Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

    Report Post
    Page 5 of 10 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 183
    1. #1
      TandaleOne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th September 2010
      Location : SF Kiosk Tandale Sokoni
      Posts : 1,151
      Rep Power : 672
      Likes Received
      176
      Likes Given
      61

      Default Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      From: Ali Rashid <[email protected]>
      To: "[email protected]" <[email protected]>
      Cc: "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>
      Sent: Tuesday, 7 August 2012, 15:33
      Subject: : Yah: Uzinduzi wa Tawi la Chadema-London Kwenye Bar(Pub).



      Kwako Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Chadema Bwana Slaa.

      Napenda kuleta kwako maoni yangu na Waislam wenzangu waliopo hapa Uingereza kwa kitendo cha Chama chako kuamua kufungua Tawi lake hapa UK Ndani ya bar ikiwa ni kipindi cha Mwezi wa Ramadhani.
      .
      Ni Jambo jema na zuri kwa chama chako kuwa na Matawi nje ya nchi kama ulivyofanya hivi karibuni nchini marekani lakini kwa hapa Uingereza ambapo uzinduzi wake utafanyika Leo majira ya saa mbili usiku takriban masaa saba kuanzia muda huu.

      Kuna Mambo kadhaa ambayo yanatuweka kwenye wakati mgumu hasa sisi Waislam ambao tuko kwenye Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwani shughuli yenyewe inafanyika Bar na hata muda wa kufuturu kwa wale tuliofunga ndio muda huo huo ambao shughuli hiyo itakuwa ikifanyika Kwenye Bar ya Thatched House maeneo ya East london.

      Mheshimiwa Katibu mkuu kama nilivyosema kuwa kitendo cha chadema kuwa na tawi hapa uingereza ni hatua kubwa katika maendeleo ya demokrasia ya nchi yetu.lakini ingekuwa vizuri zaidi kama Chama chako kingejaribu kuwatizama watanzania wote bila kujali dini zao au sehemu ya Muungano wa nchi yetu wanaotoka.

      Waislam hatuna tatizo kwenda kushiriki uzinduzi wa chama cha Chadema ndani ya Mwezi wa Ramadhan ikiwa tu muda wa shughuli uwe muafaka(Convenience)usiingilia ne na masuala kama haya ya kufuturu. watendaji wako walikuwa na fursa ya kutafuta ukumbi hata wa pound hamsini au pound mia moja lakini kwenye neutral ground ambapo hakuna pombe na kumbi za namna hiyo ziko nyingi East london.

      Mwezi huu wa Ramadhani kwa huku Uingereza sisi tuliofunga tunafuturu kuanzia saa mbili na dakika 40 na kuendelea za usiku.Hapo ndipo linapokuja tatizo la muda wa shughuli hii ambayo ni muhimu kwa kila Mtanzania mpenda demokrasia kama ambavyo chadema yenyewe imekuwa ikijipembejea(ikijinasibu) kuwa ni chama cha demokrasia. kutengwa kwa baadhi ya Watanzania kwenye kushiriki demokrasia ya nchi yetu ni kitendo ambacho hakikutegemewa kupewa nafasi na Chama makini kama chadema.

      Mheshimiwa Slaa ni vyema nikupe taarifa kuwa Watanzania wengi tuliopo hapa Uingereza wanaotoka visiwa vya Zanzibar ni wengi kwa idadi kubwa na ni washiriki wazuri wa Siasa za nchi yetu waswahili wana msemo wao "Wengi wape" na hiyo ndio demokrasia. Eneo hilo la East london watanzania wengi wao wanaoishi hapo ni Wazanzibar kuanzia barking,East Ham, Upton Park,Ilford na Dagenham wingi wao kiasi cha kuweza kununua Msikiti wao, Hapo utakapofanyika mkutano wa chadema eneo la Barking ni hatua chache sana kuna msikitiki wa Watanzania(walking distance), wamenunua Bar na kuifanya kuwa msikiti siku kama ya ijumaa huswaliwa swala tatu kutokana na wengi wao. Kitendo cha kuwa na msikiti wao eneo ni kukuthibitishia idadi kubwa ya Watanzania waislam wanaishi eneo hilo kwa hali yeyote ile ilitakiwa chadema watazame hali za Watanzania wenzi wao.

