiulize gharama za kuwapeleka tu huko utasikia tumetumia bilioni 400 kulinda mpaka dhidi ya malawi,chezea shimbo na jeikei nini?

    8. #247
      sheky's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 177
      Rep Power : 399
      Likes Received
      39
      Likes Given
      10

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Ziko nyakati za kuweza kuwaza katika mipaka ya kichama na kubishana kitabaka, ila kwa hili ni wakati wa kuweza kusema kwa sauti moja. Hatupendi na kama kuna jambo la mwisho ni vita, hata hivyo ukiona mwenzio anakula ubuyu anakupiga kokwa jiandae.

    9. #248
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,507
      Rep Power : 21688
      Likes Received
      13812
      Likes Given
      18061

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By Pasco View Post
      Sorry Boss ila nikupm nitajisikia guilt. Ukija pale eneo, njoo tuu kwenye vile viwanja, utawaona tuu kwa mivao yao, mitembeo yao, mikorogo yao na over make -ups zao huku wakibirigisha mi seductive eyes zao, please just come!.

      Hata nanii si alisema hawajui wamiliki wa Richmonduli, au hajui kwa nini Tanzania ni masikini!, na mimi naomba kusema siwajui, ile kutishia kuwataja ilikuwa ni danganya toto!.
      basi niruhusu niku pm
      bado still naona u can help me
      Pasco likes this.
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    10. #249
      MchunguZI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th June 2008
      Posts : 1,322
      Rep Power : 826
      Likes Received
      224
      Likes Given
      77

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By Pasco View Post
      Nchunguzi kwanza tuekewane katika yafuatayo.

      1. Amiri Jeshi Mkuu ni mmoja tuu ambaye ndiye mkuu wa Majeshi yetu yote ya Ulinzi na Usalama.
      2. Kijeshi chini ya Amiri Jeshi kuna
      - CDF-Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
      - CSS- Mkurugenzi wa TISS
      - IGP - Mkuu wa Jeshi la Polisi
      kuna sub component mbili ya
      CPS - Kamishna Mkuu wa Magereza na
      CIS - Kamishna Mkuu wa Uhamiaji.
      Kila mmoja wa wakuu hao ana comand majeshi yaliyo chini yake. CDF anakomand majeshi na sub components zake za JKT, Airforce na Navy na hawezi
      kuwacomand polisi, magereza wala wanausalama na hana mamlaka yoyote ya kumkamata yoyote nje ya comand yake unless ameingia ndani ya teritorial jurisdiction yake kama raia akifanya fujo ndani ya kambi ya jeshi atashughulikiwa na MP na atalazwa Qater Guard!. Vile vile mjeshi asiye Afisa akifanya fujo uraiani polisi wanamshughulikia kama mhalifu mwingine na kuliarifu jeshi husika.

      3. Kisiasa juu ya wakuu hao wa majeshi kuna wizara za Ulinzi, usalama na mambo ya ndani ambazo wakuu wa majeshi hawa wanawajibika kwa mawaziri husika hata kama hao mawaziri ni raia!. CDF anampigia saluti waziri wa Ulinzi, IGP anampigia saluti W/Mambo ya ndani etc.

      4. Waziri anawajibika kwenye kamati husika ya wizara yake na kamati isipiridhika haiungi mkono bajeji ya wizara husika.

      5. Wenyeviti wa kamati husika, wana madaraka kamili ya kuwaita watendaji wowote walio chini ya wizara za kamati hizo!.

      6. EL ni M/Kiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama hivyo Membe, Waziri wa Ulinzi na CDF wanaweza kuwa summoned mbele ya kamati anytime!.

      7. Moja ya kazi za bunge ni kuisimamia serikali kupitia kamati husika, zile bajeti unazosonewa bungeni, zimepitishwa kwanza kwenye kamati husika zikaridhiwa ndipo ukasomewa. Hivyo wabunge ndio wasimamizi wa serikali.

      8. Tunahitaji sana kuwaelimisha Watanzania wenzetu kama wewe kuhusu elimu ya uraia ili wananchi wazijue haki zao.

      9. Hata rais wa nchi, tunaoaswa kumheshimu kama binadamu mwingine yoyote kwa kustahili utu na heshima ila ni rais anayepaswa kutubyenyekea, sisi ndio tuliomuajiri na kumlipa mshahara wake na akiboronga tunaweza kunfuta kazi!.

      10. Tangu tumepata uhuru miaka 50 iliyopita CCM imekuwa ikitutawala huku inaboronga mwaka hadi mwaka na kwa ignorance ya watu wetu, tunaendelea kuichagua tena na tena na inaendelea kuboronga na kuboronga tena na tena na 2015 tutaichagua tena na tena sababu ya watu kama wewe!.
      Hapo kwenye bold. Kwa nini unaamua kukosea mpangilio wa jeshi? Nani alipanga hizi unazoita sub components?

      Mimi nilikutajia vizuri wewe unazipangua na kupanga upya. Unafahamu ni kwa nini Wizara inaitwa ni ya Ulinzi na JKT? Kwa nini JKT inatajwa pembeni ya Ulinzi?

      Kubali tu kwamba hujui mpangilio wa majeshi yetu na vyombo vya usalama. Maana naona unaanza kuiweka TISS kwenye wizara unayoiunda ya usalama na mambo ya ndani.

      Hayo uliyoyapanga na kugawa utawala haupo TZ hii. Hiyo ni nchi nyingine kabisa!!*
      The educated differ from the uneducated as much as the living from the dead --Aristotle

    11. #250
      politiki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Posts : 1,443
      Rep Power : 1358
      Likes Received
      754
      Likes Given
      136

      Default Vita na Malawi: Lowassa uko tayari kuwatanguliza wanao?

      Mzee mamvi alipotangaza kuwa jeshi liko tayari wakati wowote ni kwa ajili ya kuwapeleka watoto wenzake au na wake pia wanakwenda?

      Tunataka kuona uzalendo wake kwa kuanza kuwapeleka richard na fredrick lowassa kwanza kwenye mafunzo ya mgambo ili kitapolipuka basi tuwe nao front line na siyo kukimbilia kutangaza vita na kuwatanguliza watoto wa wenzio huku ukiwaficha wa kwako chini ya kitanda.

    12. #251
      Mwana Mpotevu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th September 2011
      Posts : 1,987
      Rep Power : 863
      Likes Received
      920
      Likes Given
      880

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      Quote By Pasco View Post
      Mwana Mpotevu, huu mjadala sio kiboko, hizi ndizo opportunities za kuelimishana ili tuelekee kwenye ukombozi wa kifikra utakaoleta ukombozi wa pili wa Mtanzania.
      Haya Pasco, nimeona elimu unayoitoa mkuu
      Pasco likes this.
      Don't break the LAW, just Bend It!

    13. #252
      ugwenousangi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th September 2012
      Posts : 41
      Rep Power : 349
      Likes Received
      6
      Likes Given
      14

      Default Re: Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi...

      PASCO ndiye mkombozi pekee wa JF

      Huna mfano kwa uchambuzi wako yakinifu

      Baba mtakatibu akuongoze salama kaka yangu

    Page 13 of 13 FirstFirst ... 3111213

    LinkBacks (?)


    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...