      Mheshimiwa Slaa katiba ya Nchi yetu imekataza ubaguzi wa kidini au kijiografia na wewe hili unalitambua.Nchi hii ya Uingereza masiala ya equal opportunity policy ni ya lazima kwa kila taasisi ambayo inafanya shughuli zake hapa uingereza na ukija kwenye discrimination nalo ni jambo ambalo halivumiliki kuna sheria nyingi za kulinda haki na hadhi ya binadamu wote.

      Mimi siamini kuwa Watanzania wawe toka kisiwani au wawe wa dini ya kikristo,waislam au wanaomini jadi wasiwe na mchango wowote kwenye kuleta demokrasia kwenye siasa ya nchi yetu.Wewe mwenyewe kuna Mambo mengi ya siasa utakuwa umejifunza kwa Wanasiasa wenzi wako kama mheshimiwa Hamad Rashid,mheshimiwa Jussa,Mabare Marando,James Mapalala,Austine Mrema,Hamad Rashid ambaye alikuwa kiongozi wako wa Kambi ya upinzani bungeni na kabla yake alikuwepo Mama Fatma Maghimbi kama kiongozi wako, nina imani hao viongozi wamekupa ujasiri na muongozo mkubwa.

      Mheshimiwa Slaa nakuandikia wewe nikijua ndiye mtendaji mkuu wa Chama hivyo una uwezo wa kulihamisha zoezi kutoka kwenye Bar ya Thatched na kutafuta neutral ground hata pale kwenye msikiti wa Watanzania kuna ukumbi ambao unakodishwa kwa bei ndogo. lakini ili kulifanya zoezi lifanikiwe vizuri kuna Community Halls ziko nyingi na unaweza kupata wakati wowote na kutumia ukumbi wa msikiti nako itakuwa ni kuwabagua wasio waislam. muda ulipo wa masaa haya saba unatosha au si vibaya hata kulifanya zoezi hili kwa weekend.

      Mheshimiwa Slaaa unaweza kutizama Blog za Mjengwa.blogspot.com au jestina George ukaona tangazo la chama chako kufanya shughuli hii muhimu na ya kihistoria lakini kwa bahati mbaya ndani ya BAR. hata imagine ya chama inaharibika kwa tukio muhimu la kihistoria kufanyikia Bar. inaonekana hamkuwa serious au hamko serious, mara nyinyi chadema mmekuwa mkija kwenye mikutano ya Chama cha Conservative cha hapa na Cuf wamekuwa wakija kwenye mikutano ya liberal Dem. hapa Uingereza hakuna mikutano inayofanyika bar huwa kwenye kumbi mbali mbali.

      Kwa heshima kubwa naomba nikurejeshe kwenye Tangazo la chama liliko kwenye blog mbali mbali.
      "Chadema inapenda kuwatangazia watanzania wote waishio London na sehemu za jirani kuwa kutakuwa na mkutano wa ufunguzi wa Tawi la Chadema london,Tawi ambalo litafunguliwa na mheshimiwa Godless Lema,ufunguzi huo utafanyika Thatched house Pub iliyopo Barking siku ya leo 7/08/2012 saa 20.00 mbili usiku Mawasiliano chris lukosi 07404279633,07903828119"

      Mheshimiwa Slaa nina amini una uwezo mkubwa wa kurekebisha kasoro hii ambayo ina misingi ya udini na ubaguzi wa kijiografia ya nchi yetu na kinyume na katiba ya nchi yetu.

      nina imani nawe kama mtu makini na Muadilifu,hatuwezi kuwasiliana na Bwana Lema kwa vile tayari mahakama kuu imekutana na hatia ya ubaguzi wa kidini kiasi cha kuvuliwa ubunge wake, mtu ambaye amewabagua Watu wa Arusha kwa dini na jinsia akileta ubaguzi huo huku ughaibuni ambako sisi Watanzania tunategemeana kwenye shida na raha, yeye ataondoka baada ya siku kadhaa huku nyuma kishatugawa na kuondoa umoja wetu wa watanzania.Hapa Uingereza kuna chama kikongwe kabisa kwa siasa za nje Cuf ambacho kina matawi Marekani na Canada na sehemu nyingine lakini hakijawahi kuwabagua watanzania walio nje mikutano yao yote hufanya kwenye kumbi ambazo mtu yeyote anaingia.halikadhalika CCM nao wana Tawi lao hapa mikutano yao haijafanyika bar katika kipindi kama hichi cha Mwezi wa Ramadhani.

      Mwisho naomba nikukumbushe maoni ya mzee Mtei muasisi wa chadema pale ilipoundwa tume ya Katiba alilalamika sana kuwa tume ina wajumbe wengi wenye majina ya kiislam hasa waliotoka Zanzibar akahisi kuwa Haki hakufuatwa na akakosa raha kabisa.

      .kitendo cha kuzindua chama Bar ni kuwakimbiza waislam wasiombe au wasishiriki nafasi za uongozi. ingekuwa Mwezi wa kawaida ambao si kama huu Ramadhai wapo waislam wanaokwenda bar lakini wengi wao ukifika mwezi mtukufu hawaendi Bar, jee watashiriki vipi kwenye Chama chako?usisahau minong'ono mingi kuwa chadema ni Chama chenye mlengo wa kikristu,kwa matendo haya ya Lema ni kuthibitisha shutuma au hisia hizo.

      Mheshimiwa Dr.Slaa samahani kwa kukuchosha ila kwa heshima na taadhima naomba kuwasilisha kilio cha Waislam watanzania waliopo Uingereza dhidi ya vitendo vya ubaguzi wa wazi unaofanywa na chama chako.

      Nakutakia kazi njema na natarajia ya kuwa utalifanyia kazi ombi letu sisi Waislam wa Uingereza.
      Ni mimi mpenda demokrasia na Maendeleo.


      From: Ali Rashid <[email protected]>
      To: "[email protected]" <[email protected]>
      Cc: "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>; "[email protected]" <[email protected]>
      Sent: Tuesday, 7 August 2012, 15:33
      Subject: : Yah: Uzinduzi wa Tawi la Chadema-London Kwenye Bar(Pub).
      Hatred is gained as much by good works as by evil.
      Niccolo Machiavelli

    2. Miaka 50

    3. #81
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,516
      Rep Power : 19751
      Likes Received
      5449
      Likes Given
      3641

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Quote By JokaKuu
      Matola,

      ..CDM wangeamua kufanya shughuli yao kwenye ukumbi wa kanisa kungekuwa na kelele kubwa zaidi.

      ..lakini mwandishi anapendekeza CDM wakakodi ukumbi wa msikiti, kwasababu hiyo ni sehemu "neutral."

      ..kwa watu hawa hakuna jema linaloweza kufanywa na CDM. wangekuwa wanaipenda CDM kwa dhati basi wangekuwepo ktk kamati ya maandalizi, na mapendekezo yao yangefanyiwa kazi.

      NB:

      ..huu ni mwezi MTUKUFU kwa ndugu zetu WAISLAMU, sasa siyo vizuri kudai kwamba wanashinda njaa
      .
      Haya maneno na ya simame kama yalivyo, kuna ndugu zetu wengi wa Kiislamu wanashinda njaa tu pengine bila wao wenyewe kujuwa. Funga na mnafki ni vitu viwili tofauti. wapo wanaofunga na funga yao inapokelewa kwa Mungu, lakini wanafki waongo na wafitini hawa bora wawe wanakula tu maana wanashinda njaa hakuna funga yoyote.
      J Mbungi likes this.
      Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.

    4. #82
      NgomaNgumu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Posts : 192
      Rep Power : 473
      Likes Received
      21
      Likes Given
      0

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Quote By Mkandara
      Lazima tukubalia makosa haya kama kweli imefanyika hivyo. Ni makosa makubwa kwa wtayarishaji ambao hawakutazama pande zote mbili na hasa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ambao hauwezi kupotea kichwani unapopanga hafla kubwa kama hii..
      Wakati mwingine tuwe wadogo kukubali makosa badala ya kuonyesha jeuri wkaati makosa kweli yamefanyika, haiwezekkani kabisa mtu upange mkutano BAR halafu muda wa kufutur kisha kuna watu mnataka kutetea ujinga huu..
      Kimsingi hii ilikua ni big mistake ktk swala zima la kiufundi na limetriger vitu vingi sana kwa uchache kabisa ni wasiwasi wa Chadema kuongoza nchi kwa uadilifu. Kuna vitu ambavyo vinawezekana njia moja tu, umeshafanya makosa kubali na jaribu kurekibisha makosa na baadae uombe msamaha. Kimsingi kama Chadema watashindwa kuandaa mkutano mwengine ambao utawajumuisha wananchi wote watakosea sana.
      Mkandara and TandaleOne like this.

    5. #83
      Janjaweed's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2010
      Posts : 3,624
      Rep Power : 1129
      Likes Received
      1391
      Likes Given
      1541

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Quote By JokaKuu
      Matola,

      ..CDM wangeamua kufanya shughuli yao kwenye ukumbi wa kanisa kungekuwa na kelele kubwa zaidi.

      ..lakini mwandishi anapendekeza CDM wakakodi ukumbi wa msikiti, kwasababu hiyo ni sehemu "neutral."

      ..kwa watu hawa hakuna jema linaloweza kufanywa na CDM. wangekuwa wanaipenda CDM kwa dhati basi wangekuwepo ktk kamati ya maandalizi, na mapendekezo yao yangefanyiwa kazi.

      NB:

      ..huu ni mwezi MTUKUFU kwa ndugu zetu WAISLAMU, sasa siyo vizuri kudai kwamba wanashinda njaa.
      umemaliza mjadala.....
      Kama Vipi nipotezee tu; ntakuboa....

    6. #84
      KAMALELA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd June 2011
      Posts : 160
      Rep Power : 438
      Likes Received
      48
      Likes Given
      355

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Quote By TandaleOne
      Nimekuwa JF kwa muda mrefu sasa, nimesoma mengi na kuandika mengi pia. Nimeanzisha post na kuchangia post, nimejibu na kujibiwa, lakini kama watu wapo makini kufuatilia kwa urahisi wanaweza kuona kuwa msingi wa post zangu si ushabiki wala guess work bali ni fact.

      Katika hizo post zangu hakuna hata moja ambayo nimezusha bali hayo niliyoyaandika yanatetewa kwa hoja na ushahidi ulio wazi.

      Mara zote nimekuwa nikisisitiza kujibiwa kwa hoja kwa maana ninachokiandika humu kina mlengwa huo wa hoja. Na hoja hupingwa ama hujibiwa kwa hoja. Si sahihi kudai kuwa post zangu ni za mlengwa mmoja bali ninaandika balanced opinion kwa pande zote, nakosoa pale kwenye makosa na nasifia pale kwenye mafanikio.

      Nimekuwa nikisisitiza kuwa msingi wa mijadala hapa JF usiwe ni ushabiki na fahari ya baadhi kujionesha wanajua kuliko wengine, ama wao ni wakusifu tu ama kupinga tuu, bali nimesisitiza kuwa madhumuni ya kujadili hapa ni kufikia ufahamu sawa(kufahamishana) na kupeana ujuzi juu ya namna serikali inavyofanya kazi zake lakini pia jamii kwa ujumla inavyoweza kupiga hatua kwa kujitathmini na kuchukua hatua za msingi katika kujiletea maendeleo.

      Haitakuwa sahihi, ku-twist mjadala huu kutoka katika maudhui yake asili na kuanza kujadiliwa mtoa thread. Nasema si sawa sawa hata kidogo. TUJADILI KWA HOJA ILI TUJENGE TAIFA LENYE FIKRA SAHIHI.
      Acha zako wewe, fact iko wapi wakati unasema uongo mtupu, eti Mh. Lema alivuliwa ubunge kwasababu ya udini! hakuna hoja ya kujadili zaidi ya ubaguzi ambao mnao kwa wabara...

    7. #85
      kilamfua's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 70
      Rep Power : 374
      Likes Received
      17
      Likes Given
      24

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      nyie wapemba hamjui kwamba uingeeeza ni nchi ya wakristo na kwamba hawatambui ramadhani?sasa mnamlaumi nini lema? Hapa ni kiti moto kwa mbele na bia kwa wingi mkitaka uisilamu wenu pelekeni afrighanistan na somalia. Huku kwetu kent hakuna msikiti hata mmoja labda huko uswahilini barking na west ham.na mkumbuke kwamba hu mwezi ni kwa nyie waisllamu tu sisi wengine tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida.

    8. RukaaJuu Final

    9. #86
      njiwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2009
      Location : ax^2+bx+c=0
      Posts : 4,968
      Rep Power : 2371
      Likes Received
      962
      Likes Given
      172

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Quote By kilamfua
      nyie wapemba hamjui kwamba uingeeeza ni nchi ya wakristo na kwamba hawatambui ramadhani?sasa mnamlaumi nini lema? Hapa ni kiti moto kwa mbele na bia kwa wingi mkitaka uisilamu wenu pelekeni afrighanistan na somalia. Huku kwetu kent hakuna msikiti hata mmoja labda huko uswahilini barking na west ham.na mkumbuke kwamba hu mwezi ni kwa nyie waisllamu tu sisi wengine tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida.
      povu la nini yakhe! hapa swala sio wapemba vs chadema.. hapa ni waislam watanzania waliopo london wakitoa malalamiko kwamba chadema imefanya makusudi kuweka mkutano muda wa iftar tena Bar .. it was like another slap to the Muslims communities toka kwa cdm kwamba "we dont give sh** about you people"
      Pure Matrimony >> Purity starts here (Quran 24:26)
      My loyalty is to reason,and as a reasonable person I reserve the right to change my mind when presented with new information that alters my perspective" Njiwa"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯


    10. #87
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,321
      Rep Power : 12589
      Likes Received
      5858
      Likes Given
      775

      Default

      Quote By kilamfua
      nyie wapemba hamjui kwamba uingeeeza ni nchi ya wakristo na kwamba hawatambui ramadhani?sasa mnamlaumi nini lema? Hapa ni kiti moto kwa mbele na bia kwa wingi mkitaka uisilamu wenu pelekeni afrighanistan na somalia. Huku kwetu kent hakuna msikiti hata mmoja labda huko uswahilini barking na west ham.na mkumbuke kwamba hu mwezi ni kwa nyie waisllamu tu sisi wengine tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida.
      Kwa hiyo Chadema na waswahili mbalimbali nyie na wazungu tu mnaleta ukaskazini mpaka Uingereza.

    11. #88
      'The Choosen''s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th November 2010
      Location : Humuhumu
      Posts : 425
      Rep Power : 516
      Likes Received
      58
      Likes Given
      17

      Default WAISLAM acheni SIASA

      Tatizo liko wapi kufungua tawi la CHADEMA London wakati wa Ramadhani? Au mnatumiwa na Wanamagamba? Nawaheshimu sana. Mna mambo mengi ya kufanya juu ya ustawi wa dini yenu na nchi kwa ujumla. CCM inawapoteza. Achaneni nao hata kwa hili tu

    12. #89
      Mkuu wa chuo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2011
      Location : Kibada
      Posts : 1,770
      Rep Power : 843
      Likes Received
      340
      Likes Given
      20

      Default Re: WAISLAM acheni SIASA

      funguka vizuri bado hujaeleweka kwani wamefanya nini?

    13. #90
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 3,978
      Rep Power : 1219
      Likes Received
      247
      Likes Given
      41

      Default

      Kama Huna kitu kitu cha kuandika bora ukae kimya kuliko kutukana dini za wenzako pumbavu.
      Quote By kilamfua
      nyie wapemba hamjui kwamba uingeeeza ni nchi ya wakristo na kwamba hawatambui ramadhani?sasa mnamlaumi nini lema? Hapa ni kiti moto kwa mbele na bia kwa wingi mkitaka uisilamu wenu pelekeni afrighanistan na somalia. Huku kwetu kent hakuna msikiti hata mmoja labda huko uswahilini barking na west ham.na mkumbuke kwamba hu mwezi ni kwa nyie waisllamu tu sisi wengine tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida.

    14. #91
      emgitty06's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd August 2012
      Posts : 87
      Rep Power : 360
      Likes Received
      20
      Likes Given
      4

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Post ya kiranja inatoa majibu yote

    15. #92
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Quote By Molemo
      Aliyeleta huu uzi ni kibaraka mwaminifu wa Magamba.Nimeamini CDM imewashika pabaya.M4C Forever
      jibuni hoja acheni viloja,bar na waislam mwezi wa ramadhani wapi na wapi au ni kweli cdm ni chama cha wakristo pekee

    16. #93
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,321
      Rep Power : 12589
      Likes Received
      5858
      Likes Given
      775

      Default

      Quote By Matola
      Kwanza walifanikiwa kutuharibia kwa Serikali ya UK na tukafutiwa Entry Viza, sasa na masuala ya Watanganyika wanataka kutuingilia wakati wao wana nchi yao na hawahitaji Muungano, hao ni wanafki watupu hakuna anayefunga hapo bali wanashinda na njaa tu. Phweeeeeeeeeeeeeew!!
      Wamewaharibia nyie kina nani nchi nyingi Tanzania wamewekewa Viza wapemba ndio wamesababisha? Swala la Tanzania kuwekewa Viza Uingereza ni rais wako Mkapa.

    17. #94
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      TandaleOne

      Magwanda hawana mpango na Waislaam wala usijihangaishe ni kupoteza muda tu.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    18. #95
      Tanganyika jeki's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th June 2011
      Posts : 95
      Rep Power : 421
      Likes Received
      33
      Likes Given
      0

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Nangojea kwa hamu 'headline' ya gazeti la Al Nuur. Oh nilisahau, na mjadala wa redio Imani. Yoyote anayepanga na kutekeleza mpango huu wa kutumia dini kwa faida za kisiasa anafanikiwa. Wazanzibari ni lini mliipokea cdm kwa mikono miwili? Je, mlikuwepo kwenye vikao vya maandalizi? Na km hamkuwepo ni kwa nini?

    19. #96
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th November 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 7,243
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1087
      Likes Given
      7

      Default

      Quote By punainen-red
      ..... Yeye na wenzake walioko London wanaolalamika wameshiriki vipi kuijenga Chadema huko waliko? .
      Tandale one awe uingereza? Huyu si yule mzanzibari mdini mwenye malaria isiyopona kada mwaminifu wa sera za Jussa? Aishi uingereza kwan umeambiwa huko kuna uhaba wa waendesha mihadhara ya uchochezi?

    20. #97
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th November 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 7,243
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1087
      Likes Given
      7

      Default

      Quote By zomba
      TandaleOne

      Magwanda hawana mpango na Waislaam wala usijihangaishe ni kupoteza muda tu.
      Wenye mpango na waislam ni kina nani?

    21. #98
      MchukiaUonevu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th February 2012
      Posts : 185
      Rep Power : 1286
      Likes Received
      57
      Likes Given
      50

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Hadi kufika 2015 kwa watakaokuwa hai, nina uhakika vyama vya siasa vyenye hamu ya kuingia ikulu vitakuwa vimebainika mrengo wake pasipo shaka kabisa. Hata kama tutakuwa biased kwa kila njia, ukweli hauzimwi na uongo hata kidogo. Vyenye mrengo wa kidini na ukabila vitajulikana,vinavyopigania haki sawa bila kujali tofauti vitajulikana. Kimsingi tu wale wanaoamini kura za dini moja zinatosha kuwapa ushindi wakubali matokeo pale itakapokuwa vinginevyo.
      Last edited by MchukiaUonevu; 8th August 2012 at 12:04.

    22. #99
      tanga kwetu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th May 2010
      Posts : 934
      Rep Power : 645
      Likes Received
      116
      Likes Given
      30

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      nimeisoma e-mail yote sikuona alipoandika kwamba, alifanya juhudi gani kuwaona waandaaji kabla ya kumlima e-mail Katibu Mkuu (Taifa) W. Slaa (PhD). Hii inaonyesha hata yeye si mtu wa kufuata utaratibu. Zipo cases nyingi kama hizi ambapo waandaji hukiri kughafirika na kubadili venue au ratiba accordingly. Pia katika e-mail hii kuna taarifa, ombi na hukumu humohumo kitu ambacho kinaweza kuleta tafsiri potofu kwamba mwandishi anajaribu kuleta uchonganishi wa CDM kwa waislam. Contents za hii e-mail ina-reveal wewe ni mtu wa aina gani kiasi kwamba hoja yako ina mashiko kwa juu juu lakini ime-serve purpose yako pia.
      Ukii-tune mind set yako kuona difficulties na impossibilities tuu kamwe hutaona possibilities!! Sasa siku nyingine fuata utaratibu...Lema hamtaki kuwasiliana nae (kwa sababu za kipuuzi ulizozitoa...kimbia na UK pia walipohararisha ushoga) na unatambua fika yeye si muandaaji wa huo mkutano bali mgeni rasmi wa kuzindua tawi, vipi kuhusu waandaaji wengine?? Nyamaza kimya ufiche upumbavu wako.
      JokaKuu likes this.

    23. #100
      Sir R's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2009
      Location : Moshi
      Posts : 1,139
      Rep Power : 715
      Likes Received
      99
      Likes Given
      24

      Default re: Ufunguzi wa tawi la CHADEMA UK leo,waislam wamwandikia barua dr Slaa kulalamika.

      Quote By Bull
      Kwa misingi hii chadema hatuiachii nchi, hawana uwezo wa kufahamu na kuelewa hata kidogo!! na logoff
      CDM haisubiri kuachiwa wanachukua nchi.

      Waislamu huwamnatumiwa au mmeamua kutumika tu. haiwezekani kila wakati ni kulalamika tu, siamini kama ni waislamu wote wenye tabia hii ya kutumika.

      Najaribu kufuatilia mienendo ya wa waislamu, huwa nakuta ni rahisi kutumiwa na CCM.

      Inatia huruma
      Umaskini wa Tanzania ni Matokeo ya Akili ndogo kuongoza Nchi

    Page 5 of 10 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...